ANGALIA JINSI ZITTO ALIVYOITEKA KIGOMA,MAPOKEZI YAKE YASHTUA WENGI

March 14, 2015

Mh zitto kabwe baada ya chama chake cha CHADEMA kutangaza kumfukuza uanachama ndani ya chama hicho ameamua kufanya ziara ya siku tatu ndani ya kigoma kuzumgumza na wananchi wake juu ya hali ya kisiasa inayomkabili kwa sasa,hizi hapa ni baadhi picha za mapokezi yake kigoma 

Ikiwa bado sakata la kufukuzwa uanachama kwa mbunge wa kigoma kaskazini (CHADEMA) mh ZITTO KABWE linaendelea kuchukua nafasi katika vichwa vya watanzania na wapenda siasa,mbunge huyo ameanza kufanya ziara ya siku tatu jimboni kwake kuzungumza na watanzania mbalimbali.
Akiwa katika ziara yake MBUNGE wa Kigoma Kaskazini,Zitto Kabwe(Chadema),amewataka wakazi wa mkoa wa kigoma wasisikitishwe na mambo yanayomkabili kwa sasa kwa kile alichoeleza kuwa asilimia kubwa ya wanasiasa makini walishapitia misuko suko kama yake.
Amewaeleza kuwa jambo la msingi ni kumuunga mkono katika hatua yoyote atakayochukua kwa ajili ya wanakigoma na Taifa kwa ujumla katika kumaliza mgogoro uliopo baina ya Chama chake na yeyeZitto ametoa kauli hiyo leo mjini Kigoma alipokutana na viongozi 250 kwenye mkutano wa ndani uliohusisha viongozi kutoka katika kila kijiji kwenye jimbo la Kigoma kaskazini yenye jumla ya vijiji 45.Aliwataja baadhi ya wanasiasa waliopita katika hatua kama yake na baadae wakageuka washindi kuwa ni Maalim Seif Sharif Hamad(Tanzania),Mahathir Mohamed(Malaysia na Indira Gandhi wa India.“Msinililie mimi kwa kuwa haya ni mapito ya kila mwanasiasa Makini,wengi walio makini walitofautiana na vyama vyao kwa sababu ya maslahi ya mataifa yao,wapo walioanzisha vyama baada ya hali hiyo na wakashinda na wapo waliopigiwa magoti na vyama vyao baada ya kugundua walichofanya si sahihi, hivyo jukumu kubwa ni kuniunga Mkono”alisema Zitto.
Alisema mpaka sasa hajapewa taarifa yoyote ya kusitishwa kwa Ubunge wake na kama hali hiyo ikijitokeza atarudi kuwafahamisha juu ya hatua atakayochukua
Zitto yupo mjini Kigoma kwa ziara ya siku tatu,ambapo atawatembelea wakulima wa mradi wa Kahawa walio katika mfuko wa hifadhi ya Jamii(NSSF), pamoja na kukabidhi gari aina ya Ambulance katika kituo cha Afya Nyarubanda na kisha kufanya mikutano miwili ya hadhara.
Juzi Mwanasheria mkuu wa Chadema Tundu Lissu,alitangaza hadharani kuvuliwa uanachama kwa Zitto kutokana na kushindwa katika kesi aliyofungua kupinga asijadiliwe na Chama Chake

SIMBA SC WAICHAPA MTIBWA SUGAR BAO 1-0 TAIFA,OKWI AWAPA RAHA

March 14, 2015
BAO la Emmanuel Anord Okwi dakika ya 90 ushei limeipa Simba SC ushindi wa 1-0 dhidi ya Mtibwa Sugar Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam jioni hii katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
Simba SC sasa inafikisha pointi 29 baada ya mechi 18 na kuendelea kukamata nafasi ya tatu, nyuma ya mabingwa watetezi, Azam FC pointi 30 za mechi 16 sawa na vinara Yanga SC, wenye pointi 31.
Okwi alifunga bao hilo, wakati tayari baadhi ya wapenzi wa Simba SC wameanza kutoka uwanjani, wakiamni matokeo ni sare.  Mganda huyo, alifunga baada ya kupata pasi ya Abdi Banda na kumchambua vizuri kipa aliyefanya kazi nzuri leo, Said Mohamed Kasarama.


