Papa Wemba Awasili Dar, Aelekea Bagamoyo Kwenye Tamasha la Karibu Music Festival 2015

November 06, 2015
Mwanamuziki Papa Wemba (kulia) akisalimiana na mwenyeji wake waandaaji wa Tamasha la Karibu Music Festival 2015 mara baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julias Nyerere (JNIA) jijini Dar es Salaam. Kulia ni Meneja wake anayeratibu safari hiyo, Chebli Msaidie akimtambulisha kwa wenyeji wao.
Mwanamuziki Papa Wemba akiwa katika picha ya pamoja na wasanii alioambatana nao waliomo katika bandi yake mara baada ya kutua Tanzania tayari kufanya mashambulizi katika Tamasha la Karibu Music Festival 2015 linalofanyika Bagamoyo.
Mapozi ya wanenguaji wa Papa Wemba katika picha mara baada ya kuwasili jijini Dar es Salaam tayari kwa kutumbuiza katika tamasha la Karibu Music Festival 2015.
Mwanamuziki Papa Wemba akiwa katika picha ya pamoja na wasanii alioambatana nao waliomo katika bandi yake mara baada ya kutua Tanzania tayari kufanya mashambulizi katika Tamasha la Karibu Music Festival 2015 linalofanyika Bagamoyo.
Msafara wa mwanamuziki Papa Wemba ukipokewa na wenyeji wao mara baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julias Nyerere (JNIA).
Mwanamuziki Papa Wemba (kushoto) akiwa na Meneja wake anayeratibu safari hiyo, Chebli Msaidie (kulia) mara baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julias Nyerere (JNIA).

MWANAMUZIKI nguli wa ndansi kutoka nchini Congo (DRC) Papa Wemba amewasili usiku huu jijini Dar es Salaam tayari kwa kutumbuiza katika tamasha la Karibu Music Festival 2015. Papa Wemba ametua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julias Nyerere (JNIA) majira ya saa nane kasoro na ndege ya shirika la Kenya (Kenya Airways-KQ). 

Mara baada ya kuwasili msanii huyo pamoja na wanamuziki wake walipokewa na Meneja wake anayeratibu safari hiyo, Chebli Msaidie pamoja na waandaaji wa Tamasha la Karibu Music Festival 2015 linalofanyika mjini Bagamoyo. 

Papa Wemba na msafara wake umeelekea Bagamoyo tayari kwa kukonga mioyo ya washabiki wa Tamasha hilo. Wasanii wengine ambao wanatarajiwa kutumbuiza katika tamasha hilo ni Jhikolaman, Isha Mashauzi, Damian Soul, Juma Nature, Barnaba, Shilole, mshindi wa pili wa BSS, Nassib Fonabo na bendi yake ya Spirit na wengine wengi. 

Tamasha hilo lililoanza Novemba 6 hadi 8 katika viwanja vya Mwanakalenge, Bagamoyo mkoani Pwani linalengo la kukuza muziki asili ya Afrika. Tamasha limeandaliwa na Kampuni ya watayarishaji wa muziki ya Legendary kwa kushirikiana na kampuni ya kinywaji cha Jebel Coconut. 

Wadhaminiwa wengine ni pamoja na Swiss Embassy, Precion Air, Coca Cola, Mwananchi Communication, Kaya fm, Magic fm, Focus Outdoor, Jovago, Kaymu na Time tickets. huku mgeni mwalikwa akiwa ni mwanamuziki kutoka Congo, Papa Wemba. *Imeandaliwa na www.thehabari.com ___________________________________________________________________________________ Joachim Mushi, Mwenyekiti wa Tanzania Bloggers Network (TBN) na Mhariri Mkuu wa Thehabari.com. Mail address:- mushi@thehabari.com/ jomushi79@yahoo.com/ info@thehabari.com Mobile:- 0717 030066 / 0756 469470 Web:- www.thehabari.com http://joemushi.blogspot.com

