WAZIRI MUKANGARA AWAFUNDA MAAFISA MAWASILIANO SERIKALI
NAIBU KATIBU MKUU WA WIZARA YA HABARI VIJANA,UTAMADUNI NA MICHEZO PROF.ELISANTE OLE GABRIEL AKIZUNGUMZA KWENYE KIKAO HICHO KABLA YA KUMKARIBISHA WAZIRI |
Na Oscar Assenga,Tanga.
WAZIRI wa Habari,Vijana ,Utamaduni na Michezo Dokta Fenella Mukangara ametoa wito
kwa Maafisa Mawasiliano wa Serikali kwenye wizara, Idara na Taasisi za serikali kuendelea kujifunza kwa weledi mambo mbalimbali yatakayosaidia kuleta tija katika kutekeleza majukumu yao ya kusimamia mawasiliano kwenye maeneo yao ya kazi.
Mukangara ametoa wito huo jana wakati wakifungua kikao cha kazi cha maafisa mawasiliano kutoka maeneo mbalimbali hapa nchini kilichofanyika kwenye ukumbi wa Hotel ya Tanga Beach Resort Mkoani Tanga.
Amesema maafisa hao wamepewa jukumu kubwa la kuiwezesha serikali kuipitia ofisi zao kufanya mawasiliano na umma kupitia vyombo vya
habari kuhusu masuala mbalimbali yanayohusu sera na miradi inayotekelezwa na serikali yenye lengo la kustawisha maendeleo kwa watanzania.
WAZIRI MUKANGARA AFUNGUA KIKAO CHA KAZI CHA MAAFISA HABARI NA MAWASILIANO HOTEL YA TANGA BEACH RESORT JANA.
NAIBU KATIBU MKUU WA WIZARA YA HABARI VIJANA,UTAMADUNI NA MICHEZO PROF.ELISANTE OLE GABRIEL AKIZUNGUMZA KWENYE KIKAO HICHO KABLA YA KUMKARIBISHA WAZIRI |
MKURUGENZI WA IDARA HABARI NA MAELEZO ASSAH MWAMBENE KUSHOTO AKITETE JAMBO NA WAZIRI MUKANGARA BAADA YA KUFUNGUA KIKAO HICHO JANA |
BAADHI YA WASHIRIKI KWENYE KIKAO HICHO CHA MAAFISA HABARI NA MAWASILIANO |
LIVE,MH:MWIGULU NCHEMBA AKUTANA NAWAFANYABIASHARA TUNDUMA MJINI
Naibu
waziri wa Fedha Mh;Mwigulu Nchemba akisisitiza jambo kwa
Wafanyabiashara wa Mji wa Tunduma hii leo alipokutana nao kwenye Mkutano
wa ndani kwenye Ukumbi wa High Class One akizungumza nao kuhusu
Maendeleo ya Biashara,Ulipaji wa kodi,Changamoto za Mpakani kwenye
Ulipaji kodi,matumizi ya Mashine za EFD kwenye makato ya TRA.
Sehemu
ya Mamia ya Wafanyabiashara waliohudhuria Mkutano wa Naibu Waziri wa
Fedha Mh;Mwigulu Nchemba wa Kujadiliana na kuelezana namna ya Kuimarisha
Ukusanyaji wa mapato nchini.
Naibu
Waziri wa Fedha Mh:Mwigulu Lameck Nchemba hii leo ameendelea na Ziara
yake ya kikazi ya Kukutana na Wafanyabiashara ndnai ya Mkoa wa Mbeya
baada ya Kufanya hivyo kwenye Mkoa wa Njombe na Ruvuma wiki iliyopita.
Hii
leo Mh:Mwigulu amezungumza na mamia ya wafanyabiashara wa Mji wa
Tunduma kuhusu nafasi yao ya Kukuza Ukusanyaji wa mapato kwa kaucha
kukwepa kulipa kodi,Kuacha kupitisha bidhaa kimagendo kwenye mpaka wa
Nchi ya Tanzania na Zambia.
Wafanyabiashara Wakitanzania wasio wazalendo
wa Kulipa kodi wamekuwa wakitumia mwanya wa Mpaka kuvuka kufanya
biashara Zambia na makazi yao yapo Tanzania kitu kinachopelekea
ukusanyaji wa Mapato kuwa Mgumu kwa TRA na taasisi husika.
Serikali
imeamua kufanya maridhiano na Serikali ya Zambia kuhakikisha kunakuwepo
na Mpaka uliotenganishwa kwa Mita 50 kila upande wa Nchi hizi mbili
ilikudhibiti ukwepaji wa kulipa kodi na biashara ya Magendo.
Naibu
waziri pia alitumia nafasi kuwaelimisha Wafanyabiashara umuhimu wa
kutumia mashine za EFD kwenye kurahizisha ukusanyaji wa mapato na kukuza
biashara zao.
Mbali na hayo wafanyabiashara walipata nafasi ya kutoa
mawazo,maoni yao kwa
Naibu waziri wa Fedha namna ya Kuimarisha
Ukusanyaji wa mapato,Uelewa wao kuhusu Mashine za EFD na Ushirikiano
watakao onesha kwenye Kudhibiti ukusanyaji mapato mpakani Mwatanzania na
Zambia.