Emmenuel Okwi akimtoka beki wa Mtibwa Sugar, Said Mkopi katika mchezo wa leo

Beki wa Simba SC, Hassan Kessy akimtoka kiungo wa Mtibwa Sugar, Shaaban Nditi 
Mchezo huo uliochezeshwa na refa Abdallah Kambuzi wa Shinyanga, aliyesaidiwa na Yussuf Sekile wa Ruvuma na Abdallah Rashid wa Pwani, Simba SC ndiyo waliotawala na kutengeneza nafasi nyingi, lakini hawakuwa na bahati ya mapema.
Mshambuliaji wa zamani wa Simba SC, Mussa Hassan Mgosi aliiongoza vyema safu ya ushambuliaji ya Mtibwa Sugar akisaidiana na Ame Ally, lakini wakaishia kuisumbua tu ngombe ya Simba, iliyoongozwa na beki chipukizi, Hassan Isihaka.
Kikosi cha Simba SC kilikuwa; Ivo Mapunda, Hassan Kessy, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Juuko Murushid, Hassan Isihaka, Jonas Mkude, Said Ndemla, Abdi Banda, Elias Maguri, Emmanuel Okwi na Simon Sserunkuma/Ramadhani Singano ‘Messi’ dk46. 
Mtibwa Sugar; Said Mohammed, Said Mkopi, Dacis Luhende, Salim Mbonde, Andrew Chikupe, Shaaban Nditi, Ally Sharrif, Henry Joseph, Ame Ally/Mohammed Mkopi dk66, Muzamil Selemba/Ally Yussuf dk86 na Mussa Hassan Mgosi/Vincent Barnabas dk75. 

MACHINGA WAMTAKA LOWASSA ACHUKUE FOMU YA URAIS

March 14, 2015
Wawakilishi wa Shirika la Umoja wa wamachinga Tanzania SHIUMA,pamoja na viongozi wa UVCCM kata za jiji la Mwanza wakiwa katika picha ya pamoja na Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa nyumbani kwake Ngarash Monduli mwishoni mwa wiki mara baada ya kumkabidhi mchango wa shilingi milioni moja ili achukue fomu kuwania urais kupitia CCM.Pia walimkabidhi Ngao na mkuki atakavyotumia katika safari yake ya matumaini.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akionesha kitambulisho cha uanachama wa shirikisho la Umoja wa wamachinga Tanzania (SHIUMA) baada ya kukabidhiwa na uongozi wa shirikisho hilo mwishoni mwa wiki huko Monduli.Pia alikabidhiwa shilingi milioni moja na ombi la kumtaka achukue fomu kuwania urais kupitia CCM.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akihesabu Fedha kiasi cha Shilingi Milioni 1, alizopewa na Shirika la Umoja wa Wamachinga Tanzania pamoja na Umoja wa Vijana wa CCM  (UVCCM) kata za jiji la Mwanza ili achukue fomu kuwania urais.

RAIS KIKWETE AFANIKISHA HARAMBEE YA KUCHANGIA UJENZI WA CHUO KIKUU CHA TUMAINI, 1.6BN/- ZAPATIKANA USIKU HUU DIAMOND JUBILEE HALL DAR ES SALAAM

March 14, 2015
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Naibu Waziri wa Elimu na Ufundi Mhe. Anne Kilango Malecela, Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dr Alex Gehaz Malasusa, Mwenyekiti wa Harambee hiyo na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Bw. Nehemia Mchechu na wachangiaji wakubwa katika harambee hiyo iliyofanyika usiku huu katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam ambapo jumla ya shilingi bilioni 1.6 kati ya shilingi bilioni 2 zinazohitajika zilipatikana. Michango hiyo ni ya kufanikisha upanuzi wa chuo hicho katika awamu ya pili.
 Rais Kikwete katika picha ya pamoja na wakuu wa majimbo ya KKKT, Wachungaji, Wainjilisti na wafanyakazi wa Parish na viongozi wengine
 Rais Kikwete katika picha ya pamoja na wakuu wa majimbo ya KKKT, Wachungaji, Wainjilisti na wafanyakazi wa Parish na viongozi wengine
 Rais Kikwete akipongezwa kwa kufanikisha harambee hiyo
Rais Kikwete katika picha ya pamoja na kamati ya maandalizi ya harambee hiyo iliyoongozwa na mwenyekiti wake Mzee Arnold Kilewo ( wa kwanza kulia mbele) baada ya harambee hiyo iliyofanyika usiku huu katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam ambapo jumla ya shilingi bilioni 1.6 kati ya shilingi bilioni 2 zinazohitajika zilipatikana. Michango hiyo ni ya kufanikisha upanuzi wa chuo hicho katika awamu ya pili.