RAIS MSTAAFU JAKAYA KIKWETE AONDOKA RASMI IKULU NA KUELEKEA KIJIJINI MSOGA LEO

November 06, 2015

 Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete wakiagana na watumishi wa Ofisi ya Rais Ikulu wakati wakiondoka rasmi katika jumba hilo waliloishi akiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa miaka 10 iliyopita na kurudi kijijini Msoga. kushoto kwake ni Rais wa awamu ya tano Dkt. John Pombe Joseph Magufuli
  Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt Jakaya Mrisho Kikwete  akiagana na watumishi wa Ofisi ya Rais Ikulu wakati akiondoka rasmi katika jumba hilo waliloishi kama Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa miaka 10 iliyopita. kushoto kwake ni Rais wa awamu ya tano Dkt. John Pombe Joseph Magufuli
  Rais wa awamu ya tano Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akimsindikiza Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt Jakaya Mrisho Kikwete   wakati akiondoka rasmi Ikulu alimoishi kama Rais  wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa miaka 10 iliyopita. 
  Rais wa awamu ya tano Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akimsindikiza Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt Jakaya Mrisho Kikwete   na mkewe mama Salma Kikwete wakati wakiondoka rasmi Ikulu alimoishi kama Rais  wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa miaka 10 iliyopita. 
 Wakielekea kwenye helikopta itayowachukua hadi kijijini Msoga
 Picha ya pamoja kabla safari ya Msoga kuanza
  Rais wa awamu ya tano Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akiagana na  Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt Jakaya Mrisho Kikwete   na mkewe mama Salma Kikwete wakati wakiondoka rasmi Ikulu walimoishi kama Rais  wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa miaka 10 iliyopita. 
 Rais wa awamu ya tano Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue na Katibu Mkuu Ikulu Mhe Peter Ilomo na watumishi wa Ofisi ya Rais wakiagana na Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt Jakaya Mrisho kikwete

BALOZI MULAMULA AWASINDIKIZA MRAIS WA DRC NA MSUMBJIA

November 06, 2015

Rais wa Jamuhuri ya Demokrasia ya Kongo, Mhe. Joseph Kabila (wa kwanza kushoto) pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Liberata Mulamula wakitizama Kikundi cha Ngoma kilichokuwa kikitoa Burudani kwenye Uwanja wa Ndege, Rais Kabila alikuja nchini kuhudhuria Sherehe za uapisho wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli iliyofanyika hapo jana katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
Rais Kabila (katikati) akielekea kwenye ndege, kulia ni Balozi Mulamula na kushoto ni Balozi wa Kongo nchini Mhe. Khalifani Mpango
Mhe. Rais Kabila akipita kwenye gwaride la heshima lililoandaliwa na Jeshi la wananchi Tanzania.
Katibu Mkuu Mhe. Balozi Liberata Mulamula (kulia) akiagana na Rais Joseph Kabila tayari kwa kuanza safari ya kuelekea nchini kwake.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Liberata Mulamula (mwenye pochi mkononi) akiagana na Rais wa Msumbiji Mhe. Filipe Nyusi
Rais Nyusi akiagana na Balozi wa Tanzania nchini Msumbiji, Mhe. Shamimu Nyanduga.
Balozi wa Tanzania nchini Ufaransa ambaye anawakilisha pia nchini Algeria, Mhe. Begun Taj akimsindikiza Waziri wa Nchi anayeshughulikia masuala ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Algeria, Mhe. Ramtane Lamamra. Mhe. Lamamra alikuja nchini kwa ajili ya kuhudhiria Sherehe za uapisho wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. John Pombe Magufuli.
Mhe. Lamamra akipanda kwenye ndege tayari kabisa kuanza safari ya kurejea nchini Algeria
Picha na Reginald Philip

