DK SHEIN ATEUA MAKADHI WA WILAYA ZA UNGUJA NA PEMBA

October 10, 2014

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohammed Shein amefanya Uteuzi wa Makadhi wa Wilaya za Unguja na Pemba.
Kwa mujibu wa Taarifa iliyotolewa na Katibu wa Baraza la Mapinduzi ambaye pia ni Katibu Mkuu Kiongozi Dkt. Abdulhamid Yahya Mzee Makadhi hao ni Sheikh Ali Haruna Ramadhan-Unguja na Sheikh Abubakar Ali Mohamed-Unguja.
Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohammed Shein ameteua Makadhi wapya
Wengine ni Mohamed Ramadhan Khamis-Unguja na Sheikh Omar Juma Othman-Pemba.
Rais Shein amefanya Uteuzi huo kwa mujibu wa uwezo aliopewa chini ya kifungu namba 5 cha Sheria ya Mhakama ya Kadhi Namba 3 ya mwaka 1985 kama ilivyorekebishwa na Sheria namba 4 ya mwaka 2003. Uteuzi huo umeanza Septemba 12,2014
IMETOLEWA NA HABARI MAELEZO ZANZIBAR

*MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL ASHIRIKI HAFLA YA CHAKULA CHA JIONI CHA HISANI KUCHANGIA MFUKO WA KAMPENI WA JITOLEE KWA AJILI YA KINAMAMA WA AFRIKA, JIJINI DAR

October 10, 2014
 Makamua wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wakati wa hafla ya Chakula cha Hisani kwa ajili ya kuchangia Mfuko wa Kampeni ya Jitolee kwa ajili ya Akinamama wa Afrika, iliyofanyika kwenye Hoteli ya Serena jana usiku Oktoba 9, 2014 jijini Dar es Salaam.
 Baadhi ya wadau, wageni waalikwa waliohudhuria hafla hiyo.

Baadhi ya wadau, wageni waalikwa waliohudhuria hafla hiyo.
 Baadhi ya wadau, wageni waalikwa waliohudhuria hafla hiyo.
Baadhi ya wadau, wageni waalikwa waliohudhuria hafla hiyo.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa meza kuu na baadhi ya viongozi wakati wa hafla hiyo.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Meneja wa  Mpango wa Kujenga Uwezo katika mradi wa Uzazi Uzima wa Amref, Dkt. Pius Chaya (kushoto) wakati alipokuwa akielezeewa kuhusu miradi inayosimamiwa na Amref Afrika, katika hafla ya Chakula cha Hisani kilichoandaliwa kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam jana usiku kwa ajili ya kuchangia Mfuko wa Kampeni ya Jitolee kwa ajili ya Akinamama wa Afrika. Kulia ni Mkurugenzi Mkazi wa Amref Health Afrika, Dkt. Festus Ilako. 
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Meneja wa  mradi wa Uzazi Uzima, Dkt. Benatus Sambili (wa pili kushoto) wakati alipokuwa akielezeewa kuhusu miradi inayosimamiwa na Amref Afrika, katika hafla ya Chakula cha Hisani kilichoandaliwa kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam jana usiku kwa ajili ya kuchangia Mfuko wa Kampeni ya Jitolee kwa ajili ya Akinamama wa Afrika.

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi Cheti, Mkurugenzi Mtendaji wa Push Mobile, Freddie Manento, wakati wa hafla ya Chakula cha Hisani kwa ajili ya kuchangia Mfuko wa Kampeni ya Jitolee kwa ajili ya Akinamama wa Afrika, iliyofanyika kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam, jana usiku Oktoba 9, 2014.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi Cheti, Mkurugenzi Mtendaji wa ITV na Redio One, Joyce Mhavile, wakati wa hafla ya Chakula cha Hisani kwa ajili ya kuchangia Mfuko wa Kampeni ya Jitolee kwa ajili ya Akinamama wa Afrika, iliyofanyika kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam, jana usiku.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi Cheti, Meneja Masoko Msaidizi wa Kampuni ya TOYOTA Tanzania, Eliavera Timoth, wakati wa hafla ya Chakula cha Hisani kwa ajili ya kuchangia Mfuko wa Kampeni ya Jitolee kwa ajili ya Akinamama wa Afrika, iliyofanyika kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam, jana usiku
 Baadhi ya kinamama wakiserebuka kucheza muziki maalum unaomtukuza mama, wakati wa hafla hiyo.
Baadhi ya kinamama wakiserebuka kucheza muziki maalum unaomtukuza mama, wakati wa hafla hiyo.
Picha ya pamoja kwa kumbukumbu na Makamu wa Rais.

