RAIS DKT. MAGUFULI AWEKA JIWE LA MSINGI DARAJA WA WAENDA KWA MIGUU LA FURAHISHA PAMOJA NA UPANUZI WA BARABARA YA MWANZA AIRPORT

August 11, 2016

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mkewe Mama Janeth Magufuli pamoja na Naibu Waziri wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Edwin Ngonyani, Mbunge wa Sumve Richard Ndassa wakipiga makofi mara baada ya tukio la uwekaji wa Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Daraja la waenda kwa miguu la Furahisha pamoja na Upanuzi wa barabara ya Mwanza-airport.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katikati akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Mitambo itakayotumika katika ujenzi wa Daraja la waenda kwa miguu la Furahisha pamoja na upanuzi wa barabara ya Mwanza-airport.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini TANROADS, Mhandisi Patrick Mfugale akitoa maelezo ya namna daraja la Furahisha litakavyokuwa mara baada ya kukamilika.

WADAU WA MAENDELEO WAKUTANA NA SERIKALI KUJADILI NAMNA YA KUBORESHA UHUSIANO

August 11, 2016



Mwenyekiti wa mkutano wa wadau wa Washirika wa Maendeleo Dkt. Donald  Kaberuka akifafanua jambo kwa wajumbe (hawapo pichani) waliohudhuria mkutano wa kutafuta njia bora ya kuhuisha na kuimarisha ushirikiano kati ya wadau hao wa maendeleo na serikali, mkutano huo umefanyika katika ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) jijini Dar es salaam.
Mmoja wa washiriki wa mkutano huo kutoka meza kuu akichangia jambo wakati wa mjadala kuhusu namna bora ya Tanzania kuhuisha na kuimarisha ushirikiano na wadau wake wa maendeleo, mkutoano huo umefanyika katika ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Jijini Dar es salaam. Kulia kwake anaonekana Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Dkt. Servacius Likwelile.
Mtaalamu Mshauri James Adams, akichokoza mada ya namna bora ya kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na wadau wake wa maendeleo, mkutano huo umefanyika katika ukumbi wa mikutano wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT), Jijini Dar es salaam.

Mwenyekiti wa mkutano unaojadili kuhusu namna ya kuboresha mahusiano kati ya Tanzania na Wadau wake wa Maendeleo, aliyewahi kuwa Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika-AfDB-Dkt. Donald Kaberuka (kushoto), akifafanua jambo kwenye ukumbi wa mikutano wa Benki Kuu, Jijini Dar es salaam, kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Dkt. Servacius Likwelile.
Washirika wa Maendeleo wakiwa katika mkutano wa pamoja kuhusu namna ya kuboresha mahusiano kati ya Tanzania na Wadau wake wa Maendeleo, mkutano huo umefanyika katika ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) jijini Dar es salaam. 
Mwenyekiti wa mkutano, aliyewahi kuwa Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika-AfDB-Dkt. Donald Kaberuka (kushoto), katikati ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Servacius Likwelile na kulia ni Bw. Steve Kayizzi Mugerwa wakisikiliza hoja ya mdau wa Maendeleo (hayupo pichani) wakati wa mjadala kuhusu namna ya kuimarisha ushirikiano.
Washirika wa Maendeleo wakiwa katika mkutano wa pamoja kuhusu namna ya kuimarisha uhusiano wa Maendeleo nchini Tanzania, mkutano umefanyika katika ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Jijini Dar es salaam. 
Kaimu Katibu Mkuu wa Tume ya Mipango Bi. Florence Mwanri (kushoto) akisikiliza kwa makini hoja ya mjumbe wa Mkutano kuhusu namna ya kuboresha ushirikiano kati ya Tanzania na Wadau wake wa Maendeleo, mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Jijini Dar es salaam. 
Washirika wa Maendeleo wakiwa katika mkutano wa pamoja kutafuta njia bora ya kuhuisha na kuimarisha ushirikiano kati ya wadau hao wa maendeleo na serikali, mkutano huo umefanyika katika ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) jijini Dar es salaam.
Washirika wa Maendeleo wakiwa katika mkutano wa pamoja kutafuta njia bora ya kuhuisha na kuimarisha ushirikiano kati ya wadau hao wa maendeleo na serikali, mkutano huo umefanyika katika ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) jijini Dar es salaam.

Suluhu ya magwangala yapatikana Mkoani Geita

August 11, 2016

Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (katikati) akifafanua jambo katika eneo la Lwenge, Nyamikoma ambalo ni moja ya maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya kuhifadhi magwangala.

Na Greyson Mwase, Geita

Mgogoro uliodumu kwa muda mrefu katika mkoa wa Geita kuhusu upatikanaji wa magwangala na eneo la kuhifadhi magwangala hayo, umepatiwa ufumbuzi baada ya Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo kukutana na mkuu wa mkoa wa Geita, uongozi wa Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM), watendaji wa halmashauri ya mkoa huo na wawakilishi kutoka Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC).

