MBUNGE ATAJA SABABU YA WILAYA YA PANGANI KURUDI NYUMA KIUCHUMI

June 03, 2017
MBUNGE wa Jimbo la Pangani (CCM) Jumaa Aweso ametaja sababu kubwa iliyoifanya wilaya hiyo kurudi nyuma kiuchumi ni kutokana na kuchelewa kuwekeza kwenye suala la elimu na miundombinu ya barabara ambacho ni kilio cha muda mrefu.

Hivyo kuitaka jamii kuona umuhimu wa kuwekeza kwenye elimu ili iwe chachu ya kuinua maendeleo yao lakini pia serikali iboreshe miundombinu ya barabara ya Tanga -Pangani hadi Sadaani ambayo imekuwa ikipigiwa kelele na wabunge waliopita bila mafanikio

Aweso aliyasema hayo hivi karibuni wakati akizungumza na wananchi wa Jimbo hilo ambapo alisema wazazi hawana budi kuwekeza kwenye elimu iliwaweze kupatikana wataalamu watakaosaidia harakati za kuinua maendeleo.

Alisema ili katika mipango mikubwa ya kufanikisha azma hiyo ndio sababu kubwa wakaanzisha mpango mahususi wa niache nisome mwaka jana ambao umepata mafanikio makubwa.

“Mpango wa niache nisome umekuwa mkombozi mkubwa wa kuihamasisha jamii ya wana pangani kuona umuhimu wa kupata elimu na mafanikio yaliyopatikana ni mengi ikiwemo kupata fursa mwaka huu kuwapeleka vijana wengi Jeshini “Alisema

Aidha aliwataka viongozi chama na serikali kuendelea kushirikiana na wataalamu ili kuwezesha kuifungua wilaya ya Pangani ambayo inahitaji kupiga hatua kubwa za kimaendeleo.

“Uchumi wa Pangani ni zao la Mnazi na mtu mpaka aje wilayani hapa lazima awe na sababu maalumu ikiwemo kufiwa nah ii inasababishwa na miundombinu mibovu ya barabara hivyo ujenzi huo utakapoanza utasaidia kufungua uchumi huo “Alisema.

Mbunge huyo aliwataka pia wananchi wa wilaya hiyo kutunza maeneo yao kwa kuacha kuyauza ovyo kutokana na fursa kubwa inayokuja mkoani hapa ikiwemo mradi mkubwa wa bomba la mafuta.

