RAIS DKT MAGUFULI AZINDUA RASMI DARAJA LA KIGAMBONI, ALIBATIZA JINA LA DARAJA LA NYERERE

RAIS DKT MAGUFULI AZINDUA RASMI DARAJA LA KIGAMBONI, ALIBATIZA JINA LA DARAJA LA NYERERE

April 19, 2016

DAR1
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akikata utepe huku viongozi wengine wakiushikilia kuashiria uzinduzi rasmi wa Daraja la Kigamboni katika wilaya mpya ya Kigamboni jijini Dar es salaam leo Aprili 19, 2016PICHA NA IKULU
DAR2
DAR4
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akipata picha ya kumbukumbu viongozi wengine baada ya  uzinduzi rasmi wa Daraja la Kigamboni katika wilaya mpya ya Kigamboni jijini Dar es salaam leo Aprili 19, 2016
DAR5
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiteta jambo na aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa 
NSSF Dkt Ramadhani Dau wakati wa  uzinduzi rasmi wa Daraja la Kigamboni katika wilaya mpya ya Kigamboni jijini Dar es salaam leo Aprili 19, 2016
DAR6
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli na viongozi wengine 
wakitembea juu ya Daraja la Kigamboni baada ya kulizindua katika wilaya mpya ya Kigamboni jijini Dar es salaam leo Aprili 19, 2016
DAR7
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli na viongozi wengine 
wakitembea juu ya Daraja la Kigamboni baada ya kulizindua katika wilaya mpya ya Kigamboni jijini Dar es salaam leo Aprili 19, 2016
RAIS DKT. MAGUFULI AMUAPISHA MATHIAS MEINRAD CHIKAWE KUWA BALOZI MPYA WA TANZANIA NCHINI JAPAN

RAIS DKT. MAGUFULI AMUAPISHA MATHIAS MEINRAD CHIKAWE KUWA BALOZI MPYA WA TANZANIA NCHINI JAPAN

April 19, 2016

CHI1
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Mathias Meinrad Chikawe kuwa Balozi mpya wa Tanzania nchini Japan, Ikulu jijini Dar es Salaam.
CHI3
Rais Dkt. Magufuli akimpongeza Mathias Meinrad Chikawe mara baada ya kumuapisha kuwa  Balozi Mpya wa Tanzania nchini Japani
CHI4
Balozi mpya wa Tanzania nchini Japan Mathias Chikawe akimshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli mara baada ya kuamuapisha Ikulu jijini Dar es Salaam.
CHI5
Rais Dkt. Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Balozi mpya wa Tanzania nchini Japan Mathias Chikawe pamoja na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Mhandisi John Kijazi Ikulu jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU
MATUKIO BUNGENI MJINI DODOMA LEO

MATUKIO BUNGENI MJINI DODOMA LEO

April 19, 2016

BU1
 Spika wa Bunge, Job Ndugai akiongozwa na Mpambe wa Bunge kuingia kwenye ukumbi wa Bunge mjini Dodoma  kuongoza kikao cha kwanza cha  mkutano wa tatu wa Bunge   Aprili 19, 2016. (Picha na ofisi ya Waziri Mkuu)
BU2
Ruth Owenya akiapa kuwa Mbunge  kwenye ukumbi wa Bunge Mjini Dodoma Aprili 19, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
BU3
 Ritta Kabati akiapa kuwa Mbunge kwenye ukumbi wa Bunge mjini Dodoma Aprili 19, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
BU4
Spika wa Bunge Job Ndugai   (kulia) akimwapisha  Ritta Kabati kuwa mbunge kwenye ukumbi wa Bunge mjini Dodoma  Aprili 19, 2016. (Picha na ofisi ya Waziri Mkuu)
BU5
 Spika wa Bunge, Job Ndugai akimwapisha Waziri Kiongozi wa Zanzibar Mstaafu,  Shamsi Vuai Nahodha kuwa Mbunge kwenye ukumbi wa Bunge  Mjini Dodoma Aprili 10, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
BU6
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimpongeza, Waziri Kiongozi  wa Zanzibar  Mstaafu , Shamsi Vuai Nahodha baada ya kuapishwa kuwa Mbunge, Bungeni mjini Dodoma, Aprili 19, 2016. (picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
BU7
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mbunge wa Bumbuli na Waziri wa nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Mazingira na Muungano, January Makamba, bungeni mjini Dodoma Aprili 19, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

MBUNGE WA VITI MAALUMU MKOA WA IRINGA RITHA KABATI AAPISHWA HII LEO MBUNGENI NA KUWA MBUNGE KAMILI.

