Bayport yakabidhi madarasa matatu yenye thamani ya shilingi m 200/- kwa kituo cha KCVC.

November 09, 2016

Mkuu wa wilaya  ya  Kibaha Mh AsumtaMshama, akishuhudia  uzinduzi  wa   moja  ya  madarasa  ya  kituo cha watoto yatima cha KCVC uliofanywa na mlezi kituo  hicho mama Anna Mkapa na mwenyekitiwabodiya Bayport Tanzania Dkt. Ken Kwaku  hafla  iliyofanyika  kijiji cha Simbani   wilaya  ya Kibaha  mkoa  wa   Pwani
Watoto  wanaolelewa    katika  kituo cha KCVC wakiimba  wimbo    maalumu.

Afisa  Mtendaji Mkuu wa Bayport Tanzania, John Mbaga  akiongea na wageni  waalikwa  katika hafla ya  uzinduzi wa  kituo cha KCVC.
Mlezi kituo  hicho mama Anna Mkapa akitoa hotuba kwa wageni waalikwa 
Mkuu wa  wilaya  ya  Kibaha  mh Asumta  Mshama akiongea na  wageni  waalikwa  katika  hafla ya uzinduzi  wa kituo cha KCVC.
Viongoziwa Bayport wakiongeana Mama Anna Mkapa.
Viongozi  wa Bayport Tanzania wakiwa  katika  picha  ya  pamojana Mkuu wa  wilaya  ya  Kibaha  Mh  Asumpta  Mshama, Mama Anna Mkapa, mtoto Esther Furaha  pamoja   na  wasimamizi wa kituo cha Kibaha Children’s village centre.


MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA AVIFUTIA USAJILI WA KUDUMU VYAMA VITATU VYA SIASA

November 09, 2016
 Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, Monica Mnanka (kushoto), akizungumza na waandishi wa habariwakati akimkaribisha msajili wa vyama kuzungumza na wanahabari Dar es Salaam leo asubuhi. Kulia ni Msaji Msaidizi wa Vyama vya Siasa, Sisty Nyahoza na Msajili wa Vyama, Jaji Francis Mutungi.
 Msajili wa VVyama vya Siasa nchini, Jaji Francis Mutungi (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, wakati akitoa taarifa ya kufutwa kwa usajili wa kudumu wa vyama vitatu vya siasa ambavyo ni Chama cha Haki na Ustawi (Chausta), chama cha The African Progressive Party of Tanzania (APPT Maendeleo) na Chama cha Jahazi Asilia. Kulia ni Msajili Msaidizi, Sisty Nyahoza.
 Mkutano na wanahabari ukiendelea.
Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.

Na Dotto Mwaibale

MSAJILI wa Vyama vya Siasa nchini Jaji Francis Mutungi kwa mamlaka aliyonayo chini ya kifungu cha 19 cha Sheria ya vyama vya Siasa namba 5 ya mwaka 1992, amevifutia usajili wa kudumu vyama vitatu vya siasa kuanzia leo hii.

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari ofisini kwake leo asubuhi Jaji Mutungi alivitaja Vyama alivyovifuta kuwa ni Chama cha Haki na Ustawi (Chausta), kilichopata usajili wake Novemba 15, 2001 kilichokuwa kikiongozwa na James Mapalala kama Mwenyekiti wa Taifa na Mwaka Lameck Mgimwa kama Katibu Mkuu.

Chama kingine alichokifutia usajili wa kudumu ni Chama cha The African Progressive Party of Tanzania (APPT Maendeleo)  kilichopata usajili Machi 4, 2003 kilichokuwa kikiongozwa na Peter Kuga Mziray kama Rais Mtendaji Taifa na Nziamwe Samwel kama Katibu Mkuu.

Jaji Mutungi alikita chama kingine alichokifuta kuwa ni  Chama cha Jahazi Asilia kilichokuwa kikiongozwa Kasimu Bakari Ally kama Mwenyekiti wa Taifa na Mtumweni Jabir Seif kama Katibu Mkuu ambacho kilipata usajili wa kudumu Novemba 17, 2004.

Mutungi alisema vyama hivyo vimepoteza sifa za usajili wa kudumu kwa kukiuka masharti ya Sheria ya Vyama vya Siasa, ambapo kila chama klipewa taarifa ya nia ya Msajili wa Vyama vya siasa kufuta usajili wake wa kudumu na kutakiwa kueleza kwanini kisifutwe ambapo vilishindwa kutoa sababu za kuridhisha kuwa havikukiuka sheria na bado vinavyo sifa za usajili wa kudumu.

