PUMA KUTANGAZA UTALII WA TANZANIA DUNIANI KWA KUTUMIA NDEGE 22 ZA ZAMANI

November 23, 2016
 Meneja wa Kampuni ya Puma Energy Tanzania, Philippe Corsaletti akiwaonesha wanahabari  (hawapo pichani) Dar es Salaam leo, moja ya picha ya ndege  22 za zamani zitakazotua nchini Novemba 28, mwaka huu, kwa mashindano ya 'Vintage Air Rally' yenye lengo la kutangaza utalii. Ndege hizo zilitengenezwa kati ya mwaka 1920 na 1930.Kushoto ni  Mkuu wa Idara ya Mafuta ya Ndege wa kampuni hiyo, Raymond Tungaraza. PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG
 Meneja wa Kampuni ya Puma Energy Tanzania, Philippe Corsaletti akiwaonesha wanahabari  (hawapo pichani) Dar es Salaam leo, Nchi za Afrika ikiwemo Tanzania ambamo Mashindano ya Ndege 22 za zamani  'Vintage Air Rally' zilizotengezwa kati ya mwaka 1920 na 1930 zitatua na kutangaza utalii pamoja na kukusanya fedha za misaada kwa jamii.  Kulia ni Meneja Rasirimali Watu wa kampuni hiyo, Loveness Hoyange.
 Meneja wa Kampuni ya Puma Energy Tanzania, Philippe Corsaletti (katikati) akizungumza katika mkutano na wanahabari (hawapo pichani) Dar es Salaam leo, kuhusu  maandalizi wa mashindano ya Ndege 22 za zamani  'Vintage Air Rally' zilizotengezwa kati ya mwaka 1920 na 1930 zitakazotua nchini Novemba 28 na kutangaza utalii pamoja na kukusanya fedha za misaada kwa jamii.  Kulia ni Meneja Rasirimali Watu wa kampuni hiyo, Loveness Hoyange na Mkuu wa Idara ya Mafuta ya Ndege wa kampuni hiyo, Raymond Tungaraza.
 Mkuu wa Idara ya Mafuta ya Ndege wa kampuni hiyo, Raymond Tungaraza.akijibu maswali ya wanahabari
 Mkuu wa Mauzo na Masoko wa Mafuta ya Ndege ya kampuni hiyo, Andrew Lauwo (kulia)  akifafanua jambo katika mkutano huo
Mkutano ulivyokuwa


