RPC LYANGA -WATU WATATU WAKIWA WAMEVAA HIJABU WANAODAIWA NI WAHALIFU WAPIGWA RISASI NA KUFARIKI DUNIA

April 03, 2017

Kamanda wa Polisi mkoani Pwani ,Onesmo Lyanga ,akizungumza jambo na waandishi wa habari. (picha na Mwamvua Mwinyi)

……………….
Na Mwamvua Mwinyi, Rufiji

WATU watatu wanaodhaniwa kuwa ni wahalifu wameuwawa kwa kupigwa risasi na polisi baada ya kukaidi amri ya kutakiwa kusimama eneo la kizuizi cha Mwembe Muhoro wilayani Rufiji, mkoani Pwani.

Watu hao walikuwa wamepakiana kwenye pikipiki moja huku wakiwa wamevaa hijabu.

Akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na tukio hilo, kamanda wa Polisi mkoani Pwani ,Onesmo Lyanga alisema pikipiki nyingine mbili zilifanikiwa kukimbia.

Akielezea juu ya tukio hilo alifafanua,lilitokea Aprili 2 mwaka huu majira ya mchana ,Muhoro ,Rufiji barabara kuu ya Dar es Salaam Lindi. “Siku ya tukio askari walipata taarifa kuwa kulikuwa na pikipiki tatu zikitokea Kibiti kwenda mikoa ya Kusini zikiwa zimebeba watu watatu kila moja “

“Miongoni mwa pikipiki hizo kati yake mbili wamebebwa watu waliovaa hijabu,” alisema Lyanga. Alieleza,askari wa barabarani walipewa taarifa katika kizuizi cha Mparange na kuwasimamisha ili wawahoji lakini walikataa na kupita ambapo waliwajulisha wenzao kwenye kizuizi cha Ikwiriri lakini walikaidi kusimama.

“Baada ya hapo walifika kizuizi cha Ikwiriri lakini bado walikaidi kusimama na kuendelea kukimbia ndipo walipofika kituo cha Muhoro “

“Hata hivyo hawakusimama na askari waliokuwa doria wakiwa kwenye gari waliwafuatilia na wakavuka daraja la Mkapa na waliwapa onyo kwa kupiga risasi hewani,” alisema Lyanga.

Aidha alibainisha baada ya hapo watu hao waliruka kwenye pikipiki na kuanza kukimbilia msituni na ndipo askari walipowapiga risasi za miguu na kiunoni na kufanikiwa kuwakamata.

“Majeruhi hao walijulikana ni wanaume hata hivyo majina yao hayakuweza kufahamika na walikuwa kwenye pikipiki yenye namba za usajili MC 272 BLW aina ya Boxer yenye rangi nyeusi”

“Watu hao wanaodhaniwa kuwa ni wahalifu kwa mwonekano wao walijaribu kuwawahisha hospitali ya Misheni ya Mchukwi,” alisema Lyanga. Lyanga alisema walipofikishwa hospitali daktari alithibitisha kuwa watu hao wamefariki dunia .

Hata hivyo majina yao hayakuweza kufahamika huku pikipiki nyingine mbili zilitoroka na kuelekea mkoa wa Lindi na taarifa zimetolewa polisi ili wawakamate.

Aliwataka wananchi kuwa watulivu pale wanaposimamishwa na askari polisi badala ya kujaribu kutoroka na kwa sasa jeshi hilo limeimarisha doria katika kukabiliana na uhalifu.