Prof. Tolly Mbwette aagwa mkoani Manyara

March 14, 2015

Mwenyekiti wa Serikali ya wanafunzi wa chuo kikuu huria kituo cha Manyara, Mwalimu Pasian Siay akizungumza wakati wa hafla ya kumuaga Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu huria (OUT) Profesa Tolly Mbwette, iliyofanyika jana mjini Babati.
Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Dk Joel Nkaya Bendera, akizungumza jana mjini Babati wakati wa kumuaga Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu huria (OUT) Profesa Tolly Mbwette, (kushoto) na aliyepo kulia ni Mkuu wa wilaya ya Babati Crispin Meela.
Mkurugenzi wa chuo kikuu huria kituo cha Manyara Dk Joseph magali (kushoto) akimpongeza Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu huria nchini (OUT) Profesa Tolly Mbwette (kulia) baada ya kuvikwa vazi la jadi la jamii ya watu wa mkoa wa Manyara jana, kwenye hafla ya kumuaga profesa huyo ambaye amechaguliwa kuwa Mwenyekiti wa vyuo vikuu vya Afrika nzima.
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu huria nchini (OUT) Profesa Tolly Mbwette (kulia) akikabidhiwa cheti cha heshima jana na Mkurugenzi wa chuo kikuu huria kituo cha Manyara kwenye hafla ya kumuaga profesa huyo ambaye amechaguliwa kuwa Mwenyekiti wa vyuo vikuu vya Afrika nzima.
Mkuu wa Wilaya ya Babati Mkoani Manyara, Crispin Meela, akizungumza kwenye hafla ya kumuaga Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu huria (OUT) Profesa Tolly Mbwette, iliyofanyika jana mjini Babati.
Baadhi ya wakazi wa Mjini Babati Mkoani Manyara waliohudhuria hafla ya kumuaga Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu huria (OUT) Profesa Tolly Mbwette, alipoagwa jana kwenye kituo cha chuo hicho mjini Babati.
• WATU WATATU WANAOSADIKIWA KUWA NI MAJAMBAZI WAJARIBU KUFANYA UNYANG’ANYI WA KUTUMIA SILAHA KWA MFANYABIASHARA WA MADINI

• WATU WATATU WANAOSADIKIWA KUWA NI MAJAMBAZI WAJARIBU KUFANYA UNYANG’ANYI WA KUTUMIA SILAHA KWA MFANYABIASHARA WA MADINI