April 19, 2016

 Mbunge wa jimbo la iringa mjini mch Petter Msigwa akimpongeza mbunge wa viti maalum Ritha Kabati mara baada ya kuapishwa sambamba na watu wengi walimpongeza mbunge huyo kama wanavyoonekana kwenye picha.
 mbunge wa jimbo la iringa mjini mch Petter Msigwa na mbunge wa jimbo la kilolo mkoani iringa Vennance Mwamoto wakimpongeza mbunge wa viti maalum Ritha Kabati mara baada ya kuapishwa.
 watu mbalimbali walijitokeza kumpongeza mbunge rita kabati mara baada ya kuapishwa hii leo. 
 
 Mbunge wa jimbo la iringa mjini mch Petter Msigwa na mbunge wa jimbo la kilolo
mkoani iringa
Vennance Mwamoto wakimpongeza mbunge wa viti maalum rita
kabati mara baada ya kuapishwa.
…………………………………………………………………………………………………
Na Fredy Mgunda Iringa.
mbunge wa viti maalumu mkoa wa iringa Ritha Kabati ameapishwa leo kuwa mbunge kamili hii imekutaja mara Baada ya kukamilika kwa Uchaguzi wa Majimbo hayo nane (8), Chama Cha Mapinduzi (CCM), Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na Chama cha Wananchi (CUF) ndivyo vilivyoendelea kupata angalau asilimia tano (5%) ya
Kura zote halali za Ubunge, kwa maana hiyo, vyama hivyo ndivyo vitaendelea kuhusishwa kwenye Mchakato wa kugawanywa hivyo Viti 3 vilivyobaki.

Tume ya Taifa ya Uchaguzi iliwatangaza ndugu Ritha Enespher Kabati na ndugu Oliver Daniel Semuguruka wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na ndugu   Lucy Fidelis Owenya wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kuwa Wabunge Wanawake wa viti Maalum katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Ikumbukwe kuwa Tume katika Kikao chake cha tarehe 11/11/2015 ilifanya Uteuzi wa Wabunge Wanawake wa Viti Maalum 113 kwa mwaka 2015. Hata hivyo, Wabunge Wanawake wa Viti Maalum walioteuliwa jumla yake
ilikuwa ni 110 kati ya 113 ambapo Viti vitatu (3) vilibakizwa kusubiri Uchaguzi wa Majimbo nane (8) ambayo Uchaguzi wake ulihairishwa kutokana na sababu mbalimbali.
Uteuzi wa awali ulihusisha Vyama vitatu vilivyofikisha asilimia tano (5%) ya Kura zote halali za Wabunge kama matakwa ya Katiba yanavyotaka.
hata hivyo mbunge wa iringa mjini mchungaji petter saimoni msingwa na mbunge wa jimbo la kilolo vennance mwamoto ambaye nia ndugu na ritta kabati kwa pamoja walimpongeza kwa kuchaguliwa  na kuapishwa kwake siku ya leo.
Katibu Mkuu Wizara ya Habari afungua mdahalo wa Vijana kujadili hatma ya ajira kwa vijana nchini

Katibu Mkuu Wizara ya Habari afungua mdahalo wa Vijana kujadili hatma ya ajira kwa vijana nchini

