WAZIRI UMMY AWATEMBELEA MAJERUHI WA AJALI YA GARI LA GESI WALIOLAZWA HOSPITALI YA RUFAA YA BOMBO

April 01, 2023



Waziri wa Afya Ummy Mwalimu na Mbunge wa Jimbo la Tanga (CCM) katikati akiwa na Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga Bombo Dkt Naima Yusuf kulia wakimsikiliza Mkuu wa Idara ya Surgery Daktari Bingwa wa Upasuaji  Dkt Rashid  wakati Waziri huyo alipotembelea majeruhi walioungua katika ajali ya Gari lililokuwa limebeba gesi eneo la Kwamkono wilayani Handeni mkoani Tanga


Waziri wa Afya Ummy Mwalimu na Mbunge wa Jimbo la Tanga (CCM) katikati akiteta jambo na  Mkuu wa Idara ya Surgery Daktari Bingwa wa Upasuaji  Dkt Rashid kushoto wakati alipowatembelea majeruhi wa ajali ya Gari la Gesi waliolazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga -Bombo kulia ni Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga Bombo Dkt Naima Yusuf

Waziri wa Afya na Mbunge wa Jimbo la Tanga (CCM) Ummy Mwalimu katikati akionyeshwa kitu na Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga Bombo Dkt Naima Yusuf wakati  alipowatembelea majeruhi wa ajali ya Gari la Gesi waliolazwa katika Hospitali  hiyo kushoto Mkuu wa Idara ya Surgery Daktari Bingwa wa Upasuaji  Dkt Rashid akifuatiwa na Katibu wa Afya wa Mkoa wa Tanga Frank Mhilu



>Ashauri wapewa rufaa ya kwenda Muhimbili


Na Mwandishi Wetu,TANGA.


WAZIRI wa Afya Ummy Mwalimu leoAprili 1,2023 ametembelea majeruhi wa ajali ya gari iliyobeba gesi na kudondoka eneo la Kwamkono wilayani Handeni mkoani Tanga ambao wamelazwa kwenye Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga Bombo.


Baada ya majadiliano na Mganga Mfawidhi wa Hospital ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga Bombo Dkt Naima Yusuf akashauri wapewe Rufaa kwenda Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa matibabu kutokana na kwamba ina sehemu maalumu ya kutibu wagonjwa walioungua.

Gari hilo ambalo lilikuwa limebeba gesi baada ya kudondoka gesi hiyo iliweza kusambaa na kutapakaa kwenye maeneo mbalimbali katika eneo hilo na hivyo kusababisha madhara hayo makubwa kwa wananchi ikiwemo baadhi yao kuungua.


Akiwa ameongozana na Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo Dkt Naima Yusuf na Katibu wa Afya Mkoa wa Tanga Frank Mhilu alipata fursa ya kuwatembelea wagonjwa wengine pia na kuwajulia hali huku akiwapongeza wauguzi na madaktari kwa kazi nzuri wanayoifanya katika kuwahudumia wananchi wanaokwenda kupata huduma kwenye hospitali hiyo.


Akizungumza kuhusu majeruhi wa ajali ya gari la gesi lililoungua eneo la kwamkono wilayani Handeni ,Waziri Ummy alisema kutokana na kwamba hali zao kutokuwa nzuri hivyo upo umuhimu wa kupewa rufaa na kupelekwa kwenye hospitali ya Taifa ya Muhimbili ili kuweza kupata huduma Zaidi.


“Kutokana na hali zao kutokuwa nzuri ninashauri majeruhi hao wapewe rufaa na kupelekwa kwenye Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa ajili ya matibabu Zaidi”Alisema


Hata hivyo Waziri Ummy alisema kwamba wanaangalia uwezekano wa kulifanyia ukarabati Jengo la Clief ambalo lipo kwenye hospitali hiyo ili liweze kuwa na muonekana mzuri tofauti na lillivyokuwa hivi sasa.

