VIJANA WATAKIWA WASIPISHANE NA FURSA KWENDA NJE YA NCHI NA KUWAACHIA WAGENI

September 24, 2017
  Kamishna wa Polisi Mussa Ali Mussa, akiwa amebeba mfano wa picha ya ndege wa kuashiria amani, kwa niaba ya Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Simon Sirro ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye Maadhimisho ya Siku ya Amani Duniani-Tanzania yaliyofanyika leo Viwanja vya Mwembe Yanga jijini Dar es Salaam.
 Maandamano ya kuadhimisha siku hiyo yakifanyika.
 Wanafunzi wakiwa kwenye maadhimisho hayo.
 Wawakilishi mbalimbali na viongozi wa dini  wakiwa wamebeba mfano wa ndege huyo.
 Maadhimisho yakiendelea.
 Sheikh Hemed Bin Jalala akizungumzia umuhimu wa amani nchini
 Afisa Habari Kitengo Cha Habari cha Umoja wa Mataifa-UNIC, Stella Vuzo, akizungumzia ushiriki wa UNIC katika kudumisha amani.
 Wanahabari wakiwa kazini katika maadhimisho hayo.
 Wananchi wakishuhudia maadhimisho hayo.
 Wasanii wakionesha umahiri wa kucheza na nyoka katika maadhimisho hayo.
 Kiongozi wa Chama cha Scout Tanzania, Kamishna Mkuu Msaidizi Kazi Maalum, Mary Anyitike akiwa na vijana wake kwenye maadhimisho hayo.
 Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa na Mkuu wa Shirika la UN linaloshughulikia wahamiaji la IOM,  Dk. Quasim Sufi, akihutubia. Kutoka kulia ni Kamishna Mwandamizi wa Polisi, Suzan Kaganda, Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam SACP, Lazaro Mambosasa, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, Kamishna Msaidizi (ACP), Emanuel Lukuya na  Kamishina wa Polisi Mussa Ali Mussa.
  Kamishina wa Polisi Mussa Ali Mussa, akihutubia.
 Maadhimisho yakifanyika

Scout wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi na viongozi mbalimbali.

Na Dotto Mwaibale

VIJANA wametakiwa wasipishane na fursa kwa kwenda nchi ya nchi kuzitafuta wakati wenzao wa nchi hizo wakija kunufaika nazo hapa nchini.

Rai hiyo imetolewa na Kamishina wa Polisi Mussa Ali Mussa wakati akihutubia kwa niaba ya Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Simon Sirro ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye Maadhimisho ya Siku ya Amani Duniani-Tanzania yaliyofanyika leo Viwanja vya Mwembe Yanga jijini Dar es Salaam.

"Vijana acheni mipango ya kwenda kuzitafuta fursa nje ya nchi kwani wenzenu kutoka nchi hizo wamekuwa wakija kunufaika nazo hapa nchini" alisema Mussa.

 Alisema serikali imeweka mazingira mazuri hivyo ni vizuri hali hiyo ikatumika kwa ajili ya kufanya shughuli za maendeleo hasa katika wakati huu nchi ikiingia katika uchumi wa viwanda.

Aliwataka wazazi na walezi kutoa malezi bora kwa watoto wao ili kuwaepusha kujiingiza katika makundi yasiofaa.

Katika hatua nyingine Kamishna Mussa alisema amani ya nchi itadumishwa na kila mtu na kuwa watu waondoe dhana ya kuwa amani hiyo italetwa na vyombo vya dola ikiwemo polisi.

Alisema suala la amani si la mtu mmoja bali ni la kila mtu jeshi la polisi kazi yake ni kuilinda na kumkamata mtu yeyote anayeonekana kusababisha viashiria vya kutoweka kwa amani hiyo.

Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa na Mkuu wa Shirika la UN linaloshughulikia wahamiaji la IOM,  Dk. Quasim Sufi alisema amani ni jambo la muhimu kwa nchi na mustakari wa maendeleo.