April 19, 2016

OL1
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel akifungua mdahalo wa hatma ya ajira kwa vijana wa Tanzania ulioandaliwa na Shirika la Kimataifa la Ajira (ILO) na kushirikisha vijana kutoka Tanzania Bara na Visiwani leo jijini Dar es Salaam
OL2
Mkurugenzi Mkazi Shirika la Kimataifa la Ajira (ILO) nchi ya Tanzania, Kenya, Uganda, Burundi na Rwanda Bibi. Mary Kawar akizungumza na vijana (hawapo pichani) wakati wa mdahalo wa hatma ya ajira kwa vijana wa Tanzania ulioandaliwa na shirikila hilo leo jijini Dar es Salaam.
OL3
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel (kushoto) akitoa mada wakati wa mdahalo wa hatma ya ajira kwa vijana wa Tanzania ulioandaliwa na Shirika la Kimataifa la Ajira (ILO) na kushirikisha vijana kutoka Tanzania Bara na Visiwani leo jijini Dar es Salaam
OL4
Mtaalam wa ajira kutoka ILO Bw. Jealous Chirore akichangia mada wakati wa mdahalo wa hatma ya ajira kwa vijana wa Tanzania ulioandaliwa na Shirika hilo na kushirikisha vijana kutoka Tanzania Bara na Visiwani leo jijini Dar es Salaam
OL5
Mwakilishi kutoka YUNA – Chuo cha Bogamoyo akiuliza swali wakati wa mdahalo wa hatma ya ajira kwa vijana wa Tanzania ulioandaliwa na Shirika la Kimataifa la Ajira (ILO) na kushirikisha vijana kutoka Tanzania Bara na Visiwani leo jijini Dar es Salaam
OL7
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel akipokea zawadi kutoka kwa Mkurugenzi Mkazi Shirika la Kimataifa la Ajira (ILO) nchi ya Tanzania, Kenya, Uganda, Burundi na Rwanda Bibi. Mary Kawar baada ya kufungua mdahalo wa hatma ya ajira kwa vijana wa Tanzania ulioandaliwa na Shirika la Kimataifa la Ajira (ILO) na kushirikisha vijana kutoka Tanzania Bara na Visiwani leo jijini Dar es Salaam.
Picha na: Genofeva Matemu – Maelezo
SERIKALI KUENDELEA KULINDA KAZI ZA WASANII NCHINI

