Mamlaka ya Vitambulisho Vya Taifa (NIDA) Umezindua Rasmi Zoezi La Utambuzi Na Usajili Wa Watu Katika Mkoa Wa Tanga

October 09, 2014


 
Joseph Makani, Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho (NIDA) akizungumza wakati wa uzinduzi. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe. Chiku Gallawa ,  Katibu Tawala Mkoa wa Tanga Bw.Salum Mohamed Chima (Alhaj) na Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Mhe. Halima Dendego

WAKUU wa Wilaya, Wakurugenzi, Watendaji katika ngazi zote Tarafa, Kata, Mitaa, Vijiji na Vitongoji, Viongozi wa Dini na Viongozi wa Vyama vya Siasa wameagizwa kuonyesha ushirikiano  katika kuhakikisha jukumu la utambuzi na usajili wa watu linaenda sawasawa na maagizo ya Serikali .
Msisitizo huo umetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe. Chiku Gallawa ambaye ameahidi kutoa ushirikiano wakati akizindua rasmi zoezi la utambuzi na usajili wa watu uliofanyika mapema leo asubuhi katika ukumbi wa mikutano wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa.
 Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho( NIDA) Bw. Joseph Makani amewataka wakazi wa Tanga kujitokeza na kutoa ushirikiano katika zoezi zima kwani zoezi  hilo Mkoani Tanga ni utekelezaji wa Mpango wa Usajili wa Wakazi waishio Kihalali Nchini kwa lengo la kuwapatia vitambulisho vya Taifa kwa hadhi ya raia, Wageni wakazi na Wakimbizi.
“Fichueni wale ambao hawastahili kupata vitambulisho vya uraia kwa kutoa taarifa katika ofisi za uhamiaji na polisi ili taifa lisije likaingia katika hatari ya kuwasajili wageni kama raia”amesisitiza Makani.
 Zoezi la Utambuzi na Usajili Mkoani Tanga linategemea kuanza Oktoba 12 mwaka huu. Wananchi wanaombwa kuhakikisha wanajisajili kwa wenyeviti wa mitaa ili kurahisisha zoezi hilo.

Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe. Chiku Gallawa akizindua rasmi zoezi la utambuzi na usajili wa watu
 Katibu Tawala Mkoa wa Tanga Bw. Salum Mohamed Chima ( Alhaji) akizunguza muda mchache kabla ya uzinduzi
Baadhi ya viongozi wawakilishi kutoka katika Wilaya za Tanga wakati wa uzinduzi,Picha zote na stori kwa hisani ya http://mkoatanga.blogspot.com

MUJUNI KUZIHUKUMU SIMBA NA YANGA OKTOBA 18

October 09, 2014


MWAMUZI Israel Mujuni Nkongo anatarajiwa kuchezesha pambano la watani wa jadi la ligi kuu Tanzania Bara kati ya Simba na Yanga.

Pambano hilo litachezwa Oktoba 18 mwaka huu katika Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.
 

Akizungumza Dar es Salaam jana, Mtendaji mkuu wa Bodi ya Ligi Tanzania, Silas Mwakibinga alisema waamuzi wa pembeni watakuwa ni Fednandi Chacha kutoka Mwanza na John Kanyenye kutoka Mbeya.

Alisema Mwamuzi wa mezani atakuwa ni Hashimu Abdalah na Kamishna wa mechi hiyo ni Salum Kikwamba.

Alisema maandalizi ya mechi hiyo yanaendelea vema huku timu zote zikiwa katika maandalizi kwa ajili ya mchezo huo.

Tayari Simba wamekwea pipa juzi kuelekea Afrika Kusini kujiandaa na mchezo huo huku Yanga ikiendelea kujifua katika viwanja vya Loyola Dar es Salaam.

Mwakibinga alisema mbali na mechi hiyo pia kwa upande wa timu nyingine mechi zitaendelea kama kawaida ambapo Mtibwa Sugar itacheza dhidi ya Polisi Morogoro katika uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.

Pia Ndanda FC itashuka dhidi ya Ruvu Shooting katika uwanja wa Nangwanda mjini Mtwara, Kagera Sugar dhidi ya Stand United utakaochezwa uwanja wa Kaitaba na Coastal Union dhidi ya Mgambo JKT katika uwanja wa Mkwakwani Tanga.

