VPL KUENDELEA WIKIENDI HII

VPL KUENDELEA WIKIENDI HII

September 18, 2015

Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara inatarajiwa kuendelea wikiendi hii kwa michezo nane kuchezwa kwa siku za jumamosi na jumapili katika viwanja nane tofauti nchini ikiwa ni mzunguko wa tatu tangu kuanza kwa ligi hiyo mwishoni mwa wiki iliyopita.
Jumamosi mabingwa watetezi wa kombe hilo klabu ya Young Africans watakuwa wenyeji wa JKT Ruvu katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, Chama la Wana Stand United watawakaribisha Wana Kimanumanu African Sports katika dimba la Kambarage mjini Shinyanga.
Jijini Mbeya kutakua na mpambano wa wenyeji wa mji huo (Mbeya Derby) kati ya Tanzania Prisons watakapokuwa wakipambana na Mbeya City katika uwanja wa Sokoine jijini humo, huku Maafande wa Mgambo Shooting wakiwakaribisha Wana Lizombe Majimaji FC kwenye uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.
Ligi hiyo itaendelea Jumapili kwa michezo minne kuchezaw, Simba SC watawakaribisha Kagera Sugar kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, huku Mwadui FC wakiwa wenyeji wa Azam FC katika uwanja wa Mwadui Complex mjini Shinyanga.
Wakata miwa wa Turiani Mtibwa Sugar watawakaribisha Ndanda FC ya Mtwara kwenye uwanja wa Manungu mkoani Morogoro na Wagosi wa Kaya Coastal Union watakua wenyeji wa Toto Africans katika uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AFANYA MAUNGUMZO NA BAADHI YA MABALOZI WANAOZIWAKILISHA NCHI ZAO HAPA NCHINI LEO

September 18, 2015

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Balozi wa Kuwait Nchini Tanzania Mhe. Jasem Najem wakati Balozi huyo alipomtembelea Makamu wa Rais Ofisini kwake Ikulu Dar es salaam leo Septemba 18, 2015.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Balozi wa Sweden Nchini Tanzania Mhe. Katarina Rangnitt wakati Balozi huyo alipomtembelea Makamu wa Rais Ofisini kwake Ikulu Dar es salaam leo Septemba 18, 2015, kwa ajili ya kujitambulisha rasmi
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Balozi wa Finland Nchini Tanzania Mhe. Pekka Hukka wakati Balozi huyo alipomtembelea Makamu wa Rais Ofisini kwake Ikulu Dar es salaam leo Septemba 18, 2015 kwa ajili ya kujitambulisha rasmi.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Finland Nchini Tanzania Mhe. Pekka Hukka wakati Balozi huyo alipomtembelea Makamu wa Rais Ofisini kwake Ikulu Dar es salaam leo Septemba 18, 2015 kwa ajili ya kujitambulisha rasmi. 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Balozi wa Finland Nchini Tanzania Mhe. Pekka Hukka Ofisini kwake Ikulu Dar es salaam leo Septemba 18, 2015. 
(Picha na OMR)

MGOSI: YANGA HAATUUMIZI KICHWA, NGOJA TUMALIZANE NA KAGERA SUGAR KWANZA

September 18, 2015

Nahodha wa Simba SC, Mussa Hassan Mgosi amesema akili zao kwa sasa zinaifikiria Kagera Sugar 

