BALOZI NCHIMBI AHUTUBIA WANANCHI NA KUSIKILIZA KERO ZAO BABATI MJINI

June 02, 2024

 




Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dk Emmanuel John Nchimbi, akihutubia wananchi na kusikiliza kero zao mbalimbali, wakati na baada ya mkutano wa hadhara, uliofanyika katika Uwanja wa Stendi ya (zamani) Babati Mjini, Jumamosi, Juni 1, 2024, ambapo alihitimisha ziara yake ya siku mbili mkoani humo.






RAIS SAMIA ASHUHUDIA UTIAJI SAINI MIKATABA BAINA YA TANZANIA NA JAMHURI YA KOREA

June 02, 2024

 


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Korea Mhe. Yoon Suk Yeol wakati wakishuhudia Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt. Ashatu Kijaji pamoja na Waziri wa Biashara wa Korea Inkyo Cheong wakisaini Tamko la Pamoja kuhusu Uanzishwaji wa Majadiliano juu ya Mkataba wa Ushirikiano Kiuchumi. Hafla ya utiaji saini imefanyika katika Ikulu nchini humo tarehe 02 Juni, 2024.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan pamoja na Mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Korea Mhe. Yoon Suk Yeol wameshuhudia utiaji saini Mkataba (1) Hati za Makubaliano (2) na Tamko la Pamoja la kuanzisha Mkataba wa Ushirikiano Kiuchumi (1) kwenye hafla iliyofanyika Ikulu nchini humo tarehe 02 Juni, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Korea Mhe. Yoon Suk Yeol wakati wakishuhudia Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. January Makamba pamoja na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Uchumi na Fedha (Jamhuri ya Korea) Choi Sang Mok wakisaini Mkataba wa Ushirikiano kati ya Tanzania na Korea kuhusu Mkopo unaotolewa na Mfuko wa Ushirikiano wa Maendeleo ya Uchumi wa Serikali ya Korea (Economic Development Cooperation Fund-EDCF). Hafla ya utiaji saini imefanyika katika Ikulu nchini humo tarehe 02 Juni, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Korea Mhe. Yoon Suk Yeol wakati wakishuhudia Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. January Makamba pamoja na Waziri wa Biashara wa Korea Inkyo Cheong wakibadilishana Hati ya Makubaliano kati ya Wizara ya Madini ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Wizara ya Biashara, Viwanda na Nishati ya Jamhuri ya Korea kuhusu Ushirikiano katika Madini ya Kimkakati. Hafla ya utiaji saini imefanyika katika Ikulu nchini humo tarehe 02 Juni, 2024.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Korea Mhe. Yoon Suk Yeol wakati wakishuhudia Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. January Makamba pamoja na Waziri wa Uvuvi na masuala ya Bahari kutoka Jamhuri ya Korea Kang Do-Hyung wakisaini Hati baina ya nchi mbili kuhusu Ushirikiano katika maendeleo ya Uchumi wa Buluu. Hafla ya utiaji saini imefanyika katika Ikulu nchini humo tarehe 02 Juni, 2024.

RAIS SAMIA AKUTANA NA KUZUNGUMZA NA RAIS WA JAMHURI YA KOREA MHE. YOON SUK YEOL, IKULU SEOUL NCHINI HUMO.

June 02, 2024

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Korea Mhe. Yoon Suk Yeol mara baada ya kuwasili katika Ikulu ya Nchi hiyo iliyopo Seoul kwa ajili ya mazungumzo na kushuhudia hafla ya utiaji saini Mikataba mbalimbali tarehe 02 Juni, 2024.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Viongozi mbalimbali wa Serikali ya Jamhuri ya Korea mara baada ya kuwasili katika Ikulu ya Nchi hiyo iliyopo Seoul tarehe 02 Juni, 2024.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye mazungumzo na Mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Korea Mhe. Yoon Suk Yeol katika Ikulu ya Nchi hiyo iliyopo Seoul tarehe 02 Juni, 2024.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Korea Mhe. Yoon Suk Yeol kabla ya kushuhudia hafla ya utiaji saini Mikataba mbalimbali baina ya nchi mbili kwenye hafla iliyofanyika Ikulu Jijini Seoul tarehe 02 Juni, 2024.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisaini Kitabu cha Wageni mara baada ya kuwasili katika Ikulu ya Jamhuri ya Korea iliyopo Jijini Seoul tarehe 02 Juni, 2024.



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiongoza ujumbe wa Tanzania kwenye mazungumzo Rasmi na Rais wa Jamhuri ya Korea Mhe. Yoon Suk Yeol katika Ikulu ya Nchi hiyo iliyopo Seoul tarehe 02 Juni, 2024.