Alisema pia siku hiyo kutakuwa na mechi kati ya Azam na Mbeya City utakaochezwa uwanja wa Sokoine jijini Mbeya na Tanzania Prison itaumana dhidi ya JKT Ruvu katika uwanja wa Azam Complex Chamazi Dar es Salaam.
MESUT OZIL NJE YA DIMBA KWA WIKI 10-12 AKIUGUZA JERAHA LA GOTI

MESUT OZIL NJE YA DIMBA KWA WIKI 10-12 AKIUGUZA JERAHA LA GOTI

October 09, 2014


Mshambuliaji wa kimataifa wa Arsenal, Mezut Ozil, ameondoka leo kutoka katika kambi aliyokuwa na timu yake ya taifa ya Ujerumani huko mjini Frankfurt na kuelekea mjini Munich kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi wa maumivu ya goti yanamsumbua kwa sasa ambayo ameyapata wakati akifanya mazoezi na timu yake hiyo ya taifa ikiwa ni maandali ya kuelekea katika mashinda ya kuwania kufuzu kushiriki michuano ya mataifa ya Ulaya 2016.
Ozil alikuwa ni sehemu ya kikosi cha Ujerumani, mabingwa wa kombe la dunia msimu uliopita, ambao walikuwa wanajiandaa kukipiga dhidi ya Poland na baadaye Jamuhuri ya Iland kuwani tiketi za kushiriki fainali za mataifa ya Ulaya ya 2016, lakini ndoto zake za kuendelea kuwa sehemu ya kikosi hicho zinaonekena kufifia kwa sababu ya majeraha hayo ambayo mpaka sasa haijawekwa bayana kwamba itamuweka nje ya dimba kwa muda gani.
Hili pia linaweza kumpa Arsene Wenger presha, kwa kuwa Ozil ni mmoja kati ya wachezaji anao wategemea sana kikosini hapo kwa sasa baada ya kuwa na idadi kubwa ya majeruhi mapema sana msimu huu. Wachezaji wengine ambao ni majeruhi katika klabu ya Arsenal mbali na Mesut Ozil ni; Olivia Giroud, Mathieu Debuchy Aron Ramsey, Mikel Arteta pamoja naye Theo Walcott ingawaje baahi yao wanaweza kurudi uwanjani muda mfupi.

MAKUNDI:
KUNDI A:
Netherlands, Czech Republic, Turkey, Latvia, Iceland, Kazakhstan.
KUNDI B: Bosnia-Hercegovina, Belgium, Israel, Wales, Cyprus, Andorra.
KUNDI C: Spain, Ukraine, Slovakia, Belarus, FYR Macedonia, Luxembourg.
KUNDI D: Germany, Republic of Ireland, Poland, Scotland, Georgia, Gibraltar.
KUNDI E: England, Switzerland, Slovenia, Estonia, Lithuania, San Marino.
KUNDI F: Greece, Hungary, Romania, Finland, Northern Ireland, Faroe Islands.
KUNDI G: Russia, Sweden, Austria, Montenegro, Moldova, Liechtenstein.
KUNDI H: Italy, Croatia, Norway, Bulgaria, Azerbaijan, Malta.
KUNDI I: Portugal, Denmark, Serbia, Armenia, Albania.


Timu mbili za juu toka kila Kundi pamoja na Timu moja Bora iliyoshika Nafasi ya 3 kwenye Makundi zitatinga Fainali na Timu 8 zilizobaki ambazo zitamaliza Nafasi ya Tatu zitapangiwa Mechi maalum za Mchujo ili kupata Timu 4 za mwisho kuingia Fainali.
Mechi za Makundi zilianza Septemba 2014 na zitaendelea hadi Oktoba 2015.

