BENKI YA CRDB YATANUA MTANDAO WA MATAWI YAKE

March 06, 2018
Muonekano wa jengo jipya la Benki ya CRDB tawi la Mlandizi mkoani Pwani.
Baadhi ya wateja wa benki ya CRDB tawi la Mlandizi wakipata huduma za kifedha katika tawi hilo.
Meneja wa Tawi jipya la Benki ya CRDB la Mlandizi mkoani Pwani, Twahibu Likungwala (kushoto), akitoa maelezo kwa mteja wa benki hiyo aliyefika tawini hapo jana namna anavyoweza kunufaika na akaunti maalum ya Wanawake (Malkia Akaunti).
Ufafanuzi kuhusu huduma za Kifedha katika Tawi la Mlandizi.
 Mteja wa Benki ya CRDB akipata ufafanuzi wa huduma mbalimbali zinazotolewa na benki hiyo kutoka kwa Meneja wa Tawi jipya la Benki ya CRDB la Mlandizi mkoani Pwani, Twahibu Likungwalakwa (kulia).
Ofisa Masoko wa Benki ya CRDB, Cassian Nombo (katikati), akimuhudumia mmoja wa wateja waliofika katika tawi la Benki ya CRDB la Mlandizi mkoani Pwani kupata huduma za kifedha.
Ofisa Masoko wa Benki ya CRDB, Getrud Mwani akimfungulia akaunti mpya mteja wa Benki ya CRDB katika tawi linalotembea la benki hiyo (Mobile Branch), kwa wakazi wa Mlandizi mkoani Pwani.
Huduma zikiendelea.
 Ofisa wa Benki ya CRDB, Husna Seif (kulia), akimwandikisha mkazi wa Mlandizi alipofika katika tawi linalotembea la benki hiyo Mlandizi mkoani Pwani.
 Wateja wa Benki ya CRDB wakiwa wamejitokeza katika gari maalum kufungua akaunti ya benki hiyo.
Ofisa Masoko wa Benki ya CRDB, Vicent Lulenga (kushoto), akimfungulia akaunti mteja  mpya wa benki hiyo katika tawi linalotembea (Mobile Branch), Kibaha mkoani Pwani.  
Ofisa Masoko wa Benki ya CRDB, Rehema Issa (kushoto), akimfungulia akaunti mpya mteja wa benki hiyo Kibaha mkoani Pwani.
Ofisa Masoko wa Benki ya CRDB, Vicent Lulenga (kushoto),  akimuunganisha na huduma ya SimBanking mteja mpya aliyefungua akaunti ya benki hiyo mjini Kibaha. 
Ofisa wa Benki ya CRDB, Omary Kilima akimpa maelekezo mteja wa benki hiyo kabla ya kufungua akaunti. 
 Ofisa Masoko wa Benki ya CRDB, Rehema Issa (kushoto), akimfungulia akaunti mpya mteja wa benki hiyo Kibaha mkoani Pwani.
 Wateja wakipata huduma katika Benki ya CRDB tawi la Kibamba. 
 Meneja wa Benki ya CRDB tawi la Kibamba, Anitha Mafumiko.
Tawi la Benki ya CRDB-Kibamba.

Wafanyakazi Wanawake wa Vodacom Tanzania Foundation, Doris Mollel Foundation waadhimisha Siku ya Wanawake Duniani kwa kutoa msaada hospitali ya Muhimbili

March 06, 2018
Wafanyakazi wanawake wa kampuni ya Vodacom Tanzania PLC na taasisi yake ya kuhudumia masuala ya jamii ya Vodacom Tanzania Foundation, leo wametembelea wodi ya wazazi katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili na kutoa vifaa mbalimbali ,ukiwa ni mwendelezo wake wa kutoa vifaa vya kuokoa zaidi ya watoto 260 wanaozaliwa kabla ya wakati kila mwaka nchini.

Akiongea wakati wa kukabidhi vifaa hivyo na kutembelea wagonjwa, Mkurugenzi wa Vodacom Tanzania Foundation, Rosalynn Mworia alisema “Tunayo furaha kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani mwaka huu kwa kutembelea hospitali ya Taifa ya Muhimbili na kutoa msaada katika wodi ya wazazi vitakavyowezesha kupunguza vifo vya watoto wachanga. Tutaendelea kuunga mkono jitihada za serikali ya Tanzania za kuboresha sekta ya afya hususani kwa wanawake wajawazito na watoto wachanga”.

