HEKAHEKA MAANDALIZI YA SHULE, TANGA
Mwanafunzi wa darasa la pili shule ya msingi ya Mwanzange halmashauri ya jiji la Tanga, Khalid Said, akisaidiwa na dada yake kujaribu kaprura ikiwa ni maandalizi ya shule ambazo zinatarajiwa kufunguliwa nchini kote Jumanne.
LOWASSA, SUMAE, NYALANDU WASHIRIKI IBADA YA KUMSIMIKA ASKOFU KKKT KIMANDOLU
Waziri
mkuu wa mstaafu na mbunge wa Monduli Mh Edward Lowassa akisalimiana na
mamia ya waumini wa kanisa la KKKT Kimandolu jijini Arusha baada ya
Ibada ya kusimikwa uaskofu mchungaji Solomon Jacob Masangwa kuwa askofu
wa dayosisi ya kaskazini Kati leo Jumamosi Waumini hao walipigana
vikumbo kumpiga picha na simu zao.
Waziri
wa Maliasili na Utalii,Lazaro Nyalandu akipunga mkono kusalimia katika
ibada ya kumweka wakfu Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kirutheri
Tanzania(KKKT)Dayosisi ya Kaskazini Kati,Solomon Massangwa jana kwenye
Usharika wa Kimandolu.
Viongozi
waliohudhuria ibada hiyo katika Usharika wa Kimandolu,kutoka kushoto ni
Waziri wa Maliasili na Utalii,Lazaro Nyalandu,Mkuu wa mkoa wa
Simiyu,Eraston Mbwilo,Balozi wa Tanzania nchini Nigeria,Daniel Ole
Njolay na Waziri Mkuu mstaafu,Frederick Sumaye.
HIVI NDIVYO ILIVYOKUWA *MBUNGE WA MBEYA MJINI MR. SUGU ALIPOPATA AJALI MLIMA KITONGA JANA
Mbunge
wa Jimbo la Mbeya Mjini,Mh. Joseph Mbilinyi akifanya mawasiliano kwa
ndugu na jamaa mara baada ya kupata ajali mbaya na kunusurika kifo,ajali
hiyo imetokea eneo la Mlima Kitonga Mkoani Iringa mchana wa leo.kwa
mujibu wa chanzo chetu cha habari kimeeleza kuwa Mh. Mbilinyi alikuwa
safarini akitokea Mkoani Mbeya kuelekea jijini Dar akiwa na jamaa zake
Wanne katika gari hilo lenye namba za usajili T 148 BQE. katika ajali
hiyo hakuna aliyepoteza maisha.
Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini,Mh. Joseph Mbilinyi (watatu kushoto) akizungumza namna hali ilivyokuwa mpaka kupata ajali hiyo.
COASTAL UNION NA MOMBASA KOMBAINI ZATOKA SARE YA KUFUNGANA 1-1,MECHI YA KIRAFIKI JANA
KIKOSI CHA COASTAL UNION KILICHOCHEZA JANA NA MOMBASA KOMBAINI NA KUMALIZKA KWA SARE YA KUFUNGANA BAO 1-1 ,MKWAKWANI |
WACHEZAJI WAKISALIMIANA HAPO |
BENCHI LA UFUNDI LA COASTAL UNION LIKIONGOZWA NA KOCHA MKUU,JAMES NANDWA WA KWANZA |
VIONGOZI WA COASTAL UNION WA KWANZA KUSHOTO NI MENEJA WA TIMU HIYO,AKIDA MACHAI,KATIKATI NI KATIBU MKUU KASSIM EL SIAGI NA MJUMBE WA KAMATI YA UTENDAJI SALIM BAWAZIRI WAKIFUATLIA MCHEZO HUO |
MAMA SALMA KIKWETE AWAANDALIA TAFRIJA YA MWAKA MPYA WENZA WA MABALOZI WA NJE WALIOPO TANZANIA
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akitoa hotuba yake wakati wa tafrija ya mwaka mpya aliyoiandaa huko Ikulu tarehe 10.1.2015 kwa ajili ya wenza wa mabalozi wa nchi za nje walioko hapa Tanzania.
Baadhi ya wageni waalikwa wakiongozwa na Mke wa Makamu wa Rais Mama Zakhia Bilal (wa kwanza kushoto) wakisikiliza hotuba ya Mke wa Rais Mama Salma Kikwete (hayupo pichani) wakati wa tarfija ya mwaka mpya aliyowaandalia wenza wa mabalozi wa nchi za nje waliopo hapa Tanzania tarehe 10.1.2015.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akisalimiana na Mama Anna Mkapa wakati wa tafrija ya mwaka mpya aliyoiandaa huko ikulu tarehe 10.1.2015 kwa ajili ya wenza wa mabalozi wa nje hapa nchini.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akipongezwa kwa hotuba yake na Mama Celine Mpango, Mke wa Balozi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo hapa nchini. Mama Mpango ni kiongozi wa wenza wa mabalozi wa nje waliopo hapa Tanzania.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akijumuika na wenza wa mabalozi na wageni waalikwa kupiga picha ya kumbukumbu.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akizungumza na na baadhi ya wenza wa mabalozi wa nje waliopo hapa Tanzania wakati wa tafrija ya mwaka mpya aliyowaandalia huko Ikulu tarehe 10.1.2015.