Alisema bila ya amani hakuna kitu kitakacho weza kufanyika na ndio maana UN imekuwa ikisisitiza amani duniani kote.Sheikh Hemed Bin Jalala alisema amani ndiyo msingi wa dini zote ya kiislam na kikristo na kuwa amani haipaswi kuchezewa kwani ndio neema tuliyopewa na mwenyezi mungu.

Jalala alisema amani ni msingi wa dini uliojengwa kiimani na kutakiwa kuihubiri na kuwa wale wanaohubiri vita na machafuko wanatoka katika dini ya mashetani.Afisa Habari Kitemgo Cha Habari cha Umoja wa Mataifa-UNIC, Stella Vuzo aliwataka vijana kuendelea kuidumisha amani iliyopo nchini kwani wao ndio rahisi kurubuniwa kutokana na kuwa wengi.

"Katika maadhimisho ya siku ya amani duniani tunapenda kuwashirikisha vijana kutokana na wingi na umuhimu wao katika kutunza amani" alisema Vuzo.Alisema vijana watumie fursa ya amani iliyopo nchini katika kufanya shughuli zao za  maendeleo badala ya kukaa bure.

Vuzo alisema Kauli Mbiu ya maadhimisho hayo mwaka huu ni  " Pamoja Katika Kudumisha Amani: Heshima, Usalama na Utu kwa wote"

Maadhimisho hayo yameandaliwa na Umoja wa Mataifa kwa kushirikiana na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na taasisi mbalimbali kama  Global Peace Tanzania, Global Network of Religions for Children- GNRC, Chama cha Scout Tanzania, Asasi ya Vijana wa Umoja wa mataifa YUNA Tanzania, wanafunzi na wananchi.

TAMASHA LA SANAA NA UTAMADUNI LA KIMATAIFA BAGAMOYO LADHAMIRIA KULETA TIJA ZAIDI KWA WASANII WA NDANI NA NJE YA NCHI

September 24, 2017
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (wapili kushoto) akiwasili na kupokelewa na Mtendaji Mkuu Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) Dkt. Herbert Makoye (kulia) wakati wa uzinduzi wa Tamasha la 36 la Sanaa na Utamaduni la kimataifa Bagamoyo Jana katika Taasisi hiyo. Kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya ushauri ya TaSUBa Bw. George Yambesi.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (wapili kulia) akimsikiliza mjasiriamali wa kazi za sanaa kutoka Dar es Salaam Bibi. Magreth Kabonge (kushoto) alipotembelea banda lake kabla ya kufungua Tamasha la 36 la Sanaa na Utamaduni la kimataifa Bagamoyo jana katika Taasisi ya TaSUBa. Kulia ni Mtendaji Mkuu Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) Dkt. Herbert Makoye.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (kulia) akiangalia moja ya kazi za sanaa iliyotengenezwa na mbunifu kutoka Arusha Bi. Joyce Lema (kushoto) alipotembelea banda lake kabla ya kufungua Tamasha la 36 la Sanaa na Utamaduni la kimataifa Bagamoyo jana katika Taasisi ya TaSUBa.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (kulia) akionyesha picha yenye mfano wa sura yake iliyochorwa na kalamu ya risasi na mwanafunzi kutoka Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) Bw. Baraka Jeje (kushoto) alipotembelea banda lake kabla ya kufungua Tamasha la 36 la Sanaa na Utamaduni la kimataifa Bagamoyo jana katika Taasisi ya TaSUBa.
Baadhi ya wanafunzi kutoka Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) wakiimba wimbo wa taifa wakati wa uzinduzi wa Tamasha la 36 la Sanaa na Utamaduni la kimataifa Bagamoyo jana katika Taasisi hiyo.
Wanafunzi kutoka Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) wakicheza ngoma wakati wa uzinduzi wa Tamasha la 36 la Sanaa na Utamaduni la kimataifa Bagamoyo jana katika Taasisi hiyo.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe akizungumza wakati wa uzinduzi wa Tamasha la 36 la Sanaa na Utamaduni la kimataifa Bagamoyo jana katika Taasisi ya TaSUBa.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (watatu kulia) akishirikiana na Mtendaji Mkuu kutoka Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo Dkt. Herbert Makoye (wapili kulia), Katibu Tawala Wilaya ya Bagamoyo Mhe. Erica Yegelea (watatu kushoto), Mtendaji Mkuu Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Bw. Godfrey Mngereza (kulia) na Mbunge wa Jimbo la Bagamoyo Mhe. Shukuru Kawambwa (wapili kushoto) kukata keki kuashiria uzinduzi wa Tamasha la 36 la Sanaa na Utamaduni la kimataifa Bagamoyo jana katika Taasisi ya TaSUBa. Picha na: Genofeva Matemu - WHUSM

