Milango ya uwekezaji ipo wazi – Muhongo

Milango ya uwekezaji ipo wazi – Muhongo

March 21, 2016


sa1
Balozi wa Afrika Kusini nchini Tanzania, Thami Mseleku,( kushoto) akisaini kitabu cha wageni ofisini kwa Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo( kulia) alipomtembelea ofisini kwake kwa  nia ya kufahamu fusra zaidi ya uwekezaji.
sa2
Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo( kushoto) akiwa na Balozi wa Afrika Kusini nchini Tanzania, Thami Mseleku,( kulia)
sa3
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo( kushoto) akiwa pamoja na Balozi wa Afrika Kusini nchini Tanzania, Thami Mseleku( kulia ) pamoja na watendaji wa Taasisi zilizochini ya Wizara ya Nishati wakati wa kikao na ujumbe kutoka nchini Afrika Kusini waliotaka kufahamu zaidi fursa za uwekezaji nchini Tanzania.
sa4
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo( kulia) akiwa pamoja na Balozi wa Afrika Kusini nchini Tanzania, Thami Mseleku( kushoto ) wakijadiliana jambo na wakati wa kikao na watendaji wa Taasisi zilizochini ya Wizara ya Nishati na ujumbe kutoka nchini Afrika Kusini waliotaka kufahamu zaidi fursa za uwekezaji nchini Tanzania.
sa5
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo( kulia) akiwa na Balozi wa Afrika Kusini nchini Tanzania, Thami Mseleku( katikati) pamoja na Patiwe Makoena Afisa anayeshughulikia masuala ya siasa katika ubalozi wa Afrika Kusini.( kushoto) wakati wa Kikao na Waziri wa Nishati nishati na madini, pamoja na watendaji wa taasisi zilizochini ya wizara hiyo hawapo pichani.
……………………………………………………………………………………………
Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo amesema kuwa milango ya uwekezaji iko wazi kwa Mataifa yote duniani yenye nia thabiti ya kufanya hivyo nchini Tanzania.
Profesa Muhongo alisema hayo jijini Dar Es Salaam wakati wa kikao chake na Balozi wa Afrika Kusini hapa nchini,Thami Mseleku, ambaye alifika Ofisi za Wizara ya Nishati na Madini kufahamu zaidi fursa za uwekezaji kwa ajili ya manufaa ya Kampuni za uwekezaji za Afrika Kusini .
Katika kikao hicho, Profesa Muhongo alimueleza Balozi Mseleku kuwa Tanzania ina fusra nyingi za uwekezaji katika masuala ya Nishati na kutaja maeneo hayo kuwa ni pamoja na makaa ya mawe, Nishati jadidifu,Upepo,mawimbi ya bahari pamoja na umeme wa jua.
Aidha Profesa Muhongo alimueleza Balozi Mseleku kuwa Kampuni za uwekezaji kutoka Afrika Kusini zimekuwa zikifanya vizuri katika Sekta ya Madini hasa katika kulipa mirabaha na tozo mbalimbali za zilizowekwa kwa mujibu wa Sheria ya Madini.
Vilevile Waziri wa Nishati na Madini alimsisitiza Balozi huyo wa Afrika Kusini kusini kuwekeza katika sekta ya gesi ambayo tayari inapatikana hapa nchini ili kuzalisha umeme kwa kuwa Tanzania inahitaji umeme mwingi, wa uhakika na wa kutosha.
Profesa Muhongo alieleza kuwa Tanzania inatarajia kufikia katika uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025 utakaotokana na uwepo wa nishati ya umeme ya kutosha nchini, pia tayari imesaini Mpango wa Umoja wa Mataifa unaoelekeza kila mtu kupata huduma ya umeme ifikapo mwaka 2030 unaofahamika kama ” SE4ALL” Nishati Endelevu kwa wote.
Kwa upande wake Balozi Afrika Kusini hapa nchini, Thami Mseleku,alisema kuwa inchi yake ipo tayari kuwekeza katika sekta mbalimbali ikiwemo nishati ya gesi, mafuta na makaa ya mawe na kwamba nchi hiyo inauzoefu zaidi katika uwekezaji wa nishati ya makaa ya mawe. Balozi huyo wa Afrika Kusini katika Mkutano huo aliambatana na Afisa anayeshughulikia masuala ya siasa, Patiwe Makoena
MHE. UMMY A. MWALIMU ATOA TAMKO KUHUSU KUNAJISIWA KWA WATOTO KATIKA MANISPAA YA MOSHI, MKOANI KILIMANJARO

