UZIBUAJI WA MITARO UKIENDELEA JIJINI MWANZA.

June 21, 2016
Uzibuaji wa Mitaro ukiendelea katika Mitaa mbalimbali ya Katikati ya Jiji la Mwanza. BMG inatoa pongezi za dhati kwa Uongozi wa halmashauri ya Jiji la Mwanza kwa zoezi hili maana lisipofanyika kwa muda mrefu, mitaro hii huziba, mvua inaponyesha huwa Mitaa ya Jiji haitamaniki tena na inapoteza hadhi ya Jiji la Mwanza.
RIPOTI YA UNHCR YAONESHA UWAPO WA WAKIMBIZI MARADUFU KATIKA HISTORIA YA BINADAMU

RIPOTI YA UNHCR YAONESHA UWAPO WA WAKIMBIZI MARADUFU KATIKA HISTORIA YA BINADAMU

June 21, 2016
TAARIFA ya hali ya wakimbizi duniani kufikia mwaka 2015 inaonesha kwamba watu milioni 65.3 wanaishi kikimbizi ikilinganishwa na watu milioni 59.5 kwa mwaka 2014.

Ongezeko hilo la watu milioni 5.8 katika kipindi cha miezi kumi na mbili kimelezwa kuwa ni la kiwango cha juu tangu kuanzishwakwa Umoja wa Mataifa.

Katika taarifa yake kuadhimisha siku ya wakimbizi duniani (Global Trends) Shirika la Kuhudumia wakimbizi (UNHCR) limesema dunia kwa sasa inakabiliwa na kundi kubwa la watu waliolazimika kuyakimbia makazi yao kwa sababu mbalimbali ikiwamo migogoro ya kivita, ubaguzi na uvunjaji wa haki za binadamu.

“Takwimu zilizopo leo hii, aina ya migogoro iliyopo na ugumu wake kumesababisha kuwapo na wimbi kubwa la wakimbizi tangu kuanzishwa tangu kuanzishwa kwa Umoja wa Mataifa; watu milioni 60 wameondolewa katika makazi yao duniani hapa. Kila siku janga la wakimbizi linatangazwa katika vyombo vya habari ; watoto, wanawake na wanaume wakipoteza maisha yao katika jaribio la kukimbia vurugu zilizopo katika eneo lao" anasema Filippo Grandi, Mkuu wa UNHCR.

Kati ya wakimbizi milioni 65.3, wakimbizi milioni 3.2 wako katika nchi zenye viwanda wakisubiri kutambuliwa hadhi zao kama wakimbizi, milioni 21.3 wametawanyika duniani kote na milioni 40.8 wamelazimika kukimbia maeneo yao lakini wapo katika nchi zao.
Mwakilishi wa UNHCR Tanzania, Bi Chansa Kapaya akizungumza kwenye maadhimisho ya siku ya wakimbizi duniani yaliyofanyika katika kambi ya wakimbizi, wilayani Kasulu, mkoani Kigoma.

Imeelezwa kuwa kwa kuzingatia idadi ya watu waliopo duniani takribani bilioni 7.349 ina maana kwamba mtu mmoja kati ya watu 113 ama anatafuta hifadhi, amekimbia makazi yake lakini yupo katika nchi hiyo hiyo au ni mkimbizi.

Kimsingi duniani kwa sasa kuna watu wengi waliolazimishwa kuhama makazi ya kuliko idadi ya watu waliopo Uingereza, Ufaransa au Italia.

Miaka 10 iliyopita, mwishoni mwa mwaka 2005, UNHCR ilirekodi wastani wa watu sita kukosa makazi kila dakika duniani lakini sasa ni wa 24 kila dakika.

Watu milioni 1.8 walilazimika kukimbia nchi zao kwa mwaka 2015 ukilinganisha na watu milioni 2.9 mwaka 2014.

Uturuki iliorodhesha idadi kubwa ya wakimbizi wapya wakiwamo 946,800 kutoka Syria. Urusi walikuwa na wakimbizi 149,600 kutoka Ukraine. Na vurugu zilipoibuka Burundi mwezi Aprili, karibu watu 123,400 walikimbilia Tanzania.
Kwa idadi hiyo Tanzania inakuwa nchi ya tatu kwa kuhifadhi wakimbizi wengi duniani.

Wakati wakimbizi wapya wa Burundi wanaingia Tanzania,UNHCR ilikuwa katika operesheni ya kuwawezesha wakimbizi waliopo kuendelea na maisha yao ya kawaida. Aidha katika kipindi hiki Tanzania ilitoa uraia kwa wakimbizi wa Burundi walioingia nchini mwaka 1972 ambao walikuwa wakiishi Tabora na Katavi na Marekani iliwapokea wakimbizi 30,000 wa Kongo waliokuwa wakiishi Nyarugusu, Kigoma.

Tangu kuanza kwa wimbi jipya la wakimbizi kutoka Burundi zaidi ya watu 141,000 wamekimbilia Tanzania kutafuta hifadhi na kuifanya Tanzania kuwa nchi inayohifadhi wakimbizi wengi kutoka Burundi.

Asilimia 77.9 ya wakimbizi hao wapya ni wanawake na watoto, Watoto wengi waliofika Tanzania ni wale waliozaliwa katika ardhi ya Tanzania (63,961) wamehifadhiwa katika kambi ya Nyarugusu, moja ya kambi kubwa duniani ikiwa na wakimbizi 131,733.Mazingira ya maisha yao yakiwa magumu. Moja ya vitu ambavyo vinafanywa na UNHCR ni kuwatawanya wakimbizi hao ili kuleta nafuu katika kambi hiyo.

Wakimbizi wengine wapo katika kambi za Nduta na Mtendeli zilizofunguliwa Oktoba 2015 na Januari 2016 kwa lengo la kupunguza msongamano katika kambi ya Nyarugusu na wakati huo huo kutoa nafasi kwa wakimbizi wapya.

Hata hivyo Nduta haraka sana ilifikia kiwango chake cha juu kinachopaswa kuwepo hapo Ilipofika Aprili mwaka huu; Kambi hiyo ina wakimbizi 55,000. Wakimbizi wapya kwa sasa wanapokelewa kambi ya Mtendeli ambapo wakazi wake waliongezeka kufikia 21,796.

