TAARIFA KWA UMMA KUJERUHIWA KWA WANAHABARI NGORONGORO

August 15, 2023

 


SERIKALI KUTUMIA HELIKOPTA KUWAONDOA TEMBO NACHINGWEA LINDI

August 15, 2023




Dr Emmanuel Masenga mtafiti Mkuu TAWIRI akitoa maelezo Kwa viongozi mbalimbali akiwepo mkuu wa wilaya ya Nachingwea Mohamed Hassan Moyo na kamishna mwandamizi na kamanda wa uhifadhi Kanda ya kusini mashariki TAWA Abraham Jullu namna ambavyo watatumia Helikopta kuwarudisha Tembo hifadhini

Wa kwanza kushoto ni Dr Emmanuel Masenga mtafiti Mkuu TAWIRI anayefaata ni mkuu wa wilaya ya Nachingwea Mohamed Hassan Moyo wakiwa pamoja na katibu wa mbunge wa jimbo la Nachingwea George Martin pamoja na kamishna mwandamizi na kamanda wa uhifadhi Kanda ya kusini mashariki TAWA Abraham Jullu wakati wa zoezi la kuwaondoa Tembo kwenye mazi ya watu na kuwarudisha hifadhini kwa njia ya helikopta katika wilaya ya Nachingwea mkoa Lindi

Mkuu wa wilaya ya Nachingwea Mohamed Hassan Moyo akiwa amepanda Helikopta Kwa ajili ya uzinduzi wa zoezi la kuwarudisha Tembo hifadhini kutoka kwenye makazi ya wananchi.



Na Fredy Mgunda, Nachingwea.

Serikali kupitia Wizara ya maliasili na utalii kwa kushirikiana na Taasisi zake ambazo ni TAWA, TAWIRI NA TFS imeendelea na kutekeleza mkakati wa kuhakikisha changamoto ya Tembo Mkoani Lindi inamalizika.

Akizungumza mara baada ya kushuka kutoka kwenye Helikopta,Mkuu wa wilaya ya Nachingwea Mohamed Hassan Moyo alisema serikali ya Dkt. Samia Suluhu Hassan inaendelea kuchukua hatua za kuhakikisha wananchi wanaishi kwa amani na utulivu huku shughuli za kiuchumi zikiendelea bila matatizo yoyote yale.

Moyo alisema kuwa Tembo wamekuwa wakiharibu mazao ya wananchi na kusababisha vifo mara kadhaa hivyo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr Samia suluhu Hassan akaamua kutuma timu ya wataalam kutoka TAWA, TAWIRI na TFS kushughulikia suala la kuwaondoa Tembo kwenye makazi ya wananchi wa wilaya ya Nachingwea mkoani Lindi.

Alisema kuwa Rais Dr Samia suluhu Hassan ameona imekuwa kero kubwa kwa wananchi hivyo serikali imeanzisha mpango madhubuti wa kutoa mafunzo ya kukabiliana na Tembo kwa vijana wanaotoka katika vijiji ambavyo vinasumbuliwa na Tembo.

Moyo alimazia kwa kusema kuwa ni kweli watu wawili wameuwawa na Tembo na serikali imeanza kuchua hatua za haraka kuwafukuza Tembo Kwa njia ya Helikopta.

Kwa upande wake Kamaishna Mwandamizi na ni kamanda wa uhifadhi Kanda ya kusini mashariki TAWA Abraham Jullu alisema kuwa Tembo wapo jirani na makazi ya watu hivyo jukumu lao ni kuhakikisha wanawarudisha Tembo hifadhini ili wasilete madhara kwa binadamu.


Kamanda Jullu alisema kuwa ni jukumu la kila mwananchi kujilinda na mnyama Tembo ili kuokoa maisha yao kabla serikali haijachua hatua za kuwaondoa Tembo hao.

Naye Dkt. Emmanuel Masenga mtafiti Mkuu TAWIRI alisema kuwa Tembo wamekuwa wanafuata maji katika mto Mbwemkuru hivyo inakuwa rahisi Tembo kuvuka mto huo na kwenda kwenye mashamba na makazi ya wananchi waliojirani na mto Mbwemkuru.