Bodi ya Ushauri ya Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) imeagizwa kukaa na kufanya tathmini ya kina kuandaa mpango mkakati mzuri wa namna ya kuliendesha tamasha la Sanaa na Utamaduni ili liweze kuwa na tija zaidi kwa wasanii na Taasisi kwa ujumla.

Rai hiyo imetolewa na Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe wakati wa uzinduzi wa tamasha la 36 la Sanaa na Utamaduni la kimataifa Bagamoyo jana katika Taasisi hiyo mjini Bagomoyo. “Tangu kuanzishwa kwa tamasha hili mwaka 1982, Tamasha limeendelea kuwa kivutio kikubwa kwa wasanii na wadau wa sanaa ndani na nje ya nchi na wananchi kwa ujumla hivyo ni vyema Bodi ya ushauri ya TaSUBa ikapanga mikakati yenye tija zaidi kwa maslahi ya wasanii wetu na Taasisi yetu” amesema Mhe. Mwakyembe.

Aidha Mhe. Mwakyembe ameipongeza Bodi, Menejimenti, wafanyakazi na wanachuo wote wa TaSUBa kwa kazi kubwa wanayoiofanya kila mwaka ya kuandaa na kuendesha Tamasha hilo kwa kipindi cha miongo mitatu na nusu mfululizo na kuwataka kutembea kifua mbele kwa rekodi hiyo iliyotukuka ndani na nje ya nchi.

Mhe. Mwakyembe amesema kuwa lengo la Tamasha hilo ni pamoja na kutunza na kuenzi sanaa na utamaduni wa mtanzania, kutengeneza jukwaa ambalo wanafunzi wa TaSUBa wanalitumia kupima kiwango chao cha umahiri katika sanaa kwa mwaka, kukutanisha watu wa tamaduni mbalimbali kutoka sehemu tofauti duniani ili kuonyesha utajiri wao wa sanaa na utamaduni, pamoja na kutengeneza jukwaa ambalo ni kiungo cha kujenga mahusiano ya wasanii wa ndani na nje ya nchi kupitia maonyesho ya sanaa na kubadilishana uzoefu na uwezo katika kuendeleza tasnia ya sanaa.

Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) Dkt. Herbert Makoye amesema kuwa taasisi inajivunia mafanikio makubwa wanayoendelea kuyapata kupitia tamasha hilo kwani kwa sasa tamasha linajumuhisha wasanii wa ndani na nje ya nchi pamoja na wanafunzi waliosoma katika taasisi hiyo miaka ya nyuma na waliopo mafunzoni.

Aidha Dkt. Makoye amewashukuru wakazi wa Bagamoyo kwa ushirikiano ambao wamekua wakiuonyesha katika kushirikiana na Taasisi kuendeleza na kuthamini sanaa na utamaduni wa mtanzania.

Naye Chifu wa Unyanyembe na Mwenyekiti wa Chama cha Machifu Tanzania Mhe. Msagati Fundikira amewapongeza watendaji wa TaSUBa kwa kutoa wataalamu wazuri katika fani ya sanaa na utamaduni kwani kwa ufanya hivyo wamekua wakiendeleza na kudumisha utamaduni wa mtanzania kwa vizazi vya leo.

Tamasha hili la 36 la Sanaa na Utamaduni la kimataifa la Bagamoyo lenye kauli mbiu isemayo “Sanaa na Utamaduni katika kupiga vita madawa ya kulevya” limeshirikisha wasanii kutoka Kenya, Ufaransa, Uingereza, Zimbabwe na Mayyote na kuudhuriwa na mabalozi mbalimbali akiwemo balozi wa Malawi, balozi wa Palestina, balozi wa uholanzi, pamoja na wawakilishi kutoka ubalozi wa Zambia, Saudi Arabia, Msumbiji, Japani, Ujerumani, Marekani, India, Shirikisho la Urusi, Angola na Kenya.