EURO 2016
RATIBA:

Alhamisi Oktoba 9
21:45 Slovenia vs Switzerland KUNDI E
21:45 Moldova vs Austria KUNDI G
21:45 Belarus vs Ukraine KUNDI C
21:45 Sweden vs Russia KUNDI G
21:45 Lithuania vs Estonia KUNDI E
21:45 Macedonia vs Luxembourg KUNDI C
21:45 Liechtenstein vs Montenegro KUNDI G
2145 England vs San Marino KUNDI E
2145 Slovakia vs Spain KUNDI C


Ijumaa Oktoba 10
2145 Cyprus vs Israel KUNDI B
2145 Malta vs Norway KUNDI H
2145 Netherlands vs Kazakstan KUNDI A
2145 Latvia vs Iceland KUNDI A
2145 Turkey vs Czech Republic KUNDI A
2145 Bulgaria vs Croatia KUNDI H
2145 Belgium vs Andorra KUNDI B
2145 Wales vs Bosnia And Herzegovina KUNDI B
2145 Italy vs Azerbaijan KUNDI H


Jumamosi Oktoba 11
19:00 Romania vs Hungary KUNDI F
19:00 Scotland vs Georgia KUNDI D
19:00 Armenia vs Serbia KUNDI I
19:00 Ireland vs Gibraltar KUNDI D
2145 Poland vs Germany KUNDI D
2145 Northern Ireland vs Faroe Islands KUNDI F
2145 Finland vs Greece KUNDI F
2145 Albania vs Denmark KUNDI I

Jumapili Oktoba 12
1900 Austria vs Montenegro KUNDI G
1900 Estonia vs England KUNDI E
1900 Russia vs Moldova KUNDI G
1900 Ukraine vs Macedonia KUNDI C
2145 Luxembourg vs Spain KUNDI C
2145 Belarus vs Slovakia KUNDI C
2145 Sweden vs Liechtenstein KUNDI G
2145 Lithuania vs Slovenia KUNDI E


Jumatatu Oktoba 13

19:00 Kazakstan vs Czech Republic KUNDI A
21:45 Malta vs Italy KUNDI H
21:45 Norway vs Bulgaria KUNDI H
21:45 Bosnia And Herzegovina vs Belgium KUNDI B
21:45 Latvia vs Turkey KUNDI A
21:45 Iceland vs Netherlands KUNDI A
21:45 Croatia vs Azerbaijan KUNDI H
21:45 Andorra vs Israel KUNDI B
21:45 Wales vs Cyprus KUNDI B

Jumanne Oktoba 14
21:45 Denmark vs Portugal KUNDI I
21:45 Poland vs Scotland KUNDI D
21:45 San Marino vs Switzerland KUNDI E
21:45 Germany vs Ireland KUNDI D
21:45 Faroe Islands vs Hungary KUNDI F
21:45 Greece vs Northern Ireland KUNDI F
21:45 Finland vs Romania KUNDI F
21:45 Serbia vs Albania KUNDI I
21:45 Gibraltar vs Georgia KUNDI D
BAADA YA KIPA DE GEA KUTISHIA KUONDOKA OLD TRAFFORD, PETER CECH NAE ATINGISHA KIBERITI DARAJANI ATISHIA KUONDOKA KAMA HATAKUWA MLINDA LANGO NAMBA MOJA

BAADA YA KIPA DE GEA KUTISHIA KUONDOKA OLD TRAFFORD, PETER CECH NAE ATINGISHA KIBERITI DARAJANI ATISHIA KUONDOKA KAMA HATAKUWA MLINDA LANGO NAMBA MOJA

October 09, 2014


Cech akitolewa nje baada ya kuumia bega la kushoto wakati Chelsea ikabiliana na Atletico Madrid dimbani Vicente Calderon msimu uliopita katika michuano ya klabu bingwa barani Ulaya mchezo ambao ulikwisha kwa timu kutoka suluhu.
Mlinda lango nyota na mwenye heshima kubwa Stanford Bridge, Petre Cech amefunguka kwenye vyomba vya habari leo hii na kusema kama ataendelea mlinda lango chaguo la pili (namba 2) katika klabu ya Chelsea, ni baro akaondoka na kutafuta klabu nyingine itakayompa nafasi ya kwanza.
Cech alipata jera kubwa katika bega lake la kushoto msimu uliopita wakati Chelsea ikipepetana na Atletical Madrid mwezi July katika mashindano ya klabu bingwa barani Ulaya hali iliyomfanya yeye kumalizia msimu wa 2013/2014 akiwa nje ya dimba tangu pale alipo pata majeraha na nafasi yake kuchukuliwa na Mark Schwarzer kabla ya Thibault Courtois kurejea Chelsea akitokea Atletical Madrid alipokuwa akicheza kwa mkopo. 
 