SADC YALIPONGEZA BARAZA LA USALAMA LA UN KWA KUONGEZA MUDA KWA MISHENI YA ULINZI DRC

April 03, 2017

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga akizungumza na Waandishi wa Habari (hawapo pichani) kuhusu mkutano wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa uliofanyika New York, Marekani na kupitisha Azimio la kuongeza muda kwa vikosi vya usalama vilivyopo DRC. Kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy. 
Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza Mhe. Mahiga (hayupo pichani). 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Mwenyekiti wa Kamati ya Mawaziri ya Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), Mhe. Dkt. Augustine Mahiga (Mb). akihutubia Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa Jijini New York, Marekani. 
 ============================================= 


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Mawaziri ya Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), Mhe. Dkt. Augustine Mahiga amelipongeza Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa (UNSC) kwa kuridhia na kupitisha azimio namba 2348 (2017) la kuongeza muda kwa Misheni ya Ulinzi wa Amani chini ya MONUSCO iliyopo Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) hadi tarehe 31 Machi, 2018.

Mhe. Mahiga ametoa pongezi hizo wakati akihutubia Baraza hilo kwenye Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa Jijini New York, Marekani hivi karibuni.

Mhe. Mahiga ambaye aliwakilisha nchi 15 za SADC alisema kuwa anaupongeza Umoja wa Mataifa kwa ujumla chini ya uongozi wa Katibu Mkuu, Bw. Antonio Guterres kwa kufikia uamuzi wa kuongeza muda kwa MONUSCO na jitihada nyingine nyingi za kutafuta suluhu ya kudumu kwa changamoto mbalimbali zinazoikabili DRC kwa muda mrefu ikiwemo ukosefu wa amani na usalama.

Mhe. Mahiga alisema kuwa, kupitishwa kwa azimio hilo kunatoa matumaini mapya kwa wananchi wa DRC na dunia kwa ujumla kwamba Umoja wa Mataifa una nia ya dhati kuhakikisha amani ya kudumu inapatikana nchini humo.

Aidha, Mhe. Waziri Mahiga alitumia nafasi hiyo kuuomba Umoja wa Mataifa kutambua mchango mkubwa unaotolewa na Kikosi Maalum cha Force Brigade Intervention-FIB kilichoundwa na SADC ambacho kinashirikiana na MONUSCO katika ulinzi wa amani nchini DRC. 

Alieleza kuwa katika kipindi cha miaka minne tangu kuanzishwa kwa FIB kimeonesha uwezo mkubwa kwa kufanya operesheni ngumu za kukabiliana na vikundi vya waasi na kuvidhibiti, hali iliyopelekea MONUSCO kuaminika zaidi. FIB ina mchango wa vikosi vya ulinzi wa amani kutoka nchi tatu za SADC ambazo ni Tanzania, Afrika Kusini na Malawi.

“Kuanzishwa kwa FIB miaka minne iliyopita ulikuwa ni uamuzi wa pekee kwa Baraza la Usalama na SADC katika masuala ya ulinzi wa amani hususan kwenye maeneo yenye changamoto kubwa za usalama na amani. Hivyo naamini pamoja na kwamba FIB ni Chombo cha muda bado kinahitaji kutambuliwa na kupongezwa” alisema Waziri Mahiga.

Kuhusu changamoto mbalimbali ambazo MONUSCO inakabiliana nazo ikiwemo matishio mapya ya usalama katika maeneo ya Kivu, mbinu mpya za mashambulizi za waasi, ukatili kwa raia na ukiukwaji wa haki za binadamu Waziri Mahiga alisema masuala haya yanailazimu pia MONUSCO kubadilisha mbinu za operesheni ikiwemo kuongezewa vifaa na bajeti ili kuweza kukabiliana kikamilifu na changamoto hizo. 

Pia aliliomba Baraza la Usalama, SADC, Umoja wa Afrika, ICGLR na Nchi zinazoongea Kifaransa kushirikiana katika kutafuta suluhu ya kudumu kwa changamoto zinazoikabili DRC kwa sasa.

