MIILI INAYODAIWA NI YA BINADAMU ILIYOKUTWA JANA JIJINI DAR IKIWA NDANI YA MIFUKO IMETUPWA

MIILI INAYODAIWA NI YA BINADAMU ILIYOKUTWA JANA JIJINI DAR IKIWA NDANI YA MIFUKO IMETUPWA

July 22, 2014

63a4c18aba35870d3d4177324b654bae
Gari likiwa limebeba mifuko yenye viuongo hivyo, ambapo Jeshi la Polisi wilaya ya Kinondoni limesema kuwa limeanza uchunguzi wa kina baada ya kukakamata viungo mbalimbali vinavyodhaniwa kuwa ni vya binadamu katika mifuko ya plastiki katika machimbo ya kokoto sehemu za Mbweni Mpiji, Magohe, nje kidogo ya jiji la Dar es salaam .http://daresalaam-yetu.blogspot.com
ad41c51ed504857ec7b80c1988a66e05
Sehemu ya mifuko ya plastiki iliyokutwa na viungo hivyo ambavyo inasemekana ni pamoja na mikono, miguu, ngozi na sehemu nyingine za miili
Rais kikwete afungua barabara wilayani Namtumbo

Rais kikwete afungua barabara wilayani Namtumbo

July 22, 2014

D92A7678
Dkt.Jakaya Kikwete na Mkurugenzi Mkazi wa Mfuko wa Changamoto za millennia(Millenium Challenge Corporation Bwana Karl Fickensher wakifunua kitambaa katika jiwe la msingi Kuzindua Barabara ya Lami ya Songea-Namtumbo yenye urefu wa kilometa 71.4 iliyojengwa kwa msaada wa Watu wa Marekani kupitia mfuko huo wakati wa hafla iliyofanyika katika kijiji cha Migelegele wilayani Namtumbo leo.
D92A7684 
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimshukuru Mkurugenzi Mkazi wa Mfuko wa Changamoto za millennia(Millenium Challenge Corporation Bwana Karl Fickensher wakati wa uzinduzi wa Barabara ya lami ya Songea-Namtumbo yenye urefu wa kilometa 71.4 iliyojengwa kwa ushirikiano kati ya serikali ya Tanzania na msaada kutoka kwa watu wa Marekani kupitia mfuko huo katika sherhe zilizofanyika katika kijiji cha Migelegele wilayani Namtumbo Mkoani Ruvuma leo.
D92A7715
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimwagilia maji mti wa kumbukumbu aliupanda muda mfupi baada ya kuzindua barabara ya Songea hadi Namtumbo yenye urefu wa kilomita 71.4 katika hafla iliyofanyika katika kijiji cha Migelegele wilayani Namtumbo leo. Wapili kushoto ni Waziri wa Ujenzi Dkt.John Pombe Magufuli, Watatu ni Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Dkt.Servacius Likwelile, Wanne ni Mkurugenzi wa Mfuko wa Changamoto za Milenia Tanzania Bwana Bernard Mchomvu,Wapili kulia ni mbunge wa Namtumbo Vita Kawawa na kulia ni Mwakilishi Mkazi wa Mfuko wa Changamoto za Milenia Bwana Karl Fickenscher.
D92A7781
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete,Balozi Mdogo wa Japan Bwana Kazuyoshi Matsunaga(katikati) na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika(African Development Bank) ADB Bibi Tonia Kondiero kulia wakifunua kitambaa katika jiwe la msingi kuzindua rasmi ujenzi wa Barabara ya Lami ya Namtumbo- Matemanga  yenye urefu wa kilomita 128.9 uliofanyika katika kijiji cha Migelegele .Wapili kushoto ni Waziri wa Ujenzi Dkt.John Pombe Magufuli na watatu kushoto ni Mke wa Rais Mama Salma Kikwete.Barabara hiyo inajengwa na serikali ya Tanzania ikisaidiwa na fedha kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika na serikali ya Japan kupitia shirika lake la misaada la JICA.
D92A7986
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na mbunge wa Namtumbo Vita Kawawa wakifunua kitambaa katika jiwe la msingi wakati wa hafla ya uzinduzi wa hospitali mpya ya wilaya ya Namtumbo Mkoani Ruvuma uliofanyika jana.Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Bwana Saidi Mwambungu.(picha na Freddy Maro)
D92A7167
Rais Kikwete aliposimama katika kijiji cha Utwango kuwasalimia wananchi akiwa njiani kuelekea mjini Namtumbo akitokea Songea mjini

AKUDO IMPACT KUPAGAWISHA BONANZA LA SIKUKUU YA IDDI MOSI MSASANI BEACH CLUB KAWE

July 22, 2014
BENDI ya Akudo Impact  “Vijana wa Masauti”watafanya onyesho kali la Bonanza wakati wa sikukuu ya Iddi Mosi kwenye Ukumbi wa Msasani  Beach Club Kawe Dar es Salaam litakaloanza saa nane mchana hadi Majogoo

Akizungumza kwa njia ya simu na TANGA RAHA BLOG,Meneja wa Akudo Impact,Juma Abajalo
  alisema maandalizi ya kuelekea bonanza hilo lililopewa jina la Shangwe za sikukuu ya Iddi limekamilika kwa asilimia kubwa.

Abajalo alisema wapenzi wa mziki wa dansi hapa nchini wakae mkao wa
  kula wakisubiria burudani kabambe itakayotolewa na wasanii wanaounda bendi hiyo maarufa hapa nchini wakiwemo Taasisi Masela Zegrebu Butam,Alen Kabasele mtoto wa pepekale Dipron aliyekuwa malaika bendi na Rap Fadii.

Alisema baada ya kumalizika onyesho hilo la Msasani Beach bendi hiyo
  itaondoka usiku kuelekea Visiwani Zanzibar Iddi Pili na siku Ijumaa inayofuata watahamia kufanya onyesho lao katika ukumbi wa Hiltech Banana Ukonga na Jumamosi watafanya kwenye ukumbi wa Cheetozi Miti Mirefu Sayansi.

Aidha alisema budurani zote hizo zitakuwa ni za kiwango cha hali ya
  juu na kuwataka wapenzi wa mziki huo kujitokeza kwa wingi kushuhudia maonyesho hayo yatakayokuwa gumzo mara baada ya kumalizika mfungo mtukufu wa ramadhani.

Hata hivyo alisema katika kuhakikisha onyesho hilo warembo

watakaokonga nyoyo wapenzi watakaojitokeza wataongozwa na Mrembo Raisa ambaye amekuwa akifanya vizuri sana hasa anapokuwa stejini.