WAZIRI MKUU AAGIZA KILOSA WAILIPE GAIRO DENI LA0

WAZIRI MKUU AAGIZA KILOSA WAILIPE GAIRO DENI LA0

June 03, 2017
GAI1
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akipokelewa na Mkuu wa Wilaya ya Gairo, Bi. Seriel Mchembe mara baada ya kuwasili wilayani humo (Juni 3, 2017) kwa ziara ya kikazi ya siku moja. Katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dkt. Stephen Kebwe. (Picha na OWM).
GAI2
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisalimiana na Mbunge wa Jimbo la Gairo, Bw. Ahmed Shabiby mara baada ya kuwasili wilayani humo (Juni 3, 2017) kwa ziara ya kikazi ya siku moja. Wa pili kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dkt. Stephen Kebwe nawa pili kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Gairo, Bi. Seriel Mchembe (Picha na OWM).
GAI3
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisalimiana na Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro, Bw. Cliford Tandari mara baada ya kuwasili wilayani humo (Juni 3, 2017) kwa ziara ya kikazi ya siku moja. Wa pili kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Mvomero. (Picha na OWM).
GAI4
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akipanda mti nje ya Ofisi ys Mkuu wa Wilaya ya Gairo mara baada ya kuwasili wilayani humo (Juni 3, 2017) ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha Siku ya Upandaji Miti Kitaifa. Wengine ni viongozi wa Mkoa na Wilaya wakishuhudia. (Picha na OWM).
GAI5
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akimwagilia mche alioupanda nje ya Ofisi ys Mkuu wa Wilaya ya Gairo mara baada ya kuwasili wilayani humo (Juni 3, 2017) ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha Siku ya Upandaji Miti Kitaifa. Wengine ni viongozi wa Mkoa na Wilaya wakishuhudia. (Picha na OWM).
GAI6
Viongozi na watumishi wa Wilaya ya Gairo wakimsikiliza Waziri Mkuu Kassim Majaliwa (hayupo pichani) katika mkutano aliouitisha mjini Gairo Juni 3, 2017. (Picha na OWM).
GAI7
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza na viongozi na watumishi wa Wilaya ya Gairo (hawapo pichani) katika mkutano aliouitisha mjini Gairo Juni 3, 2017 (Picha na OWM).
………………………………………………………………………………………..
* Ni la sh. milioni 213/- la fedha za maendeleo.
*Ataka apewe taarifa ifikapo Juni 30.       
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemwagiza Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro, Bw. Clifford Tandari aitishe kikao na uongozi wa Halmashauri ya Kilosa na kupata kauli yao ni lini watalipa zaidi ya sh. milioni 210 wanazodaiwa na Halmashauri ya Gairo.
“Katibu Tawala itisha kikao cha Mwenyekiti wa Halmashauri, Mkuu wa Wilaya na Mkurugenzi wa Halmashauri, waseme ni lini watazileta fedha hizo ambazo zilitumwa kwao wakati Halmashauri ya Wilaya ya Gairo ikiwa haijafungua akaunti zake,” amesema.
Ametoa agizo hilo leo (Jumamosi, Juni 3, 2017) wakati akizungumza na viongozi wa mkoa wa Morogoro, wilaya ya Gairo na watumishi wa Halmashauri ya Gairo mara baada ya kupokea taarifa ya mkoa na wilaya katika kikao kilichofanyika Gairo mjini
“Kilosa ni lazima wazilipe hizo fedha. Katibu Tawala simamia zoezi hilo na kama watachelewa, uzikate moja kwa moja kwenye fedha yao wanayoletwa kutoka Ofisi ya Rais (TAMISEMI). Nataka nipewe taarifa ya maamuzi hayo kabla Juni haijaisha,” amesema.
Mapema akitoa taarifa ya wilaya hiyo, Mkuu wa Wilaya ya Gairo, Bi. Siriel Mchembe alisema wanaidai Halmashauri ya Kilosa sh. 233,228,679 ambazo ziliingizwa huko wakati wilaya hiyo  inaanzishwa na hawakuwa wamefungua akaunti ya wilaya.
“Fedha hizi zilikuwa zinapitia Kilosa wakati wilaya ya Gairo imeanzishwa kwa kuwa kipindi hicho wilaya ya Gairo ilikuwa bado haijafungua akaunti. Fedha hizi zinajumuisha ruzuku ya uendeshaji, mapato ya ndani na miradi ya maendeleo,” alisema.
Alisema Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) iliagiza wilaya ya Kilosa ilipe deni hilo kabla ya Juni 2016 lakini hadi sasa wameshalipa sh. milioni 20 tu ambapo sh. milioni 10 zililipwa Desemba 2015 na nyingine milioni 10 zililipwa Mei 2017.
Akisisitiza kuhusu makusanyo ya mapato, Waziri Mkuu amewakumbusha watumishi hao kuwa Serikali imekwishatoa agizo la kutumia mashine za kielektroniki kukusanya mapato ifikapo Julai mosi.
“Makusanyo ya mapato ya ndani ni eneo muhimu sana. Tumeshaagiza, mwisho wa kutumia mifumo ya kawaida ni Juni 30. Kuanzia Julai mosi, kila eneo ni lazima litumie mashine za kielektroniki,” alisema Waziri Mkuu.
Alihoji ni kwa nini Halmashauri ya Gairo ililenga kukusanya sh.milioni 889.5 lakini kufikia Aprili mwaka huu, makusanyo halisi yalikuwa ni sh. milioni 356.2 sawa na asilimia 40.
Alitumia fursa hiyo kuwapongeza Mamlaka ya Mapato (TRA) ya wilaya hiyo ambao hadi kufikia Aprili, 2017 wameweza kukusanya sh. milioni 601.5 ikilinganishwa na makadirio yao ya kukusanya sh. milioni 471 kwa mwaka. Waziri Mkuu aliwapongeza kwa sababu wamevuka lengo kwa asilimia 127.6.
Waziri Mkuu ambaye yuko kwenye ziara ya siku ya wilaya hiyo, asubuhi alipanda mti kwenye Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ikiwa maadhimisho ya siku ya upandaji miti hapa nchini.
Pia alikagua mradi wa maji wa kijiji cha Chakwale, na mradi wa visima 10 ambayo imekuwa na mgogoro kwa muda mrefu. Pia atazungumza na wananchi wa Gairo mjini kwenye mkutano wa hadhara.

MAKAMU WA RAIS AWASILI BUTIAMA MKOANI MARA LEO

June 03, 2017

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiweka shada la maua juu ya kaburi la Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere mara baada ya kuwasili Butiama ambapo atakuwa mgeni rasmi kwenye  sherehe za siku ya mazingira Duniani ambazo Kitaifa zinafanyika Butiama mkoani Mara.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akitoa heshima mbele ya kaburi la Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere mara baada kuweka shada la maua,Makamu wa Rais yupo Butiama kuhudhuria sherehe za siku ya mazingira Duniani ambazo Kitaifa zinafanyika Butiama mkoani Mara.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye kikao cha kupokea taarifa ya mkoa wa Mara mara baada ya kuwasili Butiama kwenye makazi ya Hayati Baba wa Taifa.
                             …………………………………………………………………..