Puma Energy Tanzania Ltd
Kampuni ya puma kuwa mwenyeji wa mashindano ya ndege za zamani
23rd November 2016
Taarifa Kwa umma
Kampuni ya Puma Energy Tanzania ambayo ni sehemu ya Puma Group, Kampuni ya kimataifa inayojishughulisha usafishaji mafuta ghafi, kutunza na kusambaza mafuta yaliyosafishwa tayari kwa matumizi, inayofuraha kujulisha umma kuwa itakua mfadhili mahsusi  katika  mashindano ya anga yanayohusisha ndege za zamani kwa mwaka 2016.
Vintage Air Rally inahusiaha ndege za zamani za miaka ya 1920 na 1930 ambazo zinarushwa na marubani wenye uzoefu mkubwa kutoka sehemu mbalimbali duniani, wakiruka kukatisha Afrika kuanzia kisiwa cha Crete Ugiriki hadi Cape town Afrika ya kusini.
Shindano hili lilianza tarehe 12/11/2016 kule Crete, Ugiriki na safari yote itachukua siku 35  katika jumla ya nchi 10 ambazo ni Ugiriki, Misri, Sudan, Ethiopia, Kenya, Tanzania, Zambia, Zimbabwe, Botswana na Afrika ya Kusini.
Shindano hili linalengo la kutahini ujuzi wa marubani husika,  na wakati huohuo kuchangisha fedha kwa ajili ya mashirika ya Kimataifa ya hiari UNICEF, Bird life International and Seed Bombing. Sisi kama Puma tunasikia fahari sana kuwa sehemu ya uvumbuzi huu wa ajabu. 
 Kampuni ya Puma Energy inayofuraha kuwa mwenyeji wa mashindano haya.   Ndege zinazotumika katika aina hii ya mashindano huwa zinahitaji aina maalumu ya matengenezo kwa kuzingatia umri wake pamoja na teknolojia iliyotumika. Tumejikita katika kuendela kufanya vyema na pia kuwa na uhakika wa uapatikanaji wa bidhaa ya mafuta na tunafuraha kutoa mchango wetu katika kuhakikisha kwamba mashindano yanayafanyika vyema. Jukumu letu katika kusaidia
kuendeleza utalii ndani ya nchi yetu linabaki kuwa sehemu muhimu sana katika masula yetu ya kijamii kama kampuni katika kutimiza majukumu yetu ya kila siku, Alisema Philippe Corsaletti, Meneja Mkuu wa Puma Enery Tanzania.
 Vintage Air Rally watatua Tanzania (KIA) tarehe 28/11/2016 wakitokea uwanja wa ndege wa Wilson Nairobi. Marubani watakua na muda mzuri wa kutembelea mbuga zetu za wanyama kama sehemu ya safari yao. Hili pekee pia litasaidia katika kuweka utalii wa nchi yetu katika mtizamo wa kimataifa Zaidi kwani shindano hili linafuatiliwa na maelfu ya watu katika maeneo mbalimbali duniani.
 Kampuni ya Puma Energy Tanzania imejiandaa kabisa kupokea ugeni huu ikiwa ni pamoja na kuhakikisha huduma zote za kujaza mafuta ili kuhakikisha urukaji ulio salama. Ndege hizi zinatumia mafuta aina ya Avgas ambayo kwa sasa ni kampuni ya Puma pekee inayotunza hapa nchini. Timu ya watu wetu imejiandaa kupokea na kuhudumia msafara mzima katika kiwanga cha juu cha ubora na ufanisi. Uwepo wa bohari zetu za mafuta ya ndege katika maeneo mbalimbali nchini unafanya iwe rahisi kuhudumia ndege hizo ambao msafara huu utapita.
Kwa hapa Tanzania, Vintage Air Rally Aircrafts zitajaza mafuta Kilimanjaro, Arusha, Dar es salaam, Zanzibar, Dodoma, and Songwe kabla ya kuelekea Zambia ambapo watapokelewa na kuhudumiwa na wenzetu wa Puma Zambia.
Tanzania itaweka historia kwa kuwa moja ya nchi chache duniani ambapo mashindano haya yatapita. “Tunawakaribisha wananchi wote katika tukio hili la kihistoria wakati ndege za Vintage zitakapokua zikipita maeneo yenu na kutumia fursa hii kuendeleza utalii”, Alisema Ndugu Philippe.

Kuhusu njia itakayotumika:
Njia inayotumika ni sawa kabisa na ufuatishaji wa safari ya shirika la ndge la Imperial ya mwaka 1931 “safari ya Afrika” ambapo ndege itakua ikiruka chini kupitia Nile kutokea kongo hadi Khartoum, kupitia nyanda za juu za Ethiopia, uwanda wa chini wa Kenya,  na hatimaye sehemu yenye changamko sana ya Afrika Mashariki.  Baada ya hapo itaondoka tena kupitia Kilimanjaro hadi Serengeti, na hatimaye hadi kwenye visiwa vya marashi ya Zanzibar na hadi chini Zaidi, kupitia Zambia, juu ya maporomoko ya Victoria, hadi Bulawayo Zimbabwe. Siku za mwisho za safari hii ndefu inayohitaji pumzi nyingi itawafikisha Botswana na Afrika ya Kusini - Capetown ambapo utakua mwisho wa safari

Kampuni ya Puma Energy ni kampuni ya kimataifa ya viwango vya kati ambayo imejikita katika kusafisha mafuta ghafi, kutunza na kusambaza mafuta masafi kwa watumiaji katika zaidi ya nchi 45 duniani. Puma Energy iliingia Tanzania mwaka 2012 na hadi sasa inaongoza katika  soko na pia kampuni pekee yenye uwepo katika viwanja vinane hapa Tanzania  ambavyo ni Kilimanjaro, Zanzibar, Songwe, Mwanza, Tabora, Dodoma, Arusha, na Julius Nyerere.