MECHI ZIJAZO LIGI KUU YA VODACOM TZ BARA

Septemba 19, 2015
Stand United Vs African Sports
Mgambo Shooting Vs Majimaji FC
Prisons Vs Mbeya City
Yanga SC Vs JKT Ruvu
Septemba 20, 2015
Mwadui FC Vs Azam FC
Mtibwa Sugar Vs Ndanda FC
Simba SC Vs Kagera Sugar
Coastal Union Vs Toto Africans
Septemba 26, 2015
Simba SC Vs Yanga SC
Coastal Union Vs Mwadui FC
Prisons Vs Mgambo Shooting
JKT Ruvu Vs Stand United
Mtibwa Sugar Vs Majimaji FC
Kagera Sugar Vs Toto Africans
Septemba 27, 2015
African Sports Vs Ndanda FC
Azam FC Vs Mbeya City
Na Princess Asia, DAR ES SALAAM
NAHODHA wa Simba SC, Mussa Hassan Mgosi amesema kwamba akili zao zipo kwenye mechi yao ya Jumapili dhidi ya Kagera Sugar na hawaumizwi kichwa hata dogo na mahasimu wao, Yanga SC.
Akizungumza na BIN ZUBEIRY juzi mjini Tanga, Mgosi amesema baada ya kushinda mechi mbili za mwanzo za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara sasa wanaelekeza nguvu zao katika mchezo wa tatu dhidi ya Kagera.
“Sioni sababu ya kuwazungumzia Yanga kwa sasa wakati mechi ijayo tunacheza na Kagera. Kwanza nataka nikuambie, hao Yanga hawatuumizi kichwa kabisa,”amesema.
Mgosi amesema kwamba wachezaji wote wa Simba SC kwa sasa akili yao inafikiria namna gani wataifunga Kagera Sugar ili kufikisha pointi tisa ndani ya mechi tatu.
Simba SC imeanza vyema Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara baada ya kushinda mechi zake zote mbili za mwanzo Uwanja wa Mkwakwani, Tanga 1-0 dhidi ya African Sports na 2-0 dhidi ya JKT Mgambo.
Sasa Wekundi hao wa Msimbazi walio chini ya kocha Muingereza, Dylan Kerr watacheza mechi yao kwanza nyumbani mwishoni mwa wiki, dhidi ya Kagera Sugar Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

MAGALULA AIPA SOMO BODI YA MAJENGO

September 18, 2015


 Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Tanga ambaye amehamishiwa Mkoa wa Rukwa, Said Magalula, akimulikiwa mwanga kwa kutumia tochi ya simu na mshiriki  wa kongamano hilo, Flavian Rugaimukamu kufuatia umeme kukatika mara kwa mara wakati akifungua kongamano la Bodi ya Usajili wa Wabunifu Majengo na Ukadiriaji wa Majenzi uliofanyika mkoani Tanga



NA SALUM MOHAMED wa tangakumekuchablog
ALIEKUWA MKUU wa Mkoa wa Tanga ambaye amehamishiwa Mkoa wa Rukwa, Said Magalulla, ameiagiza bodi ya Usajili wa Wabinu Majengo na Wakadiriaji Majenzi, kuwachukulia hatua kali za kisheria wabadhrifu na wala rushwa ndani ya bodi hiyo.
Akifungua kongamano la 24 ya bodi ya Usajili Mkoani hapa leo, Magalula, alisema kuna baadhi ya watendaji wamekuwa wakivunja maadili ya kazi zao ikiwemo kujihusisha la ulaji rushwa jambo ambalo limekuwa likirudisha nyuma bodi hiyo.
Alisema ili kuweza kupiga hatua za kuwaletea maendeleo wananchi ni vyema bodi ya Usajili ikifanya ukaguzi mikataba ya makampuni kwa madai kuwa huko ndiko ubadhrifu unakoanzia.
“Jambo la faraja ni kuona wenyeviti wakuu wa taasisi na watendaji mbalimbali muko kwa pamoja hapa na hiki ambacho mutakijadili na kuadhimia kitakuwa cha faida kwa maslahi ya maendeleo ya wananchi” alisema Mgalula na kuongeza
“Ila jambo la msingi naiagiza bodi ya usajili wa ubunifu majengo kusafisha wala rushwa kila idara-----jambo hili limekuwa likirudisha nyuma jitihada za bodi” alisema
Alisema wala rushwa wamejificha kila idara na hivyo kuitaka bodi hiyo kufichua makucha yake kwa kuwafichua na kuwaweka hadharani ikiwa na pamoja na kuwafikisha katika vyombo vya sheria.
Akizungumza katika kongamano hilo, Msajili wa bodi, Abdalla Jihad, alisema bodi hiyo imewachukulia hatua za kisheria wataalamu waliokiuka taaluma zao 92 na makampuni 57 yamefutiwa usajili kwa kukiuka sheria.
Alisema hatua hizo imesaidia kwa baadhi ya wataalamu kuzingatia maadili na nafasi zao ikiwa na pamoja na makampuni kuzingatia sheria za usajili jambo ambalo imekuwa msaada kwa bodi.
“Katika kusimamia sheria bodi imeweza kuwachukulia hatua za kisheria wataalamu tisini na mbili sambamba na makapuni 57 yaliyokiuka sheria” alisema Jihad
Alisema kwa mantiki hiyo bodi imejipanga kuhakikisha wataalamu wanazitumia nafasi zao na kuziba mianya yote ya rushwa na ubadhrifu wa pesa ili kuweza kufikia malengo iliyojiwekea.
                                                  Mwisho


Mkutano wa Kampeni ya Mgombea wa Urais CCM Dk Ali Mohamed Shein,Jimbo la Mkoani Pemba.