DK.SHEIN AWAAPISHA VIONGOZI MBALI MBALI LEO

September 24, 2017
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akimuapisha Dkt,Idris Muslim Hija kuwa Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais,hafla iliyofanyika leo katika ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar,kabla ya Uteuzi huo alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja,[Picha na Ikulu.] 24/09/2017.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akimuapisha Bw.Joseph Abdalla Meza kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo,Maliasili,Mifugo na Uvuvi,hafla iliyofanyika leo katika ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar,kabla ya Uteuzi huo alikuwa Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais,[Picha na Ikulu.] 24/09/2017.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akimuapisha Bw.Juma Ali Juma kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Biashara,Viwanda na Masoko,hafla iliyofanyika leo katika ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar,kabla ya Uteuzi huo alikuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo,Maliasili,Mifugo na Uvuvi
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akimuapisha Bw.Bakari Haji Bakari kuwa Katibu Mtendaji wa Bazara la Biashara la Zanzibar hafla iliyofanyika leo katika ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar,kabla ya Uteuzi huo alikuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Biashara,Viwanda na Masoko,[Picha na Ikulu.] 24/09/2017.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akimuapisha Bw.Ali Khamis Juma kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Biashara,Viwanda na Masoko,hafla iliyofanyika leo katika ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar,kabla ya Uteuzi huo alikuwa Naibu Katibu Wizara ya Fedha na Mipango,[Picha na Ikulu.] 24/09/2017.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akimuapisha Bw.Iddi Haji Makame kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, hafla iliyofanyika leo katika ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar,[Picha na Ikulu.] 24/09/2017. 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akimuapisha Bw.Abeid Juma Ali kuwa Mkuu wa Wilaya ya Wete Pemba katika hafla iliyofanyika leo ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar,kabla ya uteuzi huo alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba[Picha na Ikulu.] 24/09/2017. 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akimuapisha Bw.Rashid Hadid Rashid kuwa Mkuu wa Wilaya ya Chakechake Mkoa wa Kusini Pemba katika hafla iliyofanyika leo ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar,kabla ya uteuzi huo alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba[Picha na Ikulu.] 24/09/2017. 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akimuapisha Bibi Salama Mbarouk Khatibu kuwa Mkuu wa Wilaya yaMicheweni Pemba katika hafla iliyofanyika leo ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar,kabla ya uteuzi huo alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Chakechake Mkoa wa Kusini Pemba[Picha na Ikulu.] 24/09/2017.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akimuapisha Kapteni Khatib Khamis Mwadini kuwa Mkuu wa Wilaya ya Magharibi A.Unguja, hafla iliyofanyika leo katika ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar,[Picha na Ikulu.] 24/09/2017.

SERIKALI KUTATUA CHANGAMOTO YA KODI SHULE BINAFSI

September 24, 2017
Benny Mwaipaja, WFM, Pwani

SERIKALI imeahidi kuyafanyiakazi malalamiko ya wamiliki wa shule za binafsi nchini kuhusu kodi mbalimbali wanazotozwa kwa kuwa Serikali inathamini mchango mkubwa wa taasisi binafsi za elimu katika mapambano dhidi ya adui ujinga.

Ahadi hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji, wakati wa sherehe za mahafali ya kumi ya kidato cha nne katika Shule ya Sekondari Baobab, iliyoko Mapinga, Wilayani Bagamoyo, mkoani Pwani.

Dokta Kijaji amesema kuwa tayari Serikali imeondoa baadhi ya kodi kwa shule hizo ikiwemo kodi ya mabango, Usalama mahali pa kazi-OSHA, Ada ya zimamoto, na kwamba kikosi kazi kilichoundwa na Serikali kupitia upya kodi zingine zinazoonekana kuwa kikwazo katika utoaji wa elimu, kinaendelea na kazi na matokeo yake yataonekana hivi karibuni.