MHE. UMMY A. MWALIMU ATOA TAMKO KUHUSU KUNAJISIWA KWA WATOTO KATIKA MANISPAA YA MOSHI, MKOANI KILIMANJARO

March 21, 2016

Ummy Mwalimu 
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imepokea kwa masikitiko makubwa tukio la kunajisiwa kwa watoto watatu wa kike wenye umri kati ya miaka minane hadi tisa, wanafunzi wa darasa la tatu wa Shule ya Msingi Msaranga manispaa ya Moshi, mkoani Kilimanjaro, ambao limeripotiwa na vyombo vya habari.
Tukio hili la kunajisi watoto ni ukiukwaji mkubwa wa haki za mtoto ambao Serikali imekuwa ikihimiza wazazi, walezi, na jamii kuhakikisha kuwa mtoto analelezwa na kuendelezwa katika mazingira salama na rafiki kwa mujibu wa Sheria ya Mtoto Na. 21 ya mwaka 2009.
Wizara imesikitishwa na taarifa kuwa, kuna baadhi ya wanajamii wanaowafanyia ukatili watoto wa kike kwa kuwashurutisha kuwa na mahusiano na watoto hao katika umri mdogo, kitendo ambacho kwa kiasi kikubwa kinarudisha nyuma jitihada za Serikali kuhakikisha kuwa jamii zetu zinakuwa mahala salama kwa watoto kuishi. 
Wizara inalaani vikali unyanyasaji waliofanyiwa watoto hao kwani katika umri huo mdogo hawakustahili kufanyiwa ukatili huo. Aidha, wazazi na walezi tutambue kuwa tunaowajibu mkubwa wa kufuatilia mienendo ya watoto wetu mara kwa mara ili kuwanusuru na matukio ya ukatili. 
Wizara inatoa pongezi ya dhati kwa wananchi, Jeshi la Polisi, wanahabari na wadau wote ambao wameonesha ushirikiano kuripoti na matukio ya ukatili dhidi ya watoto hapa nchini.  Aidha, Wizara inapongeza Jeshi la Polisi katika Mkoa wa Kilimanjaro kwa kufanikiwa kumkamata mtuhumiwa mmoja anayehusishwa tukio la kunajisi watoto hao. Tunahimiza Polisi katika mkoa wa Kilimanjaro kumsaka mtuhumiwa wa pili na kumjumuisha katika shauri hili.
Maagizo yanatolewa kwa Mganga Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro kuhakikisha anatoa huduma stahiki ya vipimo na tiba kuokoa afya za watoto hao. Aidha, Afisa Ustawi wa Jamii na Afisa Maendeleo ya Jamii wa Mkoa wa Kilimanjaro wahakikishe wanafuatilia shauri la watoto hawa kwa karibu, ikiwa ni pamoja na maendeleo ya afya za watoto hao; na kutoa ushauri nasaha kwa watoto, wazazi na walezi wa familia za watoto hao na kutoa taarifa mara kwa mara.
STARS YAJIFUA D’JAMENA

STARS YAJIFUA D’JAMENA

March 21, 2016
Timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ inayodhaminiwa na bia ya Kilimanjaro Premium Lager leo imefanya mazoezi katika uwanja wa Omnisports Idriss Mahamat Ouya ulipo katika jiji la D’jamena ikiwa ni maandalizi ya mchezo dhidi ya wenyeji Chad siku ya Jumatano.
Taifa Stars imefanya mazoezi kuanzia majira ya saa 9 alasiri, ikiwa ni sawa na muda utakaochezwa mchezo siku ya Jumatano sawa na saa 11 kwa saa za nyumbani Tanzania na Afrika Mashariki.
Akiongelea maandalizi ya mchezo huo, Kocha Mkuu wa Taif Stars Charles Boniface Mkwasa amesema anashukuru vijana wake waliotangulia wamefika salama, hakuna majeruhi na wote wameweza kufanya mazoezi aliyoyapangilia.
“Hapa D’jamena hali ya hewa ni joto kali tofauti na nyumbani, kwa hizi siku mbili tutakazofanya mazoezi hapa, naimani vijana wataweza kuzoea hali ya hewa na kufanya vizuri katika mchezo wa Jumatano” alisema Mkwasa.
Mkwasa amesema wachezaji wake wametoka katika vilabu vyao ambavyo vilikua na michezo mwishoni mwa wiki, wote bado wako fit kikubwa wanafanya maandalizi ya mwisho kwa ajili ya mchezo huo.
“Hatujapata muda mrefu wa kufanya mazoezi kwa pamoja, wachezaji walikua na majukumu katika vilabu vyao, nashukuru wote wamewasili wakiwa salama na kesho wataungana na wachezaji wenzao wanaokuja katika kundi la pili kwa ajili ya mazoezi ya mwisho na mchezo wenyewe” aliongeza Mkwasa.
RAIS DKT. JOHN POMBE MAGUFULI ATEKELEZA AGIZO LA MKUU WA MKOA WA DAR ES SALAAM PAUL MAKONDA LA KUHAKIKI SILAHA