September 18, 2015

Mgombea Urais wa Zanzibar Kupitia CCM Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Ndg Vuai Ali Vuai alipowasili katika viwanja vya mkutano vya Chokocho Wilaya ya Mkoani Pemba kwa ajili ya kampeni yake kwa wananchi wa Jimbo hilo la Mkoani.
Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia CCM Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein, akiwa na Viongozi wa Siasa jukwaa kuu baada ya kuwasili katikac viwanja hivyo kwa ajili ya mkutano wake wa Kampeni katika viwanja vya mpira Black Wizard Chokocho Wilaya ya Mkoani Pemba.
Wanachama wa CCM wakimshangilia Mgombea Urais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein, alipowasili katika viwanja vya Mkutano wake wa Kampeni Jimbo la Mkoani Pemba.
Wanachama wa Chama cha Mapinduzi wakiwa katika viwanja vya mkutano wa Kampeni ya Urais wa Zanzibar kupitia CCM katika viwanja vya Mpira Black Wizard Chokocho Pemba ,
Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Ndg Vuai Ali Vuai, akizungumza na Wananchi wa Wilaya Mkoani Jimbo la Mkoani Pemba akiwatambulisha Viongozi waliofuatana na Dk Shein wakati wa Mkutano wake wa Kampeni Pemba.Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Pemba Mkoa wa Kaskazini Pemba Ndg Mberwa Hamad Mberwa akizungumza wakati wa Mkutano huo wa Kampeni ya Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein.

WATAKAO HUJUMU MIUNDOMBINU YA DART KULIPA FAINI YA LAKI TATU.

September 18, 2015

 Mkurugenzi wa Mifumo Juhn Mlingi kutoka Taasisi ya Mabasi yaendayo Haraka (Dar es Salaam Rapid Transport) akitoa ufafanuzi wa maendeleo ya ujenzi wa mradi huo kwa wafanyakazi wa Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads) na waandishi wa habari walipokuwa katika ziara ya kukagua miundo mbinu ya mradi huo katika kituo cha Kivukoni jana jijini Dar es Salaam.
 Baadhi ya wafanyakazi wa Tanroads wakipanda  gari la Mradi  wa Mabasi yaendayo Haraka jana  jijini Dar es Salaam katika  ziara ya kukagua Miundo Mbinu ya Mradi  wa DART kabla  ya kuanza kutumika .
 Baadhi ya wafanyakazi wa Tanroads wakikagua  kituo cha mabasi yaendayo haraka kilichopo Kimara  ambacho ujenzi wake  umekamilika  kwa asilimia mia moja jana jijini Dar es Salaam.
 Mmoja wa  Afisa wa Tanroads akikagua kibanda cha kukatia tiketi kilichopo ndani ya kituo cha Kimara katika mradi wa mabasi yaendayo haraka wakati wa ziara ya ukaguzi wa miundo mbinu ya mradi huo jana jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wanyakazi wa Tanroads wakiwa ndani ya moja ya mabasi ya mradi wa mabasi yaendayo haraka walipokuwa wakifanya  ziara ya kukagua miundo mbinu ya mradi huo jana jijini Dar es Salaam.
Na Ally Daud- MAELEZO.
Wafanyakazi wa Mradi wa Mabasi ya endayo haraka Dar es salaam (DART ),Wakalawa Barabara(TANROADS) pamoja na Umoja wa wamiliki wa Daladala Dar es Salaam (UDART) wamefanya ziara ya kufahamu na kuelewa miundo mbinu ya mradi huo.

Akizungumza na waandishiwa Habari jana jijini Dar es Salaam Mkurugenzi wa Mifumo DART Bw. Junn Mlingi alisema mabasi hayo yatatumia dakika 45 mpaka 35 kutoka kituo cha Kivukoni mpaka kituo cha Kimara na kutumia dakika mbili kusimama kila kituo ili kuruhusu basi lingine lifike katika kituo husika baada ya dakika tano.