March 14, 2015

index 
WATU WATATU WANAOSADIKIWA KUWA NI MAJAMBAZI WAJARIBU KUFANYA UNYANG’ANYI WA KUTUMIA SILAHA KWA MFANYABIASHARA WA MADINI AINA YA DHAHABU WILAYANI CHUNYA.
 WALINZI WAWILI WA CITY PUB JIJINI MBEYA WANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI KWA KOSA LA KUMSHAMBULIA NA KUMJERUHI MFANYABIASHARA MMOJA MKAZI WA ISANGA.
 MWANAMKE MMOJA AMBAYE HAJAFAHAMIKA JINA WILA MAKAZI YAKE ANATAFUTWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA KOSA LA KUTUPA MTOTO CHOONI MWENYE UMRI WA SIKU MOJA.
 WATU WANNE WANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA KOSA LA KUINGIZA BIDHAA NCHINI BILA KIBALI.
 JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAMSHIKILIA MWANAMKE MMOJA MKAZI WA ILEMI JIJINI MBEYA AKIWA NA POMBE YA MOSHI NUSU LITA.
 JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WATU WAKIWA NA VIPANDE SITA VYA MENO YA TEMBO.
KATIKA TUKIO LA KWANZA:
MTU MMOJA AITWAE ROBERT MBUKWA (50) MFANYABIASHARA YA MADINI AINA YA DHAHABU NA MKAZI WA MIANZINI WILAYANI CHUNYA ALIVAMIWA NA VIJANA WATATU WANAOSADIKIWA KUWA NI MAJAMBAZI WAKIWA NA SILAHA MOJA BUNDUKI AINA YA SHOT GUN 12 BORE YENYE NAMBA 64943 ILIYOTENGENEZWA KATIKA KIWANDA CHA WEMBLEY @ SCOTT LTD KILICHOPO BIRMINGHAM ENGLAND NA KUFYATUA RISASI MOJA HEWANI.
TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 13.03.2015 MAJIRA YA SAA 20:00 USIKU HUKO KATIKA MTAA WA MIANZINI, KATA YA BWAWANI, TARAFA YA KIPEMBAWE, KATIKA MJI MDOGO WA MAKONGOLOSI, WILAYA YA CHUNYA, MKOA WA MBEYA.
INADAIWA KUWA, MHANGA BAADA YA KUYAONA MAJAMBAZI HAYO ALIPIGA KELELE NA KUPATA MSAADA KUTOKA KWA MAJIRANI HALI ILIYOPELEKEA MAJAMBAZI HAYO KUTUPA SILAHA NA KUTOKOMEA KWENYE SHAMBA LA MAHINDI.
BAADA YA KUIPATA BUNDUKI HIYO NA KUIKAGUA ILIKUTWA IKIWA IMEKATWA MTUTU NA KITAKO. AIDHA ENEO LA TUKIO LIMEOKOTWA GANDA MOJA LA RISASI. UPELELEZI ZAIDI WA TUKIO HILO UNAENDELEA IKIWA NI PAMOJA NA MSAKO MKALI WA KUYATAFUTA MAJAMBAZI HAYO.
KATIKA TUKIO LA PILI
WALINZI @ MABAUNSA WAWILI WA CITY PUB ILIYOPO JIJINI MBEYA WALIOTAMBULIKA KWA MAJINA YA 1. GOODLUCK KAGALI (23) MKAZI WA ILOMBA NA 2. MAHAMUD MUINGA (25) MKAZI WA ILOMBA WANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA BAADA YA KUMSHAMBULIA KWA KUMPIGA NGUMI NA MATEKE NA KISHA KUMPIGA NA KITU KIZITO MGUU WA KULIA MFANYABIASHARA MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA BAHATI SANDE (32) MKAZI WA ISANGA NA KUSABABISHA MGUU HUO KUVUNJIKA.
TUKIO HILO LIMETOKEA USIKU WA KUAMKIA LEO MAJIRA YA SAA 01.00 HUKO KATIKA CITY PUB, KATA YA RUANDA, TARAFA YA IYUNGA, JIJI NA MKOA WA MBEYA. INADAIWA KUWA, CHANZO CHA TUKIO HILO NI MZOZO ULIOTOKEA BAINA YAO NA MFANYABIASHARA HUYO. WATUHUMIWA WAMEKAMATWA NA MHANGA AMELAZWA KATIKA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA.
KATIKA TUKIO LA TATU:
MWANAMKE MMOJA AMBAYE BADO HAJAFAHAMIKA JINA WALA MAKAZI YAKE ANATAFUTWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA KOSA LA KUTUPA CHOONI MTOTO MCHANGA MWENYE UMRI WA SIKU MARA BAADA YA KUJIFUNGUA.
TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 13.03.2015 MAJIRA YA SAA 22:30 USIKU HUKO ENEO LA MLIMARELI, KATA YA UTENGULE –USONGWE, TARAFA YA BONDE LA USONGWE, WILAYA YA MBEYA VIJIJINI, MKOA WA MBEYA.
INADAIWA KUWA, MSAMALIA MWEMA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA JAPHET SANGA (41) MWALIMU NA MKAZI WA MLIMARELI ALIGUNDUA KUTUPWA KWA MTOTO HUYO MCHANGA NDANI YA SHIMO LA CHOO CHA NJE KATIKA NYUMBA ANAYOISHI YEYE NA WAPANGAJI WENZAKE BAADA YA KUSIKIA SAUTI YA MTOTO HUYO AKILIA.
MTOTO HUYO MWENYE JINSI YA KIKE AMEOKOLEWA AKIWA HAI KWA USHIRIKIANO KATI YA JESHI LA POLISI NA WANANCHI NA AMELAZWA KATIKA HOSPITALI TEULE YA IFISI KWA MATIBABU/UCHUNGUZI ZAIDI. UPELELEZI WA TUKIO HILI UNAENDELEA IKIWA NI PAMOJA NA KUMTAFUTA MTUHUMIWA WA TUKIO HILI.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA WAZAZI KUACHA TABIA YA KUTUPA WATOTO KWANI NI KITENDO CHA KINYAMA, KINYUME CHA MAADILI NA NI KINYUME CHA SHERIA ZA NCHINI. AIDHA ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA MAHALI ALIPO MTUHUMIWA WA TUKIO HILI [MAMA WA MTOTO HUYO] AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI AKAMATWE NA HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAKE.
KATIKA TUKIO LA NNE:
WATU WANNE WALIOFAHAMIKA KWA MAJINA YA 1. ZULFUA ABUBAKAR (30) KONDAKTA WA BASI LA KAMPUNI YA TAQWA NA MKAZI WA DSM 2. CHRISTOPHER FREDY (28) MFANYABIASHARA, MKAZI WA MKOMBOZI TUNDUMA 3. EMANUEL MWASHAMBWA (35) MKAZI WA MPEMBA NA 4. STEPHEN KALINGA (29) MKAZI WA MPEMBA WANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA KOSA LA KUINGIZA BIDHAA NCHINI BILA KIBALI.
WATUHUMIWA HAO WALIKAMATWA MNAMO TAREHE 13.03.2015 MAJIRA YA SAA 09:30 ASUBUHI WAKIWA NA MAZIWA AINA YA LACTOGEN DAZANI 24, SAWA NA KOPO 1,032 YENYE UJAZO WA GRAM 400 KILA MOJA. THAMANI HALISI YA BIDHAA HIZO NI TSHS 17,000,000/=.
AIDHA BIDHAA HIZO AMBAZO ZILIKUWA ZIKIINGIZWA NCHINI BILA KULIPIA USHURU KUTOKA NCHINI AFRIKA KUSINI, KUPITIA NCHINI ZAMBIA KWA NJIA ZA PANYA.
KATIKA TAARIFA ZA MISAKO:
KATIKA MSAKO WA KWANZA, JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAMSHIKILIA MWANAMKE MMOJA MKAZI WA ILEMI JIJINI MBEYA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA EDITHA JOHN (34) AKIWA NA POMBE YA MOSHI UJAZO WA NUSU LITA .
MTUHUMIWA ALIKAMATWA KATIKA MSAKO ULIOFANYIKA MNAMO TAREHE 13.03.2015 MAJIRA YA 12:00 MCHANA HUKO KATIKA MTAA MAPELELE, KATA YA ILEMI, TARAFA YA SISIMBA, JIJI NA MKOA WA MBEYA. MTUHUMIWA NI MUUZAJI WA POMBE HIYO, TARATIBU ZA KUMFIKISHA MAHAKAMANI ZINAENDELEA.
KATIKA MSAKO WA PILI, JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WATU WAWILI WALIOFAHAMIKA KWA MAJINA YA 1. NEHEMIA EMANUEL (22) MKAZI WA KIJIJI CHA MATUNDASI AMBAYE ALIKUWA AKIENDESHA PIKIPIKI YENYE NAMBA ZA USAJILI T.622 BJV AINA YA SANLG AKIWA AMEPAKIA ABIRIA WAWILI KATIKA PIKIPIKI HIYO MMOJA WA ABIRIA HAO AKIFAHAMIKA KWA JINA LA MAHENGULA BONIFACE (30) MKAZI WA MSWISWI NA MWINGINE AMBAYE ALIRUKA NA KUKIMBIA BAADA YA KUWAONA ASKARI WAKIWA NA MENO YA TEMBO VIPANDE SITA [06].
WATUHUMIWA WALIKAMATWA MNAMO TAREHE 13.03.2015 MAJIRA YA SAA 13:00 MCHANA HUKO KATIKA KIJIJI CHA MAHANGO-MSWISWI, KATA NA TARAFA YA ILONGO, WILAYA YA MBARALI, MKOA WA MBEYA.
WATUHUMIWA HAO WALIKAMATWA BAADA YA KUSIMAMISHWA NA KISHA KUPEKULIWA NA NDIPO KATIKA PIKIPIKI HIYO KULIKUTWA MFUKO WA SANDARUSI AMBAO NDANI YAKE KULIKUWA NA MENO HAYO YA TEMBO.
Imesainiwa na: [AHMED Z. MSANGI – SACP] KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