KAMATI YA PIC YARIDHISHWA NA MRADI WA KITEGAUCHUMI CHA JENGO LA KIBIASHARA (THE ROCK CITY MALL) LA PSSSF

April 01, 2023

 

NA MWINDISHI WETU, MWANZA

KAMATI ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (Public Investment Committee PIC) imepongeza uwekezaji uliofanywa na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) kwenye Mradi wa kitegauchumi cha jengo la kibiashara (the rock city mall) jijini mwanza.

Wajumbe hao wakiongozwa na Mwenyekiti wa PIC, Mhe. Jerry Silaa wametoa pongezi hizo Machi 30, 2023 baada kutembelea mradi huo kwa lengo la kuona tija iliyopo kwenye uwekezaji huo.

 Walisema uwekezaji wa jengo hilo umebadilisha sura ya jiji la Mwanza  ambapo zamani eneo hilo lilitapakaa vibanda tu na kwamba uwekezaji umebadilisha sura ya jiji la Mwanza jambo ambalo limeleta thamani ya kijamii (social value),” alisema

Aidha wamesema uwekezaji wa mradi wa “the rock city mall” ni moja ya miradi iliyokamilika na yenye kutia matumaini hata hivyo walishauri kufanywe marekebisho sehemu ambazo zina mapungufu ili kuvutia wapangaji kwenye maeneo ambayo bado hayana wapangaji.

Walioungana na Menejimenti juu ya athari za ugonjwa wa Korona (COVID-19) kwenye Biashara ambapo umeleta mtikisiko wa uchumi Duniani biashara nyingi zimeanguka au kusua sua na hivyo wakashauri nafasi ambazo bado hazijapata wapangaji kutokana na bei ya pango menejimenti ikae na kuangalia upya viwango hivyo vya kodi ya pango.

Aidha licha ya kupongeza uwekezaji huo pia walisema ripoti ya mradi imekaa vizuri na hasa kwa Kamati inayoangalia Uwekezaji wa Mitaji ya Umma na Vipindi vya Miradi kuanza Kuingiza Faida iliyokusudiwa.(Payback period).

Mwenyekiti wa PIC Mhe. Jerry Silaa licha ya kupongeza amebainisha kuwa pesa zilizowekezwa kwenye miradi ni pesa za wanachama na sio za serikali hivyo akashauri umakini ili kufikia malengo yaliyokusudiwa.

“mbele ya safari wajumbe tutakaa na kufanya uchambuzi kuona uwekezaji wa jumla wa sasa wa Mfuko ili kuwa na hakika ya uwekezaji wenye tija.” Alifafanua.

Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya PSSSF Dkt. Aggrey Mlimuka alisema Bodi yake imepokea ushauri wa Wajumbe na kuahidi kuyafanyia kazi maelekezo hayo ili kuongeza tija katika uwekezaji huo.

“Bodi imeweka mikakati ya kuweza kufanya maamuzi ya kibiashara ambayo yanapaswa kufanyika mara kwa mara kulingana na wakati uliopo” Alisema Dkt. Mlimuka.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF, CPA. Hosea Kashimba alisema Jengo lina eneo la upangishaji lenye sqm 21,151.82 ambapo hadi mwezi Febrauri 2023 kampuni imeweza kupangisha jengo kwa kiwango cha asilimia 82%.

Alisema maeneo ambayo tayari yamepangishwa kwa ujumla yana meta za mraba 17,436.07; kwa upande wa maeneo ambayo bado hayajapangishwa yana ujumla ya meta za mraba 3,715.75 ambayo ni sawa na asilimia 18%.

Hata hivyo tayari wapo waombaji ambao wamechukua offer kwa baadhi ya maeneo hayo ikiwemo, vyumba kwa ajili ya maduka, na ofisi mbali mbali na tayari tulishatoa maelekezo ya jinsi ya kujaza nafasi zilizobaki wazi ikiwa ni pamoja na kupata wapangaji wakubwa na tayari wameanza kupatikana na kutolea mfano Woolworth.

Aidha kuhusu wapangaji ambao wana madeni ya pango alisema kumekuwepo na maendeleo mazuri ya ulipaji kwa wale wanaodaiwa baada ya ugonjwa wa Korona (Covid19).

