RC GALLAWA AANZA ZIARA YA KUANGALIA MAENDELEO YA UJENZI WA MAABARA WILAYA YA TANGA LEO

October 28, 2014


KATIKATI NI MKUU WA MKOA WA TANGA,LUTENI MSTAAFU CHIKU GALLAWA KUSHOTO NI MKUU WA WILAYA YA TANGA HALIMA DENDEGO LEO AKIWA KWENYE SHULE YA SEKONDARI MAWENI


HAPA KUSHOTO NI MKUU WA WILAYA YA TANGA HALIMA DENDEGO AKISISITIZA JAMBO KWA MKUU WA MKOA WA TANGA,LUTENI MSTAAFU CHIKU GALLAWA LEO WAKATI WA ZIARA YAKEE


HAPA NI ENEO LA STENDI MPYA YA MABASI YA KANGE AKIZUNGUMZA NA VIONGOZI WA WILAYA YA TANGA MARA BAADA YA KUITEMBELEA LEO






PINDA AWASILI OMAN KWA ZIARA YA KIKAZI

PINDA AWASILI OMAN KWA ZIARA YA KIKAZI

October 28, 2014

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akikagua gwaride baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Muscut wa Royal  Airport kwa ziara ya kikazi ya siku mbili nchini Oman Oktoba 27, 2014. Kushoto ni Naibu Waziri Mkuu wa Oman Mheshimiwa Sayyid Fahad Mahmoud Al Said. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) unnamed4 
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda  akiongozana na Naibu Waziri Mkuu wa Oman,  Mheshimiwa Sayyid Fahad Mahmoud Al Said  (kushoto kwake) baada  ya kuwasili kwenye  uwanja wa ndege wa  Kimataifa wa  Muscut wa Royal Airport kwa ziara ya siku mbili nchini humo Oktoba  27, 2014. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) unnamed5 
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na baadhi ya Watanzania waishio Oman baada ya kuwasili kwenye hoteli ya AL Bustan Palace mjini Muscut kuanza ziara ya siku mbili nchini humo, Oktoba  27, 2014. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) unnamed6 unnamed7
 HABARI KUTOKA BARAZA LA WAWAKILISHI ZANZIBAR

HABARI KUTOKA BARAZA LA WAWAKILISHI ZANZIBAR

October 28, 2014

index 
Na Maryam himid kidiko na Kijakazi Abdallah-Maelezo Zanzibar
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itaendelea na juhudi zake za kuwaelimisha Wananchi ili waachane na tabia ya kujenga karibu na  maeneo ya Kambi za Kijeshi kwa lengo la kuepuka usumbufu pamoja na madhara yanayoweza kuwakumba baadae.
Hayo yameelezwa na Waziri wa nchi Ofisi ya Makamo wa pili wa Rais Mohamed Abuod wakati akijibu suala la Mwakilishi wa Jimbo la Wawi Saleh Nassor Juma katika kikao cha tano kinachoendelea cha Baraza la Wawakilishi. 
Saleh alitaka kujua kuwa lini Serikali itafikiria kuzihamisha kambi za kijeshi zilizopo karibu na Makaazi ya Raia na kuzipeleka nje ya Miji na Vijiji.
Waziri Aboud alifahamisha kuwa katika nchi yoyote ile duniani kambi za kijeshi huwekwa Kimkakati kwa lengo la kuimarisha ulinzi na usalama katika nchi husika ikiwemo Zanzibar.
Alisema Kambi zilizopo nchini sio tatizo na kwamba zimewekwa kwa kuzingatia haja ya kiulinzi, usalama na mazingira ya Zanzibar ilivyo.
Ameongeza kuwa Jeshi la Wananchi linahitaji maeneo maalum yakiwemo ya kufanyia mazoezi ili kujiweka tayari kwa adui yoyote Yule atakaeingia katika nchi kwa kufanya uadui.
Hata hivyo aliongeza kuwa kwa sasa kambi zilizopo zilijegwa kwa miaka mingi iliyopita na kwa wakati huo maeneo hayo hayakuwa karibu na makaazi ya raia.
Amesema kutokana na maeneo ya Kambi hizo kuvamiwa na Wananchi kwa lengo la kuanzisha Makaazi limekuwa tatizo na kwamba juhudi zinafanywa kuondokana na tatizo hilo ikiwemo kuwaelimisha Wananchi juu ya Madhara yanayoweza kujitokeza
Tanzania yaeleza mipango yake ya kuendeleza Jotoardhi

