Na Mahmoud Zubeiry, Mlandizi
AZAM FC imeibwaga mabao 3-0 timu ya Ruvu Shooting kwenye Uwanja wake wa Mabatini, Mlandizi mkoani Pwani katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara jioni hii.
Ushindi huo unaisogeza karibu kabisa na ubingwa wa Ligi Kuu Azam FC kwa kufikisha pointi 56 baada ya kucheza mechi 24, ikifuatia na mabingwa watetezi, Yanga SC wenye pointi 52 za mechi 24 pia.
Azam FC ilikwenda kupumzika ikiwa inaongoza mabao 2-0 yaliyotiwa kimiani na Gaudence Mwaikimba dakika ya tisa na Himid Mao dakika ya 36, wote wakimalizia kona za Erasto Nyoni.

Mfungaji wa bao la tatu la Azam FC, Kipre Tchetche akishangilia baada ya kufunga |