ZIARA YA NAIBU WAZIRI WIZARA YA NISHATI MH.SUBIRA MGALU MKOANI KILIMANJARO

February 06, 2018
Tarehe 24 - 26/01/2018 Mh. Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu ametembelea na kukagua utekelezaji wa Miradi ya umeme vijijini (REA II & REA III) kwenye jumla ya vijiji 18 katika wilaya za Rombo,Mwanga na Same Mkoani Kilimanjaro.

Katika ziara hiyo Naibu Waziri aliongea na wananchi, pia kutambulisha wakandarasi wa miradi ambapo aliwaagiza wakandarasi waepuke kurudia makosa yaliyojitokeza awali na kuhakikisha wanakamilisha kazi ndani ya muda uliopangwa.

Pia Katika ziara hiyo Mh. Naibu waziri alitembelea bwawa la kuzalisha umeme la Nyumba ya Mungu  kujionea shughuli za uzalishaji.

Mh Naibu waziri amemaliza ziara yake 26/01/2018 saa 12:00 jioni na kuelekea mkoani TANGA.

RCRO KILIMANJARO.

Mh. Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu akiwaeleza wananchi wa kijiji cha Mkisha kuhusu kifaa kijulikanacho kama UMETA (REDY BODY) kifaa hicho hutumika kama mbadala wa kusuka mifumo ya waya (wiring) ndani ya nyumba. Aliyeshika kifaa hicho ni Afisa uhusiano Tanesco Mkoani Kilimanjaro  Samuel Mandari.

 Mh. Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu akiwasikiliza wanakijiji na kueleza uhitaji wa huduma ya umeme.

Wanakijiji wakimsikiliza Mh. Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (hayupo pichani) akieleza uhitaji wa huduma ya umeme.


Mh. Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu, Mkuu wa wilaya ya Same Mh. Rosemary Senyamule, Kamati ya Ulinzi na usalama wilaya, wakiwa na viongozi wa Tanesco Mkoani Kilimanjaro walipo tembelea Kijiji cha Vunta wilayani Same.

RAIS MHE. DKT. MAGUFULI AFUNGUA KITUO CHA MAFUNZO MAALUM YA KIJESHI KILICHOPO MAPINGA MKOANI PWANI

RAIS MHE. DKT. MAGUFULI AFUNGUA KITUO CHA MAFUNZO MAALUM YA KIJESHI KILICHOPO MAPINGA MKOANI PWANI

February 06, 2018
2
Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akivuta utepe kuashiria ufunguzi wa Kituo cha Mafunzo Maalum ya Kijeshi kilichopo Mapinga, Bagamoyo Mkoani Pwani. Wa Pili kushoto anayevuta utepe ni Naibu Mkuu wa Idara ya Usimamizi wa Mafunzo kutoka tume Kuu ya Kijeshi ya China Meja Jenerali Yang Jian na wa kwanza kushoto anayepiga makofi ni Balozi wa China hapa nchini Wang Ke
1 3
Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi ya Wananchi wa Tanzania (CDF) Jenerali Venance Mabeyo mara baada ya kufungua Kituo hicho cha Mafunzo Maalum ya Kijeshi kilichopo Mapinga, Bagamoyo Mkoani Pwani
4
Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimshukuru Naibu Mkuu wa Idara ya Usimamizi wa Mafunzo kutoka tume Kuu ya Kijeshi ya China Meja Jenerali Yang Jian mara baada ya ufunguzi wa kituo hicho ambacho kimejengwa kwa msaada kutoka Jeshi la Ukombozi la watu wa China.
5
Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimsikiliza Waziri wa Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa Dkt. Husein Mwinyi wakati alipokuwa akiandika jambo katika hotuba yake.
7
Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia wananchi mara baada ya kufungua Kituo cha Mafunzo Maalum ya Kijeshi kilichopo Mapinga, Bagamoyo Mkoani Pwani.
8 9
Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Balozi wa China hapa nchini, Wang Ke mara baada ya kukifungua kituo hicho cha Mafunzo Maalum ya Kijeshi.
10
Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Naibu Mkuu wa Idara ya Usimamizi wa Mafunzo kutoka tume Kuu ya Kijeshi ya China Meja Jenerali Yang Jian mara baada ya kukifungua kituo hicho cha Mafunzo Maalum ya Kijeshi.
12
Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo wakati alipokuwa akizungumza na Mbunge wa Bagamoyo Dkt. Shukuru Kawambwa, Mbunge wa Chalinze Ridhiwan Kikwete pamoja na Mkuu wa mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo mara baada ya kufungua kituo hicho cha Mafunzo Maalum ya Kijeshi.
13
Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa Mapinga(hawaonekani pichani) waliokuwa wakiwasilisha kero mbalimbali za ardhi wakati alipokuwa akirejea jijini jijini Dar es Salaam mara baada ya kufungua kituo hicho cha Mafunzo Maalum ya Kijeshi kilichopo Mapinga mkoani Pwani.17
Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Makomandoo wa JWTZ ambao walishiriki katika mazoezi ya Kijeshi kabla ya ufunguzi wa kituo hicho.
18
Kikundi cha Ngoma za asili cha Makao makuu ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania kikitumbuiza wakati wa sherehe za ufunguzi wa kituo hicho cha Mafunzo maalum ya Kijeshi kilichopo Mapinga mkoani Pwani. PICHA NA IKULU