Dkt Masenga alisema kuwa wanaendelea kutafuta njia mbalimbali za kuwazuia Tembo kwenda kwenye makazi ya wananchi na kuwaomba wananchi waendelea kujilinda kutokana na elimu waliyopewa na wataalam mbalimbali wa wanyama pori.

Salma Kingwande ni mwananchi wa Kijiji cha Narung’ombe alisema kuwa anamshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr Samia suluhu Hassan kwa kupeleka chopa kuwafukuza Tembo kwenye makazi ya wananchi kwa kuwa wamekuwa wakileta maafa ya vifo na kuharibu mazao ya wananchi

TUNATAKA KUWA NA MIFUMO MICHACHE YA TAARIFA ZA AFYA INAYOWASILIANA; DKT. SHEKALAGHE

TUNATAKA KUWA NA MIFUMO MICHACHE YA TAARIFA ZA AFYA INAYOWASILIANA; DKT. SHEKALAGHE

August 15, 2023

 

Na WAF, Dodoma.

Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Seif Shekalaghe amewataka wataalam wa TEHAMA kufanyia kazi mifumo ya taarifa ya Wizara ili iweze kuwasiliana na kuwa na mifumo michache yenye kuleta tija na kurahisisha utoaji wa huduma.

Dkt. Shekalaghe amesema hayo alipokuwa akifungua kituo cha umahiri katika masuala ya afya kidigitali Jijini Dodoma.

“Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan aliagiza kuanza kwa matumizi ya tiba mtandao lakini pia ameelekeza kwamba lazima mifumo yetu ipungue, ninafurahi siku ya leo ni moja ya hatua ya utekelezaji wa maelekezo ya Mhe. Rais. Wataalam wetu wakikaa hapa wataweza kuja na suluhisho la changamoto za mifumo iliyopo na kuwa na mifumo michache yenye tija” amesema Dkt. Shekalaghe


Amesema, kituo hicho cha umahiri katika masuala ya kidigitali (CDH) kitasaidia kuunganisha mifumo ya Sekta ya Afya pamoja na kupunguza mifumo iliyopo katika Wizara ya Afya.

“Kituo hiki kitasaidia kupungua kwa mifumo mingi ambayo haitazidi mifumo Minne au Mitano lakini pia kuwezesha kuunganisha mifumo iliyopo kwa kuweza kusomana ndani ya Wizara ya Afya”, amesema Dkt. Shekalaghe

Vile vile, Dkt. Shekalaghe amesema kuwa taarifa zinazotolewa na kituo hicho ziweze kutumika kwa ajili ya tafiti zitakazotuwezesha kufanya maamuzi mazuri zaidi.

“Tunataka kuwa na taarifa zote kamilifu na muhimu zinazosaidia utoaji wa huduma za matibabu, mtu ukifika hospitalini taarifa zako kuanzia mapokezi, vipimo na matibabu ziweze kuingizwa na kutunzwa kwenye mifumo yetu hii na iweze kuzungumza na kwa kuanzia tayari tunayo AFYA CARE, ambayo ipo tayari kwenye hospitali ngazi ya Mikoa kwenda juu, na GOTHOMIS ambayo inatumika kweney vituo vya kutolea huduma za afya ngazi ya msingi” amesema Dkt. Shekalaghe.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Kimataifa la PATH Bw. Amos Mugisha amesema wamewezesha kukarabati wa kituo hicho, kuweka samani pamoja na vifaa vya kiteknolojia.

Amesema, moja ya umuhimu wa kituo hicho ni kuweza kutengeneza mifumo ambayo inazungumza na kupunguza mifumo mingi iliyopo katika Sekta ya Afya kwa sasa.

