PATI LA UBINGWA WA MTANI JEMBE SIMBA SC JANA...ILIKUWA RAHA BWAAAA!

December 22, 2013

Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba SC, Zacharia Hans Poppe katikati akiwa ameinua Kombe la Mtani Jembe Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam baada ya kuifunga Yanga SC mabao 3-1.

Wachezaji wa Simba na Kombe na Medali zao
Rais wa TFF, Jamal Malinzi akimkumbatia kipa wa Simba SC, Ivo Mapunda
Malinzi akimvisha Medali Ramadhai SIngano 'Messi'
Malinzi akimpongeza Hans Poppe
Waziri wa Sheria na Katiba, Mathias Chikawe akimkabidhi Kaimu Makamu Mwenyekiti wa Simba SC, Joseph Itang'are 'Kinesi' mfano wa hundi ya SH. Milioni 1
Meneja wa Yanga, Hafidh Saleh akipokea hundi ya Sh. Milioni 98.9
Malinzi akimkabidhi Nahodha wa Yanga, Jerry Tegete Kombe dogo
Nahodha wa Simba SC, Haruna Shamte akipokea Kombe
Jonas Mkude akivalishwa Medali
Amri Kiemba akivalishwa Medali
Hans Poppe na Ivo
IMEWEKWA DESEMBA 23 SAA 2:13 USIKU.

DC GAMBO AFUNGA MAFUNZO YA MGAMBO KATA YA KWASHEMSHI WILAYANI KOROGWE

December 22, 2013
MKUU WA WILAYA YA KOROGWE,MRISHO GAMBO (KATIKATI MWENYE SHUTI NYEUSI )AKIWA MEZA KUU AKIFUATILIA KWA UMAKINI GWARIDE LA MGAMBO HAO KABLA YA KULIKAGUA LEO.

ASKARI MGAMBO WAKITOA SALAMU.


MKUU WA WILAYA YA KOROGWE,MRISHO GAMBO AKILIKAGUA GWARIDR LA MGAMBO HAO KABLA YA KUFUNGA MAFUNZO YA MGAMBO WILAYANI HUMO LEO.


 WANANCHI WA MGILA KATA YA KWESHEMSHI WAKIFUATILIA MATUKIO YA UFUNGAJI WA MAFUNZO HAYO LEO.

PICHA ZOTE KWA HISANI YA MKUU WA WILAYA YA KOROGWE,MRISHO GAMBO.

IMEWEKWA DESEMA 23 SAA 01:53 USIKU.

DR SHEIN, SADIFAH WAFUNGUA MATEMBEZI YA VIJANA KUADHIMISHA MIAKA 50 YA MAPINDUZI.

December 22, 2013
Imewekwa Sunday, December 22, 2013 Saa 12:51 Usiku.
Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Dr Shein,Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Vijana (UVCCM) Ndg Sadifah Juma wakiongoza matembezi ya Vijana.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein amesema, katika kuyaenzi na kuyaendeleza Mapinduzi, vijana hawana budi kuzingatia mafunzo ya msingi ya mwenendo wa waasisi wa Mapinduzi hayo.
Dk. Shein amesema hayo leo wakati alipokuwa akizungumza katika ufunguzi wa matembezi ya Umoja wa Vijana wa CCM kuadhimisha miaka 50 ya Mapinduzi ya mwaka 1964 huko Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba.
 ZITTO KABWE AFANYA MAKUBWA KASULU, KIGOMA ..... AITEKA NA KUACHA HISTORIA ..... TAZAMA KILA HATUA ILIYOJILI ...

ZITTO KABWE AFANYA MAKUBWA KASULU, KIGOMA ..... AITEKA NA KUACHA HISTORIA ..... TAZAMA KILA HATUA ILIYOJILI ...

December 22, 2013
Imewekwa Sunday, December 22, 2013 Saa 10:15 Usiku.


Mh.Zitto Kabwe akiwashukulu sana Wanakasulu kwa namna walivyojitokeza kwenye mapokezi hapa kasulu

Ni maelfu ya Wananchi wapo kwenye maandamano ya kumpokea Mbunge wa Kigoma Kaskazini Mh.Zitto kabwe.