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan amewasili mkoani Mara alasiri ya leo 3-June-2017 akitokea mkoani Mwanza ambapo hapo kesho atakuwa ni mgeni rasmi katika kilele cha Siku ya Mazingira Duniani.
 
Alipowasili kijijini Butiama, Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan amepokelewa na Viongozi wa vyama vya siasa na watendaji mbalimbali wa Serikali ambao wameongozwa na Mkuu wa mkoa wa Mara Dkt Charles Mlingwa pamoja na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira January Makamba.
 
Makamu wa Rais pia amepokea taarifa ya maendeleo ya mkoa wa Mara na amepata fursa ya kuwasha mshumaa na kuweka shada la maua katika kaburi la baba wa Taifa Hayati Julius Nyerere lililopo Mwitongo kijijini Butiama.
 
Hapo kesho tarehe 4-June-2017 Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan ataongoza mamia ya wananchi wa mkoa wa Mara na mikoa ya Jirani katika Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani ambapo kitaifa sherehe hizo zitafanyika katika kijiji cha Butiama mkoani Mara.
Waziri Mavunde azindua mpango wa mafunzo ya ufundi wa kisasa wa kutengeneza viatu na bidhaa za ngozi jijini Mwanza

Waziri Mavunde azindua mpango wa mafunzo ya ufundi wa kisasa wa kutengeneza viatu na bidhaa za ngozi jijini Mwanza

June 03, 2017
DIT1
Naibu waziri ofisi ya waziri mkuu anaeshughulikia kazi, jira na maendeleo ya Vijana Mh Anthony Mavunde akizungumza wakati wa  uzinduzi wa  mpango wa mafunzo ya ufundi wa kisasa wa kutengeneza viatu kwa njia za kisasa uliofanyika kwenye chuo cha DIT Karakana ya Viatu jijini Mwanza leo.
DIT02
Baadhi ya wanafunzi walioshiriki katika uzinduzi huyo uliofanyika kwenye cho cha DIT Karakana ya Viatu jijini Mwanza.
DIT2
Naibu waziri ofisi ya waziri mkuu anaeshughulikia kazi, jira na maendeleo ya Vijana Mh Anthony Mavunde  akiwa katika picha ya pamoja na waalikwa waliohudhuria katika uzinduzi huo wa  mpango wa mafunzo ya ufundi wa kisasa wa kutengeneza viatu kwa njia za kisasa.
………………………………………………………………………………….
Naibu waziri ofisi ya waziri mkuu anaeshughulikia kazi, jira na maendeleo ya Vijana Mh Anthony Mavunde amefungua mpango wa mafunzo ya ufundi wa kisasa wa kutengeneza viatu kwa njia za kisasa kwa vijana 1000 wanaotaka mikoa zaidi ya kumi nchini. Akizundua mpango huo, Mhe Mavunde, amesema mpango huo unalenga kuwajengea uwezo wa kujiajiri vijana na pia kutumia bidhaa zitokanazo na mazao ya mifugo kwa ajili ya kuzalisha viatu na bidhaa za ngozi nchini. Amesema, serikali ya awamu ya tano chini ya Rais John Pombe Magufuli imejipanga kuhakikisha inatekeleza azma ya ujenzi wa viwanda kwa kuwajengea uwezo vijana ambao ni nguvu kazi ya taifa katika kujiandaa na mfumo wa mapinduzi ya viwanda ambavyo vimeshaanza kujengwa nchini. Aidha amewataka vijana kutochagua kazi au kubweteka kuwa kazi rasmi ni zile za ajira ya moja kwa moja serikali au sekta binafsi, amewataka vijana kubadilisha mtazamo wa maaana ya Ajira kwa kutokukaa na kusubiri nafasi za ajira. Amesema mpango huu wa miaka mitano unalenga kuwafikia vijana zaidi ya milioni 4 nchini katika kuwajengea uwezo ambao utawafanya kujiajiri au kuajiriwa katika Tanzania ya viwanda.
Imetolewa na Idara ya Habari na Mawasiliano. Wizara ya kazi,ajira, ulemavu na maendeleo ya vijana 03/06/2017