“Mradi huu unatarajiwa kukabidhiwa mnamo Novemba mwaka huu kwani mpaka sasa mradi umekamilika kwa asilimia 80 katika kipindi cha kwanza  ambapo unaanzia Kivukoni mpaka Kimara mwisho na Sheria ya matumizi ya miundombinu ya DART  ipo na inasema kwa yeyote atakayekamatwa akihujumu miundombinu atatozwa faini ya shilingi laki tatu au kutumikia kifungo cha miezi sita hadi mwaka mmoja ama kutumikia adhabu zote mbili”, alisema Bw. Mlingi.

Akiendelea kuzungumza katika ziara hiyo Bw. Mlingi alisema waratibu wa mradi huo wamejipanga kuhakikisha wanatoa huduma bora za usafiri kwa wananchi na wakazi wa jiji la Dar es salaam kwa kuboresha sheria , taratibu na miundombinu itayotumika kutumia usafiri huo wa mabasi yaendayo harakakatika barabara zake maalumu.

Aidha Mratibu wa Mji DART Bw. Edwin Hema alisema Mabasi hayo yatakua yanatembea kwa mwendo wa kawaida kwa kilomita 50 kwa saa ikiwa ni kasi ya juu na kilomita 20 kwa saa ikiwa ni kasi ya wastani kutoka kituo cha Kivukoni mpaka kituo cha Kimara na kuwa na muda maalumu wa kushusha abiria na kupakia.

Mbali na hayo Bw.Hema alisema wananchi hawatatakiwa kugombania mabasi kwani yatazingatia muda uliyopangwa katika taratibu zakubeba abiria na pale gari itakapohitaji kusimama dereva atatangaza kituo na abiria watatakiwa kukaa mbali na mlango mpaka milango itakapofunguka.

Naye Mkurugenzi wa Mifumo alisema wameweka utaratibu kwa walemavu wote watakaotumia usafiri huo kwa urahisi na haraka na kuweza kuwahi kwenye shughuli zao bila yausumbufu kwa kuwa wana sehemu zao za kukaa na kwa wale wanaotumia baiskeli za kusukumwa wataweza kupanda na baiskeli zao ndani ya basi hilo.

Kwa upande wa Msemaji Mkuu wa Umoja wa Wamiliki wa Daladala Dar es Salaam (UDART) na mradi wa mabasi hayo Bw. Sabri Mabruki amesema mpaka sasa wameingia mkataba wa kuleta mabasi 76 ya kuanzia kupitia Kampuni ya Golden  Dragon  kutoka  Japan.