Lipo eneo jingine linafikiriwa kufanywa kambi ya wakimbizi eneo la Karago, lakini eneo hili lina matatizo ya maji na haifikiriwi kwamba inaweza kubeba wakimbizi 50,000 wanaotarajiwa kuingia Tanzania kutoka Burundi.

“Wahisani wa kimataifa wameweza kuitikia wito wa kukabiliana na wimbi la wakimbizi wa Burundi na hivyo kuipunguzia mzigo serikali ya Tanzania,UNHCR na Mashirika mengine ya Umoja wa pamoja na taasisi zisizo za kiserikali. hata hivyo bado kunatakiwa raslimali nyingi zaidi ili kukabilina na wimbi hilo,” anasema Mwakilishi wa UNHCR Tanzania, Bi Chansa Kapaya.

UNHCR Tanzania imepata asilimia 40 ya mahitaji yake kusaidia wakimbizi wa Burundi mwaka kukiwa na pengo la dola za Marekani milioni 44.8 hadi kufikia Juni 19,2016.Kwa mantiki hiyo fedha kwa ajili ya kusaidia wakimbizi wa Burundi wanaotarajiwa kufikia 330,000 mwishoni mwa mwaka huu zipo kidogo sana.
Geofrey Adroph BLOGGER P.O.BOX 24793, Mob: +255 755 274953 /+255 713 363965, Email: pamojapure@gmail.com. Blog: http://www.pamoja.co.tz/ DAR ES SALAAM, TANZANIA
MERCY KITOMARI: MJASIRIAMALI KIJANA ANAYEFIKIRIA MAKUBWA

MERCY KITOMARI: MJASIRIAMALI KIJANA ANAYEFIKIRIA MAKUBWA

June 21, 2016
Mjasiriamali kijana Mercy Kitomari akiwa ofisini kwake wakati wa mahojiano.

Modewjiblog ilipata bahati ya kuzungumza ana kwa ana na Mercy Kitomari mmoja wa wajasiriamali wanawake vijana ambaye anafikiria kuwa na kiwanda kikubwa cha ashkrimu (ice cream) ifikapo mwaka 2020 akizisafirisha na kuziuza Tanzania nzima na Afrika Mashariki. Wapi alipotokea, yuko wapi kwa sasa, ni machungu gani aliyokumbana nayo na anaishauri nini serikali na wajasiriamali wenzake. Haya yote utayajua katika mahojiano haya .Soma…

MODEWJI BLOG: Role model wako nani?
MERCY: Magufuli. You know why?(unajua kwanini?) ametuweka wazi kabisa kwamba maisha ni changamoto na tusikubali kushindwa ni lazima kupambana na kufanyakazi kwa bidii na maarifa kuondoa vigingi vyote vinavyotukwamisha. Amenifanya nifanye kazi kwa bidii. Nataka kuwa mwanamke anayefanya mabadiliko. Hakuna kitu kinachokuja kirahisi. Nataka kuwa mwanamke yule ambaye anaonesha tofauti nataka kuifanya nchi yangu iniringie.

Sijisikii vibaya kwa kuwa niko mpweke, kitu cha kwanza ni kazi, nataka kuifanya mwenyewe ili wanawake wenzangu watambue kwamba tunaweza kufanya wenyewe, bila msaada wa mwanaume. Ndio unahitaji mume lakini si katika hili suala la ujasiriamali, mwanamke peke yako unaweza kuleta mabadiliko.

Nataka kuwa mwanamke ambaye Afrika itaniringia na taifa langu litanichekelea kwamba mimi ni binti yao.

MODEWJI BLOG: Turejee katika masuala ya kodi. Kodi ni muhimu sana kwa mapato ya serikali. Je Kodi zinazowatoza zinawasaidia au zinawavunja moyo?

MERCY: To be honest (kusema ukweli) zinatuvunja moyo. Nyingi ya hizi kodi hazitusaidii sisi watu wa hali ya chini kunyanyuka, zinatukwamisha.Kodi zimewekwa bila kujali madaraja. Anayeanza na aliyemo, mwenye kipato kidogo na kikubwa. Na yote hayo yanafanyika bila kuzingatia kwamba kuwapo kwa wajasiriamali wengi ndio kuchangamka kwa soko la wakulima na pia ajira viwandani.

Mimi ninayetengeneza ashkrimu natengeneza ajira; ninatengeneza soko kwa yule anayeleta matunda sokoni kwani naenda kununua matunda kwa ajili ya ashkrimu. Kodi nyingi zinakandamiza, haziangalii ukubwa na udogo wa biashara. Mtu anabiashara inayoingiza mamilioni kwa siku anawekwa kundi moja na anayeingiza laki moja.
Muonekano wa nje wa duka la Ice Cream la Nelwa’s Gelato la Mercy Kitomari lililopo ndani ya Petrol Station ya SOPCO barabara ya Morogoro-Magomeni Mwembechai karibu na kwa Sheikh Yahya.

MODEWJI BLOG: Ukikutakana na role model wako utamuomba nini?

MERCY: Nikikutana na Magufuli? Kwanza naomba nikutane naye! Nikikutana naye nitamwambia ofisi zote za huduma kwa wananchi ziwe katika mtandao (online) watu tuweze kufanya kila kitu katika mtandao. Na Serikali za mitaa lazima zirejeshe faida kwa wananchi kwa kodi zao.

Wanatakiwa watufundishe vitu vingi. Watufundishe kuwa wajasiriamali namna ya kufunga na kuuza bidhaa zetu wasifanye tu shughuli za kukusanya ushuru na kodi, watuambie namna ya kuendelea mbele ili waendelee kukusanya ushuru na kodi au hawatakusanya kitu tukikwama.

Ni lazima wawekeze kwa wajasiriamali ili kuwepo na hali bora zaidi.

