Redd's Miss Tanga 2013 Lulu Mbonela.

June 23, 2013
Redd's Miss Tanga 2013,Lulu Mbonela akiwapungia mikono wannchi waliojitokeza kushuhudia shindano hilo mara baada ya kutangazwa mshindi jana usiku kulia kwake ni mshindi wa tatu Like Abduraham na mshindi wa tatu Hawa Twaybu shindano hilo lilifanyika kwenye uwanja wa Mkwakwani mjini hapa.

Nasi pia kucheza tunaweza

June 23, 2013
WAREMBO waliokuwa wakiwania taji la Redd's Miss Tanga 2013 wakitoa burudani katika onyesho hilo ambalo lilifanyika jana kwenye uwanja wa Mkwakwani mjini.

LULU Mbonela Redd's Miss Tanga 2013

June 23, 2013

Na Mwandishi Wetu,Tanga.
LULU Mbonela jana alivikwa rasmi taji la   Redds Miss Tanga 2013 baada ya kushika nafasi ya kwanza katika shindano la kumtafuta mrembo wa mkoa wa Tanga lililofanyika Uwanja wa Mkwakwani Jijini hapa.

Aliyeshinda nafasi ya pili katika mchuano huo uliohudhuriwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi Omari Chambo na Mkuu wa Wilaya ya Tanga,Halima Dendego ni Like Kipenga huku nafasi ya tatu ikienda kwa Hawa Ramadhani,Hawa Twayb aliyekuwa mshindi wa nne wa tano akiwa Judith Molel.

Washindi hao wamejipatia tiketi ya kushiriki shindano la kumtafuta
mrembo wa mikoa ya Kanda ya Kaskazini Taji la Miss Talent 2013 lilikwenda kwa Azina Mbaga aliyewashinda washiriki  wenzie 12 kwa ucezaji wa ngoma za asili ya Kiafrika.

Katika shindano hilo mshindi wa kwanza alizawadiwa kitita cha sh.500, 000 mshindi wa pili 300,000, mshindi wa tatu 250,000 huku mshindi wanne na tano kila mmoja akipata kitita cha sh.200,000 kila mmoja.


 Aidha pia washiriki wengine waliokuwa wanawania taji hilo  kila mmoja alizawadiwa kitita cha sh.100,000kila mmoja kutoka kwa muaandaaji wa mashindano hayo

Jopo la majaji katika shindano hilo  lilohudhuriwa na mashabiki  wengi lililongozwa na Boniface Shelufumo huku wasani walionogesha ni pamoja na Beatrice Nabisha,Fabby Dady,Dr John ,Tunda Man na Afua Suleyman huku wasema chochote  wakiwa Sakina Lyoka  na fred Mwanjala.

 

Katika shindano hilo,Mkuu wa Wilaya  ya Tanga,Dendego aliweza
kukabidhiwa cheti cha shukrani kwa kumwezesha mwandaaji  Asha
Kigundula kufanikisha onyesho hilo.

Wengine waliopata vyeti ni kampuni ya Al Hayat,CXC Africa,Redds Original,Mkwabi Enterprises,Clauds Media,Jambo leoLavida loca na Michuzi Media Group na Assenga Oscar.blogspot.com

                     MWISHO