Profesa Muhongo alifanya ziara katika mkoa huo ikiwa ni utekelezaji wa agizo lililotolewa na Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania John Magufuli lililotolewa Julai 31 mwaka huu la wachimbaji wadogo kupatiwa magwangala pamoja na maeneo ya kuhifadhi magwangala hayo ili kuchenjua na kupata dhahabu.
Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (kushoto) akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Geita. Kulia ni mkuu wa mkoa huo, Meja Jenerali Mstaafu, Ezekiel Kyunga.

Akizungumza katika kikao kilichokutanisha watendaji kutoka Mkoa wa Geita, Wizara ya Nishati na Madini, Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM) na Baraza la Taifa la Uhifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), Profesa Muhongo alisema maeneo ya awali yaliyopatikana kwa ajilli ya kuhifadhi magwangala hayo ni pamoja na Lwenge- Nyamikoma, Kasota B na Samina B yaliyopo mkoani Geita.

Aliagiza Ofisi ya Madini Mkoani Geita kutoa leseni za uchenjuaji madini mara moja kwa vikundi vyote vya wachimbaji madini ili waanze kazi mara moja ya uchenjuaji madini kwa kutumia magwangala hayo.

“Ninaagiza Ofisi ya Madini Mkoani Geita kutoa leseni za uchenjuaji madini kwa vikundi vilivyoundwa kupitia halmashauri mara moja bila vikwanzo vyovyote ili waanze na shughuli za uchenjuaji madini mara moja,’ alisema Profesa Muhongo. Akizungumzia suala la usafirishaji wa magwangala katika maeneo hayo Profesa Muhongo alisema ni jukumu la vikundi vilivyopewa magwangala hayo kusafirisha kutoka kwenye mgodi hadi kwenye maeneo yaliyoainishwa.
Mkuu wa Mkoa wa Geita, Meja Jenerali Mstaafu, Ezekiel Kyunga (mbele) akisoma taarifa ya utekelezaji wa mpango wa kubaini maeneo kwa ajili ya kuhifadhia magwangala mbele ya Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo na watendaji kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Baraza la Taifa la Uhifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) na Halmashauri ya Geita.

Aliongeza kuwa iwapo vikundi vitakosa uwezo wa kusafirisha magwangala hayo, halmashauri inaweza kufanya mazungumzo na Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM) kwa ajili ya gharama ya kusafirisha magwangala hayo.

Aidha katika kikao hicho Waziri Muhongo alikubaliana na uongozi wa Mgodi wa Dhahabu (GGM) kwa ajili ya kusafirisha tani 10 kwa kila eneo kwa kuanzia kama njia ya kuonesha nia ya kuwasaidia wachimbaji wadogo.

Profesa Muhongo alisema kuwa lengo la serikali ni kuhakikisha kuwa wachimbaji wadogo wa madini wananufaika na sekta ya madini kupitia shughuli za uchenjuaji madini na kuwataka kuomba ruzuku pindi zinapotangazwa.
Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (kulia) akifuatilia maelezo yaliyokuwa yanatolewa na Mkuu wa Mkoa wa Geita, Meja Jenerali Mstaafu, Ezekiel Kyunga (hayupo pichani) Katikati ni Kamishna Msaidizi wa Madini-Uchimbaji Mdogo, Julius Sarota.

Awali akiwasilisha taarifa ya mkoa wa Geita kuhusu utekelezaji wa mpango wa uainishaji wa maeneo ya kuhifadhia magwangala, mkuu wa mkoa huo Meja Jenerali Mstaafu Ezekiel Kyunga alisema kuwa suala la magwangala limekuwa la muda mrefu ambapo wananchi wa Geita wamekuwa wakihitaji magwangala hayo ili wafanye shughuli za uchenjuaji kwa lengo la kujipatia kipato.

Kyunga alisema kuwa ili kutekeleza azma hiyo ya kuwapatia wananchi magwangala, jitihada mbalimbali zimekuwa zikifanyika kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu kwa kushirikisha viongozi wa serikali, taasisi za kimazingira pamoja na wadau mbalimbali.

Alisema katika utekelezaji wa agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Joseph Pombe Magufuli alilolitoa Julai 31 mwaka huu la kuwapatia wananchi magwangala tayari mkoa umefanya hatua za awali kwa kutafuta maeneo tisa yatakayofaa kwa ajili ya uhifadhi wa magwangala.
Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo akisisitiza jambo katika kikao hicho.

Aliainisha maeneo yaliyopatikana ni pamoja na Magogo, Lwenge-Nyamikoma, Kasota A, Kasota B, Bugulula A, Bugulula B, Manga- Saragulwa, Mgusu, Samina A na Samina B.

