February 27, 2014

MKOSAJI MKUU WA HAKI ZA BINADAMU NI SERIKALI – JAJI MSTAAFU MIHAYO

DSC_0259
Mjumbe wa Bodi ya Mtandao wa watetezi wa Haki za Binadamu nchini (Tanzania Human Rights Defenders Coalition) Dkt. Hellen Kijo Bisimba akitoa neno la ufunguzi wakati wa warsha ya siku moja iliyowakutanisha watetezi wa Haki za Binadamu nchini na Jeshi la Polisi jijini Dar leo.
.Asema dunia nzima inajua mvunjifu wa kwanza wa haki za binadamu ni dola
.Polisi pia ni binadamu wanahitaji kutetewa na mitandao ya haki za binadamu nchini
Na Damas Makangale, MOblog Tanzania
MKOSAJI na mvunjifu mkubwa wa haki za binadamu ni serikali kutokana na mazingira halisi ya utendaji na mfumo mzima wa utawala katika serikali nyingi duniani. Imeelezwa.
Akizungumza kwenye warsha ya siku moja iliyoandaliwa na Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu nchini, Tanzania Human Rights Defenders Coalition (THRDC) kwa wakuu na makamanda wa Jeshi la Polisi nchini, Jaji Mstaafu, Thomas Mihayo amesema kwa mfumo wa utawala katika nchi nyingi duniani mkosaji mkuu wa haki za binadamu ni serikali.
“dunia nzima inajua kwamba serikali ndio mkosaji mkuu wa haki za binadamu na maana halisi ya serikali ni dola na mahakama tu kwisha,” amesema Jaji Mihayo
Jaji Mihayo amesema kuwa kwa hali ya kawaida dola ikimkamata mtu au mhalifu lazima mpeleke katika mahakama ili sheria ichukue mkondo wake wa kawaida.
DSC_0316
Naibu Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP), Abdurahman Kaniki, akitoa hotuba yake ya ufunguzi kwa niaba ya IGP Ernest Mangu, kwenye warsha ya siku moja iliyowakutanisha viongozi waandamizi wa Jeshi hilo na watetezi wa Haki za Binadamu nchini.
Kwa upande wake, Mjumbe wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu, Dkt Helen Kijo Bisimba akitoa neno la ufunguzi amesema warsha hiyo inatoa fursa nzuri kwa watetezi wa haki za binadamu na Jeshi la Polisi kuboresha kazi zao za utetezi wa haki za binadamu nchini.
Amesema kwa ujumla haki za binadamu hazipewi bali ni haki ya msingi ambayo mtu anazaliwa nayo ili zinaminywa aidha kupitia mtu kwa mtu au taasisi au mfumo wa utawala.
“Kazi za watetezi wa haki za binadamu na Jeshi la Polisi zinaendama na msingi ni utetezi wa haki za binadamu pamoja na mali zao,” alisisitiza
Naye, Mratibu wa kitaifa wa Mtandao huo, Onesmo Olengurumwa akiwasilisha mada yake ya (The Concept of Protection and Security Management for Human Rights Defenders and Social Organization) amesema kuwa taaluma inaweza kutumika kutetea haki za binadamu katika maeneo mengi hapa duniani.
DSC_0334
DSC_0379
Jaji Mstaafu Thomas Mihayo akizungumza na Makamanda wa Jeshi la Polisi nchini, umuhimu wa kushirikiana kati ya Jeshi hilo na Asasi za kutetea Haki za Binadamu ili kuleta tija katika nyanja za kiuchumi, kijamii na kisiasa.
Amesema pia kupitia mada hiyo kwamba jamii inadhani kwamba anayepaswa kutetewa ni mwananchi tu lakini pia hata polisi naye ni binadamu anapaswa kuwa na mtetezi pale ambapo haki yake ya msingi inapovunjwa.
“Mpaka sasa Tanzania haina sheria yeyote inayomlinda mtetezi wa haki za binadamu lakini tunaendelea na mchakato na ni matumaini yetu serikali itaridhia kuwa na sheria hiyo hapa nyumbani,” alilisitiza
Naibu Inspekta Jenerali wa Jeshi la Polisi nchini, Abdurahman Kaniki amesema kuwa jeshi la polisi nchini litaendelea kuimarisha mahusiano kati ya jeshi hilo na watetezi wa haki za binadamu nia ni kudumisha amani na utulivu nchini.
DSC_0325
Sehemu ya makamishina na makamanda wa mikoa na maafisa waandamizi wa Jeshi la Polisi nchini wakifuatilia mada mbalimbali kwenye warsha hiyo ya siku moja jijini Dar es Salaam.
“majukumu ya jeshi la polisi na watetezi wa haki za binadamu nchini yanafanana kwa kila hali ni kulinda na kutetea haki za wananchi na mali zao,” amesema Naibu IGP Kaniki
Kamishina Kaniki alilisitiza kwamba ni muhimu wadau wote kuzingatia sheria za nchi, taratibu na kanuni katika kutafuta haki mbalimbali ili kudumisha amani na utulivu nchini.
“nachukua nafasi kuwakaribisha wadau wote wa haki za binadamu na makundi mengine kushirikiana na jeshi la polisi katika kulinda na kutetea haki za binadamu nchini,” alisisitiza
Kamanda wa Polisi Arusha, RPC Liberatus Sabas amesema kwa muda mrefu watu wa utetezi wa haki za binadamu na makundi mengine huwa wanasahau kwamba polisi pia ni binadamu nao wanahitaji utetezi kutoka kwa watetezi hao wa haki za binadamu.
February 27, 2014
NYALANDU AAPA KUSAKA MAJANGILI, MAGARI, BUNDUKI ZA AK47 ZASHUSHWA
WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu, akizindua moja kati ya magari zaidi ya 20 aina ya Toyota Land Cruiser ambayo yametolewa na wizara hiyo kwa ajili ya kukabiliana na ujangili katika baadhi ya hifadhi za taifa nchini. Hatua hiyo ni mpango wa serikali kutekeleza kwa vitendo mapambano dhidi ya ujangili. Picha zingine Nyalandu akiwa kwenye matukio tofauti wakati wa uzinduzi huo uliofanyika wizara hapo jana.
**********
 NA MWANDISHI WETU
SERIKALI imeendelea na dhamira yake ya kuhakikisha inatokomeza vitendo vya ujangili wa wanyama na nyara zao baada ya 'kushusha' bunduku 500 aina ya AK 47, imeelezwa.