BREKING NEWZZSS kocha msaidi wa taifa stars Sylvester Marsh,afariki dunia

March 14, 2015

Sylvester Marsh,

  ALIYEKUWA kocha Msaidizi wa timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Sylvester Marsh amefariki dunia Alfajiri ya leo katika hospitali ya Muhimbili alikokuwa amelazwa.

 

Taarifa zinasema Marsh alikuwa amefika Muhimbili kuhudhuria kliniki yake ya kawaida juu ya maradhi ya saratani ya koo yanayomsumbua na ghafla hali yake ilibadilika juzi hadi kufariki dunia.

Marsh alianza kuwa Kocha Msaidizi wa timu za vijana Tanzania mwaka 2003 chini ya Alhaj Abdallah Athumani Seif ‘King Kibadeni’ kabla ya mwaka 2006 kupandishwa timu ya wakubwa, akianza kumsaidia Mbrazil, Marcio Maximo na baadaye Wadenmark, Jan Poulsen na Kim Poulsen. 


Hata hivyo, baada ya Jamal Malinzi kushinda Urais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Oktoba mwaka juzi, alibadilisha benchi zima la ufundi la Taifa Stars na Marsh akaondoka pamoja na Kim Poulsen. Sasa Mholanzi, Mart Nooij ndiye kocha Stars, anasaidiwa na Salum Mayanga Tangu hapo Marsh amerudi kufanya kazi katika kituo chake cha Marsh Academy mjini Mwanza, lakini mwaka jana ndipo maradhi ya saratani koo yalipoibuka na akaletwa Muhimbili kwa matibabu.



Mfanyabiashara Abdulfatah Salim, mmiliki wa hoteli ya Sapphire Court, alimsaidia kocha huyo hadi akafanyiwa upasuaji na hali yake kuimarika Februari mwaka jana na kurejea Mwanza.


Marsh alipata ahueni ya kutosha na kuanza tena kazi ya kufundisha watoto wake wa Marsh Academy, kabla ya wiki hii kuletwa Dar es Salaam kuhudhuria kliniki.


Mbali na timu za taifa, Marsh pia amefundisha klabu za Toto Africans ya Mwanza, Kagera Sugar ya Bukoba na Azam FC ya Dar es Salaam
CHANZO: http://wwwmzukakamili-mzuka.blogspot.com

NHIF KUPIMA AFYA NA KUKUSANYA DAMU KWA USHIRIKIANO WA MPANGO WA TAIFA WA DAMU SALAMA KATIKA MIKOA SITA

March 14, 2015
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Michael Mhando akizungumza na Waandishi wa habari Dar es Salaam jana kuhusiana na zoezi la upimaji afya na kukusanya damu salama kwa ushirikiano na Mpango wa damu salama katika mikoa sita nchini.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Michael Mhando akizungumza na Waandishi wa habari Dar es Salaam jana kuhusiana na zoezi la upimaji afya na kukusanya damu salama kwa ushirikiano na Mpango wa damu salama katika mikoa sita nchini. Kushoto ni Afisa Uhusiano wa Mpango wa taifa wa Damu Salama, Rajab Mwenda.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Michael Mhando akizungumza na Waandishi wa habari Dar es Salaam jana kuhusiana na zoezi la upimaji afya na kukusanya damu salama kwa ushirikiano na Mpango wa damu salama katika mikoa sita nchini. Kushoto ni Afisa Uhusiano wa Mpango wa taifa wa Damu Salama, Rajab Mwenda na kulia ni Mkurugenzi wa Rasilami watu na Utawalawa wa NHIF, Beatus Chijumba.
Baadhi ya maofisa wa NHIF walioshiriki mkutano huo na waandishi wa habari wakifuatilia kwa makini.