TANZANIA NA NORWAY KUIMARISHA USHIRIKIANO KATIKA SEKTA YA BIASHARA NA UWEKEZAJI

September 18, 2015

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) akihutubia katika ufunguzi rasmi wa Semina ya Ushirikiano wa Kibiashara na Uwekezaji kati ya Tanzania na Norway iliyofanyika kwenye Hoteli ya Hyatt Regency ya Jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na Waziri wa Biashara na Viwanda wa Norway, Mhe. Monica Maeland, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Liberata Mulamula, Balozi wa Norway nchini, Mhe. Hanna-Marie Kaarstad na wadau wengine katika sekta ya biashara na uwekezaji kutoka Norway na hapa nchini.
Waziri wa Biashara na Viwanda wa Norway, Mhe. Maeland (kulia) akimsikiliza Mhe. Membe (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza wakati wa ufunguzi wa semina hiyo. Kushoto ni  Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Liberata Mulamula na katikati ni  Balozi wa Norway hapa nchini, Mhe. Kaarstad. 
Waziri Membe akiendelea kuzungumza
Waziri wa Biasha na Viwanda nchini Norway Mhe. Monica Maeland naye alipata fursa ya kuzungumza wakati wa ufunguzi wa semina ya Ushirikiano wa kibiashara na uwekezaji kati ya Tanzania na Norway, Mhe. Maeland yupo nchini kwa lengo la kuvutia wawekezaji na wafanyabiashara wa Tanzania nchini Norway. Pia wakati wa ziara hiyo Mhe. Maeland amezindua mtambo wa mbolea wa Yara ulioko kwenye Bandari ya Dar es Salaam na pia atatembelea Jumuiya ya Afrika Mashariki Jijini Arusha.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bi. Mindi Kasiga (kulia) na mmoja wa wadau katika semina hiyo Bw. John Ulanga (kushoto) wakifuatilia Hotuba mbalimbali zilizokuwa zikiendelea kutolewa na Mhe. Membe na Mhe. Maeland (hawapo pichani). 
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bi. Tunsume Mwangolombe (katikati) naye akifuatilia ufunguzi wa Semina hiyo.
Sehemu ya wadau wakifuatilia ufunguzi wa Semina hiyo 
Semina ikiendelea
Waziri Membe (katikati) na Waziri Maeland kwa pamoja na wajumbe waliofuatana nao wakiwa kwenye mazungumzo mara baada ya kumaliza ufunguzi wa semina.
Waziri Membe (kulia) akizungumza na Waandishi wa Habari (hawapo pichani) juu ya  faida ya semina hiyo ya wafanyabiashara wa Tanzania na Norway
Mkutano na waandishi wa habari ukiendelea
Picha na Reginald Philip
 TANZANIA NA NORWAY KUIMARISHA USHIRIKIANO KATIKA SEKTA YA BIASHARA NA UWEKEZAJI
Waziri wa Mmabo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe ameisifu Serikali ya Norway kwa kuwa mshirika wa karibu wa maendeleo wa Tanzania hususan katika sekta za biashara na uwekezaji.
Waziri Membe alitoa kauli hiyo kwa niaba ya Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Abdallah Kigoda wakati akifungua rasmi semina kuhusu kuimarisha ushirikiano wa Kibiashara  na Uwekezaji kati ya Tanzania na Norway iliyofanyika katika Hoteli ya Hyatt Regency Jijini Dar es Salaam leo.
Katika ufunguzi huo ambao ulihudhuriwa pia na Waziri wa Biashara na Viwanda wa Norway, Mhe. Monica Maeland ambaye yupo nchini kwa ziara ya kikazi, Mhe. Membe alisema kuwa Tanzania na Norway zimekuwa na ushirikiano wa kidiplomasia kwa miaka mingi lakini sasa nchi hizi zimeamua kushirikiana zaidi katika masuala ya uwekezaji na biashara ili kukuza uchumi kwa maendeleo ya nchi zote mbili.
Aliongeza kuwa, kwa miaka mingi Tanzania imefaidika na  ushirikiano na Norway katika sekta mbalimbali ambapo nchi hiyo imechangia kwa kiasi kikubwa katika kuisaidia Tanzania kupambana na umaskini na kukuza uchumi. Hata hivyo alisema umefika wakati sasa nchi hizi mbili zinufaike kupitia biashara na uwekezaji ambapo nchi zote zina fursa nyingi katika maeneo hayo ikiwemo gesi na mafuta, kilimo na madini.
Mhe. Membe alisema kuwa kufanyika kwa semina hii itakayowakutanisha wafanyabiashara na wawekezaji itaongeza thamani katika uhusiano wa kidiplomasia uliopo kati ya nchi hizi mbili ambapo Tanzania ina mengi ya kujifunza kutoka Norway ambayo ni miongoni mwa nchi zinazosafirisha zaidi gesi asilia na mafuta duniani. Hivyo aliwaasa Watanznaia kutumia semina hiyo kujifunza ili kuimarisha sekta ya nishati ya hapa nchini. 
“Semina hii ni fursa kwa Kampuni za Tanzania na Norway kujifunza na kubadilisha uzoefu na mawazo ya namna bora ya kuboresha sekta za biashara na uwekezaji kwa manufaa ya nchi zote mbili” alisema Waziri Membe.
Akizungumzia biashara inayofanyika kati ya Tanzania na Norway, Mhe. Membe alisema kuwa Tanzania inatakiwa kuongeza biashara yake nje ya nchi ili kuimarisha uchumi wake. Alieleza kuwa kwa sasa biashara kati ya Tanzania na Norway imeongezeka kutoka shilingi bilioni 1.6 mwaka 2010 hadi kufikia shilingi bilioni 6.9 mwaka 2014 kwa bidhaa zilizozwa Norway kutokea Tanzania ikiwemo kahawa, chai, viungo, maua, mbogamboga, mbao na madini. 
Kwa upande wa bidhaa kutoka Norway, Tanzania imenunua kwa ongezeko la kutoka bilioni 22.3 mwaka 2010 hadi kufikia shilingi bilioni 73 mwaka 2014. Bidhaa hizo ni pamoja na dawa za binadamu na bidhaa za viwandani.
Kwa upande wake Waziri wa Viwanda na Biashara wa Norway, Mhe. Monica aliipongeza Tanzania kwa kupiga hatua kubwa katika maendeleo na ukuaji wa uchumi ambao umefikia asilimia 7. Alieleza kuwa Tanzania itafikia azma yake ya kuwa nchi ya uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025 kwa vile inayo dhamira ya dhati na imejipanga kupitia uvumbuzi wa gesi na mafuta, nguvukazi ya vijana na mageuzi yaliyopo katika sekta ya uchumi.
Alieleza kuwa Norway ipo tayari kuendelea kuisadia Tanzania katika sekta ya gesi na mafuta kwa vile nchi hiyo imepiga hatua kubwa katika eneo hilo hususan katika masuala ya teknolojia. Aidha, aliongeza kuwa Tanzania ni mshirika wa kweli wa Norway katika maendeleo hivyo nchi yake itashirikiana kikamilifu na Tanzania.