Vifaa tiba mbalimbali vya kuwasaidia watoto wanaozaliwa kabla ya wakati (Njiti) vilitolewa, baadhi ya vifaa hivyo ni vya kuwasadia watoto kupumua, kuongeza joto, kupima na kuratibu uzito kidijitali, pampasi na khanga, [oxygen concentrators, nebulizer machines, digital weigh scales, surfactants, infusion pumps and continuous positive airway machines, as well as Pampers and khangas].
 Mkurugenzi wa Vodacom Tanzania Foundation, Rosalynn Mworia (wa tatu kushoto) akikabidhi sehemu ya vifaa tiba maalum kwa ajili ya watoto wanaozaliwa kabla ya wakati (Njiti), kwa Dkt. Mariam Kalomo aliyemwakilisha mgeni rasmi naibu waziri, wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Wazee, jinsia na watoto, Dr Faustine Ndugulile. Wa pili kulia ni Muasisi wa Taasisi ya Doris Mollel na Balozi wa Watoto Njiti, Doris Mollel.

Vodacom Tanzania Foundation inaelewa changamoto mbalimbali wanazokutana nazo wanawake nchini, wakati wa ujauzito na wakati wa kujifungua ndio maana imeamua kulivalia njuga changamoto zao na kuhakikisha vifo vya wanawake na watoto vinavyosababishwa na matatizo ya uzazi vinapungua.

“Kusaidia kuboresha afya za wanawake na watoto na lishe bora ni moja ya malengo ya taasisi yetu ya Vodacom Tanzania Foundation. Tunaamini msaada mkubwa unatakiwa kunusuru maisha ya wanawake na watoto kutokana na changamoto mbalimbali zinazowazunguka, tunaamini msaada huu utafanikisha kuleta matokeo chanya ya kuboresha na kuokoa maisha ya watoto wachanga,”alisema Mworia.
Msaada huu ni mwendelezo wa taasisi ya Vodacom Tanzania Foundation, kutoa vifaa vya kisasa vinavyowezesha kuokoa maisha ya watoto wanaozaliwa kabla ya wakati (Njiti) sambamba na miradi mingine inayolenga kuboresha afya ya uzazi na kupunguza vifo vya watoto wachanga nchini, inayotekeleza kwa kushirikiana na wadau mbalimbali.

Baadhi ya miradi hiyo ni kuwasafirisha wanawake wenye ugonjwa wa Fistula hadi hospitali na kugharamia matibabu yao, kutoa jumbe za afya ya uzazi kwa wanawake wajawazito bure kupitia simu zao za mkononi za mtandao wa Vodacom sambamba na kuwawezesha wanawake wajawazito kuwahishwa katika vituo vya afya vyenye wataalamu wakati wanapokaribia kujifungua, kwa ajili ya kuokoa maisha yao na watoto wanaozaliwa.
 Akizungumza katika hafla hiyo, Dr Mariam Kalomo aliyemwakilisha mgeni rasmi naibu waziri, wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Wazee, jinsia na watoto, Dr Faustine Ndugulile aliwapongeza Vodacm Tanzania Foundation kwa msaada huo waliojitolea huku akiwaomba wadau wengine kujitokeza pia.

“Nawashukuruni sana kwa msaada huu, maana tuna uhakika utapunguza vifo vya watoto wachanga kwa kiasi kikubwa, hiki mlichojitolea ni kikubwa mno kwa vile hospitali nyingi zinakabiliwa na upungufu wa vifaa tiba, kwa hiyo tunapopokea vifaa hivi tunakuwa na uhakika wa kuokoa maisha ya watoto wengi Zaidi,” alisema Dr Kalomo.

Kwa upande wake, Sister Zuhura Mahona aliyemuwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa hospitali ya Taifa ya Muhimbili aliwahahakishia wafanyakazi wa Vodacom Tanzania Foundation kwamba vifa walivyojitolea vitatumika kwa usahihi kama vilivyoombwa.

Naye mkurugenzi wa Taasisi ya Doris Mollel , Doris Mollel aliwashukuru wafanyakazi wa Vodacom Tanzania Foundation kwa kujali watoto waliozaliwa kabla ya wakati na kuwaokoa kwa kuwaletea vifaa tiba hivyo.

 “Vifaa hivi ni muhimu sana kwa ajili ya watoto, kwa mfano ukimpatia mtoto hewa ya oxygen unakuwa umeokoa maisha yake ambayo labda angeyapoteza kwa kukosa hewa hiyo muhimu,” alisema Mollel.

