LAPF WATOA REFLECTOR JACKET 500 KUSAIDIA BODA BODA WILAYANI KISARAWE MKOANI PWANI

March 19, 2017
 Muonekano wa jengo la mikutano la Halmashauri ya 
Wilaya ya Kisarawe.

 Meneja Masoko na Mawasiliano wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF, James Mlowe (wa pili kulia), akimkabidhi moja ya jaketi angavu (Reflector Jacket) kati ya majaketi 500 Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Happyness Seneda katika hafla iliyofanyika wilayani humo jana. LAPF imetoa majaketi hayo kwa ajili ya kusaidia waendesha bodaboda ili waweze kutambulika wakiwa katika shughuli zao za kila siku.Kutoka kushoto ni Meneja wa Mfumo wa Uchangiaji wa Hiari wa LAPF, Hanim Babiker, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe, William Gama na Meneja wa LAPF, Kanda ya Mashariki,  Lulyalya Sayi. 
 Waendesha boda boda wa Wilaya ya Kisarawe wakiwa kwenye mkutano huo.

MAKADA WA CCM WACHUKUA FOMU KUWANIA NAFASI YA UBUNGE, BUNGE LA AFRIKA MASHARIKI.

March 19, 2017


 Katibu Msaidizi Idara ya Organizeshen CCM Ofisi ndogo Dar es Salaam, Said Bakari Is-hak (kulia) akimkabidhi fomu za kugombea nafasi ya Ubunge, Bunge la Afrika Mashariki, Kada wa CCM, Daktari Bingwa wa magonjwa ya ndani, Dkt. Egina Makwabe, wakati wagombea hao walipofika kuchukua fomu hizo kwenye Ofisi ndogo za CCM zilizopo Lumumba jijinin Dar es Salaam, leo. 
 Katibu Msaidizi Idara ya Organizeshen CCM Ofisi ndogo Dar es Salaam, Said Bakari Is-hak (kulia) akimkabidhi fomu za kugombea nafasi ya Ubunge, Bunge la Afrika Mashariki, Kada wa CCM, Leonce Nicholaus Mulenda, wakati wagombea hao walipofika kuchukua fomu hizo kwenye Ofisi ndogo za CCM zilizopo Lumumba jijinin Dar es Salaam, leo. 
 Katibu Msaidizi Idara ya Organizeshen CCM Ofisi ndogo Dar es Salaam, Said Bakari Is-hak (kulia) akimkabidhi fomu za kugombea nafasi ya Ubunge, Bunge la Afrika Mashariki, Kada wa CCM, Zainab Kawawa, wakati wagombea hao walipofika kuchukua fomu hizo kwenye Ofisi ndogo za CCM zilizopo Lumumba jijinin Dar es Salaam, jana. Katikati ni dada zake Mariam Kawawa na Zamaradi Kawawa.  Picha na Mafoto Blog
 Katibu Msaidizi Idara ya Organizeshen CCM Ofisi ndogo Dar es Salaam, Said Bakari Is-hak (kulia) akimkabidhi fomu za kugombea nafasi ya Ubunge, Bunge la Afrika Mashariki, Kada wa CCM, anayetetea nafasi yake, Charles Makongoro Nyerere, wakati wagombea hao walipofika kuchukua fomu hizo kwenye Ofisi ndogo za CCM zilizopo Lumumba jijinin Dar es Salaam.
 Katibu Msaidizi Idara ya Organizeshen CCM Ofisi ndogo Dar es Salaam, Said Bakari Is-hak (kulia) akimkabidhi fomu za kugombea nafasi ya Ubunge, Bunge la Afrika Mashariki, Kada wa CCM, Dkt. Evance Mujuni Rweikiza, wakati wagombea hao walipofika kuchukua fomu hizo kwenye Ofisi ndogo za CCM zilizopo Lumumba jijinin Dar es Salaam.
 Katibu Msaidizi Idara ya Organizeshen CCM Ofisi ndogo Dar es Salaam, Said Bakari Is-hak (kulia) akimkabidhi fomu za kugombea nafasi ya Ubunge, Bunge la Afrika Mashariki, Kada wa CCM, Shedrack Mana Mashauri, wakati wagombea hao walipofika kuchukua fomu hizo kwenye Ofisi ndogo za CCM zilizopo Lumumba jijinin Dar es Salaam.
 Aliyewahi kuwa Miss Tanzania wa mwaka 1998, Kada wa CCM, Basila Kalabha Mwanukuzi akiongozana na mtoto wake, Patrick Nubi, wakitoka Ofisi ndogo za CCM Lumumba, jijini Dar es Salaam, kuchukua Fomu za kuwania nafasi ya Ubunge Bunge la Afrika Mashariki. Baadhi ya Makada wa CCM jana walijitokeza katika Ofisi hizo kuchukua Fomu baada ya kutangazwa kuanza kutolewa fomu hizo. 
 Wagombea wakipishana kuingia kuchukua fomu kwenye Ofisi hizo Lumumba jijini Dar leo.
 Baadhi ya Vijana waliojitokeza kuchukua fomu kuwania nafasi hiyo wakiwa katika foleni ya kuiingia kuchukua fomu.

MD KAYOMBO AKAGUA UKARABATI WA BARABARA YA SIMU 2000

March 19, 2017

Trekta ambalo linafanya kazi ya kukarabari barabara ya Simu 2000
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo akikagua barabara ya simu 2000 ambayo ipo kwenye matengenezo ya dharura
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo akielekeza jambo kuhusu ukarabati wa barabara hiyo, Wengine ni Meneja wa stendi ya Simu 2000 Bakari Shehoza na Injinia wa Ujenzi katika Manispaa ya Ubungo Ndg Goodluck Mbanga
MD Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo akisisitiza jambo