Philippe Corsaletti
Meneja Mkuu

UZINDUZI WA SIKU 16 ZA KUPINGA UKATILI WA KIJINSIA KWA KANDA YA KASKAZINI KUFANYIKA KESHO IJUMAA KILIMANJARO

November 23, 2016
Wajumbe wa Kamati ya maandalizi ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia Kanda ya Kaskazini walipokutana na wanahabri mkoa Kilimanjaro kuzungumzia tukio la uzinduzi litakalo fanyika kesho Ijumaa katika viwanja vya kituo kikuu cha Mabasi mjini Moshi.
Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia Kanda ya Kaskazini ,Elizabeth Mushi akizungmza walipkkutana na wanahabari mkoani Kilimanjaro.
Wajumbe wa Kamati ya maandalizi ya siku 16 za kupinga ukatili kutoka Mtandao wa Jinsia wa jeshi la Polisi (TPF Network) , Grace Lyimo (Kushoto) na Theresia Nyangasa.(Kulia).
Meneja Programu wa Shirika lisililo la Kiserikali linalojishughulisha na kupinga ukeketaji (NAFGEM) Honorata Nasuwa akizungumza mbele ya wanahabri juu ya uzinduzi rasmi wa siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia .
Afisa Programu wa Shirika linalotoa msaada wa Kisheria Kilimanjaro-KIWECO,Hilaly Tesha akizungumza wakati wa mkutano wa na wanahabari kuzungumzia tukio hilo .
Baadhi ya wanahabari wa vyombo mbalimbali mkoa wa Kilimanjaro wakifuatilia maelezo yaliyokuwa yakitolewa.
Mwenyekiti wa Dawati la Jinsia la Jeshi la Polisi ,Elina Maro akizungumza katika mkutano huo na wanahabari.
Baadhi ya Wanahabari wakiwa katika mkutano huo.
Mkutano na Wanhabari mkoa wa Kilimanjaro ukiendelea.
Baadhi ya Wanahabri mkoa wa Kilimajaro wakiwa katika mkutano huo.

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.

ESRF YASHIRIKIANA NA GETENERGY KUANDAA MKUTANO WA AFRIKA WA MAFUTA NA GESI

November 23, 2016

Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Jamii (ESRF) imeshirikiana na kampuni ya Getenrgy kuandaa mkutano wa Afrika wa Mafuta na Gesi (GETENERGY VTEC AFRICA 2016) ambao unafanyika nchini kwa siku tatu kuanzia Novemba, 21-23, 2016.

Katika hotuba yake ya utangulizi, Mkurugenzi Mtendaji wa ESRF, Dk. Tausi Kida alisema kuwa mkutano huo umekutanisha wadau mbalimbali wa sekta ya mafuta na gesi kutoka nchi mbalimbali Afrika ikiwepo serikali, viwanda, mashirika ya maendeleo na vyuo ambavyo vinatoa elimu ya mafuta na gesi.

Mkurugenzi Mtendaji wa ESRF, Dk. Tausi Kida akitoa neno la utangulizi katika Mkutano wa Afrika wa Mafuta na Gesi.

"Malengo ya mkutano huu ni kuangalia changamoto gani ambazo zinalikabili Bara la Afrika katika sekta ya mafuta na gesi, kubadilisha ujuzi kwa wataalamu wa mataifa ambayo yameshiriki na kujadili hatua ya kuchukua ili kuboresha sekta hii lakini pia utasaidia kukuza ushirikiano baina ya nchi washiriki,

"Katika mkutano washiriki wataisaidia Serikali na wadau kuweka mikakati ya kutekeleza na yenye ufanisi kuhusu sekta ya mafuta na gesi na kama Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Kijamiii tutaendelea kushirikiana na wadau kutafuta changamoto zinazokabili sekta na mbinu za kutumia ili kuyatatua," alisema Dkt. Kida.

Mgeni rasmi katika mkutano huo, Makamu wa Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu akizungumza umuhimu wa mkutano huo na jinsi ambavyo unaweza kuwanufaisha Watanzania.

Kwa upande wa mgeni rasmi katika mkutano huo, Makamu wa Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu alisema, Serikali kwa sasa inataka kuhakikisha kunakuwapo na wataalamu wengi ili kunapokuwepo na sehemu ambazo kunapatikana mafuta au gesi waweze kushiriki wenyewe ili kipato kinachopatikana kiwanufaishe wananchi na Taifa kwa ujumla.

"Nchi ina akiba nyingi ya gesi na tunategemea kupata mafuta baadae lakini tunangaalia upande wa wataalamu, tunahitaji kuwa na wataalamu katika sekta ya mafuta na gesi ili tutakapoanza shughuli ya uchimbaji tayari tuwe na wataalamu wanaohitajika hapa nchini,

"Huu ndiyo mchango wa ndani, hatuwezi kufanya sisi pekee lazima tuwe na wageni lakini pia tuwe na Watanzania wanaotumikia sekta hii na wanaofaidika na uchimbaji wa hayo mafuta," alisema Mama Samia.

Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo akieleza jinsi ambavyo Serikali imejipanga kuinua sekta na mafuta na gesi ili Watanzania wengi wanufaike na uwepo wa mafuta na gesi nchini.

Nae Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo alisema Serikali imejipanga kuboresha sekta ya mafuta na gesi kwa kutoa elimu kuhusu sekta hiyo katika baadhi ya vyuo mbalimbali nchini ili wahitimu wanapomaliza waweze kuingia moja kwa moja katika sekta hii.

"Tupo katika orodha ya nchi 20 Afrika ambazo zinafanya vizuri, baada ya miaka mitano tutakuwa tumepiga hatua na mtaona ni jinsi gani tumefanikiwa, kwasasa tuna wanafunzi wamehitimu UDOM na tunashirikiana na China na Uingereza kwahiyo niwahakikishie kuwa tumejipanga," alisema Prof. Muhongo.

Mkurugenzi wa kampuni ya Getenergy, Virginia Baker akitoa taarifa kuhusu kampuni hiyo, malengo na umuhimu wa kufanyika kwa mikutano hiyo.

Mikutano ya GETENERGY VTEC kwa mwaka 2016 tayari imeshafanyika katika nchi ya Mexico na Uingereza na imekuwa ikikutanisha wadau mbalimbali wa sekta ya mafuta na gesi ili kujadili jinsi sekta hiyo inaweza kuboreshwa na kuwa bora zaidi kuliko ilivyo sasa.

Wadau mbalimbali wa sekta ya mafuta na gesi kutoka mataifa mbalimbali wakifuatilia mkutano wa mafuta na gesi ambao mgeni rasmi alikuwa ni Makamu wa Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu.



Makamu wa Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu akipewa maelekezo kutoka kwa msimamizi wa banda la Chuo cha AGR TRACS kuhusu masomo yanayotolewa na chuo hicho. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa ESRF, Dk. Tausi Kida.

MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA AFUNGUA MKUTANO WA MAHAKAMA YA AFRIKA MJINI ARUSHA

November 23, 2016
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiongozana na Mkuu wa mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo wakati wa kuelekea kwenye ufunguzi wa Mkutano wa Tano wa kila Mwaka wa Ngazi ya juu wa Makama ya Afrika unaojadili kuhusu masuala ya Haki za binadamu, demokrasia na Utawala katika bara la Afrika
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akifuatilia kwa makini hotuba mbali mbali kabla hajahutubia hotuba yake ya  ufunguzi wa Mkutano wa Tano wa kila Mwaka wa Ngazi ya juu wa Makama ya Afrika unaojadili kuhusu masuala ya Haki za binadamu, demokrasia na Utawala katika bara la Afrika
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Tano wa kila Mwaka wa Ngazi ya juu wa Makama ya Afrika unaoendelea kujadili kuhusu masuala ya Haki za binadamu, demokrasia na Utawala katika bara la Afrika uliofanyika kwenye Hoteli ya Mount Meru, mjini Arusha.
 Rais wa Mahakama ya Afrika Mhe. Jaji Justice Sylvain Ore akihutubia wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Tano wa kila Mwaka wa Ngazi ya juu wa Makama ya Afrika unaoendelea kujadili kuhusu masuala ya Haki za binadamu, demokrasia na Utawala katika bara la Afrika uliofanyika kwenye Hoteli ya Mount Meru mjini Arusha.
 Wajumbe wakifuatilia kwa makini Mkutano wa Tano wa kila Mwaka wa Ngazi ya juu wa Makama ya Afrika unaoendelea kujadili kuhusu masuala ya Haki za binadamu, demokrasia na Utawala katika bara la Afrika uliofanyika kwenye Hoteli ya Mount Meru mjini Arusha.
Wajumbe wakipewa jarida la Mahakama ya Afrika mara baada ya kuzinduliwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan mara  baada kuhutubia Mkutano wa Tano wa kila Mwaka wa Ngazi ya juu wa Makama ya Afrika unaoendelea kujadili kuhusu masuala ya Haki za binadamu, demokrasia na Utawala katika bara la Afrika uliofanyika kwenye Hoteli ya Mount Meru mjini Arusha.
                                   ……………………………………………………………..
 

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amesema Serikali ya Tanzania imepiga hatua kubwa katika kulinda na kutetea haki za binadamu kwa kuzingatia maazimio mbalimbali ya ndani ya nchi na ya kimataifa ikiwemo haki ya kuishi.
Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan ametoa kauli hiyo jijini Arusha kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli wakati anafungua mkutano wa mazungumzo wa masuala ya demokrasia na haki za binadamu ya Mahakama ya Afrika ya Watu na Haki za binadamu.
 
