Rais Kikwete aweka jiwe la Msingi Jengo la Kitega uchumi Mamlaka ya Ngorongoro

Rais Kikwete aweka jiwe la Msingi Jengo la Kitega uchumi Mamlaka ya Ngorongoro

September 12, 2015

1 
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikiwete akiweka jiwe la msingi katika jengo la kitega uchumi linalomilikiwa na Mamlaka ya hifadhi ya Bonde la Ngorongoro lililopo mjini Arusha jana jioni.
unnamedMwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Mamlaka ya Uhifadhi ya Bonde la Ngorongoro Balozi Mwanaidi Maajar akimkabidhi Rais Kikwete zawadi mbalimbali pamoja na pasi ya kudumu ya kuingia katika hifadhi ya Ngorongoro muda mfupi baada ya Rais Kuzindua ujenzi wa jengo la Kitega uchumi la Hifadhi hiyo mjini Arusha jana.
e

IDARA YA MIPANGO MIJI NA VIJIJI ZANZIBAR YAANDAA MRADI WA KUBORESHA MAENEO MATANO YA WAZI YA MJI WA ZANZIBAR CHINI YA UFADHILI WA SHIRIKA LA SDC LA SWITZERLAND.

September 12, 2015


 Mkuu wa Ushirikiano wa  Ubalozi wa Switzerland nchini Tanzaania Romana Tedeschi akizungumza na wananchi (hawapo pichani) walioshiriki uzinduzi wa Mradi wa kuboresha maeneo matano ya wazi ya Mji wa Zanzibar kwa kuanzia na  Kiwanja cha Demokrasia Kibandamaiti utakaofadhiliwa na Shirika la SDC la nchi hiyo.
 Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Abdalla Mwinyi Khamis akizindua  Mradi wa kuboresha maeneo ya wazi ya Mjini  Zanzibar katika hafla iliyofanyika Idara ya Ardhi na Upimaji Forodhani Mjini Zanzibar, (kulia) Mkurugenzi wa Mipango Miji na Vijiji Muhamad Juma
  Msaidizi  Fundi Mkuu wa Kampuni ya Ujenzi ya Landscape ya Switzerland Roland Raderschall akitoa maelezo ya  Mradi wa  mwanzo wa kuboresha  Kiwanja cha Demokrasia cha Kibandamaiti katika hafla ya uzinduzi wa mradi huo.
 Mkurugenzi wa Mipango Miji na Vijiji Zanzibar Muhamad Juma akitoa ufafanuzi kwa wananchi walioshiriki uzinduzi wa Mradi wa kuboresha eneo la wazi  la Kibandamaiti., (kulia) Mkuu wa Mkoa Mjini Mgharibi Abdalla Mwinyi Khamis.
Ramani ya maeneo matano  ya wazi yatakayofanyiwa  uboreshaji  na Idara ya Mipango na Vijiji ambayo ni Kibandamaiti, Lumumba, Darajani, Chumbuni na Darajabovu. Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.

WIZARA YA AFYA KWA KUSHIRIKIIANA NA SHIRIKA LA HELPAGE INTERNATIONAL WAMEANDAA MKUTANO WA SIKU MBILI WA KUTATHMINI HUDUMA BORA ZA WAZEE ZANZIBAR KATIKA HOTELI YA OCEAN VIEW.

September 12, 2015

 Naibu Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo akifungua Mkutano wa kutathmini huduma za Wazee Zanzibar ulioandaliwa na Wizara yake kwa ufadhili wa Shirika la HelpAge International katika Hoteli ya Ocean View Kilimani Mjini Zanzibar.
 Naibu Mkurugenzi wa Shirika la HelpAge Internalinal  Smart Daniel akizungumza na washiriki wa Mkutano wa kutathmini huduma za Wazee Zanzibar katika Hoteli ya Ocean View Kilmani (kushoto) Naibu Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo na kushoto Mwenyekiti wa Mkutano huo  Mkuu wa Wilaya ya Kusini Unguja Haji Makungu Mgongo. PICHA NA RAMADHANI ALI / MAELEZO ZANZIBAR.
 Washiriki wa Mkutano  huo wakiwa katika kazi za vikundi wakijadiliana juu ya mikakati itakayofanikisha kuandaliwa mazingira bora ya maisha ya Wazee Zanzibar.
 Daktari Dhamana  Wilaya ya Wete akiwasilisha kazi za vikundi katika mkutano wa kutathmini huduma za Wazee Zanzibar uliofanyika Hoteli ya Ocean View Kilimani Mjini Zanzibar
 Katibu Mkuu Wizara ya Afya Saleh Muhammed Jidawi akifunga mkutano wa kutathmini huduma za Wazee Zanzibar uliofanyika katika Hoteli ya Ocean View Kilimani Mjini Zanzibar.
Picha ya pamoja ya wajumbe wa Mkutano huo uliohudhuriwa na Wakuu wa Wilaya za Zanzibar, Madaktari dhamana wa Hospitali kuu za Wilaya, Jumuia ya Wazee  na Taasisi za kiraia baadhi ya maofisa wa Wizara ya Afya.