Aliongeza kuwa maeneo yaliyopewa kipaumbele cha kwanza ni pamoja na Lwenge- Nyamikoma, Samina A, Manga-Saragulwa, Kasota B na Mgusu. Aliongeza maeneo yaliyopewa kipaumbele cha pili ni pamoja na Samina A, Samina B (Mpomvu), Bugulula A na Bugulula B.

“Kipaumbele cha tatu ni Magogo, pamoja na mapendekezo hayo bado tuliona maeneo mawili ya Manga- Saragulwa na Mgusu ambayo yanaweza kutumika kwa kuanzia kwa kuzingatia suala la usalama, idadi ya askari waliopo kulingana na changamoto ya uhalifu unaoweza kujitokeza na kufanya tathmini ya uendeshaji wa shughuli hiyo,” alisisitiza Kyunga.

Akielezea matokeo ya uwepo wa shughuli za magwangala mkoani Geita Kyunga alieleza kuwa ni pamoja na ongezeko la watu katika maeneo hayo na kuhitaji uimarishwaji wa ulinzi.
Sehemu ya watendaji kutoka Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM) wakifuatilia maelezo yaliyokuwa yanatolewa na Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (hayupo pichani).
Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (katikati) akizungumza na watendaji kutoka Mkoa wa Geita, Wizara ya Nishati na Madini, Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM) na Baraza la Taifa la Uhifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) (hawapo pichani) Kushoto ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Geita, Selestine Gesimba na kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Geita, Meja Jenerali Mstaafu, Ezekiel Kyunga
Sehemu ya watendaji kutoka Mkoa wa Geita, Wizara ya Nishati na Madini, Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM) na Baraza la Taifa la Uhifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) wakifuatilia maelezo yaliyokuwa yanatolewa na Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (hayupo pichani).

Tigo yatangaza punguzo bei ya tiketi, vifurushi vya bure Fiesta 2016

August 11, 2016
 Mratibu wa fiesta, Shafii Dauda  akiongea na waandishi jinsi ya  kulipia tiketi ya fiesta kupitia Tigo Pesa na katikati ni Meneja chapa wa Tigo, William Mpinga , Kulia ni na Mtaalam wa mitandao ya jamii wa Tigo, Samira Baamar.

Waandishi wa habari wakichukua matukio kwenye mkutano huo uliofanyika mapema  leo jijini Dar es salaam.


Dar es Salaam Agosti 9, 2016- Katika kuhakikisha kuwa kila Mtanzania ambaye anapenda kushirki katika tamasha la Fiesta 2016  mdhamini mkuu wa tukio hilo la aina yake Tigo Tanzania leo imetangaza  punguzo la asilimia kumi  kwa tiketi  itakayonunuliwa  kwa Tigo Pesa kwa msimu huu wa Fiesta.
Tofauti na matukio  yaliyotangulia, washiriki wote kutyoka mtandao wowote kwa tamasha la mwaka huu watakuwa na chaguo la kuzipata tiketi zao kupitia Tigo Pesa  bila tozo za ziada.
Tiketi hizo zitawawezesha washiriki kulifikia kwa urahisi tamasha hilo ambalo litaanza rasmi Agosti 20, 2016 jijini Mwanza. Bei kamili za tiketi zitatangazwa hivi karibuni.
Akizungumza katika mkutano wa waandishi wa habari  uliofanyika Tip Top Manzese, Meneja Chapa wa Tigo William Mpinga alisema, “Njia ya  kulipia tiketi  kupitia Tigo Pesa  lengo lake kubwa ni kuwapatia Watanzania  njia rahisi na ya kawaida  ya kupata tiketi zaoambayo ni ya kwanza na ya aina yake nchini Tanzania.”
Mpinga alibainisha kwamba  huduma hiyo mpya imepanda chati  kufuatia hivi karibuni kampuni hiyo ya simu  kuanzisha kampeni ya NitigoPesa ambapo mtu yeyote kutoka  mitandao mingine mikubwa nchini Tanzania  anaweza kutuma na kupokea pesa  kutoka kwa mteja wa TigoPesa.
Meneja chapa huyo  aliongeza kwamba ikiwa kama kampuni ya mtindo wa maisha ya kidijitali Tigo inawahakikishia  kuwa  kwa kununua  tiketi kupitia Tigo Pesa, wateja kutoka Tigo na mitandao mingine wataweza  kuzifurahia huduma za Tigo Pesa bila tozo zozote za ziada.
Mpinga alieleza ili  kununua tiketi  kwa Tigo Pesa wateja kutoka mtandao wowote  anatakiwa kupiga namba ya mfumo wa kifedha kwa njia ya simu (mfano: *150*01# kwa  Tigo),  chagua “Tuma Pesa” halafu chagua, “Mitandao mingine”, ikifuatiwa na, Tigo Pesa na hatua ya mwisho  ingiza namba: 0678 888 888.  Mbali na  punguzo la asilimia kumi, wateja wa Tigo ambao watanunua tiketi za Fiesta  kwa Tigo Pesa pia watapata  kifurushi cha zawadi cha thamani ya shilingi 20,000 ambacho kinajumuisha dakika 400, SMS 400 na MB 400 zitakazotumika ndani ya siku saba.
Aliendelea kusema, “Kwa wateja wa mitandao mingine  tiketi itakayonunuliwa kwa Tigo Pesa kutoka mitandao mingine  watapata kadi ya 4G ikiwa na dakika 60 SMS 60 na MB 60 papo hapo  pamoja na dakika nyingine 400, SMS 400 na MB 400 zitakazotumika ndani ya siku saba zikianza kutumika  ndani ya saa 24”.
Huku akiwakaribisha Watanzania wote kushiriki katika Tamasha hilio la Fiesta, Mpinga aliwashauri  washiriki kununua  tiketi zao  mapema ili kuepuka usumbufu  unaoweza kujitokeza katika dakika za mwisho.
 Tamasha la Tigo Fiesta 2016 linafanyika kwa ushirikiano kati ya Prime Time Promotions na Tigo Tanzania  ambaye ni mdhamini mkuu.