SBL yatoa elimu kuhusu unywaji pombe kistaarabu Mkoani Dodoma

November 09, 2016
 Meneja wa SBL wa Uwajibikaji Katika Jamii, Hawa Ladha, akitoa semina  elekezi kuhusu kampeni unywaji kistaarabu kampeni ambayo imezinduliwa mapema leo katika Hotel ya Morena mkoani Dodoma 

Meneja wa mauzo wa SBL  mkoa wa Dodoma Adam Nelson akiteta jambo na Mwakilishi wa Mkuu wa Usalama wa Barabarani wa Mkoa wa Dodoma CP Steven Nchai katika mkutano uliokutanisha wadau mbali mbali katika mkoa wa Dodoma wakati wa uzinduzi wa kampeni ya Unywaji kistaarabu uliofanyika katika Hoteli ya Morena mapema leo mkoani Dodoma
Wadau mbali mbali kutoka mkoa wa Dodoma wakifuatilia kwa makini mkutano huo wa uzinduzi wa kampeni ya Unywaji kistarabu uliofanyika mapema leo Morena Hoteli Mkoani Dodoma.

Mwakilishi wa Mkuu wa Usalama wa Barabarani wa Mkoa wa Dodoma CP Steven Nchai akitoa hotuba   katika mkutano uliokutanisha wadau mbali mbali katika mkoa wa Dodoma wakati wa uzinduzi wa kampeni ya Unywaji kistaarabu uliofanyika katika Hoteli ya Morena mapema leo mkoani Dodoma
 Meneja wa SBL wa Uwajibikaji Katika Jamii, Hawa Ladha akitoa maelezo kwa waandishi wa habari mara baada ya    uzinduzi wa kampeni ya Unywaji kistaarabu  katika mkutano uliokutanisha wadau mbali mbali kutoka mkoa wa Dodoma wakati wauliofanyika katika Hoteli ya Morena mapema leo mkoani Dodoma  

Picha ya pamoja mara baada ya uzinduzi wa kampeni ya unywaji kistaarabu



Meneja wa SBL wa Uwajibikaji Katika Jamii, Hawa Ladha Akisaidiana na Mwakilishi wa Mkuu wa Usalama wa Barabarani wa Mkoa wa Dodoma CP Steven Nchai na Meneja wa mauzo wa SBL mkoa wa  Dodoma Adam Nelson kuvisha kava la gari lenye ujumbe unaoendana na kampeni ya unywaji kistaarau iliyozinduliwa mapema leo Morena Hoteli Mkoani Dodoma.

Mwakilishi wa Mkuu wa Usalama wa Barabarani wa Mkoa wa Dodoma CP Steven Nchai akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya uzinduzi wa kampeni ya Unywaji kistaarabu iliyozinudliwa na SBl mapema leo katika Mkoa wa  Dodoma.