Wadau wa Vijana washiriki mdahala katika Wiki ya Vijana mkoani Tabora

October 10, 2014

Mkurugenzi Msaidizi wa Maendeleo ya Vijana kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Steven Kissuiakizungumza katika mdahalo wa vijana leo mkoani Tabora ambapo mdahalo huo umefanyika ikiwa ni kuadhimisha Wiki ya Vijana ambayo kitaifa inafanyika mkoani hapa.
Mchumi Mkuu Sekretariat ya Mkoa wa Tabora Bw.Nicholas Kileka akitoa mada kuhusu ijue Tabora leo mkoani humo wakati wa mdahalo uliohusisha vijana mbalimbali wanaoshiriki maadhimisho ya Wiki ya Vijana ambayo kitaifa yanafanyika mkoani humo.
Afisa Vijana Mwandamizi kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Florent Karist akitoa mada kuhusu maudhui ya Wiki ya Vijana leo mkoani humo wakati wa mdahalo uliohusisha vijana mbalimbali wanaoshiriki maadhimisho ya Wiki ya Vijana ambayo kitaifa yanafanyika mkoani humo.
Baadhi ya Washiriki wa mdahalo wa Vijana katika kuadhimisha Wiki ya Vijana wakichangia mada katika mdahalo huo leo mkoani Tabora.
Baadhi ya Washiriki wa mdahalo wa Vijana katika kuadhimisha Wiki ya Vijana wakifuatilia mada katika mdahalo huo leo mkoani Tabora. Picha na Frank Shija, WHVUM.

*HABARI KUTOKA TFF LEO, MASTAA NYOTA WA BENIN WATUA DAR KUIKABILI STARS JUMAPILI

October 10, 2014
*NYOTA WA BENIN WATUA DAR
Kikosi cha wachezaji 18 na viongozi 11 wa timu ya Taifa ya Benin, kimetua jijini Dar es Salaam tayari kwa mechi ya Kalenda ya FIFA dhidi ya Taifa Stars itakayochezwa Jumapili (Oktoba 12 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. 
Wachezaji wa timu ya Benin ambayo imefikia hoteli ya JB Belmont waliwasili jana (Oktoba 9 mwaka huu) Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) kwa nyakati tofauti.
Kikosi hicho kitafanya mazoezi yake ya kwanza leo (Oktoba 10 mwaka huu) saa 10 jioni kwenye Uwanja wa Gymkhana. Benin watafanya mazoezi yao ya mwisho kesho (Oktoba 11 mwaka huu) saa 10 jioni Uwanja wa Taifa.
Wachezaji walioko kwenye kikosi cha Benin ni Stephane Sessegnon (West Bromwich Albion, Uingereza), Didier Sossa (USS Krake, Benin), Abdel Fadel Suanon (Etoile Sportive du Sahel, Tunisia), Jodel Dossou (Red Bull Salzburg, Austria), Sessi D’almeida (FC Girondis Bordeaux, Ufaransa), Mohamed Aoudou (JS Saoura, Algeria) na Saturnin Allagbe (Niort, Ufaransa).
Steve Mounie (Montpellier, Ufaransa), Farnolle Fabien (Clermont Foot Auvergne 63, Ufaransa), Jordan Adeoti (Caen, Ufaransa), Michael Pote (Omonia Nikosia, Cyprus), David Djigla (FC Girondis Bordeaux, Ufaransa) na Seidou Baraze (Kawkab Marrakech, Morocco).
Jean Ogouchi, Centre Mberie Sportif Club, Gabon), Nafiou Badarou (ASO Chlef, Algeria), Eric Tossavi (Avrankou Omnisport, Benin), Fortune Ore (USS Krake, Benin) na Seibou Mama (Aspac, Benin).
Nayo Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager leo (Oktoba 10 mwaka huu) itafanya mazoezi kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam saa 10 jioni.
Wakati huo huo, makocha wa Taifa Stars, Mart Nooij na wa Benin Didier Nicolle Olle watakuwa na mkutano na waandishi wa habari kesho (Oktoba 11 mwaka huu). Mkutano huo utafanyika saa 5 asubuhi kwenye ofisi za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) katika Jengo la PPF Tower.

