WAZIRI MAKAMBA AKAGUA MIRADI INAYOFADHILIWA NA OFISI YAKE

WAZIRI MAKAMBA AKAGUA MIRADI INAYOFADHILIWA NA OFISI YAKE

January 01, 2017
kamba
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais – Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba akiongea na Diwani wa Kata ya  Buguruni Mhe.  Adam Fugame (katikati) wakati wa ziara ya kikazi ya kukagua ujenzi wa mfereji wa maji taka katika eneo la Ilala Bungoni
kamba-2
Sehemu ya Mfereji wa Maji taka unaojengwa eneo la Ilala Bungoni chini ya Ofisi ya Makamu wa Rais kupitia  Mradi wa Kuhimili Mabadiliko ya Tabianchi na  unafadhiliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa kuhusu Mazingira (UNEP).
kamba-3
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais – Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba akiongea na Wananchi wakazi wa Ilala Bungoni, mara baada ya
kamba-4
kukagua ujenzi wa mrefeji wa maji taka
Bw. Gervas wa Kampuni ya Dezo Civil Contractors Co. Ltd (kulia) akifanunua jambo kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais – Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba katika eneo la Temeke – Mtoni kwa Azizi Ali ambapo Kampuni hiyo imepewa kazi ya kusafisha na kujenga mfumo wa maji taka.
kamba-5
Mwakilishi wa UNOPS Bw Bernard Omondi akifanunua jambo kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais – Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba katika eneo la Temeke – Mtoni kwa Azizi Ali ambapo kazi ya kusafisha na kujenga mfumo wa maji taka inaendelea.
kamba-6
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Prof. Faustin Kamuzora ( wa tatu kutoka kulia) akifafanua jambo kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais – Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba mara baada ya ziara ya kukagua hatua za ujenzi kwa miradi inayosimamiwa na Ofisi ya Makamu wa Rais.  Kulia ni Bw. Kanizio Manyika Afisa Mazingira Mkuu na Msimamizi wa Mradi na Bw. Richard Muyungi Kaimu Mkurugenzi wa Mazingira.
……………..
Na Lulu Mussa
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais – Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba hii leo amefanyia ziara ya kikazi ya kukagua hatua za ujenzi katika miradi inayofadhiliwa na Ofisi yake.
Akiwa katika Wilaya ya Ilala, Waziri Makamba ametembelea ujenzi wa Mfereji wa kupitishia maji taka katika eneo la Ilala Bungoni na kuongea na wananchi wa eneo hilo.
Waziri Makamba ameugiza uongozi wa Dezo  Civil Constractors Co. Ltd kuhakikisha ujenzi wa Miundombinu ya maji taka katika Manispaa za Ilala na Temeke unakamilika kwa muda uliopangwa na kwa ubora wa hali ya juu kwa kuzingatia makubaliano yaliyopo katika mkataba.
“Nataka mradi huu uwe wa mfano kwa ubora na viwango vya hali ya juu, ikiwa ni jitihada za kukabiliana na athari za mabadiliko ya Tabianchi, kwa kuweka mfumo mzuri wa kukusanya maji taka na kuyaelekeza sehemu stahiki” Makamba alisisitiza.
Aidha, Waziri Makamba amewataka wakazi wanaozuka eneo hilo kuacha mara moja utupaji wa taka maji na taka ngumu katika mfereji huo unaojengwa, na kumuagiza Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala Bw. Palela Msongela kutoa adhabu kali kwa yeyote atakayekiuka agizo hilo.
“Kwa kupitia kamati za Mazingira za vitongoji na sheria ndogo ndogo mlizojiwekea hakikisheni kuwa hifadhi ya mazingira inazingatiwa kwa mstakabali wa vizazi vya sasa na vizazi vijavyo.”
Pia, Waziri Makamba amemuagiza Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala kuhakikisha Wakandarasi wanaopewa kazi za ukusanyaji wa taka, wanakuwa na vifaa na uwezo wa kutosha kwa kuhakikisha taka zote zinazolewa kwa wakati ili kuepuka mrundikano wa taka katika makazi ya watu.
“Natoa wito pia kwa vijana wa maeneo haya kuunda vikundi vidogo vya kuzoa taka ili kuwa chanzo cha ajira kwenu.” Makamba alisisitiza.
Waziri Makamba ameliagiza Baraza la Taifa La Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira –  NEMC kutembelea eneo hilo la Ilala Bungoni na kutoa maelekezo kwa Gereji bubu  zinazokiuka hifadhi na usimamizi wa Mazingira kwa kufanya shughuli zao pembezoni mwa mfereji unaojengwa.
Ujenzi wa Ukuta wa (Obama/Ocean Road na Kigamboni) na Miundombinu ya maji taka katika Manispaa za Ilala na Temeke unatekelezwa chini ya Ofisi ya Makamu wa Rais kupitia  Mradi wa Kuhimili Mabadiliko ya Tabianchi na  unafadhiliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa kuhusu Mazingira (UNEP). Aidha, Kampuni ya Dezo Civil Contractors ndio inafanya kazi ya ujenzi huu na kazi zinatarajiwa kukamilika mwezi Julai 2017.
Waziri Makamba katika ziara yake hii leo ametembelea Ilala Bungoni, Mtoni kwa Azizi Ali, Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere na Kutembelea eneo la Ujenzi wa Ukuta Barabara ya Obama.