Wanawake Watakiwa Kujiamini Ili Wafanikiwe Katika Uongozi

June 03, 2017
Spika Mstaafu Anne Makinda akizungumza wakati wa hafla ya kuzindua Mradi wa “Wanawake Viongozi -Nguvu ya Mabadiliko” leo Jijini Dar es Salaam. Mradi huo wa miaka mitatu unalengo la kuwajengea uwezo wanawake 200 katika medani za uongozi wa kisiasa ili kufikia idadi ya asilimia 40 ya wanawake katika uongozi wa Serikali za Mitaa na Uchaguzi Mkuu 2020. unashirikisha asasi tatu ambazo ni Women Fund Tanzania, Kituo cha Utawala Bora na Maendeleo ya Uchumi (CGG & ED) na Taasisi ya Hanns Seidel Foundation (HSF) chini ya udhamini wa Umoja wa Nchi za Ulaya (EU).
Mkurugenzi wa Taasisi ya Hanns Seidel Foundation (HSF), Dkt. Susanne Luther akizungumza wakati wa hafla ya kuzindua Mradi wa “Wanawake Viongozi - Nguvu ya Mabadiliko” leo Jijini Dar es Salaam. Mradi huo wa miaka mitatu unalengo la kuwajengea uwezo wanawake 200 katika medani za uongozi wa kisiasa ili kufikia idadi ya asilimia 40 ya wanawake katika uongozi wa Serikali za Mitaa na Uchaguzi Mkuu 2020. Kulia ni Mkuu wa Sehemu ya Uchumi na Utawala kutoka Umoja wa Ulaya (EU), Oliveier COUPLEUX na Mwakilishi Mkazi wa HSF Tanzania na Uganda, Bi. Julia Berger.
Baadhi ya washiriki wakifuatilia hotuba ya Spika Mstaa Anne Makinda (hayupo pichani) wakati wa hafla ya uzinduzi wa Mradi wa “Wanawake Viongozi - Nguvu ya Mabadiliko” leo Jijini Dar es Salaam. Mradi huo wa miaka mitatu unalengo la kuwajengea uwezo wanawake 200 katika medani za uongozi wa kisiasa ili kufikia idadi ya asilimia 40 ya wanawake katika uongozi wa Serikali za Mitaa na Uchaguzi Mkuu 2020. unashirikisha asasi tatu ambazo ni Women Fund Tanzania, Kituo cha Utawala Bora na Maendeleo ya Uchumi (CGG & ED) na Taasisi ya Hanns Seidel Foundation (HSF) chini ya udhamini wa Umoja wa Nchi za Ulaya (EU).
Mratibu wa Mradi wa “Wanawake Viongozi - Nguvu ya Mabadiliko” Bw. Herry Lugala akifafanua jambo kuhusu mradi huo alipokuwa akiongea na waandishi wa habari mara baada ya kumalizika kwa hafla ya uzinduzi rasmi wa mradi huo leo Jijini Dar es Salaam. Mradi huo wa miaka mitatu unalengo la kuwajengea uwezo wanawake 200 katika medani za uongozi wa kisiasa ili kufikia idadi ya asilimia 40 ya wanawake katika uongozi wa Serikali za Mitaa na Uchaguzi Mkuu 2020, unashirikisha asasi tatu ambazo ni Women Fund Tanzania, Kituo cha Utawala Bora na Maendeleo ya Uchumi (CGG & ED) na Taasisi ya Hanns Seidel Foundation (HSF) chini ya udhamini wa Umoja wa Nchi za Ulaya (EU).
Spika Mstaafu Anne Makinda akiteta jambo na Mkurugenzi wa Taasisi ya Hanns Seidel Foundation (HSF), Dkt. Susanne Luther wakati wa hafla ya uzinduzi wa Mradi wa “Wanawake Viongozi -Nguvu ya Mabadiliko” leo Jijini Dar es Salaam. Mradi huo wa miaka mitatu kuanzia 2017 umelenga la kuwajengea uwezo wanawake 200 katika medani za uongozi wa kisiasa ili kufikia idadi ya asilimia 40 ya wanawake katika uongozi wa Serikali za Mitaa na Uchaguzi Mkuu 2020. unashirikisha asasi tatu ambazo ni Women Fund Tanzania, Kituo cha Utawala Bora na Maendeleo ya Uchumi (CGG & ED) na Taasisi ya Hanns Seidel Foundation (HSF) chini ya udhamini wa Umoja wa Nchi za Ulaya (EU).
Spika Mstaafu Anne Makinda akisikiliza maelezo kutoka kwa Afisa WA Taasisi ya Women Fund Tanzania Bi. Rose Julius (kulia) wakati alipokuwa akitendelea maonyesho yaliyoenda sambamba na uzinduzi wa Mradi wa “Wanawake Viongozi -Nguvu ya Mabadiliko” leo Jijini Dar es Salaam. Mradi huo wa miaka mitatu kuanzia 2017 umelenga la kuwajengea uwezo wanawake 200 katika medani za uongozi wa kisiasa ili kufikia idadi ya asilimia 40 ya wanawake katika uongozi wa Serikali za Mitaa na Uchaguzi Mkuu 2020. unashirikisha asasi tatu ambazo ni Women Fund Tanzania, Kituo cha Utawala Bora na Maendeleo ya Uchumi (CGG & ED) na Taasisi ya Hanns Seidel Foundation (HSF) chini ya udhamini wa Umoja wa Nchi za Ulaya (EU).
Spika Mstaafu Anne Makinda akiagana na Mwakilishi Mkazi wa HSF Tanzania na Uganda, Bi. Julia Berger wakati wa hafla ya uzinduzi wa Mradi wa “Wanawake Viongozi -Nguvu ya Mabadiliko” leo Jijini Dar es Salaam. Mradi huo wa miaka mitatu kuanzia 2017 umelenga la kuwajengea uwezo wanawake 200 katika medani za uongozi wa kisiasa ili kufikia idadi ya asilimia 40 ya wanawake katika uongozi wa Serikali za Mitaa na Uchaguzi Mkuu 2020. unashirikisha asasi tatu ambazo ni Women Fund Tanzania, Kituo cha Utawala Bora na Maendeleo ya Uchumi (CGG & ED) na Taasisi ya Hanns Seidel Foundation (HSF) chini ya udhamini wa Umoja wa Nchi za Ulaya (EU). Kushoto ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Hanns Seidel Foundation (HSF), Dkt. Susanne Luther.
Spika Mstaafu Anne Makinda na Mkurugenzi wa Taasisi ya Hanns Seidel Foundation (HSF), Dkt. Susanne Luther wakati katika picha ya pamoja mara baada ya kumaliza hafla ya uzinduzi wa Mradi wa “Wanawake Viongozi -Nguvu ya Mabadiliko” leo Jijini Dar es Salaam. Mradi huo wa miaka mitatu kuanzia 2017 umelenga la kuwajengea uwezo wanawake 200 katika medani za uongozi wa kisiasa ili kufikia idadi ya asilimia 40 ya wanawake katika uongozi wa Serikali za Mitaa na Uchaguzi Mkuu 2020. unashirikisha asasi tatu ambazo ni Women Fund Tanzania, Kituo cha Utawala Bora na Maendeleo ya Uchumi (CGG & ED) na Taasisi ya Hanns Seidel Foundation (HSF) chini ya udhamini wa Umoja wa Nchi za Ulaya (EU). Picha zote: Frank Shija - MAELEZO
MAADHIMISHO YA SIKU YA MAZINGIRA YAFANYIKA MKOANI MARA