TNRF WAMTAKA MAGUFULI ADHIBITI UPOTEVU WA MALIASILI NCHINI

November 06, 2015
 Mwenyekiti wa Jumuiko la Maliasili nchini (TNRF) ,Dr.Suma Kaare akizungumza katika mkutano wa 7 wa jumuiko hilo uliofanyika jijini Arusha na kuhudhuriwa na mashirika binafsi pamoja na wawakilishi kutoka wizara ya maliasili.Picha na Gadiola Emmanuel
  Mkurugenzi wa Shirika la Haki kazi Catalyst Alais Moridant akifafanua jambo  katika mkutano wa 7 wa jumuiko hilo uliofanyika jijini Arusha na kuhudhuriwa na mashirika binafsi pamoja na wawakilishi kutoka wizara ya maliasili.Picha na Gadiola Emmanuel
  Mkurugenzi wa Shirika la AWF ,John Salehe  akifafanua jambo  katika mkutano wa 7 wa jumuiko hilo uliofanyika jijini Arusha na kuhudhuriwa na mashirika binafsi pamoja na wawakilishi kutoka wizara ya maliasili.Picha na Gadiola Emmanuel
  Washiriki wa  mkutano wa 7 wa jumuiko la maliasili  uliofanyika jijini Arusha na kuhudhuriwa na mashirika binafsi pamoja na wawakilishi kutoka wizara ya maliasili.Picha na Gadiola Emmanuel
  Viongozi mbalimbali wa jumuiko la maliasili wakiwa katika mkutano wa 7 wa jumuiko hilo uliofanyika jijini Arusha na kuhudhuriwa na mashirika binafsi pamoja na wawakilishi kutoka wizara ya maliasili.Picha na Gadiola Emmanuel
 Washiriki wa  mkutano wa 7 wa jumuiko la maliasili  uliofanyika jijini Arusha wakiwa katika picha ya pamoja, ,mkutano huo ulihudhuriwa na mashirika binafsi pamoja na wawakilishi kutoka wizara ya maliasili.Picha na Gadiola Emmanuel
Washiriki wa  mkutano wa 7 wa jumuiko la maliasili  uliofanyika jijini Arusha na kuhudhuriwa na mashirika binafsi pamoja na wawakilishi kutoka wizara ya maliasili.Picha na Gadiola Emmanuel 
Washiriki wa  mkutano wa 7 wa jumuiko la maliasili  uliofanyika jijini Arusha na kuhudhuriwa na mashirika binafsi pamoja na wawakilishi kutoka wizara ya maliasili.Picha na Gadiola Emmanuel 
Mwakilishi wa Shirika la WWF ,Sware Semesi  akizungumza katika  mkutano wa 7 wa jumuiko la maliasili  uliofanyika jijini Arusha na kuhudhuriwa na mashirika binafsi pamoja na wawakilishi kutoka wizara ya maliasili.Picha na Gadiola Emmanuel 
 Washiriki wa  mkutano wa 7 wa jumuiko la maliasili  uliofanyika jijini Arusha na kuhudhuriwa na mashirika binafsi pamoja na wawakilishi kutoka wizara ya maliasili.Picha na Gadiola Emmanuel
Wasemaji Wakuu wa   mkutano wa 7 wa jumuiko la maliasili  uliofanyika jijini Arusha na kuhudhuriwa na mashirika binafsi pamoja na wawakilishi kutoka wizara ya maliasili.Picha na Gadiola Emmanuel 

Na Ferdinand Shayo wa Wazalendo 25 Blog ,Arusha.



Mwenyekiti wa Jumuiko la Maliasili nchini Dr.Suma Kaare amemtaka Raisi John Pombe Magufuli adhibiti upotevu wa mali asili za wanyama pori na misitu uliokithiri katika maeneo mengi nchini ili kunusuru uhai wa maliasili.



Suma Kaare amesema  hayo katika mkutano wa 7 wa jumuiko la maliasili  unaoendelea jijini Arusha,Kaare amesema kuwa jukwaa hilo litashirikiana na Rais huyo katika  kuhakikisha kuwa maliasili zinalindwa na kuwanufaisha Watanzania kwa kiwango stahiki.



“Tunajua Rais wetu mpya ana kazi  kubwa  ya kulinda maliasili za nchi hii kama ilivyo kauli mbiu yake ya “kazi tu” tunaamini atazuia upotevu mkubwa wa rasilimali unaofanywa na watendaji wasio waaminifu” Alisema Kaare



Mratibu wa Masuala ya misitu katika shirika la uhifadhi wa maliasili na Mazingira (wwf) ,Isaac Malungu amesema kuwa asilimia 90% ya nishati inayotumika nchini inatokana na kuni pamoja na mkaa hali ambayo inaathiri misitu na kutishia uhai wa maliasili nchini hivyo ameitaka serikali ihimize matumizi ya nishati mbadala ili kunusuru mazingira yanaoharibiwa kila kukicha.