“Kuna msemo maarufu unasema kama unataka kwenda mbio nenda peke yako, lakini kama utanaka kufika mbali nenda pamoja na mwenzako. Hivyo Norway inataka kwenda pamoja na Tanzania ili kuziwezesha nchi hizi kufika mbali kimaendeleo” alisisitiza Mhe. Monica.
Awali akizungumza wakati wa ufunguzi wa semina hiyo, Balozi wa Norway hapa nchini Mhe. Hanne-Marie Kaarstad alisema kuwa upo umuhimu mkubwa kwa nchi hizi mbili kukuza biashara kwa kuishirikisha sekta binafsi kikamilifu kwani ni nyenzo muhimu kwa maendeleo endelevu. 

Semina hiyo ambayo imeandaliwa kwa ushirikiano kati ya Ubalozi wa Norway, Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) na Shirikisho la Wenye Viwanda Tanzania (CTI) ilihudhuriwa na Makampuni 34 kutoka Norway na Tanzania na pia wadau mbalimbali wa biashara na uwekezaji.
 VPL KUENDELEA WIKIENDI HII

VPL KUENDELEA WIKIENDI HII

September 18, 2015
Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara inatarajiwa kuendelea wikiendi hii kwa michezo nane kuchezwa kwa siku za jumamosi na jumapili katika viwanja nane tofauti nchini ikiwa ni mzunguko wa tatu tangu kuanza kwa ligi hiyo mwishoni mwa wiki iliyopita.
Jumamosi mabingwa watetezi wa kombe hilo klabu ya Young Africans watakuwa wenyeji wa JKT Ruvu katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, Chama la Wana Stand United watawakaribisha Wana Kimanumanu African Sports katika dimba la Kambarage mjini Shinyanga.
Jijini Mbeya kutakua na mpambano wa wenyeji wa mji huo (Mbeya Derby) kati ya Tanzania Prisons watakapokuwa wakipambana na Mbeya City katika uwanja wa Sokoine jijini humo, huku Maafande wa Mgambo Shooting wakiwakaribisha Wana Lizombe Majimaji FC kwenye uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.
Ligi hiyo itaendelea Jumapili kwa michezo minne kuchezaw, Simba SC watawakaribisha Kagera Sugar kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, huku Mwadui FC wakiwa wenyeji wa Azam FC katika uwanja wa Mwadui Complex mjini Shinyanga.
Wakata miwa wa Turiani Mtibwa Sugar watawakaribisha Ndanda FC ya Mtwara kwenye uwanja wa Manungu mkoani Morogoro na Wagosi wa Kaya Coastal Union watakua wenyeji wa Toto Africans katika uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AFANYA MAUNGUMZO NA BAADHI YA MABALOZI WANAOZIWAKILISHA NCHI ZAO HAPA NCHINI LEO