“Niko kwenye kikosikazi kinachoshughulikia changamoto za kodi kwenye shule za watu binafsi ninaamini suluhisho litapatikana kutokana na Serikali kuthamini mchango wenu mkubwa katika kuwapatia vijana wetu elimu” alisema Dkt. Kijaji

Alieleza kuwa katika Bajeti Kuu ya Serikali ya mwaka 2017/2018, suala hilo litazingatiwa na kuwataka wamiliki wa shule binafsi nchini kuwa watulivu wakati jambo hilo linafanyiwakazi tena kwa umakini mkubwa.

Awali Mwanzilishi na Mkurugenzi wa Shule ya Sekondari Baobab, Bw. Halfan Swai, pamoja na kuiomba Serikali ifute kodi mbalimbali wanazotozwa kwa kuwa hawafanyibiashara bali wanaisaidia Serikali kutoa huduma kwa jamii, ameomba pia isaidie  kuangalia viwango vya riba vinavyotozwa na taasisi za fedha nchini kwa kuwa zinawawekeka katika mazingira magumu wanapohitaji mikopo ya kuendeleza shule zao.

Wanafunzi 149, (wavulana 14 na wasichana 135)  wa Shule hiyo wanaotarajiwa kuhitimu masomo yao ya kidato cha nne hivi karibuni, wameahidi kufanya vizuri katika mitihani yao kwa kuwa wameandaliwa vizuri na walimu waliobobea katika ufundishaji pamoja na mazingira mazuri ya kufundishia na kujifunzia shuleni hapo.

Dokta Ashatu Kijaji, mbali na kuwa mgeni rasmi katika mahafali hayo, yeye na familia yake wameshuhudia mtoto wao Samira, akiagwa wakati wa mahafali hayo yaliyohudhuriwa na watu mbalimbali wakiwemo wazazi, ndugu na jamaa wa wanafunzi hao.
Meza Kuu ikiongozwa na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) (Katikati), wakiimba Wimbo wa Taifa wakati wa Mahafali ya 10 ya Kidato cha Nne ya Shule mchanganyiko ya Sekondari Baobab, iliyoko eneo la Mapinga, Wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani, ambapo wanafunzi 149 wanatarajiwa kuhitimu masomo yao majuma machache yajayo.
Mwanzilishi na Mkurugenzi wa Shule ya Sekondari Baobab Bw. Halfan Swai, akiiomba Serikali iangalie changamoto ya riba ya mikopo inayotolewa an taasisi za fedha pamoja na kuondoa kodi mbalimbali zinazotozwa shule binafsi kwakuwa taasisi hizo zinaisaidia Serikali kutoa huduma kwa wananchi wake, wakati wa Mahafali ya 10 ya Kidato cha Nne ya Shule hiyo.
Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari Baobab, wakionyesha ishara ya umoja, upendo na mshikamano wakati wakiimba wimbo wa kuwaaga wanafunzi wenzao wakati wa Mahafali ya 10 ya Kidato cha Nne ya shule yao.
Mgeni Rasmi katika Mahafali ya 10 ya Shule ya Sekondari Baobab, Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), akihutubia Jumuiya ya Shule ya Sekondari Baobab, wakati wa mahafali ya kuwaaga wanafunzi wa Kidato cha Nne wanaotarajiwa kufanya mitihani yao siku chache zijazo.
Mgeni Rasmi katika Mahafali ya 10 ya Kidato cha Nne ya Shule ya Sekondari Baobab, Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), akimkabidhi zawadi mmoja wa wanafunzi mwenye ulemavu aliyefanya vizuri katika baadhi ya masomo wakati wa sherehe ya kuwaaga, iliyofanyika shuleni hapo.
Mgeni Rasmi katika Mahafali ya 10 ya Kidato cha Nne ya Shule ya Sekondari Baobab, Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), (Katikati), akikabidhi keki kwa wanafunzi wa Shule ya Sekondari Baobab, iliyoko Mapinga, Bagamoyo, mkoani Pwani, ikiwa ni alama ya kusherehekea siku yao ya kuagwa shuleni hapo.
Mgeni Rasmi katika Mahafali ya 10 ya Kidato cha Nne ya Shule ya Sekondari Baobab, Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), akiwa katika Picha ya pamoja na baadhi ya wanafunzi wa Kidato cha Nne wanaotarajiwa kuhitimu masomo yao hivi karibuni, wakati wa sherehe ya kuwaaga shuleni hapo.
Familia ya Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), akiwa na mumewe Dkt. Kachwamba, wakimpongeza binti yao Samira anayetarajiwa kuhitimu masomo yake ya Kidato cha Nne katika Shule ya Seondari Baobab, iliyoko Mapinga, Bagamoyo mkoani Pwani ambapo Naibu Waziri alikuwa Mgeni Rasmi katika Mahafali hayo ya 10 ya Kidato cha Nne. Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Wizara ya Fedha na Mipango.
JESHI LA POLISI LAFUNGA MAFUNZO YA UTAYARI KATIKA CHUO CHA POLISI KIDATU