Vile vile, Mhe. Waziri Mahiga alitumia nafasi hiyo kwa niaba ya SADC kuiomba na kuialika Jumuiya za Kimataifa kuisaidia Tume ya Uchaguzi ya DRC ili iweze kuandikisha wapiga kura na kuandaa uchaguzi nchi nzima. Pia aliwaomba wanasiasa wa nchini DRC kukabiliana na vurugu za kisiasa zinazoendelea nchini humo kwa sasa na kukwamisha utekelezaji wa Mkataba uliofikiwa mwezi Desemba 2016 chini ya Baraza la Maaskofu (SENCO) la DRC.

Mhe. Mahiga aliongeza kusema kuwa SADC itatuma Misheni Maalum ya Mawaziri nchini DRC katika kipindi cha majuma mawili kuanzia sasa kwa ajili ya kwenda kuzungumza na kushauriana na wadau mbalimbali wa masuala ya siasa nchini DRC ili kutafuta suluhu.”Sisi , nchi wanachama wa SADC hatupo tayari kuona Mkataba wa Desemba unakwama” alisisitiza Waziri Mahiga.


Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki
Dar es Salaam, 03 Aprili, 2017.

Watanzania kufanya miamala ya kifedha kupitia Halopesa na NMB

April 03, 2017


Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya simu ya Halotel Le Van Dai akitiliana saini hati za makubaliano na Kaimu Mkuu wa Akiba za watu Binafsi wa benki ya NMB, Boma Raballa ambapo wateja wa Halotel watafaidika na huduma za kifedha za Halopesa kwa ataweza kuchukua na kuweka fedha zake kutoka katika akaunti yake ya NMB. Makubaliano hayo yalifanyika jijini Dar es Salaam jana. Kushoto ni Afisa Mwendeshaji wa Halopesa, Henry Mavula na kulia ni Meneja wa Huduma za Ziada wa benki ya NMB,Stephen Adili
Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Halotel Le Van Dai (kushoto) akibadilishana hati za makubaliano na Kaimu Mkuu wa Akiba za watu Binafsi wa benki ya NMB,Boma Raballa ambapo wateja wa Halotel watafaidika na huduma za kifedha ya Halopesa ambapo mteja wa Halotel ataweza kuchukua na kuweka fedha zake kutoka katika akaunti yake ya NMB. Makubaliano hayo yalifanyika jijini Dar es Salaam leo. 
Pichani kati ni Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya simu ya Halotel Le Van Dai akizungumza mbele ya Waandishi wa habari (hawapo pichani),kuhusiana na azma ya kupanua wigo wa huduma za kifedha kwa wananchi wenye vipato tofauti, kampuni ya mawasiliano ya Halotel na benki ya NMB zimeingia katika ushirikiano utakao wawezesha mamilioni ya watanzania kunufaika na huduma za kifedha nchi nzima. 
Kaimu Mkuu wa Akiba za watu Binafsi wa benki ya NMB, Boma Raballa akizungimza na Wanahabari mapema leo jijini Dar,Katika kufanikisha azma ya kupanua wigo wa huduma za kifedha kwa wananchi wenye vipato tofauti, kampuni ya mawasiliano ya Halotel na benki ya NMB zimeingia katika ushirikiano utakao wawezesha mamilioni ya watanzania kunufaika na huduma za kifedha nchi nzima.

Katika kufanikisha azma ya kupanua wigo wa huduma za kifedha kwa wananchi wenye vipato tofauti, kampuni ya mawasiliano ya Halotel na benki ya NMB zimeingia katika ushirikiano utakao wawezesha mamilioni ya watanzania kunufaika na huduma za kifedha nchi nzima.

Hatua hii itawawezesha watanzania wengi zaidi kufikiwa na huduma za kifedha kwa njia ya mtandao ikiwa ni sehemu ya kufanikisha azma ya serikali ambayo inazitaka taasisi mbalimbali za kifedha kuwafikia wananchi na huduma zao hasa kwa maeneo ya vijijini.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Naibu Mkurugenzi wa Kampuni ya Halotel, Bw. Le Van Dai amesema kuwa ni hatua nyingine kubwa katika utoaji wa huduma za kifedha kupitia simu za mkononi ambapo sasa huduma ya Halopesa itakuwa imeunganishwa na benki ya NMB ili kuwawezesha wateja kufanya miamala kwa urahisi zaidi.