 Dodoma , Novemba 9 , 2016. Kampuni ya bia ya Serengeti imezindua kampeni inayohamasisha matumizi sahihi ya pombe au unywaji pombe kistaarabu. Kampeni hii ni hatua muhimu katika sekta ya biashara ya pombe kwa kutambua changamoto inazokabiliana nazo hususan katika masuala ya uwajibikaji kwa jamii.  
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo Mwakilishi wa Mkuu wa Usalama wa Barabarani wa Mkoa wa Dodoma CP Steven Nchai, amesema kulishirikisha jeshi la polisi, kikosi cha usalama barabarani, kunaonyesha ni kwa jinsi gani SBL wanatilia maanani suala zima la usalama barabarani hasa matokeo ya ulevi na uendeshaji vyombo vya moto. Uzoefu unaonyesha kwamba watu wengi hujisahau na kujiingiza katika ulevi wa kupindukia  bila kuzingati vyombo vya moto wanavyoendesha.
“Ni jambo lilisilopingika kuwa uzembe na unywaji wa pombe kupita kiasi vina athari kubwa kwa jamii. Madhara hayo hayamuathiri mtumiaji wa pombe peke yake, bali uhatarisha maisha na kuathiri mustakabali wa watu wengi” aliongeza Nchai.
“Kwa matinki hiyo, ni janga la jamii nzima – huduma zetu za afya zimeelemewa kwa kiasi kikubwa na wale waliojeruhiwa katika masuala yanayohusiana na ajali na uhalifu; taasisi zetu za masuala ya sheria zimeelemewa vilivyo; uzalishaji unaathirika mno na kwa mlolongo huo, ukuaji wa pato la taifa hubakia kuwa wa kiwango cha chini”, alisema Nchai.
Akielezea jinsi kampeni hii itakavyosaidia CP Nchai anasema “ama kwa hakika, sote kwa ujumla wetu tunaathirika – na sote tunalo jukumu la kuchangia namna bora ya kukabiliana na tatizo la ulevi. Nafurahi kuona kwamba wazalishaji wenyewe wa vinywaji vya pombe wametambua kuwa biashara wanayofanya kwa wateja wao inahitaji uwajibikaji na umakini wakati wa kutumia”.  
Kampeni hii ya unywaji wa kistaarabu inakusudia kuwafikia vijana wengi pamoja na watu wa rika la juu kwa kuwataka kuelewa hatari ya matumizi ya pombe na kufanya maamuzi kwa faida zao – maamuzi ambayo yatanusuru mustakabali wao wa baadaye.
Naye Meneja wa SBL wa Uwajibikaji Katika Jamii, Hawa Ladha, amesema kampeni ya unywaji pombe kistaarabu inalenga kuwapa walengwa elimu kwamba mtumiaji wa pombe hahitaji kutawaliwa na pombe na kuipa nafasi ibadili mustakabali wa maisha wake na kuongeza kwamba vifo na ajali nyingi hutokana na uzembe au ulevi wa watu ambao si waathirika wakubwa wa pombe – ambao wangeweza kuwa waangalifu kama wangechukua tahadhari na kujifikiria marambili au kama marafiki zao wasingewahamasisha ku-“ongeza moja …au mbili”, alisema.

NAIBU SPIKA TULIA AKSON AWA KINARA UCHEZAJI NETIBOLI DODOMA

November 09, 2016

 Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Tulia Akson (kulia), wa timu ya Bunge  akidaka mpira ulioelekezwa golini kwake walipocheza na timu ya Wilaya ya Chato katika mchezo wa kirafiki wa netiboli uliofanyika hivi karibuni kwenye Uwanja wa Jamhuri Dodoma. PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG







DONALD TRUPMP ASHINDA URAIS MAREKANI

DONALD TRUPMP ASHINDA URAIS MAREKANI

November 09, 2016
trump
Rais Mteule wa Marekani, Donard Trump akiwahutubia wananchi wa Marekani muda mfupi baada ya kutangazwa mshindi wa kiti hicho, mapema leo. Trump anakuwa Rais wa 45 wa nchi hiyo akitokea chama cha Republican. Kulia kwake ni aliekuwa mgombea mwenza wake, Mike Pence na kushoto kwake ni Mtoto wake, Barron Trump.
trump1
Hali halisi inavyoonekana katika majimbo ambayo Donald Trump ameshinda
MATUKIO KATIKA PICHA KUTOKA BUNGENI DODOMA NOVEMBA 9, 2016