Mbali ya hilo, imeligawanya pori la akiba la Selous lenye ukubwa wa kilomita za mraba 55,000 kwa kuzipandisha hadhi kanda nane ili ziweze kujitegemea kiuendeshaji.

Hayo yalisema jana na Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari mjini Dar es Salaam, wakati akikabidhi magari maalumu yatakayosaidia kukabiliana na ujangili kwenye hifadhi na mapori ya akiba nchini.

DIAMOND AWASHANGAA WASANII WANAOPENDA KUNUNUA UGOMVI NA YEYE

February 27, 2014
Muda si mrefu Diamond Amefunguka haya hapa chini kuhusu wasanii wanasanii wanao tafuta beef za lazima kutoka kwake ...Jisomee

RAIS KIKWETE AZINDUA MTAMBO WA KUHAKIKI TAKWIMU ZA MAWASILIANO

February 27, 2014
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe kuzindua rasmi Mtambo wa Kuhakiki Takwimu za Mawasiliano (Telecommunication Traffic Monitoring System) leo February 27, 2014 katika jengo la Mawasiliano Towers jijini Dar es salaam. Kulia ni Waziri wa Mawasiliano Sayansi na Teknolojia wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Pro, Makame Mnyaa Mbarawa, Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt Fenella Mukangara, Mkurugenzi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Prof. John Nkoma, Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Saidi Meck Sadick na wadau wengine wa tehama.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akibofya kitufe  kuzindua rasmi Mtambo wa Kuhakiki Takwimu za Mawasiliano (Telecommunication Traffic Monitoring System) leo February 27, 2014 katika jengo la Mawasiliano Towers jijini Dar es salaam.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipata maelezo ya  Mtambo wa Kuhakiki Takwimu za Mawasiliano (Telecommunication Traffic Monitoring System) aliouzindua leo February 27, 2014 katika jengo la Mawasiliano Towers jijini Dar es salaam. Kulia ni Waziri wa Mawasiliano Sayansi na Teknolojia wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Pro, Makame Mnyaa Mbarawa, Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt Fenella Mukangara, Mkurugenzi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Prof. John Nkoma, Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Saidi Meck Sadick na wadau wengine wa tehama.
PICHA NA IKULU
February 27, 2014

RAIS KIKWETE AUNGANA NA JUMUIYA YA CHUO KIKUU KUTOA HESHIMA ZA MWISHO KWA MWILI WA BALOZI KAZAURA

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiweka saini katika kitabu cha maombolezo wakati alipowasili kwenye hafla rasmi ya mazishi ya Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam Marehemu Balozi Fulgence Kazaura katika ukumbi wa Nkrumah Chuoni hapo leo February 27, 2014. Nyuma yake ni Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Cha Dar es salaam Profesa Rwekaza Mukandara na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe saidi Meck Sadick.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na waombolezaji wengine kwenye hafla rasmi ya mazishi ya Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam Marehemu Balozi Fulgence Kazaura katika ukumbi wa Nkrumah Chuoni hapo leo February 27, 2014. 