Ukitazama soka katika televisheni unaona matangazo mengi ya krisp hapa kwetu wapo wadada wanaotembeza za ndizi au viazi hawa wakifundishwa namna nzuri ya kuweka chakula chao ni dhahiri tutakuwa na wajasiriamali wengi. Wanatakiwa watuelekeze mambo mengi bidhaa za kwenye ‘super market’ zinakuaje na kadhalika wasibaki kudai na kuvuna hela tu watusaidie tuweze kuwapatia fedha zaidi. Lakini nambieni lini nitakutana na role model wangu huyu…….ha ha ha ha….kicheko….!

MODEWJI BLOG: Wasaidizi wake wakisoma makala haya watajua nini unahitaji na pasi shaka watakukutanisha naye.Ni watu wema hawa, hawawezi kukosa kukupangia muda wa kumuona Role Model wako umweleze mambo ya kukusaidia wewe na wengine wa aina yako.

MERCY: Nakudai hilo kwani natamani sana atukutanishe wanawake vijana wajasiriamali ili azungumze nasi. Najua ameshazungumza na wafanyabiashara wakubwa, lakini akituona na sisi atatambua uwezo wetu na namna ambavyo angetusaidia tungeibuka wengi na kuweka ndoto ya Tanzania ya viwanda katika ukweli.

You know (unajua) nilikutana na wanawake wenzetu wajasiriamali kutoka Uganda na Rwanda naona wameendelea kwelikweli na siri ni serikali zao kuhakikisha kwamba wanaendelea.

Wapo wanawake waliokata tamaa hapa, nimekutana nao nikasema tusichoke hata kidogo serikali ya sasa inataka viwanda ni lazima kuisaidia kujua tunawezaje kufikia ndoto hiyo, kuna vizingiti hapa wakiviondoa tutaweza.

Hatupaswi kukata tama hasa kutokana na serikali ya sasa kutaka kuwapo na viwanda.

-- Zainul A. Mzige, Operation Manager, MO BLOG, www.modewjiblog.com +255714940992.

MAKAMU WA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MHE. SAMIA SULUHU HASSAN AFUNGUA MAFUNZO YA WANAWAKE WAJASIRIAMALI JIJINI DAR ES SALAAM

June 21, 2016


 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati wa kufungua Mafunzo ya siku tatu ya Wanawake Wajasiriamali  yalioandaliwa na Mfuko wa Fursa Sawa kwa Wote (EOTF) kwenye ukumbi wa Bwalo la JKT Mgulani, Dar es Salaam.
 Mwenyekiti wa Mfuko wa Fursa Sawa kwa Wote (EOTF), Mhe. Mama Anna Mkapa akihutubia kwenye ufunguzi wa mafunzo kwa wanawake wajasiriamali ambapo mgeni Rasmi wa ufunguzi huo alikuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan.
 Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Fursa Sawa kwa Wote Ndugu Steven Martin akielezea kwa ufupi mafanikio ya mafunzo ambayo yametimiza miaka 19.
 Sehemu ya wakina ama waliohudhuria ufunguzi wa Mafunzo ya Wanawake Wajasiriamali kwenye ukumbi wa Bwalo la JKT Mgulani,Dar Es Salaam.
Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini ya Mfuko wa Fursa Sawa kwa Wote (EOTF) Esther Mkwizu akizungumza na wajumbe walihudhuria mara baada ya unfunguzi rasmi wa mafunzo kufanyika kwenye ukumbi wa Bwalo la JKT Mgulani jijini Dar es Salaam.


  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan (wa pili kushoto) akiwa pamoja na Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janetth Magufuli ,Mkuu wa Wilaya ya Temeke Mhe. Sophia Mjema wakifurahia jambo wakati wa shughuli za ufunguzi wa mafunzo ya wajasiriamali wanawake ,kushoto ni Mwenyekiti wa wa Mfuko wa Fursa Sawa kwa Wote, Mke wa Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Mama Anna Mkapa.
 Baadhi ya wakina Mama waliohudhuria wakifuatilia kwa makini hotuba za  ufunguzi wa mafunzo ya wanawake wajasiriamali.
 Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE) Bi.Jacline Maleko akisalimiana na  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan pamoja na Mwenyekiti wa Mfuko wa Fursa Sawa kwa Wote Mama Anna Mkapa mara baada ya ufunguzi wa mafunzo kwa Wanawake Wajasiriamali yaliofanyika kwenye Bwalo la JKT Mgulani jijini Dar es Salaam.

ASKARI WA CHUO CHA MAFUNZO ZANZIBAR WAPATA MAFUNZO

June 21, 2016

Kaimu Mkurugenzi Tume ya Taifa ya Kudhibiti na Kupambana na Madawa ya Kulevya Zanzibar, Dkt. Mahmoud Ibrahim Mussa akitoa mafunzo juu ya kuwasaidia watumiaji wa madawa ya kulevya kwa Askari wa Chuo cha Mafunzo Zanzibar katika ukumbi wa Chuo hicho Kilimani Mjini Zanzibar.
Baadhi ya washiriki wa mafunzo ya kuwasaidia watumiaji wa madawa ya kulevya wakimsikiliza Kaimu Mkurugenzi Tume ya Taifa ya Kudhibiti na Kupambana na Madawa ya Kulevya Zanzibar Dkt. Mahmoud Ibrahim (hayupo pichani) katika mafunzo ya siku moja yaliyofanyika ukumbi wa Chuo hicho. Picha na Haji Ramadhan Suweid.

Na Miza kona – Maelezo Zanzibar

Matumizi ya dawa za kulevya ni janga linaloathiri vijana na kupoteza mwelekeo ambao hupelekea kufanya maamuzi yasiyo sahihi na kupoteza kumbukumbu jambo ambalo linarejesha nyuma maendeleo ya Taifa.

Akitoa mafunzo kwa watendaji wa Chuo cha Mafunzo Kaimu Mkurugenzi Tume ya Taifa ya Kudhibiti na Kupambana na Madawa ya Kulevya Dkt Mahmoud Ibrahim Mussa katika shamra shamra za kuadhimisha siku ya kudhibiti madawa ya kulevya.