MATUKIO KATIKA PICHA KUTOKA BUNGENI DODOMA NOVEMBA 9, 2016

November 09, 2016
dl1
Baadhi ya wabunge na mawaziri wakiwasili katika viwanja vya Bunge kuhudhuria kikao cha saba cha mkutano wa tano wa Bunge la 11 linaloendelea Mjini Dodoma Novemba 9, 2016.
dl2
Baadhi ya wabunge na mawaziri wakiwasili katika viwanja vya Bunge kuhudhuria kikao cha saba cha mkutano wa tano wa Bunge la 11 linaloendelea Mjini Dodoma Novemba 9, 2016.
dl4
Baadhi ya wabunge na mawaziri wakiwasili katika viwanja vya Bunge kuhudhuria kikao cha saba cha mkutano wa tano wa Bunge la 11 linaloendelea Mjini Dodoma Novemba 9, 2016.
dl5 dl7
dl07
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Tulia Ackson akiongoza kikao cha saba cha mkutano wa tano wa Bunge la 11 linaloendelea Mjini Dodoma Novemba 9, 2016.
dl11
Naibu Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Mhandisi Edwin Ngonyani  akijibu hoja mbalimbali kutoka kwa wabunge katika kikao cha saba cha mkutano wa tano wa Bunge la 11 linaloendelea Mjini Dodoma Novemba 9, 2016.
dl12
Naibu Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi Mhe. William Ole Nashi  akijibu hoja mbalimbali kutoka kwa wabunge katika kikao cha saba cha mkutano wa tano wa Bunge la 11 linaloendelea Mjini Dodoma Novemba 9, 2016.
dl13
Naibu Waziri wa Nishati na Madini Mhe. Medard Kalemani  akijibu hoja mbalimbali kutoka kwa wabunge katika kikao cha saba cha mkutano wa tano wa Bunge la 11 linaloendelea Mjini Dodoma Novemba 9, 2016.
dl14
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Mwigulu Nchemba  akijibu hoja mbalimbali kutoka kwa wabunge katika kikao cha saba cha mkutano wa tano wa Bunge la 11 linaloendelea Mjini Dodoma Novemba 9, 2016.
dl15
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Philip Mpango akijibu hoja mbalimbali kutoka kwa wabunge katika kikao cha saba cha mkutano wa tano wa Bunge la 11 linaloendelea Mjini Dodoma Novemba 9, 2016.
dl16
Mbunge wa Viti maalum Mkoa wa Iringa Mhe. Dkt Christine Ishengoma akiuliza swali  katika kikao cha saba cha mkutano wa tano wa Bunge la 11 linaloendelea Mjini Dodoma Novemba 9, 2016.
dl17
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa akijadilana jambo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge Kazi Ajira na Watu wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama katika kikao cha saba cha mkutano wa tano wa Bunge la 11 linaloendelea Mjini Dodoma Novemba 9, 2016.
dl18
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora Mhe. Angella Kairuki (kulia) akijadilana jambo na Wazirin wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. George Simbachawene katika kikao cha saba cha mkutano wa tano wa Bunge la 11 linaloendelea Mjini Dodoma Novemba 9, 2016.
Picha zote na Idara ya Habari MAELEZO Dodoma.

MWAKA MMOJA WA RAIS MAGUFULI: PPF YATEKELEZA KWA VITENDO UWEKEZAJI KWENYE VIWANDA

November 09, 2016


NA DAUDI MANONGI, MAELEaZO.

Novemba 5 mwaka 2016 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt.John Pombe Magufuli ametimiza mwaka mmoja tangu alipoingia madarakani akiwa na dhamira mpya ya serikali ya awamu ya tano ya kuifanya Tanzania kuwa nchi ya viwanda na uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.

Mara kadhaa Rais Magufuli amekuwa akisisitiza umuhimu wa viwanda ambapo anasema vinaweza kutengeneza ajira kwa watanzania waliojiajiri wakiwemo vijana wanaohitimu vyuo mbalimbali nchini.Katika kutimiza azma iyo aliagiza mifuko ya Hifadhi ya Jamii ijikite zaidi kwenye uwekezaji wa viwanda ili kuunga mkono lengo la Serikali.

Katika kutekeleza agizo la Rais Magufuli tayari mfuko wa Pensheni wa PPF umeanza kutekeleza agizo hilo kwa kuingia ubia na jeshi la Magereza na kuanzisha kiwanda cha kuzalisha viatu na bidhaa za ngozi.Makubaliano haya yalisainiwa na Mkurugenzi Mkuu wa PPF Bw.William Erio na Kamishna Jenerali wa Magereza Bw.John Minja Octoba 4, 2016 katika ukumbi wa mikutano wa makao Makuu ya Jeshi la Magereza uliopo Jijini Dar es Salaam.

Aidha katika makubaliano hayo PPF itakarabati na kuboresha miundombinu ya kiwanda cha viatu cha karanga ambacho uzalishaji ulianza mwaka 1977 na kufunguliwa na Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Pamoja na kiwanda cha sasa PPF itajenga kiwanda kipya cha kisasa ambacho kitakuwa kikisindika ngozi na kuzalisha bidhaa zitokanazo na ngozi kwa kutumia mashine za kisasa na teknolojia ya hali ya juu na hivyo kuongeza uzalishaji na kupanua masoko ya viatu nchini na kuongeza pato la Taifa.

Akizungumza wakati wa kutiwa saini mkataba wa makubaliano Mkurugenzi Mkuu wa PPF Bw. William Erio alisema kuwa ujenzi wa kiwanda hicho ni utekelezaji wa lengo la Serikali la kuwa na uchumi wa viwanda na faida kubwa kwa nchi kwa kutumia malighafi zinazopatikana hapa nchini kwa ajili ya soko la ndani na hivyo kuokoa matumizi ya fedha za kigeni ambazo zingetumika kununua malighafi mbalimbali kutoka nje ya nchi.

Vile vile kiwanda hicho kipya kitatoa ajira kwa watanzania lakini pia PPF itanufaika kwa faida itokanayo na uwekezaji pamoja na kupata wananchama wapya watakaojiunga na mfuko huo.