Dai ameendelea kuwa ushirikiano huo, umeunganisha taasisi kubwa zenye wateja wengi na zilizosambaa kwa kiasi kikubwa nchini. Tunatarajia huduma hii itapunguza kadhia kwa watumishi wa taasisi za umma, wakiwemo walimu na watu wa sekta zingine wakiwemo wakulima, wavuvi na wafanya biashara wanaoishi vijijini ambako huduma za kibenki hazijafika kote. Maeneo haya kwa kiasi kikubwa hutegemea njia ya simu za mkononi kuweza kutoa fedha au kuweka kwa njia ya haraka na usalama zaidi.

“Ushirikiano huu ni wa kipekee katika kurahisisha maisha ya watanzania ambao wamekuwa wakipata tabu kupata huduma za kifedha kutokana na maeneo wanayoishi. Sisi kama Halotel hadi sasa tumewafikia watanzania kwa zaidi ya asilimia 95. Hivyo ni dhahiri kwamba wateja watakaojiunga nasi wataweza kutoa au kuweka fedha huko huko waliko kupitia kwa mawakala wetu ambao wameenea nchi nzima,” aliongezea Dai.


“Tunatambua changamoto ambazo kwa kiasi kikubwa zimekuwa zikiwasibu Watanzania hasa wa kipato cha chini. Kwani wengi wao walikuwa wanakwama kuweza kupata huduma za kifedha kutokana na miundombinu kutowafikia. Mpaka hivi sasa Halotel ina mawakala zaidi ya 30,000 walioenea nchi nzima. Hii itawawezesha wakazi wa maeneo ambayo hayakuwahi kuwa na mawasiliano kabisa au huduma za kibenki sasa kuweza kupata huduma za kifedha kupitia simu zao za mkononi,” alimalizia Naibu Mkurugenzi wa kampuni hiyo.

Kwa upande wake Kaimu Mkuu wa Huduma Binafsi za Kibenki wa NMB, Boma Raballa, amesema ushirikiano huo ni mafanikio mengine makubwa ya kibiashara kwao hususani katika kupanua wigo wa huduma zake na namna itakavyoweza kuunganisha teknolojia ili kuwarahisishia watanzania kupata huduma za kifedha popote walipo.

“Benki ya NMB ni ya kwanza kutoa huduma za kipekee na zenye ubunifu wa hali ya juu na tunaamini ushirikiano huu utatuwezesha kuwafikia watanzania wengi zaidi. Watanzania wanahitaji huduma za kifedha muda wowote na mahali popote walipo. Hivyo kuja kwa ushirikiano huu kutawaletea uhakika wa kupata fedha tena kwa njia rahisi kabisa kwa kutumia simu zao za mkononi maana sio muda wote watakuwa karibu na mashine zetu za kutolea fedha (ATM) au matawi ya benki yetu,” alisema Raballa

“Kwa kushirikiana na Halotel tunaamini tutakuwa tumefanikisha lengo la serikali na benki yetu kwa ujumla katika kuwafikia watanzania wengi zaidi. Hii inamaanisha kuwa wateja wa kampuni hizi mbili ambazo hawajafikia na huduma aidha za NMB au Halotel basi watafikiwa kwa pamoja. Mbali na kurahisisha huduma lakini pia itasaidia kwa kiasi kikubwa kurahisisha kuboresha na kurahisisha hali ya maisha na uchumi kwa watanzania, yaani kwa watoa na wapokea huduma,” aliongezea Raballa.