Amesema mtumiaji wa madawa ya kulevya huathirika ubongo ambao hawezi kuacha kutumia madawa hayo kwa kuongeza kiwango hali ambayo inayopelekea kutoweza kufanya shughuli za kimaendeleo.

Ameeleza kuwa maambukizi makubwa ya virusi vya ukimwi yanasababishwa zaidi na watumiaji wa madaya ya kulevya kwa njia ya kujidunga sindano ambayo yanaathiri jamii na kupoteza nguvu ya taifa.

“Sigara ina madhara makubwa nacho pia ni kilevi ina kemikali 4000 ambayo huleta madhara kwa binadamu na kuharibu viungo, husababisha maradhi ya moyo, kansa pia hupelekea ugonjwa wa akili,” alitanabahisha Dkt Mahamoud.

Amefahamisha jamii itanabahishwe zaidi juu ya madhara ya matumizi dawa za kulevya pamoja na uvutaji wa sigara jinsi ya kuyaepuka na na kuwasaidia watumiaji wa madawa ya kulevya ili kuweza kuyaacha madawa hayo.

Dkt Mahamoud amefahamisha kuwa kinga ya msingi ya kuachana matumizi ya dawa za kulevya imo ndani ya familia ambayo iweze kumkubali muathirika ili aweze kuachana na kilevi kwa kumpa huduma nzuri bila ya kunyanyapaa.

Aidha wameshauri kutafuta njia ya kuweza kudhibiti utumiaji wa dawa za kulevya katika Vyuo vya mafunzo kwa wafungwa kwani imebainika kuwa baadhi yao hutumia dawa hizo wakati wanatumia kifungo.

Nao washiriki wa mafunzo hayo wameiomba jamii kutoa mashiriakiano makubwa na vyombo vya kudhibiti madawa ya kulevya ili kuweza kuwafichua na kuwadhibiti wale wote wanaoingiza, wanaosambaza na watumiaji pamoja na kutoa elimu hiyo kupitia skuli mbali mbali ili kuhakikisha kuwa jambo hilo linadhibitiwa nchini.

Aidha wameitaka Tume ya Kudhibiti Madawa ya Kulevya kuwa huru katika kutoa huduma zake ii iweze kufanyakazi kwa uwazi pamoja na wazazi kuwafundisha watoto wao maadili mema na kukua katika misingi mizuri kwani vishawishi vya madhara hayo ni vijana.

Mafunzo hayo ni ya siku moja ambayo yaliyowashirikisha watendaji wa Chuo cha Mafunzo ambapo kilele chake kinatarajiwa kufanyika tarehe 26 mwezi huu.
SEKTA ISIYO RASMI KUNUFAIKA NA HUDUMA ZA HIFADHI YA JAMII.

SEKTA ISIYO RASMI KUNUFAIKA NA HUDUMA ZA HIFADHI YA JAMII.

June 21, 2016

KIBO1Mkurugenzi wa Sheria kutoka Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Bw. Onorius Njole akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam kuhusu Mpango Maalum wa kutoa huduma ya hifadhi ya jamii kwa sekta isiyo rasmi maarufu kama Informal Sector Scheme ambayo inajumuisha waendesha bodaboda, bajaji na mama lishe. Kulia ni Mkuu wa Uhusiano na Uhamasishaji wa SSRA, Bi. Sarah Kibonde.
KIBO2 
Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Uhamasishaji  kutoka Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Bi. Sarah Kibonde akiwaeleza waandishi wa habari juhudi za Serikali katika kuboresha na kupanua wigo wa huduma za hifadhi ya jamii hasa kwa wananchi walio kwenye sekta isiyo rasmi. Kushoto ni  Mkurugenzi wa Sheria kutoka SSRA, Bw. Onorius Njole.
KIBO3Mkurugenzi wa Sheria kutoka Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Bw. Onorius Njole akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam kuhusu Program maalum ya kutoa elimu ya hifadhi ya jamii kwa Wakurugenzi wa Halmashauri za Wilaya na Waratibu wa Mifuko ya Bima ya Afya ya Jamii nchini kote. Zoezi hilo linaenda sambamba na usajili wa mifuko hiyo. Kulia ni Mkuu wa Uhusiano na Uhamasishaji wa SSRA, Bi. Sarah Kibonde na kushoto ni Afisa Uhusiano Ally Masaninga.
KIBO4 
Baadhi ya Waandishi wa Habari wakifuatilia mkutano wa SSRA uliofanyika leo jijini Dar es Salaam ambao ulilenga kuufahamisha umma maboresho mbalimbali katika sekta ya hifadhi ya jamii nchini.
……………………………………………………………………………………………………………….
Na Fatma Salum (MAELEZO)
Serikali kupitia Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA) imejizatiti kupanua wigo na kuboresha huduma za hifadhi ya jamii hasa kwa kundi la watu walio kwenye sekta isiyo rasmi.
Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi wa Sheria kutoka Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Bw. Onorius Njole wakati  akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam kuhusu Mpango Maalum wa kutoa huduma ya hifadhi ya jamii kwa sekta isiyo rasmi maarufu kama Informal Sector Scheme ambayo inajumuisha waendesha bodaboda, bajaji na mama lishe.
Bw. Njole alisema kuwa katika kuhakikisha watanzania wote wananufaika na huduma za hifadhi ya jamii, SSRA inafanya tafiti mbalimbali na kuhamasisha Mifuko ya Hifadhi ya Jamii kubuni mafao mbalimbali yanayolenga kuwafikia wananchi wote walio kwenye sekta isiyo rasmi.
Ili kufanikisha hilo, mwaka 2015 SSRA ilifanya utafiti katika sekta ya usafirishaji na kubaini kuwa asilimia 83 ya waendesha vyombo vya usafiri mijini wakiwemo waendesha bodaboda wako tayari kuchangia kwa hiari katika Mifuko ya Hifadhi ya Jamii.
“Kutokana na matokeo hayo mamlaka ilipendekeza kuanzishwa kwa Mpango Maalum ujulikanao kama Informal Sector Scheme ambapo watu waliojiajiri kwenye sekta isiyo rasmi watapata nafasi ya kunufaika na huduma ya hifadhi ya jamii.” Alisema Njole.
Njole aliongeza kuwa tayari baadhi ya mifuko imekwishaandaa mafao maalum yanayowalenga waendesha bodaboda, bajaji, daladala na mama lishe ambao watapata fursa ya kuchangia kiasi kidogo kila siku kulingana na kipato chao ili kupata huduma za hifadhi ya jamii kama vile akiba ya uzeeni, matibabu na mikopo.
Aidha, Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Uhamasishaji wa SSRA, Bi. Sarah Kibonde alieleza kuwa mamlaka hiyo inaendelea na zoezi la kutambua na kusajili Mifuko yote ya Bima ya Afya ya Jamii (CHFs) kwa lengo la kuboresha huduma na kuimarisha mfumo wa utoaji huduma za afya kwa wananchi.
Pia Bi. Sarah alisema kuwa SSRA imeandaa program maalum kwa ajili ya kutoa elimu ya hifadhi ya jamii kwa Wakurugenzi wa Halmashauri na Waratibu wa Mifuko ya Bima ya Afya ya Jamii nchini kote na zoezi hilo linaenda sambamba na usajili wa mifuko hiyo kwa mujibu wa Sheria ya SSRA, Sura ya 135.
“Program hii imeanzia Kanda ya Kati ambako ilihusisha Wilaya 27 na jumla ya CHF 5 zilisajiliwa na nyingine 22 zinakamilisha taratibu za usajili. Zoezi hili linatarajiwa kuendelea Juni 22 kwa mikoa ya Nyanda za Juu Kusini ambako jumla ya CHF 25 zinatarajiwa kusajiliwa.”
Sambamba na program hiyo Serikali kupitia Wizara ya Afya na Wizara yenye dhamana ya masuala ya hifadhi ya jamii na SSRA inafanya mapitio ya mfumo wa usimamizi wa Mifuko ya Bima ya Afya ya Jamii (CHF) ili kupata mfumo utakaoweza kutoa huduma ya afya kwa watanzania wote.
MATUKIO KATIKA PICHA KUTOKA BUNGENI MJINI DODOMA LEO