*FDL YAANZA KUTIMUA VUMBI

Michuano ya Ligi Daraja la Kwanza (FDL) msimu wa 2014/2015 inaanza kutimua vumbi kesho (Oktoba 11 mwaka huu) katika viwanja tisa tofauti kwenye miji ya Moshi, Arusha, Musoma, Mwanza, Geita, Mbozi, Songea, Mufindi na Dar es Salaam.
Kundi A litakuwa na mechi kati ya Kimondo FC na Villa Squad itachezwa Uwanja wa Vwawa mjini Mbozi wakati Majimaji itaumana na Ashanti United (Uwanja wa Majimaji, Songea).
Nyingine ni Kurugenzi Mafinga na Tessema FC kwenye Uwanja wa Mufindi huku Friends Rangers ikioneshana kazi na Lipuli ya Iringa kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Dar es Salaam.
Kundi B ni Panone itaikabili Kanembwa JKT (Uwanja wa Ushirika, Moshi), Oljoro JKT itapambana na Polisi Dodoma (Uwanja wa Sheikh Kaluta Amri Abedi, Arusha), Polisi Mara na Rhino Rangers (Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Musoma).

Mechi nyingine ni kati ya Toto Africans na Mwadui itakayofanyika Uwanja wa CCM Kirumba, jijini Mwanza na Geita Gold na Burkina Faso (Uwanja wa Waja, Geita).
Mkutano wa kundi namba 1 la nchi za Afrika waendelea – Benki ya Dunia

Mkutano wa kundi namba 1 la nchi za Afrika waendelea – Benki ya Dunia

October 10, 2014
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa serikali Dr. Servacius Likwelile akisoma nyaraka za mkutano wa kundi namba 1 la nchi za Afrika- Benki ya Dunia ambao umefanyika leo hapa mjini Washington DC. Aliye kaa nyuma yake ni Kamishna wa Fedha za Nje Bw. Saidi Ngosha Magonya DSCI0059 
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa serikali Dr. Servacius Likwelile akisoma nyaraka za mkutano wa kundi namba 1 la nchi za Afrika- Benki ya Dunia ambao umefanyika leo hapa mjini Washington DC.
?????????? 
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa serikali Dr. Servacius Likwelile akisoma nyaraka za mkutano wa kundi namba 1 la nchi za Afrika- Benki ya Dunia ambao umefanyika leo hapa mjini Washington DC.
?????????? 
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa serikali Dr. Servacius Likwelile akifuatilia kwa makini mkutano wa kundi namba 1 la nchi za Afrika- Benki ya Dunia ambao umefanyika leo hapa mjini Washington DC.
…………………………………………………………
Na Ingiahedi Mduma-Washington D.C
Mkutano wa kundi namba 1 la nchi za Afrika hufanyika kila mwaka wakati wa mikutani ya Benki ya Dunia na IMF na unahusisha kundi la nchi za Benki ya Dunia ambazo zinapata mikopo nafuu kutoka IDA. IDA ni shirika au mfuko wa maendeleo kwa ajili ya kutoa mikopo nafuu kwa nchi zinazoendelea kwa kundi la Benki ya Dunia. Katika mikutano hii wanazungumzia zaidi masuala ya sera za kibenki na mambo ya utawala kama vile ajira , uchaguzi wa wenyeviti wa mikutano hiyo na kamati mbalimbali. Mkutano huo unaudhuriwa na Mawaziri wa Fedha. Kwa mwaka 2014 -16 Mwenyekiti atakuwa Waziri wa Fedha kutoka Ethiopia na Makamu wake anatoka Gambia. Viongozi hawa wataongoza mpaka mwaka 2016. Mwaziri wa Fedha ni Magavana na Matibu wakuu ni MaGavana mbadala, hivi ni vyeo vya uwakilishi kattika Benki ya Dunia. Akiongea katika mkutano huo mwenyekiti aliyemaliza muda wake alisema kuwa”tumepata Mkurugenzi Mtendaji mpya wa kundi la kwanza la nchi za Afrika ambaye anatoka visiwa vya Shelisheli na Mbadala wake anatoka Zimbabwe “ alisema. Akiendelea kuzungumza katika mkutano huo aliwaambia wajumbe kuwa anayemaliza muda wake anatoka Zambia na kuwa Viongozi hawa wanachaguliwa kwa kupigiwa kura na kila nchi. “Hawa watakuwa watendaji moja kwa moja kuanzia sasa na nafasi hizi zinapatikana kwa mzunguko.”alisisitiza.. Vilevile katika kundi hilo kutakuwa na kamati ya maendeleo ambayo itakuwa na mwenyekiti ambaye atatoka Uganda na wajumbe watatoka Tanzania, Namibia pamoja na Sierralion. Jambo lingune ambalo limeongelewa kwenye mkutano huo muhimu ni kwamba Benki itaendelea kutoa misaada ya fedha kwa nchi zinazoendelea toka kwenye mfuko wa IDA kwa kuzingatia vipaumbele vya nchi husika. Vilevile walisisistiza suala la gonjwa la EBOLA. Walielezea kuwa wataendelea kusaidia kupeleka misaada kwa nchi zinazokabiliwa na hilo tatizo. Pia Benki ya Dunia itaendelea kupeleka wafanyakazi kujifunza jinsi Benki ya Dunia inavyofanya kazi na kusisitiza kuwa ni muhimu kuchagua watu wazuri ambao wana uwezo ili wanaporudi nchini kwao waweze kutumia ujuzi wanao upata. Mwisho walimalizia kwa kusema kuwa Benki itaendelea kusaidia jitihada ambazo zinalenga matokeo makubwa sasa kwani hata wao wanafanya kazi kwa kuzingatia matwakwa ya BRN. Hivyo wanatagemea fedha zinazotolewa zitafanikisha kuwa na matokeo makubwa sasa.