Tanzania yaeleza mipango yake ya kuendeleza Jotoardhi

October 28, 2014

1a 
Wajumbe wa Kamati ya Watoa Maamuzi Kamati ya Watoa Maamuzi ya nchi zilizo katika Bonde la Ufa katika kongamano la Tano la Kimataifa la Jotoardhi wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kumalizika kwa kikao hicho.
2a 
Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Watoa Maamuzi wa nchi zilizo katika Bonde la Ufa wakijadiliano jambo wakati wa kikao cha wajumbe hao kujadilia masuala mbalimbali kuhusu utekelezaji wa Jotoardhi kwa nchi wananchama.
3a 
Baadhi wa Wajumbe wa Kamati ya Watoa Maamuzi wan chi zilizo katika Bonde la Ufa wakiendelea na kikao kujadili hatua mbalimbali zilizofikiwa na nchi wananchama katika masuala ya jotoardhi katika nchi zao, kuangalia faida zalke, changamoto na namna ya kuzitatua.
4a 
Mmoja wa Wakufunzi wa mafunzo yanayoendelea leo kabla ya kufunguliwa rasmi Kongamano la Tano la Kimataifa ya Jotoardhi akitoa mafunzo kwa baadhi ya washiriki wanaohudhuria mafunzo hayo jijini Arusha.
…………………………………………………
Na Asteria Muhozya, Arusha
Tanzania imeeleza mipango yake ya kuendeleza masuala yanayohusu nishati jadidifu mbele ya Kamati ya Watoa Maamuzi ya nchi zilizo katika Bonde la Ufa katika kongamano la Tano la Kimtaifa la Jotoardhi linaloendelea jijjini Arusha.
Akizungumza mara baada ya kikao hicho kwa niaba ya Kamishna Msaidizi anayeshughulikia masuala ya Jotoardhi Wizara ya Nishati na Madini, Bw. Paul Kiwele amesema kuwa lengo la kukutana kwa kamati hiyo ni kuzungumzia hatua zilizofikiwa na nchi wananchama katika masuala ya jotoardhi katika nchi zao.
Bw. Kiwele ambaye pia ni mjumbe wa Kamati ya Maandalizi ya Kongamano hilo ameeleza kuwa, lengo jingine la kikao hicho ni kuangalia faida zilizopatikana kupitia nishati hiyo pamoja na kuangalia changamoto mbalimbali na kuona namna bora ya kuzitatua.
Ameongeza kuwa, pendekezo la nchi wanachama kupata misaada mbalimbali ya kuendeleza masuala ya jotoardhi katika nchi zao ikiwemo ya kifedha limepitishwa na mashirika kadhaa ikiwemo Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia masuala ya Uhifadhi wa Mazingira ( UNEP) na Umoja wa nchi zilizo katika bonde la Ufa (ARGEO)
Aidha, Bw, Kiwele ameongeza kuwa, kikao hicho kimeamua kuipa nafasi Tanzania kusaidiwa kuendeleza masuala ya jotoardhi katika eneo lenye viashiria vya jotoardhi la Ngozi, Mkoani Mbeya.
Kikao hicho cha Kamati ya Watoa Maamuzi ni miongoni mwa shughuli zinazoendelea katika kongamano la tano la jotoardhi ambapo linakwenda sambamba na mafunzo mbalimbali yanayotolewa kuhusu masuala ya jotoardhi ikiwemo masuala ya utafiti, uchorongaji na masuala ya fedha.
Kongamano hilo litafunguliwa rasmi tarehe 29 Oktoba, 2014, na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dk. Mohamed Gharib Bilal jijini Arusha na litawashirikisha washiriki zaidi ya 400 kutoka nchi mbalimbali duniani.
MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AFUNGUA MAONESHO YA MWEZI WA WANAWAKE WAJASILIAMALI (MOWE) JIJINI DAR ES SALAAM.