RAIS DKT. JOHN POMBE MAGUFULI ATEKELEZA AGIZO LA MKUU WA MKOA WA DAR ES SALAAM PAUL MAKONDA LA KUHAKIKI SILAHA

March 21, 2016

1
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia kwa makini zoezi la uhakiki wa silaha zake lililokuwa likifanywa na Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Neema Laizer Ikulu jijini Dar es salaam. Mhe. Rais amekuwa mtu wa kwanza kutekeleza agizo la Mkuu wa Mko wa Dar es Salaam Paul Makonda.
2 
Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Neema Laizer (kulia) akiendelea na zoezi la kuhakiki Silaha za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es Salaam
3 4 5 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiitoa silaha yake aina Bastola kwa ajili ya uhakiki Ikulu jijini Dar es Salaam.
6
Kamanda wa Kanda Maalum ya Mkoa wa  Dar es Salaam Kamishna CP Simon Sirro  kulia akimkabidhi Silaha aina ya Bastola Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli mara baada ya uhakiki uliofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.
7 
Kamanda wa Kanda Maalum ya Mkoa wa  Dar es Salaam Kamishna CP Simon Sirro  kulia akimkabidhi silaha aina ya shortgun Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli mara baada ya uhakiki uliofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam
8 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiiweka silaha yake vizuri mara baada ya kuhakikiwa Ikulu jijini Dar es Salaam
9 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiweka vizuri silaha yake aina ya Shortgun mara baada ya uhakiki uliofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.
10 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza mara baada ya kumaliza zoezi la kuhakiki silaha zake Ikulu jijini Dar es Salaam. Mheshimiwa Rais amewataka wananchi wote wanaomiliki silaha kujitokeza kuhakiki silaha zao kama alivyoagiza  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda.
11 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiweka vizuri silaha yake mezani kwa ajili ya uhakiki.
12 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiweka dole gumba katika moja ya fomu za uhakiki Ikulu jijini Dar es Salaam. Picha na IKULU
DK ALI MOHAMED SHEIN ASHINDA UCHAGUZI ZANZIBAR

DK ALI MOHAMED SHEIN ASHINDA UCHAGUZI ZANZIBAR

March 21, 2016

EN1
Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar  ZEC  Jecha Salim Jecha amemtangaza Dk Ali Mohamed Shein kuwa
mshindi wa kiti cha urais visiwani humo baada ya kupata kura 299.982 sawa na asilimia 91.4 ya kura zote zilizopigwa  ambapo chama cha wananchi CUF kilitangaza kususia huku vyama vingine vikishiriki .
Uchaguzi wa Zanzibar ulifutwa  Oktoba 25 mwaka jana baada ya dosari mbalimbali kujitokeza ikiwemo aliyekuwa mgombea wa urais kupitia chama hicho Maalim Seif Sharif Hamad kujitangazia ushindi jambo lililopelekea  Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi ya Zanzibar ZEC Jecha Salim Jecha kutangaza kuufuta uchaguzi huo
TUME YAKUTANA NA WADAU KUPITIA MAPENDEKEZO YA SHERIA YA UNUNUZI WA UMMA