Mke wa Makamu wa Rais Mama Zakhia Bilal akijadiana jambo na Kiongozi wa wenza wa mabalozi waliopo hapa nchini Mama Celine Mpango wakati wa tafrija ya mwaka mpya. PICHA NA JOHN LUKUWI.
Mh. Makalla akagua miundombinu ya maji jijini Mbeya
Naibu
Waziri wa Waji,Mh. Amos Makalla amefanya ziara ya kikazi jijini Mbeya na
kufanikiwa kutembelea vyanzo mvali mbali vya maji vilivyo chini ya
Mamlaka ya Maji Safi jijini humo.
Mh.
Makalla amevutiwa sana na utendaji kazi wa Mamlaka hiyo na kuupongeza
kwa kuongeza idadi kuwa wateja wa maji kutoka 9000 mwaka 2002 na kufikia
40,000 hivi sasa na pia kuwa mamlaka ya tatu kitaifa kuwa na
miundombinu ya majitaka.
Mh.
Makalla ameiagiza Mamlaka hiyo kuhakikisha inadhibiti upotevu wa maji
kutoka asilimia 34 ya sasa na wafikie kiwango cha kimataifa asilimia 20.
Naibu
Waziri wa Waji,Mh. Amos Makalla (katikati) akimsikiliza Ing. Martin
Kimambo wakati akimwonyesha na kumpa maelezo kuhusu miundombinu ya maji
taka eneo la Kalobe.
Naibu Waziri wa Waji,Mh. Amos Makalla akiangalia chujio la maji eneo la Swaya.
Naibu Waziri wa Waji,Mh. Amos Makalla akishuka kwenda kukagua tanki la maji la kadege,jijini Mbeya.
Naibu Waziri wa Waji,Mh. Amos Makalla akishuka kukagua mitambo eneo la Kadege.
Naibu Waziri wa Waji,Mh. Amos Makalla akielekeza jambo wakati akikagua chanzo cha chemchem Nzovwe.
Naibu Waziri wa Waji,Mh. Amos Makalla akimsiliza mwenyekiti wa bodi ya maji jijini Mbeya,Jaji Atuganile Ngwale.
Naibu Waziri wa Waji,Mh. Amos Makalla akiongea na bodi na Menejimenti ya Mamlaka Maji jiji la Mbeya.
DKT. SHEIN AYAPOKEA MATEMBEZI YA VIJANA WA UVCCM,ZANZIBAR
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein
pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar akikagua gwaride la Chipukizi wa
UVCCM wakati alipofika katika viwanja vya Mnazi Mmoja leo Mjini Zanzinar
kupokea matembezi ya Umoja wa UVCCM yenye lengo la kuwaenzi Viongozi
na kuadhimisha miaka 51 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Vijana
wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi UVCCM wakiwa wamebeba Bendera
na Picha za Viongozi wakati wa kilele cha matembezi ya Umoja wa UVCCM
yenye lengo la kuwaenzi Viongozi na kuadhimisha miaka 51 ya Mapinduzi ya
Zanzibar yaliyopokelewa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza
la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar
leo katika viwanja vya Mnazi Mmoja Mjini Unguja.
Vijana
wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi UVCCM wakiwa katika
matembezi ya Umoja wa UVCCM yenye lengo la kuwaenzi Viongozi na
kuadhimisha miaka 51 ya Mapinduzi ya Zanzibar yaliyopokelewa na Rais wa
Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein
pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibarleo katika viwanja vya Mnazi Mmoja
Mjini Unguja.
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein
pia Makamo Mwenyekti wa CCM Zanzibar akipokea matembezi ya Vijana wa
Umoja wa UVCCM yaliyofikia kilele chake leo katika Viwanja vya Mnazi
Mmoja Mjini Unguja ikiwa ni kuadhimisha miaka 51 ya Mapinduzi Matukufu
ya Zanzibar (kushoto) Mwenyekiti wa UVCCM Sadifa Juma Khamis.
