COASTAL UNION YAWAANDALIWA WACHEZAJI WAO FUTARI LEO.

August 04, 2013


WALIMU WANAOINOA TIMU YA COASTAL UNION YA TANGA KULIA NI KOCHA MKUU HEMED MORROCO,KUSHOTO NI KOCHA MSAIDIZI ALLY KIDS NA KOCHA WA MAKIPA KATIKATI JUMA PONDAMALI "MENSA"

MWENYEKITI WA KLABU YA COASTAL UNION YA TANGA HEMED AURORA KUSHOTO KATIKAATI NI MPENZI WA TIMU HIYO NA ANAYEFUATIA NI MJUMBE WA KAMATI YA UTENDAJI ALBERT PETER MARA BAADA YA KUMALIZIKA FUTARI ILIYOANDALIWA NA UONGOZI HUO.


MWENYEKITI WA KLABU YA COASTAL UNION HEMED AURORA"MPIGANAJI"MWENYE KOTI JEUSI KATIKA KUSHOTO KWAKE NI MJUMBE WA KAMATI YA UTENDAJI ALBERT PETER NA KATIBU WA ZAMANI WA TIMU HIYO SALIM BAWAZIRI NA KULIA KWAKE NI MSHAMBULIAJI WA TIMU HIYO JERRY SANTO.

LIGI YA KIKAPU TANGA KUANZA AGOSTI 21-31MKWAKWANI.

August 04, 2013
Na Oscar Assenga,Tanga.
LIGI ya Kikapu ngazi ya Mkoa wa Tanga inatarajiwa kuanza kutimua vumbi Agosti 24 mpaka 31 mwaka katika uwanja Mkwakwani mjini hapa na itashirikisha timu sita.

Akizungumza na blog hii,Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Kikapu mkoa wa Tanga(TRBA)Hamisi Jaffary alisema maandalizi ya ligi hiyo yanaendelea vema kutokana na timu zote hizo kuthibitisha ushiriki ikiwemo kuanza kujiaanda wao binafasi.

Jaffary alizitaja timu hizo kuwa ni Bandari Tanga,Bombo Giants,Tanga United,Tanga City,Raskazone na timu ya Korogwe ambapo watachuana ili kuweza kumpata bingwa wa mkoa huu.

      "Ligi ya msimu uliopita ilikuwa na upinzani mkubwa sana hivyo ni matumaini yetu na hii itakuwa na ushindani kwani lengo likiwa ni kupata timu nzuri "Alisema Jaffary.

Mwenyekiti huyo alieleza kuwa chama hicho kitafanya uchaguzi wa viongozi wake mwezi huo huo ili uweza kupata safu mpya ya uongozi itakayokuwa na jukumu la kusimamia shughuli za chama hicho baada ya uongozi uliopo kumaliza muda wake. 

BANDA:AIOTA STARS.

August 04, 2013
Na Oscar Assenga,Tanga.

BEKI wa kushoto wa Klabu ya Coastal Union ,Abdi Banda amesema malengo yake msimu huu ni kutaka kuichezea timu hiyo kwa mafanikio ili kuweza kupata nafasi ya kucheza timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars).

Akizungumza na blogg hii,Banda alisema muda huo ni wakati wake na hakusajiliwa Coastal Union kutembea bali kuhakikisha anaipa mafanikio ikiwemo kutoa mchango wake mkubwa kwa ajili ya kuiwezesha timu hiyo kutimza ndoto yake ya kuchukua ubingwa wa ligi kuu msimu ujao.

Banda alisema uwezo huo anao na umejihakikishia kwa asilimia kubwa kutokana na maandalizi ambayo anayafanya na wachezaji wenzake na kuwamwagia sifa walimu wao,Hemed Morroco na Ally Kids kwa kuwapa mbinu nzuri mazoezini ambazo zimeonekana kuzaa matunda hasa kwenye mechi zao mbili za kirafiki.