September 18, 2015

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Balozi wa Kuwait Nchini Tanzania Mhe. Jasem Najem wakati Balozi huyo alipomtembelea Makamu wa Rais Ofisini kwake Ikulu Dar es salaam leo Septemba 18, 2015.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Balozi wa Sweden Nchini Tanzania Mhe. Katarina Rangnitt wakati Balozi huyo alipomtembelea Makamu wa Rais Ofisini kwake Ikulu Dar es salaam leo Septemba 18, 2015, kwa ajili ya kujitambulisha rasmi
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Balozi wa Finland Nchini Tanzania Mhe. Pekka Hukka wakati Balozi huyo alipomtembelea Makamu wa Rais Ofisini kwake Ikulu Dar es salaam leo Septemba 18, 2015 kwa ajili ya kujitambulisha rasmi.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Finland Nchini Tanzania Mhe. Pekka Hukka wakati Balozi huyo alipomtembelea Makamu wa Rais Ofisini kwake Ikulu Dar es salaam leo Septemba 18, 2015 kwa ajili ya kujitambulisha rasmi. 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Balozi wa Finland Nchini Tanzania Mhe. Pekka Hukka Ofisini kwake Ikulu Dar es salaam leo Septemba 18, 2015. 
(Picha na OMR)
FDL KUTIMUA VUMBI KESHO

FDL KUTIMUA VUMBI KESHO

September 18, 2015
Ligi Daraja la Kwanza nchini (FDL) inatarajiwa kuanza kutimua vumbi kesho Jumamosi Septemba 19 kwa michezo 10 kuchezwa katika viwanja mbalimbali nchini, ambapo jumla ya timu 24 zinashirki ligi hiyo zitaanza kusaka nafasi tatu za juu ili kuweza kupanda Ligi Kuu msimu ujao.
Kundi A, Polisi Dar watakuwa wenyeji wa Friends Rangers kwenye uwanja Mabatini mkoani Pwani, Mjii Mkuu ya Dodoma watapambana na  Polisi Dodoma kwenye uwanja wa Jamhuri mjini humo.
Kundi B, Polisi Morogoro watacheza na Burkina Faso uwanja wa Jamhuri Morogoro, Njombe Mji FC watacheza na Kurugenzi uwanja wa Amani mjini Njombe, Lipuli ya Iringa watawaribisha Kimondo FC uwanja wa Wambi- Iringa na JKT Mlale watakua wenyeji wa Ruvu Shooting katika uwanja wa Majimaji mkoani Ruvuma.
Kundi C, Mbao FC watawakaribisha Geita Gold uwanja wa CCM Kirumba, Rhino Rangers watacheza dhidi ya Polisi Tabora uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora, Panone FC watawakaribisha JKT Oljoro katika uwanja wa Ushirka mjini Moshi na Polisi Mara watakua wenyeji wa JKT Kanembwa kwenye uwanja wa Karume mkoani Mara.
Nchi za Afrika zimeaswa kuimarisha mawasiliano katika utoaji wa taarifa zinazohusiana na magonjwa ya mafua makali.

Nchi za Afrika zimeaswa kuimarisha mawasiliano katika utoaji wa taarifa zinazohusiana na magonjwa ya mafua makali.

