January 29, 2014

WAZIRI MKUCHIKA AELEZA SABABU ZA TANZANIA

Add caption
MOSHI, Tanzania
WAZIRI wa Nchi ofisi ya Rais anayeshuhulikia Utawala Bora, Kaptein mstaafu, George Mkuchika amesema migogoro ya ardhi, mauaji ya maalbino na vikongwe, wanachi kujichukulia sheria mikononi, rushwa pamoja na ujangili zinadaiwa kuwa moja ya sababu zinazochangia kuporomoka kwa Tanzania katika viwango vya utawala bora duniani.
Mkuchika aliyasema hayo alipokuwa akizungumza katika kikao cha 30 cha kamati ya ushauri wa mkoa wa Kilimanjaro (RCC) kikao ambacho ni cha kwanza kwa mwaka 2014 na maalum kwa ajili ya kujadili vipauumbele vya Bajeti ya Mkoa huo kwa mwaka 2014/2015.

Kaptein Mkuchika alisema kutokana na taarifa zilizotolewa hivi karibuni, Tanzania inashika nafasi ya pili kwa utawala bora nyuma ya Rwanda kwa nchi za ukanda wa Afrika mashariki nyuma ya Rwanda, 17 katika ukanda wa Afrika na 102  kati ya nchi 176  duniani ambapo kwa mujibu wa taarifa hizo Tanzania imeshuka kiwango katika ukanda wa Afrika katika kipindi cha miaka miwili.

Alisema katika taarifa hizo, Tanzania ilikuwa ikishika nafasi ya 10 miaka miwili iliyopita na kuongeza kuwa kuporomoka huko kunatokana na kukithiri kwa ukiukwaji wa haki za binadamu, mauaji ya albino na vikongwe, mapigano ya wakulima na wafugaji, Ujangili, ambapo zaidi ya watu kumi walikufa mkoani Manyara.
MAUAJI YATIKISA POLISI.

MAUAJI YATIKISA POLISI.

January 29, 2014
Mkuu wa Polisi nchini, IGP Ernest Mangu.
*********
Mauaji ya kutisha yametikisha wilaya ya Tarime kiasi cha kumfanya Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Ernest Mangu, kutuma timu maalum kutoka makao makuu ya jeshi hilo inayohusisha kamisheni ya Operesheni kufanya uchunguzi.

Hatua ya kupelekwa kwa timu hiyo inatokana na mauaji ya mfululizo katika mji wa Tarime ambayo ipo kwenye himaya ya Kanda Maalum ya Polisi ya Tarime na Rorya ambayo yametokea kwa watu wanane katika kipindi cha siku tatu.

 
Mauaji hayo yanadaiwa kufanywa na jambazi mwenye silaha katika mji wa Tarime mkoani Mara kwa siku tatu kuanzia Jumatatu hadi jana.

Mmoja wa watu waliouawa ni askari mstaafu wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Koplo Zakaria Chacha Mwita ambaye ni mtoto wa marehemu Meja Jenerali Mwita Marwa.

Pia wamo aliyekuwa Mhandisi Ujenzi Wilaya ya Rorya, aliyetajwa kwa jina la David Mwasi Misiwa.

Wengine ni mfanyabiashara, Samuel Richard Mohenga na huku Jeshi la Polisi likisema kuwa linaendesha msako.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Tarime/Royra, Justus Kamugisha, alithibitisha kutokea kwa mauaji hayo na kusema kuwa mtu anayesadikiwa kuwa jambazi akiwa na bunduki kwa siku tatu kuanzia Januari 26, mwaka huu usiku aliua watu saba kwa kuwapiga risasi  na kujeruhi kadhaa.

Aliwataja wengine kuwa ni mwendesha bodaboda, mkazi wa kijiji cha Nkende, Juma  Marwa Nyaitara, Erick Lucas Makanya, mfanyabiashara  wa bucha mkazi wa kijiji cha Rebu, Juma Mwita Mroni na mkazi wa kijiji cha Kenyamanyori, Robert Chacha Kisiri.

Jana asubuhi, wakazi wa mji wa Tarime na vitongoji vyake walimfananisha mtu aliyekuwa amevaa koti refu na mtuhumiwa wa mauaji hayo na kutaka kumshushia kipigo, lakini aliokolewa na polisi waliorusha risasi hewani na kumpeleka katika kituo cha polisi.