MADEREVA WA MABASI YA UDA WAGOMA, ABIRIA WALAZIMIKA KUTEMBEA KWA MIGUU

October 10, 2014



Na Mwandishi wetu
MADEREVA wa Kampuni ya Usafiri Dar es Salaam (UDA), wanaofanya safari kati ya Mnazimmoja na Kivukoni jana waligoma kufanya kazi wakipinga agizo la uongozi kuwataka wapeleke hesabu ya sh 300,000 kwa siku.
Kutokana na mgomo huo abiria wanaosafiri katika njia hiyo, walipata usumbufu hadi pale ufumbuzi wa mgogoro huo ulipopatikana majira ya saa moja asubuhi.
Akizungumza niaba ya madereva na makondakta jijini Dar es Salaam, mmoja wa madereva, ambaye hakupenda jina lake liandikwe kwenye mtandao huu wa eddy blog, alisema, wamekuwa wakifanya kazi katika manyanyaso makubwa kuhusu hesabu.
Alisema sababu zilizowafanya wagome zimetokana na ukweli kwamba kutokana na ushindani wamagari katika njia hiyo, wanauhakika fedha hizo haziwezi kupatikana kirahisi.

“Sisi tunaulaumu uongozi wa kampuni hii kwani umekuwa ukiendeshwa kikabila na mabavu, pindi wafanyakazi tunapo hoji haki zetu za msingi,”alisema dereva hyo.

Alisema baada ya uongozi kupata taarifa kuwa wamegoma, alifikia mmoja wa viongozi katika eneo la Mmnazimmoja ambako walikuwepo madreva hao na kuwashawishi waanze kazi kwa kutumia hesabu ya awali ambayo ni sh 205,000.

Hata hivyo kiongozi huyo, aliwashangaza madereva hao pale alipowaambia kuwa wataanza kukusanya hesabu hiyo y ash 300,000 baada ya kuzisimamisha kampuni nyingine zinazotoa huduma hiyo katika njia hiyo.

“Unajua watu wakituona hivi wanajua tunalipwa vizuri kumbe wala sio hivyo kwa mfano makondakta wote hawakuajiriwa, tulioajiriwa ni sisi madereva ambao hata mshahara wenyewe hatuupati kwa wakati huku tukitakiwa kununua sare za kazi na kupeleka sh 5000 ya kuoshea gari kila siku,”alisema.

Aliongeza kuwa viongozi wa kampuni hiyo wamekuwa mara kwa wakitoa lugha za vitisho za kumfukuza kazi kila mfanyakazi anayepingana na maamuzi ya uongozi hata kama unakandamiza haki zao.

Akizungumzia kuhusu ajira katika kampuni hiyo, alisema kwa kuwa kiongozi mkuu wa kampuni hiyo anatoka Kanda ya Ziwa, hivyo nafasi nyingi za ajira zimekuwa zikienda kwa kabila la wasukuma.

Alipotafutwa msemaji wa UDA, George Maziku, kuyatolea ufafanuzi malalamiko hayo, alisema madereva wote waliojaribu kugoma wamewaondoa na kuwapeleka njia nyingine kauli ambayo imetofautiana na madereva.

Akisema madereva waliopelekwa baada ya kuondolewa hao waliopinga wamekubali kupeleka hesabu y ash 300,000.

“Kuhusu suala la ukabila huyo dereva aliyesema hivyo ni mpumbavu kama yeye siyo msukuma ungemuuliza ameingiaje, na hili la kuondolewa kampuni nyingine katika njia hii, hili halina ukweli wowote,”alisema Maziku.