“Azma ya benki ya NMB ni kuzidi kuwa wabunifu na kuongeza kasi ya maboresho katika utoaji wa huduma zake. Lakini pia kushirikiana na wadau wengine katika sekta ya kifedha kuhakikisha inaendelea kuwapatia wateja wigo mpana Zaidi wa machaguo ya kupata huduma zake ikiwemo kuongeza mashine za kutolea fedha, matawi na huduma nyinginezo kwa lengo la kusogeza karibu huduma za kibenki nchi nzima,” Alihitimisha.

MAKAMU WA RAIS CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM (DARUSO) SHAMIRA MSHANGAMA AKUTANISHA WADAU KUJADILI DHANA YA “MWANAMKE NA UONGOZI” UDSM

April 03, 2017
Aliyekuwa Mgeni Rasmi katika kongamano hilo lililo andaliwa na Makamu wa Rais wa Serikali ya wanafunzi wa  Chuo Kikuu cha Dar es salaam Bi. Shamira Mshangama Mh. Sophia Mjema akitoa nasaha zake kwa wote waliohudhuria katika kongamano hilo lililofanyika katika Ukumbi wa Nkurumah Chuo kikuu cha Dar es salaam.
  Makamu wa Rais wa Serikali ya wanafunzi Chuo Kikuu cha Dar es salaam Bi. Shamira Mshangama akieleza kwa ufupi juu ya Kongamano hilo na Kumkaribisha Mkurugenzi wa Maswala ya Jinsia Chuo Kikuu Cha Dar es salaam Dkt. Kafanabo
Mkurugenzi wa Maswala ya Jinsia Chuo Kikuu Cha Dar es salaam Dkt. Kafanabo akielezea kwa undani juu ya jinsia na uongozi katika kongamano hilo
 Mkurugenzi Mkazi wa Asasi ya Kiraia ya Global Peace Foundation(GPF) nchini Tanzania Bi. Martha Nghambi akielezea shughuli za asasi hiyo na nafasi ya mwanamke katika uongozi.
Meneja wa Benki ya NMB PLC tawi la Chuo Kikuu cha Dar es salalaam Bi. Rehema Mwibura akielezea safari yake ya uongozi mpaka hapa alipofikia sasa na kuwaatha vijana wakike wasikate tamaa kwa kuwa wanaweza.
 Mwanachama wa zamani wa USRC Bi. Yunge Kanuda akiwasihi vijana wanawake kuwa wanayo nafasi ya kugombea ngazi mbalimbali za uongozi hivyo wanatakiwa wathubutu ili waweze kushika nyadhifa mbalimbali.
Washiriki wa Kongamano hilo wakifuatilia kwa makini mijadala mbalimbali inayoendelea
Aliyekuwa Spika wa Bunge la USRC kwa mwaka 2014/2015 Protus Petro akielezea juu ya uongozi 
Aliyekuwa Makamu wa Rais wa Serikali ya wanafunzi Chuo Kikuu cha Dar es salaam Irene Ishengoma na aliyeshiriki Shindano la Maisha Plus 2016 akielezea mambo mbalimbali yanayowahusu wanawake na kuwasihi kuto bweteka kwa kuwa wanaweza.
 Baadhi ya Washiriki wa Kongamano hilo wakiuliza maswali na kuchangia mawazo katika Kongamano hilo.
 Mwanzilishi na Rais wa Taasisi ya wanafunzi wanawake kutoka Chuo Kikuu cha Dar es salaam Consolata Chikoti akifuatilia kwa makini mijadala ikiendelea.
 Mh. Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mh. Sophia Mjema (wa nne kutoka kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na waliokuwa wazungumzaji wakati wa Kongamano hilo.
  Mh. Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mh. Sophia Mjema (wa nne kutoka kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na kamati ya maandalizi ya Kongamano la Wanawake na Uongozi
  Mh. Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mh. Sophia Mjema (wa nne kutoka kushoto) kwa waliokaa akiwa katika picha ya pamoja na Baadhi ya viongozi wa Serikali ya wanafunzi Chuo kikuu cha Dar es salaam.
 Picha ya pamoja ya viongozi kutoka maeneo mbalimbali ikiwa ni Asasi,vyuo na shule shule mbalimbali
Washiriki wakiwa katika Kongamano hilo.
Picha zote na Fredy Njeje