TUME YAKUTANA NA WADAU KUPITIA MAPENDEKEZO YA SHERIA YA UNUNUZI WA UMMA

March 21, 2016

she1
Mwenyekiti wa Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania Mhe. Jaji Aloysius Mujulizi akifungua warsha ya siku moja baina ya Tume na Wadau kujadili mapendekezo ya Sheria ya Ununuzi wa Umma Sura ya 410 ya Mwaka 2011, iiliyofanyika katika ukumbi wa Tume Dra es Salaam.
she2
Baadhi ya wadau wakifuatilia vipengele vya sheria wakati wa kupitia mapendekezo ya Sheria ya Ununuzi wa Umma.
she3
Tesha amabaye ni mjumbe kutoka Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB) akiongoza kikao cha kupitia mapendekezo ya Sheria ya Ununuzi wa Umma Sura ya 410.
she4
Sekretarieti ya Tume ikiwa makini kufuatilia hoja zilizokuwa zikiwasilishwa wakati wa kupitia mapendekezo ya maboresho ya Sheria ya Ununuzi wa Umma (Picha zote na Munir Shemweta, Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania)

Tigo yazindua jukwaa la kujifunza la mtandao wa SMS kwa shule za sekondari

March 21, 2016


Mkurugenzi Mtendaji wa  Shule Direct, Faraja K. Nyalandu (wa kwanza kulia) Meneja wa Huduma za jamii wa Tigo  , Woinde Shishael(wa pili kulia), Mkuu wa Mfuko wa Human Development Innovation Fund (HDIF), David B. McGinty, (wa kwanza kushoto), Mwanafunzi aliyefanya vizuri katika  mtihani wa kidato cha nnemwaka 2015/16 kutokea shule ya wavulana Fezza ya jijini Dar es Salaam, Innocent Lawrence (wa pili kushoto) na Mkurungezi wa Tume ya sayansi na teknolojia Flora Ismail Tibazarwa (wa tatukushoto)wakitazama namna mfumo wa huduma mpya ya wanafunzi kujifunza kupitia ujumbe mfupi wa maandishi, MAKINI SMS unavyoweza kufanya kazi kupitia simu ya mkononi


Wanafunzi i wa shule ya sekondari Azania na wageni waalikwa wakishuhudia uzinduzi wa  wa jukwaa  la kielimu  la SMS Makini ambalo litakuwa linatoa masuala mbalimbali ya kijifunza  kupitia mtandao  kwa walimu na wanafunzi wa shule za sekondari nchini mapema mwishoni mwa wiki iliyopita ,Hafla ya uzinduzi ilifanyika katika shule ya sekondari Azania Jijini Dar es salaam. 

Meneja wa Huduma za jamii wa Tigo  , Woinde Shishael (Wa kwanza kulia ) akizungumza na waandishi wa habari ,Pembeni yake ni Mkurugenzi Mtendaji wa  Shule Direct, Faraja K. Nyalandu mara baada ya uzinduzi  wa jukwaa  la kielimu  la SMS Makini ambalo litakuwa linatoa masuala mbalimbali ya kujifunza  kupitia mtandao  kwa walimu na wanafunzi wa shule za sekondari nchini mapema mwishoni mwa wiki iliyopita ,Hafla ya uzinduzi ilifanyika katika shule ya sekondari Azania Jijini Dar es salaam. 

Mkurugenzi Mtendaji wa  Shule Direct, Faraja K. Nyalandu akizungumza na vyombo mara baada ya mara baada ya uzinduzi  wa jukwaa  la kielimu  la SMS Makini ambalo litakuwa linatoa masuala mbalimbali ya kijifunza  kupitia mtandao  kwa walimu na wanafunzi wa shule za sekondari nchini mapema mwishoni mwa wiki iliyopita ,Hafla ya uzinduzi ilifanyika katika shule ya sekondari Azania Jijini Dar es salaam. 

Wanafunzi wa shule ya sekondari Azania ya jijini Dar es Salaam wakielekezana namna ya kutumia  jukwaa  la kielimu  la SMS Makini ambalo litakuwa linatoa masuala mbalimbali ya kijifunza  kupitia mtandao  kwa walimu na wanafunzi wa shule za sekondari nchini mapema mwishoni mwa wiki iliyopita ,Hafla ya uzinduzi ilifanyika katika shule ya sekondari Azania Jijini Dar es salaam.