WALEMAVU WA KIJIJI CHA LULANZI WAMLILIA MBUNGE RITTA KABATI

January 01, 2017
 Mbunge wa viti maalum mkoa waIringa(CCM) Rita Kabati akiongea na familia ya watu watano wenye ulemavu wa viungo alipowatembea katika kijiji cha Lulanzi kata ya Mtitu wilayani Kilolo mkoa wa Iringa wakati wa kuwasaidia msaada kukarabati nyumba yao pamoja na kuwapa vitu vingine vya kimsaada
Leah mwamoto mtoto wa mbunge wa jimbo la kilolo Vennance Mwamoto naye alishuhudia maisha magumu wanaoishi familia ya watu watano wenye ulemavu wa viungo alipowatembea katika kijiji cha Lulanzi kata ya Mtitu wilayani Kilolo mkoa wa Iringa na hapo aliposimama ndio choo kinachotumiwa na familia hiyo kwa sasa huku wakisubili ujenzi wa choo kipya kinachoendelea kujengwa kwa hisani ya mbunge Ritta kabati
 Hivi ni baadhi ya vifaa vilivyoletwa na mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Rita Kabati kwa ajili ya kuwasidia familia ya watu watano wenye ulemavu wa viungo alipowatembea katika kijiji cha Lulanzi kata ya Mtitu wilayani Kilolo mkoa wa Iringa

Na fredy mgunda,Iringa

FAMILIA ya watu watano wenye ulemavu wa viungo wamemuomba mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Rita Kabati kuendelea kuilea familia hiyo kama familia yake.

Akizungumza na blog hii mmoja wa wanafamilia hiyo,Elias Mpogole ambaye ni mlemavu alisema kuwa mbunge huyo amekuwa akiwasaidia toka siku ya kwanza walipokutana naye katika kijiji hicho cha Lulanzi.

“Zamani tulikuwa tunaishi kwenye nyumba ambayo inavuja haina dilisha wala mlango pia tulikuwa tunalala chini lakini mbunge Kabati katusaidia nyumba nzuri kama mnavyoiona waandishi,katuletea magodoro,mashuka,blanket na sasa ameanza kutujenga choo cha kisasa na ameshawalipa mafundi pesa zote ndio maana tunaomba anendelee kuwa na sisi.”Alisema Mpogole

Mpogole alishukuru msaada waliopatiwa na kuwataka wadau wengine waweze kujitokeza zaidi kuwasaidia kuwapatia vyakula na radio za kuwezakusikiliza nyimbo za dini.

Kwa upenda wake mbunge wa viti maalum mkoa waIringa(CCM) Rita Kabati ametoa msaada wa vitu mbalimbali ikiwemo ukarabati wanyumba kwa familia yenye watoto walemavu wanne wa kijiji cha Lulanzi kilichoko kata ya Mtitu wilayani Kilolo mkoa wa Iringa. 

Msaada huo wa ukarabati wa nyumba,umeambatana na magodoro, vyakula na ujenzi wa choo cha kisasa ameutoa baada yakuwahidi kufanyia matengenezo ya nyumba ambayo walikuwa wakipata shida kipindicha masika mara baada ya kufanya ziara mapema mwaka huu katika kijiji hicho nakugundua mateso wanayokumbana nayo familia hiyo. 