Na Dickson Mulashani

Makamu wa Rais wa Serikali ya wanafunzi katika Chuo kikuu cha Dar es salaam Bi. Shamira Mshangama, aliandaa kongamano kubwa lililohusisha watu mbalimbali wakiwemo wanafunzi kutoka shule za Sekondari,wanavyuo,taasisi na asasi za kijamii kwa lengo la kuzungimzia masuala mbalimbali yanayowahusu vijana hasa vijana wa kike na dhana ya uongozi ikiwa ni pamoja na nafasi ya mwanamke katika uthubutu wa kuwa katika nafasi mbalimbali za uongozi.

Akizungumza katika kongamano hilo mgeni Rasmi katika ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mh. Sophia Mjema aliwaeleza washiriki wa kongamano hilo safari nzima ya maisha yake katika uongozi lengo likiwa kuwapa mwanga kuwa wanawake wanaweza kushika nafasi mbalimbali bila wasiwasi.

Mh. Sophia aliwaatha vijana hasa wa vyuoni na mashuleni kuto danganyika na kutoa rushwa ya ngono na kuto kujirahisiha maeneo ya kazi ili mtu fulani ampende amchukue ili apate kitu fulani na kusisitiza kuwa hayo ni mambo yanapita na waepuke tamaa hizo.

Kadhalika aliongeza kuwa kwa wanawake wote ambao wanania ya kugombea nafasi kama Ubunge pindi wanapopata wawe mbele zaidi katika kutetea maslahi ya wanawake kwa kuwa wao wanaona mambo mengi zaidi katika jami.

Mwisho alisisitiza kuwa mambo yote yanawezekana endapo amani itadumishwa katika eneo la kazi kwa kuwa sehemu ambayo haina amani hata utendaji wa kazi huwa ni mgumu, alisema kuwa watu wakipendana na swala zima la kazi litakuwa na ufanisi zaidi.     

Kwa upande wake Mkurugenzi mkazi wa Asasi ya kiraia ya Global Peace Foundation (GPF) Martha Nghambi alielezea kwa undani kuwa " GPF ni ni Taasisi isiyo ya kiserikali,ambayo si ya kidini na haitengenezi faida ya aina yoyote ile ina makao yake makuu  katika jiji la Washington DC nchini Marekani na lenye matawi yapatayo 23 duniani kote, yakiwemo mabara ya Afrika,Ulaya, Asia na Marekani ni “Taasisi hii kwa Tanzania ilianzishwa kati kati ya Mwaka juzi 2015 ambapo pamoja na uchaga wake wameonesha juhudi kubwa katika kuhamasisha amani nchini kuanzia ngazi ya familia na jamii kwa ujumla."

Mathalan Mkurugenzi huyo akiongelea umuhimu wa wanawake katika nafasi mbalimbali za uongozi aliwasihi vijana wakike tangu wakiwa wadogo wawe na watu ambao ndio mfano kwao "Role Model" watakao wafanya kutimiza ndoto zao, pia kuwa na uthubutu kwa kuwa wanaweza kushika nyadhifa mbalimbali kuanzia ngazi ya chini mpaka uongozi wa juu.

Nae Mkurugenzi wa  wa Maswala ya Jinsia Chuo Kikuu Cha Dar es salaam Dkt. Kafanabo pamoja na kutoa ufafanuzi wa historia za viongozi wanawake waliowahi kushika nyadhifa mbalimbali nchini Tanzania alisema kuwa nia ya wanawake katika uthubutu wa katika kutafuta nafasi mbalimbali bado hauridhishi kwani safari ya kupambana na mfumo dume hata kwa wanawake wasomi bado ni ndefu