ASKARI MWENYE BIDII HATIMAYE AMEJISHINDIA MILLION MBILI
Kwa
wale wapitao Mwai Kibaki Road zamani Old Bagamoyo Road watakuwa
wanamjua Askari huyu ambaye amekuwa akijituma vilivyo pale darajani
Mlalakuwa, Kawe. Askari huyu alikuwa akimbii mvua, yuko mapema asubuhi,
yuko usiku na achoki, labda tu kama ana weakness zake mchana kama vile
kwenda kuganga njaa sehemu nyingine kama ilivyo desturi ya askari
wengine wa usalama barabarani.
Kamanda
wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam Suleiman Kova(wa tatu toka
kushoto) akiwa kwenye picha ya pamoja na Askari wa usalama barabarani,
Moses Alphage (wa pili kushoto) aliyeibu ka kidedea kwenye program ya
kuhamasisha na kupongeza utendaji kazi wa askari wa usalam barabarani
jijini Dar es salaam iliyonedeshwa na kituo hicho cha Redio na
kujishindia Sh 2 Milioni. Wa kwanza kushoto ni Mfanyakazi wa Vodacom
Tanzania Albert Maneno na kulia ni mtangazaji wa Clouds Said Mohamed
maarufu Bonge.
Mfanyakazi
wa Idara ya Masoko wa Kampuni ya Vodacom Albert Maneno (wa tatu
kushoto) akiongea kabla ya kukabidhi Sh. 2 milioni kwa askari wa kikosi
cha Usalama Barabarani Moses Alphage (wa kwanza kushoto) aliyeibuka
kidedea katika program ya kuibua hamasa ya kazi kwa askari hao jijini
Dar es Salaam iliyoendeshwa na kituo cha Redio Clouds FM. Fedha hizo
zimetolewa na wafanyakazi wa Vodacom pamoja na wananchi mbalimbali
walioguswa na programu hiyo. Wa kwanza kulia ni Kamanda wa Polisi Kanda
Maalum ya Dar es salaam Kamishna Suleiman Kova.