Naye, Kaimu Mkurugenzi wa TEHAMA Wizara ya Afya Bw. Silvanus Ilomo amesema kuwa kituo hicho kitatumiwa siyo tu na Wizara ya Afya bali wataalam wengine wa Sekta ya Afya kwa ajili ya kukutana na kuja na mifumo yenye tija katika uboreshaji wa huduma za afya nchini.

“Kituo hiki ni mali ya Serikali, wataalam wote wa Sekta mnakaribishwa kuja kufanya kazi hapa kwa kuwa hii ni Serikali moja na haya ni mafanikio ya Serikali hii”, amesema Bw. Ilimo.    


RAIS DKT. SAMIA SULUHU HASSAN AZINDUA KANISA LA ANGLICAN DAYOSISI YA KATI DODOMA

RAIS DKT. SAMIA SULUHU HASSAN AZINDUA KANISA LA ANGLICAN DAYOSISI YA KATI DODOMA

August 15, 2023




Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akivuta utepe pamoja na Askofu wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Central Tanganyika (DCT) Dkt. Dickson Chilongani kuashiria ufunguzi Rasmi wa Jengo la Kitega Uchumi (Safina House) la Kanisa hilo kwenye Sherehe zilizofanyika katika viwanja vya Kanisa Kuu la Roho Mtakatifu Jijini Dodoma tarehe 15 Agosti, 2023. Wengine katika picha ni Mkuu wa Kanisa la Anglikana Tanzania Mhashamu Dkt. Maimbo Mndolwa pamoja na Maaskofu wengine wa Kanisa hilo nchini.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa pamoja na Maaskofu wa Kanisa la Anglikana Tanzania wakati akikata utepe kuashiria ufunguzi Rasmi wa Jengo la Kitega Uchumi (Safina House) la Kanisa hilo kwenye Sherehe zilizofanyika katika viwanja vya Kanisa Kuu la Roho Mtakatifu Jijini Dodoma tarehe 15 Agosti, 2023.
Muonekano wa Jengo la Kitega Uchumi (Safina House) la Kanisa la Anglikana Tanzania, Dayosisi ya Central Tanganyika ambalo limefunguliwa Rasmi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwenye hafla iliyofanyika katika viwanja vya Kanisa Kuu la Roho Mtakatifu tarehe 15 Agosti, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akicheza pamoja na waimbaji wa Kwaya ya Safina wakati wa Sherehe za ufunguzi wa Jengo la Kitega Uchumi (Safina House) la Kanisa hilo lililopo katika viwanja vya Kanisa Kuu la Roho Mtakatifu Jijini Dodoma tarehe 15 Agosti, 2023.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Askofu wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Central Tanganyika (DCT) Dkt. Dickson Chilongani wakati wa Sherehe za ufunguzi wa Jengo la Kitega Uchumi (Safina House) la Kanisa hilo lililopo katika viwanja vya Kanisa Kuu la Roho Mtakatifu Jijini Dodoma tarehe 15 Agosti, 2023.

WASANII IRINGA WATAKIWA KUCHANGAMKIA FURSA

August 15, 2023

 NA DENIS MLOWE, IRINGA


KAIMU Katibu Tawala Msaidizi Viwanda na Bishara, Asifiwe Mwakibete amewataka wasanii wa mkoani Iringa kuichangamkia fursa za mkopo kwa wasanii inayotolewa na Serikali kupitia fedha za Mfuko wa Sanaa.

Akizungumza hivi karibuni alipokuwa mgeni rasmi Katika semina juu ya Mikopo kwa wasanii, Mwakibete alisema kuwa wasanii mkoani hapa wahakikishe wakifanikiwa kupata wanatumia fedha za mfuko huo kuinua sanaa na kazi zao kwa ujumla ziwe kwenye ubora unaotakiwa.

Alisema kuwa kupitia fedha hizo waongeze ubunifu ili kujiweka katika mazingira ya kupata soko la uhakika ndani na nje ya nchi.

Mwakibete amewataka wasanii watakaonufaika na mpango huo kuwa waaminifu katika urejeshaji wa mikopo hiyo ili iweze kuwasaidia wasanii wengine kukopa.