 "Uwezo wa kucheza timu ya Taifa ninao na ninaimani nitaonekana na kuweza kupewa nafasi labda yatokee majeraha madogo madogo lakini mimi ninajiamini ninauwezo mzuri wa kulitumikia Taifa kupitia Taifa Stars "Alisema Banda.

Alisema lazima vilabu vya soka hapa nchini ikiwemo Simba ,Yanga na Azam FC wafahamu kuwa msimu huu ubingwa wa ligi hiyo hautakuwa mikononi mwao bali kwa Coastal Union hivyo wao wajiandae kushika nafasi zinazofuata na sio ya kwanza.
MAKAMBA:AMFAGILIA LOWASSA

MAKAMBA:AMFAGILIA LOWASSA

August 04, 2013
Na Oscar Assenga,Tanga.
KATIBU MKUU Mstaafu wa Chama cha Mapinduzi (CCM)Yusuph Makamba amemwagia sifa Waziri Mkuu wa Mstaafu Edward Lowassa kwa kusema ni mtu mzuri na bora ambaye anawafaa watanzania katika mambo mbalimbali ya maendeleo.

Makamba alitoa kauli hiyo mwishoni mwa wiki wakati wa futari iliyoandaliwa na hotel ya Tanga Beach Resort ambayo ilihudhuriwa na viongozi wa serikali,dini wakiwemo wabunge  wa vyama vya kisiasa mkoani hapa na kamati ya miundo mbinu ambayo inautembelea mkoa huu.

Alisema kuwa Lowasa aliwahi kufanya nae kazi akiwa katika nyazifa mbalimbali bila kuwepo mikwaruzano na ni mkweli ambayo hupenda ushirikiano katika uongozi wa nchini.

Aidha alisema kuwa lowassa ni kiongozi hodari na shupavu ambaye anaweza kuwaleletea maendeleo wananchi wa Tanzania kwani ana mipango makini inayoweza kutekelezeka na huwajali watu wote bila kuangalia itikadi zao za dini na vyama .

  "Lowassa ni kiongozi bora sana,na ni mtu ambaye anatufaa na kunakushukuru umetufaa mwenyezi mungu akupe heri na baraka tele ili kuweza kufanikisha malengo yao iliyojiwekea "Alisema Makamba.

Kwa upande wake,Lowassa aliwasalimia  wananchi waliojitokeza kwenye halfa hiyo na kuwatakia kila heri waislamu kwa kuwatakia mfungo mwema wa mwezi wa ramadhani na kuwataka kuendelea kudumisha amani hapa nchini.

Mwisho.

FUTARI

August 04, 2013
WAZIRI MKUU MSTAAFU,EDWARD LOWASSA AKIWA KATIKA FUTARI JANA KWENYE HOTEL YA TANGA BEACH RESORT AMBAYO ILIANDALIWA NA HOTEL HIYO.
WAZIRI MKUU MSTAAFU ,EDWARD LOWASSA AKIZUNGUMZA KATIKA FUTARI HIYO ILIYOANDALIWA NA HOTEL YA TANGA BEACH RESORT.
KATIBU MKUU MSTAAFU WA CCM YUSUPH MAKAMBA AKIZUNGUMZA KATIKA FUTARI HIYO.
MEYA WA JIJI LA TANGA OMARI GULEDI AKIZUNGUMZA.

NYANDA ASISITIZA MSHIKAMANO KWA WANACHAMA NA WAPENZI WA YANGA.

NYANDA ASISITIZA MSHIKAMANO KWA WANACHAMA NA WAPENZI WA YANGA.

August 04, 2013
Na Oscar Assenga,Tanga.
MJUMBE wa Kamati ya Utendaji wa Klabu ya Yanga,Aron Nyanda amewataka wanachama na wapenzi wa
timu hiyo waliopo maeneo mbalimbali hapa nchini kudumisha umoja na mshikamano miongoni mwao.