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AFUNGUA MAONESHO YA MWEZI WA WANAWAKE WAJASILIAMALI (MOWE) JIJINI DAR ES SALAAM.

October 28, 2014


1Makamu wa Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Janeth Mbene, wakati aliwasili kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, leo Oktoba 28, 2014 kwa ajili ya kufungua rasmi Maonesho ya mwezi wa Wanawake Wajasiliamali (MOWE). Picha na OMR 2Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Meneja Masoko wa Kampuni ya GS 1, Ester Budili, wakati alipokuwa akitembelea katika mabanda ya maonesho ya Wajasiliamali, wakati wa ufunguzi wa Maonesho hayo ya mwezi ya Wanawakae wajasaliamali (MOWE) yaliyofanyika kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam leo. Oktoba 28, 2014. Kulia ni Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Janeth Mbene. Picha na OMR 3Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Mkurugenzi msaidizi wa Kampuni ya Kazymate, Mariam Mjewa, kuhusu Jarida maalum la ‘Mchakarikaji’  wakati alipokuwa akitembelea katika mabanda ya maonesho ya Wajasiliamali, wakati wa ufunguzi wa Maonesho hayo ya mwezi ya Wanawakae wajasaliamali (MOWE) yaliyofanyika kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam leo. Oktoba 28, 2014. Picha na OMR 4Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitembelea katika mabanda ya maonesho ya Wajasiliamali, wakati wa ufunguzi wa Maonesho hayo ya mwezi ya Wanawakae wajasaliamali (MOWE) yaliyofanyika kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam leo. Oktoba 28, 2014. Picha na OMR 5Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiangalia Chupa ya kinywaji cha Dodoma Wine wakati alipokuwa akitembelea katika mabanda ya maonesho ya Wajasiliamali, wakati wa ufunguzi wa Maonesho hayo ya mwezi ya Wanawakae wajasaliamali (MOWE) yaliyofanyika kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam leo. Oktoba 28, 2014. Picha na OMR 6 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiangalia Viatu (makubazi) na kusikiliza maelezo kutoka kwa Bi Hadija Rashid wa Kikundi cha Wajasiliamali cha Vumilia Corporation kutoka Pemba, wakati alipokuwa akitembelea katika mabanda ya maonesho ya Wajasiliamali, wakati wa ufunguzi wa Maonesho hayo ya mwezi ya Wanawakae wajasaliamali (MOWE) yaliyofanyika kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam leo. Oktoba 28, 2014. Picha na OMR 7 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiangalia bidhaa na kusikiliza maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Kikundi cha Wajasiliamali Walemavu cha Women Clief Mafinga, Fatina Kangessa, wakati alipokuwa akitembelea katika mabanda ya maonesho ya Wajasiliamali, wakati wa ufunguzi wa Maonesho hayo ya mwezi ya Wanawakae wajasaliamali (MOWE) yaliyofanyika kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam leo. Oktoba 28, 2014. Picha na OMR 8Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Mratibu wa Kitaifa wa Program kuendeleza Ujasiliamali kwa Wanawake, Noreen Toroka, wakati alipokuwa akitembelea katika mabanda ya maonesho ya Wajasiliamali, wakati wa ufunguzi wa Maonesho hayo ya mwezi ya Wanawakae wajasaliamali (MOWE) yaliyofanyika kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam leo. Oktoba 28, 2014. Picha na OMR
9Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisoma hotuba yake ya ufunguzi rasmi wa Maonesho ya mwezi ya Wanawakae wajasaliamali (MOWE) yaliyofanyika kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam leo. Oktoba 28, 2014. Picha na OMR
10Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa vikundi mbalimbali na wageni waalikwa katika maonesho hayo. Picha na OMR 11Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa vikundi mbalimbali na wageni waalikwa katika maonesho hayo. Picha na OMR