TAARIFA ZA KIMICHEZO KUTOKA SHIRIKISHO LA MPIRA TANZANIA WA MIGUU TFF

TAARIFA ZA KIMICHEZO KUTOKA SHIRIKISHO LA MPIRA TANZANIA WA MIGUU TFF

June 05, 2015

download-41 
YAH: MGOGORO KATI YA MCHEZAJI RAMADHAN SINGANO NA KLABU YA SIMBA.
 TFF imepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za mgogoro wa kimkataba kati ya Mchezaji Ramadhani Singano wa klabu ya Simba.
 TFF imeagiza mwakilishi wa klabu ya Simba pamoja na mchezaji wa Simba wafike ofisi za TFF siku ya Jumanne tarehe 09/06/2015 kwa mazungumzo.
 Kila upande umetakiwa uje na vielelezo vyake.
Katika kipindi hiki cha kuelekea kwenye mazungumzo,TFF inaziasa pande zote mbili zijiepushe na kutoa matamko yanayoweza kuchochea hali ya kutoelewana na kuamsha hisia mbaya katika familia ya mpira wa Miguu Tanzania.
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)
MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AADHIMISHA KILELE CHA SIKU YA MAZINGIRA DUNIANI, MKOANI TANGA

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AADHIMISHA KILELE CHA SIKU YA MAZINGIRA DUNIANI, MKOANI TANGA

June 05, 2015

1
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wakati wa sherehe za maadhimisho ya Kilele cha Siku ya Mazingira Duniani, zilizofanyika kwenye wa Viwanja Vya Tangamani, mkoano Tanga, leo Juni 5, 2015.
Picha zote na OMR
13
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akikata utepe kuzindua rasmi Jarida la muongozo wa Usafi wa Mazingira, wakati wa sherehe za maadhimisho ya Kilele cha Siku ya Mazingira Duniani, zilizofanyika kwenye wa Viwanja Vya Tangamani, mkoano Tanga, leo Juni 5, 2015. Kushoto kwake ni Waziri wa Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais, Dkt. Binilith Mahenge, Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano, Samia Suluhu, na Naibu Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Stephen Masele.
14
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akikata utepe kuzindua rasmi Filamu ya Mamba wa Zigi, wakati wa sherehe za maadhimisho ya Kilele cha Siku ya Mazingira Duniani, zilizofanyika kwenye wa Viwanja Vya Tangamani, mkoano Tanga, leo Juni 5, 2015. Kushoto kwake ni Waziri wa Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais, Dkt. Binilith Mahenge, Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano, Samia Suluhu.
3
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi Tuzo ya mshindi wa tatu katika usimamizi wa usafi wa mazingira, Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Felix Ntibenda, wakati wa sherehe za maadhimisho ya Kilele cha Siku ya Mazingira Duniani, zilizofanyika kwenye wa Viwanja Vya Tangamani, mkoano Tanga, leo Juni 5, 2015.
5
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi Tuzo ya mshindi wa pili katika usimamizi wa usafi wa mazingira, Mwakilishi wa Manispaa ya Kinondoni, wakati wa sherehe za maadhimisho ya Kilele cha Siku ya Mazingira Duniani, zilizofanyika kwenye wa Viwanja Vya Tangamani, mkoano Tanga, leo Juni 5, 2015.
9
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi Tuzo ya mshindi wa kwanza katika usimamizi wa usafi wa mazingira, Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Leonidas Gama, wakati wa sherehe za maadhimisho ya Kilele cha Siku ya Mazingira Duniani, zilizofanyika kwenye wa Viwanja Vya Tangamani, mkoano Tanga, leo Juni 5,
11
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi Tuzo ya usimamizi wa usafi wa mazingira, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Kpt . Chiku Galawa wakati wa sherehe za maadhimisho ya Kilele cha Siku ya Mazingira Duniani, zilizofanyika kwenye wa Viwanja Vya Tangamani, mkoano Tanga, leo Juni 5, 2015.
12
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akikabidhi zawadi ya Pikipiki kwa mmoja kati ya washindi.
6
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitembelea mabanda wakati wa sherehe za maadhimisho ya Kilele cha Siku ya Mazingira Duniani, zilizofanyika kwenye wa Viwanja Vya Tangamani, mkoano Tanga, leo Juni 5, 2015.
10
8
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa mtoa huduma wa dawa za asili, Karunde Amadi, wakati alipotembelea kwenye banda wafanyabiashara za dawa asili, kwenye Sherehe za maadhimisho ya Kilele cha Siku ya Mazingira Duniani, zilizofanyika kwenye wa Viwanja Vya Tangamano, mkoani Tanga, leo Juni 5,
2 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Mazingira wa Ofisi yake, Dkt. Julius Ningu, wakati alipotembelea kwenye banda la maonyesho la Ofisi ya Makamu wa Rais, kwenye Sherehe za maadhimisho ya Kilele cha Siku ya Mazingira Duniani, zilizofanyika kwenye wa Viwanja Vya Tangamano, mkoani Tanga, leo Juni 5, 2015.
4
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kuhusu utunzaji wa nyaraka kutoka kwa Mkurugenzi wa Msaidizi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Lupi Mwaikambo, wakati alipotembelea kwenye banda la maonyesho la Ofisi ya Makamu wa Rais, kwenye Sherehe za maadhimisho ya Kilele cha Siku ya Mazingira Duniani, zilizofanyika kwenye wa Viwanja Vya Tangamano, mkoani Tanga, leo Juni 5,