 "Nimeitembelea familia hiinimeumia sana kwani maisha wanayoishi ni ya shida sana hawana msaada wowotenyumba yao inavuja hawana chakula maishayao ni ya kuunganga unga mpaka watu  wajekama sisi kuwaletea vitu  vidogo vidogokama mchele na mafuta na mbaya Zaidi hata watoto hao wote watatu hakuna hatammoja aliyewahi kukanyaga shule ingawa wanaonekana ni wakubwa hivyo jamii tunapaswa kuwasaidia watoto hawa” alisema Kabati  

Familia hiyo ambayo baba mzazi Mzee LucasMpogole mbaye kwa sasa amelazwa hospitali ya mkoa wa Iringa kwa ugonjwa wakupooza ina watoto wanne wote wakiwa walemavu wa viungo hivyo kukosa msaadakabisa pindi mvua zikianza kijiji hapo. 

Akizungumza wakati wa kukabidhimsaada huo , Kabati alisema kuwa jamii ya walemavu wanahitaji msaada wa hali namali kutoka kwa wadau wenye uwezo na kuacha tabia ya kuiacha serikali peke yakekatika kutatua kero zao na kuwahudumia.

Alisema kuwa msaada huo utawafarijiwalemavu hao waone kuwa pamoja na upungufu walionao bado jamii ya watanzaniainawathamini na kuwajali katika maisha yao ya kila siku.

 Aliongeza kuwa walemavu wanayo hakiya kuishi na kujitegemea iwapo jamii itawajengea uwezo badala ya kuwafungiandani na kuwaona kama ni mkosi katika familia ila kugundua vipajiwalivyonavyo na kuiwezesha serikali kuwaingiza katika mipango mbalimbali yakuwapatia huduma. 

Kabati alitoa wito kwa serikalikuona umuhimu wa kutumia vituo mbalimbali vinavyolea watoto wenye ulemavukuhakikisha vinawejengea miundo mbinu rafiki na uboreshaji mipango na mfumo wautoaji elimu, afya na usafiri kulingana na tofauti za umri wa watoto nchini. Aidha Kabati alitoa wito kwa Mfukowa Maendeleo ya Jamii (TASAF) kuangalia kwa jicho la tatu familia ya Mpogolekwa kuwaongezea kipato zaidi cha kila mwezi kwani kwa hali waliyonayo nakiwango wanachopata kila baada ya miezi miwili hakiendani na uwingi wa walemavuwa familia hiyo maskini. 

Naye baba mdogo wa watoto hao akiongea kwa niaba ya baba mzazi wa walemavu hao, Juma Mpogole alimshukurumbunge huyo kwa msaada aliotoa na kumtaka awasomeshe watoto wake ambao tangu wazaliwe hawajawahi pata elimu yoyote licha ya kufikisha umri wa miaka zaidi 20.

Lakini naomba nitoe rai kwa wale wanasiasa na wananchi wengine wanaokuja kupiga picha nah ii familia ya watu wenye ulemavu wa viungo kwa ajili ya kujitafutia umaarufu waache tabia hiyo.

“Kila mara tunaona waandishi na wapiga picha wanafika hapa na viongozi mbalimbali lakini kila siku wanatoa ahadi tu sioni msaada wowote ule unaotolewa zaidi ya kuona wanajitafutia umaarufu huko mitaani naomba waacha tabia hiyo sisi tunamuona mbunge Ritta Kabati na kaka yake mbunge wa jimbo hili la kilolo Vennence mwamoto ndio wanaosaidia familia hii,kweli familia hii inaitaji msaada hivyo njooni kutoa msaada sio kupiga picha pekee yake”.alisema Mpogole
RAIS DKT.JOHN POMBE MAGUFULI ASHIRIKI IBADA YA JUMAPILI YA MWAKA MPYA KATIKA KANISA KUU JIMBO KATOLIKI LA BUKOBA MKOANI KAGERA JANUARI 01,2017

RAIS DKT.JOHN POMBE MAGUFULI ASHIRIKI IBADA YA JUMAPILI YA MWAKA MPYA KATIKA KANISA KUU JIMBO KATOLIKI LA BUKOBA MKOANI KAGERA JANUARI 01,2017

