WAZIRI MPINA ATOA MAAGIZO KWA KATIBU MKUU MIFUGO YANAYOTAKIWA KUTEKELEZWA NDANI YA WIKI MBILI

February 25, 2018

Katika Picha Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Luhaga Mpina na ujumbe wake akiwa akiwa katika ziara katika kituo cha Taifa cha uzalishaji Mbegu bora za Mifugo kwa njia ya chupa, (NAIC) kilichopo Mjini Arusha.

 
Katikati Katibu Mkuu Mifugo Dkt. Maria Mashingo akisoma Hotuba katika zoezi la uzinduzi wa madume ya kisasa ya mbegu bora za Ng’ombe katika kituo cha taifa cha uzalishaji mbegu bora kilichopo mjini Arusha, Kushoto ni waziri wa Mfugo na Uvuvu Mhe. Luhaga Mpina, na kulia ni Mkurugenzi wa Uzalishaji Mifugo na Masoko  wa Wizara hiyo, Dkt.Lowlence Asiimwe.
 
Katikati Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Luhaga Mpina akiangalia dume bora la kisasa kutoka nchi ya New Zealand katika kituo cha Taifa cha Uhimilishaji cha (NAIC) Arusha jana alipokuwa katika ziara maalum ya uzinduzi wa Madume hayo.kulia ni  Dkt Paul Mollel, Mkurugenzi wa Kituo hicho.
Katika Picha Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Luhaga Mpina akikata utepe kuashiria uzinduzi wa madume bora ya kisasa kutoka nchi ya South Africa na New Zealand  yaliyoletwa nchini kwa ajili ya uzalishaji wa mbegu bora za mifugo. Pembeni yake ni katibu Mkuu Mifugo Dkt  Maria Mashingo na ujumbe wake.
NA, MWANDISHI MAALUM - ARUMERU
Wizara ya Mifugo na Uvuvi imepewa wiki mbili  kufanya tathmini kuona kama kuna haja ya kuagiza maziwa na mazao yake kutoka nje ya nchi na kama waagizaji wanafuata taratibu na masharti ya kisheria yaliyowekwa na Serikali.
Hayo yameelezwa jana na Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Luhaga Mpina alipokuwa katika ziara ya kutembelea kituo cha Taifa za uzalishaji wa mbegu Bora za Mifugo kwa njia ya chupa kilichopo Wilayani Arumeru Mkoani Arusha.
Waziri Mpina pia aliitaka Wizara yake kuandaa mpango kazi utakao wezesha kuzalisha Ng’ombe milioni moja kwa mwaka  kuanzia mwaka wa fedha 2018/19 ili kuweza kusaidia kujenga viwanda vya maziwa na  kuweza kumudu soko la ndani  na hata kuhudumia bara zima la Afrika  na kusaidia kuongeza pato la Taifa.
“Kuna makampuni 43 nchini yanayoingiza maziwa toka nje ya nchi,na makampuni 81 yanayojishughulisha na maziwa na mazao yake,Wizara ifanye tathmini kama kweli tunahitaji kuingiza maziwa hayo. Alisisitiza Mpina.”
Aliongeza kuwa maziwa mengi yanaingia ndani ya nchi kwa kupitia njia za panya, na kusema kuwa wale wote wanaojishughulisha na biashara hizo wapo hatarini kukamatwa na sheria itachukua mkondo wake. “Mimi na Wizara na yangu tumejipanga kimwili kiroho na kiakili tutawashughulikia wote wanaofanya biashara hizi kimagendo hakuna suluhu kwa yeyote atakaye kamwatwa. Alisisitiza.”
Sambamba na hilo, Waziri Mpina pia alimpongeza katibu Mkuu Mifugo Dkt Maria Mashingo kwa kazi kubwa ya kuhakikisha kuna kuwepo na mbegu za kutosha kwa kuwepo kwa madume bora 26 hadi sasa yenye uwezo wa kuzalisha jumla ya dozi 3,120,000 kwa mwaka.
Kwa upande wake, Dkt. Mashingo alimshukuru Waziri kwa kutoa maelekezo ambayo yanalenga kuleta mapinduzi ya mifugo na kwamba ameyapokea na yatatekelezwa  mara moja kama alivyoagiza.