Siku ya Wanawake Duniani huadhimishwa Machi 8 kila mwaka, ambapo hutumika kufikisha ujumbe wa kupambana na changamoto mbalimbali zinazokwamisha kupata haki zao na usawa na kutoa wito wa kuhakikisha maisha ya wanawake yanaboreshwa katika Nyanja mbalimbali ikiwemo elimu, lishe bora, afya ya uzazi, na maisha bora kwa ujumla.

Vodacom Tanzania Foundation inaendelea kusaidia Wanawake na Wasichana nchini pote kuboresha maisha yao katika Nyanja za afya, elimu bora na kuwawezesha kujikomboa kiuchumi kupitia ujasiriamali. Kwa kushirikiana na mashirika yasiyo ya kiserikali ya hapa nchini na wadau wengine, taasisi imesaidia zaidi ya miradi 120 mpaka sasa ikiwa imewekeza zaidi ya shilingi Bilioni 15 kwa ajili ya kuboresha maisha ya watanzania.


MDAHALO WAKUWANIA UONGOZI WA URAIS JUMUIYA YA WATANZANIA DMV (PART 2)

March 06, 2018
Wakurugenzi: Mdahalo wa sehemu ya pili wa kugombania kinyang'anyiro cha wa Wakurugenzi kupitia Jumuiya ya Watanzania waishio DMV, ulioandaliwa na Tume ya Uchaguzi, Siku ya Jumamosi March 3, 2018 katika ukumbi wa Indiana Springs Terrance Local Park Sliver Spring Maryland Nchini Marekani.

NAIBU WAZIRI MAVUNDE AIAGIZA WCF KUWAFIKISHA MAHAKAMANI WAAJIRI 6,907 AMBAO WAMESHINDWA KUJISAJILI NA MFUKO WA FIDIA KWA WAFANYAKAZI

March 06, 2018
  NA K-VIS BLOG/KHALFAN SAID

SERIKALI imesema haitabadili msimamo wake wa kuwapeleka mahakamani waajiri wote ambao bado hawajajisajili na Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi, (WCF), Naibu  Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, anayeshughulikia Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Antony Mavunde amewaambia waandishi wa habari leo Machi 6, 2018 jijini Dar es Salaam.

Naibu Waziri ametoa tamko hilo wakati wa ziara yake ya kushtukiza aliyoifanya wilayani Temeke jijini Dar es Salaam, kuwabaini waajiri ambao bado hawajatekelkeza takwa hilo la Kisheria ikiwa ni pamoja na wale ambao hawateketekelezi inavyopasa Sheria ya ajira na mahusiano kazini.

Akiwa kwenye kiwanda cha kugandisha barafu cha Boghal kilichoko Chamazi, Naibu Waziri pia aliahgiza kukamatwa mara moja wafanyakazi watatu raia wa kigeni ambao walikutwa hawana vibali vya kufanyia kazi.

“Dar es Salaam kuna jumla ya waajiri 14,484, na kati ya hao, 6,907, tumebaini bado hawajajisajili na nimewaagiza maafisa wa WCF kuwafikisha mahakamani mara moja kuanzia kesho mashtaka dhidi yao yaandaliwe, (leo).” Aliagiza Naibu Waziri Mavudne ambaye alifuatana na Kamaishna wa Kazi Bi. Hilda Kabisa, na Kaimu Mkurugenzi wa Uendeshaji Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi, (WCF), Bi. Rehema Kabongo.

Aidha Naibu Waziri Mavunde, aliagiza wafanyakazi watatu wa kiwanda cha kugandisha barafu cha Bhogal, kilichoko Chamazi nje kidogo ya jiji kukamatwa na polisi na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria kwa kutokuwa na vibali vya kufanya kazi nchini.

“Nitoe wito kwa waajiri nchini, kwa mujibu wa kifungu cha 9 cha uratibu ajira za wageni, kinaelekeza kuwa hataruhusiwa mgeni yoyote kufanya kazi nchini bila ya kuwa na kibali, na hawa tumewauliza vibali vyao hawakuwa navyo kwa hivyo nimeagiza wakamatwe na wapelekwe polisi na kasha wafikishe mahakamani.” Alisema Mhe. Naibu Waziri Mavunde.

Ziara ya naibu waziri ni muendelezo wa operesheni inayoendelea nchini kote kuwabaini waajiri ambao hawajajisajili na Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi, ikiwa ni pamoja na kuwabaini wale ambao hawatekelezi Sheria ya ajira na mahusiano kazini.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Uendeshaji WCF, Bi. Rehema Kabongo, alisema Mfuko umeanza kutekeleza maagizo ya serikali kwa kuwafikisha mahakamani wale wote ambao bado hawajajisajili na Mfuko ambao wanakabiliwa na adhabu ya kulipa faini isiyopungua shuklingi Milioni 50, (Milioni Hamsini) au kifungo cha miaka mitano jela au vyote kwa pamoja.