DC MAKONDA AKAGUA MIUNDOMBINU YA BARABARA NA MADARAJA KATIKA WILAYA YAKE

March 14, 2015



 Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda (wa pili kushoto), akipata maelezo kutoka kwa Mhandisi wa Kampuni ya Delmonte (T) Ltd, Theophile Kireo (mwenye kofia), ambayo kampuni yake inakarabati barabara ya Mwai Kibaki eneo la Msasani Dar es Salaam jana. Wengine ni Wataalamu wa barabara Manispaa ya Kinondoni. 
 Mhandisi wa Kampuni ya Delmonte (T) Ltd, Theophile Kireo (mwenye kofia wa pili kulia), akitoa maelezo kwa DC Makonda.
 DC Makonda (wa kwanza kushoto), akizungumza na wakazi wa Msasani kuhusu kuzingatia usafi wa mazingira.
 DC Makonda akikagua mitaro inayojengwa na Kampuni ya Delmonte (T) Ltd.
 DC Makonda akiangalia mfereji unaotiririsha maji taka kutoka Hospitali ya TMJ.
 Fundi bomba wa Hospitali ya TMJ, Mansoul Mramba akitoa maelezo kwa DC Makonda kuhusu utiririshaji wa maji taka hayo.
DC Makonda (wa pili kulia akinagalia maji taka eneo la Msasani karibu na Ofisi za Tanesco Wilaya ya Kinondoni.

Na Dotto Mwaibale
MKUU wa Wilaya ya Kinondoni Paul Makonda ametoa siku saba kwa uongozi wa Hospitali ya TMJ iliyopo Mikocheni jijini Dar es Salaam kuacha kutiririsha maji taka kwenyenda barabarani na kwenye makazi ya watu.

Agizo hilo amelitoa leo jijini Dar es Salaam wakati alipofanya ziara ya kushitukiza ya kukagua barabara, madaraja na miundombinu eneo la Msasani ambalo kwa muda mrefu limekuwa likikumbwa na mafuriko ya mara kwa mara hasa wakati wa mvua za masika.

"Natoa siku saba kwa uongozi wa Hospitali ya TMJ kuhakikisha wanaacha kutiririsha maji taka kutoka katika hospitali hiyo kinyumbe cha agizo langu zitafuata hatua kali za kisheria" alisema Makonda.

Katika hatua nyingine Makonda aliwataka wakazi wa eneo hilo la Msasani kuacha kutupa takataka kwenye mitaro ambazo zimekuwa zikichangia kwa kiasi kikubwa kuziba kwa mitaro hiyo na kuwa mtu yeyote atakayebainika akitupa taka taka hizo atachukuliwa hatua kali.

Makonda alisema Serikali imekuwa ikitumia fedha nyingi kujenga na kutengeneza barabara lakini watu wachache wamekuwa wakiharibu kwa kutupa taka taka hovyo.
(Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com)

JUMUIYA YA VIJANA WA CHAMA CHA MAPINDUZI (UVCCM) MKOA WA KILIMANJARO WAKUTANA JIMBO LA VUNJO.

March 14, 2015


Baadhi ya wananchama wa Jumuiya ya Vijana wa Chama cha Mapinuzi (UVCCM) wakiwa katika kikao kilichochanyika Jimbo la Vunjo.
Kamanda Msaidizi wa Jumuiya ya Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) wilaya ya Moshi Vijijini ,Innocent Mellecky akizungumza katika kikao hicho kilicho shirikisha wenyeviti wote wa jumuiya hiyo mkoa wa Kilimanjaro.
Baadhi ya wajumbe wa Jumuiya hiyo.
Mwenyekiti mstaafu wa Jumuiya ya Vijana wa Chama cha Mapinduzi mkoa wa Kilimanjaro,Godliving Mushi akizungumza katika kikao hicho.
Kaimu katibu wa Jumuiya ya Vijana wa Chama cha Mapinduzi mkoa wa Kilimanjaro Joel Makwaia akizungumza jambo katika kikao hicho.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Vijana (UVCCM) mkoa wa Kilimanjaro Fredrick Mushi akizungumza katika kikao hicho ,
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.

DIAMOND HAWEZI TENA KUFOCUS MAMBO YA WEMA SEPETU!