BITEKO AUTAKA MGODI WA KATAVI NA KAPUFI KUAJIRI WATANZANIA

February 25, 2018
Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko ameupa Siku 14 Mgodi wa Dhahabu wa Katavi & Kapufi uliopo Mkoani Katavi kuhakikisha uwe umekamilisha taratibu za kuajiri Watanzania na kupunguza wafanyakazi wa kigeni kwenye nafasi ambazo Watanzania wanazimudu kama Sheria inavyoelekeza.

Alitoa agizo hili jana Tarehe 24 Februari, 2018 alipofanya ziara kwenya mgodi huo ili kujionea shughuli zinazofanyika katika mgodi huo.

Taarifa ya mgodi iliyowasilishwa kwake ilibainisha kuwa jumla ya wageni 48 wameajiriwa na huku 36 kati yao wakiwa hawana ujuzi na wanafanya shughuli ambazo Watanzania wanamudu, ikiwemo ya ulinzi.

Biteko alisema dhamira ya Serikali ni kuona Watanzania wananufaika na Sekta ya Madini kwa namna mbalimbali ikiwemo ya kujipatia ajira kwenye migodi na kwamba suala hilo la kuajiri wageni kwenye nafasi wanazomudu Watanzania halivumiliki.

Alimuagiza Mkuu wa Wilaya na Afisa Madini kuhakikisha wanalifuatilia jambo hilo na liwe limemalizika baada ya wiki mbili kuanzia Tarehe 24 Februari, 2018 na apatiwe mrejesho wake.

“Mnawafanyakazi wengi ambao wanafanya kazi ambazo Watanzania wanaziweza. Hatuwabagui lakini tunataka manufaa ya madini yabaki kwa Watanzania,” alisema Biteko.

Biteko aliiagiza Idara ya Uhamiaji Nchini kufuatilia Wafanyakazi wakigeni waliopo migodini ili kukagua kama wanavyo vibali vya kufanya kazi hapa nchini. “Mnavyotoa vibali muwe makini, ili shughuli zinazokuja kufanywa na wageni ziwe kweli Watanzania hawazimudu,” alisisitiza.

Alihimiza migodi yote nchini kuepuka kuwanyanyasa wafanyakazi sambamba na kuwataka wafanyakazi waliaoajiriwa migodini kufanya kazi kwa uaminifu ili kulijengea Taifa heshima inayokubalika.
aibu Waziri wa Madini, Doto Biteko (kushoto) akijadiliana jambo na Mkuu wa Wilaya ya Mpanda, Lilian Matinga (katikati) wakati wa kukagua shughuli ziazofanyika kwenye Mgodi wa Dhahabu wa Katavi & Kapufi Ltd uliopo Mkoani Katavi.
 Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko (wa pili kulia) akitembelea maeneo mbalimbali ya Mgodi wa Dhahabu wa Katavi & Kapufi Ltd uliopo Mkoani Katavi ili kujionea shughuli zinazoendelea mgodini hapo. Wa pili kulia ni Mbia na Makamu Mwenyekiti wa Mgodi wa Katavi & Kapufi Ltd, Sebastian Kapufi
 Moja ya eneo la mitambo kwenye mgodi wa Dhahabu wa  Katavi & Kapufi Ltd uliopo Mkoani Katavi
TRA: SASA UNAWEZA KULIPA KODI YA MAJENGO KIELEKTRONIKI