WAZIRI WA UJENZI NA UCHUKUZI WA LESOTHO ATEMBELEA MRADI WA DART

February 06, 2018
 Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), Bw. Hija Malamla akizungumza katika kikao cha pamoja kati ya wataalamu wa sekta ya barabara nchini na ujumbe wa Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi wa Serikali ya Lesotho uliko nchini kwa ziara ya mafunzo.
 Ofisa Mtendaji Mkuu wa Mabasi yaendayo haraka (DART), Eng. Ronald Lwakatare (aliyesimama) akifafanua jambo kwa ujumbe wa Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi wa Serikali ya Lesotho walipotembelea mradi huo.
 Mkuu wa Kitengo cha Manunuzi cha Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), Bw. Lyanga (wa pili kushoto) akiwasilisha mada kwa ujumbe wa Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi wa Serikali ya Lesotho walipotembelea ofisi za TANROADS jijini Dar es Salaam.
 Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi wa Lesotho, Mathabathe Hlalele (wa pili kulia) akisisitiza jambo kwenye kikao cha kubadilishana uzoefu kati ya ujumbe wa nchi hiyo na Tanzania.
 Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi wa Lesotho, Mhe. Lehlohonolo Moramotse (wa tatu kulia) akisisitiza jambo akiwa kwenye moja ya Mabasi yaendayo haraka (DART) alipotembelea mradi huo jijini Dar es Salaam. Wa pili kulia ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Mabasi yaendayo haraka (DART), Eng. Ronald Lwakatare.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Mabasi yaendayo haraka (DART), Eng. Ronald Lwakatare (katikati) akifafanua jambo kwa Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi wa Lesotho, Mhe. Moramotse (kulia) alipo tembelea kukagua mradi huo.

Imetolewa na Kitengo cha Habari na Mawasiliano Serikalini Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.

DK. KIGWANGALLA AFANYA MAZUNGUMZO NA MUWAKILISHI WA BENKI YA DUNIA NCHINI KWA AJILI YA KUBORESHA MRADI WA REGROW

February 06, 2018
Waziri wa Maliasili na Utalii Dk. Hamisi Kigwangalla (kulia) akizungumza na Muwakilishi wa Benki ya Dunia nchini Tanzania, Daniel Mira-Salama ambaye pia ni Mratibu wa Mradi wa REGROW kwa ajili ya kusimamia maliasili na kuendeleza utalii wa Ukanda wa Kusini ofisini kwake mjini Dodoma leo Januari 06, 2018 ambapo wamejadili mambo mbalimbali ya kuboresha mradi huo wakati wa utekelezaji. 

Miongoni mwa mambo waliyojadili ni kuboresha miundombinu ya barabara kuunganisha maeneo ya vivutio na miji ya ukanda huo pamoja na viwanja vya ndege ndani ya hifadhi viwe na hadhi na ubora wa kutua ndege kubwa ikiwemo za Air Tanzania. 