March 14, 2015
Mwanamziki Ommy Dimpoz ameyasema hayo leo kwenye kipindi cha XXL cha Clouds FM alipokuwa anautambulisha wimbo wake wa Wanjera ambao mrembo Wema Sepetu amecheza kama Wanjera kwenye video wa wimbo huo na kushiriki kupiga picha za kuutangaza wimbo huo.
 ALICHOKISEMA ZITTO KABWE KUHUSU KUGOMBEA UBUNGE TENA MWAKA HUU

ALICHOKISEMA ZITTO KABWE KUHUSU KUGOMBEA UBUNGE TENA MWAKA HUU

March 14, 2015

 Mbunge wa Kigoma Kaskazini Mh. Zitto Zubery kabwe Leo Alikutana na Wazee wa Jimbo Lake na Kutoa Maamuzi magumu mbele ya wazee hao kama hatogombea tena Ubunge kwenye jimbo hilo alilolitumikia kwa muongo moja (miaka 10) huku wazee wakimbariki achukue maamuzi yanayofaa kulingana na hali ya kisiasa inayoendelea hivi sasa.
Katika page yake ya facebook amepost ujumbe huu kama unavyosomeka hapa chini
MSIPOKEE MAHARI ZA WATOTO WENU WAKIWA WANAFUNZI – MAMA SALMA KIKWETE

MSIPOKEE MAHARI ZA WATOTO WENU WAKIWA WANAFUNZI – MAMA SALMA KIKWETE

March 14, 2015

9
………………………………………………………………………………………………………………………
Na Anna Nkinda – Maelezo, Mafia 
Wazazi na walezi wilayani  Mafia wametakiwa  kutokubali kupokea mahari za watoto wao wakiwa wanafunzi  bali wawasimamie na kuhakikisha wanasoma kwa bidii na kufika elimu ya chuo kikuu. Rai hiyo imetolewa jana na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete wakati akiongea na wanafunzi pamoja na wazazi wa shule ya Sekondari Bweni iliyopo kata ya Kanga wilaya ya Mafia mkoani Pwani. Mama Kikwete ambaye ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) alisema baadhi ya wazazi wanapokea mahari za watoto wao na kuwaozesha wakiwa na umri mdogo jambo ambalo huwafanya kukatisha   masomo  yao na wanawanyima haki yao ya msingi ya kupata elimu. “Mtoto akisoma  atakuwa na maisha mazuri hapo baadaye ataweza kufanya kazi za kitaalamu za kuajiriwa au kujiajiri yeye mwenyewe, kujikomboa na umaskini, kuwasaidia wazazi wake, ataepukana  na mimba za utotoni na kujiepusha  na maradhi yanayotokana na ngono zembe  kwani elimu ni msingi wa kila kitu”. Wanawake wenzangu mtoto wako wa kike akiwa mwali  usikubali kumuweka ndani ili asubiri mwanaume wa kumuoa na ukisikia mmeo kapokea mahari ili binti huyo aolewe katoe taarifa sehemu inayohusika ili sheria iweze kuchukua mkondo wake”, alisisitiza Mama Kikwete. Kwa upande wa wanafunzi aliwaasa kujiepusha na kitendo cha kujiingiza katika mapenzi wakiwa na umri mdogo bali wasome kwa bidhii , wawe na nidhamu kwa walimu wao  na kuwa na malengo katika maisha yao kwa kufanya hivyo watatimiza  ndoto zao. Alisema, “Wanangu someni kwa bidii msitake utajiri wa haraka, watoto wa kiume mnaacha kwenda shule, mnakatisha masomo na kukimbilia kuvua samaki  kwa kudhani kuwa mtapata maendeleo kumbukeni elimu ni urithi usioweza kutoweka katika maisha yenu”,. Aidha Mwenyekiti huyo wa WAMA aliwahimiza wazazi kwenda Hospitali kupima ugonjwa wa saratani za shingo ya kizazi, matiti na tezi dume ambazo zikigundulika katika hatua ya awali mgonjwa anaweza kutibiwa   na kupona kabisa. Kuhusu utunzaji wa ardhi Mama Kikwete alisema wilaya hiyo imejaliwa kuwa na ardhi nzuri yenye rutuba  inayowavutia watu wengi na kuwasihi wananchi kutoiuza kiholela  bali waitunze,  kama kuna wawekezaji utaratibu maalum ufuatwe. Naye  Mkuu wa Mkoa wa Pwani Eng. Evarist Ndekilo aliwahimiza wananchi hao kuona umuhimu wa kuwarithisha watoto wao elimu ambayo ni ufunguo wa maisha na siyo mali kama uvuvi, ng’ombe na mashamba. Eng. Ndekilo alisema atakuwa mkali kwa mtu yoyote atakayekatisha elimu ya mtoto wake na katika suala la mtoto kuacha  shule baada ya kupewa ujauzito mahakama ndiyo itakayotoa  maamuzi na siyo wazazi kumalizana wenyewe kwa wenyewe. Akisoma taarifa ya shule Mwalimu mkuu Mohamed Msossow alisema shule hiyo ilifunguliwa mwaka 2007 ikiwa na walimu wanne  na wanafunzi 199 kati ya hao wavulana walikuwa 147 na wasichana 52 . Hivi sasa kuna walimu 20 na wanafunzi 131 kati ya hao wavulana  61 wasichana 70 na walimu 20. Aliyataja mafanikio waliyo nayo ni walimu wa kutosha wa masomo ya sanaa, vitabu vya kutosha vya masomo ya sayansi na sanaa kwa uwiano wa mwanafunzi mmoja kwa kitabu kimoja, madarasa ya kutosha, ushirikiano mzuri na jamii inayowazunguka na matokeo mazuri ya kitaaluma katika mitihani ya kidato cha pili na cha nne. “Changamoto zinazotukabili ni upungufu wa walimu wa masomo ya sayansi na hisabati, nyumba za walimu na vifaa vya maabara, kutokana na mazingira ya mahali shule ilipo shule inahitajika kuwa na usafiri ili kurahisisha walimu kufika wilayani”. Idadi ndogo ya wanafunzi inayosababisha kupata mgao mdogo wa fedha ya ruzuku kutoka Serikalini na kusababisha ugumu katika kuendesha shughuli mbalimbali za shule, ukosefu wa umeme na uhaba wa vyanzo vya maji”,alisema Mwalimu Msossow. Mama Kikwete yuko wilayani humo kwa ziara ya kikazi ya siku mbili na akiwa shuleni hapo aliwapatia wanafunzi zawadi ya shilingi milioni moja. Shule ya Sekondari Bweni imejengwa na Taasisi ya Maendeleo ya Kisiwa cha Mafia (MIDEF) chini ya usimamizi wa Dkt. Ramadhan Dau ambaye ni Mkurugenzi wa Shirika la Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) na kuikabidhi kwa Serikali ambapo hivi sasa ni Shule ya Sekondari ya kata ya Kanga.
MAMA SALMA KIKWETE AWASILI MAFIA / ATEMBELEA SHULE YA SEKONDARI BWENI

