WAZIRI WA NCHI OFISI YA RAISI TAMISEMI, SIMBACHAWENE ATEMBELEA MFUKO WA PENSHENI WA LAPF MJINI DODOMA LEO.

February 04, 2016

WAZIRI wa nchi Ofisi ya Rais Tamisemi, George Simba chawene ametembelea ofisi za Mfuko wa Pension wa LAPF mjini Dodoma Leo. Katika ziara hiyo mh. Waziri amepongeza jitihada za Mfuko kuongeza Wanachana kila mwaka pamoja na huduma bora zinazotolewa kwa wanachama hasa katika kulipa mapema madai ya wananchama.

Akiongea na watumishi wa Mfuko wa LAPF amepongeza jitihada za watumishi kwa utendaji wao mzuri unaopelekea utendaji bora wa Mfuko. Mh. waziri amepongeza uwekezaji unaofanywa na LAPF katika kuhakikisha Mfuko unakuwa endelevu . 

Pia ameahidi kushirikiana na Mfuko ili kuhakikisha unaendelea kufanya 
vizuri zaidi.
Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Tamisemi, George Simba chawene akisalimiana na kiongozi wa LAPF leo alipotembelea ofisi za Mfuko wa Pension wa LAPF mjini Dodoma.
 Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Tamisemi, George Simba chawene akisaini kitabu cha wageni leo alipotembelea ofisi za Mfuko wa Pension wa LAPF mjini Dodoma.
Wafanyakazi wa Mfuko wa Pension wa LAPF  wakimsikiliza Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Tamisemi, George Simba chawene alipotembelea ofisi za Mfuko huo mjini Dodoma.
Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Tamisemi, George Simba chawene akizungumza na wafanyakazi wa  Mfuko wa Pension wa LAPF alipotembelea ofisi za Mfuko huo leo mjini Dodoma. 
Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Tamisemi, George Simba chaweneakizungumza na wafanyakazi wa mfuko huo leo alipotembelea ofisi za Mfuko wa Pension wa LAPF mjini Dodoma.

NDANDA YAIBUKA NA USHINDI MWEMBAMBA WA BAO 1-0 DHIDI YA COASTAL UNION

February 04, 2016


 Wachezaji wa Coastal Union ya Tanga wakiomba Dua kabla ya mchezo wao  dhidi ya Ndanda FC  Mtwara leo na NDANDA SC KUSHINDA BAO 1-0




 Mshambuliaji wa Ndanda FC ya Mtwara, Braison Raphael (kulia) akishangilia goli alilofunga wakati wa mchezo wa ligi kuu Tanzania Bara baina ya Coastal Union uwanja wa Mkwakwani Leo


  Wachezaji wa Ndanda FC kutoka Mtwara wakishangilia goli wakati wa mchezo na Coastal union wakati wa mchezo wa ligi kuu Tanzania Bara uwanja wa Mkwakwani
leo
 Mchezaji wa Ndanda FC, Burhan Rashid akijaribu kumtoka beki wa Coastal Union wakati wa ligi kuu Tanzania Bara leo  walipokutana uwanja wa Mkwakwani.
 Wachezaji wa Ndanda FC, wakijaribu kuwatoka wachezaji wa Coastal Union wakati wa mchezo ligi kuu Tanzania Bara uwanja wa Mkwakwani.

Mchezaji wa Ndanda FC akiugulia maumivu wakati wa mtanange na Coastal Union ya Tanga leo

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli Mgeni Rasmi Siku ya Sheria nchini, Asisitiza Ufanisi wa Mahakama na utoaji wa Haki kwa Wakati