TRA: SASA UNAWEZA KULIPA KODI YA MAJENGO KIELEKTRONIKI

February 25, 2018

TR
Na: Veronica Kazimoto,
Dar es Salaam,
Wito umetolewa kwa wananchi wote kuanza kulipa Kodi ya Majengo ya mwaka 2017/18 mapema kwa kuwa ulipaji wa kodi hiyo umerahisishwa  ambapo wanaweza kulipa kwa kutumia njia ya kielektroniki.
Akizungumza jijini Dar es Salaam hivi karibuni Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Charles Kichere alisema hakuna muda utakao ongezwa ifikapo Juni 30, mwaka huu na badala yake faini itatozwa kwa kila mmiliki wa jengo atakayechelewa kulipa kodi hiyo.
“Kama mamlaka hatuoni sababu ya kuongeza muda wa kulipa Kodi ya Majengo ifikapo tarehe 30 Juni 2018 kwasababu tumewarahisishia wananchi ulipaji wa Kodi hii ambapo wanaweza kupata ankara ya malipo kwa majengo yaliyosajiliwa kwenye tovuti ya TRA au simu ya mkononi na kufanya malipo katika tawi lolote la Benki ya NMB au CRDB popote nchini au kwa njia ya mitandao ya simu ya Mpesa, Tigopesa au Halopesa”, alisema Kichere.
Kamishna Mkuu Kichere alisema kuwa, wananchi wafuatilie matangazo ya namna ya kulipa Kodi ya Majengo kwa njia ya kielektroniki katika mitandao ya kijamii na kwenye vyombo mbalimbali vya habari au wafike katika ofisi za TRA zilizo karibu na maeneo yao nchi nzima wapate utaratibu wa kulipa kodi hiyo kielektroniki.
Kichere aliongeza kuwa Kodi ya Majengo inalipwa kwa mujibu wa Sheria hivyo, ni muhimu wananchi walipe mapema kodi hiyo ili kuepuka usumbufu unaoweza kujitokeza mwishoni ikiwa ni pamoja na msongamano wa watu.
“Natoa wito kwa wananchi kwamba, wasisubiri mpaka mwisho ndio waanze kupanga foleni kwenye ofisi za TRA, wanatakiwa kulipa kuanzia sasa hivi katika ofisi zetu na wanaweza kulipa kwa kutumia njia ya kielektroniki kama nilivyoeleza hapo awali, kinyume na hapo itatubidi tutoze faini kwa atakayechelewa kulipa kodi hii ya majengo,” alisisitiza Kichere.
Kodi ya Majengo hulipwa kuanzia mwezi Julai mosi ya mwaka wa fedha husika hadi Juni 30 ya mwaka unaofuatia kwa kufuata Sheria, kanuni na taratibu,  hivyo, muda huu ni muafaka kwa wananchi kuanza kulipia kodi ya majengo mpaka ifikapo tarehe 30 Juni, 2018.
NAIBU WAZIRI ANGELINA MABULA ASHUHUDIA UZINDUZI WA HUDUMA ZA KISASA KITUO CHA AFYA NYAMWAGA TARIME