Alimshukuru rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania Dk. Samia Hassan Suluhu kwa kuwaona wasanii kupitia Mfuko huo kwani utakuwa mkombozi kwao katika kuboresha kazi zao na kukuza kipato wasanii wa mikoani na Tanzania kwa ujumla.

Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Utamaduni na Sanaa Tanzania, Nyakaho Mahemba amewataka wasanii wa fani mbalimbali mkoani Iringa kujiandaa kunufaika na mfuko huo kwa kuandaa sanaa zitakazoboresha maslai yao na kukuza uchumi wao.

Alisema kuwa serikali kwa kupitia benki za NBC na CRDB, mfuko huo unatarajia kutoa mikopo mipya ya zaidi ya Sh bilioni 20 kwa wasanii mbalimbali hapa nchini kwa mwaka huu wa fedha 2023/2024 ambapo Hadi sasa Kuna wasanii wameza kunufaika na mkopo huo.

“Serikali ya awamu ya sita kupitia Mfuko wa Sanaa imeamua kutatua changamoto ya wasanii ambayo ni mtaji kwa kuwapatia fursa ya mikopo na elimu ya namna itakayowawezesha kuboresha kazi zao ili mikopo watakayopata iwape tija, na kuboresha Kazi zao za sanaa” Alisema

Mahemba alisema mfuko huo unatoa huduma katika maeneo ya urithi wa utamaduni, lugha na fasihi, sanaa za maonesho, sanaa za ufundi, filamu, muziki na fani nyingine zenye mlengo wa utamaduni na sanaa kwa watu binafsi, vikundi au makundi.

Alisema tangu uzinduliwe Disemba mwaka jana umekwisha wanufaisha wasanii 45 kiasi Cha Sh bilioni 1.077 ambao kati ya wanaume ni 29 waliowezeshwa Sh milioni 737, wanawake 12 Sh milioni 275, kikundi kimoja Sh milioni 10 na makampumi matatu Sh milioni 55.

Aliongeza kuwa miongoni mwa wanufaika mkopo huo ni kundi la walemavu lenye wanachama 22 wanaojishughulisha na uandaaji wa tamthilia, uibuaji wa vipaji vya tasnia kwa walemavu wenzao na watoto.

Naye Meneja wa Bidhaa na Huduma benki NBC kuroka makao makuu, Jonathan Bitababaje alisema benki yao imejipanga vyema kufanikisha mpango huo wa utoaji wa mikopo yenye masharti nafuu kwa wasanii ambapo wanaanza Mikopo inaanzia Sh 200,000 hadi Sh milioni 100 kwa mkopaji mmoja.

Alisema kuwa wasanii mkoani hapa wanachotakiwa kufanya ni kwenda katika ofisi za utamaduni katika wilaya walipo au mkoa ili wakajiandikishe na kuanza taratibu za kunufaika na mikopo huo wenye riba nafuu kwao.

Na mwenyekiti wa Chama cha Waigizaji Mkoa wa Iringa Hamis Nurdin ameishukuru serikali kwa kuwaletea fursa hiyo akisema watahakikisha wanaitumia ipasavyo ili isaidie kuboresha kazi zao na hatimaye kuwaingiza katika soko la ushindani katika kutengeneza kazi Bora zaidi.

Alisema kuwa awali walikuwa wakiandaa Kazi za Sanaa kwa kiwango hafifu kutokana na ufinyu wa bajeti hivyo kuja kwa fursa hii itasaidia kwa kiasi kikubwa kufanya filamu zenye ubora tofauti na awali.
Kaimu Katibu Tawala Msaidizi Viwanda na Bishara, Asifiwe Mwakibete
Baadhi ya wasanii wa mkoani Iringa
Meneja wa Bidhaa na Huduma benki NBC kuroka makao makuu, Jonathan Bitababaje
Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Utamaduni na Sanaa Tanzania, Nyakaho Mahemba

WAZIRI MABULA ATAHADHARISHA WANAOTUMIA WIZARA KAMA REJEA KUFANYA UHALIFU

August 15, 2023


Na Munir Shemweta, WANMM

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula ametoa tahadhari kwa wale wanaotumia wizara yake kama rejea kufanya uhalifu na kujipatia mali au fedha isivyo halali.