SERIKALI KUENDELEA KULINDA KAZI ZA WASANII NCHINI

April 19, 2016

FIS1
Mkurugenzi wa Elimu kwa mlipa kodi toka Mamlaka ya Mapato    Tanzania (TRA) Bw. Richard Kayombo akionesha kwa waandishi wa Habari leo Jijini Dar es salaam moja ya CD zilizokamatwa wakati wa msako wa kubaini wale wote wanaojihusisha na uuzaji na usambazaji wa kazi za wasanii bila kuwa na stempu za kodi katika bidhaa za filamu na muziki. Kulia ni Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Bi Joyce Fissoo na mwisho kulia ni Afisa Habari wa Mamlaka ya Mapato Tanzania Bi Mariam Mwayera.
FIS2
Mkurugenzi wa Elimu kwa mlipa kodi toka Mamlaka ya Mapato    Tanzania (TRA) Bw. Richard Kayombo (katikati) akitoa wito leo Jijini Dar es salaam  kwa wasambazaji na wauzaji wa kazi za Filamu na muziki kuzingatia sheria na Kanuni zinazosimamia sekta hiyo kwa kuwa Serikali itawachukulia hatua kali wale wote watakaoenda kinyume cha sheria na taratibu zilizopo ikiwemo kutozwa faini isiyopungua milioni tano au kifungo kisichopungua miaka mitatu jela. Kulia ni Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Bi Joyce Fissoo,Kushoto ni Afisa Utamaduni wa Bodi ya filamu Bw. Wilhadi Tairo.
FIS3
Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Bi Joyce Fissoo akifafanua kwa waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam kuhusu mikakati ya Bodi hiyo kuhakiksha kuwa kazi za wasanii wa filamu zinaendana na maadili ya Taifa.kushoto ni Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania Bw. Richard Kayombo.
FIS4
Baadhi ya waandishi wa Habari wakifuatilia mkutano wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na Bodi ya Filamu Tanzania ukilenga kueleza Mikakati ya Serikali katika kulinda haki za wasanii wa filamu na Muziki zinalindwa.
( Picha na Frank Mvungi- Maelezo)
……………………………………………………………………………………………………………..
Na Fatma Salum (MAELEZO)
Serikali kupitia Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imeahidi kuendeleza msako wa wafanyabiashara wote wanaouza kazi za filamu na muziki bila kubandikwa stempu halali za kodi ili kuzilinda kazi hizo kwa ajili ya kuwanufaisha wasanii na kuhakikisha Serikali inapata mapato yake.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Huduma kwa Mlipa Kodi kutoka TRA Richard Kayombo wakati akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam.
Kayombo amesema TRA kwa kushirikiana na wadau wa tasnia ya muziki na filamu imedhamiria kuhakikisha kuwa bidhaa za filamu na muziki zenye stempu za kodi ndizo zinazoingizwa sokoni ili kulinda kazi za wasanii wa taifa letu dhidi ya dhuluma zinazofanywa na baadhi ya wafanyabiashara.
“Msako huu endelevu utahusisha kukamata bidhaa zote ambazo hazijabandikwa stempu za kodi na kuwachukulia hatua wahusika kwa mujibu wa sheria.” Alieleza Kayombo.
Aidha Kayombo amefafanua kuwa kwa kipindi cha mwezi Februari na Machi 2016, TRA kwa kushirikiana na Dalali wa Mahakama Yono Auction Mart & Company Limited ilifanya msako jijini Dar es Salaam na kukamata jumla ya CD na DVD zenye thamani zaidi ya shilingi Bilioni 1.3 ambazo zilisambazwa bila kufuata sheria hivyo kukwepa kodi ya ushuru ipatayo shilingi Milioni 31.9 na gharama za stempu zaidi ya shilingi Milioni 11.1.
TRA inawatahadharisha wale wote wanaosambaza na kuuza kazi za filamu na muziki ambazo hazijabandikwa stempu kuacha mara moja na kufuata utaratibu wa kupata stempu hizo katika ofisi za TRA ili wawe na uhalali wa kuuza bidhaa hizo kinyume chake hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.

VICHAKA HATARISHI KATIKA KITUO CHA AFYA BUZURUGA JIJINI MWANZA VYAFYEKWA

April 19, 2016
Hali ya Usalama katika Kituo cha Afya cha Kata ya Buzuruga kilichopo Manispaa ya Ilemela Mkoani Mwanza imeimarika, baada ya Wakazi wa Kata hiyo wanaounda Kikundi cha Kijamii cha “Ulipo Tupo” kufyeka vichaka vilivyokuwa katika kituo hicho ambavyo vilikuwa vikitumiwa na wahalifu kama maficho yao.

Baada ya kufyeka vichaka hivyo jumamosi iliyopita, Mwenyekiti wa Kikundi hicho, Ndaisaba Aron alisema kuwa vichaka hivyo vilikuwa hatarishi kwa wananchi, wagonjwa pamoja na wahudumu wa Afya katika Kituo hicho, kutokana na kupata malalamiko kwamba vibaka walikuwa wakikimbilia katika vichaka hivyo baada ya kufanya uhalifu.

Hidaya Bashiru ambae ni mwanachama wa kikundi hicho pamoja na Sixtus Ijugo ambae ni Katibu, waliwasihi wananchi wengine kuwa na desturi ya kushiriki katika shughuli za kijamii ikiwemo katika maeneo mbalimbali kama hospitali, shule na kwingineko kwa ajili ya maendeleo yao wenyewe.