"Nawapongeza kwa mradi huu ambao ni mzuri sana kwenye uhifadhi lakini una mapungufu kidogo kwenye biashara ya utalii jambo ambalo ni muhimu kuangaliwa ili uwe na tija zaidi kwa jamii na taifa kwa ujumla" alisema Dk. Kigwangalla.

Alimuomba mratibu huyo kuona namna ya kubadilisha vipengele vya utekelezaji wa mradi huo ili uweze kuwa na tija zaidi hususan suala la miundombinu ya kuunganisha hifadhi mbalimbali za ukanda huo na miji ili kurahisisha usafiri wa kufikia vivutio hivyo kwa muda mfupi na kwa wakati.

Kwa upande wake mratibu huyo alisema jambo hilo linajadilika na kwamba uendelezaji wa maeneo hayo ni mtambuka ukihusisha Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi ambazo nazo zimeahidi kuboresha miundombinu ya maeneo hayo.

Mradi wa REGROW unatarajiwa kuzinduliwa rasmi tarehe 12 Februari mwaka huu Mjini Iringa na Mhe. Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan. Mwezi Agosti mwaka jana Serikali ya Tanzania ilisaini mkopo wa masharti nafuu wa Dola za Kimarekani Milioni 150 sawa na takriban bilioni 340 za Tanzania kwa ajili ya kuendeleza mradi huo.
Waziri wa Maliasili na Utalii Dk. Hamisi Kigwangalla (katikati) akisisitiza jambo wakati wa mazungumzo na Muwakilishi wa Benki ya Dunia nchini Tanzania, Daniel Mira-Salama ambaye pia ni Mratibu wa Mradi wa REGROW kwa ajili ya kusimamia maliasili na kuendeleza utalii wa Ukanda wa Kusini ofisini kwake mjini Dodoma leo Januari 06, 2018 ambapo wamejadili mambo mbalimbali ya kuboresha mradi huo wakati wa utekelezaji. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dk. Aloyce Nzuki. 
Waziri wa Maliasili na Utalii Dk. Hamisi Kigwangalla (kulia) akimsikiliza Muwakilishi wa Benki ya Dunia nchini Tanzania, Daniel Mira-Salama ambaye pia ni Mratibu wa Mradi wa REGROW kwa ajili ya kusimamia maliasili na kuendeleza utalii wa Ukanda wa Kusini ofisini kwake mjini Dodoma leo Januari 06, 2018 ambapo wamejadili mambo mbalimbali ya kuboresha mradi huo wakati wa utekelezaji. 
Waziri wa Maliasili na Utalii Dk. Hamisi Kigwangalla (kulia) akiagana na Muwakilishi wa Benki ya Dunia nchini Tanzania, Daniel Mira-Salama ambaye pia ni Mratibu wa Mradi wa REGROW kwa ajili ya kusimamia maliasili na kuendeleza utalii wa Ukanda wa Kusini ofisini kwake mjini Dodoma leo Januari 06, 2018 baada ya kujadili mambo kadhaa ya kuboresha mradi huo wakati wa utekelezaji. Katikati ni Mratibu wa mradi huo kutoka Tanzania, Someni Mteleka. (PICHA NA HAMZA TEMBA-WMU)

KATIBU WA CCM ELIREHEMA NASSAR NITAWASHUGHULIKIA WATENDAJI WA SERIKALI WANAKWAMISHA JUHUDI ZA RAIS

February 06, 2018
Katibu wa wilaya wa chama cha mapinduzi (CCM) wilaya ya Mufindi mkoani Iringa Elirehema Nassar akiwa kwenye ziara ya kusherekea miaka 41 ya chama hicho kwa kufanya shughuli mbalimbali za kijamii

Na Fredy Mgunda,Mufindi.

CHAMA cha mapinduzi wilaya ya Mufindi mkoani Iringa kimewataka viongozi wa halmashauri ya mji wa mafinga kufanyakazi kwa weledi unaotakiwa kuwatumikia wananchi katika kutatua changamoto zinazozuia kuleta maendeleo.