MAMA SALMA KIKWETE AWASILI MAFIA / ATEMBELEA SHULE YA SEKONDARI BWENI

March 14, 2015

1
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akipokewa na Mkuu wa Mkoa wa Pwani Injinia Evarist Ndikilo mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Mafia kuanza ziara ya siku mbili wilayani humo tarehe 13.3.2015.
2
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akipokea ua kutoka kwa Mwalimu Mariam Halfan Haji mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Mafia kama ishara ya upendo na kumkaribisha rasmi kutembelea wilaya ya Mafia.
4
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Jamii (NSSF) Dkt. Ramadhan Dau alikuwa ni miongoni mwa viongozi mbalimbali waliofika kwenye uwanja wa ndege wa Mafia kwa ajili ya kumpokea Mke wa Rais Mama Salma Kikwete alipowasili wilayani humo tarehe 13.3.2013 kwa ziara ya kikazi ya siku mbili.
3
Akina mama wa Mafia waliofika kumpokea Mama Salma Kikwete wakati akiwasili kwenye uwanja wa ndege wa Mafia wanaonekana wakiwa wamebeba mabango ya kumkarisha wilayani humo.
  5
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akimsalimia mtoto mwenye ulemavu wa ngozi/albino aliyekuwa amebebwa na mama yake. Mama Salma alikutana na mtoto huyo wakati alipowasili kwenye ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Mafia.
6
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Jamii (NSSF) Dkt. Ramadhan Dau akitoa maelezo mafupi kuhusu Shule ya Sekondari Bweni iliyoko katika Kata ya Kanga wilayani Mafia ambayo imejengwa na “Mafia Island Development Foundation, MIDEF”. Dkt. Dau ni mmoja wa viongozi wa Taasisi hiyo. Mama Salma alitembelea  Shule hiyo tarehe 13.3.2015. Waliokaa kutoka kushoto ni Mbunge wa Mafia Mheshimiwa Abdulkarim Shah, Mkuu wa Mkoa wa Pwani Injinia Evarist Ndikilo,  Ndugu Mohamed Msosa, Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo na mwisho ni Mwenyekiti wa CCM wa Wilaya ya Mafia.
10
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akizungumza na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Bweni iliyoko katika Kata ya Kanga wilayani Mafia.
12
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiongea na wananchi wa Kijiji cha Bweni katika Kata ya Kanga waliofika shuleni hapo kwa ajili ya kusalimiana naye.
13 14
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akifurahia zawadi alizopewa na akina mama wajasiriamali wa Kata ya Kanga huko Mafia mara baada ya kumaliza kuzungumza na wanafunzi na wananchi wa eneo hilo.
15
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akizungumza na walimu wa Shule ya Sekondari Bweni iliyoko huko Mafia mara baada kuongea na wanafunzi.
PICHA ZOTE NA JOHN LUKUWI