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitoa heshima zake za mwisho kwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam Marehemu Balozi Fulgence Kazaura katika ukumbi wa Nkrumah Chuoni hapo leo February 27, 2014.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifariji familia ya marehemu kwenye hafla rasmi ya mazishi ya Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam Marehemu Balozi Fulgence Kazaura katika ukumbi wa Nkrumah Chuoni hapo leo February 27, 2014. PICHA NA IKULU
February 27, 2014

COASTAL UNION WAITWA WAWILI TAIFA STARS.

Abdi Banda
                                                             Shaaban Kado

Kutokana na mechi dhidi ya kirafiki dhidi ya Namibia itakayochezwa Machi 5 mwaka huu jijini Windhoek, Stars itaongozwa na Kaimu Mkurugenzi wa Ufundi, Salum Madadi akisaidiwa na kocha Hafidh Badru kutoka Zanzibar.

Katika hatua nyingine, Kocha Madadi amewaondoa wachezaji watano wa Yanga katika kikosi kilichotajwa awali ili wapate fursa ya kuitumikia timu yao kwenye mechi mbili za Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Al-Ahly ya Misri.

February 27, 2014

MAAFISA Afya na Mifugo wametakiwa kutobweteka maofisini na kufanyia kazi kwenye makaratasi(Paper Work) badala yake wafanye kazi kwa vitendo

Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mkoa wa Mbeya, Dk. Agnes Buchwa, alipokuwa akifungua kikao cha watendaji wa Halmashauri za Wilaya na Jiji la Mbeya kuhusu Shughuli za Mamlaka ya Udhibiti wa Chakula, Dawa, Vipodozi na Vifaa tiba(TFDA) kilichofanyika katika ukumbi wa Hospitali ya Mkoa wa Mbeya uliopo Forest Mpya Jijini hapa.

Kaimu Meneja wa Mamlaka ya udhibiti wa Chakula, Dawa, vipodozi na vifaa tiba(TFDA) Kanda ya Nyanda za juu Kusini, Rodney Alananga,ambao ndiyo wandaaji wa mafunzo hayo alisema yamewalenga Maafisa afya, Mifugo, Famasia na wahasibu kutoka Halmashauri za Wilaya na Jiji la Mbeya.


MAAFISA Afya na Mifugo wakiwa katika semina hiyo







MAAFISA Afya na Mifugo wametakiwa kutobweteka maofisini na kufanyia kazi kwenye makaratasi(Paper Work) badala yake watumie taaluma yao kama walivyofundishwa mashuleni kwa kufanya kazi ya vitendo.

Mwito huo umetolewa na Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mkoa wa Mbeya, Dk. Agnes Buchwa, alipokuwa akifungua kikao cha watendaji wa Halmashauri za Wilaya na Jiji la Mbeya kuhusu Shughuli za Mamlaka ya Udhibiti wa Chakula, Dawa, Vipodozi na Vifaa tiba(TFDA) kilichofanyika leo katika ukumbi wa Hospitali ya Mkoa wa Mbeya uliopo Forest Mpya Jijini hapa.
February 27, 2014

MASELE AENDELEA KUTIMIZA AHADI AWAWEZESHA WAKINA MAMA LISHE SHINYANGA

 Mbunge wa Shinyanga mjini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Madini Ndugu Stephen Masele akizungumza kwenye mkutano na wakina Mama na Baba Lishe wa Shinyanga mjini ambapo aliwasaidia kufungua SACCOS na kuwaongezea mtaji wa biashara yao.

 Wakina Mama Lishe ambao wengi ni Wajane na Yatima wa Shinyanga mjini wakishangilia jambo wakati wa hotuba ya Mbunge wao Ndugu Stephen Masele,kwenye ukumbi wa NSSF CCM mkoa wa Shinyanga uliofanyika jana tarehe 26 Februari 2014.
February 27, 2014

