TAARIFA YA KUPOTEA KWA MTOTO DAMIAN JAMES WA KATORO MKOANI GEITA

December 27, 2016

ASAKARI JESHI NA WANAHABARI WALIVYOSHEREHEKEA MIAKA 55 YA UHURU KATIKA KILELE CHA UHURU ,MLIMA KILIMANJARO.

December 27, 2016
Safari ya kuekea kilele cha Uhuru inaanza majira ya saa 5:00 usiku kwa kuianza safafri kutoka Kibo Hut.
Safari ilikuwa ni usiku kucha 
Jua likachomoka wakati safari ikiendelea.
Kadri kulivyokucha ndivyo washiriki walivyoendelea kupata nguvu ya kuendelea na safari ya kufika Uhuru Peak.
Matumaini yakaana kuonekana baada ya alama ya Gilmans Point kuanza kuonekana.
Mdogo mdogo ndo ilikua kauli ya kuongeza morali kwa wapandaji.
Gilmans Point hatiaye washiriki wakafika lakini hii ni hatua ya kwanza bado hatua mbili ili kufika Uhuru Peak.
Miongoni mwa waliofika Gilmans Point ni Naibuu Kamanda wa kikosi cha nchi kavu cha jeshi la Ulinzi ,Brigedia Jenerali ,Jairo Mwaseba.
Safari ya kueelkea Uhuru Peak ikaendelea.
Hatimaye wapandaji wakapita kituo chha Pili ambachi ni Stella na mongoni mwa waliofika hapa ni aliyekuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) Balozi Charles Sanga.
a Safari ilivyoendelea kuelekea Uhuru Peak ,safu ya vilima vikiwa vyenye barafu ndio vilitawala eneo hilo.
Hatimaye safari ya siku sita ya Wanahabari na askari wa jeshi la Ulinzi ya kupanda Mlim Kilimanjaro kwa ajili ya kumbukumbu ya miaka 55 ya Uhuru wa Tanganyika ikafika tamati.

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini aliykuwepo katika safari hiyo.

TIGO YAWAPIGA "TAFU" KITUO CHA MSAMARIA MWEMA FOUNDATION MKOANI KILIMANJARO

December 27, 2016
Meneja wa Kampuni ya Mawasiliano  TIGO Kanda ya Kaskazini Hendri Kinabo Kulia,akimkabidhi treyi la mayai ya kuangulia vifaranga kama sehemu ya msaada kwa Mwenyekiti wa kituo cha Msamaria Mwema Foundation, Folkward Mapunda (kushoto),Hafla hiyo ilifanyika jana kituoni hapo.msaada huu unathamani ya milioni 7.9



Meneja wa Kampuni ya Mawasiliano Tigo Kanda ya Kaskazini,Hendri Kinabo Kulia akimkabidhi mfuko wa chakula cha kuku mwenyekiti wa Kituo cha Msamaria Mwema Foundation Kilichopo Rau Manispaa ya Moshi ,Folkward Mapunda huku wa wafanyakazi wa Tigo wakishuhudia tukio hilo lilifanyika jana kituo hapo.



Meneja wa Kampuni ya Mawasiliano Tigo Kanda ya Kaskazini, Hendri Kinabo (kulia) akimkabidhi mashine ya kuangulia vifaranga mwenyekiti wa Kituo cha Msamaria Mwema Foundation Kilichopo Rau Manispaa ya Moshi ,Folkward Mapunda huku wa wafanyakazi wa Tigo wakishuhudia tukio hilo lilifanyika jana kituo hapo.

MJENGO WA GHOROFA ALIOUACHA MPOKI BUKUKU TABATA DAR

December 27, 2016
 Nyumba ya ghorofa moja iliyopo Tabata Bwawani, Dar es Salaam, aliyoiacha aliyekuwa MpigaPicha Mwandamizi wa  The Guardian, marehemu Mpoki Bukuku. Waliopo nje ni baadhi ya waombolezaji akiwemo Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe (katikati).PICHA NA RICHARD MWAIKENDA:KAMANDA WA MATUKIO BLOG
Upande wa nyuma wa mjengo huo.