KAMATI ZA MAAFA MKOANI DODOMA WAFANYA TATHMINI YA MPANGO WA KUJIANDAA NA KUKABILIANA NA MAAFA

September 12, 2015

 Mkuu wa Mkoa Dodoma, Luteni Mstaafu, Chiku Galawa akisisitiza jambo wakati akifungua Mkutano wa kuwasilisha Taarifa ya Tathmini ya Utekelezaji wa Mpango ya Kujiandaa na Kukabiliana na Maafa kwa Halmashauri za Chamwino, Kondoa na Mpwapwa mjini Dodoma,  tarehe 12 Septemba, 2015.
 Mjumbe wa Kamati ya Maafa wilayani Mpwampwa, Shekh, Sabah Seif akisisitiza jambo wakati wa Mkutano wa kujadili Taarifa ya Tathmini ya Utekelezaji wa Mpango ya Kujiandaa na Kukabiliana na Maafa kwa Halmashauri za Chamwino, Kondoa na Mpwapwa mjini Dodoma,  tarehe 12 Septemba, 2015.
 Wakuu wa wilya za Mkoa wa Dodoma ambao pia ni Wajumbe wa Kamati za Wilaya za Maafa wakifuatilia uwasilishaji Taarifa ya Tathmini ya Utekelezaji wa Mpango ya Kujiandaa na Kukabiliana na Maafa kwa Halmashauri za Chamwino, Kondoa na Mpwapwa mjini Dodoma,  tarehe 12 Septemba, 2015. Wakwanza ni; Shaban Kisu (Kondoa), Ramadhani Maneno (Chemba), Francis Kimoga (Bahi) na Bituni Msangi (Mpwapwa).
 Mratibu Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Charles Msangi  akisisitiza jambo wakati akiwasilisha Taarifa ya Tathmini ya Utekelezaji wa Mpango ya Kujiandaa na Kukabiliana na Maafa wa Halmashauri ya  Chamwino, wakati wa Mkutano wa kujadili  Utekelezaji wa Mpango kwa Halmashauri za Chamwino, Kondoa na Mpwapwa mjini Dodoma,  tarehe 12 Septemba, 2015.
Mkuu wa Mkoa Dodoma, Luteni. Mstaafu, Chiku Galawa (walio kaa katikati) akiwa na wajumbe wa Kamati za maafa za wilaya mkoani Dodoma mara baada kufungua Mkutano wa kuwasilisha Taarifa ya Tathmini ya Utekelezaji wa Mpango ya Kujiandaa na Kukabiliana na Maafa kwa Halmashauri za Chamwino, Kondoa na Mpwapwa , tarehe 12 Septemba, 2015.

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL ATEMBELEA KUKAGUA NA KUKABIDHI MRADI WA MAJI SAFI NA SALAMA WA CHWAKA, UNGUJA

September 12, 2015

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na wakazi wa Kijiji cha Chwaka, Unguja, wakati alipofika kutembelea kukagua na kukabidhi Mradi wa Maji safi na salama wa Chwaka, leo Sept 12, 2015.
 Msimamizi wa Mradi wa Maji safi na salama wa Chwaka, Malcom Nyanda, akizungumza kuelezea changamoto za mradi huo wakati wa hafla hiyo ya makabidhiano ya mradi.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Fundi mkuu wa Tanki la maji, Yohana Mkoloma, wakati alipotembelea kukagua Mradi wa Maji safi na Salama wa Chwaka, Unguja leo Sept 12, 2015.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitoka kukagua mradi wa Maji safi na salama baada ya kukabidhi mradi huo kwa Kamati ya Maendeleo ya Kijiji cha Chwaka, leo Sept 12, 2015.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na baadhi ya viongozi wa Kijiji cha Chwaka baada ya kutembelea kukagua na kukabidhi mradi ya Maji safi na salama wa Chwaka, leo Sept 12, 2015 Unguja. Picha na OMR
UZINDUZI WA CHEZA KWA MADOIDO WAFANA DAR LIVE!

UZINDUZI WA CHEZA KWA MADOIDO WAFANA DAR LIVE!