Kamanda Kamugisha aliwashauri wananchi kutoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi kwa kutoa taarifa mara watakapomuona mtuhumiwa.
January 29, 2014

*MAHAKAMA YA KISUTU YAWAACHIA HURU WANAHABARI KIBANDA,MAKUNGA NA MAKADA WA CHADEMA WASHINDA KESI YA UCHOCHEZI

Habari zilizoufikia mtandao huu hivi punde zinasema kuwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ya jijini Dar es Salaam  imewaachia huru aliyekuwa Mhariri Mtendaji wa Gazeti la Tanzania Daima ambaye kwa sasa ni Mhariri Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya New Habari (2006) Ltd, Absalom Kibanda,  Meneja Uendeshaji Biashara wa Kampuni ya Mwananchi Communications Ltd (MCL), Theophil Makunga, Mwenyekiti wa zamani wa Chadema Mkoa wa Arusha, Samson Mwigamba. 
Mahakama hiyo imetowaachia huru watuhumiwa hao waliokuwa wakikabiriwa na kesi ya iliydaiwa kuwa ilikuwa ni uchochezi baada ya kutoa hukumu leo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi na watuhumiwa hao kuibuka kidedea kutokana na ushahidi wa upande wa mashitaka kutojitokeza mahakamani hapo.
January 29, 2014

*MSANII WA BONGO MOVIE ALIYEJINYONGA GESTI HUYU HAPA SOMA CHANZO

 
 Marehemu Victor Peter enzi za uhai wake.
Na Mwandishi Wetu
MSANII Victor Peter kutoka Bongo Movie amefariki dunia usiku wa juzi kuamkia jana 28/01/2014 kwa kujinyonga katika gest moja iliyotambulika kwa jina la SAFARI JUNIOUR iliyoko maeneo ya Kisosora mkoani Tanga.

Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospitali ya Bombo mkoani Tanga .

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi, mmoja kati ya wasanii walioshirikishwa na marehemu katika filamu yake ya mpya ya mwisho inayokwendakwa jina la Chozi, aliyokuwa akirekodi kabla ya kujinyonga, ambayo hadi sasa  bado haijatoka, Msanii huyo aliyetambulika kwa jina la Koba alisema kuwa ''Siku moja kabla ya tukio hilo Victor, alifanya nao Shooting ya filamu iliyotambulika kwa jina OUR FAMILY ambayo ilikuwa ndio filamu ya pili ya marehemu Vicktor tangu ajikite katika tasnia ya filamu Bongo Movie.
January 29, 2014

KUELEKEA KILELE CHA MIAKA 37, CCM YAJIVUNIA MAFANIKIO YAK

Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akizungumza na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa mkutano wa CCM Mkoa wa Mbeya.
*********************************

   Wakati CCM inatimiza miaka 37 tangia kuanzishwa kwake februari 5 mwaka 1977,Chama hicho kinajivunia sana mafanikio makubwa kiliyopata hasa katika kudumisha Umoja na Mshikamano kwa  Watanzania ,kutunza na kuilinda Amani ya nchi hii na kujenga misingi imara ya uchumi wa nchi,akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa mikutano CCM Mkoa wa Mbeya Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye  alisema  sherehe za miaka 37 zimeanza nchi nzima na zilizinduliwa rasmi tarehe 26 na Makamu Mwenyekiti wa CCM (Zanzibar) Dk.Ali Mohamed Shein Unguja Zanzibar.


  Kilele cha sherehe hizi  kitakua tarehe 2 februari ,Nape alisema “kwa nini tarehe mbili na sio tano ni kwa sababu tarehe tano ni siku ya kazi hivyo tumeona tufanye tarehe mbili ili tuwaruhusu watu wengi zaidi waweze kushiriki”
January 29, 2014
BREAKING NEWssssssssssssss WANAHABARI KIBANDA NA MAKUNGA NA MAKADA WA CHADEMA WASHINDA KESI YA UCHOCHEZI

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam  imetoa hukumu ya kesi ya makala iliyodaiwa kuwa ya uchochezi iliyokuwa inawakabili Meneja Uendeshaji Biashara wa Kampuni ya Mwananchi Communications Ltd (MCL), Theophil Makunga, Mwenyekiti wa zamani wa Chadema Mkoa wa Arusha, Samson Mwigamba na aliyekuwa Mhariri Mtendaji wa Gazeti la Tanzania Daima ambaye sasa ni Mhariri Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya New Habari (2006), Absalom Kibanda  ambapo wameibuka kidedea baada ya ushahidi upande wa mashitaka kutojitoshelez