Diwani wa Kata ya Buzuruga, Richard Machemba, alijumuika na Kikundi hicho kwa ajili ya kufanya usafi katika Kituo hicho ambapo alipongeza juhudi mbalimbali zinazofanywa na wakazi pamoja na vikundi mbalimbali vya maendeleo katika Kata yake ambapo amewasihi wananchi kuendelea kujitoa kwa ajili ya kushiriki shughuli za maendeleo.
Sikiliza Sauti HAPA Au Bonyeza Play Hapa Chini
                                                                    Tazama Picha HAPA
SERENGETI BOYS KUJIPIMA NA MAREKANI, KOREA KUSINI

SERENGETI BOYS KUJIPIMA NA MAREKANI, KOREA KUSINI

April 19, 2016
Timu ya taifa ya Tanzania vijana wenye umri chini ya miaka 17 ‘Serengeti Boys’ inatarajiwa kushiriki mashindano maalumu ya vijana wenye umri chini ya miaka 17 nchini India, yatakayozishirikisha nchi za Marekani, Malasyia na Korea Kusini na wenyeji mapema mwezi Mei, 2016.
Chama cha Soka nchini India (AIFF) kimeandaa mashindano ya vijana wenye umri chini ya miaka 17, ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya kikosi chao kwa ajili ya Fainali za Kombe la Dunia kwa Vijana zitakazofanyika nchini humo mwaka 2017.
umla ya nchi tano zitashiriki mashindano hayo yatakayofanyika katika mji wa Goa kuanzia Mei 15-25, 2016 ambapo michezo itachezwa kwa mfumo wa ligi kwa kila timu kucheza michezo minne, kabla ya mchezo wa mwisho wa fainali wa kumpata Bingwa wa mashiandano hayo.
Serengeti Boys ambayo imeshacheza michezo mitatu ya kirafiki ya kimataifa mpaka sasa, mmoja dhidi ya Burundi na miwili dhidi ya timu ya vijana wa Misri (The Pharaohs) inatarajiwa kuingia kambini mwishoni mwa mwezi Aprili, 2016 katika hosteli za TFF zilizopo Karume kujiandaa kwa safari ya kuelekea nchini India kushiriki michuano hiyo.
Kikosi cha Serengeti Boys kinachonolewa na kocha Bakari Shime, akisaidiwa na Sebastian Mkomwa chini ya mshauri wa ufundi wa timu za vijana Kim Poulsen, kinatarajiwa kuwa kambini kwa muda wa wiki mbili kabla ya safari kuelekea Goa India kushirki mashindano hayo.
Kupata nafasi ya kushiriki mashindano hayo maalumu ya vijana kimataifa ni sehemu ya maandalizi ya kikosi cha Serengeti Boys, kujiandaa na mchezo wa kuwania kufuzu kwa Fainali za Vijanaa barani Afrika dhidi ya Shelisheli Juni 25 – 2 Julai, 2016.
 KILA LA KHERI AZAM, YANGA

KILA LA KHERI AZAM, YANGA

April 19, 2016
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limezitakia kila la kheri timu za Azam FC na Yanga SC katika michezo yao ya kimataifa inayoandaliwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu barani Afrika (CAF).
TFF imezitaka Azam FC na Yanga kupambana katika michezo yao ugenini ili kupata matokeo mazuri yatakayozifanya ziweze kusonga mbele katika hatua inayofuata, ikiwa kwa sasa ndio wawakilishi pekee wa Tanzania katika michuano ya kimataifa.
Azam FC inayoshirki michuano ya Kombe la Shirkisho barani Afrika (CAF CC), leo saa 3 usiku kwa saa za Afrika Mashariki inashuka dimba la Olymique 07 November, Rades jijini Tunis kuwakabili wenyeji Esperance ST katika mchezo wa marudiano.
Kesho Jumatano, Yanga SC watakuwa ugenini kuwakabili wenyeji Al Ahly SC katika mchezo wa marudiano wa Ligi ya mabingwa barani Afrika (CAF CL), mchezo utakaochezwa saa 2:30 usiku katika uwanja wa Borg El Arab kwa saa za Afrika Mashariki na Kati.