Malungu alisema kuwa kilimo cha kuhama hama pamoja na ukataji miti ovyo umekua ukisababisha uharibifu wa mazingira na hata kupelekea hecta laki 4 za misitu kupotea kila mwaka kutokana na shughuli hizo.



Mkurugenzi wa  Shirika la AWF,John Salehe Alisema kuwa mabadiliko ya tabia ya nchi yamesababisha hali ya ukame inayowaathiri wanyama pamoja na mimea hivyo kuathiri uhifadhi kwa ujumla .



Salehe alisema kuwa juhudi zaidi zinapaswa kuchukuliwa ikiwemo upandaji wa miti pamoja na kutunza misitu ili kurejesha uoto wa asili uliopotea.
-- Gadiel E.W. U (Gadiola Emanuel) IT/ PR /Photojournalist /Event Planner / Photographer (Northern Shots ) and Blogger -Based in Arusha, Tanzania. Mob :+255 715 /755 643 633 E-mail: gadiola25@gmail.com WEB: www.wazalendo25.blogspot.com : www.arushapublicity.com :www.northernshotstz.com
Rais Magufuli afanya Ziara ya Kushtukiza Hazina.

Rais Magufuli afanya Ziara ya Kushtukiza Hazina.

November 06, 2015

1
Rais Dkt.John Pombe Magufuli akisaini kitabu cha wageni muda mfupi baada ya kuwasili katika makao makuu ya Wizara ya Fedha(HAZINA) kwa ziara ya kushtukiza leo mchana.Kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt.Servacius Likwelile.Rais Magufuli alitembelea na kukagua ofisi zote wizarani hapo na kisha kuongea na viongozi waandamizi.
haz2
Rais Dkt.John Pombe Magufuli akizungumza na viongozi waandamizi wa Wizara ya Fedha wakati alipofanya ziara ya kushtukiza Wizarani hapo ambapo alitoa maagizo ya kuziba mianya ya wakwepa kodi.
haz3
Rais Dkt.John Pombe Magufuli akiwa na wafanyakazi wawili wa Wizara ya Fedha ambao ni walemavu Bwana Fundi Maruma na Frank Mkyama wakati Rais alipofanya ziara ya kushtukiza wizarani hapo leo.(picha na Freddy Maro)
STARS YAENDELEA KUJIFUA SAUZI

STARS YAENDELEA KUJIFUA SAUZI

November 06, 2015

Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ inayodhaminiwa na bia ya Kilimanjaro Premium Lager, Charles Boniface Mkwasa ameendelea na mazoezi ya kukinoa kikosi chake kujiandaa na mchezo dhidi ya Algeria Novemba 14 jijini Dar es salaam kuwania kufuzu kwa kombe la Dunia nchini Urusi mwaka 2018.
Baada ya kufanya mazoezi kutwa mara mbili (asubuhi na jioni) kwa siku tatu, leo Ijumaa kocha Mkwasa amekiongoza kikosi chake kufanya mazoezi mara moja wakati wa jioni katika uwanja wa Edenvale.
Mkwasa amesema baada ya kufanya mazoezi ya kujenga mwili, stamina, na pumzi sasa kazi anayoifanya ni kutengeneza mfumo wa kikosi chake kinachojiandaa na mchezo dhidi ya Mbweha wa Jangwani.
“Tulipofika tulianza na mazoezi ya utimamu wa mwili, stamina na pumzi ili kuhakikisha wachezaji wote waliopo kambini wanakuwa katika kiwango kimoja kutokana na kuwa wachezaji wanatoka katika timu tofauti na zenye walimu na mifumo tofauti” Alisema Mkwasa.
“Sasa baada ya wachezaji kufanya mazoezi kwa siku nne kuweka uwiano sawa kiwango cha kimazoezi (fitness level) kwa sasa tunafanya kazi kutengeneza mfumo na jinsi ya uchezaji” aliongeza Mkwasa.
Stars inaendelea na mazoezi leo jioni na kesho Jumamosi itafanya mazoezi asubuhi katika uwanja wa Edenvale
NB: Namba ya Afisa Habari wa TFF aliyepo nchini Afrika Kusini +27 78 641 1595
Rais Magufuli awakutanisha Rais Uhuru na Mhe.Raila Odinga