“Wateja wapya wanaoingia sasa tumekubaliana wanalipa kila baada ya miezi mitatu (3), miezi 6 na mwaka mzima, hilo limetusaidia kwa kiasi kikubwa.” Alifafanua CPA. Kashimba.

Jengo la The Rock City Mall linamilikiwa na Kampuni inayojulikana kama Mwanza City Commercial Complex Company Limited (MCCCCL). Kampuni hii imeundwa kwa ubia kati ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa watumishi wa Umma (PSSSF), Halmashauri ya Jiji la Mwanza na Halimashauri ya Manispaa ya Ilemela.

Awali ubia ulikua kati ya LAPF na Jiji la Mwanza na baada ya mgawanyo wa Jiji la Mwanza na kuundwa kwa Halmashauri ya Jiji la Mwanza na Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela, Hivyo basi mradi huu sasa unamilikiwa na wabia watatu ambao ni Halmashauri ya Jiji la Mwanza, Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), Alisema CPA. Kashimba wakati akiwasilisha ripoti ya uwekezaji .

Alisema PSSSF ina miliki asilimia 90 na wabia wengine wanamiliki asilimia 10 ya hisa, kwa mchanganua wa Halmashauri ya jiji la Mwanza (MCC) kumiliki asilimia 6 na Manispaa ya Ilemela (IMC) wanamiliki asilimia 4 ya hisa hukuthamani ya mradi kwa maana ya uwekezaji ni shilingi bilioni 80.

Mwenyekiti wa PIC Mhe. Jerry Silaa
Mhe. Silaa (katikati) akiongozana na Makamu Mwenyekiti wa Bodi yaWadhamini ya PSSSF, Dkt. Aggrey Mlimuka (wapili kulia), Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF, CPA. Hosea Kashimba na wajumbe wengine wa Kamati wakitembelea mradi wa jengo la kibiashara la the Rock City Mall jijini Mwanza Machi 30, 2023.
Mkurugenzi Mkuu PSSSF, CPA. Hosea Kashimba
Mhe. Silaa (katikati) akiongozana na Makamu Mwenyekiti wa Bodi yaWadhamini ya PSSSF, Dkt. Aggrey Mlimuka (wapili kulia), Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF, CPA. Hosea Kashimba na wajumbe wengine wa Kamati wakitembelea mradi wa jengo la kibiashara la the Rock City Mall jijini Mwanza Machi 30, 2023.


 

BODI YA MICHEZO YA KUBAHATISHA (GBT) YATOA ELIMU KWA WATENDAJI WA MKOA WA PWANI

April 01, 2023

 

 

NA MWANDISHI WETU, KIBAHA

MKUU wa Mkoa wa Pwani Alhaj Aboubakar Kunenge amehimiza ushirikiano baina ya Taasisi za Umma, Binafsi na watendaji kwenye Halmashauri ili kazi ya kuwatumikia wananchi iwe rahisi.

Ameyasema hayo wakati akifungua semina ya kujenga uelewa wa shughuli za taasisi mbalimbali za umma na binafsi ikiwemo Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania (GBT) na watendaji kutoka Halmashauri za Mkoa wa Pwani Machi 30, 2023.

 GBT ni taasisi ya Kiserikali ambayo iko chini ya Wizara ya Fedha na Mipango ikisimamiwa na Msajili wa Hazina. (TR).

 RC Kunenge alisema wataalamu lazima wajue viongozi wa kisiasa hawawezi kuwa na maamuzi mazuri kama wataalamu hawatafanya kazi ya kitaalamu inavyotakiwa.

 “Lazima tuelewe, serikali ni moja, mlipaji ni mmoja, fedha inatoka fungu moja na inavyopatikana iwe ni Halmashauri au Bodi ya Michezo ya kubahatisha yote inaingia sehemu moja kwa Katibu Mkuu Wizara ya Fedha au PST.” Alisema na kuongeza ….