 Amesema Tanzania ni mfano wa kuigwa barani Afrika kwa kuzingatia na kutekeleza ipasavyo mikataba mbalimbali ya kimataifa inayolenga kuhakikisha wananchi wake wanapata huduma bora na za msingi ikiwemo huduma ya afya na elimu bila kubaguliwa kutokana na ulemavu,jinsia,rangi au dini.
Amesisitiza kuwa Serikali itaendelea kutekeleza na kuzingatia matamko mbalimbali ya Dunia yanayolenga kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora za kijamii ikiwemo haki ya kuishi.
Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan ameonyesha kufurahishwa na hatua zinazochukuliwa na baadhi ya nchi za Afrika katika kulinda na kutetea haki za binadamu hasa haki za wanawake na kusema kuwa bado kuna umuhimu mkubwa kwa nchi ambazo zinazosuasua kutekeleza mikataba hiyo kufanya hivyo ili kuhakikisha wanawake na watoto wanapata haki sawa katika jamii.
Katika hatua nyingine, Makamu wa Rais amesema kuwa Serikali ya Tanzania imepiga hatua kubwa katika kuingiza wanawake katika ngazi za maamuzi na kwa sasa mpango kabambe unafanyiwa kazi ili kuhakikisha sekta binafsi ambayo bado inaidadi ndogo ya wanawake kwenye ngazi za maamuzi kufanya hivyo na kwamba tafiti mbalimbali zilizofanyika nchini zinaonyesha kuwa wanawake wengi walioingizwa kwenye bodi mbalimbali bodi hizo kwa sasa zimeongeza ufanisi wa kazi maradufu.
Kwa upande wake, Rais wa Mahakama ya Afrika ya Watu na Haki za Binadamu Justice Sylvain Ore amesema kuwa mkutano huo ni muhimu kwani unalenga kujadili na kuweka mikakati inayolenga kuhakikisha nchi za Afrika zinazingatia na kulinda haki za bindamu hasa haki za wanawake kwa kiwango kikubwa.
Mkutano huo wa Mahakama ya Afrika ya Watu na Haki za Binadamu ambao unafanyika Jijini  Arusha umehudhuriwa na wajumbe kutoka mataifa mbalimbali ya Afrika wakiwemo wajumbe kutoka Umoja wa Afrika AU na lengo la mkutano huo  ni kutajadili masuala ya demokrasia na haki za binadamu katika nchi za Afrika.
RAIS DKT. MAGUFULI AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA RAIS MSTAAFU WA AWAMU YA PILI MZEE ALI HASSAN MWINYI IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

RAIS DKT. MAGUFULI AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA RAIS MSTAAFU WA AWAMU YA PILI MZEE ALI HASSAN MWINYI IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

November 23, 2016
miny1
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Rais mstaafu wa awamu ya pili Mzee Ali Hassan Mwinyi Ikulu jijini Dar es Salaam.
miny2
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Rais mstaafu wa awamu ya pili Mzee Ali Hassan Mwinyi Ikulu jijini Dar es Salaam.
miny3
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo na Rais mstaafu wa awamu ya pili Mzee Ali Hassan Mwinyi mara baada ya kumaliza mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam.
miny4
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na  Waziri wa Ardhi  Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi kabla ya kuanza mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU

HOW UZIKWASA CONTRIBUTES TO THE 16 DAYS OF ACTIVISM AGAINST GENDER VIOLENCE IN PANGANI

November 23, 2016
November 25th is the International Day for the elimination of Violence against women in the world. The 16 days up to December 10th the Human Rights Day is a period of global activism dedicated to fight gender violence in all settings.
UZIKWASA, an organization based in Pangani, Tanzania has become known for its innovative interventions that encourage a voice among rural communities and the development of capable grass roots leaders who are committed to fight gender rights violations in Pangani.
UZIKWASA’s multimedia work that has addressed violence against women and girls (VAWG) includes:
-Pangani FM radio programs
*Leadership that Touches (UongoziwaMguso)
*Womens’ Voice (Sauti ya Mwanamke)
-Feature films
*Fimboya Baba (Father’s Stick: Early and forced marriage)
*Chukua Pipi (Sweet deceit, sexual abuse of school children)
*AISHA (Gang rape)
-Comic books
* Varangati
*Halafu series
*AISHA book
-Forum Theatre and Theatre for Development
-A series of TV spots
On December 2 UZIKWASA will participate in the 16 days of activism by launching theMinna Dada Day, abig bang event to create awareness on VAWGin Pangani District.The campaign is designed to start a deep reflection process among the Pangani people and their leaders about atrocities committed against women and girls including Intimate Partner violence.
Minna dada introductory TV Spot

