KARIBU LEO ESCAPE ONE UCHEZE MZIKI MZURI NA BENDI YAKO YA SKYLIGHT
Sony Masamba akichana mistari na mashabiki wa Skylight Band wakiendelea kuzirudi huku Joniko Flower, Sam Mapenzi na Kasongo Junior wakimsikindiza kwa miondoko ya aina yake. Hakika hii sio ya kukosa leo Jumapili.
Kasongo Junior na Suzy wakiwapa raha mashabiki wa Skylight Band (hawapo pichani) ndani ya kiota cha Escape One jumapili iliyopita, bila kukosa ya leo itakuwa pale pale.
Kasongo Junior na Suzy wakiendelea wakizirudi kwenye kiota cha Escape One
Joniko Flower akizirudi pamoja na Mashabiki wa Bandi ya Skylight pamoja na waimbaji wa bendi hiyo
Waimbaji wa Bendi ya Skylight wakiendelea kutoa burudani huku wakiongozwa na Rapa Mkongwe wa muziki wa dansi wa Skylight Band, Joniko Flower
Kifaa kipya cha Bandi ya Skylight, Leah akitoa burudani ya nguvu mbele ya mashabiki wao huku akisindikizwa na Kasongo Junior
Waimbaji wa Bendi ya Skylight pamoja na mashabiki wa bendi hiyo wakiendelea kuzirudi katika kiota cha Escape One Jijini Dar es Salaam
KAMATI KUU YA CCM KUKUTANA KESHO MJINI DODOMA
Kamati Kuu ya Taifa ya CCM inatarajiwa kufanya kikao chake cha siku moja mjini Dodoma kesho Novemba 15, 2015 kujadili majina ya wana-CCM walioomba ridhaa ya kuteuliwa kugombea Uspika na Unaibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Kamati Kuu itafanya kikao chake
kesho saa sita kamili mchana chini ya Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu
Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete.
Kikao cha Kamati Kuu kitafuatiwa
na Kikao cha Kamati ya Wabunge wote wa CCM kitakachofanyika Novemba 16,
2015 saa nne asubuhi katika ofisi za Makao Makuu ya CCM Dodoma.
Imetolewa na:-
Nape Moses Nnauye
KATIBU WA HALMASHAURI KUU YA TAIFA,
ITIKADI NA UENEZI
14/11/2015
TAIFA STARS YAING’ANG’ANIA VIBAYA ALGERIA YATOKA SARE YA 2-2 UWANJA WA TAIFA.
Wachezaji wa timu ya Taifa Stars
na Algeria wakichuana vikali kuwania mpira katikati yao wakati wa mchezo
wa kufuzu fainali za kombe la dunia uliofanyika kwenye uwanja wa Taifa
jijini Dar es salaam huku timu hizo zikitoshana nguvu kwa kufungana
magoli 2-2 na kuifanya Taifa Stars kuwa na kibarua kigumu wakati wa
mchezo wa maruduano utakaofanyika Novemba 17 mjini Algers Algeria ili
kusonga mbele katika michuano hiyo.Taifa Stars inahitaji kushinda
katika mchezo wake huo ili iweze kusonga mbele.
Baadhi ya washangilianji wakishangilia kwa nguvu wakati wa mchezo huo uliofanyika kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Hii ni staili moja wapo iliyotumiwa na washngiliaji wa timu ya Taifa Stars katika mchezo huo.
Mdau Muddy, Bariki na marafiki zao walikuwa ni mmoja wa mashuhuda wa mchezo huo kwenye uwanja wa Taifa
Kikosi cha Timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars.
Kikosi cha timu ya Taifa ya Algeria kikiwa katika picha ya pamoja.
MAANDALIZI YA KIKAO CHA BUNGE YAENDELEA
Mtaalamu wa Upasuaji wa Uti wa Mgongo na Magonjwa ya Mfumo wa Fahamu kutoka Hospitali za Apollo kuendesha huduma Dar.
Dr
Alok Ranjan, mtaalamu wa magonjwa ya mfumo wa fahamu na uti wa mgongo
kutoka hospitali ya Apollo akitoa huduma kwa mtoto Zulea akiwa na mama
yake Shamila Idd katika kliniki iliyofanyika siku
tatu.’
Dr
Alok Ranjan, mtaalamu wa magonjwa ya mfumo wa fahamu na uti wa mgongo
kutoka hospitali ya Apollo akiongea na waandish wa habari katika cliniki
iliyoanza tarehe 11 na kuendelea mpaka tarehe 13 katika hospitali ya
hindumandal.
Bwana
Hafidhi Rashid Waziri, mmoja wa wagonjwa waliofanyiwa upasuaji wa uti
wa mgongo na Dr Alok Ranjan katika hospitali ya Apollo Hyderebad
akiongea na waandishi wa habari katika Klinik hiyo.
Na Mwandishi Wetu,
Tanzania
ni moja ya nchi ambazo ina uhaba mkubwa wa madaktari bingwa wa mfumo wa fahamu
kitendo kinachopelekea nchi kupoteza fedha nyingi kwa kuwapeleka wagonjwa wa
matatizo ya aina hiyo nje ya nchi kupata matibabu na ushauri.
Inakadiriwa
kuwa watoto wachanga 1000 kati 4000 wanaozaliwa na tatizo la mfumo wa fahamu
hupatiwa matibabu huku wengine 3000 wakishindwa kupatiwa matibabu.
Kutokana
na hali hiyo, Hospitali ya Apollo ya nchini India imemleta nchini daktari
bingwa wa upasuaji wa uti wa mgongo na mfumo wa fahamu ambaye pia ni Mkuu wa
idara ya upasuaji wa magonjwa ya fahamu katika hospitali hiyo DKT ALOK RANJAN ambaye
atakuwa akitoa
huduma na kuwaona wagonjwa wake aliowafanyia upasuaji siku za
nyuma.
Nao baadhi
ya wagonjwa waliofika katika kliniki hiyo inayofanyikia katika hospitali ya
hindu mandal jijini Dar es Salaam wameiomba serikali kuhakikisha kwamba
inasaidia katika gharama za matibabu ya watu wanaosafiri nje ya nchi kufuata
matibabu ya magonjwa mbali mbali.
Wamezitaka
pia kampuni za bima ya afya kuhudumia wateja wake katika hospitali za kimataifa
badala ya kujikita katika hospitali za hapa nchini pekee.
Katika mkutano huo na waandishi wa
habari ulofanyika tarehe 12 katika hospitali ya hindumandali Dk. Alok Ranjan kutoka Hospitali
za Apollo amewashauri watanzania kubadilisha mtindo wa maisha ili kuepukana
na magonjwa ya mfumo wa fahamu na uti wa mgongo. anasema kuwa kwa watu wazima
ugonjwa huu mara nying husababishwa na namna mbovu ya ukaaji ambao hudhuru uti
wa mgongo, trauma, shinikizo la damu, ajali, kisukari, uzito wa kupitiliza na
sababu nyinginezo.
Tanzania
kwa sasa inakadiriwa kuwa na madaktari wa mfumo wa fahamu 7 ambao wote kwa sasa
ni watendaji katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dar es Salaam.
Subscribe to:
Posts (Atom)