MAADHIMISHO YA SIKU YA MAZINGIRA YAFANYIKA MKOANI MARA

June 03, 2017
bund1
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba akitoa maelezo ya awali ya ufunguzi katika mijadala ya kuadhimisha siku Mazingira Duniani Wilayani Butiama Mkoni Mara. Kauli mbiu ya mwaka huu ni “Mahusiano Endelevu Kati ya Binadamu na Mazingira.”
bund2
Wanajopo wa mada ya kwanza ya “Tanzania Bila Mkaa na Kuni Inawezekana?” kutoka kushoto ni Ndugu Charles Meshack Mkurugenzi Mkuu, Shirika la Kuhifadhi Misitu Asili Tanzania, Prof. Dos Santos Silayo Mkurugenzi Mkuu, Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) na Eng. Estomih Sawe Mkurugenzi Mtendaji TaTEDO (Center for Sustainable Modern Energy Initiative in Tanzania). Mjadala unaendelea Butiama katika kuadhimisha Siku ya Mazingira Duniani.
bund3
Mjadala ukiendelelea pichani, Wanajopo wa mada ya kwanza ya “Tanzania Bila Mkaa na Kuni Inawezekana?” kutoka kushoto ni Ndugu Charles Meshack Mkurugenzi Mkuu, Shirika la Kuhifadhi Misitu Asili Tanzania, Prof. Dos Santos Silayo Mkurugenzi Mkuu, wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), Bi. Maria Sarungi (Mwendesha Mada) na Eng. Estomih Sawe Mkurugenzi Mtendaji TaTEDO (Center for Sustainable Modern Energy Initiative in Tanzania). Kongamano linaendelea Butiama katika kuadhimisha Siku ya Mazingira Duniani.
bund4
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mhe. January Makamba akifuatilia mjadala katika Ukumbi wa Kanisa Katoliki Butiama- Mara. Wapili kushoto ni Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Prof. Faustin Kamuzora. Mijadala mbalimbali inaendelea katika kuadhimisha siku ya Mazingira Duniani. Kauli mbiu ya mwaka huu ni “Mahusiano Endelevu Kati ya Binadamu na Mazingira.”

MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA AFUNGUA SEMINA KWA WASTAAFU WATARAJIWA WA MFUKO WA PENSHENI WA PSPF

June 03, 2017
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu
Hassan akizungumza na Mkurugenzi Mkuu wa PSPF Bw. Adam Mayingu kabla ya
ufunguzi wa Semina kwa wastaafu watarajiwa iliyofanyika kwenye ukumbi wa
Benki Kuu jijini Mwanza
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati wa ufunguzi wa Semina kwa wastaafu watarajiwa iliyofanyika kwenye ukumbi wa
Benki Kuu jijini Mwanza
 Baadhi ya washiriki wa Semina ya Wastaafu Watarajiwa wakisikiliza kwa makini hotuba ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan iliyofanyika kwenye ukumbi wa Benki Kuu Mwanza.
 Baadhi ya washiriki wa Semina ya Wastaafu Watarajiwa wakisikiliza kwa makini hotuba ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan iliyofanyika kwenye ukumbi wa Benki Kuu Mwanza.
 Baadhi ya Wadau wakifuatilia ufunguzi wa Semina kwa Wastaafu Watarajiwa.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akionyesha Vitabu vya PSPF kwenye kutoa elimu kwa Wanachama wa mfuko huo.
                             …………………………………………………………
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan amewaagiza waajira wasiopeleka au kuchelewesha michango ya wanachama kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii nchini wachukuliwe hatua za kisheria ili kukomesha tabia hiyo.
Makamu wa Rais ametoa kauli hiyo 3-June-2017 Jijini
Mwanza wakati anafungua semina ya maisha baada ya kustaafu,fursa ya mafao,uwekezaji iliyoandaliwa na Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF) kwa ajili ya wastaafu watarajiwa 450 kutoka wilaya zote za mkoa wa Mwanza.
Makamu wa Rais amesisitiza kuwa waajiri wakichangia kwa mujibu wa sheria kwenye mifuko hiyo watawezesha wanachama wao kupata mafao kikamilifu na kwa wakati.
 
Kuhusu madeni ya Serikali kwa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii nchini, Makamu wa Rais amewahakikishia Wakurugenzi wa mifuko hiyo kuwa Serikali inashughulikia madeni hayo na baada ya kukamilika kwa zoezi la uhakiki wa madeni hayo basi malipo yatafanyika haraka iwezekanavyo.
 
Makamu wa Rais amesisitiza kuwa Serikali itaendelea kuhakikisha michango ya pensheni kwa wafanyakazi wa taasisi zinazopata ruzuku kutoka Serikalini inalipwa kwenye
mifuko hiyo kwa wakati.
 
Aidha, Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan amewahimiza wastaafu watarajiwa kote nchini waache tabia ya kukata tamaa baada ya kustaafu bali wajipange vyema na
kuwekeza katika miradi mbalimbali ya kiuchumi ikiwemo viwanda vidogo, kilimo na
biashara.
 
Amesema kuwa kama wastaafu hao watawekeza katika maeneo hayo watatoa ajira kubwa kwa vijana badala ya kutumia mafao yao kwenye matumizi yasiyo ya lazima.
 
“Wazee ni rasilimali na
hazina kubwa kwa taifa kama waswahili wasemavyo panapo wazee hapaharibiki jambo hivyo basi ni matumaini yangu kuwa mfuko wa PSPF mtaendelea kufanya kazi kwa bidii na kwa uadilifu kuhakikisha kuwa hazina hii ya wazee wetu wanapata haki zao kwa mujihu wa sheria za nchi pale wanapohitaji huduma toka kwenu
.”Amesisitiza Makamu wa Rais.
 
Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan ameonya wastaafu hao watarajiwa kupunguza matumizi yasiyo ya lazima bali watumie fedha watakazopata katika shughuli za kiuchumi
kwa ajili ya maslahi yao ya baadaye.
 
Makamu wa Rais pia amepongeza jitihada zinazofanywa na mfuko wa PSPF kwa kutoa mafunzo kwa wastaafu watarajiwa kwa ajili ya kuwasaidia kujipanga vyema pindi watakapostaafu
utumishi wao.
 
Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt Ashatu Kijaji amewahakikishia wastaafu hao watarajiwa kuwa wa mkoa wa Mwanza kuwa Serikali itaendelea kusimamia vyema mifuko ya hifadhi ya jamii ili iweze kutoa mafao bora na kwa
wakati.
 