January 01, 2017

unnamed Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Askofu wa Jimbo Katoliki la Bukoba Desiderius Rwoma mara baada ya kuwasili katika Kanisa Kuu la Jimbo katoliki Bukoba mkoani Kagera.
1nwgwgfsg Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akibusu mkono wa Askofu Msaidizi Jimbo Katoliki la Bukoba Askofu Methodius Kilaini mara baada ya kuwasili katika Kanisa Kuu la Jimbo katoliki Bukoba mkoani Kagera kwa ajili ya Ibada.
unnamed-2Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akielekea katika katika Kanisa Kuu la Jimbo katoliki Bukoba mkoani Kagera mara baada ya kuwasili na kupokewa na Askofu wa Jimbo Katoliki la Bukoba Desiderius Rwoma (katikati) pamoja na Askofu Msaidizi Jimbo Katoliki la Bukoba Askofu Methodius Kilaini wa kwanza (kulia)
unnamed-3

unnamed-4 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika ibada ya mwaka mpya katika Kanisa Kuu la Jimbo katoliki Bukoba mkoani Kagera
unnamed-5Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Askofu wa Jimbo Katoliki la Bukoba Desiderius Rwoma mara baada ya Ibada
unnamed-6 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na waumini wa Kanisa Kuu la Jimbo katoliki Bukoba mkoani Kagera mara baada ya Ibada.
unnamed-7 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisali katika kaburi la Marehemu Kadinali Rugambwa mara baada ya Ibada kanisani hapo.
unnamed-8Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimshukuru Askofu wa Jimbo Katoliki la Bukoba Desiderius Rwoma mara baada ya kushiriki Misa ya Mwaka mpya kanisani hapo. Katikati ni Askofu Msaidizi wa Jimbo Katoliki la Bukoba Askofu Methodius Kilaini.
unnamed-10 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Askofu wa Jimbo Katoliki la Bukoba Desiderius Rwoma kushoto pamoja na Askofu Msaidizi wa Jimbo Katoliki la Bukoba Askofu Methodius Kilaini.
unnamed-11Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na masista kanisani hapo mara baada ya Ibada.

PAPA FRANCIS KUWA MGENI RASMI MAADHIMISHO YA MIAKA 500 YA KANISA LA KILUTHERI

January 01, 2017
Papa Francis
Mwinjilisti wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Mtaa wa Kivule, Ukonga Dar es Salaam Michael Mgaya (wa pili kushoto) akiwa na wazee wa kanisa hilo baada ya kumalizika kwa ibada. PICHA NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG

Na Richard Mwaikenda
KIONGOZI Kanisa la Katoliki Duniani, Papa Francis amekubali mwaliko wa kuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya miaka 500 ya kuasisiwa kwa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Duniani.

Taarifa hiyo imetangazwa leo wakati wa Ibada ya Jumapili ya kuukaribisha mwaka mpya katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Mtaa wa Kivule Ukonga, Dar es Salaam.

Maadhimisho hayo yatafanyika hivi karibuni eneo ambapo kanisa hilo liliasisiwa nchini Ujerumani ambapo kutakuwa na shamrashamra za kila aina zitakazoshuhudiwa na wageni kutoka nchi mbalimbali.

Kwa hapa nchini maadhimisho hayo yatafanyika katika Chuo cha Dini cha Makumira, mkoani Arusha, ambapo mnara wa kumbukumbu utajengwa. Kanisa hilo liliasisiwa mwaka 1557.

NAIBU SPIKA AONGOZA MKESHA MKUBWA WA KITAIFA 2017 KWA NIABA YA RAIS DK.JOHN MAGUFULI UWANJA WA UHURU JIJINI DAR ES SALAM

January 01, 2017
Naibu Spika wa Bunge, Dk.Tulia Akson, akipeperusha bendera ya Taifa wakati wa mkesha mkubwa wa kitaifa wa dua maalumu uliofanyika Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam jana. Dk.Akson alimwakilisha Rais Dk.John Magufuli kwenye mkesha huo ambaye alikuwa mgeni rasmi.
Naibu Spika wa Bunge, Dk.Tulia Akson (katikati), Mratibu wa mkesha huo Askofu Godfrey Malesi na Askofu Damas Kenasi (kulia), wakishiriki kuomba katika mkesha huo.
Waimbaji wa Kwaya ya Mass ya Sinza jijini Dar es Salaam wakiimba nyimbo za kumsifu mungu.
Watoto waimbaji wa Kwaya ya Mass ya Sinza jijini Dar es Salaam wakifanya vitu vyao kwenye mkesha huo.
Waumini wakiwa wameinua mikono kwenye mkesha huo.
Maombi yakiendelea.
Wananchi wakisubiri kuupokea mwaka mpya wa 2017 katika uwanja huo.