Petre Cech ni mmoja wa wachezaji nguli katika klabu ya The Blues, kwani mpaka sasa amedumu klabu hapo kwa takaribani miaka 10, huku akifanikiwa kuichezea klabu hiyo michezo 500. Lakini, tangu msimu wa 2014/2015 uanze Cech hakuendelea kuwa golikipa chaguo namba moja katika klabu ya Chelsea kwani mlinda lango anayechipukia kwa kasi,Thibault Courtois 22, ameoneka kufanya vizuri sana kitendo kilichomfanya Jose Mourinho kumuamini zaidi.

Huyu pia ni goli kipa bora wa ligi kuu nchiniUingereza msimu uliopita wa 2013/2014
Cech amekariri akilalama kuwa, haoni sababu yeye kusugua benji akiwa kama chaguo namba mbili kwa Mourinho kwani kuna michezo mikubwa na migumu ipo mbele yake kama vile, michuano ya mabingwa wa Ulaya ya 2016 pamoja na majukumu makubwa aliyonayo katika timu ya taifa, hivyo kucheza kama chaguo namba mbili kwa Chelsea anaona ni hatari sana kwani anaamini itadhoofisha uwezo wake.
Petre Cech alichechea Chelsea kwa mara ya kwanza tangu msimu huu uanze wakati Chelsea ikicheza dhidi ya Arsenal Juma pili iliyopita Dimbani Stanford Bridge, baada ya Courtois kuumia. Mchezo huo ulimalizika kwa Chelsea kuibuka na ushindi wa magoli 2-0, kichapo ambacho kiliendelea kumpa Arsena rekodi mbaya ya kuchezea kichapo mara kwamara wanapokutana na Chelsea kwa muda mrefu.

REDD'S MISS TANZANIA 2014 KUFANYIKA MLIMANI CITY JUMAMOSI HII

October 09, 2014



Mkurugenzi wa Kampuni ya Rino International Agency ambao ni waratibu wakuu wa Mashindano ya Miss Tanzania,Hashim Lundenga (kulia) akizungumza na vyombo vya habari jijini Dar es Salaam leo,juu ya onyesho la Redd's Miss Tanzania 2014 linalotarajiwa kufanyika Oktoba 11,2014 katika Ukumbi wa Mlimani City,Jijini Dar.Katikati ni Meneja wa Kinywaji cha Redd's ambao ni Wadhamini Wakuu wa Mashindano hayo,Victoria Kimaro na kushoto ni Meneja Maria Stopes Tanzania,Anna Shanalingigwa.Picha zote na Othman Michuzi.

Meneja wa Kinywaji cha Redd's ambao ni Wadhamini Wakuu wa Mashindano ya Miss Tanzania,Victoria Kimaro (kushoto) akizungumzia zawadi watakayotoa kwa Washindi watakaopatikana kwenye Shindano hilo la Redd's Miss Tanzania 2014,ambapo mwaka huu mshindi wa kwanza katika kinyang'anyiro hicho atajinyakulia kitita cha sh. Mil. 18 taslim huku washindi wengine wakiendelea kuondoka na zawadi mbali mbali.Katikati ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Rino International Agency ambao ni waratibu wakuu wa Mashindano ya Miss Tanzania,Hashim Lundenga na kulia ni Meneja wa Hoteli ya JB Belmont,Gillian Macheche pamoja na Afisa Habari wa Miss Tanzania,Hidan Ricco.

Sehemu ya Wanahabari pamoja na Warembo watakaoshiriki kwenye kinyang'anyiro cha Redd's Miss Tanzania 2014 wakimsikiliza kwa makini Mkurugenzi wa Kampuni ya Rino International Agency ambao ni waratibu wakuu wa Mashindano ya Miss Tanzania,Hashim Lundenga alipokuwa akizungumza.




Sehemu ya Warembo watakaoshiriki kwenye kinyang'anyiro cha Redd's Miss Tanzania 2014

Warembo watakaoshiriki kwenye kinyang'anyiro cha Redd's Miss Tanzania 2014 wakipata "SELFIE" mwanana kabisa.