Hayo yamesemwa na katibu wa wilaya wa chama hicho Elirehema Nassar wakati wa kusikiliza kero za wananchi walipokuwa wanasherekea miaka 41 ya chama cha mapinduzi katika wilaya hiyo.

Nassar alisema kuwa mmezisikia kero za wananchi lakini hapa mnajibu kisiasa na sio kitaalamu,sasa naomba nipatiwe majibu ya kutosha na yenye ukweli na sio uongo mnaotudanya hapa.

“Hapa mnaleta siasa kwenye kero za wananchi sitaki kusikia siasa kwenu watendaji mnaulizwa maswali ya msingi ambayo ni kero za wananchi harafu mnajibu majibu mepesi hivyo haiwezekani” alisema Nassar

Nassar aliwataka viongozi wa serikali ya halmashauri ya mji wa Mafinga kuacha kukaa maofisini na badala yake wanatakiwa kwenda kutatua kero za wananchi waliokiweka madarakani chama cha mapinduzi hivyo achene kufanya kazi kimazoea

“Wiki nzima unamkuta mfanyakazi wa serikali yeye ni kupiga soga tu ofisi huku wananchi wanateseka na kero mbalimbali ambazo muda mwingine hazina tija hivyo nikibaini hili nitalala mbele na huyo mtumishi” alisema Nassar

Aidha Nassar amewataka wafanyakazi kubuni viradi iliyofanyiwa utafiti na iwe inatija kwa wananchi kwa ajili ya kuleta maendeleo ambayo yatadumu kwa miaka mingi.

“Mnaanzisha miradi ambayo haina tija mfano hapa mmeanzia mradi wa soko la kuchoma nyama lakini hakuna mwananchi au mfanyabiashara anajua jinsi gani ya kufanya biashara hiyo hivyo ni marufuku kufanya miradi ambayo sio shirikishi kwa wananchi” alisema Nassar.

Pia Katibu huyo aliwataka watumishi hao wa serikali kuhakikisha wanaenda kuwaelimisha wananchi kuhusu kodi wanazozita zilipwe kuliko kumwambia mwananchi alipe kodi ambayo hajui inatokana na nini na kwa nini analipa,lakini kukuwa na elimu ya kutosha hakutakuwa na migongano.

Sambamba na kuwaasa watumishi wa serikali Katibu Nassar aliwaambia wananchi na mafinga na wanachama wa CCM wa Wilaya ya Mufindi kuacha kujenga nyumba bila ya vibali vya serikali na mwisho wa siku mwananchi anakuja kupata hasara pale anapoambia abomoe kwani ikon je ya mipango miji.

Nao wananchi na Wanaccm wa Wilaya walitoa kero zao mbalimbli kwa watendaji wa Halmashauri ya Mji wa Mafinga,ambapo walizitaka kero hizo kama uchafu wa Mazingira kwa baadhi ya maeneo,huduma mbovu katika Hospitali ya Wilaya baadhi ya mitaa na kata moja kutokuwa na watendaji wa kabisa.

Nyingine ni baadhi ya shule za mshingi kukosa miundo mbinu kama matundu vyoo sanjali na upungufu wa vyumba vya madarasa, na tatizo la upatikanaji wa mbolea za kilimo sambamba na dawa ya kuulia wadudu waharibifu wanaokula mazao, na kuwataka  watendaji hao kushugulikia kero hizo haraka.