ASKOFU MOKIWA AWAONGOZA WAUMINI WAKE KUTOA MSAADA NA KUFANYA USAFI HOSPITALI YA MWANANYAMALA JIJINI DAR ES SALAAM

January 01, 2017

 Askofu Mkuu wa Kanisa la Anglikana Tanzania Dk.Valentino Mokiwa (katikati), akiwaongoza waumini wa kanisa hilo Archidikonari ya Kinondoni kufanya usafi katika viwanja vya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Mwananyamala Dar es Salaam leo asubuhi wakati kanisa hilo lilipotoa msaada wa vitanda na magodoro katika hospitali hiyo vyote vikiwa na thamani ya sh.milioni 12.

UONGOZI WA SERIKALI YA MTAA WA MARUZUKU BUGURUNI JIJINI DAR ES SALAAM WATOA SARE ZA SHULE KWA WATOTO 200

January 01, 2017
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Maruzuku katika Kata ya Mnyamani Buguruni Manispaa ya Ilala, kupitia Chama cha Wananchi (CUF), Jabiri Sanze (kulia), akimkabidhi sare za shule mtoto, Hamad Ali Dar es Salaamleo, ambaye ataanza darasa la kwanza mwezi huu. Serikali ya mtaa huo imetoa sare za shule, daftari na penseli kwa  watoto 200 watakaoanza darasa la kwanza mwaka huu wa 2017. Katikati ni mama wa mtoto huyo, Farida Rashid.

MKUU WA WILAYA YA ROMBO,AGNES HOKORORO AKAMATA NA KUTEKETEZA LITA 4000 YA POMBE CHAFU.

January 01, 2017
Mkuu wa wilaya ya Rombo Agnes Hokororo akiangalia namna pombe ya kienyeji inavyoandaliwa baada ya kukamata kiwanda bubu cha kutengenezea pombe bila ya kufuata taratibu.
Mmiliki wa kiwanda cha kutengeneza pombe ya kienyeji  aliyefahamik kwa jina moja la Carlos akitoa maelezo kwa Mkuu wa wilaya ya Rombo Agnes Hokororo namna wanavyoandaa pombe hiyo.
Carlos akifungua madumu makubwa yaliyohifadhi Pombe ya Kienyeji wakati wa utengenezaji wake katika kijiji cha Useri wilayani Rombo.
Sehemu ya Pombe ikiwa katika Mapipa baada ya kuvundikwa.
Kreti za Chupa za Banana ambazo zimekuwa zikitumika pia katika kuwekea pombe hiyo mara baada ya kutengenezwa.
Askari Mgambo akiweka ndizi zilizovundikwa katika ndoo ambazo pia hutumika katika utengenezaji wa pombe hiyo ya kienyeji.
Mkuu wa wilaya ya Rombo,Agnes Hokororo akimwaga pombe hiyo iliyokuwa katika Chupa.
Mkuu wa wilaya ya Rombo Agnes Hokororo akitizama daftari la mauzo lililokutwa katika kiwanda hicho.
Nyumba ambayo imekuwa iktumika kutengenezea Pombeza kienyeji kulipokutwa mitambo wa kutegeneza pamoja na pombe iliyokuwa katika maandalizi.
Mkuu wa wilaya ya Rombo Agnes Hokororo akimwaga pombe ya kienyeji iliyokuwa ikiandaliwa katika moja ya kiwanda bubu kilichokutwa katika kijiji cha Useri wilayani humo.
Katibu tawala wa wilaya ya Rombo ,Abubakar Asenga akimwaga pombe hiyo mara baada ya kufanya operesheni ya kushtukiza katika maeneo mbalimbali ya wilaya ya Rombo.
Pombe iliyokuwa katika maandalizi ikimwagwa katika kiwanda hicho.
Vizibo ambavyo vimekuwa vikitumika katika kufunika pombe hiyo mara baada ya kujazwa katika chupa.
Katibu tawala wa wilaya ya Rombo,Abubakar Asenga akipakia madumu makubwa yaliyokutwa yakitumika katika utengenezaji wa Pombe katika kijiji cha Useri wilaya Rombo.

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii,Kanda ya Kaskazini.