*MASHINDANO YA SHIMIWI YAFIKIA HATUA YA NUSU FAINALI MJINI MOROGORO

October 09, 2014


 Timu ya kuvuta kamba ya wanawake ya Ikulu wakiwavuta timu ya Wizara ya Kilimo, Ushirika na Chakula (hawapo pichani) wakati wa mashindano ya kuingia hatua ya nusu fainali mashindano ya SHIMIWI  leo mjini Morogoro ambapo Ikulu imefuzu kucheza hatua hiyo.
 Timu ya kuvuta kamba ya wanaume ya Ikulu wakiwavuta timu ya Wakala wa Hifadhi ya Chakula ya Taifa (NFRA- hawapo pichani) wakati wa mashindano ya kuingia hatua ya nusu fainali mashindano ya SHIMIWI leo mjini Morogoro ambapo Ikulu imefuzu kucheza hatua hiyo.
 Mshindi wa kwanza wa mchezo wa drafti wanaume Salumu Simba (kushoto) kutoka RAS Dodoma akichuana na mshindi wa tatu wa mchezo huo Ramadhani Mtenga (kulia)kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo wakati wa mashindano ya SHIMIWI leo mjini Morogoro.
 Mshindi wa kwanza wa mchezo wa drafti wanaume Salumu Simba (kulia) kutoka RAS Dodoma akichuana na mshindi wa tatu wa mchezo huo Dkt. Idris Lukindo (kushoto) wakati wa mashindano ya SHIMIWI leo mjini Morogoro.
 Baadhi ya watumishi wanaoshabikia mchezo wa drafti wakishuhudia pambano la kuwatafuta  washindi wa mcheo huo  leo katika kiwanja cha Jamhuri mjini Morogoro.
 Mchezaji wa timu ya mpira wa pete Ikulu Mwadawa Twalibu (GA) akimiliki mpira wakati wa mchezo wa robo fainali kati ya timu ya Ikulu na Bunge wa kumsaka mshindi atakayecheza nusu fainali, timu ya Ikulu imefuzu kwa kuwashinda timu ya Bunge kwa magoli 67 kwa 24.
 Wachezaji wa timu ya mpira wa miguu ya Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo (waliovalia sare ya bluu) wakisalimiana na wachezaji wa mchezo huo kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu (waliovalia sare ya rangi ya machungwa) kabla ya mchezo wa robo fainali ambapo timu ya Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo wameibuka washindi na kuingia nusu fainali katika mshindano ya SHIMIWI kwa kuifunga timu ya Ofisi ya Waziri Mkuu 1- 0.
 Timu ya mpira wa miguu ya Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo (kushoto) na timu ya Ofisi ya Waziri Mkuu (kulia) wakiomba dua kabla ya mchezo wa hatua ya robo fainali leo mjini Morogoro.
Baadhi ya watumishi wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo wakishangilia ushindi wa timu yao wa kuifunga timu ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa goli 1- 0 leo mjini Morogoro. Picha zote na Eleuteri Mangi- MAELEZO
**************************************
Na Eleuteri Mangi-MAELEZO
Michuano ya Shirikisho la Michezo ya Wizara na Idara za Serikali (SHIMIWI) imefikia hatua ya nusu fainali kwa michezo ya kuvuta kamba, mpira wa miguu na mpira wa pete kwenye mashindano yanayoendelea mjini Morogoro.

Katika mchezo wa kuvuta kamba timu za wanaume zilizoingia hatua hiyo ni Ikulu, Uchukuzi, Hazina na Mahakama wakati kwa upande wa wanawake timu zilizoingia hatua hiyo ni  Ikulu, Uchukuzi, Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) na RAS Iringa.
Kwa upande wa mpira wa pete timu zilizofuzu ni Ikulu, Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Wizara ya Uchukuzi na timu ya Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma.
Wakati huo huo, timu zilizokata tiketi ya kucheza hatua ya nusu fainali kwa mpira wa miguu ni Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Wizara ya Uchukuzi, Idara ya Mahakama na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi.

Aidha, mchezo wa drafti umefikia ukingoni ambapo kwa wanaume bingwa wa mchezo huo imedchukuliwa na Salumu Simba kutoka timu ya RAS Dodoma, nafasi ya pili imekwenda kwa Dkt. Idris Lukindo kutoka Wakala wa Jiolojia Tanzania (GST) na nafasi ya tatu  imekwenda kwa Ramadhani Mtenga kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo.

Kwa upande wa wanawake, Leocadia Mwang’ombe kutoka RAS Morogoro ameibuka bingwa kwa mchezo wa drafti huku nafasi ya pili imekwenda kwa Sophia Mpema kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi na nafasi ya tatu imeenda kwa Madaraka Kabaka kutoka RAS Mwanza.