Kampuni  inayoongoza kwa mtindo wa maisha ya kidijitali Tigo Tanzania  kwa kushirikiana na asasi ya ndani inayofanya ujasiriamali kwa njia  ya mtandao, Shule Direct  imezindua  jukwaa  la kielimu  la SMS Makini ambalo litakuwa linatoa masuala mbalimbali ya kijifunza  kupitia mtandao  kwa walimu na wanafunzi wa shule za sekondari nchini.
Meneja wa Huduma za jamii wa Tigo  , Woinde Shishael alisema wakati wa hafla  ya uzinduzi huo kwenye Shule ya Sekondari Azania jijini Dar es Salaam leo kwamba SMS Makini zitawawezesha wanafunzi  kuzifikia zana za kujifunza kidijitali  kupitia mtandao na hivyo kuziba pengo lililopo  la rasilimali za kujifunzia  kwenye sekta ya elimu.
“Kupitia  matumizi ya SMS Makini watumiaji wa Tigo, na hususan wanafunzi na walimu wa shule za sekondari wataweza kuipata miuhtasari ya kidijitali, mafunzo, mazoezi, kupata maelezo pamoja na video moja kwa moja kupitia simu ya mkononi,” alisema Woinde.
Alieleza kwamba madarasa yatakayohusishwa  kwenye jukwaa hilo ni kuanzia kidato cha kwanza hadi cha nne  na kuongeza kuwa maelezo ya mafunzo yatakuwa yanazingatia mtaala wa elimu wa Tanzania ukihusisha masomo tisa.
Masomo hayo ni pamoja na Historia, Uraia, Jiografia. Fizikia, Kemia, Kiingereza, Hisabati na Kiswahili.
Kwa mujibu wa Woinde SMS Makini za Tigo pia zitawaunganisha walimu na wanafunzi na fursa ya kujadiliana, kushirikishana mawazo, kurejea, na kupakua mitihani iliyopita ya Baraza la Mitihani la Taifa na hali kadhalika kuwasiliana kwenye mtandao na wanafunzi 10,000 waliosajiliwa.
Wateja wa Tigo wataweza kuipata huduma hiyo bure kwa mwezi mmoja na baada ya hapo watakuwa wanatozwa ada ya siku ya shilingi 100 na ada ya  wiki ya shilingi 500, alisema Woinde.
Kuipata huduma hiyo  wateja wa Tigo wanatakiwa kutuma  neno ‘Makini’ kwenda namba 15397 na baadaye kufuata maelekezo yatakayokuwa yanatolewa.
Ushirikiano na asasi ya Shule Direct ni sehemu ya mkakati wa Tigo wa kuunga mkono miradi ambayo ina manufaa makubwa ndani ya jamii.
MAJALIWA AKUTANA NA VIONGOZI WA TFF

MAJALIWA AKUTANA NA VIONGOZI WA TFF

March 21, 2016

tff1
Waziri  Mkuu, Kassim Majaliwa  akizungumza na viongozi wa  Tanzania Footbal Federation (TFF) ofisini kwake jijini Dar es salaam Machi  21, 2016  Kutoka kushoto ni Katibu Mkuu wa TFF, Selestine Mwesigwa, Rais wa TFF, Jamal Malinzi, Mkurugenzi wa Ufundi Salum Madadi na  Msaidizi wa Rais wa TFF, Juma Matandika.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
tff2
WAZIRI NAPE AZINDUA MSIMU MPYA WA MASHINDANO YA UREMBO YA MISS TANZANIA 2016