MATUKIO KATIKA PICHA KUTOKA BUNGENI MJINI DODOMA LEO

June 21, 2016

MHA1 
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Uratibu na Bunge, Mhe Jenista Mhagama akizungumza bungeni mjini Dodoma  katika vikao vya bunge la bajeti vinavyofanyika mjini humo.
MHA3 
Mh. George Masaju Mwanasheria Mkuu wa Serikali akijadiliana jambo na Mh. Ummy Mwalimu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto wakati wa vikao vya bunge m leo mjini Dodoma.
MHA4Waziri wa Sheria na Katiba Dk. Harisson Mwakyembe akijibu moja ya masawali ya waheshimiwa wabunge wakati wa kikao hicho.
MHA5 
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Uratibu na Bunge, Mhe Jenista Mhagama akiteta jambo na Mbunge wa jimbo la Mtera Mh. Livingstone Lusinde.
MHA6
Naibu Spika Mh. Tulia Akson akiongoza kikao cha bunge mjini Dodoma leo
MHA7 
Baadhi ya wageni wanafunzi waliohudhuria kikao cha leo wakifuatilia kwa karibu shughuli za bunge mjini Dodoma

WANANZENGO WA 102.5 LAKE FM MWANZA WALIVYOFURAHIA BIRTH DAY YA MHARIRI WAO.

June 21, 2016
June 21,2016, Mhariri wa 102.5 Lake Fm Mwanza #RahaYaRockCity #RedioYaWananzengo, Amos Gomba, anatimiza miaka 36 ikiwa ni jumla ya miaka yake tangu azaliwe June 21,1980 katika Kijiji cha Handali mkoani Dodoma.

Katika kusherehekea siku yake ya kuzaliwa, Uongozi wa #LakeFm umemuandalia hafla fupi ya kumpongeza, iliyofanyika katika ofisi za redio hiyo zilizopo Mtaa wa Liberty Jijini Mwanza.
Pichani ni Meneja wa Lake Fm, Genipher Deus, akimmwagia maji mtoto aliezaliwa hii leo kama ishara ya kumuogesha.
Imeandaliwa na BMG

MACHINGA JIJINI MWANZA WAKUTANA KUAMUA HATIMA YAO.

June 21, 2016
Mgeni Rasmi, Dkt.Kissui Steven Kissui ambae ni Mwenyekiti wa Shindano la Uwezeshaji Kiuchumi na Ajira Tanzania, akifungua Mkutano wa Wafanyabiashara ndogondogo (Machinga) Jijini Mwanza uliofanyika hii leo.
Na BMG

TIGO PESA YATOA FURSA ZA BIASHARA KWA WAJASIRIAMALI

June 21, 2016
Mkuu wa Huduma za Kifedha za Tigo, Ruan Swanepoel (katikati), akizungumza na waandishi wa habari Makao Makuu ya Tigo Makumbusho Dar es Salaam leo asubuhi kuhusu Tigo Pesa kutoa fursa za biashara kwa wajasiriamali. Kulia ni Mkuu wa Masoko wa Tigo, Temitope Ayedum na kushoto ni Meneja Chapa wa Tigo, William Mpinga.
Meneja Chapa wa Tigo, William Mpinga (kushoto), akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari.
Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.
Mkutano ukiendelea.



Na Dotto Mwaibale 
 WAJASIRIAMALI wa kidijitali pamoja na wabunifu wa matumizi ya simu Tanzania hivi sasa wanaweza kuleta ufumbuzi zaidi kwa mteja katika soko na kuongeza  shughuli zao za kibiashara  kupitia  jukwaa  la huduma za kifedha kwa simu la Tigo Pesa.
Tigo Pesa ambayo inaongoza Tanzania kwa kutoa  huduma za kifedha kwa njia ya simu imefuatilia  uhusiano wake wa karibu na Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) kwa kuanzisha programu ambazo zinatoa mwongozo wa hatua kwa hatua  kwa wajasiliamali wa kijitali kwa kuiunganisha Tigo Pesa katika matumizi yao. Hatua hiyo inajionesha katika wavuti wa www.tigo.co.tz.