Nyanda alitoa kauli hiyo mwishoni mwa wiki wakati akifungua tawi la Yanga "Umoja ni Nguvu mkoa wa
Tanga lililopo Chumbageni jijini hapa na kuwataka wanachama hao na wapenzi kuhakikisha wanakuwa na ushirikiano ili kuliletea tawi hilo maendeleo.

Alisema kikubwa ambacho kitaleta maendeleo kwenye klabu hiyo ni kuondoa utegemezi ambapo alisema wanaandaa utaratibu mzuri wa kutengeneza tisheti ambazo zitapelekwa kwenye matawi yao nchini nzima ili ziweze kusimamiwa na kuuzwa nao ili klabu hiyo iweze kunufaika kuliko ilivyokuwa hivi sasa.

"Inahitajika nguvu kubwa ili kuongeza idadi ya wanachama na tunapokuwa na wanachama wengi itatusaidia kuleta maendeleo makubwa sana kwetu "Alisema Nyanda.

Akizungumza suala la usajili katika timu hiyo,Nyanda alisema uongozi ulikubaliana mchezaji yoyote ambaye anataka kusajiliwa kwao lazima afanye majaribio lengo likiwa ni kuepuka kupata wachezaji ambao sio msaada katika msimu wa ligi utakapoanza.

Aliongeza kuwa hivi sasa technologia ya kuonyesha mpira Tanzania ni kubwa na kueleza mfumo wa TV unaotaka kutimika hivi sasa tenda zake ziliwashirikisha watu gani kwenye usimamizi wa ligi na kueleza pesa ambazo zilitolewa zinatakiwa zigawiwe kwa utofauti kutokana na idadi ya mashabiki walionao klabu zinazoshiriki ligi hiyo.

  "Ukiangali klabu kama Yanga ina mashabiki na wapenzi zaidi Milioni 10 halafu unataka kuipa gawiwo sawa na klabu nyengine ambazo hazina hata mashabiki wanaolingana na timu hiyo "Alisema Nyanda.

Katika ufunguzi wa tawi hilo kulifanyika harambee ambapo zilipatikana 250,000 ambazo kati ya hizo ahadi ni sh.170000 na pesa taslimu zilipatikana sh.80,000.

Awali akizungumza katika ufunguzi wa tawi hilo,Katibu wa CCM Mkoa wa Tanga,Gustav Mubba aliwataka wanachama hao kudumisha umoja, mshikamano na amani lengo likiwa kuhakikisha wanaisapoti timu yao ili iweze kufanya vizuri pamoja na kujiepusha na migogoro isiyo na tija.

Tawi la Yanga Umoja ni Nguvu linawachama wapatao 105 waliojiunga kutoka maeneo mbalimbali wilayani hapa .
Mwisho.

HIZI NDIVYO ILIVYOKUWA KATIKA UFUNGUZI WA TAWI LA YANGA TANGA.

August 04, 2013
MJUMBE WA KAMATI YA UTENDAJI YANGA,ARONI NYANDA AKIZUNGUMZA NA MMOJA WA WANACHAMA WA YANGA MKOA WA TANGA MARA BAADA YA KUWASILI MIZANI JANA.

MJUMBE WA KAMATI YA UTENDAJI YANGA ARONI NYANDA AKIFUNGUA TAWI LA YANGA TANGA JANA.

U
ARONI NYANDA AKIFUNGUA TAWI LA YANGA TANGA MWISHONI MWA WIKI.

MJUMBE WA KAMATI YA UTENDAJI YANGA ARONI NYANDA AKIWA KATIKA PICHA YA PAMOJA NA VIONGOZI NA WANACHAMA WA YANGA TANGA.

WANACHAMA NA WAPENZI WA KLABU YA YANGA TANGA WAKIMSIKILIZA MJUMBE WA KAMATI YA UTENDAJI ARONI NYANDA WAKATI ALIPOKUWA AKIWAHUTUBIA JANA MARA BAADA YA UFUNGUZI WA TAWI HILO LA UMOJA NI NGUVU MKOANI TANGA.