Dkt Ashatu Kijaji pia amehimiza wastaafu hao watarajiwa kutumia vizuri mafao wanayopata kwa ajili ya maisha yao ya baadaye.
MASAUNI AZINDUA MPANGO WA KUWASAIDIA WAKIMBIZI NA NCHI ZINAZOHIFADHI WAKIMBIZI LEO JIJINI DAR ES SALAAM

MASAUNI AZINDUA MPANGO WA KUWASAIDIA WAKIMBIZI NA NCHI ZINAZOHIFADHI WAKIMBIZI LEO JIJINI DAR ES SALAAM

June 03, 2017
MASA1
Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza na waandishi wa habari baada ya Kuzindua Mpango wa Kuwasaidia Wakimbizi na Nchi zinazohifadhi Wakimbizi (CRRF Tanzania). Uzinduzi huo umefanyika leo katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Kuhudumia Wakimbizi, Harrison Mseke.  Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
MASA2
Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Hassan Simba Yahya akizungumza wakati wa uzinduzi wa  Mpango wa Kuwasaidia Wakimbizi na Nchi zinazohifadhi Wakimbizi (CRRF Tanzania). Uzinduzi huo umefanyika leo katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi  
MASA3
Mbunge wa Jimbo la Muhambwe Kigoma (CCM), Mhandisi  Atashasta Nditiye (kushoto), akifuatiwa na Mbunge wa Jimbo la Kasulu Mjini Daniel Nsanzugwako pamoja na Mkurugenzi wa Idara ya Kuhudumia Wakimbizi, Harrison Mseke, wakifuatilia Mada inayohusu Mpango wa Kuwasaidia Wakimbizi na Nchi zinazohifadhi Wakimbizi iliyokuwa inatolewa na Mratibu wa Mpango huo kutoka Idara ya Huduma za Wakimbizi, Dk. John Jingu (hayupo pichani), muda mfupi kabla ya Uzinduzi wa Mpango huo.
MASA4
Sehemu ya Wawakilishi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa yanayofanya kazi zake nchini  pamoja na Wawakilishi wa Taasisi za Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wakimsikiliza Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (hayupo pichani) wakati wa uzinduzi wa Mpango wa Kuwasaidia Wakimbizi na Nchi zinazohifadhi Wakimbizi (CRRF Tanzania). Uzinduzi huo umefanyika leo katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
MASA5
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Brigedia Jenerali Mstaafu Emanuel Maganga, akijibu maswali ya waandishi wa habari  wakati wa uzinduzi wa  Mpango wa Kuwasaidia Wakimbizi na Nchi zinazohifadhi Wakimbizi (CRRF Tanzania). Uzinduzi huo umefanyika leo katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
MASA6
Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamadi Masauni (katikati), akiwa katika picha ya pamoja na Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala wa Mikoa ya Katavi, Tabora, Kagera na Kigoma, watendaji wa serikali na Baadhi ya Mabalozi na Wawakilishi wa Mashirika ya Kimataifa yanayofanya kazi nchini, wakati wa uzinduzi wa Mpango wa Kuwasaidia Wakimbizi na Nchi zinazohifadhi Wakimbizi (CRRF Tanzania). Uzinduzi huo umefanyika leo katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.

WADAU WA PSPF WAWATANGAZIA FURSA WASTAAFU WATARAJIWA

June 03, 2017
NA K-VIS BLOG/Khalfan Said, Mwanza
MFUKO wa Pensheni wa PSPF umewaleta poamoja watumishi wa umma kutoka wilaya zote za mkoa wa Mwanza zaidi ya 450, ambao wanatarajiwa kustaafu hivi karibuni ili kuwapatia semina ya mafunzo itakayowawezwesha kujiandaa kustaafu kwa amani.
Katika semina hiyo iliyoanza leo Juni 2, 2017 kwenye ukumbi wa chuo cha BoT Capri-point  jijini Mwanza, wadau wa PSPF ambao ni taasisi za fedha nao wametumia fursa hiyo kutangaza fursa mbalimbali ambazo wastaafu hao wanaweza kuzitumia ili kuendeleza maisha yao ya baadaye.
Wadau hao ni pamoja na Mwalimu Commercial Bank, (MCB), NMB, CRDB, TPB na Mfuko wa UTT-AMIS, pia Shirika la Viwanda Vidogovidogo SIDO.
Mkuu wa Kitengo cha Biashara na Masoko, Mwalimu Commercial Bank, (MCB),Bw. Valence Luteganya, akizungumzia huduma mbalimbali zitolewazo na benki hiyo. “Beni hii imeanzishwa hivi karibuni na wamiliki wa benki hii kwa karibu asilimia 30 ni walimu. na huduma tunazozitoa ni pamoja na utoaji mikopo nafuu, ushauri wa kifedha lakini pia katika jiyihada za kurahisisha huduma za kibenki, MCB imo kwenye mtandao wa Umoja Switch ambao umetapakaa nchi nzima.” hayo ni baadhi ya maneno ya Bw. Lutenganya
 Bw. Lutenganya, akifafanua zaidi huduma zitolewazo na benki ya MCB