“Nitoe wito kwa wafanyakazi, operesheni hii ndio imeanza na kama bado kuna mwajiri ambaye bado hajatekeleza wajibu wake asisubiri kufikishwa mahakamani.” Alisema.
 Naibu  Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, anayeshughulikia Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Antony Mavunde(katikati), akizu nguzma jambo wakati alipofanya ziara ya kushtukiza kubaini waajiri ambao bado hawajajisajili na Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi, (WCF), jijini Dar es Salaam Machi 6, 2018. Wakwanza kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Mfuko huo, Bi. Rehema Kabongo.
 Mhe. Mavunde, na Bi. Rehema wakipitia nyaraka
 Raia wa kigeni waliojuwa wafanyakazi wa kiwanda cha kugandisha barafu, wakiwa kwenye gari kupelekwa kituo cha polisi kwa kosa la kufanya kazi nchini bila kibali.
  Raia wa kigeni waliojuwa wafanyakazi wa kiwanda cha kugandisha barafu, wakiwa kwenye gari kupelekwa kituo cha polisi kwa kosa la kufanya kazi nchini bila kibali.
 Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi, Bi. Laura Kunenge, (kushoto), akizungumza jambo na Kamishna wa Kazi kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Vijana na Ajira, Bi.Hilda Kabisama.
 Afisa Mwajiri kiwanda cha Carmel Concrete cha Mbagala Kizuiani akijieleza kwa Naibu Waziri Mavunde baada ya kubainika kiwanda hicho kinakiuka Sheria ya Kazi na Mahusiano Kazini. kwa kutowalinda wafanyakazi kwa kuwapatia vifaa vya kujihami.Kiwanda hicho kimetozwa faini ya zaidi ya shilingi Milioni 10 kwa kosa hilo na mengineyo.
 Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughhulikia Kazi, Ajira na Vijana, Antony Mavunde, (mwenye suti), akizunhumza jambo wakati alifanya ziara ya kushtukiza kwenye kiwanda cha Carmel Concrete cha Mbagala Kizuiani jijini Dar es Salaam jana (Machi 6, 2018), ili kubaini waajiri ambao bado hawajajisajili na Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi, (WCF), na ambao hawatekelezi Sheria ya ajira na mahusiano kazini. Jumla ya waajiri 6,907 jijini Dar es Salaam, hawajajisajili na Mfuko na watapelekwa mahakamani. 
Mfanyakazi wa kiwanda cha Carmel akilalamika mbele ya Naibu Waziri Mavunde, kuhusu mazingira mabovu ya kufanyia kazi na mishahara midogo kinyume na maelekezo ya serikali


 Naibu Waziri akiumuuliza mfanyakazi huyo wa kiwanda cha kugandisha barafu, ambacho pia kimebainika kufanya shughuli za kuchomelea vyuma, baada ya kumkuta hana viatu vigumu (gumboots)
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughhulikia Kazi, Ajira na Vijana, Antony Mavunde, akizunguzma mbele ya Meneja wa kiwanda cha Carmel Concrete, Nabil Kassim, (kushoto),  kuhusu kutowalinda wafanyakazi wake.
Naibu Waziri akiongozana na Kamishana wa Kazi, Bi.Hilda Kabisa na maafisa wengine wakati wakiwasili kiwanda cha kugandisha barafu cha Bhogal, huko Mbagala Chamazi nje kidogo ya jiji.
Khalfan Said Chief Photographer/Owner K-VIS MEDIA P.Box 77807 Mobile; +255 646-453/+255-653-813-033 Office; Mivinjeni Opp.Tanesco, Kilwa RD Blog:http//khalfansaid.blogspot.com Dar es Salaam, Tanzania

DC MATIRO AFUNGUA KIKAO CHA UELIMISHAJI KUHUSU MPANGO WA ANWANI ZA MAKAZI NA POSTIKODI SHINYANGA

March 06, 2018
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro amefungua kikao  cha uelimishaji kuhusu Mpango wa Anwani za Makazi na Postikodi  kwa ajili ya kuwajengea uelewa na uwezo viongozi na watendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga ili waweze kutekeleza mpango huo ipasavyo kwa kushirikisha wadau mbalimbali.