TAARIFA KUTOKA NDANI YA SHIRIKISHO LA SOKA NCHINI TFF LEO

January 17, 2014
Release No. 008
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Januari 17, 2014

TFF YANOA MAKATIBU MABORESHO TAIFA STARS
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limeandaa semina ya siku mbili kwa makatibu wa vyama vya mpira wa miguu vya mikoa kuhusu maboresho ya timu ya Taifa (Taifa Stars).

Semina hiyo inafanyika ukumbi wa Singida Motel, mjini Singida kuanzia kesho (Januari 18 mwaka huu) ambapo mada mbalimbali zitawasilishwa kwa washiriki kuhusu maboresho hayo.

TFF imeandaa mpango wa maboresho kwa Taifa Stars ambapo pamoja na mambo mengine umepanga kusaka vipaji nchini nzima kwa lengo la kupanua wigo wa kupata wachezaji wanaoweza kuchezea timu hiyo.

Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager mwaka huu inakabiliwa na mechi za mchujo za Kombe la Afrika (AFCON) ambalo fainali zake zitafanyika mwakani nchini Morocco.

Mechi hizo za mchujo zitachezwa kati ya Septemba na Novemba mwaka huu ili kupata timu 16 zitakazofuzu kucheza fainali hizo.

KUZIONA SIMBA NA MTIBWA SUGAR LEO SH.5000.

January 17, 2014

                                     
                               Asha Kigundula,Dar.
MABINGWA wa michuano ya mtani Jembe, timu ya Simba,
leo  inashuka katika Uwanja wa Taifa kuvaana na timu ya
Mtibwa Sugar, huku kiingilio cha chini kikiwa sh.5000.
Mchezo huo utakaoanza saa 10 jioni, ukiwa wa kirafiki,
kwa ajili ya kuziweka timu hizo sawa kabla ya kuanza kwa
Ligi Kuu tanzania Bara, inayoanza kutimua vumbi wiki
ijayo.