 Akizungumza katika mkutano na waandioshi wa habari jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Huduma za 
Kifedha za Tigo, Ruan Swanepoel alisema, “Tigo imewekeza  zaidi ya dola milioni 15 katika kipindi cha miaka miwili iliyopita  katika kuboresha jukwaa la ngazi ya kimataifa  na huduma  ili kuendelea  kutoa  huduma sahihi za uhakika, zinazofikiwa na salama  kwa wateja.”
Swanepoel  alifafanua:“Jukwaa hilo la kuwanunganisha wateja wa Tigo Pesa na mitandao mingine  kwa kiwango kikubwa itapunguza  changamoto ambazo wajasiriamali wanakumbana nazo  katika kuunganisha huduma za kifedha kwa njia ya simu katika kupokea malipo  kutoka kwa wateja wake katika hali isiyo na hitilafu na hivyo kuongeza  wigo jumuishi kifedha kote nchini.”
Swanepoel  aliongeza kwamba, “Tigo pesa imejikita kuangalia  hali na uwezo wa kuwezesha maendeleo ya  huduma za ubunifu na kujumuisha bila tatizo mitandao mingine  ili kuwapa wateja  faida zaidi za huduma ya fedha kwa njia ya simu.”
Itakumbukwa kwamba kuanzia mwanzoni mwa mwaka 2016, Tigo Pesa  ilikamilisha  ushirikiano wake na  watoaji wengine wa huduma za fedha kwa njia ya simu  na benki nchini  kwa kuzifanya huduma hizo kupatikana kwa watu wengi zaidi.  Tigo Pesa pia ilizindua kifaa cha wateja kwa Android kwa watumiaji IOS, kwa kuwapatia njia rahisi watumiaji pindi wanapotumia  huduma zake.
Mfumo wa kuendesha na kutumia program hii ijulikanayo kama ‘Application Program Interface (API)  ni muundo wa maelekezo  na viwango vya kufikia mtandao  kwa kutumia zana  za kompyuta au zana za kimtandao. Ili kuzifikia programu za Tigo Pesa  inamaanisha wanafunzi wa vyuo, wajasiriamali wa biashara elektroniki , wabunifu wa vifaa  na wataalamu wengine wa teknolojia ya habari  wanaweza kuibuka na  vifaa  au kuwezesha  vifaa vilivyopo  kwa kuunganisha  ufumbuzi wao na Tigo Pesa.


Mchezo wa Shuga wabadilisha tabia za vijana

June 21, 2016
Mratibu wa mradi wa Shuga akijibu maswali yaliyokua yanaulizwa na kikundi cha wasikilizaji cha Iwawa- Makete mkoani Njombe

Wakionyesha furaha zao baada ya kuelewa mada ya siku ukihusianisha na maisha yao ya kila siku

Mwezeshaji wa kikundi cha wasikilizaji wa Kihesa, Manispaa ya Iringa mjini akitimiza jukumu lake la kuelimisha wenzake na kuwawezesha kushiriki katika majadiliano baada ya kusikiliza kipindi

Vijana wa Iringa wakionyesha nyuso zenye furaha baada ya kuongeza uelewa kupitia majadiliano baada ya kipindi cha saba cha mfululizo wa vipindi vya Shuga


 Kikundi cha wasikilizaji kutoka kijiji cha Kabanga, Kyela wakifurahia uelewa walioupata juu ya kukabiliana na changamoto zinazowakumba katika maisha yao


Kikundi cha wasikilizaji Jitambue 1 kutoka wilaya ya Kyela mkoani Mbeya wakijadiliana sehemu ya saba ya mfululizo wa vipindi vya mchezo wa redio wa Shuga.

Wakina mama wakifuatilia mjadala kuhusu kujitambua na namna ya kujikinga na Virusi vya UKIMWI pamoja 


 Mwana kikundi wa AMKA- Njombe vijijini akiwashirikisha wanakikundi wenzie uzoefu wake katika kukabiliana na changamoto za kutakwa kimapenzi na wanaume waliomzidi umri

Mwanachama ambaye amekua baba katika umri wa miaka 19 akionyesha shukrani zake kwa vipindi vya Shuga kwa kumuwezesha kujitambua, kwenda kupima afya yake na kujiwekea malengo ya kujilinda yeye, mama pamoja na mtoto dhidi ya maambukizi ya VVU


Tunajitambua, Tunajipenda na Tunajilinda na VVU. Tumepima - Kikundi cha AMKA kutoka Njombe




UGONJWA  wa UKIMWI umekuwa janga kubwa sana duniani huku wadau mbalimbali wakiendelea kutoa elimu na kuhamasisha katika kuanzisha programu mbalimbali za kubadilisha tabia chanya kwa jamii.


Akizungumza mwishoni mwa wiki, Mratibu wa mchezo wa redio wa Shuga alisema  tayari wameanzisha programu mbalimbali za vipindi vinavyolenga kuelimisha jamii hususani  vijana juu ya  maambukizi ya Virusi vya ukosefu wa kinga mwilini (UKIMWI), usawa wa jinsia, kufanya maamuzi sahihi, matumizi sahihi ya kinga na kuepukana na msongo rika.

Alisema mfululizo huu wa mchezo wa redio wa Shuga unawalenga zaidi vijana hususan wasichana, kwa kuangalia mtazamo wao, matarajio  pamoja na changamoto wanazopitia kwa  njia sahihi za kukabiliana na changamoto ili kutimiza malengo yao. 

"Mchezo wa redio wa Shuga ulianzishwa mnamo mwaka 2014 kwa ushirikiano kati ya MTV, HIV and AIDS Free Generation, Shirika la TACAIDS pamoja na UNICEF. Baada ya mafanikio makubwa msimu wa kwanza, TACAIDS na UNICEF pamoja na wadau wengine waliamua kupanua wigo wa program hii kwa kuandaa vipindi zaidi ili kuimarisha tabia chanya zilizojengwa katika msimu wa kwanza wa vipindi vya Shuga," alisema Laizer 

Alisema mfululizo wa vipindi vya redio vya Shuga awamu ya pili vilianza kupitia redio mbalimbali nchini kuanzia wiki ya pili ya mwezi wa nne 2016 kwa lengo la kuendeleza elimu ya masula ya UKIMWI.