Aidha Mkurugenzi Mkuu wa PPF Bw.William Erio alisema uzalishaji katika kiwanda kipya cha uchakataji ngozi unatarajiwa kuanza mwaka 2018 na kwamba katika kipindi ambacho ujenzi wa kiwanda kipya utakuwa unaendelea kile cha zamani kitaboreshwa ili kuongeza zaidi ufanisi wa uzalishaji.

Katika hatua nyingine mfuko wa PPF umeanza hatua za awali za kuwekeza katika kiwanda cha Sukari eneo la Mkulazi lililopo kilometa 195 kutoka Manispaa ya Morogoro na km 75 kutoka Ubena-Zomozi barabara kuu ya Dar es Salaam na Morogoro ambapo uwekezaji huo utafanyika kwa ubia kati ya PPF na NSSF kwenye eneo lenye ukubwa wa zaidi ya hekta 63000 ambapo tayari kampuni ya pamoja imeshaanzishwa azma hiyo.

Kiuchumi eneo la Mkulazi liko karibu na Reli ya kati kwenye kituo cha Ngerengere na lipo karibu na Reli ya TAZARA kupitia kituo cha kidunda hivyo uwekezaji katika eneo hilo utafanya usafirishaji wa malighai na bidhaa kuwa rahisi.

Kiwanda hicho kitazalisha zaidi ya tani 200,000 za Sukari kwa mwaka lakini pia kitatoa ajira za moja kwa moja na ajira shirikishi kwa watanzania zaidi ya 100000 na hivyo kutimiza lengo la Rais na Serikali yake katika kutatua changamoto ya ukosefu wa ajira pamoja na kuongeza pato la Taifa.

Mkurugenzi Mkuu wa PPF Bw.William Erio alisema uwekezaji huu utafanyika katika awamu mbili ambapo awamu ya kwanza itahusisha uzalishaji wa Miwa na ujenzi wa kiwanda cha Sukari na awamu ya pili utahusisha kilimo cha nafaka kama vile Mahindi,Mpunga na Mtama.

PPF itaendelea kuunga mkono juhudi za Rais Magufuli katika kufanikisha azma yake ya Tanzania ya viwanda kwa kuwekeza katika maeneo yenye tija kwa mfuko ili kukuza uwekezaji na tija kwa wanachama na jamii kwa ujumla.

Katika kuzidi kuunga mkono Serikali ya awamu ya tano na falsafa yake ya “Hapa kazi tu” PPF itafanya uwekezaji wa ujenzi wa jengo la kiwanda kwenye kiwanda cha nguo cha Touku kilichopo eneo la Mabibo katika ukanda maalumu wa kiuchumi wa Benjamin Mkapa ambapo kiwanda hiki huzalisha nguo zenye ubora kwa ajiri ya soko la Marekani kupitia mpango wa ukuzaji fursa za kiuchumi Afrika AGOA(African Growth and Opportunity Act uku uwekezaji wa Jengo la kiwanda utapanua wigo wa ajira kwa watanzania kutoka 1600 waliopo sasa mpaka kufikia ajira 7000.

Mfuko wa PPF unaendelea kuunga mkono juhudi za Rais Magufuli za kuwafikia watanzania wajasiriamali ili kuboresha biashara na maisha yao.

Sanjari na hilo tayari PPF imeanzisha mfumo wa uchangiaji wa hiari ujulikanao kama Wote Scheme ambao unawalenga wanachama waliojiajiri wenyewe katika sekta isiyo rasmi ambao kwa mujibu wa takwimu za kitaifa sekta hiyo inachukua zaidi ya asilimia 90 ya nguvu kazi ya Taifa.

Mfuko huu unawalenga watu waliojiajiri katika makundi ama mtu mmoja wakiwemo wakulima, wavuvi, wafugaji, madereva wa daladala, bodaboda ,mabasi,Teksi,Mama lishe,Wajasiriamali mbalimbali wenye maduka na biashara nyingine pamoja na vikundi vya Vikoba.

Kwa kupitia mfumo wa wote Scheme watanzania watakuwa na uhakika wa kupata bima ya afya,mkopo wa elimu na maendeleo ya biashara pamoja na pensheni ya uzeeni endapo mwanachama atafikia kiwango cha kustaafu.

Kupitia mfumo wa wote scheme watanzania watakuwa na uhakika wa kupata bima ya afya,mkopo wa elimu na maendeleo ya biashara pamoja na pensheni ya uzeeni endapo mwanachama atafikia kiwango cha kustaafu.