NAIBU WAZIRI ANGELINA MABULA ASHUHUDIA UZINDUZI WA HUDUMA ZA KISASA KITUO CHA AFYA NYAMWAGA TARIME

February 25, 2018

????????????????????????????????????
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Angelina Mabula akilakiwa nawananchi wakati alipokwenda kushuhudia uzinduzi wa huduma za kisasa katika kituo cha Afya cha Nyamwaga kilichopo wilaya ya Tarime mkoa wa Mara wakati wa ziara yake mkoani humo mbali na mambo mengine kukagua mfumo wa ukusanyaji kodi ya ardhi na kukagua mpaka wa Tanzania na Kenya.
????????????????????????????????????
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Angelina Mabula akiangalia vifaa vilivyopo katika kituo cha afya cha Nyamwaga kilichopo wilaya ya Tarime mkoa wa Mara.
????????????????????????????????????
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Angelina Mabula akitoa nasaha wakati alipokwenda kushuhudia uzinduzi wa huduma za kisasa katika kituo cha Afya cha Nyamwaga kilichopo Wilaya ya Tarime mkoa wa Mara.
????????????????????????????????????
Baadhi ya wananchi wakisikiliza nasaha zilizokuwa zikitolewa na Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Angelina Mabula wakati wa uzinduzi wa kituo cha afya cha Nyamwaga kilichopo Tarime mkoa wa Mara.
????????????????????????????????????
Baadhi ya wananchi wakisikiliza nasaha zilizokuwa zikitolewa na Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Angelina Mabula wakati wa uzinduzi wa kituo cha afya cha Nyamwaga kilichopo Tarime mkoa wa Mara.
dawa
Sehemu ya majengo ya kituo cha Afya cha Nyamwaga kilichopo Tarime mkoa wa Mara
PICHA ZOTE NA WIZARA YA ARDHI NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI-WANMM
RAIS MHE.DKT JOHN POMBE MAGUFULI ASHIRIKI IBADA YA MISA TAKATIFU ILIYOFANYIKA KATIKA KANISA LA KIGANGO CHA MLIMANI (PAROKIA TEULE YA MLIMANI)LILILOPO WILAYANI CHATO GEITA.FEBRUARI 25,2018

RAIS MHE.DKT JOHN POMBE MAGUFULI ASHIRIKI IBADA YA MISA TAKATIFU ILIYOFANYIKA KATIKA KANISA LA KIGANGO CHA MLIMANI (PAROKIA TEULE YA MLIMANI)LILILOPO WILAYANI CHATO GEITA.FEBRUARI 25,2018

February 25, 2018

1 2
Rais Mhe.Dkt John Pombe Magufuli akishiriki Ibada ya misa Takatifu katika kanisa la kigango cha Mlimani (Parokia teule ya mlimani)lililopo Wilayani Chato Geita.Februari 25,2018.
4
Rais Mhe.Dkt John Pombe Magufuli akipiga makofi baada ya mahubiri kutoka kwa Padre Alex Bulandi wakati wa Ibada ya misa Takatifu katika kanisa la kigango cha Mlimani (Parokia teule ya mlimani)lililopo Wilayani Chato Geita.Februari 25,2018.
5 6 7
Rais Mhe.Dkt John Pombe Magufuli akiwasalimia waumini wa kanisa hilo mara baada ya kukaribishwa na Padre Alex Bulandi wakati wa Ibada ya misa Takatifu katika kanisa la kigango cha Mlimani (Parokia teule ya mlimani)lililopo Wilayani Chato Geita.Februari 25,2018.
8
Rais Mhe.Dkt John Pombe Magufuli akimshukuru Padre Alex Bulandi baada ya kusalimia wakati wa Ibada ya misa Takatifu iliyofanyika katika kanisa la kigango cha Mlimani (Parokia teule ya mlimani)lililopo Wilayani Chato Geita.Februari 25,2018.
10
Waziri wa Nishati ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Chato Mhe.Medradi Kalemani akiwasalimia waumini wa kanisa wakati wa Ibada ya misa Takatifu iliyofanyika katika kanisa la kigango cha Mlimani (Parokia teule ya mlimani)lililopo Wilayani Chato Geita.Februari 25,2018.
11
Rais Mhe.Dkt John Pombe Magufuli akiagana na Padre Alex Bulandi baada ya Ibada ya misa Takatifu iliyofanyika katika kanisa la kigango cha Mlimani (Parokia teule ya mlimani)lililopo Wilayani Chato Geita.Februari 25,2018.
13
Rais Mhe.Dkt John Pombe Magufuli akiagana na Waziri wa Nishati amabaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Chato Mhe.Medrad Kalemani mara baada ya Ibada ya misa Takatifu iliyofanyika katika kanisa la kigango cha Mlimani (Parokia teule ya mlimani)lililopo Wilayani Chato Geita.Februari 25,2018.
14
Rais Mhe.Dkt John Pombe Magufuli akiagana na Waziri wa Nishati amabaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Chato Mhe.Medrad Kalemani na viongozi wa kanisa hilo mara baada ya Ibada ya misa Takatifu iliyofanyika katika kanisa la kigango cha Mlimani (Parokia teule ya mlimani)lililopo Wilayani Chato Geita.Februari 25,2018.
PICHA NA IKULU.