"Katika kuboresha utoaji elimu kuhusiana na maudhui ya vipindi, kampuni ya True Vision Production imefanya ufuatiliaji wa utekelezaji wa awamu ya pili ya  mfululizo wa vipindi vya redio vya Shuga katika kuhakikisha jamii inakuwa na uelewa juu ya masuala hayo." alisema Laizer. "Kwa sasa, vituo mbalimbali vya redio vinarusha sehemu ya nane ya mfululizo wa vipindi vya Shuga." Aliongezea Laizer. 


Alisema Matokeo ya mradi huu yameanza kuonekana na vijana ambao ni walengwa wakuu wametoa ushuhuda wao kuhusiana na kipindi hicho cha Shuga na kusema kuwa klipindi kimewaletea mabadiliko makubwa.


‘Vijana tunajitambua, tumehamasika kwenda kupima afya zetu, tunajua njia sahihi za kujilinda na magonjwa ya zinaa na pia tunajiwekea mipango endelevu," alisema Abbas Boniphace, mmoja wa wasikilizaji wa kipindi cha Shuga kutoka Njombe

"Ningepata nafasi ya kusikia Shuga mapema nisingepata ujauzito katika umri mdogo. Sikua na uelewa wakati huo, sasa najitambua, nimepima na najilinda, siwezi kudanganyika" alisema Herieth kutoka Njombe.

"Wazazi huogopa kutuambia ukweli juu ya maswala yahusuyo VVU na UKIMWI ila Shuga inaelezea kwa uwazi zaidi." Alisema Shamila Juma, mwana kikundi cha wasikilizaji wa vipindi vya Shuga

photo Krantz Mwantepele Founder & CEO , KONCEPT Phone: +255-712579102 /+255-767392840 Email: krantzcharles@gmail.com Blog: www.mwanaharakatimzalendo.blogspot.com
SERIKALI YAAGIZA WAKIMBIZI WANAJESHI, WENYE SILAHA WAJISALIMISHE

SERIKALI YAAGIZA WAKIMBIZI WANAJESHI, WENYE SILAHA WAJISALIMISHE

June 21, 2016
Serikali ya Tanzania imewataka wakimbizi wote ambao walikuwa wanajeshi kutoka nchi walizokuwepo, kuripoti kwenye mamlaka husika ili waweze kupewa uangalizi maalum (special protection) kama wanajeshi.
Kauli hiyo ya serikali imetolewa na Mkuu wa mkoa wa Kigoma, Brigedia Jenerali (Mstaafu) Emmanuel Maganga, wakati wa maadhimisho ya siku ya wakimbizi duniani yaliyofanyika kambi ya wakimbizi Nyarugusu, wilayani Kasulu, mkoani Kigoma.

Alisisitiza kuwa wakimbizi ambao wako nchini wakijua ni wanajeshi ni lazima wasajiliwe na mamlaka husika.
Aidha Maganga aliwataka vile vile wakimbizi wote ambao wanamiliki silaha wazisalimishe kwa hiari yao wenyewe.
Alisema kumekuwa na matukio mengi ya ujambazi wa kutumia silaha na hivyo kuhatarisha amani na kuwaamuru wenye silaha kuzisalimisha mara moja ili waende sawa na sheria za nchi walikopata hifadhi.
Maandamano ya wakimbizi yakiingia uwanjani katika sherehe za maadhimisho ya siku ya wakimbizi duniani yaliyofanyika katika kambi ya wakimbizi Nyarugusu, wilayani Kasulu, mkoani Kigoma. (Picha na story Modewjiblog)

Mkuu huyo wa mkoa pia alitoa wito kwa mashirika ya misaada duniani kutoa misaada inayoowana na misaada inayotolewa kwa nchi zilizoendelea na kuongeza kuwa mahitaji ya binadamu ya msingi hayatofautiani iwe nchi zilizoendelea au zinazoendelea.

Alisema kuwa wakimbizi waliopo kwenye nchi zilizoendelea hupewa makazi ya kudumu na vyakula tofauti tofauti wakati waliopo kwenye nchi zinazoendelea hupewa mahema na chakula aina moja ambayo ni mahindi.

“Mwaka jana tulishindwa kuadhimisha siku ya wakimbizi duniani kwa kuwa tulikuwa tunawapokea wakimbizi kutoka Burundi,” alisema.

Alisema wakimbizi wameongezeka sana nchini na sasa hivi kuna makambi matatu yanayowahifadhi wakimbizi nchini.

Wakati huo huo Tanzania imepongezwa kwa ukarimu wake kwa kuwahifadhi wakimbizi kwa zaidi ya miongo minne sio tu kwenye ukanda wa Afrika Mashariki na hata duniani.

Mwakilishi mkazi wa shirika la kuhudumia wakimbizi UNHCR , Chansa Kapaya alisema hayo katika sherehe za kuadhimisha siku ya wakimbizi duniani yenye kauli mbiu kuwa “Tupo Pamoja na Wakimbizi, Tafadhali ungana nasi”.

“Tanzania ni mfano wa kuigwa kwa mfano mzuri wa kuwahifadhi wakimbizi wengi duniani na pia kuwatafutia suluhu,” alisema.

Mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Brigedia Jenerali Mstaafu, Emmanuel Maganga akizungumza na hadhira iliyokusanyika katika sherehe za maadhimisho ya siku ya wakimbizi duniani yaliyofanyika katika kambi ya wakimbizi Nyarugusu, wilayani Kasulu, mkoani Kigoma.

Alisema mwaka 2014 Tanzania iliwapa uraia wakimbizi zaidia ya 162,000 baada ya kuishi nchini kwa zaidi ya miaka 40.

Aliongeza kuwa, wakimbizi wanapaswa kuthaminiwa kama binadamu wengine kwa kuwa hakuna mtu anayechagua kuwa mkimbizi.

Kapaya alisema kuwa kwa sasa kambi ya Nyarugusu ina wakimbizi zaidi ya 131,733 ambao ni wengi zaidi na kusababisha msongamano unaohatarisha maisha yao.

Mwakilishi wa Shirika linalohudumia wakimbizi nchini (UNHCR), Chansa Kapaya akisoma risala wakati wa sherehe za maadhimisho ya siku ya wakimbizi duniani yaliyofanyika katika kambi ya wakimbizi Nyarugusu, wilayani Kasulu, mkoani Kigoma.
Pichani juu na chini ni baadhi ya wageni waalikwa, wafanyakazi wa Shirika la UNHCR na wadau wa maendeleo waliohudhuria sherehe hizo wakifuatilia hotuba mbalimbali.
Mwakilishi wa Shirika linalohudumia wakimbizi nchini (UNHCR), Chansa Kapaya akipitia ratiba ya maadhimisho ya siku ya wakimbizi duniani ambapo kitaifa yamefanyika mkoani Kigoma katika kambi ya wakimbizi Nyarugusu. Kulia kwake ni mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Brigedia Jenerali Mstaafu, Emmanuel Maganga akifuatiwa na Mkuu wa Wilaya ya Kasulu, Gerald Guninita.
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Brigedia Jenerali Mstaafu, Emmanuel Maganga (kulia) akifurahi jambo na Mkuu wa Wilaya ya Kasulu, Gerald Guninita wakati burudani mbalimbali zikiendelea kwenye maadhimisho ya siku ya wakimbizi duniani ambapo kitaifa yamefanyika katika kambi ya wakimbizi Nyarugusu, wilayani Kasulu, mkoani Kigoma.
Mwakilishi wa Shirika linalohudumia wakimbizi nchini (UNHCR), Chansa Kapaya akiteta jambo na Ofisa wa UNHCR Tanzania anayeshughulika na mambo ya usalama kambini, David Mulbah (kulia) wakati wa sherehe za maadhimisho ya siku ya wakimbizi duniani yaliyobeba kauli mbiu "Tupo Pamoja na wakimbizi. Tafadhali ungana nasi." ambapo kitaifa yamefanyika katika kambi ya Nyarugusu, wilayani Kasulu, mkoani Kigoma.
Bendi ya muziki wa Live ya vijana wakimbizi inayojulikana kama Nyota ya Asubuhi ya kambi ya Nyarugusu ikitoa burudani ya aina yake wakati wa sherehe za maadhimisho ya siku ya wakimbizi duniani.
Wanamuziki wa bendi ya Nyota ya Asubuhi wakisakata sebene kwenye maadhimisho ya siku ya wakimbizi duniani.
Mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Brigedia Jenerali Mstaafu, Emmanuel Maganga na Mwakilishi wa Shirika linalohudumia wakimbizi nchini (UNHCR), Chansa Kapaya kwa pamoja wakikabidhi jezi na zawadi kwa timu wakimbizi ya vijana ya wanawake ya mpira wa miguu katika maadhimisho ya siku ya wakimbizi duniani ambapo kitaifa yamefanyika mkoani Kigoma katika kambi ya wakimbizi Nyarugusu.
Mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Brigedia Jenerali Mstaafu, Emmanuel Maganga na Mwakilishi wa Shirika linalohudumia wakimbizi nchini (UNHCR), Chansa Kapaya kwa pamoja wakikabidhi zawadi kwa baadhi ya watoto wakimbizi waliofanya vizuri kwenye masomo yao.

Mkuu wa ofisi ya Shirika la Umoja wa Mtaifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) Kasulu, Kigoma, Amah Assiama-Hillgartner akitoa neno la kufunga sherehe za maadhimisho ya siku ya wakimbizi duniani.
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Brigedia Jenerali Mstaafu, Emmanuel Maganga akiongozwa na Mkuu wa Kambi ya Wakimbizi Nyarugusu, Sospeter Boyo (kulia) kutembelea mabanda yenye bidhaa mbalimbali zinazotengenezwa kwa mikono na vikundi mbalimbali vya wakimbizi wanaoishi kwenye kambi hiyo wakati wa sherehe za maadhimisho hayo.
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Brigedia Jenerali Mstaafu, Emmanuel Maganga akiwa kwenye banda la kinamama wajasiriamali wa mikate.
Mabanda yenye bidhaa mbalimbali zinazotengenezwa kwa mikono na vikundi mbalimbali vya wakimbizi wa Congo na Burundi walipata fursa ya kuonyesha kazi zao kwa mgeni rasmi, Mkuu wa Mkoa wa Kigoma.
Mwakilishi wa Shirika linalohudumia wakimbizi nchini (UNHCR), Chansa Kapaya (tisheti nyeusi) akipata maelezo kutoka kwa moja ya kikundi kinachojishughulisha na ufugaji wa Kuku na Kware alipowasili kwenye viwanja vya kambi ya Nyarugusu na kutembelea mabanda mbalimbali katika sherehe za maadhimisho ya siku ya wakimbizi duniani ambapo kitaifa yamefanyika Kigoma, kambi ya Nyarugusu.
Mkuu wa ofisi ya Shirika la Umoja wa Mtaifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) Kasulu, Kigoma, Amah Assiama-Hillgartner (kushoto) akitoa maelezo ya kifaa maalum cha kutotolea vifaranga kilichotengenezwa kienyeji (incubator) na wakimbizi wa Nyarugusu kwa Mwakilishi wa Shirika linalohudumia wakimbizi nchini (UNHCR), Chansa Kapaya (kulia) wakati wa maadhimisho ya siku ya wakimbizi duniani.
Mabinti wa kirundi wakitoa burudani kwenye maadhimisho hayo.
Burudani ya ngoma za wakimbizi wa Congo DRC.
Pichani juu na chini ni Baadhi ya wakimbizi wa Congo na Burundi waliohudhuria sherehe za maadhimisho ya siku ya wakimbizi duniani ambapo kitaifa yamefanyika katika kambi ya Nyarugusu, wilayani Kasulu, mkoani Kigoma.

-- Zainul A. Mzige, Operation Manager, MO BLOG, www.modewjiblog.com +255714940992.