Mashindano hayo yanatarajiwa kufikia tamati siku ya Jumamosi Oktoba 11 mwaka huu na kuhusisha fainali za michezo mbalimbali ambazo zitachezwa kuhitimisha mashindano hayo ambapo yatafungwa rasmi kwa maandamano ya wanamichezo yatakayopokewa na Mgeni Rasmi atakayefunga michezo hiyo.

DKT JAKAYA MRISHO KIKWETE APOKEA RASIMU YA MWISHO YA KATIBA INAYOPENDE​KEZWA OKTOBA 08,2014 – UWANJA WA JAMHURI DODOMA

October 09, 2014


 Mwenyekiti wa Bunge maalum la katiba Mhe.Samuel Sitta akikabidhi rasimu ya katiba inayopendekezwa kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Jakaya Mrisho kikwete na Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dkt.1mohamed Ali Shein katika hafla iliyofanyika katika uwanja wa michezo wa Jamhuri mjini Dodoma.
Rais jakaya Kikwete na Rais wa Zanzibar, Dk. Alli Mohamed Shein wakionesha Katiba hiyo iliyopendekezwa na Bunge Maalum la Mabadiliko ya Katiba
October 09, 2014

KATIBU MKUU WA CCM NDUGU ABDULRAHMAN KINANA AENDELEA NA ZIARA JIMBO LA KILOLO

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwasalimu wakazi wa Kilolo Mnadani waliojitokeza kumlaki katika ziara yake wilayani Kilolo Kinana yuko mkoani Iringa kwa ziara ya siku sita ya kikazi akiongozana na Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi, Siasa na Uenezi, Ziara hiyo ina lengo la kukagua utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2014 na kuhimiza uhai wa Chama.

MBUNGE wa jimbo la Kilolo mkoani Iringa Profesa Peter Msolla akiwasalimia wananchi wakati wa mapokezi ya Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kufyatua matofali ya kikundi cha vijana cha Muungano ambacho kina jumla ya vijana arobaini waliopata mafunzo ya kufyatua matofali na ujenzi.
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiongea na wajumbe wa halmashauri kuu ya wilaya ya Kilolo katika ukumbi wa halmashauri ya wilaya ya Kilolo.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa kijiji cha Utengule kata ya Ihimbo ambapo aliwaambia wananchi hao kuwa uchaguzi wa Serikali za mitaa mwezi Desemba CCM itashinda kwa kishindo.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wananchi  wa kijiji cha utengule kata ya Ihimbo wilaya ya Kilolo mkoani Iringa ambapo aliwaambia viongozi wa Kata na Vijiji pamoja na ngazi ya wilaya wafanye mikutano na wananchi wao na waruhusu maswali ilikujua changamoto zinazowakabili wananchi .
 Mwenyekiti wa Kijiji cha Utengule Ndugu Pancras Mkakatu ambaye ni mwanachama wa Chadema akiongea na wananchi mbele ya Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana ambapo  alimpongeza sana Katibu Mkuu wa CCm kwa kazi nzuri anayofanya na kueleza kuwa yeye ni CCM ila alitoka tu kwa sababu ya migongano na viongozi wengine wa CCM .
 Zahanati ya Kijiji cha Utengule ambayo imekamilika ilabado haijapata madaktari
 Mwenyekiti wa Kamati ya ujenzi wa shule ya sekondari ya Uwindi Ndugu Charles Kigwile akiuliza swali linalohusu ujenzi wa madarasa ya shule hiyo ambao umesimama.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akikabidhiwa mkuki kama ishallah ya kuwa Mtemi wa Wahehe.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwashukuru wananchi wa kijiji cha Utengule kwa kumpa heshima ya kuwa Mtemi kwenye kijiji chao
 Katibu Mkuu wa CCM akiwa kwenye picha ya pamoja na Watemi wenzake wa kijiji cha Utengule.
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwaaga wananchi waliofurika kwa wingi kwenye mkutano wake.
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipeana mikono ya kwa heri na wananchi wa kijiji cha Utengule.
 Madarasa ya shule ya msingi Iwindi wilayani Kilolo mkoani Iringa
Mwalimu Josephine Konga wa Shule ya msingi akimuonyesha  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana uchache wa vyumba vya madarasa katika shule hiyo kiasi kupata shida sana katika kufundisha.