SERIKALI YATOA SIKU SABA WANANCHI WALIOVAMIA JUMUIYA HIFADHI WANYAMAPORI YA JUKUMU KUONDOKA

February 06, 2018
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga akizungumza waliovamia eneo la Mkesa ndani ya Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori ya JUKUMU iliyopo Morogoro vijijini wakati walipofanya ziara na Naibu Waziri wa Tamisemi, Joseph kakunda kutembelea eneo hilo kwa lengo la kuwasikiliza wananchi hao kwa ajili ya kujionea uharibifu unaoendelea katika eneo hilo . Wengine ni Naibu Waziri wa TAMISEMI, Joseph Kakunda (wa pili kulia) akiwa na Mkuu wa wilaya ya Morogoro,Regina Chonjo (katikati
Naibu Waziri wa TAMISEMI, Joseph Kakunda (katikati) akizungumza na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga ( kulia) pamoja na na Mkuu wa wilaya ya Morogoro,Regina Chonjo (kushoto) ofisis kwa mkuu wa wilaya hiyo kabla ya kuanza kwa ziara iliyofanyika jana ya kutembelea eneo la Mkesa liliopo ndani ya Jumuiya Hifadhi ya Wanyamapori ya JUKUMU kwa lengo la kuwasikiliza wananchi hao na kujionea uharibifu unaoendelea katika eneo hilo.
Naibu Waziri wa TAMISEMI, Joseph Kakunda akizungumza na wananchi waliovamia eneo la Mkesa ndani ya Jumiya Hifadhi ya Wanyamapori ya JUKUMU iliyopo Morogoro vijijini wakati walipofanya ziara na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga kutembelea eneo hilo kwa lengo la kuwasikiliza wananchi hao kwa ajili ya kujionea uharibifu unaoendelea katika eneo hilo . Wengine ni Naibu Waziri wa TAMISEMI, Joseph Kakunda (wa pili kulia) akiwa na Mkuu wa wilaya ya Morogoro,Regina Chonjo (katikatiNaibu Waziri wa TAMISEMI, Joseph Kakunda (wa pili kulia) Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga ( wa kwanza kulia) pamoja na na Mkuu wa wilaya ya Morogoro,Regina Chonjo ( wa pili kushoto) wakiangalia nyaraka feki iliyowasilishwa na miongoni mwa wananachi aliyedai kuwa yeye ni mkazi halali katiaka eneo hilo la Mkesa liliopo ndani ya Jumuiya Hifadhi ya Wanyamapori ya JUKUMU wakatia wa ziara iliyofanyika jana ikiwa na Manaibu wa wawili wa Maliasili na Utalii pamoja na wa TAMISEMI.Mkuu wa wilaya ya Morogoro akizungumza na wananchi waliovamia eneo la Mkesa lililopo ndani ya Jumuiya Hifadhi ya Wanyamapori ya JUKUMU iliyopo Morogoro vijijini wakati walipofanya ziara akiwa ameongozana na Manaibu wawili wa Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga pamoja na Naibu Waziri wa TAMISEMI, Joseph Kakunda wakati walipotembelea eneo hilo kwa lengo la kuwasikiliza wananchi hao na kujionea uharibifu unaoendelea katika .


Naibu Waziri wa TAMISEMI, Joseph Kakunda (wa pili kulia akiwa na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga ( wa kwanza kulia) pamoja na na Mkuu wa wilaya ya Morogoro,Regina Chonjo ( wa pili kushoto) wakimsikiliza miongoni mwa wananachi aliyedai kuwa yeye ni mkazi halali katika eneo hilo la Mkesa liliopo ndani ya Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori ya JUKUMU wakati wa ziara iliyofanyika jana kwa ajili ya kuwasikiliza wananchi hao na kujionea uharibifu unaoendelea katika .Baadhi wananchi wakiwasilikiliza Manaibu Waziri katika mkutano uliofanyiak jana katika eneo la Mkesa lililopo ndani ya Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori ya JUKUMU iliyopo Morogoro vijijini wakati wakati wa ziara kutembelea eneo hilo kwa lengo la kuwasikiliza wananchi hao na kujionea uharibifu unaoendelea katika .Naye Mwenyekiti wa Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori ya JUKUMU, Shaban Kolahili akisalimia na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga wakati Naibu Waziri huyo alipowasili katika kijiji cha Mbwade akiwa ameongozana naNaibu Waziri wa Tamisemi, Joseph Kakunda.
( PICHA ZOTE NA LUSUNGU HELELA- MNRT


Serikali kupitia Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii na wa TAMISEMI imetoa siku saba kwa wananchi waliovamia kwa kuendesha maisha yao na kufanya shughuli za kilimo pamoja na kulisha mifugo ndani ya Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori ya JUKUMU iliyopo katika Halmashuri ya Morogoro vijijini kuondoka katika hifadhi hiyo.