Picha na Habari Kwanza Blog
SIKU YA SHERIA DUNIANI YAFANYIKA MKOANI DODOMA, WALIA NA UPUNGUFU WA MAJAJI.
Wakili wa Serekali Mfawidhi mkoa wa Dodoma, Angaza
Mwaipopo akifafanua jambo wakati wa sherehe ya siku ya sheria mjini Dodoma leo.
Jaji Mfawidhi wa mahakama kuu kanda ya Dodoma, Crecensia
Makuru akizangumza jambo mbele ya watendaji na wadau wa mahakama wakati
sherehe za siku ya Sheria zilizofanyika leo.
Wakili wa kujitegemea Mary Munissi wa mkoani Dodoma
akielezea jambo wakati wa maadhimisho ya siku ya sheria yaliyofanyika
leo
Mahakimu, Mawakili na watendaji wengine wa
mahakama wakifuatila jambo walipokuwa kwenye maadhimisho ya siku ya
sheria yaliyofanyika leo Dodoma.
Jaji
Mfawidhi wa Mahakama kuu kanda ya Dodoma akizungumza
jambo na Kaimu mkuu wa mkoa wa Dodoma ambaye pia ni mkuu wa mkoa wa
Singida, Mh. Pasiseko Konne mara baada ya kumalizika shughuli za
maadhimisho
ya siku ya sheria leo.
UCHELEWESHWAJI wa kesi nyingi mahakamani katika mahakama ya kanda ya Dodoma kunasababishwa na upungufu mkubwa wa majaji.
Hayo yalisemwa na Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma,
Crecencia Makuru leo mjini humo wakati wa maadhimisho ya siku ya sheria nchini yaliyofanyika katika viwanja vya mahakama kuu.
Alisema kuna upungufu mkubwa wa majaji ambao haulingani na
kesi zilizopo hali inayosabisha kuzolotatesha mienendo ya kesi mbalimbali.
Crecencia alisema majaji katika kanda ya Dodoma ni wachache kulingana na kesi zilizopo ambapo hadi kufikia Desemba 31, 2013 kulikuwa na jumla ya mashauri na 1364 na kuna majaji wawili tu.
*MAMIA WAMZIKA MEJA MSTAAFU SAMWEL ISAAC CHEKINGO KWENYE MAKABURI YA KINONDONI DAR
Askari
wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wakibeba mwili wa marehemu Meja
Mstaafu Samwel Isaac Chekingo mara baada ya kuwasili nyumbani kwake
Kinondoni kwa ajili ya ibada maalum.
Marafiki
wa karibu wa familia ya marehemu wakiwa wamesimama kuupoke mwili wa
marehemu Meja Mstaafu Isaac Chekingo ulipowasili nyumbani kwake
Kinondoni jijini Dar mwishoni mwa Juma.
Mtoto
mkubwa wa marehemu (mwenye koti la suti jeusi) akijadiliana jambo na
baadhi ya wanakamati wa msiba ulioongozwa na Afande Thomas Ndonde wa
JWTZ.
RAIS KIKWETE ATEMBELEA KUKAGUA MAJENGO YA BUNGE DODOMA KUELEKEA BUNGE LA KATIBA
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akikagua sehemu ya Siti za kukaa ndani ya ukumbi
wa Bunge mjijini Dodoma wakati alipotembelea na kukagua kampuni
inayokarabati na kufanya marekebisho kwa ajili ya kupokea wajumbe wa
Bunge la katiba linalotarajia kuanza baadaye mwezi huu.
Rais Jakaya Kikwete, akijaribu kipaza sauti katika moja ya siti za ukumbi huo.
Muonekano wa siti za ukumbini humo baada ya marekebisho...
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akitembezwa sehemu mbalimbali za majengo ya Bunge
mjijini Dodoma alipotembelea kukagua maendeleo ya ukarabati na
marekebisho ya ukumbi wa Bunge kujiandaa na Bunge la Katiba marekebisho
tayari kwa kupokea wajumbe wa Bunge la katiba baadaye mwezi huu.
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa
kampuni ya ujenzi inayokarabati na kufanyia marekebisho ukumbi wa bunge
mjini Dodoma tayari kwa kupokea wajumbe wa Bunge la katiba baadaye mwezi
huu.
MSHABIKI MBARONI KWA MADAI YA TIKETI FEKI
Release No. 018
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Februari 3, 2014
Mshabiki
mmoja anashikiliwa na Jeshi la Polisi akidaiwa kukutwa na tiketi bandia kwenye
mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kati ya Yanga na Simba iliyochezwa jana
(Februari 2 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Matei
Cosmas (28) ambaye ni mkazi wa Buza Njiapanda Kitunda, Dar es Salaam
amefunguliwa jalada namba CHA/IR/900/2014 kwenye Kituo cha Polisi Chang’ombe
akidaiwa kupatikana na tiketi bandia.
Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) leo asubuhi (Februari 3 mwaka huu) limeamkia
Kituo cha Polisi Chang’ombe kusaini hati ya maelezo dhidi ya mtuhumiwa.
Ni
imani ya Shirikisho kuwa mtuhumiwa atachukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria za
nchini.
Tunatoa
mwito kwa washabiki wa mpira wa miguu kuepuka kununua tiketi kutoka mikononi
mwa watu, kwani kufanya hivyo ni kosa. Tiketi zinauzwa kwenye sehemu maalumu
zenye chapa ya TFF.
RAIS WA TFF
ATEMBELEA RUANGWA
Rais
wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi ametembelea Chama
cha Mpira wa Miguu Wilaya ya Ruangwa mkoani Lindi.
Katika
ziara hiyo aliyoifanya jana (Februari 2 mwaka huu), pia alikuwa mgeni rasmi
mechi ya kugombea Kombe la Majaliwa kati ya Hull City na Mbagala City, na
kuahidi kuwa TFF itaandaa kozi za awali za ukocha na uamuzi kwa Wilaya ya
Ruangwa.
RAMBIRAMBI MSIBA
WA OMARI CHANGA
Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limepokea kwa masikitiko kifo cha aliyekuwa
mchezaji wa Vijana, Moro United na Yanga, Omari Changa kilichotokea juzi (Februari
1 mwaka huu) jijini Dar es Salaam.
Msiba
huo ni mkubwa katika familia ya mpira wa miguu kwani Changa wakati wake
uwanjani akichezea timu mbalimbali alitoa mchango mkubwa ambao tutaukumbuka
daima.
TFF
tunatoa pole kwa familia ya marehemu Changa, klabu ya Moro United na Chama cha
Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) na kuwataka kuwa na subira na
uvumilivu katika kipindi hiki kigumu cha msiba huo mzito.
Katika
maziko TFF itawakilishwa na mjumbe wa Kamati ya Utendaji, Kidao Wilfred, na
imetoa rambirambi ya sh. 200,000.
Boniface Wambura Mgoyo
Ofisa Habari na Mawasiliano
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
Release No. 017
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Februari 3, 2014
TFF
YAADHIMISHA MIAKA 50 FIFA
Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) litaadhimisha miaka 50 tangu lipate uanachama
wa Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (TFF) kwa shughuli mbalimbili
ikiwemo michezo na makongamano.
Kamati
maalumu itaundwa kwa ajili ya kupanga na kuratibu shughuli hiyo ambayo TFF
imepanga kuadhimisha nchini nzima kwa kutumia wanachama wake.
TFF
wakati huo ikiitwa Chama cha Mpira wa Miguu Tanzania (FAT) ilijiunga na FIFA
Oktoba 8, 1964.
PAMBANO LA
YANGA, MBEYA CITY LAINGIZA MIL 175
Pambano
la Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kati ya wenyeji Yanga na Mbeya City lililofanyika
jana (Februari 2 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam limeingiza sh.
175,285,000.
Watazamaji
30,411 walikata tiketi kushuhudia mechi hiyo kwa viingilio sh. 5,000, sh.
15,000 na sh. 20,000 kwa VIP A. Yanga ndiyo iliyoibuka na ushindi wa bao 1-0.
Mgawanyo
wa mapato ulikuwa Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) sh. 26,738,389.83, gharama
za kuchapa tiketi sh. 2,919,200 wakati kila klabu ilipata sh. 42,960,086.50.
Uwanja
sh. 21,844,111.53, gharama za mechi sh. 13,106,466.92, Bodi ya Ligi sh. 13,106,466.92,
Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 6,553,233.46 na Chama cha Mpira
wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 5,096,959.36.
Nayo
mechi ya Simba na Oljoro JKT iliyochezwa Februari 1 mwaka huu kwenye Uwanja wa
Taifa, Dar es Salaam imeingiza sh. 47,705,000 ambapo kila timu imepata sh.
11,254,122 kutokana na watazamaji 8,267.
Mgawanyo
mwingine katika mechi hiyo iliyomalizika kwa Simba kushinda mabao 4-0 ni Kodi
ya Ongezeko la Thamani (VAT) sh. 7,277,033.90 na gharama za kuchapa tiketi sh.
2,278,400.
Uwanja
sh. 5,722,434.92, gharama za mechi sh. 3,433,460.95, Bodi ya Ligi sh. 3,433,460.95,
Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 1,716,730.47 na Chama cha Mpira
wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 1,335,234.81.
TFF YAPATA
HATI YA KIWANJA TANGA
Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limepata hati ya kiwanja chake kilichopo eneo
la Mnyanjani katika Jiji la Tanga.
Hati
hiyo ya miaka 99 ya kiwanja hicho namba 75 Block D chenye ukubwa wa ekari 7.6
ilikabidhiwa kwa TFF, Januari 13 mwaka huu.
Kiwanja
hicho kitaendelezwa kwa matumizi mbalimbali, kubwa ikiwa ni uwanja wa mpira wa
miguu.
Boniface Wambura Mgoyo
Ofisa Habari na Mawasiliano
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
Subscribe to:
Posts (Atom)