Waziri
wa Nchi Ofisi Waziri Mkuu Sera, Bunge,Kazi, Ajira,Vijana na wenye
Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama(kulia) akimkabidhi hundi ya shilingi
bilioni 1.5 zilizotolewa na NSSF kama mkopo kwa ajili ya upanuzi wa
kiwanda cha chaki Maswa, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya
Maswa, Dkt.Fredrick Sagamiko.
Na Stella Kalinga, Simiyu
Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) umekabidhi hundi ya shilingi bilioni 1.5 kwa
Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Maswa Mkoani Simiyu, fedha ambazo ni mkopo
kwa ajili ya upanuzi wa kiwanda cha Chaki Wilayani humo na kuongeza uzalishaji.
Hundi hiyo imekabidhiwa kwa Waziri wa Nchi Ofisi Waziri Mkuu Sera, Bunge,Kazi, Ajira,Vijana na
wenye Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama kwa niaba ya Serikali na Mkurugenzi Mkuu wa NSSF
Prof.Godius Kahyarara wilayani Maswa mkoani Simiyu.
Akizungumza wakati wa makabidhiano ya hundi hiyo Mkurugenzi Mkuu wa NSSF Prof.Godius
Kahyarara amepongeza Mkoa wa Simiyu kwa kutekeleza Sera ya Ujenzi wa Uchumi wa Viwanda
kwa vitendo na kuwataka viongozi wa mkoa huo kutokatishwa tamaa.
Amesema NSSF kama Shirika la Umma linatekeleza sera na maelekezo ya Serikali na wametoa
mkopo huo kwa Halmashauri ya Wilaya ya Maswa ili wafanye upanuzi wa kiwanda cha chaki na
kuongeza uzalshaji kwa kuwa suala la Viwanda ni la kipaumbele.
Mkurugenzi
Mkuu wa NSSF Prof.Godius Kahyarara(kushoto) akimkabidhi Waziri wa Nchi
Ofisi Waziri Mkuu Sera, Bunge,Kazi, Ajira,Vijana na wenye Ulemavu, Mhe.
Jenista Mhagama hundi ya shilingi bilioni 1.5 zilizotolewa na NSSF kama
mkopo kwa ajili ya upanuzi wa kiwanda cha chaki Maswa, (kulia) Mkuu wa
Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka.
Waziri wa Nchi Ofisi Waziri Mkuu Sera, Bunge,Kazi, Ajira,Vijana na watu wenye Ulemavu, Mhe.
Jenista Mhagama amesema kiwanda cha Chaki Maswa kimebeba ujumbe na dhana ya Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli ya kushikamanisha Uchumi wa
Viwanda na Maendeleo ya watu kwa sababu kinatumia malighafi ya hapa nchini.
Aidha, amesema kiwanda hiki kitawanufaisha Watanzania hususani vijana wa Mkoa wa Simiyu
ambao watafanya kazi moja moja katika kiwanda na wale wataohusika katika uchimbaji wa
malighafi ambayo inapatikana maeneo mengine hapa nchini.
Waziri wa
Nchi Ofisi Waziri Mkuu Sera, Bunge,Kazi, Ajira,Vijana na wenye Ulemavu,
Mhe. Jenista Mhagama akipokea taarifa ya Upembuzi yakinifu wa panuzi wa
kiwanda cha chaki cha Maswa kutoka kwa mtalaam wa Taasisi ya Masuala ya
Kiuchumi na Kijamii(ESRF), Deodatus Sagamiko.