Hali hiyo inafuatia baada ya wananchi hao kwenda mjini Dodoma kuonana na Waziri Mkuu, Kassimu Majaliwa na kumuelezea malalamiko yao kuwa wao ni wakazi halali katika eneo hilo lakini hata hivyo Mkuu wa Wilaya ya hiyo, Regina Chonjo amekuwa akiwalazimisha kuondoka.

Kufuatia hali hiyo , Waziri Mkuu K Majaliwa alimuagiza Waziri wa Maliasili na Utalii pamoja na Waziri wa TAMISEMI kwenda huko kwa ajili ya kushughulikia tatizo hilo ambapo Mawaziri hao kutokana na kubwana na majukumu mengine waliwaagiza Manaibu Waziri wao kutembelea eneo. .

Katika ziara hiyo, Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga pamoja na Naibu Waziri wa TAMISEMI, Joseph Kakunda jana walitembelea eneo hilo na kujionea uharibifu unaoendelea.Katika ziarz hiyo Manaibu Waziri hao walizungumza na wananchi hao kwa kumtaka mwananchi yeyote mwenye nyaraka halali za kuishi katika eneo hilo aziwasilishe katika mkutano huo lakini hata hivyo hakuna mwananchi yeyote aliyeziwasilisha

Kutokana na wananchi hao kukiri kuishi kinyume na sheria katika eneo hilo la Hifadhi, Wananchi hao waliowaomba viongozi hao wapewe muda ili waweze kutafuta sehemu ya kuhamia kwa vile hawana sehemu ya kwenda,Kulingana uharibifu mkubwa waliojionea katika eneo hilo hali ya mazingira, Mnaaibu Waziri hao waliweza kuagiza mambo yafuatayo huyo. Kama.

Manaibu Waziri hao waliagiza kuwa materekta yote yatakayoonekana katika eneo hilo la hifadhi baada ya siku saba kupita yataifishwe.Pia, Waliagiza kuwa yakamatwe na hatimaye kupigwa mnada kwa mujibu wa sheria kwa mifugo yote itakayooneka katika eneo hilo la hifadhi.Aidha, Waliagiza kuwa mwananchi yeyote atakayekutwa ndani ya hifadhi hiyo baada ya siku saba kuwa atakamatwa na kufunguliwa mashtaka kwa kosa la kuvamia hifadhi.

Awali, Mkuu wa Wilaya hiyo, Regina Chonjo aliwaeleza Manaibu Waziri hao kuwa wananchi hao wamekuwa wakilima na kuchunga mifugo katika maeneo hayo hali iliyopelekea wanyamapori katika maeneo hayo kuhama.Naye Mwenyekiti wa Jumuiya ya JUKUMU, Shaban Kolahili ameiomba Wizara ya Maliasili na Utalii iwasaidie kuhakikisha kuwa hifadhi hhiyo inalindwa ili kuzuia vitendo vya ujangili na uvamizi unaoendelea ili kuwavutia wawekezaji ili hatimaye iweze kujitegemea.

Wananchi wa eneo hilo mnamo mwaka 2010 walituma maombi kwa Wizara ya Maliasili na Utalii ya kuomba wasaidiwe katika kulihifadhi eneo hilo ambalo hutumiwa na wanyapori kupimzika na kuzaliana