MAXMALIPO YAZINDUA MFUMO WA UWEKAJI SALIO KWENYE KADI ZA MABASI YA MWENDO HARAKA KUPITIA KWA MAWAKALA WA MAXMALIPO

August 11, 2016
 Mkuu wa kitengo cha biashara Kampuni ya Maxmalipo Bw.Deogratius Lazari  Akifafanua Jambo kwa Waandishi wa habari na Kushoto ni Mkuu wa uendeshaji Kampuni ya Maxmalipo Bw. Ahmed Lussasi


Mkurugenzi Uendeshaji wa kampuni ya Maxmalipo (kulia) Bw. Ahmed Lussasi Akielezea Jinsi kampuni ilivyo piga hatua katika teknolojia, Kushoto ni Msemaji wa kampuni ya Uendeshaji wa Mabasi ya mwendo haraka Bw. Deus Bugaywa .

Msemaji wa Kampuni ya Undeshaji wa mabasi ya Mwendo haraka Bw. Deus Bugaywa (Kushoto)  Akifafanua Jambo kwa wanahabari na Kulia ni Mkuu wa Uendeshaji wa kampuni ya Maxmalipo Bw.Ahmed Lussasi




Kuanzia sasa wasafiri wenye kadi maalumu za Usafiri (Dart card) wameongezewa njia mbadala za kuweka salio katika kadi zao za Usafiri kwa kuwatumia mawakala wa Maxmalipo. Mteja mwenye kadi hii ya usafiri anaweza kufika kwa Wakala yeyote wa Maxmalipo na kuweka salio kiasi chochote kwenye kadi yake

Akiongea kwenye uzinduzi huu afisa Mwendesgaji mkuu wa Maxmalipo Bw. Ahmed Lussasi Amesema “ Lengo kubwa la kampuni ya Maxcom Africa imekua ni kujenga na kutengeneza mifumo imara na madhubuti ambayo inalenga kurahisisha ukusanyaji wa mapato kwa njia ya kielektroniki pia kusimamia na kudhibiti mianya ya upotevu wa mapato kwa kutumia mifumo ya Kielektroniki. Bw. Ahmed ameendelea kuelezea kwamba  Tangu Mradi huu wa Mwendo kasi umeanza  kumekua na maboresho mbalimbali na mbinu za kitaalamu zinazopelekea kukua kwa makusanyo, kuepusha na kudhibiti upotevu wa Mapato na kuhakikisha kuna uwazi wa hali ya juu katika utoaji wa taarifa za makusanyo (Real time Revenue reporting)”

Naye Msemaji wa kampuni ya undeshaji wa Mabasi haya ya Mwendokasi Bw. Deus Bugaywa  Ameelezea kwa Ufupi mafanikio kampuni iliyo yapata kwa kutumia mifumo hii ya kielektroniki moja ikiwa ni uhakika wa mapato, ukuaji wa mapato pamoja na usalama wa fedha zao”. Deus ameongeza kwa kusema “ Naweza kuwadhihirishia kwa ushirikiano huu tulio nao na Maxmalipo katika mradi huu umeleta Mageuzi makubwa katika sekta ya usafirishaji nchini kwetu barani Africa na Duniani kwa ujumla; Huu ndio mfumo pekee unaowezesha watu kuweka salio katika kadi zao kupitia MItandao ya simu na ndio mfumo Pekee uliokua kiteknolojia ndani ya muda mfupi Zaidi, na leo salio na ticket vinaweza kupatikana kwa mawakala waliopo hata mitaani (hawa wa Maxmalipo). Ni pongezi kwa Maxmalipo kama kampuni ya kitanzania kwa kufanya haya, lakini Zaidi Tutoe shukrani zetu kwa serikali kwa kuunga mkono Jitihada hizi katika sekta nzima ya usafiri.
Naye Mkuu wa Kitengo cha biashara katika kampuni ya Maxmalipo – Bw. Deogratius Lazari , amwewaambia wana habari kwamba Maxcom Africa ina Zaidi ya mawakala 15000 nchi nzima ambao wamewezeshwa kutoa huduma hii kwa watumiaji wa kadi hizi za mwendo haraka. Bw Deogratius ameainisha pia kwamba Mawakala hawa wa Maxmalipo wapo jirani na makazi ya watu hvyo wasafiri wanaweza kujipatia huduma hii kabla ya kufika kwnye vituo vya mabasi ya mwendo haraka.
Kufuatia Uzinduzi huu kampuni ya Maxcom Africa inatarajia kupungua kwa foleni za abiria kwnye vituo vya mabasi ya mwendo hasa wale wanaokua wakihitaji kuweka salio kwnye kadi zao pia wanataraji kuongezeka kwa Ajira katika sekta isiyo rasmi kwa watanzania wengi kuchamgamkia Fursa ya kuwa mawakala wa Maxmalipo ambayo itawaongezea kipato.