September 18, 2015

x1
Muwakilishi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) nchi Kenya Dkt. Custodia Mandlhate akuitoa hotuba ya ufungua wa semina ya inayohusu namna ya kuimarisha mawasiliano na utoaji wa taarifa sahihi zinazohusiana na magonjwa ya mafua makali katika ukanda wa nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika wa siku tatu unaoendelea jijini Nairobi.
x2Baadhi ya washiriki wa semina ya inayohusu namna ya kuimarisha mawasiliano na utoaji wa taarifa sahihi zinazohusiana na magonjwa ya mafua makali katika ukanda wa nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika wa siku tatu unaoendelea jijini Nairobi.
x3Muwakilishi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) nchi Kenya Dkt. Custodia Mandlhate (aliyesimama katikati mstari wa mbele) akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa semina ya inayohusu namna ya kuimarisha mawasiliano na utoaji wa taarifa sahihi zinazohusiana na magonjwa ya mafua makali katika ukanda wa nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika mara baada ya ufunguzi wa Semina hiyo.
…………………………………………………..
Na Mwandishi wetu
Nchi za Afrika zimeaswa kuimarisha mawasiliano katika utoaji wa taarifa zinazohusiana na magonjwa ya mafua makali yanayosababishwa na virusi vya influenza ili kuokoa maisha ya watu kwa haraka unapotokea mlipuko wa magonjwa hayo.
Kauli hiyo imetolewa na Mwakilishi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) nchini Kenya Dkt. Custodia Mandlhate alipokuwa akifungua semina ya inayohusu namna ya kuimarisha mawasiliano na utoaji wa taarifa sahihi zinazohusiana na magonjwa ya mafua makali katika ukanda wa nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika, semina hiyo inayoendelea jijini Nairobi.
Mawasiliano ya haraka wakati wa dharura za kiafya yanahusu ngazi zote kuanzia kimataifa wakati wa hatari ni yetu sote, ni ya kimataifa, kikanda na kitaifa, hivyo basi kipaumbele cha WHO ni kuhamasisha watu, mashirika na serikali kushiriki katika kutoa taarifa na elimu juu ya namna ya kuokoa maisha ili kuchukua hatua sahihi za kuzuia,  kujikinga na kujilinda dhidi ya vitisho ugonjwa huo” alisema Dkt. Custodia.
Dkt. Custodia alisema kuwa hatua ya kupata elimu sahihi ya namna ya kujikinga na magonjwa hayo inatekelezwa kwa kupitia matumizi bora ya mawasiliano ya umma juu ya afya, ushiriki wa jamii na uhamasishaji wa kijamii kwa kutumia vyombo vya habari, sera na tafiti zinazofaywa ili kuokoa maisha ya watu katika eneo husika.
Malengo ya mkutano huo ni kuwajengea uwezo washiriki ambao utaimarisha mawasiliano kwa watoa maamuzi muhimu ya kitaifa na kikanda katika kuimarisha hatua za dharura katika kuzuia, kujikinga na kujilinda dhidi ya vitisho ugonjwa wa mafua makali.
Malengo mengine ni pamoja na washiriki kupata uelewa juu ya njia bora za kutoa taarifa wakati inapotokea hatari ya magonjwa ya mlipuko yanayoweza kusababisha madhara makubwa ya kiafya ambayo yanahitaji dharura katika utekelezaji wake pamoja na kuimarisha mitandao ya kikanda ya watoa maamuzi na watendaji ili kubadilishana uzoefu na utaalamu kupitia nchi wanazoziwakilisha.
Kwa upande wake muwakilishi kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Tanzania Dkt. Vida Makundi alisema kuwa semina hiyo ina manufaa makubwa kwa taifa hilo kwa kuwa nchi hiyo tayari ina viashiria vya kuapata yanayotokana na wanyama yakiwemo mafua makali ya ndege na mengine hivyo hivyo ni vema kujifunza na kuchukua tahadhari ikiwaa ni pamoja na kuelimisha jamii namna ya kujikinga majanga mbalimbali ya magonjwa na matukio yanayoathiri afya ya binadamu yanapotokea.
Dkt. Vida alisisitiza kuwa wataalamu wa afya na sekta nyingine zinzohusika na afya ya binadamu wakaelewa kuwa ili kufanikisha mawasiliano kwa jamii hawana budi kushirikiana kwa karibu na  wanahabari kutoa habari kwa jamii ili kuokoa maisha ya watu kwa haraka unapotokea mlipuko wa magonjwa ambapo kunahitajika kuwepo na uelewa mpana wa kisiasa, kijamii na kiutamaduni na kuzingatia eneo lililoathiriwa na ugojwa wa mlipuko.
Mkutano huo unaoendelea Nairobi nchini Kenya unaongozwa na kaulimbiu inayosema “Okoa maisha na zuia ugonjwa kuenea” unajumisha ya zaidi ya washiriki 65 kutoka nchi 21 zilizopo katika ukanda wa Mashariki na Kusini mwa Afrika ambapo washiriki wanatoka katika Wizara za Afya, Habari na Muwakilishi mmoja wa WHO kutoka nchi anayowakilisha katika ukanda huo.
Nchi hizo ni pamoja na Tanzania, Uganda, Msumbiji, Malawi, Botswana, Lesotho, Sudani ya Kusini, Madagaska, Visiwa vya Shelisheli, Comoro, Swaziland, Rwanda, Mauritius, Eritrea, Namibia, Ethiopia, Afrika Kusini na Zimbabwe.na Kenya ambayo ni mwenyeji wa semina hiyo.