Picha inazungumza wazi namna Msafara ulivyomkubwa sana na umejaa vijana,akina mama na wazee pamoja na watoto wanaotoa sapoti ya kutosha kwa MH.Zitto Kabwe

 
Maduka Yamefunga watu wote wanaelekea eneo la Mkutano,Hii ni wazi Zitto ni mtu wa watu,Ni mbunge anayekubalika Kigoma na Tanzania

UZINDUZI WA RIPOTI YA UWEZO

December 22, 2013
 Msanii Mrisho Mpoto akielezea kupitia mashairi
 Mama Zaida Mgalla akitoa ufafanuzi kwa ripota wa Uwezo TV Bi. Melania Mhagama
 Mgeni Rasmi akionyesha ripoti baada ya kuzindua.

Wakati ambapo asilimia 100 ya watoto wa Darasa la 3 na kuendelea wanapaswa kuweza kusoma na kufanya hesabu za kiwango fulani, matokeo ya Uwezo yanaonyesha kwamba ni wachache tu ndiyo wanaoweza kufanya hivyo.

Katika Darasa la 3, mmoja kati ya watoto wanne anaweza kusoma Kiswahili kwa kiwango sahihi. Shule za binafsi zinafanya vizuri zaidi kidogo kulinganisha na zile za Serikali, ambapo asilimia 61 ya watoto walio na umri chini ya miaka 9 hawawezi kusoma Kiswahili na kufanya Hesabu za Kuzidisha kulinganisha na asilimia 85 ya wenzao walio katika shule za Serikali.

BAADA YA KUPIGWA BAO 1-0 NA SIMBA JANA,MWENYEKITI WA YANGA YUSUPH MANJI AMBEBA MGOGONI KASEJA

December 22, 2013

IMEWEKWA DESEMBA 22.

 Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam

MWENYEKITI wa Yanga, Yusuph Manji, amesema kwamba klabu yao haijamsajili kipa Juma Kaseja ili aweze kuifunga timu ya Simba, badala yake wametaka kuboresha kikosi chao katika michuano ya Kimataifa, ikiwamo ligi ya Mabingwa Afrika.
Mwenyekiti wa Yanga, Yusuph Manji, pichani.
Jana katika mechi yao ya bonanza inayojulikana kama Nani Mtani Jembe, ilimalizika kwa Simba kuwafunga Yanga bao 3-1 na kuwasononesha mashabiki wa jangwani walioamini kuwa kikosi chao ni imara dhidi ya Simba.

Akizungumza leo asubuhi Makao Makuu ya Yanga, Manji alisema kuwa wanaoamini Yanga inastahili kuifunga Simba kwasababu yupo Kaseja langoni hao wanajidanganya, maana si lengo lao.

Alisema Yanga pamoja na benchi lote la ufundi linaamini kwa kuboresha kikosi chao kwa kuwa na wachezaji wazuri ni safari nzuri ya kutafuta heshima Barani Afrika.

“Mpira una matokeo ya kufungwa na kutoka sare au kushinda, hivyo wenzetu Simba jana walituzidi lakini sio sababu ya kushindwa kuisapoti timu yetu katika michezo yake.

"Mimi jana niliinuka kuwahamasisha mashabiki wote tuendelee kuiunga mkono, hivyo yasitokee malalamiko yoyote au wale wanaotaka jamii ielewe kuwa Kaseja si kipa mzuri au alipaswa kukaa langoni na kuisaidia Yanga iibuke na ushindi dhidi ya Simba,” alisema Manji.

Aidha Manji alizungumzia mipango kabambe ya kuhakikisha kuwa klabu yao inafanya vyema katika michuano ya Kimatataifa itakayoanza mapema mwakani.

WILAYA YA HANDENI YAFURAHIA UTAMADUNI KUENZIWA.

December 22, 2013

Na Kambi Mbwana, Aliyekuwa Handeni

IMEWEKWA DESEMBA 22.
 AFISA Utamaduni wilayani Handeni, mkoani Tanga, Godfray Munga, amesema kwamba kufanyika kwa Tamasha la Utamaduni wilayani humo kumechangia kwa kiasi kikubwa kuitangaza wilaya yao.