UMOJA WA WANAWAKE WA MAKANISA YA (E.P.CT) WATEMBELEA KITUO CHA (YDPC) TANGA

June 03, 2017
Tanga, SERIKALI imeshauriwa kuweka kanuni ya majengo ya gorofa na taasisi za huduma za kijamiii kujenga  miundombinu maalumu kwa walemavu lengo ikiwa ni kuzifikia  huduma kama ilivyo kwa wengine.
Wakizungumza katika hafla fupi ya makabidhiano ya vifaa mbalimbali vilivyokabidhiwa kwa uongozi wa Kituo cha Watoto Walemavu (YDPC), na kuishauri  kutoruhusu ujenzi wa majengo ya huduma za kijamii bila kuwepo kwa miundombinu ya walemavu.
Imesemwa kuwa majengo mengi ya huduma za kijamii hayana miundombinu kwa walemavu  hivyo kunyimwa fursa ya kupata huduma kama ilivyo kwa wengine.
Imesemwa  katika kongamano hilo, kuwa  kutokuwepo kwa sheria watu wengi hujenga majengo bila kuweka miundombinu ya walemavu.
Imesemwa kuna baadhi ya walemavu wa viungo  wenye elimu hupoteza nafasi ya kazi kutokana na majengo wanayopangiwa kazi kutokuwa na njia maalumu kwa walemavu wa viungo na kuwa kero kwao.



 Mtaalamu wa tiba sanifu kwa njia ya Mazoezi kwa njia ya Mazoezi na Vitendo, Amina Mbowe, akitoa maelekezo ya kazi wanazozifanya katika kitengo chake ikiwa na pamoja na kuwaonyesha vifaa vya mazoezi kwa watoto wenye ulemavu.


Mwanafunzi mlemavu kituo cha Watoto wenye Ulemavu wa viungo na ngozi, Imamu Amir, akipanda mbegu ya muhongo katika shamba la kituo hicho kijiji cha Mleni Amboni Tanga, ujumbe huo pia ulitembelea katika shamba hilo ambalo watoto walemavu wamekuwa wakiendesha kilimo cha chakula na mbogamboga.
 Mtaalamu wa kilimo kwa watoto walemavu kituo cha Walemavu, Sabra Swai akitoa maelekezo kwa ujumbe wa umoja wa wanawake wa Makanisa ya Free Pentacostal Church of Tanzania wakati walipotembelea shamba la Mleni ambalo watoto walemavu wa viungo, ngozi, viziwi na wengineo huendesha kilimo shamba lililoko kilometa 20 kutoka Tanga mjini.
Mkurugenzi wa kituo cha Watoto Walemavu (YDPC) William Hendry wa pili kulia akiongoza maombi na kutoa shukurani kwa Ujumbe wa Umoja wa Wanawake Makanisa Free Pentacoastal Church of Tanzania wakati alipopokea zawadi mbalimbali kwa kituo hicho

UZINDUZI WA iSwapMyBookS.COM WASAIDIA KUHAMASISHA USOMAJI WA VITABU NCHINI TANZANIA

June 03, 2017

Mkurungezi Mtendaji na Muanzilishi wa IswapMyBooks.Com Shafiq Mpanja akifafanua jambo kwa wageni waalikwa wakati wa uzinduzi wa Mtandao huo unaowezesha wasomaji wa vitabu kubadilishana vitabu mara tu wanapomaliza kuvisoma kwa njia ya mtandao huo.Hafla ya uzinduzi huo zilifanyika mapema jana katika makao makuu ya SOMA BOOK Cafe iliyopo Mikocheni jijini Dar Es Salaam.
Meneja Uendeshaji wa IswapMyBooks.com  Viola Massawe akifafanua taratibu za matumizi ya mtandao huo , wakati wa uzinduzi wa Mtandao huo unaowezesha wasomaji wa vitabu kubadilishana vitabu mara tu wanapomaliza kuvisoma kwa njia ya mtandao huo.Hafla ya uzinduzi huo zilifanyika mapema jana katika makao makuu ya SOMA BOOK Cafe iliyopo Mikocheni jijini Dar Es Salaam.


Mkurungezi Mtendaji wa Soma Book Cafe Demera Kitunga akielezea umuhimu wa kujisomea kwa wageni waalikwa wakati wa uzinduzi  wakati wa uzinduzi wa Mtandao wa IswapMyBooks.com, Mtandao huo unaowezesha wasomaji wa vitabu kubadilishana vitabu mara tu wanapomaliza kuvisoma kwa njia ya mtandao huo.Hafla ya uzinduzi huo zilifanyika mapema jana katika makao makuu ya SOMA BOOK Cafe iliyopo Mikocheni jijini Dar Es Salaam.


Mdau akichangia jambo wakati wa uzinduzi wa IswapMyBooks.com , Mtandao huo unaowezesha wasomaji wa vitabu kubadilishana vitabu mara tu wanapomaliza kuvisoma kwa njia ya mtandao huo.Hafla ya uzinduzi huo zilifanyika mapema jana katika makao makuu ya SOMA BOOK Cafe iliyopo Mikocheni jijini Dar Es Salaam.