DK.KAMANI AWAONYA VIONGOZI VYAMA VYA USHIRIKA NCHINI

February 25, 2018
Na Said Nwishehe,Globu ya Jamii

MWENYEKITI wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika,Dk.Titus Kamani amesema Serikali kupitia tume hiyo ni awaelekeza viongozi wa Vyama vya Ushirika kutojihusisha kuuza mali za vyama hivyo pasipo kuzingatia sheria.

Hivyo amesema hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi ya watakaobainika kuuza mali za vyama hivyo na kufafanua ili kudhibiti hali hiyo Ofisi za Mrajisi wa vyama vya ushirika imekuwa ikichukua hatua ikiwa pamoja na kuwaondoa viongozi wanaokiuka sheria.

Dk.Kamani amesema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati anaelezea udhibito wa mali za ushirika na mpango wa makusanyo na mauzo ya mazao makuu matano ya kimkakati kupitia mfumo wa ushirika.

Amesema vyama vya ushirika nchini vinaendeshwa kwa kuzingatia sheria ya vyama vya ushirika namba 6 ya mwaka 2013.Hivyo vyama vinapaswa kuzingatia sheria wanapotekeleza majukumu yao.Dk.Kamani amesema Serikali kupitia Tume ya Maendeleo ya Ushirika inaelekeza viongozi wa vyama hivyo kuwa makini kuzingatia sheria.

Amefafanua vyama vina haki ya kumiliki mali na kuuza mali hizo pale itakapoona inafaa kwa kuzingatia shetia iliyopo.Pia mali zinazomilikiwa na vyama zinapaswa kuwa zimerasimishwa ili kuleta uhalali wa umiliki.

Dk.Kamani amesema pamoja na uwepo wa taratibu za kisheria zinazoelekeza namna ya ununuzi ,uuzaji na urasimishaji wa mali zake,baadhi ya viongozi wa vyama wamekuwa hawazingatii na matokeo yake wamekuwa wakiingia kwenye migogoro na wanaushirika.

Amesema kutokana na uzito wa jambo hill la umiliki wa mali, mwaka 2016 akiwahutubia wananchi wa Jiji la Mwanza, Rais Dk.John Magufuli alieleza jinsi viongozi wa vyama vya Ushirika wanavyohujumu vyama na kujinufaisha.

Hivyo alitoa maelekezo yakiwamo ya kurejeshwa kwa mali zote za vyama vya vikuu vya Ushirika vya NCU (1984)Ltd na Shirecu (1984)Ltd zilizouzwa kinyemela ambapo kutokana na agizo hill hadi sasa kati ya mali za NCU ,7 tayari zimerejeshwa na kati ya mali 2 za Shorecu zote zimerejeshwa .

"Kwa dhati ya moyo wangu,nawashukuru na kuwapongeza viongozi wetu wakuu wa nchi kwa imani kubwa waliyonayo juu ya Ushirika kwa kuutetea na kuhakikisha unatumika kumkomboa mwananchi wa kipato cha chini," amesema Dk.Kamani.Amesema pia Serikali inawakumbusha wakurugenzi wa halmashauri za majiji ,manispaa ,wilaya na miji kuhakikisha vinakodi maghala kwa ajili ya kuhifadhi pamba.

Hiyo ikiwa ni maandalizi kwa vyama vya Ushirika katika msimu wa mwaka 2018/2019 kama yalivyo maelekezo ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.

DC TEMEKE AHIMIZA WAENDESHA BODABODA KUZINGATIA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI

February 25, 2018
Na Emmanuel ,Globu ya Jamii

MKUU wa Wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam, Felix Lyaniva amewataka madereva wa pikipiki na Bajaj kuwa makini na kuzingatia sheria za usalama barabarani ikiwemo kuvaa kofia ngumu na viatu wakati wanapoendesha vyombo vya moto.