February 04, 2016


 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akipokewa na Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Mohamed Chande Othman leo jijini Dar es salaam wakati wa maadhimisho ya Siku ya Sheria nchini. Rais, Dkt. John Magufuli alikua mgeni rasmi. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli (katikati) akisalimiana na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson wakati wa maadhimisho ya Siku ya Sheria leo jijini Dar es salaam.
 Wimbo wa Taifa ukipigwa wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Sheria. Kulia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli (Kulia) akiwa na Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Mohamed Chande Othman 
Baadhi ya Viongozi waliohudhuria Maadhimisho ya Siku ya Sheria wakiwa wamesimama wakati wimbo wa Taifa ukipigwa. Kutoka kulia ni Jaji Mkuu wa Kenya Dkt. Willy Mutunga, Jaji Kiongozi wa Tanzania Mhe. Shaaban Lila (katikati) na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Said Mecki Sadiki.
Baadhi ya Viongozi wa vyombo vya ulinzi na usalama  nchini na wadau muhimu wa Mahakama waliohudhuria Maadhimisho ya Siku ya Sheria wakitoa heshima zao wakati wimbo wa Taifa ukipigwa.
Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Charles Rwechungura akitoa salam na ujumbe wa Chama hicho wakati wa maadhimisho ya Siku ya Sheria leo jijini Dar es salaam.
Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue (kulia) akifuatilia hotuba zilizokuwa zikitolewa na viongozi mbalimbali wakati wa maadhimisho ya Siku ya Sheria. Kulia kwake ni Mtendaji Mkuu wa Mahakama Bw. Hussein Katanga.
 Jaji Mkuu wa  Mkuu wa Tanzania Mhe. Mohamed Chande Othman akiwahutubia viongozi, mabalozi na wageni mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi waliohudhuria maadhimisho ya Siku ya Sheria.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akisisitiza jambo kuhusu utendaji wa Mahakama na Utoaji wa Haki kwa wananchi kwa wakati kwenye maadhimisho ya Siku ya Sheria. Mhe. Rais alikuwa mgeni rasmi kwenye maadhimisho hayo yaliyohudhuriwa na viongozi na wageni mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Majaji wa Mahakama ya Tanzania leo wakati wa kilele cha Siku ya Sheria nchini.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa dini na baadhi ya wakuu wa vyombo vya ulinzi na Usalama na mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao Tanzania wakati wa kilele cha Siku ya Sheria.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Mawakili.
Jaji Mkuu wa Kenya Dkt. Willy Mutunga (kulia) akimkabidhi zawadi ya kumbukumbu kutoka nchini Kenya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo jijini Dar es salaam. Jaji Mkuu wa Kenya alikua miongoni mwa wageni mashuhuri walioalikwa na Mahakama ya Tanzania kuhudhuria maadhimisho ya Siku ya Sheria.
Wageni mbalimbali waliohudhuria maadhimisho ya Siku ya Sheria wakifurahia Hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.John Pombe Magufuli aliyokua akiitoa leo jijini Dar es salaam.
……………………………………………………………………….
(Na. Jacquiline Mrisho/Aron Msigwa – Dar es salaam)
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amewataka Mahakimu na Majaji wa Mahakama ya Tanzania kufanya kazi kwa kuzingatia weledi wa taaluma ya Sheria katika kushughulikia mashauri  yanayopelekwa Mahakamani.
Aidha amewataka Majaji na Mahakimu kutoa hukumu za mashauri  yanayowasilishwa Mahakamani kwa haraka ili kuwasidia wananchi wanaotafuta haki.
Akizungumza na mamia ya wageni kutoka ndani na nje ya nchi waliohudhuria Maadhimisho ya Siku ya sheria, Dkt. Magufuli amewataka Majaji na Mahakimu hao kutanguliza Uzalendo na maslahi ya taifa mbele pindi wanapotoa maamuzi ya mashauri yaliyoko Mahakamani.
 Mhe. Rais amemtaka Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Mohamed Chande Othman  kuchukua hatua kwa watendaji wa Mahakama wanaokiuka maadili kwa kufanya vitendo vinavyochafua taswira ya Mahakama mbele ya macho ya jamii.
Aidha, Katika hotuba yake Mhe. Rais amesema kuwa Serikali ya awamu ya tano itaendelea kuijengea uwezo wa kifedha Mahakama ili iweze kutekeleza majukumu yake ipasavyo.

MWENYEKITI WA CCM, JAKAYA KIKWETE AWASILI SINGIDA KWENYE MAADHIMISHO YA MIAKA 39 YA KUZALIWA CCM

February 04, 2016
 Mwenyekiti wa CCM, Rais mstaafu Jakaya Kikwete akilakiwa na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana alipowasili mjini Singida jioni leo, kwa ajili ya maadhimisho ya miaka 39 ya kuzaliwa kwa CCM yatakayofanyika kesho kutwa mjini Singida.