Waziri Mabula amesema mtu yoyote akihisi kuna udanganyifu ndani na nje ya Wizara ya Ardhi atoe taarifa mapema ili kukomesha uhalifu huo.

Dkt Mabula alitoa kauli hiyo leo tarehe 14 Agosti 2023 mbele ya waandishi wa habari jijini Dodoma kufuatia wizara yake kupokea malalamiko ya muda mrefu kutoka kwa familia ya marehemu Zuberi Mzee Mwinyimvua inayodai kwamba wizara yake haitaki kuondoa Hati ya kuwekesha (Notice of Deposit) iliyosajiliwa katika daftari la Msajili wa Hati kuhusu kiwanja Na 895 kilichopo eneo la viwanda mbezi mkoani Dar es Salaam iliyiosajiliwa ili kutoa kinga ya uwekezaji.

Kwa mujibu wa Dkt Mabula, kiwanja hicho kinamilikiwa na Mwinyimvua ambaye kwa sasa ni marehemu.

Akifafanua zaidi, alisema awali mmiliki wa kiwanja hicho aliingia mkataba wa uwekezaji na Velence Simon Matunda na Badi Nkya wanaotambulika kama wawekezaji.

Uwekezaji huo ulikuwa ni kujenga maduka 40 ambapo kati ya hayo maduka 33 yangesimamiwa na wawekezaji kwa kipindi cha miaka 15 na baada ya hapo wangekabidhi maduka hayo 15 kwa mmiliki ambapo katika kipindi hicho cha miaka 15 wawekezaji wangekusanya kodi ya pango.

Kwa mujibu wa mkataba, mmiliki alipewa kiasi cha shilingi 90,000,000 kwa ajili ya kulipa madeni ikiwemo kodi ya pango la ardhi la kiwanja hicho.

Waziri Mabula alisema suala la mgogoro huo limekuwa likishughulikiwa kiutawala kupitia wizara ya ardhi kwa zaidi ya miaka 8 kuhakikisha kwamba wawekezaji wanalipwa fedha hizo kama mahakama ilivyoamuru ili hatimaye msajili wa hati aondoe hati ya kuwekesha katika daftari la msajili na kukabidhi hati husika.

Kwa mujibu wa waziri Mabula, mpaka sasa suluhu ya mgogoro huo haijapatiakana kutokana na pande mbili za mgogogoro yaani msimamizi wa mirathi na wawekezaji kutotekeleza yale waliyokubaliana hususan upande wa uwekezaji.

Kimsingi mgogoro huo unatokana na ukiukwaji wa makubaliano baina ya mmilikina wawekezaji ambapo pia mahakama ilishatoa maamuzi. Wizara inatimiza wajibu wake kiutawala katika kutatua mgogoro pamoja na kuwa suala hilo linahusu mkataba wa uwekezaji na siyo umiliki wa ardhi.

Waziri Mabula alisema kwa kuwa mgogorio huo ni wa muda mrefu na wahusika wanaihusisha wizara ambayo si sehemu ya makubaliano na hivyo kuharibu taswira ya wizara ameelekeza pande zote za mgogoro kuheshimu na kutekeleza hukumu ya mahakama sambamba na pande hizo kutekeleza yale wanayokubaliana katika vikao vya usuluhusshi .

Pia amemuelekeza katibu Mkuu wizara ya ardhi kushirikiana na vyombo vya dola kuingilia kati suala hilo kwa kuwa una sura ya kijinai na utapeli ndani yake.


Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na mgogoro wa kiwanja kilichopo eneo la Viwanda Mbezi jijini Dar es Salaam tarehe 14 Agosti 2023

.
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na mgogoro wa kiwanja kilichopo eneo la Viwanda Mbezi jijini Dar es Salaam Agosti 14, 2023.