Kupitia mfumo wa wote scheme mwanachama anaweza kuchangia kiwango kisichopungua elfu ishirini kwa mwezi au zaidi na mfumo huu ni rahisi sana ambapo wanachama wanaweza kulipa michango yao kwa simu ya mkononi kupitia mifumo kama vile M-pesa,Airtel Money,Tigo Pesa popote pale walipo eneo lao la kazi bila hata kufika ofisi za PPF.

Pamoja na hayo tunayaomba makundi mbalimbali ya wajasiriamali walioko katika sekta isiyo rasmi kujiunga na mfumo huu kwa faida ya maisha yao ili waweze kufaidika na huduma mbalimbali zinazotolewa katika mfumo huu.

Pamoja na Mfuko wa PPF kusajili wanachama kukusanya michango kuwekeza na kulipa mafao imekuwa mstari wa mbele kuchangia katika shughuli za kijamii kama vile afya,elimu na kuchangia kwenye maendeleo ya jamii katika kuendelea kuunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya tano kwenye sekta ya elimu mfuko wa PPF umekuwa mstari wa mbele kuchangia changamoto ya upungufu wa madawati kwa shule za msingi na sekondari kitaifa.

PPF imeendelea kuunga mkono mpango wa serikali katika kutatua changamoto ya madawati kwenye shule mbalimbali ambapo mfuko umechangia shilingi milioni 200 katika kufanikisha mpango huo uku lengo kuu la mfuko wa PPF likiwa ni kuhakikisha wanafunzi hawasomi wakiwa wamekaa chini kwani ndio nguvu kazi ya Taifa la Kesho na ni wanachama watarajiwa katika mifuko ya hifadhi ya jamii ikiwemo PPF.

WAKUU WA MIKOA NA WILAYA WAASWA KUENDELEA KUTOA USHIRIKIANO KWA WAWEKEZAJI NCHINI

November 09, 2016


Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji Dkt.Adelhelm Meru akiwasili katika kiwanda cha kutengeneza Vifungashio kilichopo Wilayani Kibaha Mkoani Pwani kwa ajili ya kuweka Jiwe la Msingi, Katikati ni Mtendaji Mkuu wa Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC) Mlingi Mkucha na kulia ni Mkurugenzi Muendeshaji wa Kiwanda hicho Bw. Joseph Wasonga.
Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji Dkt.Adelhelm Meru akisalimiana na baadhi ya wageni waliohudhuria hafla ya uwekaji jiwe la msingi katika kiwanda cha kutengeneza vifungashio cha Global Packaging Limited kilichopo Wilayani Kibaha Mkoani Pwani.
Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji Dkt.Adelhelm Meru akisaini kitabu cha wageni alipofika katika kiwanda cha kutengeneza Vifungashio kilichopo Wilayani Kibaha Mkoani Pwani kwa ajili ya kuweka Jiwe la Msingi.
Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji Dkt.Adelhelm Meru (Katikati), Mkurugenzi Muendeshaji wa Kiwanda hicho Bw. Joseph Wasonga(kushoto) na Mtendaji Mkuu wa Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC) Mlingi Mkucha wakielekea ndani ya kiwanda kuangalia mitambo na hatua iliyofikiwa kabla ya kuanza kazi ya kiwanda hicho.
Mitambo itakayotumika katika kuzalishia vifungashio ikiwa tayari imekwisha fungwa tayari kwa kuanza kazi.
Mkurugenzi Muendeshaji wa Kiwanda cha kutengeneza vifungashio cha Global Packaging Limited Bw. Joseph Wasonga na wafanyakazi wa kiwanda wakimtembeza Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji Dkt.Adelhelm Meru na kumpa maelekezo mbalimbali juu ya hatua iliyofikiwa kabla ya kiwanda hicho hakijaanza kufanya kazi na kuzalisha vifungashio.
Mtendaji Mkuu wa Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC) Mlingi Mkucha akiongea wakati wa hafla ya uwekaji jiwe la msingi katika kiwanda cha kutengeneza vifungashio cha Global Packaging Limited kilichopo Wilayani Kibaha Mkoani Pwani na kuwataka watanzania wenye nia ya kuwekeza katika sekta ya viwanda kupeleka maandiko ya miradi yao katika shirika hilo na watampa ushirikiano wa kutosha ili kuweza kutimiza lengo la serikali ya awamu ya tano ya kuwa na serikali ya viwanda.