 Mwenyekiti wa CCM, Rais mstaafu Jakaya Kikwete salimiana na wananchi alipowasili mjini Singida jioni leo, kwa ajili ya maadhimisho ya miaka 39 ya kuzaliwa kwa CCM yatakayofanyika kesho kutwa mjini Singida.
 Mwenyekiti wa CCM, Rais mstaafu Jakaya Kikwete salimiana na wananchi alipowasili mjini Singida jioni leo, kwa ajili ya maadhimisho ya miaka 39 ya kuzaliwa kwa CCM yatakayofanyika kesho kutwa mjini Singida.

 Akina mama wakicheza ngoma mbele ya Mwenyekiti wa CCM, Jakaya Kikwete (kushoto).

 Kikwete akiwapungia mkono wananchi
 Mwenyekiti wa CCM, Rais mstaafu Jakaya Kikwete akijadiliana jambo na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (kulia) pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Singida, Parseko Kone. Kulia ni Katibu Mwenezi wa CCM, Nape Nnauye.
 Kikwete akiwa na Nape, Kone na Kinana baada ya kuwasili
 Mwenyekiti wa CCM, Rais mstaafu Jakaya Kikwete akijadiliana jambo na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (kulia) pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Singida, Said Amanzi.
 Mke wa Rais, Salma Kikwete akizungumza na Mkuu wa Wilaya ya Singida, Said Amanzi
Katibu Mkuu wa CCM, Komredi Kinana akijadiliana jambo na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye baada ya kumlaki Mwenyekiti wa chama hicho, Jakaya Kikwete mjini Singida.

MADIWANI WA CHADEMA WALALAMIKA KUBURUZWA NA MSTAHILI MEYA WA JIJI LA MWANZA

February 04, 2016
John Pambalu ambae ni diwani wa Kata ya Butimba (Chadema) akiwasilisha mchango wake katika kikao cha baraza la madiwani Jijini Mwanza.
Na:George Binagi-GB Pazzo
Madiwani wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Jijini Mwanza, wamemlalamikia Mstahiki Meya wa Jiji hilo kwa madai ya kuliongoza kibabe baraza la Madiwani.

Wakizungumza baada ya kikao cha baraza la Madiwani kilichoketi hii leo, Madiwani hao wamelalamikia kitendo cha kuzuiliwa kujadili taarifa ya Kamati ya fedha iliyowasilisha katika kikao hicho kwa madai kwamba jukumu la baraza hilo ni kupitisha taarifa hiyo na si kuijadili.

Samwel Range ambae ni diwani wa Kata ya Pamba pamoja na John Pambalu ambae ni diwani wa Kata ya Butimba (Wote Chadema), wamesema wamesikitishwa kuona kanuni za vikao zikivunjwa huku madiwani wakinyimwa fursa ya kujadili taarifa ya kamati ya fedha iliyowasilishwa.

“Tumeshuhudia utawala wa kibabe ukianza katika halmashauri yetu huku mhe.Mwenyekiti wa kikao (Meya) pamoja na Mkurugenzi wake wakiamua kutofuata kanuni na kuamua kufuata matakwa yao binafsi. Tumeletewa taarifa ya kamati ya fedha, wakati wa kujadili tunaambiwa hakuna sababu ya kuijadili isipokuwa kuipitia na kuiidhinisha taarifa hiyo, kitu ambacho madiwani wa Chadema na Upinzani tunakilalamikia”. Alisema Pambalu.

Nae Samwel Range amesema “Kamati ya fedha haina mamlaka ya kuidhinisha chochote ndani ya halmashauri ya Jiji la Mwanza. Inapaswa ilete taarifa yake na kuileta katika baraza la Madiwani ambapo sisi tunauwepo wa kuikubali au kuikataa”.

Hata hivyo malalamiko hayo yamepingwa na James Bwire ambae ndie Mstahiki Meya wa Jiji la Mwanza na diwani wa Kata ya Mahina (CCM), ambapo amefafanua kwamba malalamiko ya madiwani wa Chadema hayana msingi wowote ikizingatiwa kwamba taarifa iliyowasilishwa na kamati ya fedha iliishajadiliwa ndani ya kamati hivyo hakukuwa na umuhimu wa kuijadili tena ndani ya baraza la madiwani bali kuipokea na kuipitisha.

Baraza la Madiwani Jijini Mwanza linaundwa na Madiwani 24 na linaongozwa na Chama cha Mapinduzi CCM kwa upande wa Mstahiki Meya pamoja na Naibu Meya ambapo kuna Madiwani 19 kutoka CCM huku Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema kikiwa na Madiwani Watano.