Rais Magufuli awakutanisha Rais Uhuru na Mhe.Raila Odinga

November 06, 2015


1
Rais Dkt.John Pombe Magufuli akipongezwa na Rais wa Msumbiji Felipe Jacinto Nyusi Muda mfupi baada ya Dkt.Magufuli kuapishwa kuwa Rais wa Awamu ya Tano katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam leo.Wengine waliomzunguka Rais Magufuli ni kutoka kushoto Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya,Rais Jacob Zuma wa Afrika ya Kusini na Rais Joseph Kabila wa DRC.
2
Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni akimpongeza Rais Dkt.John Pombe Magufuli kwa kuapishwa kuwa Rais wa awamu ya Tano Tanzania wakati wa hafla ya chakula cha mchana iliyofanyika ikulu jijini Dar es Salaam jana.
3
Rais Dkt.John Pombe Magufuli akiwa amwashikanisha mikono Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya na Raila Odinga wakati wa hafla ya chakula cha mchana iliyofanyika ikulu jijini Dar es Salaam jana.wanaoshuhudia tukio hili kutoka kushoto ni Mke wa Rais Uhuru Kenyatta,Mke wa Rais Mama Janet Magufuli na kulia ni Mke wa Mhe.Raila Odinga
4
Rais Dkt.John Pombe Magufuli akiwa amwashikanisha mikono Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya na Raila Odinga ikulu jijini Dar es Salaam wakati wa hafla ya chakula cha mchana alichoandaa Rais Magufuli kwa heshima ya wageni waliohudhuria sherehe ya kuapishwa kwake kuwa Rais wa awamu ya tano.

SHEREHE ZA KUMUAPISHA RAIS MPYA DK. JOHN MAGUFULI ZAFANA JIJINI DAR

November 06, 2015
Rais Dk. John Magufuli akila kiapo cha kuwa Rais wa Tanzania, mbele ya Jaji Mkuu Othman Chande. Katikati ni Katibu Mkuu Kiongozi, Ombeni Sefue na kushoto ni Rais mstaafu Jakaya Kikwete. 
PICHA ZOTE NA CATHBERT KAJUNA WA KAJUNASON BLOG.
Rais Dk. John Magufuli akiwa ameshika mkuki na ngao baada ya kukabidhiwa na wazee katika hafla ya kumuapisha iliyofanyika jana kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.
Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan akila kiapo cha kuwa Rais wa Tanzania, mbele ya Jaji Mkuu Othman Chande. Katikati ni Katibu Mkuu Kiongozi, Ombeni Sefue na kushoto ni Rais mstaafu Jakaya Kikwete.
Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dk Alex Malasusa akisoma neno la baraka mara baada ya kumaliza kuapishwa rais Dk. Magufuli.
Viongozi wa dini wakitoka jukwaani mara baada kumaliza zoezi la kuapishwa Rais Dk. John Magufuli.
Rais aliyemaliza muda wake Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Makamu wake Dk. Bilal mara baada ya kumaliza kuwapishwa rais mpya Dk. John Mafufuli.
Rais Dk. John Magufuliakikagua gwaride.
Wageni waalikwa.
Rais aliyemaliza muda wake Dk. Jakaya Kikwete akiwasalimia wananchi mara baada ya kuwasili uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Rais aliyemaliza muda wake Dk. Jakaya Kikwete akikagua gwaride.
 Rais aliyemaliza muda wake Dk. Jakaya Kikwete akiimbiwa wimbo wa taifa.
 
Rais Dk. John Magufuli  akisalimia na mkewe mama Janeth Magufuli.
Rais Dk. John Magufuli akiteta jambo na rais aliyemaliza muda wake Dk. Jakaya Kikwete.
Rais aliyemaliza muda wake Dk. Jakaya Kikwete akiwa na makamu wake Dk. Bilal wakiaga wananchi.
-- ---- Cathbert Angelo Kajuna, Founder and Mananging Director Kajunason Blog, P.O Box 6482, Dar es Salaam. Tel: +255 787 999 774 Alt: +255 765 253 445 www.kajunason.blogspot.com "Everything is Possible Through Peace & Stability''