Maxcom Africa imekua ni Moja ya Kampuni za Kitanzania iliyofanikiwa sana katika uwekaji wa mifumo madhubuti ya ukusanyaji na usimamizi wa mapato hapa Tanzania hasa katika miradi mikubwa ikiwamo huu wa mabasi ya Mwendo Kasi, TRA, Vivuko, Mahospitali (Moi)  na kwenye Kodi za halmashauri.

photo Best Regards Krantz Mwantepele| Managing Director KONCEPT | Mikocheni B, House No 58. Opp Clouds Media. Dar es Salaam, Tanzania | M: + 255 624053989 / +255 712579102 E: Krantz.charles@koncept.co.tz Blog: www.mwanaharakatimzalendo.blogspot.com W: www.koncept.co.tz

RAIS DKT MAGUFULI AHUTUBIA MAELFU YA WANANCHI WA JIJI LA MWANZA UWANJA WA FURAHISHA LEO

August 11, 2016


 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akihutubia maelfu ya wananchi wa mkoa wa Mwanza na maeneo ya kanda ya ziwa katika mkutano wa hadhara katika uwanja wa Furahisha eneo la Kirumba jijini humo. PICHA NA IKULU


SHULE ZA FEZA HAZITAFUNGWA

August 11, 2016

                          Na Dotto Mwaibale

UONGOZI wa  Shule za Feza nchini umeibuka na kukanusha taarifa zilizozagaa kwenye mitandao ya kijamii,  kuwa wao  hawana uhusiano na  Fethullah Gulen wala serikali ya Uturuki  kwa vile   hawajawahi kupokea misaada toka pande hizo mbili za uendeshaji na kuwa shule hizo hazitafungwa.

Kauli hiyo imetolewa baada ya hivi karibuni kuenea kwa uvumi kuwa shule za Feza  zipo hatarini kufungwa kwa madai kuwa  mmiliki wake ni yule aliyejihusisha na jaribio la kuipindua serikani nchini Uturuki.

Mwenyekiti wa Bodi wa Shule hizo, Habibu Miradji aliyasema hayo alipokuwa akizungumza na wanahabari Kawe jijini Dar es Salaam leo asubuhi.

Alisema Watanzania wanapaswa kufahamu kuwa Shule za Feza ni kama asasi  zingine zilizosajiliwa kishera na serikali, hivyo ni mali ya watanzania.

“Shule za Feza zitabaki kuwa kiwanda  cha kuzalisha wazalendo wa kitanzania  na raia bora wa duniani, hivyo wazazi wanapaswa kuondoa hofu,” alisema.

Alisema toka mwaka 1995 shule hiyo imepata mafanikio ya kujenga shule za awali tatu, shule za msingi mbili, sekondari tatu na shule ya kimataifa moja.

Aliongeza kuwa  huo ni uwekezaji  wenye mchango katika kukuza pato la taifa, kutoka awamu ya pili, tatu, nne hadi awamu ya tano chini ya Rais John Magufuli.
\Alisema shule ya Feza ni hazina kwa Tanzania kwani shule zake zimekuwa zikishika nafasi ya 10 bora toka mwaka 2004 hadi leo.

Alisema  wanatoa  wito kwa wazazi  kuwasiliana na uongozi wa shule hiyo  kujua kinachoendelea kwenye shule husika kwa manufaa ya wanafunzi wetu na taifa bila kusikiliza uvumi huo unaoenezwa na watu wasiopenda maendeleo ya shule hizo.

(Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)

HUU UHARIBIFU WA VIFAA VYA KUHIFADHIA TAKA KATIKA VITUO VYA MABASI YA MWENDOKASI VIPI?

August 11, 2016
Ikiwa ni Takribani miezi michache kupita tangia mabasi ya mwendo kasi yaanze kufanya kazi kwa ufanisi mzuri, kumekuwa na mambo kadha wa kadha yakiendelea ikiwa ni pamoja na kuharibika kwa miundombinu ya vituo hivyo vya mabasi hayo.