Kutokana na Uwiano huyo, Madiwani wa Chadema wanalalamika kuburuzwa katika baraza hilo kutokana na uchache wao, madai ambayo hata hivyo yanapingwa na Madiwani kutoka CCM ambao wanasema suala lolote lenye maslahi kwa umma linapewa nafasi sawa ndani ya baraza hilo bila kujadi itikadi za vyama vya siasa. 
Kushoto ni Naibu Meya Jiji la Mwanza, Katikati ni Mstahiki Meya na Kulia ni Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza
Waheshimiwa Madiwani Jijini Mwanza
Waheshimiwa Madiwani Jijini Mwanza
Watendaji wa Idara mbalimbali Jijini Mwanza.

KOMREDI KINANA AANZA KUCHAPA KAZI MAADHIMISHO YA MIAKA 39 YA KUZALIWA CCM SINGIDA

February 04, 2016
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akishiriki kupalilia katika shamba la mtama la mkulima wa kujitegemea Elisha Mdaa (kushoto) katika Kata ya Mtamaa, Singida leo, ikiwa ni shamrashamra ya maadhimisho ya miaka 39 ya kuzaliwa CCM yatakayofanyika kitaifa mkoani  Singida kesho. Kauli mbiu ya maadhimisho hayo ni kuhimiza kila mwananchi kuchapa kazi. (PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG)

 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akishiriki kupaka rangi Jengo la Ofisi ya CCM Mkoa wa Singida leo, ikiwa ni shamrashamra ya maadhimisho ya miaka 39 ya kuzaliwa CCM yatakayofanyika kitaifa mkoani  Singida kesho kutwa
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akishiriki ujenzi wa majengo ya Shule ya Sekondari ya Unyianga, Singida leo, ikiwa ni shamrashamra ya maadhimisho ya miaka 39 ya kuzaliwa CCM yatakayofanyika kitaifa mkoani  Singida kesho kutwa.

 Komredi Kinana akihutubia baada ya kushiriki ujenzi wa majengo ya shule ya Unyianga ambapo alihimiza wananchi kuwa na moyo wa kujitolea katika ujenzi wa miradi mbalimbali ya kijamii pamoja na kujenga tabia ya kuchapa kazi.
 Mkulima wa mfano wa shamba la mtama lililotembelewa na Komredi Kinana, Elisha Mbaa akielezea jinsi anavyotumia jembe la kukokotwa na ng'ombe  katika kilimo hicho, ambapo katika heka moja na nusu huvuna magunia 15 ya mtama na fedha zinazopatikana kwa kuuza mtama huo zinasaidia kusomesha watoto na kupata mahitaji mengine.
 Katibu wa Waendesha Bodaboda Mkoa wa Singida, akisoma risala ya pamoja ya wajasiriamali wakati wa mkutano na Katibu Mkuu wa CCM, Komredi Kinana mjini Singida leo. Komredi Kinana alitumia wasaa huo kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili wajasiriamali.
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimkabidhi  kadi ya uanachama wa Umoja wa Wanawake wa CCM (UWT), Mwajuma wakati wa mkutano na Wajasiriamali uliofanyika katika ukumbi wa Jengo la CCM Mkoa wa Singida leo, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 39 ya kuzaliwa CCM yatakayofanyika kitaifa kesho kutwa mjini Singida.
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimkabidhi  kadi ya uanachama wa Umoja wa Wanawake wa CCM (UWT), Hawa Mtipa wakati wa mkutano na Wajasiriamali uliofanyika katika ukumbi wa Jengo la CCM Mkoa wa Singida leo, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 39 ya kuzaliwa CCM yatakayofanyika kitaifa kesho kutwa mjini Singida.
 Komredi Kinana akizungumza na wajasiriamali mjini Singida leo
Ofisa Biashara wa Manispaa ya Singida, Erick Sinkwembe akitoa maelezo kwa Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana katika mkutano wa Wajasiriamali wa manispaa hiyo,  kuhusu uendeshaji wa mafunzo kwa waendesha Bodaboda pamoja na utekelezaji wa sheria mbalimbali za kodi ambazo mara nyingine si rafiki kwa wajasiriamali. Mkutano huo ulifanyika katika Jengo la Ofisi ya CCM ya Mkoa huo.