The following four “Minna Dada” TV spots paint a picture of how intimate partner violence affects the lives of local Pangani women. Cinema Zetu of AZAM TV will broadcast the four spots during the next four months.
1.Economic exploitation of women by their male partners

2. Rape in marriage

3.Male partners hindering women to access leadership position

4.Emotional violence through public humiliation

NAIBU WAZIRI MPINA AFANYA ZIARA KAHAMA

November 23, 2016


Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina katika Ziara ya kukagua DAMPO la Majitaka Mjini Kahama akionyesha namna ambavyo maji taka yanayomwagwa kiholela yalivyoenea kwa wingi katika eneo  la karibu na barabara.



 Kushoto ni NaibuWaziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina akiwa na wataalam katikati ni Bw. Jamali Baruti kutoka Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira ( NEMC) kanda ya ziwa na Kulia ni Mwanasheria wa Ofisi ya Makamu wa Rais Bw. Abraham Mdee wakijadili jambo katika siku ya Pili ya Ziara Na Naibu Waziri Mjini Kahama.
Mabwawa ya Maji Taka ya Mgodi wa Dhahabu wa Bulyanhulu Mjini Kahama uliojengwa kitaalam na ado umekuwa ukilalamikiwa na wananchi wa vijiji jirani kuwa katika msimu wa mvua mabwawa hayo yanajaa maji yenye sumu na kumwagika katika mashamba ya wakazi hayo hivyo kuhatarisha maisha ya wakazi hao , mazingira na viumbe hai wengine.

SERIKALI KUJENGA VITUO VYA AFYA KILA MWAKA NCHINI NZIMA

November 23, 2016
Naibu Waziri wa ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za mikoa na serikali za mitaa TAMISEMI Suleiman Jaffo akikagua kitabu cha Risiti kulia anayemwangalia ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Pangani Sabas Chambasi

Katikati ni Naibu Waziri wa ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za mikoa na serikali za mitaa TAMISEMI Suleiman Jaffo akitembelea shule ya Sekondari Pangani wakati wa ziara yake kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Pangani,Zainabu Issa na Mbunge wa Jimbo la Pangani (CCM)Jumaa Aweso mwenye suti nyuma 
Mkuu wa wilaya ya Pangani, Zainabu Issa kushoto akiteta jambo na Naibu Waziri  wa ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za mikoa na serikali za mitaa TAMISEMI Suleiman Jaffo aliyeketi katikati wakati wa ziara yake hiyo.
Naibu Waziri wa Tamisemi akiwa na wanafunzi wa shule ya Sekondari Pangani wakati wa ziara yake leo.
Serikali ipo kwenye mpango wa  kuanza utekelezaji wa ujenzi wa vituo vya afya katika kila kata nchi mzima ili kumaliza changamoto ya upungufu huo uliopo kwa sasa katika maeneo mengi.

Rai hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za mikoa na serikali za mitaa TAMISEMI Suleiman Jaffo hapo Jana wakati wa ziara yake wilayani Pangani.

Alisema kuwa mpango huo unatarajiwa kuanza utekelezaji wake kuanzia mwaka ujao wa fedha kwa kila Halimashauri kujengewa kituo kimoja cha afya katika ngazi yakata .
  Alisema kuwa kupitia mpango huo serikali itaweza kwa kiasi fulani kufikia lengo la lake iliyojiwekea la kila kata kuwa na kituo cha afya ili kusogeza huduma karibu na wananchi.

 Aidha Naibu Waziri huyo alisema kuwa licha ya utekelezaji wa Sera ya afya kutiliwa mkazo katika maeneo mengi hapa nchini bado  mpaka sasa Tanzania mzima inavituo vya afya 440 pekee.

 Kwa Upande wake Mkuu wa Wilaya yaPangani Zainab Abdallah alisema kuwa wilaya hiyo inakata 14 lakini ina kituo cha afya kimoja hali inayosababisha changamoto ya utoaji wa huduma.

 "Wilaya yetu maeneo kata nyingine zimetenganishwa na mto Pangani hivyo kutoka na hali hiyo tumelazimika kujenga kituo cha afya katika kata za ngambo ili tuweze kuwahudumia wananchi wote" alisema Dc huyo.