Amesema lengo ni kuepuka ajali zinazosababishwa na madereva wazembe na kuwataka kufanya kazi kwa kuzingatia sheria zilizopo.

Lyaniva ameyasema hayo leo, wakati wa utambulishaji rasmi wa mfumo wa namba utakaowatambulisha madereva pikipiki na bajaji katika vituo vyao mbalimbali katika katika Kata ya Kibondemaji, Mbagala Jijini Dar es salaamu uliofadhiliwa na Diwani wa Kata hiyo Abdallah. 

Diwani huyo ameshirikiana na Kampuni ya Tanzania Motorcycle and Bajaji Association (TAMOBA) kwa ajili ya kuzisajili Pikipiki na Bajaji katika mfumo wa GPS utakaowawezesha kujua Pikipiki iliyoibiwa ipo eneo gani na kuweza kupatikana kwa haraka zaidi.

Akizungumza zaidi Lyaniva amewapiga marufuku mgambo wa wilaya hiyo kutokamata pikipiki na Bajaj kwani wengi wao wamekuwa wakikamata pikipiki hizo bila ya kuzingatia sheria.

Amesena kazi ya kukamata bodaboda itafanywa na askari wenye weledi na wenye kujua sheria za usalama barabarani.Lyaniva pia amewapongeza TAMOBA kwa kuwafikia madereva bodaboda na bajaj kwani walikuwa na wasiwasi wa kuibiwa vyombo vyao na kuporwa na majambazi.

Ameongeza Diwani huyo ameleta maendeleo makubwa na mazuri katika Kata hiyo na pia TAMOBA imeleta usalama mzuri kabisa wa kisasa kwa kuwa madereva hao watafanya kazi zao wakiwa hawana wasiwasi wa kuibiwa Pikipiki zao na mali zao wawapo katika majukumu yao hayo pamoja na abiria wao.

Naye Diwani wa Kata ya Kibondemaji, Abdallah Mtinika amewashukuru TAMOBA kwani wameweza kumpatia refrector 300 kwa ajili ya madereva pikipiki katika kata yake hiyo na kuahidi kushirikiana na Bodaboda hao wa Kata yake.

Kwa upande wake, Ofisa Utumishi wa TAMOBA Erasto Lahi amesema Kampuni hiyo ilianzishwa rasmi mwaka 2006 na lengo ni kuwalinda madereva wa pikipiki na Bajaj na vyombo vyao.

Hivyo ameahidi kila bodaboda atapata sare ili kutambulika pia kuingizwa katika mfumo wa utambulishi utakaowatambua na kueleza mfumo huo utasaidia kuokoa gharama za kulipia Bima kubwa kwa kuwa kipengele cha hofu ya usalama wa chombo chake kitafanyiwa kazi masaa 24 labda iwe kwa sababu zingine, mfumo huu unawahakikishia wamiliki kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi watakuwa salama.

“Kila atakayesajiliwa na Kampuni hii atasajiliwa na mfumo maalum wa GPS utakaowezesha kujua Pikipiki iliyoibiwa ipo wapi, inatumiwa na nani na kuwezesha kui-lock hapohapo ilipo."Mtu aliye katika mfumo huu atapata msaada wa kulindwa kwenye mfumo muda wote saa 24, hivyo mmiliki wa chombo muda wowote akihitaji taarifa za chombo kilipo, kilipopita na kinapoelekea atazipata," amesema.

Amesisitiza pia mfumo huu utaunganishwa na Jeshi la Polisi moja kwa moja ili kuharakisha zaidi huduma za kiusalama.