NMB YASOGEZA HUDUMA KARIBU ZAIDI KWA WAKAZI WA BARABARA YA MANDELA

      Vilevile imetoa msaada wa  vifaa vya hospitali vyenye thamani ya shilingi milioni kumi kwa ajili ya Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na Amana
IMG_9875Mheshimiwa mkuu wa mkoa wa  Dar es salaam, Bw. Meck Sadick akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa tawi la NMB Mandela Road . Kwanza kushoto ni Meneja wa NMB kanda ya Dar es salaam , Bw. Salie Mlay na kwanza kushoto ni  Mkuu  wa kitengo cha Huduma kwa wateja wakubwa  NMB, Bw.Gerald Kamugisha wakishuhudia ufunguzi huu uliofanyika jana jijini Dar es salaam.
Menejawa NMB kanda ya Dar es salaam, Bw.Salie Mlay akimwelezea  Mheshimiwa Mkuu wa mkoa wa  Dar es salaam (kwanza kushoto, Bw. Meck Sadick huduma mbalimbali zitolewazo na tawi jipya la NMB mandela Road
February 27, 2014

NAPE AUNGURUMA SHINYANGA, AWAZOA WAWILI KUTOKA CHADEMA

Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiangalia matembezi ya mshikamano wakati yakiingia uwanjani kabla hajaanza kuhutubia wakazi wa Shinyanga mjini.
Wakazi wa Shinyanga mjini wakiwa na Furaha ya kuwakaribisha wanachama wapya ambao walikuwa madiwani kwa kupitia Chadema ambao tarehe 25 walijiuzuru na tarehe 26 Februari 2014 kujiunga na CCM.
Zakaria Martin Mfuko aliyekuwa Diwani wa Chadema Kata ya Masekelo akihutubia wakazi wa Shinyanga mjini kwenye viwanja vya Mahakama ya Mwanzo na kuwaambia wananchi hao ameamua kurudi CCM kutokana na ufisadi na ukiukwaji ya maadili ya Uongozi ndani ya Chadema.
February 27, 2014
27 WAREJESHA FOMU UCHAGUZI TASWA
Waombaji 27 kati ya 28 wamerejesha fomu kuomba kuwania nafasi mbalimbali za uongozi kwenye uchaguzi wa Kamati mpya ya Utendaji ya Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA) utakaofanyika Machi 2, 2014 jijini Dar es Salaam.
Mwisho wa kuchukua na kurudisha fomu hizo ilikuwa leo Alhamisi (Februari 27 mwaka huu) saa 9 alasiri.
February 27, 2014
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Februari 27, 2014



TFF, POULSEN WAKUBALIANA KUVUNJA MKATABA

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na Kocha wa Taifa Stars, Kim Poulsen wamekubaliana kuvunja mkataba katika makubaliano ambayo ni siri kwa pande zote mbili.

Uamuzi huo umetangazwa leo (Februari 27 mwaka huu) jijini Dar es Salaam kwa pamoja na Rais wa TFF, Jamal Malinzi na Kocha Poulsen mbele ya waandishi wa habari.

Rais Malinzi kwa niaba ya TFF ametoa shukrani za dhati kwa Kocha Poulsen kwa ushirikiano na mchango ambao ameutoa kwa Tanzania kuanzia kwenye mpira wa miguu wa vijana.
Naye Kim amewashukuru Watanzania kwa ushirikiano waliompatia kwa kipindi cha miaka mitatu alichokaa nchini kuanzia Mei 2011 alipoteuliwa kuwa kocha wa timu za Taifa za vijana, na baadaye Taifa Stars.

Akizungumzia benchi jipya la ufundi la Taifa Stars, Rais Malinzi amesema linatarajiwa kutangazwa hivi karibuni likiongozwa na kocha kutoka nje ya Tanzania.

Amesema kwa upande wa mechi dhidi ya Namibia itakayochezwa Machi 5 mwaka huu jijini Windhoek, Stars itaongozwa na Kaimu Mkurugenzi wa Ufundi, Salum Madadi akisaidiwa na kocha Hafidh Badru kutoka Zanzibar.

Katika hatua nyingine, Kocha Madadi amewaondoa wachezaji watano wa Yanga katika kikosi kilichotajwa awali ili wapate fursa ya kuitumikia timu yao kwenye mechi mbili za Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Al-Ahly ya Misri.

Wachezaji hao ni Athuman Idd, David Luhende, Deogratius Munishi, Frank Domayo, Kelvin Yondani na Mrisho Ngasa. Pia kipa Ivo Mapunda ameondolewa katika kikosi hicho baada ya kupata msiba.

Nafasi zao zimezibwa na wachezaji Abdi Banda (Coastal Union), Himid Mao (Azam), Juma Luizio (Mtibwa Sugar), Said Moradi (Azam) na Shabani Kado (Coastal Union).

Taifa Stars itaingia kambini keshokutwa (Machi 1 mwaka huu) jioni kwenye hoteli ya Accomondia jijini Dar es Salaam, na itaondoka Machi 3 mwaka huu alfajiri kwa ndege ya South African Airways na kurejea nchini Machi 7 mwaka huu saa 8.15 mchana.