Hili limeonekana bila chenga Morogoro Road ambapo kipande cha kutokea Jangwani mpaka Manzese kikionesha wazi  vifaa vya kuhifadhia taka vimeharibika, huku vingine vikionekana kuchomolewa, kupinda, na kulegea. 

 Swali la kujiuliza hapa ni kwamba kwa jinsi miundombinu hii ilivyo kaa  ni ngumu sana hata mtu kugonga kwa mguu sasa inakuwaje inaharibika kiasi hiki?
Hapa upande wa kulia ukionekana kuwa kifaa cha kuhifadhia taka kilisha chomolewa na kubakiza mfuniko tuu na papo hivi kwa zaidi ya mwezi sasa.
Hapa Kifaa cha kuhifadhia taka taka kikiwa kimepinda haijulikani kiligongwa au kuna watu walikuwa wanataka chomoa.
Hiki kikiwa kimelegea kabisa amambapo muda wowote litachomoka
Hapa mfuniko ndio ulisha potea tena
Hili nalo tayari linaelekea kudondoshwa chini
Hii hapa ndio funga kazi kabisa yani wamesha chomoa muundo mbinu wote wa kushoto 

Picha na Fredy Njeje
Regards Tone Multimedia Company Limited Plot No.223/225 Block 46, Umoja Street Kijitonyama P.O Box 32529 Dar es salaam Tanzania Tel +255 22 2772919 Fax +255 22 2772892 E-Mail blogszamikoa@live.com Facebook: www.facebook.com/blogszamikoa Web: www.blogszamikoa.com
Vijana nchini wapewa elimu kuhusu kujihusisha na shughuli za maendeleo

Vijana nchini wapewa elimu kuhusu kujihusisha na shughuli za maendeleo

August 11, 2016


Kuelekea kilele cha siku ya vijana duniani, vijana mbalimbali nchini wamekutanishwa kwa pamoja na kupewa elimu jinsi wanavyoweza kukabiliana na changamoto mbalimbali za maisha pamoja na kukamilisha Mpango wa Maendeleo Endelevu (SDGs).

Akizungumza katika kongamano hilo mgeni rasmi ambaye ni Mwakilishi Msaidizi wa Shirika la Mfuko wa Idadi ya Watu la Umoja wa Mataifa (UNFPA), Christine Mwanukuzi-Kwayu, aliwataka vijana kushiriki katika shughuli za maendeleo ili kusaidia kubadilisha maisha yao binafsi na kwa taifa.
Mgeni rsmi katika kongamano hilo Mwakilishi Msaidizi wa Shirika la Mfuko wa Idadi ya Watu la Umoja wa Mataifa (UNFPA), Christine Mwanukuzi-Kwayu akizungumza na vijana.

Alisema vijana wengi wamekuwa hawajihusishi na mambo ya maendeleo na hivyo ni wasaa sasa na wao waanze kujihusisha ili waweze kuchangia kuleta maendeleo katika taifa kwani hata takwimu kwa sasa zinaonyesha vijana wanashiriki kwa kiasi kidogo kutokana na wengi wao kutokuwa na ujuzi.

"Vijana hivi mnajua kama nyie ndiyo mnatarajiwa kuongoza taifa lakini bado mmelala hata katika uchunguzi uliofanyika unaonyesha vijana asilimia nne ndiyo wanajihusisha kwa karibu na shughuli za maendeleo kwa nchi yetu ila wengi mnakuwa hmajui," alisema Mwanukuzi-Kwayu.

Nae Meneja Miradi wa Shirika la Restless Development Bw. Oscar Kimaro amesema kuwa matatizo wanayoyapata vijana duniani yanatokana na kutokua na ushirikishwaji wa vijana katika masuala mbalimbali ya kimaendeleo katika nchi.
Meneja Miradi wa Shirika la Restless Development Bw. Oscar Kimaro akiwapa vijana njia za kupata mafanikio na kuwaeleza mambo ambayo yanachangia wao kushindwa kufikia malengo.

“Changamoto zinazomkabili kijana nchini Tanzania ndio hizo hizo zinazoweza kumkabili kijana nchi nyingine, lakini haya yote hutokana na kutoshirikishwa kwa vijana katika sekta mbalimbali za uzaliashji na za kimaendeleo chini,” alisema Oscar

Na Hashimu Ibrahim
Mtendaji Mkuu wa Chama cha Vijana wa Shirika la Umoja wa Mataifa (YUNA), Arafat Bakar akitoa burudani kwa vijana waliohudhuria kongamano hilo.
Baadhi ya vijana waliohudhuria kongamano hilo.

Washiriki wakiwa katika picha ya pamoja.