Awali akisoma risala mbele ya mgeni rasmi Katibu wa Bodaboda Kata hiyo ya Kibondemaji Hassan Habibu amemshukuru Diwani huyo ambae ni mlezi wao na kueleza changamoto wanazokutana nazo ni pamoja na baadhi ya askari shirikishi maarufu kama mgambo kuwakamata nyakati za usiku bila utaratibu wa kisheria na kuwapiga kwa kutumia magongo bila ya kujua makosa yao.

Pia kutopata mikataba ya uhakika kutoka kwa wamiliki wa pikipiki hizo wanazoziendesha.


Mkuu wa Wilaya ya Temeke Mhe Felix Lyaniva akizungumza na madereva wa pikipiki na Bajaj juu ya kuzingatia sheria za usalama Barabarani ikiwemo kuvaa kofia ngumu na viatu wakati wanapoendesha vyombo vya moto,leo jijini Dar es Salaam.(picha na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii)
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es Salaam Kate Sylivia Magdalena Kamba akizungumza na akizungumza na madereva wa pikipiki na Bajaj juu ya kufanya kazi kwa kuzingatia sheria zilizopo, leo jijini Dar es Salaam.

Afisa Utumishi wa TAMOBA Bw. Erasto Lahi akizungumza na madereva wa pikipiki na Bajaj juu ya kuzisajili Pikipiki na Bajaj katika mfumo wa GPS utakaowawezesha kujua Pikipiki iliyoibiwa ipo eneo gani na kuweza kupatikana kwa haraka zaidi, le,jijini Dar es Salaam.
Semu ya madereva wa pikipiki na Bajaj piki na Bajaj wakiwa kwenye mkutano utambulishaji rasmi wa mfumo wa namba utakaowatambulisha madereva pikipiki na bajaji katika vituo vyao mbalimbali vya Kata ya Kibondemaji, Mbagala Jijini Dar es salaamu.

BENKI YA CRDB YADHAMINI MKUTANO MKUU WA GS1

February 25, 2018
 Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Tully Mwambapa (wa pili kulia), akishiriki maandamano ya washiriki wa Mkutano Mkuu wa Taasisi ya GS1 jijini Dar es Salaam. Maandamano yakielekea ukumbini. 
 Brass Band ikiongoza maandamano hayo. 
Mwenyekiti wa Bodi ya GS1 Tanzania, Gideon Mazara (wa kwanza kulia), akiwashiriki maandamano wakati wa kuingia ukumbini katika Mkutano Mkuu wa Mwakwa wa taasisi hiyo.
Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Fedha wa Benki ya CRDB, Frederick Nshakanabo, Mkurugenzi wa Huduma Mbadala wa Benki ya CRDB, Philip Alfred na Msaidizi wa Mkurugezi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Kenny Kasigila.
 Maandamano kuelekea katika ukumbi wa mikutano. 
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa (katikati), akipokea maandamano ya washiriki wa mkutano wa GS1. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akimkabidhi cheti cha shukrani Mkurugenzi Mtendaji wa Benki wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei, kwa kutambua udhamini wa benki ya CRDB katika Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Global Standard (GS1), taasisi hiyo inajishughulisha na uwekaji wa Barcodes katika bidhaa za kitanzania ili ziweze kukubalika katika soko la kimataifa na pia kuwa mdau wa kufanikisha sekta ya viwanda nchi mkutano huo ulifanyika jijini Dar es Salaam. Katikati ni Mwenyekiti wa Bodi ya GS1 Tanzania, Gideon Mazara.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei,akizungumza katika Mkutano wa Mkuu wa Taasisi ya GS1 ambao ni watumiaji wa Simbomilia (Barcodes).
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei (kushoto), akiwa na baadhi ya watendaji wa benki hiyo katika mkutano wa Mwaka wa taasisi ya GS1.
Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa Wateja wa Benmki ya CRDB, Tully Mwambapa akiteta jambo na Mkurugenzi wa Fedha wa Benki hiyo, Frederick Nshakanabo, katika mkutano huo. 
Mkutano ukiendelea.
Washiriki wa mkutano huo.