Viongozi
wa Chama cha Mapinduzi wakiwepo wa UVCCM wakisimama wakati Makamo
Mwenyekti wa CCM Zanzibar na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akipokea matembezi ya Vijana wa Umoja wa
UVCCM yaliyofikia kilele chake leo katika Viwanja vya Mnazi Mmoja Mjini
Unguja ikiwa ni kuadhimisha miaka 51 ya mapinduzi Matukufu ya Zanzibar
Vijana
wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi UVCCM wa Mkoa wa Kaskazini
Unguja wakiwa katika matembezi ya Umoja wa UVCCM yenye lengo la
kuwaenzi Viongozi na kuadhimisha miaka 51 ya Mapinduzi ya Zanzibar
yaliyopokelewa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar leo
ambapo kilele chake katika viwanja vya Mnazi Mmoja Mjini Unguja.
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein
pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar akipokea picha za Viongozi kutoka
kwa kiongozi wa Matembezi ya UVCCM Daudi Ismail Juma Mjumbe wa
Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC) kupitia UVCCM wakati wa kilele cha
Matembezi ya kuwaenzi Viongozi na kuadhimisha miaka 51 ya Mapinduzi
Matukufu ya Zanzibar leo katika viwanja vya Mnazi Mmoja Mjini Unguja.
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein
pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar akimkabidhi Picha ya Mwenyekiti wa
CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Jakaya Mrisho
Kikwete,Mwenyekiti wa UVCCM Sadifa Juma Khamis baada ya kuyapokea
matembezi ya Vijana wa UVCCM yaliyofikia kilele chake leo katika viwanja
wa Mnazi Mmjoa Mjini Unguja katika kuadhimisha miaka 51 ya Mapinduzi
Matukufu ya Zanzibar
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein
pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar akipokea Bendera kutoka kwa
Kiongozi wa Matembezi ya UVCCM Daudi Ismail Juma Mjumbe wa Halmashauri
Kuu ya CCM Taifa (NEC)kupitia UVCCM wakati wa kilele cha Matembezi ya
kuwaenzi Viongozi na kuadhimisha miaka 51 ya Mapinduzi Matukufu ya
Zanzibar leo katika viwanja vya Mnazi Mmoja Mjini Unguja.
Vijana
wa Chipukizi wakipita kwa gwaride la mwendo wa haraka mbele ya mgeni
rasmi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali
Mohamed Shein pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibarwakati wa kilele cha
matembezi ya Umoja wa UVCCM yenye lengo la kuwaenzi Viongozi na
kuadhimisha miaka 51 ya Mapinduzi ya Zanzibar leo katika viwanja vya
Mnazi mmoja mjini Unguja.
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein
pia Makamo Mwenyekti wa CCM Zanzibar akimkabidhi Cheti Mke wa Makamo wa
Pili wa Rais Mama Asha Suleiman kwa niaba ya Makamo wa Pili wa Rais
Balozi Seif Ali Idii kwa mchango wake mkubwa kufanikisha matembezi ya
Vijana wa Umoja wa UVCCM yaliyofikia kilele chake leo katika Viwanja vya
Mnazi Mmoja Mjini Unguja ikiwa ni kuadhimisha miaka 51 ya Mapinduzi
Matukufu ya Zanzibar (kushoto) Mwenyekiti wa UVCCM Sadifa Juma Khamis.
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein
pia Makamo Mwenyekti wa CCM Zanzibar akimkabidhi Cheti Makamo
Mwenyekiti wa Chipukizi Taifa Pili Hassan Suluhu wakati wa matembezi
ya Vijana wa Umoja wa UVCCM yaliyofikia kilele chake leo katika Viwanja
vya Mnazi Mmoja Mjini Unguja ikiwa ni kuadhimisha miaka 51 ya Mapinduzi
Matukufu ya Zanzibar (kushoto) Mwenyekiti wa UVCCM Sadifa Juma Khamis.
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein
pia Makamo Mwenyekti wa CCM Zanzibar akitoa hutuba yake wakati wa Kilele
cha matembezi ya Vijana wa Umoja wa UVCCM yaliyofikia leo katika
Viwanja vya Mnazi Mmoja Mjini Unguja ikiwa ni kuadhimisha miaka 51 ya
Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar (kushoto) Mwenyekiti wa UVCCM Sadifa Juma
Khamis.
Baadhi
ya Vijana wa UVCCM wakimasikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa
Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein pia Makamo Mwenyekti wa CCM
Zanzibar alipokuwa akitoa hutuba yake wakati wa Kilele cha matembezi
ya Vijana wa Umoja wa UVCCM yaliyofikia leo katika Viwanja vya Mnazi
Mmoja Mjini Unguja ikiwa ni kuadhimisha miaka 51 ya Mapinduzi Matukufu
ya Zanzibar (kushoto) Mwenyekiti wa UVCCM Sadifa Juma Khamis.Picha na
Ikulu.
Subscribe to:
Posts (Atom)