Meneja wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii NSSF Mkoa wa Tanga, Frank Maduga, akiperuzi katika gazeti huku akiwa ni miongoni mwa wadau waliohudhuria tamasha la Handeni Kwetu lililofanyika Jumamosi ya wiki iliyopita, wilayani Handeni, mkoani Tanga.
Tamasha hilo lilifanyika Jumamosi ya Desemba 14 mwaka huu, huku likishirikisha wadau mbalimbali sanjari na viongozi wa serikali, ikiwamo ofisi ya Mkuu wa Wilaya Muhingo Rweyemamu.
Akizungumza mapema wiki hii, Munga alisema akiwa kama Afisa Utamaduni, amefurahi kuona eneo lake la kazi linakusanya watu wengi kwa ajili ya kuenzi jitihada za maendeleo kwa kupitia sekta ya utamaduni.
“Hili ni jambo ambalo limenifanya nione faraja sana katika kuhakikisha kuwa utamaduni wa Mtanzania unaenziwa hususan kwa wakazi na wananchi wa Handeni.
“Naamini mambo yatazidi kuwa mazuri katika siku zijazo kulifanya tamasha lifike mbali zaidi kwa kushirikisha wasanii na wadau mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi,” alisema.
Katika Tamasha hilo, mgeni rasmi alikuwa DC Rweyemamu, ambapo alishuhudia umati wa watu ukihudhuria kwa mara ya kwanza na kulifanya kwa mafanikio makubwa.

HAJI JUMA KUZICHAPA NA MZUNGU WA ZANZIBAR PAMBANO LA KUWANIA UBINGWA WA TANZANIA (TPBO)

December 22, 2013
Na Oscar Assenga,Tanga.
BONDIA Haji Juma wa Tanga anatarajiwa kupanda ulingoni kuzichapa na Mohamed Mzungu wa Zanzibar katika pambano la kuwania Ubingwa wa Tanzania (TPBO) kg 52 superfly la raundi 10 litakaofanyika Desemba 25 mwaka huu kwenye uwanja wa Tangamano jijini Tanga.
Mratibu wa Pambano hilo, Promota Ally Mwazoa alisema pambano hilo linatarajiwa kuwa la aina yake kutokana maandalizi yaliyofanywa na uwezo walionao mabondia hao.
Mwazoa aliyataja mapambano ya utangulizi kuwa ni bondia Rajabu Mahoja na Jumanne Mohamed wote kutoka mkoani Tanga wataonyeshana kazi pambano la raundi 10 lenye uzito wa kg 57 feith weight.
Licha ya kuwepo pambano hilo mabondia wengine watakaozichapa ni Hamisi Mwakinyo wa Tanga atapambana na Said Mundi litakalokuwa la uzito wa kg 59 super feather raundi 6 huku Saimon Zabron naye atapigana na Athumani Boxers pambalo litakalo kuwa na uzito wa kg 61 Light weight raundi sita.
Mratibu huyo alisema pambalo lengine litakalo hitimisha raundi sita ni bondia J.J Ngotiko wa Tanga ambaye atapanda ulingoni kuzichapa na Zuberi Kitandula litakalokuwa la raundi sita super bantam.
Aliyataja mapambano ya mwisho siku hiyo yatakuwa na raundi nne nne ambapo bondia Jacob Maganga atazichapa na Mohamed Kidari pambano lenye uzito wa kg 65 light walter raundi nne wakati Juma Mustapha atapambana na Selemani Hamza litakalokuwa la raundi nne lenye uzito wa kg 55 super bantam.
Mratibu huyo alisema siku ya mapambano hayo,mgeni rasmi anatarajiwa kuwa msanii nguli wa filamu hapa nchini King Majuto.

*EDWARD LOWASSA AFUNGUA TAMASHA LA MADEREVA WA BODABODA JIJINI DAR

December 22, 2013
 Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa akiwapungia mkono kuwaaga madereva wa  bodaboda  baada ya kumaliza kufungua tamasha lao lililofanyika kwenye Viwanja vya Leaders club Kinondoni, jijini Dar es Salaam jana. 
 Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa, akipokea maandamano ya madereva wa Bodaboda kwenye Viwanja w=vya Leaders Cluc jana.