SERIKALI YAIPONGEZA HOSPITALI YA HUBERT KAIRUKI KWA UJENZI WA JENGO LA KISASA KUSAIDIA WAJAWAZITO

February 06, 2018

Mganga Mkuu wa Manispaa ya Kinodnoni, Dkt. Festo Dugange (kwanza) na  Mama Kokushubira Kairuki ambaye ni mke wa Marehemu Hubert Kairuki (wa pili)  wakiangalia ramani ya ujenzi wa kituo cha kisasa cha kuwasaidia watu wenye matatizo ya kupata ujauzito kwa njia ya kawaida kinachotarajiwa kujengwa na Hospitali ya Hubert Kairuki hivi karibuni Bunju jijini Dar es Salaam. 
Na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG
Serikali imetoa pongeza kwa Shirika la Afya na Elimu la Kairuki kupitia Hospitali ya Hubert Kairuki kwa kujipanga kujenga kituo cha kusaidia watu wenye matatizo ya kupata ujauzito kwa njia ya kawaida. Hayo yamesemwa Dar es Salaam na Mganga Mkuu wa Manispaa ya Kinodnoni, Dkt. Festo Dugange ambaye alimwakilisha Mkuu wa Wilaya Ya Kinondoni Ali Hapi kwenye uwekaji wa jiwe la msingi wa ujenzi wa kituo kitakachosaidia watu wenye matatizo ya kupata ujauzito kwa njia ya kawaida kitakachojengwa Bunju jijini Dar es Salaam ikiwa ni maadhimisho ya Miaka 19 ya Kumbukizi ya Pro. Hubert Kairuki ambaye alifariki Februari 2, 1999. "Hatua Moja nzuri sana kwa manispaa yetu, maana huduma hii itapatikana hapa nchini jambo ambalo linaleta faraja sana kwa kuboresha huduma za afya kwa vile awali huduma kama hizo zilikuwa zikipatikana nje ya bara la Afrika... Mungu ni mwema itapatikana Tanzania," alisema Dkt. Dugange. Nae Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Akinamama na Wajawazito wa Hospitali ya Hubert Kairuki, Dkt. Clementina Kairuki ambaye ni mtoto wa Marehemu Hubert Kairuki alisema kuwa tatizo hilo lipo dunia nzima, na shirika la afya duniani lilitoa takwimu milioni 48 wanachangamoto ya kupata watoto. Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Akinamama na Wajawazito wa Hospitali ya Hubert Kairuki, Dkt. Clementina Kairuki ambaye ni mtoto wa Marehemu Hubert Kairuki akielezea juu ya ujenzi wa kituo hicho cha kisasa.
Mkurugenzi wa Hospitali ya Hubert Kairuki, Dkt. Assey Mchomvu akisoma risala ya kumkaribisha mgeni rasmi ili aweze kujionea shughuli mbali mbali zilizokuwa zikiendeshwa na Shirika la Afya na Elimu la Kairuki (KHEN) kwa kipindi chote tokea Febriari 1-6, 2018 katika kuadhimisha Miaka 19 ya Kumbukizi ya Pro. Hubert Kairuki ambaye alifariki Februari 2, 1999. Kutoka kushoto ni Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Hubert Kairuki (HKMU), Professa Charles Mgone, Mama Kokushubira Kairuki ambaye ni mke wa Marehemu Hubert Kairuki pamoja na mgeni rasmi Mganga Mkuu wa Manispaa ya Kinodnoni, Dkt. Festo Dugange.
Wageni waliohudhuriwa sherehe hiyo.
Mganga Mkuu wa Manispaa ya Kinodnoni, Dkt. Festo Dugange akipatiwa huduma za afya wakati aliposhiriki kwenye uwekaji wa jiwe la msingi wa ujenzi wa kituo kitakachosaidia watu wenye matatizo ya kupata ujauzito kwa njia ya kawaida kitakachojengwa Bunju jijini Dar es Salaam ikiwa ni maadhimisho ya Miaka 19 ya Kumbukizi ya Pro. Hubert Kairuki ambaye alifariki Februari 2, 1999.
Huduma za afya zikitolewa bure kwa wananchi waliohudhuria maadhimisho hayo.
Mpiga picha wa Gazeti la Nipashe, Mpochi akipatiwa huduma. Mwandishi na mpiga picha wa Kajunason/MMG akipatiwa huduma.
-- Cathbert Angelo Kajuna, Founder and Mananging Director Kajunason Blog, P.O Box 6482, Dar es Salaam. Tel: +255 787 999 774 Alt: +255 765 253 445 www.kajunason.com "Everything is Possible Through Peace & Stability''