SERIKALI KUCHUNGUZA MKATABA WA JENGO LA MACHINGA COMPLEX

April 19, 2016
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaa, Paul Makonda (kulia), akikagua vizimba katika Jengo la Machinga Complex Dar es Salaam jana, baada ya kufanyika kikao cha kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa kilichoketi jana kujadili uendeshaji wa biashara wa katika jengo hilo pamoja na kamati ya mkoa iliyoundwa kuchunguza mkataba wa jengo.
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaa, Paul Makonda akizungumza na wafanyabiashara katika Jengo la Machinga Complex Dar es Salaam jana, kuhusu uendeshaji wa jengo hilo.
 Makonda akiwasili katika viwanja vya Jengo la Machinga Complex kuzungumza na wafanyabiashara na wadau wengine. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi wengine ni viongozi wa jengo hilo.

Makonda akiangalia Uwanja wa Karume akiwa jengo la Machinga Complex.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, CP Simon Sirro akimuaga Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda baada ya kumaliza kuzungumza na wananchi.


Na Dotto Mwaibale

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ameagiza kufanyika kwa uchunguzi katika ujenzi wa jengo la Machinga Ciomplex ili kubaini uhalali wa mkataba uliotumika kujenga jengo hilo.

Aidha, amebainisha kuwa jengo la Machinga Complex kwa sasa linadaiwa zaidi ya Sh bilioni 36 kiasi ambacho ni mara tatu ya thamani halisi ya jengo hilo ambayo ni Sh 12 ambazo zinatakiwa kulipwa na wafanyabiashara wa jengo hilo.

Makonda aliyasema hayo Dar es Salaam  jana wakati alipotembelea jengo hilo lililopo Manispaa ya Ilala ili kujionea mazingira ya kufanyia biashara. Alisema kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa itaanza kufanya uchambuzi wa mikataba ili kupata uhalali wa gharama na kujua kiwango kinachostahili kulipwa na wafanyabiashara hao.

Alisema kamati hiyo ya ulinzi na usalama imekubali kutengeza kamati ndogo itakayoanza kazi leo ya kuchambua na kuanza mikataba.

“Ingekuwa vyema tungekuwa na mkutano wa kuwasikilizeni na kujua kero zenu, lakini tunayo sababu moja ya msingi ya kutowasikiliza , kwanza tunatafuta uhalali na utaratibu wa jengo hili lilivyojengwa.

Katika maelezo ya awali tuliyoyapata jengo hili uko mkanganyiko mkubwa,  inawezekana ni miongoni mwa mradi mkubwa uliofanyiwa ufisadi Tanzania, sasa hatuwezi kukaa kusikiliza habari ya kizimba change, kwanza tupate uhalali wa mkataba uliopelekea kujenga jengo hili,” alisema Makonda.

Alisema kamati ya wafanyabiashara wa soko hilo itakayoundwa chini ya usimamizi wake itaanza kazi ya kuchunguza ili kubaini uhalali wa mkataba na kujua kama waliongia mikataba hiyo walikuwa sahihi.

Makonda alitoa rai kwa wafanyabiashara kuwa rai ya Rais Magufuli ni kuwapigania wanyonge na kuhakikish awanatoka sehemu moja kwenda nyingine, hivyo wasaidiza wake kwa kupenda au kutokupenda wana jukumu la kuhakikisha wanafanikisha hilo.

Hivi karibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais TAMISEMI, George Simbachawene aliifuta bodi inayosimamia jengo hilo na kumsimamisha kazi meneja anayesimamia jengo hilo na kumtaka kwenda katika ofisi za jiji kwa ajili ya kumpangia kazi nyingine.

Katika hatua nyingine, Simbachawene alilikabidhi jengo hilo kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kwa ajili ya kuandaa mpango wa kuwaingiza wafanyabiashara bila masharti huku ukiangaliwa utaratibu mpya kwa wafanyabiashara hao.


Katika mkutano wake na Jumuiya ya Wafanyabiashara nchini, Simbachawene alisema, jengo hilo limekuwa likitumiwa kinyume na lengo ambalo walitakiwa wafanyabiashara kulitumia kwa gharama kidogo lakini limekuwa likitumiwa na watu wengine tofauti na wafanyabiashara jambo ambalo limesababisha kushindwa kulipa deni linalodaiwa na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF).