Tigo 4G LTE yaingia kwenye miji 5 kanda ya ziwa

May 04, 2016


Meneja Mkuu wa Tigo Diego Gutierrez akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu mpango wa Tigo kusambaza mtandao wa 4G lte nchi nzima pembeni yake ni Afisa Mkuu wa Ufundi wa teknolojia ya mawasiliano wa Tigo Jerome Albou katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika mapema leo katika ofisi za makao makuu ya Tigo Kijitonyama Jijini Dar es salaam.

Waandishi wa habari wakichukua taaarifa


                                Mtandao wa Tigo 4G LTE ni mpana na wa kasi Tanzania

Dar es Salaam, Mei 4, 2016-Kampuni ya simu ya Tigo ambayo inaendesha maisha ya kidijitali Tanzania imetangaza kuzinduliwa kwa  huduma ya 4G LTE katika miji mingine mitano ya kanda ya ambayo  ni Tabora, Musoma, Bukoba, Kigoma na Shinyanga.

 Kampuni hiyo awali ilizindua  huduma hiyo  jijini Dar es Salaam  mwanzoni mwa mwaka jana  na baadaye kuisambaza katika miji ya Arusha, Tanga, Dodoma, Morogoro, Moshi na Mwanza na hivyo kuifanya  kuwa kampuni ya simu  yenye mtandao mpana na wa kasi  wa 4G LTE nchini Tanzania.
Ikiwa inachukuliwa kuwa ni  teknolojia  nzuri  na  ya uhakika katika sekta ya mawasiliano ya simu duniani ya kupata  intaneti, kasi ya teknolojia ya 4G LTE  ni takribani mara tano zaidi ya teknolojia ya 3G na Tigo inaifanyia kazi kwa kina ili kuongeza ubora wa huduma hiyo na mtandao wa 4G kutokana na matumizi ya wateja kuwa  nayo yanaongezeka kwa kasi  kubwa.

Hivi sasa Tigo ina timu inayofanya kazi saa zote  kuimarisha na  kukuza ubora wa teknolojia ya 4G. Matokeo yake ni kwamba  mtandao wa 4G umekuwa unategemewa  kwenye miji ambamo upo (Arusha, Tanga, Dodoma, Morogoro, Moshi na Mwanza).

Mtandao wa 4G LTE unatoa intaneti ya kasi ya kurambaza (surf) na kupakua vitu, kufanya  miito ya simu ya kuonana (Skype)  isiyo na kikomo.  Kutokana na uzinduzi wa hivi karibuni  wa video za bure  kupitia YouTube nyakati za usiku,  mtandao wa 4G LTE unawawezesha wateja kwa kiwango kikubwa  kupata uzoefu wa kutiririsha video zilizo na uangavu mkubwa. Aidha kutokana na ushirikiano na   Facebook mteja wetu wa 4G pia anaweza kufurahia kutiririsha video zilizomo kwenye  mitandao maarufu ya kijamii  duniani.

Pia,  mteja akiwa na  4G LTE  anaweza kupakua mafaili  makubwa  (sinema, mafaili yanayohusiana na kazi) au vifaa  na hali kadhalika kucheza michezo kwa njia ya mtandao.

Akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam  leo, Meneja Mkuu wa Tigo Diego Gutierrez,   alisema  mpango wa kupanua  teknolojia ya 4G hadi kwenye maeneo yote ya nchi upo mbioni  ambapo kampuni hiyo imejikita kwenye kuwapa wateja wake huduma  zenye ubora  duniani ambazo zitawawezesha  kufurahia  mtindo wa maisha ya kidijitali.

 “Kupanua mtandao wa 4G LTE nchi nnzima  kwa mara nyingine kunaonesha sio tu Tigo kuongoza  kwenye kutoa  teknolojia  na ubunifu wa kisasa  ndani ya soko  bali pia kusisitizia  kujituma kwetu  katika kuongeza fursa ya kufikia  intaneti kwa Watanzania walio  wengi kwa kadri iwezekanavyo,’ alisema Gutierrez.

Kwa mwaka huu 2016,  Tigo itawekeza  zaidi ya dola milioni 75 kwenye upanuzi wa mtandao na kuimarisha ubora wake kwa  kukuza maeneo ya teknolojia ya 4G na 3G, mkongo wa mawasiliano na hali kadhalika kuongeza idadi ya sehemu za kutolea  huduma kwa wateja  nchi nzima.
 “Tukiwa kama kampuni tunatambua  umuhimu wa  wa ubora na ukaribu  kwa wateja wetu na tunafanya kazi  ili kufikia malengo hayo katika siku za karibuni,” alisema Gutierrez.
 “Hivi sasa pia tuna programu ya kufanya mtandao  kuwa wa kisasa ambao unajumuisha  kuongeza  uwezo wa 4G  kwenye miji yote 12 ambako tuna mtandao wa 4G  pamoja na kuongeza  mtandao wa 3G kufika maeneo yote nchini,” alisema Gutierrez  na kuongeza kuwa wateja wa Tigo  katika miji ya Mbeya, Mtwara na Lindi  wajitayarishe  kufurahia  huduma ya Tigo 4G LTE  itakayoanza kutolewa  siku za hivi karibuni.


MWISHO 
photo Krantz Mwanteple C.E.O & Founder, MWANAHARAKATI MZALENDO MEDIA Phone: +255-712579102 /+255-767392840 Email: krantzcharles@gmail.com Website: www.mwanaharakatimzalendo.blogspot.com Whatsapp: 0712579102 "HABARI MAKINI KWA WATU MAKINI"

VYOMBO VYA HABARI ASILIA (wa makaratasini) TAABAN WAKATI VYA digitali (wa mitandaoni) VYAPETA

May 04, 2016
Vyombo vya habari vya asilia hususan magazeti vinakufa. Hivi sasa vvyombo hivyo vinajikongoja kutokana na  mauzo hafifu  na mdororo wa mapato kutoka matangazo na kupunguza wafanyakazi. 
Ila wakati idadi ya wasomaji wa habari mtandaoni ikizidi kukua, wanaoperuzi mtandaoni  humo hawatumii muda mwingi kwenye magazeti tando, utafiti wa Pew Research Centre unaeleza. 

Katika utafiti wake wa hali ya vyombo vya habari 2015 ("State of the News Media 2015,”) imeonesha kwamba katika vyombo vya habari vya karatasi (print media), Digitali na TV, imeonesha Dhahiri kwamba magazeti yanaelekea kuzimu. 
Utafiti huo umetolea mfano magazeti makubwa ambapo wasomaji wake wa mtandaoni wamewashinda kwa mbali kwa idadi ya wasomaji wa makaratasini, ambapo gazeti kubwa sana la New York Times la Marekani limetangaza kuwa nakala zake zipatazo 650,000 kwa wiki zimepitwa kwa mbali sana na wa mitandaoni 
 Hivi sasa kuna mjadala mitandaoni endapo kama Tanzania iko ama itafika huko. Mabishano ni makali ambapo wa makaratasini wanashikilia msimamo wao kuwa nchini hapa tasni ya habari mtandaoni bado ni change sana kuweza kutishia amani ya magazeti. 
Upande wa digitali unajibu kwamba endapo kama kuna wahariri viburi wanaobeza kasi ya mitandao, basi wakae mkao wa kulala njaa muda si mrefu ujao, maana ni wachache wanaoendelea kupata habari kwa njia asili ya magazeti. 
Upande wa digitali umeyasifia magazeti ya Global Publishers na la Mwananchi  anbayo ni dhahiri yana wahariri wanaokwenda na wakati na wanaojua nini wanachokifanya kwa kuanza na mapema kuogelea bahari ya maendeleo ya tasnia kwa vitendo kwa kuwa na vitengo vya mtandao vinavyopelekesha mbio magazeti yanayobeza technolojia hio kwa kubuni.
"Ni kweli kwamba Tanzania ni bado sana kiteknolojia na miundombini kiasi cha habari za mtandaoni zikatishia uhai wa habari za makaratasini, lakini si uwongo kwamba ukizingatia uharaka na gharama pamoja na kwenda na wakati muda si mrefu print media itakwenda na maji", amesema blogger mmoja ambaye pia ni mwanahabari kwenye moja ya magazeti makubwa nchini.

___________________________________________________________________________________ Joachim Mushi, Mwenyekiti wa Tanzania Bloggers Network (TBN) na Mhariri Mkuu wa Thehabari.com. Mail address:- mushi@thehabari.com/ jomushi79@yahoo.com/ info@thehabari.com Mobile:- 0717 030066 / 0756 469470 Web:- www.thehabari.com http://joemushi.blogspot.com
SERIKALI ITAENDELEA KUSIMAMIA HAKI ZA MTOTO WA KIKE

SERIKALI ITAENDELEA KUSIMAMIA HAKI ZA MTOTO WA KIKE

May 04, 2016

download 
Na Eleuteri Mangi-MAELEZO, Dodoma
…………………………………………..
Serikali itaendelea kusimamia haki ya mtoto wa kike ya kupata elimu na kuwachukulia hatua kali za kisheria ikiwemo kuwapeleka mahakamani wale wote wanaowapa ujauzito wanafunzi na kuwakosesha kupata elimu ambayo ni haki yao ya msingi.
Kauli hiyo imetolewa na Naibu Waziri Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Seriklali za Mitaa (TAMISEMI) Seleman Jafo alipokuwa akijibu swali la nyongeza la Janeth Mbene wa Ileje baada ya kujibu swali la msingi lililohoji kuhusu kushuka kwa kiwango cha elimu nchini.
“Serikali haitamvumilia mwanaume yeyote atakayempa ujauzito mwananfunzi na kukwamisha kupata elimu kwa wakati na kumharibia malengo ya maisha yake” alisema Naibu Waziri Jafo.
Hatua hiyo ya Serikali itawahakikishia na kuwawezesha watoto wa kike nchini kusoma na kumaliza masomo yao hatua ambayo itakuwa msaada kwa watoto hao wa kike, familia zao na taifa kwa ujumla.
Akisistiza msimamo wa Serikali kuhusu wanaume wanaowapa ujauzito wanafunzi, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu alisema kuwa Serikali haipo tayari kuwavumilia wanaume wenye tabia ya kuwakwamisha watoto wa kike kupata elimu kwa kuwapa ujauzito na itahakikisha sheria inachukua mkondo wake ili kukomesha tabia hiyo.
Akizungumzia tatizo hilo la wanafunzi kupata ujauzito wakiwa shuleni, Mbunge wa Jimbo la Igunga Seif Khamis Gulamali alisema kuwa tatizo hilo lipo sehemu mbalimbali nchini ambapo watoto hubebeshwa mimba wakiwa katika umri mdogo wa kuwa shuleni na tatizo hilo linaendelea kuleta hasara kubwa kwa wanafunzi wenyewe, familia zao na taifa kwa ujumla.
Gulamali alisema kuwa hali hiyo inatokana na hulka ya makabila mengi nchini hasa ya wafugaji hali inayosababishwa na tabia ya kuhama hama kutafuta malisho na maji kwa ajili ya mifugo yao.
“Wapo wazazi wanaowapa maelekezo watoto wao wasifaulu mitihani yao ili waweze kuolewa na wamegeuzwa kuwa sehemu ya kipato cha familia zao kwa kupata mahari” alisema Gulamali.
Ili kukomesha tabia hiyo ya kuwapa ujauzito watoto wenye umri mdogo hasa kwa wafugaji, Gulamali alisema kuwa ipo haja ya Serikali kupitia Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi pamoja na Wizara ya Maji na Umwagiliaji kuweka mazingira mazuri ambayo yatawapa wananchi wengi fursa ya  kuwekeza kwenye sekta ya kilimo na mifugo kwa kuwahakikishia upatikanaji wa maji kwa wingi ili wananchi wazalishe na kuondokana na tabia ya kuhama hama kwa wazazi wao ambayo imekuwa kikwazo kikubwa kwa watoto kupata elimu.
Kuhusu shilingi milioni 50 zilizoahidiwa na Serikali kwa kila kijiji hapa nchini, Gulamali alisema kuwa ni vema ufikiriwe mfumo wa kupeleka hizo fedha ambao utakuwa wa tija kwa wananchi na taifa kwa ujumla utakaohkikisha fedha hizo zitakuwa endelevu na kuwarahisishia wananchi kazi na kuongeza uzalishaji wa mazao yatakayowaongezea kipato.
Hatua hiyo itasaidia taifa kuwa na matumizi bora ya rasilimali fedha zinazotolewa na Serikali kwa kuwekeza kwenye sekta za viwanda, mifugo, uvuvi na kilimo ambapo Tanzania kuna mvua ya kutosha, mabonde yenye rutuba, mito, maziwa, bahari pamoja na watu ambao ndio msingi wa maendeleo kwa taifa kwa kuongozwa na Dira ya Maendeleo ya Taifa ifikapo 2025 Tanzania kuwa nchi ya uchumi wa kati.
LAPF YAKABIDHI MADAWATI YA SHILINGI MILIONI KUMI KWA MKUU WA WILAYA YA KINONDONI

LAPF YAKABIDHI MADAWATI YA SHILINGI MILIONI KUMI KWA MKUU WA WILAYA YA KINONDONI

May 04, 2016

Meneja Mawasiliano wa Mfuko  wa Pensheni LAPF Bw. James Mlowe amekabidhi Jumla ya madawati 124  kwa ajili ya shule za Manispaa ya Kinondoni, msaada huo umetolewa na taasisi hiyo unagharimu kiasi cha shilingi milioni  10,000,000/= yamekabidhiwa kwa  Mgeni rasmi Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh. Salum Ali Hapi. JAMES1 
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh. Salum Ally Hapi (wa pili kushoto) akimshukuru Meneja Masoko na Mawasiliano wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF James Mlowe mara baada ya kupokea msaada wa madawati 124 kwa ajili ya Shule ya Msingi Nakasangwe iliyopo Kata ya Wazo. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam jana.  Kulia ni Ofisa Elimu Msingi Wilaya ya Kinondoni, Kiduma Mageni.
JAMES2 
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Mh. Salum Ally Hapi (kulia) akipokea msaada wa madawati 124 kutoka kwa Meneja Masoko na Mawasiliano wa mfuko wa pensheni wa LAPF, James Mlowe kwa ajili ya shule za Serikali Manispaa ya Kinondoni. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam jana. Katikati ni Ofisa Elimu Msingi  Wilaya ya Kinondoni, Kiduma Mageni. 
JAMES3
Mkuu wa Wilayaya Kinondoni, Salum  Ally Hapi akizungumza katika hafla ya kupokea madawati 124 yaliyotolewa na Mfuko wa Pensheni wa LAPF jijini Dar es Salaam jana.
JAMES4 
Kaimu Meneja wa Mfuko wa Pensheni wa  LAPF Kanda ya Dar es Salaam, Bw. Yesaya Mwakifulefule akizungumza katika hafla hiyo.
JAMES5 
Meneja Masoko na Mawasiliano wa  Mfuko wa Pensheni wa LAPF, Bw. James Mlowe akizungumza katika hafla hiyo.

HOTUBA YA MHESHIMIWA DKT. JOHN POMBE JOSEPH MAGUFULI, RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, KWENYE KILELE CHA SIKUKUU YA WAFANYAKAZI DUNIANI MEI MOSI 2016 ITAKAYOFANYIKA DODOMA

May 04, 2016

HOTUBA YA MHESHIMIWA DKT. JOHN POMBE JOSEPH MAGUFULI, RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, KWENYE KILELE CHA SIKUKUU YA WAFANYAKAZI DUNIANI MEI MOSI 2016 ITAKAYOFANYIKA DODOMA

Mhe. Samia Hassan, Makamu wa Rais;
Mhe. Kassim Majaliwa, Waziri Mkuu;
Ndugu Gratian Mukoba, Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA);
Mama Nortubunga Maskini, Makamu wa Rais wa TUCTA;
Mheshimiwa Jenista Mhagama, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu;
Mhe. Tulia Ackson, Naibu Spika;
Balozi Injinia John Kijazi, Katibu Mkuu Kiongozi;

Mheshimiwa Jordan Rugimbana, Mkuu wa Mkoa wa   Dodoma;
Waheshimiwa Mawaziri wote, na Waheshimiwa Wabunge mliopo;
Bi. Mary Kawar, Mkurugenzi wa Shirika la Kazi Duniani (ILO), Ofisi ya Nchi za Afrika Mashariki;
Waheshimiwa Mabalozi mliopo;
Waheshimiwa Majaji,
Mheshimiwa Almas Maige, Mwenyekiti wa Chama cha Waajiri Tanzania;
Dr. Aggrey Mlimuka, Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Waajiri Tanzania (ATE);
Ndugu Nicholaus Mgaya, Katibu Mkuu wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (TUCTA);
Viongozi wa Vyama vya Wafanyakazi;
Viongozi na Maafisa wa Serikali mliopo;
Wawakilishi wa Vyama vya Siasa mliopo; Mzee Mangula, Makamu Mwenyekiti wa CCM
Bwana Kimbisa (Mb), Mwenyekiti wa CCM Mkoa;
Wanahabari;
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Dodoma;
Ndugu Wananchi;
Ndugu Wafanyakazi;
Mabibi na Mabwana.
Awali ya yote napenda kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutupa uhai na afya njema na kuweza kukutana hapa. Leo ni siku muhimu sana. Tupo hapa kwa ajili ya kuenzi na kuthamini mchango wa wafanyakazi wa Tanzania, wake kwa waume, walioko sekta binafsi na ya umma, na ambao kila siku tangu asubuhi hadi jioni wamekuwa wakivuja jasho kwa ajili ya maendeleo ya taifa letu.
Hii si mara yangu ya kwanza nashiriki Sherehe ya Siku ya Wafanyakazi, maarufu kama Mei Mosi. Nimeshiriki kwenye sherehe hizi mara kadhaa. Lakini leo nashiriki kipekee kabisa. Nashiriki kwa mara ya kwanza tangu nichaguliwe kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mwezi Oktoba 2015. Hivyo, napenda kuchukua nafasi hii kuwashukuru Viongozi wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (TUCTA) na Vyama vyote vya Wafanyakazi nchini kwa kunialika ili nijumuike nanyi kwenye Sherehe hizi za Siku ya Wafanyakazi Duniani mwaka huu. Aidha, napenda kuwashukuru wafanyakazi wote wa Tanzania kwa kunipa kura nyingi zilizoniwezesha  kuchaguliwa kuwa Rais wa nchi hii. Naahidi kwenu kuwa sitawaangusha.
Nitumie fursa hii pia kuwapongeza sana wananchi wa  Mkoa Dodoma chini ya Uongozi wa Mkuu wa Mkoa, Mheshimiwa Jordan Rugimbana kwa kukubali kuwa wenyeji  wa Sherehe hizi pamoja na maandalizi mazuri mliyofanya kufanikisha sherehe hizi. Sherehe zimefana, hongereni sana! Nawashukuru pia wananchi wa Dodoma kwa kunipa kura nyingi wakati wa uchaguzi Mkuu wa mwaka jana.
Aidha, ninawashukuru sana Wafanyakazi na Wananchi wote mliojitokeza hapa leo kwa wingi ili kujiunga na wenzetu duniani kote kusherehekea siku hii muhimu ya Wafanyakazi Duniani.
Ndugu Wafanyakazi na Wananchi kwa ujumla;
Duniani kote wafanyakazi ni nguzo muhimu ya maendeleo. Hakuna taifa lolote duniani ambalo limeweza kuendelea bila kutegemea wafanyakazi wake. Hapa nchini, wafanyakazi wametoa mchango mkubwa kwa maendeleo ya taifa letu tangu kipindi cha ukoloni hadi sasa. Bila shaka wengi wetu hapa tunafahamu namna wafanyakazi na vyama vya wafanyakazi vilivyoshiriki kikamilifu katika harakati za ukombozi wa nchi yetu. Baada ya nchi yetu kupata uhuru, wafanyakazi wameendelea kutoa mchango mkubwa kwa maendeleo ya nchi yetu.
Nitumie fursa hii kuwapongeza wafanyakazi kote nchini kwa kazi kubwa na nzuri mnayoifanya kwa maendeleo ya taifa letu. Ninyi ndio mmejenga miundombinu mbalimbali tunayoitumia hivi sasa, ninyi ndio mnahakakikisha Watanzania wanapata huduma bora za elimu na afya lakini hata ulinzi na usalama wa taifa letu kwa kiwango kikubwa unategemea ninyi wafanyakazi. Hongereni sana wafanyakazi!

HUAWEI YAUNGANA NA WATENGENEZAJI MASHUHURI WA KAMERA DUNIANI, LEICA KUTENGENEZA SIMU P9

May 04, 2016

Huziangyang Jacko, Meneja wa Huawei nchini Tanzania.
                                                      
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
29 Aprili 2016
Dar es Salaam
Mkakati wa Huawei katika kubadili namna uonavyo dunia iliyokuzunguka

Mwezi Aprili, Huawei wamezindua simu iliyokua ikisubiriwa kwa muda mrefu katika mlolongo wao wa simu zao za P Series; Huawei P9. Uzinduzi wa Huawei P9 umezingatia kipaumbele cha teknolojia ya hali ya juu. Toleo hili la tisa la P Series limewezeshwa na Kampuni ya Huawei pamoja na kampuni mashuhuri kwa utengenezaji wa camera duniani Leica. Simu hii ina kamera ya kipekee yenye lenzi mbili, ambayo imeweka rekodi katika teknolojia ya kamera za simu za kisasa, ikiwa na mwanga Zaidi na ubora Zaidi, kupata picha zenye rangi nzuri Zaidi katika staili ya Leica ya kipekee.

KUTANA NA ‘GREEN VOICES’, SAUTI ZA AKINAMAMA WAPAMBANAO NA MABADILIKO YA TABIANCHI

May 04, 2016
Akinamama wanaoshiriki katika mradi wa kupaza sauti za wanawake wanaopambana na mabdiliko ya tabianchi – Green Vocies katika picha ya pamoja na viongozi wa Foundation For Women of Africa na wafadhili wa mradi huo, mara baada ya uzinduzi wa mradi huo Madrid, Spain hivi karibuni.

Mama Maria Tereza (katikati) - Rais wa taasisi ya Foundation for Women of Africa akiwa na waandishi wa habari wanaotekelza mradi wa Green Voices wakati wa hafla ya kuwakaribisha kinamama nchini Spain. Kutoka kushoto ni Secelela Balisidya, Tukuswiga Mwaisumbe, Farida Hamis, Siddy Mgumia na aliyechuchumaa Judica Losai.


Akinamama wanaoshiriki katika mradi wa kupaza sauti za wanawake wanaopambana na mabdiliko ya tabianchi – Green Vocies katika picha ya pamoja na uongozi wa chuo kikuu cha Universitad Automous De Madrid, mara baada ya kutembelea mazingira ya chuo hicho Madrid, Spain hivi karibuni.

Ziara ya mafunzo kujifunza jinsi ya kutengeneza mbolea ya mboji.

Ziara ya mafunzo kujifunza majiko yanayotumia nishati ya jua.

Ziara ya mafunzo katika chumba cha habari cha gazeti la El Pais.

Akimama na wawezeshaji wa mafunzo katika picha ya pamoja darasani.


WANAWAKE wapatao 15 hivi karibuni walihudhuria mafunzo ya kuongeza ujuzi wa jinsi ya kupambana na mabadiliko ya tabianchi nchini Spain. Mafunzo na mradi huo vinafadhiliwa na Taasisi inayojihusisha na maendeleo ya wanawake wa Afrika, ijulikanayo kama Foundation for Women of Africa  inayoongozwa na Makamu wa Rais mstaafu waSpain Mama  María Teresa Fernández de laVega.
Taasisi hiyo itafanya kazi na wanawake hao 15 wa kitanzania kupitia miradi inayosaidia nchi kupambana na mabadiliko ya tabianchi. Wanawake hao ambao kati yao watano ni waandishi wa habari kila mmoja atatekeleza mradi mmoja, huku waandishi wa habari wakisaidia kupaza sauti za akinamama hao kupitia vyombo mbalimbali vya habari nchini.
Mradi huu unaojulikana kama GREEN VOICES una lengo la kupaza sauti za akinamama kueneza ujuzi wao wa kupambana na mabadiliko ya tabianchi ili jamii nzima ya kitanzania iweze kujifunza zaidi na kuzitumia mbinu hizo katika kupambana na mabadiliko ya tabianchi.
Mradi huo unaoratibiwa hapa nchini na Mtandao wa wanahabari wa Mazingira (EMNet) kwa niaba ya Foundation for Women of Africa unatekelezwa katika mikoa sita ya Kigoma, Kilimanjaro, Mwanza, Morogoro, Dar es Salaam na Pwani ukihusisha miradi ya kilimo, usindikaji, ufugaji na utafiti.
Mratibu wa EMNet Secelela Balisidya amesema akinamama hao wanatekeleza miradi ambayo inachangia moja kwa moja aidha kupambana au kupunguza athari za mabadiliko ya tabianchi. Amesema miradi hiyo ni mradi wa kilimo cha miti ya matunda mkoani Kigoma, kilimo cha viazi lishe visiwani Ukerewe mkoani Mwanza, Ufugaji Nyuki mkoani Morogoro na Pwani na ukaushaji wa mbogamboga kwa kutumia nishati ya jua mkoani Morogoro. Miradi mingine ni usindikaji wa vyakula mbalimbali kutokana na muhogo mkoani Pwani, kilimo hai cha mbogamboga na kilimo cha uyoga mkoani Dar es Salaam, mradi wa majiko banifu mkoani Pwani na mradi wa utafiti wa jiko linalotumia nishati ya jua mkoani Kilimanajro.
Mradi huo unaotarajiwa kutelekezwa kwa mwaka mmoja unatoa fursa kwa kinamama kutoa ujuzo wao wa kupambana na mabadiliko ya tabianchi na sauti zao kusikika. Hiyo ni kwa sabuabu kinamama wana uhusiano mkubwa na mazingira kutokana na kazi wanazozifanya kila siku za kilimo na utunzaji wa familia kuhusiana moja kwa moja na mazingira hivyo kuyaelewa zaidi mazingira na jinsi ya kupambana na mabadiliko ya tabianchi.
Wakiwa Madrid nchini Spain walikopata mafunzo wa wiki mbili katika chuo kikuu cha Autonomus Universitad De Madrid, akinamama hao na waandishi wa habari walijifunza kwa nadharia na vitendo jinsi nchi ya Spain inavyokabiliana na mabadiliko ya tabianchi na kuona njia ambazo na huku nchini zinaweza kutumika kupambana na mabadiliko ya tabianchi. Mafunzo kwa vitendo pia yalihusisha ziara za mafunzo kujifunza kilimo hai, na jinsi nishati jua inavyoweza kusaidia kupambana na mabadiliko ya tabianchi.
Waandishi wa habari pia walipata nafasi ya kutembelea chumba cha habari cha gazeti la Serikali ya Sapin la El Pais an kujifunza zaidi jinsi waandishi wa huko wanavyoandika habari zihusianazo na mabadiliko ya tabianchi.  

Tovuti: Green Voices