WAZIRI MKUU AKAGUA TIMU ZA VIONGOZI WA DINI

October 10, 2014

*Ataka Watanzania wajitokeze kwa wingi Oktoba 12
 WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amewataka Watanzania wajitokeze kwa wingi kushangilia mechi ya viongozi wa dini wa mkoa wa Dar es Salaam itakayochezwa Jumapili, Oktoba 12, mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.
 Ametoa kauli hiyo leo asubuhi (Ijumaa, Oktoba 10, 2014) wakati akizungumza na wachezaji wa timu za AMANI na MSHIKAMANO zinazoundwa na Masheikh, Maaskofu, Maimamu na Wachungaji kutoka madhehebu mbalimbali ya mkoa wa Dar es Salaam ambao wamepiga kambi mjini Morogoro.
 “Hii haijapata kutokea… katika hali ya kawaida mkusanyiko kama huu siyo rahisi na katika nchi nyingine kupata mjumuiko kama huu haiwezekani,” alisema wakati akiongea nao kwenye viwanja vya michezo vya taasisi ya Highlands Baptist Mission iliyoko Kigurunyembe, Morogoro.
 Alisema uamuzi wa viongozi wa dini kukaa pamoja na kucheza mechi hiyo ni kutaka kuonyesha dhamira ya kweli ya kufanya mshikamano na amani kuwa ajenda ya kudumu kwa Taifa hili.
 “Mimi ninaamini kinachotuunganisha siyo dini bali ni kutambua kwamba sisi sote tumeumbwa na Mungu… sisi sote ni bin-adam. Dini ni milango tu ya kutusaidia tufike kule ambako Mwenyezi Mungu anataka tuende,” alisema.
 “Ukichukulia mfano wa wakristo, kuna madhehebu mengi. Kwa hiyo hawa wakigombana tayari ni tatizo. Hivyo uamuzi wa kuwachanganya katika timu ni jambo zuri, ni kudumisha umoja, amani na mshikamano,” aliongeza.
 “Hii ni hatua ya kwanza kinachofuata sasa ni kuwa na One Destiny, One People, One Nation,” akimaanisha kuwa na Lengo Moja, Watu Wamoja na Taifa Moja. Alisema hiyo ni kama sura ya kwanza imefunguliwa hivyo, hawana budi kuendelea mbele.
 Mapema, Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Sheikh Alhad Mussa Saleem alimweleza Waziri Mkuu kwamba timu hizo ziko kambini hapo tangu Jumatano, Mei 8, 2014.
Alisema leo baada ya mazoezi watakwenda kutembelea Hifadhi ya Taifa ya Mikumi na kurejea kambini Morogoro. Wanatarajia kurejea jijini Dar es Salaam kesho (Jumamosi) tayari kwa pambano lao la Jumapili, Oktoba 12, 2014.
 Waziri Mkuu ambaye aliwasili Morogoro jana mchana akitokea Dodoma, alifanya ziara ya siku kwa kutembelea Chuo Kikuu cha Sokoine na leo atatembelea Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Chuo Kikuu Huria kukagua miradi kama hiyo.
MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL ASHIRIKI HAFLA YA CHAKULA CHA JIONI CHA HISANI KUCHANGIA MFUKO WA KAMPENI WA JITOLEE KWA AJILI YA KINAMAMA WA AFRIKA, JIJINI DAR

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL ASHIRIKI HAFLA YA CHAKULA CHA JIONI CHA HISANI KUCHANGIA MFUKO WA KAMPENI WA JITOLEE KWA AJILI YA KINAMAMA WA AFRIKA, JIJINI DAR

October 10, 2014

02 
Makamua wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wakati wa hafla ya Chakula cha Hisani kwa ajili ya kuchangia Mfuko wa Kampeni ya Jitolee kwa ajili ya Akinamama wa Afrika, iliyofanyika kwenye Hoteli ya Serena jana usiku Oktoba 9, 2014 jijini Dar es Salaam. Picha na OMR
1  
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi Cheti, Mkurugenzi Mtendaji wa ITV na Redio One, Joyce Mhavile, wakati wa hafla ya Chakula cha Hisani kwa ajili ya kuchangia Mfuko wa Kampeni ya Jitolee kwa ajili ya Akinamama wa Afrika, iliyofanyika kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam, jana usiku Oktoba 9, 2014. Picha na OMR
9
Baadhi ya wadau, wageni waalikwa waliohudhuria hafla hiyo.