WADHAMINI WARUDISHA HADHI YA SHINDANO LA MISS TANGA 2016

August 11, 2016
 Miss Tanga 2016, Eligiva Mwasha akiwapungia mikono wananchi waliojitokeza kushuhudia shindano hilo mara baada ya kutangazwa kuwa mshindi
 Miss Tanga 2016, Eligiva Mwasha akiwapungia mikono watazamaji waliojitokeza akiwa na mshindi wa pili na tatu katika Shindano hilo ambalo liliandaliwa na Radio Tanga Kunani (TK) na Hotel ya Tanga Beach Resort.
Warembo walioingia tano bora wakiwa jukwaani

Kamati ya Miss Tanzania nao walikuwepo wakifuatilia shindano hilo ambalo lilifanyika kwenye ukumbi wa Hotel ya Tanga Beach Resort mjini Tanga.

 Mbunge wa Jimbo la Tanga (CUF) Mussa Mbaruku akizungu mza wakati wa shindano hilo
Msanii Nevy Kenzo akitumbuiza wakati wa shindano la kumtafuta mlimbwende wa mkoa wa Tanga (Miss Tanga 2016)lililofanyika hivi karibuni kwenye hotel ya Tanga Beach Resort
WAKATI shindano la kumsaka malkia wa Mkoa wa Tanga (Miss Tanga 2016)likifanyika mwishoni mwa wiki na hatimaye mrembo Eligiva Mwasha kuibuka na ushindi kwenye kinyang’anyiro hicho dhidi ya washiriki wengine 10.
Shindano hilo ambalo lilisimama kwa muda baada ya serikali
kulisimamisha lile la Taifa msimu huu lilionekana kuwa na msisimuko wa hali ya juu kuanzia wapenzi,wadau na washiriki iliyochangiwa na waratibu wa shindano hilo Radio ya Tanga Kunani FM (TK) wakishirikiana na Hotel ya Tanga Beach Resort.

Ushindani wa washiriki hao ulianza kuonekana tokea wakati warembo hao wakiwa kwenye kambi yao ambayo ilifanyika kwenye hotel hiyo ambapo kila mmoja alionekana kuwa na shauku kubwa ya kutaka kuondoka na taji hilo.

Hali iliendelea kuwa ya mvutano zaidi baada ya baadhi ya washiriki
kuaga mashindano hayo na kutoa fursa yaw engine kuingia nafasi ya tano bora katika kinyanganyiro hicho ambacho kilihudhuriwa na wapenzi wengi kuliko kawaida.

Kitendo hicho kinaonekana kinawezesha kurudisha hamasa na heshima ya shindano hilo ambalo hufanyika kila mwaka mkoani hapa lakini pia kuhamasisha hasa vijana kujitokeza kwa wingi kushiriki msimu ujao.

Katika shindano hilo nafasi ya pili ilichukuliwa na Aisha Ally huku
nafasi ya tatu ikitwaliwa na Rukaiya Hassani katika shindano hilo
ambalo lilikuwa na ushindani mkubwa kutokana na kusheheni warembo wakali.

Halikadhalika nafasi ya mrembo kwenye kipaji katika shindano hilo
ilinyakuliwa na Edna Chisabo ambapo kinyang’anyiro hicho kilifanyika siku moja kabla ya onyesho la kumsaka mrembo wa mkoa huu  kwenye ukumbi wa Tanga City Lounge uliopo mjini hapa.

Licha ya kufanyika shindano hilo lakini yapo mambo ambayo kimsingi yameweza kuleta msisimuko na kulifanya kuonekana kuwa na ubora wa hali ya juu.

Mambo hayo ndio yamechangia kwa asilimia kubwa kupelekea shindano hilo kuwa na mvuto mkubwa kuliko mashindano mengine ambaye yalikwisha kufanyika mkoani hapa lakini pia uwepo wa  watazamaji wengi.

La kwanza ni eneo ambapo onyesho hilo limefanyika,moja kati ya mambo ambayo yalichangia kuonekana kuwa na mvuta mkubwa ilitokana na shindano hilo msimu huu kufanyika kwenye Hotel ya Tanga Beach Resort.

Tunasema hivyo kwa sababu kila mtu anapokwenda kuangalia burudani ya aina yoyote lazima aangalia ulinzi na uimara wa eneo husika hasa ukizingatia wapo baadhi yao huenda na vyombo vyao vya usafiri.

Kama ujuavyo ulinzi wa mahali husika ndio huwafanya watu kwenda kupata burudani lakini pia ni eneo tulivu ambalowatu wanaweza kufanya mambo yao kila kupata usumbufu wa aina yoyote.

Jambo hilo limesababisha baadhi wa watu kuacha kwenda kwenye maeneo yaliyopo karibu nao na kwenda maeneo mengine ya mbali kwa ajili yakusaka utulivu lakini pia ulinzi.

Jambo jingine ambalo lilisababisha onyesho hilo kuwa bora ni uwepo wa warembo makini na wenye muonekana bomba na hivyo kupelekea wapenzi na wadau wao kujitokeza kwa wingi kushuhudia mtanange huo ambao ulikuwa wa aina yake.