WAZIRI NAPE AZINDUA MSIMU MPYA WA MASHINDANO YA UREMBO YA MISS TANZANIA 2016

March 21, 2016
Nape Nnauye
Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akiwasili kwenye hoteli ya Ramada Resort akiambatana na Mkurugenzi wa Lino International Agency ambao ni waandaaji wa shindano la Miss Tanzania, Hashim Lundenga (kulia).(Picha zote na Zainul Mzige wa Modewjiblog)
Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye amezindua rasmi msimu mpya wa mashindano ya urembo ya Miss Tanzania kwa mwaka 2016 katika hafla ya kukata na shoka iliyofanyika kwenye Hotel ya Ramada Resort iliyopo eneo la Kunduchi, Dar es Salaam.
Uzinduzi huo umewakutanisha wadau mbalimbali wa tasnia ya urembo wakiwemo wabunifu wa mavazi, warembo waliowahi kushika taji la Miss Tanzania miaka iliyopita na mawakala wanaoandaa mashindano ya Miss Tanzania katika ngazi mbalimbali hapa nchini.
Nape Nnauye
Mkurugenzi wa Lino International Agency ambao ni waandaaji wa shindano la Miss Tanzania, Hashim Lundenga akitoa mukhtasari wa mashindano hayo kwa mwaka huu 2016 kwa Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (wa pili kushoto). Kushoto ni Mlezi wa kamati ya Miss Tanzania ambaye pia ni Balozi wa Tanzania nchini Botswana, Mh. Emmanuel Ole Naiko na kulia ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Bw. Godfrey Mngereza.
Nape Nnauye
Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (kushoto) akifurahi jambo na mmoja wa wajumbe wa kamati ya Miss Tanzania.
Hoyce Temu
Kutoka kushoto ni Miss Tanzania 2014/2015, Lilian Kamazima, Miss Tanzania 1999, Hoyce Temu pamoja na Miss Tanzania 2008, Nasreen Kareem wakimsikiliza Waziri Nape Nnauye (hayupo pichani).
Hoyce Temu
Miss Tanzania 2014/2015, Lilian Kamazima na Miss Tanzania 1999, Hoyce Temu katika ubora wao.
Nape Nnauye
Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akiendelea na mazungumzo na waandaaji wa mashindano ya Miss Tanzania na Wajumbe wa kamati hiyo kabla ya kuelekea kwenye uzinduzi rasmi.
Wanne Star
Kikundi cha sanaa cha Wanne Star kikitoa burudani kwenye hafla ya uzinduzi wa Msimu mpya wa mashindano ya urembo ya Miss Tanzania 2016 iliyofanyika mwishoni mwa wiki kwenye hoteli ya Ramada Resort ya jijini Dar es Salaam.
Lilian Kamazima
Miss Tanzania 2014/2015, Lilian Kamazima na wadau wa tasnia ya urembo wakitazama burudani mbalimbali zilizokuwa zikijiri katika hoteli ya Ramada Resort ulipofanyika uzinduzi huo mwishoni mwa wiki.
Nape Nnauye
Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (wa pili kushoto), Mkurugenzi wa Lino International Agency ambao ni waandaaji wa shindano la Miss Tanzania, Hashim Lundenga (wa pili kulia) pamoja na Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Bw. Godfrey Mngereza wakishuhudia burudani mbalimbali zilizokuwa zikiendelea ukumbini hapo.
Hashim Lundenga
Mkurugenzi wa Lino International Agency ambao ni waandaaji wa shindano la Miss Tanzania, Hashim Lundenga akizungumza jambo kabla ya kumkaribisha Waziri Nape (hayupo pichani) kuzindua msimu mpya wa mashindano hayo.
Nape Nnauye
Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akitoa baraka kwenye uzinduzi wa msimu mpya wa mashindano ya urembo ya Miss Tanzania 2016 uliofanyika katika hoteli ya Ramada Resort jijini Dar es Salaam.
Nape Nnauye
Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye na Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Bw. Godfrey Mngereza wakishuhudia uzinduzi wa nembo mpya ya mashindano ya Miss Tanzania 2016 yaliyobeba kauli mbiu ya "Mrembo na Mazingira Safi"
IMG_7035
IMG_6959
Pichani juu na chini ni wadau wa tasnia ya urembo na wageni waalikwa waliohudhuria uzinduzi wa Msimu mpya wa mashindano ya urembo ya Miss Tanzania 2016.
Miss Tanzania 2016
Linah Sanga
Msanii wa Bongo flava, Linah Sanga na ma-dancers wake wakitoa burudani kwenye uzinduzi wa msimu mpya wa mashindano ya urembo ya Miss Tanzania 2016.
Linah Sanga
Msanii wa Bongo Flava, Linah Sanga katika ubora wake.
IMG_6980
Wajumbe wa kamati ya mashindano ya Miss Tanzania 2016 wakitambulishwa mbele ya mgeni rasmi Waziri Nape Nnauye (hayupo pichani).
Hoyce Temu
Kutoka kushoto ni Miss Tanzania 1998, Basila Mwanukuzi, Miss Tanzania 1999, Hoyce Temu, Miss Tanzania 2008, Nasreen Kareem pamoja na Miss Tanzania 2014/2015, Lilian Kamazima wakipozi katika picha ya pamoja kwenye uzinduzi wa Msimu mpya wa mashindano ya urembo ya Miss Tanzania 2016. Kwa picha zaidi bofya link hii