JESHI LA POLISI LAFUNGA MAFUNZO YA UTAYARI KATIKA CHUO CHA POLISI KIDATU

September 24, 2017

1
Mkuu wa Utawala wa Jeshi la Polisi (DCP) Leonard Paulo (katikati),  akiwa ameongozana na Naibu Kamishna wa Polisi mstaafu (DCP) Venance Tossi (Kushoto) na Mkuu wa chuo cha Polisi Kidatu kilichopo mkoani Morogoro, kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Zarau Mpangule, wakati alipowasili katika chuo hicho kwa ajili ya kufunga mafunzo ya Utayari ya kuwajengea uwezo askari wakati wanapotekeleza majukumu yao.
2
Naibu Kamishna wa Polisi mstaafu (DCP) Venance Tossi (Kushoto), akizungumza jambo na Mkuu wa Utawala wa Jeshi la Polisi (DCP) Leonard Paulo (katikati),  muda mfupi kabla ya kufunga mafunzo ya Utayari ya kuwajengea uwezo askari wakati wanapotekeleza majukumu yao ya kazi za Polisi.
3
Mkuu wa Utawala wa Jeshi la Polisi (DCP) Leonard Paulo, akifanya mazoezi ya viungo na baadhi ya askari wanaoshiriki Mafunzo ya Utayari na kujengewa uwezo wakati wanapotekeleza majukumu yao ya kazi za Polisi, mafunzo yanayofanyika katika Chuo cha Polisi Kidatu Kilichopo mkoani Morogoro.
Picha na Jeshi la Polisi

TAMASHA LA TIGO FIESTA LATIKISA JIJI LA MWANZA JUMAMOSI HII

September 24, 2017
Ben Pol  na Maua Sama wakipagawisha  wakazi wa jiji la Mwanza katika Tamasha  la Tigo Fiesta usiku wa kuamkia jumapili katika viwanja vya CCM Kirumba.




Ommy Dimpoz akiburudisha wakazi wa jiji la Mwanza katika vviwanja via Tigo Fiesta mapema jana katika vviwanja vya CCM kirumba usiku wa kuamkia jumapili.

Alikba na Ommy dimpoz wakilishambulia jukwaa la Tigo fiesta mapema usiku wa jana katika vviwanja vya CCM kirumba 

GNAKO na JUX wakiwaburudisha maelfu ya wakazi wa Mwanza katika Tamasha la Tigo Fiesta.



Lulu DIVA akiwa na wacheza shoo wake wakitoa burudani ya kukata na shoka.

NanDy akiimba kwa hisia katika jukwaa la Tigo Fiesta mapema jana katika viwanja via CCM kirumba.



Maua Sama naye akilishambulia jukwaa la Tigo fiesta


Msanii wa bongo fleva Rayvanny akiwapa burudani wapenzi wa muziki kwenye tamasha la Tigo Fiesta katika uwanja wa CCM kirumba jijini Mwanza usiku wa kuamkia Jumapili.



Rosa Ree akipagawawisha maelfu ya wakazi wa Jiji la Mwanza.