Kilicholifanya shindano hilo kuendelea kuvutia wapenzi na mashabiki ambao walijitokeza  ni wasanii ambao walikuwa wakitumbuiza kabla ya kuanza.

Wasanii wanaounda kundi la Nevy Kenzo wazee wa Kamati Chini ilikuwa ni kichocheo kikubwa cha umati mkubwa wa wadau wa tasnia ya urembo na burudani kujitokeza kwa wingi kushuhudia shindano .

Nevy Kenzo ambao walipanda jukwaani kutumbuiza walisababisha ukumbi mzima kulipuka kwa shangwe na nderemo huku baadhi yao wakiimba nyimbo zao ikionyesha namna wanavyokubalika.

Nevy Kenzo wakati akiimba ilifikia wakati mpaka wapenzi na mashabiki wa tasnia ya urembo waliviona viti vyao vya moto na kulazimika kupanda jukwaani kucheza sambamba na wasanii hao.

Haikuishia hapo lakini wasanii ambao walipanda jukwaani kabla ya Nevy Kenzo kutumbuiza wa Kundi la Wazenji Classic lenye makazi yake mjini Tanga walikuwa na moto na kusababisha shangwe  kila mahali.

Shangwe hizo zinaonyesha namna kundi hilo lilivyoweza kujizolea
umaarufu mkubwa ndani na nje ya Tanga hasa kwa kipindi kifupi kutokana na aina ya mziki ambao wanaufanya staili ya mduara na bongo fleva.

Sababu kubwa ya kuona kundi hilo kuonekana litakuwa hatari ni namna wanayoweza kulitawala jukwaa wanapokuwa stejini na kuonekana kuinua mara kwa mara wapenzi na mashabiki wao

Suala jingine ambalo lilikuwa kivutio kikubwa ni namna warembo
walivyokuwa wakipanda jukwaani na kuanza kujitambulisha na kujielezea kwa watazamaji.

Hali hiyo ilisababisha wakati mwengine baadhi ya warembo kupanda jukwaani kwa madoido makubwa kwa lengo la kuonyesha umahiri wao ili kuwashawisha majaji kuwapa alama nzuri.

Mbunge wa Jimbo la Tanga atinga Miss Tanga.
 

Kitendo cha Mbunge wa Jimbo la Tanga (CUF)Mussa Mbaruku kuhudhuria shindano la kumsaka mlimbwende wa mkoa wa Tanga mwaka huu kilionyesha namna alivyokuwa kiongozi mpenda michezo na kuithamini.

Mbunge huyo ambaye alikuwa kwenye shughuli zake za kikazi lakini alilazimika kuungana na wakazi wa jimbo lake kumshuhudia mrembo ambaye anapatikana.

Akizungumza mara kabla ya kutangaza mshindi wa Taji la Miss Tanga 2016,Mbunge Mussa alisema tasnia ya urembo imekuwa ikiwapa vijana maisha mazuri lakini pia imekuwa ni daraja la wao kupata mafanikio

Alisema lazima watanzania ikiwemo wazazi kubadilika na kuondokana na dhana ya kuwa  ya kuwa urembo ni suala la uhuni kwani imekuwa ikisaidia vijana wengi kupata maendeleo.

  "Ndugu zangu lazima tubadilike na kuishi kutokana na utandawazi
uliopo ile dhana ya kuwa urembo ni uhuni mimi nadhani imepitwa na wakati na uhuni mtu anaweza kuwa nao hata asiposhiriki mashindano hayo hivyo wazazi na walezi ruhusuni watoto wenu washiri kwenye mashindano haya "Alisema.

Mussa alisema kuwa anaamini washindi wa shindano hilo wataweza
kuuwakilisha vema mkoa wa Tanga kwenye mashindano ya Kitaifa na kuweza kushinda kama walivyofanya kwenye onyesho hilo.

  “Ninaimani kubwa na washindi ambao wamepatikana kwenye shindano hilo wanaweza kuwa chachu ya mabadiliko kwenye tasnia ya urembo mkoa huu kwani wanaweza hata kuleta taji la Miss Tanzania msimu huu “Alisema.

"Neno la Mshindi wa taji la Miss Tanga 2016 Eligiva Mwasha" Alisema kuwa kwanza anawashukuru wakazi wa Mkoa wa Tanga  kwa ujumla kwa sapoti yao walionyesha katika  fainali za miss tanga 2016 na yeye kupata fursa ya  kunyakua taji hilo

Licha ya kuibuka na ushindi lakini niwaombe niombea kwani kwa sasa safari aliokua nayo bado kubwa sana kwani anamtihani  wakwenda kuiwakilisha Tanga katika fainali za Miss Kanda  na  badae kulekea Katika fainali za miss Tanzania baadae mwaka huu.