 Haiwezekani kwenye Halmashauri kukawa na watendaji kutoka kila taasisi ya serikali na kushauri ili utendaji wa taasisi hizo kwenye maeneo ambayo ni vigumu kwa watendaji wao kuwepo ili kuwatumikia wananchi ni vema kukawepo na makubaliano yatakayowezesha utendaji kazi ukawa rahisi bila ya vikwazo, alifafanua Alhaj Kunenge ambaye alifuatana na Wakuu wote wa wilaya za Mkoa huo.

 “Kama tuna majukumu ambayo tunaweza kufanya kwa niaba ya wenzetu mnaweza kukasimu shughuli zenu na zikafanywa na watu wa Halmashauri, lazima tufanye kazi kwa kushirikiana kwani serikali ni moja.” Alisema.

 Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania (GBT), Bw. James Mbalwe alisema Bodi imefika Mkoani humo kwa lengo la kujitambulisha rasmi kwa watendaji wa Mkoa ili kuongeza ufahamu wa kamati, uwepo wa taasisi na kuongeza ufahamu juu ya usimamizi na uendeshaji wa michezo ya kubahatisha hapa nchini.

 Pia kuimarisha ushirikiano katika usimamizi na udhibiti wa sekta na kuomba kamati ya Ulinz na Usalama ya Mkoa kushirikiana na GBT ili kudhibiti wavunjaji wa sheria ya michezo ya kubahatisha hapa mkoa wa Pwani, alisema Bw. Mbalwe.

Alisema wanaona umuhimu wa kutoa elimu mara kwa mara kwa vile GBT ni taasisi change iliyoanzishwa mwaka 2003

 Alisema semina kama hizo zimekuwa na manufaa makubwa katika kurahisisha utendaji wa GBT na kutolea mfano Mkoa wa Kigoma ambako baada ya kutolewa elimu kama hiyo utendaji wa Michezo ya Kubahatisha Mkoani humo imekuwa rahisi.

“Kazi yetu ni udhibiti, kusimamia na kuratibu uendeshaji wa michezo ya kubahatisha nchini na ieleweke kuwa GBT haifanyi biashara na iko chini ya Wizara ya Fedha chini ya Msajili wa Hazina.” Alifafanua

 Bw. Mbalwe alihimiza kuimarisha ushirikiano katika usimamizi wa sekta na kuiomba kamati ya usalama ya mkoa kuongeza ushirikiano zaidi katika kudhibiti wavunja sheria ya Michezo ya Kubahatisha.

“Nina sisitiza Michezo ya Kubahatisha ni Burudani na sio Ajira au njia ya kujitafutia kipato.” Alifafanua Bw. Mbalwe.

Kuanzishwa kwa GBT kumewezesha sekta ya michezo ya kubahatisha kuratibiwa vizuri zaidi na iweze kuchangia ipasavyo katika pato la taifa na wananchi wanaojishughulisha kwenye michezo hiyo wanalindwa ipasavyo.

 “Sekta inakuwa kwa kasi na kwa sababu hiyo kunahitaji uratibu makini ili iendelee kukua katika namna ambayo utaratibu unaopasa bila kupoteza malengo ya msingi ya kuanzishwa kwake.” Alifafanua Bw. Mbalwe.

Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhe. Alhaj Aboubakar Kunenge akifungua semina hiyo kwenye Mji wa Kibaha Machi 30, 2023
Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha (GBT), Bw. James Mbalwe akizunguzma kwenye semina hiyo.
Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Pwani
Baadhi ya Wakuu wa Wilaya na watendaji wengine kutoka Halmashauri za Mkoa huo
Mkurugenzi Mkuu wa GBT, Bw. James Mbalwe (wakwanza kulia), Mkurugenzi wa Huduma za (DCS) Bw. Daniel Ole Sumayan (katikati) na Mkurugenzi wa Ukaguzi na Matekelezo Bw. Sadick Elimsu
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhe. Alhaj Aboubakar Kunenge (kulia) akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa GBT, Bw. James Mbalwe (wapili kushoto) Mkurugenzi wa Masuala ya Shirika, Bw. Daniel Ole Sumayan (wakwanza kushoto). Katikati ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Pwani Bw. Rashid Mchatta.

Picha ya pamoja