September 12, 2015

1.3.
Yamoto Band wakizindua rasmi video yao mpya inayofahamika kwa jina la Cheza kwa Madoido katika Ukumbi wa Dar Live uliopo Mbagala, Zakhem jijini Dar es Salaam usiku wa kuamkia leo.
 Wasanii wa Yamoto Band, Enock Bella (wa kwanza kushoto) akifanya yake na Aslay (kulia).
4.Msanii Ruby akiwa stejini kufanya yake.
Msanii wa Bongo Fleva, Hellen George 'Ruby' akifanya yake stejini.
9.
...Ruby akiimba wimbo wake 'Na Yule'.
5.Shetta akitoa burudani kwa mashabiki wake.
Msanii wa Bongo Fleva,  Shetta akitoa burudani kwa mashabiki wake.
6.Shetta akikonga nyoyo za mashabiki wake.
Shetta akiendelea kuwapa burudani mashabiki zake.
7.Chegge na Temba mzuka ukiwa umewapanda stejini.
Chegge na Temba wakikamua stejini.
7
...Chege akiendeleza makamuzi.
10.Queen Dar leen akitoa burudani katika mashabiki wake.
Queen Darleen akitoa burudani kwa mashabiki wake.
8.
Makamuzi yakiendelea ndani ya Ukumbi wa Dar Live.
11.Mwimbaji wa Taarabu kutoka Bendi mpya ya Moyo Medern Taarab akiimba.
Mwimbaji wa Moyo Modern Taarab akiimba jukwaani.
12.Bebdi ya Moyo Modern Taarab ikitoa burudani.131415
Bendi ya Moyo Modern Taarab ikitoa burudani.
16.Mpiga kinanda wa Moyo Modern Taarab akifanya yake.
Mpiga kinanda  wa Moyo Modern Taarab akifanya yake.
17.Bonge la Nyau akionesha manjonjo.18.1920.
Madansa wakifanya yao ndani ya ukumbi wa Dar Live jana usiku.
VIJANA wanaounda Bendi ya Yamoto, usiku wa kuamkia leo wameangusha burudani ya aina yake katika Ukumbi wa Dar Live, Mbagala-Zakhem jijini Dar wakati vijana hao wakizindua rasmi video yao mpya inayofahamika kwa jina la Cheza kwa Madoido.

Kabla ya uzinduzi wa Cheza kwa Madoido, wasanii mbalimbali walipanda jukwaani kutoa burudani ikiwemo bendi mpya ya Taarab iitwayo  Moyo Modern Taarab inayomilikiwa na kiongozi wa Yamoto Band, Said Fela.
Wasanii mbalimbali wa chipukizi nao walipata nafasi ya kuonesha vipaji vyao kwa kuimba nyimbo mbalimbali ambapo wapenzi wa burudani waliburudika vya kutosha.

Katika listi ya wasani waliotumbuiza jukwaani ni pamoja na Ruby, Dulla Yeyo, Izeman huku Moyo Modern Taarab wakipagawisha na nyimbo zao kali zinazojulikana kama Haijalishi, Dongo la Gizani na Zetu Duwa.

Wengine waliokamua jukwaani ni Chegge, Temba, Queen Darleen, Shetta, Ditto na wengine kibao kisha uzinduzi wa Cheza kwa Madoido kufanyika katika ‘skrini’ kubwa kisha Yamoto Band kutumbuiza shoo kali.
(HABARI/ PICHA: DENIS MTIMA/GPL)
SAFARI ZA MO LEMON MINT SODA YAVUKA MIPAKA YAFIKA MJI WA SANTORINI

SAFARI ZA MO LEMON MINT SODA YAVUKA MIPAKA YAFIKA MJI WA SANTORINI

September 12, 2015
lemonMo Lemon Mint imefika hadi Santorini, Greece! Umeifikisha wapi Mo soda yako kutoka hapo Dar? Tutumie picha yako 'smile emoticon' ikichaguliwa tutaiweka kwenye ukurasa wetu wa facebook.
Na Andrew Chale, modewjiblog
Kampuni ya Mohammed Enterprises Tanzania Limited (METL GROUP), imeendelea kufanya vizuri sokoni kupitia upande wa vinywaji vyake mbalimbali vikiwemo: MO Cola, MO Portello na, MO Malt, MO Lemon Mint, MO chungwa na MO Bomba (Energy drink).
Kupitia ukurasa wa Facebook wa MeTL GROUP, (https://www.facebook.com/MeTLGroup) wamebainisha kuwa kampuni hiyo yenye kauli mbiu ya ‘The People’s Brand’, imeendelea kuwa karibu na wateja wao ilikuweza kushirikisha mawazo mbalimbali katika kufikia malengo ya kimaisha.
Mbali na kushirikishana mawazo hayo na wateja wao waliopo kwenye ukurusa huo maalum wa facebook, pia imeweza kutoa elimu na namna ya hatua za kufuatwa kwa watu ikiwemo mazoezi, vyakula vinavyofaa kuliwa na mambo mengine.
Pia kupitia ukurasa huo wa facebook, wateja wameombwa kutuma picha zao wakiwa na vinywaji kutoka MeTL GROUP, ikiwemo MO Bomba, MO Cola, MO Lemon Mint, MO Portello, Mo Embe, MO Chungwa nakisha kutuma katika ukurasa huo na 'Ku-SHARE'. Huku wakitakiwa kupiga picha na kinywaji hicho na kueleza mahala walipo!
mo caHuwezi kujua ukiwezacho mpaka umejaribu ‪#‎UsikateTamaa‬
Ndoto yako ni nini..Ndoto yako ni nini?
mo boa
mmo
Vitu vya kuzingatia na kuchukua unapoenda kufanya mazoezi ya viungo...mpango mzima na MO Bomba iwepo kukuongezea nguvu na kukuweka na nguvu zaidi..
pote
Mchezaji bora wa Basketball MICHAEL JORDAN hakuchaguliwa kwenye timu ya basketball kwenye shule yake ya Sekondari kwasababu alikuwa mfupi kuliko wenzake. #‎UsikateTamaa‬