DC ALI HAPI AZIPONGEZA DAWASA NA DAWASCO KWA USIMAMIZI MZURI UTEKELEZAJI WA UJENZI WA MIRADI YA UBORESHAJI MAJI

January 13, 2018

 Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam, Mhe., Ali Hapi, (katikati), akiteremka kutoka juu ya tenki kubwa la kuhifadhia maji linalojengwa huko Mabwepande nje kidogo ya jiji, wakati wa ziara yake ya kukagua maendeleo ya utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa miundombinu ya maji wilayani kwake Januari 13, 2018.
  NA K-VIS BLOG/Khalfan Said

MKUU wa wilaya ya Kinondoni Mhe. Ali Hapi, amewataka wakandarasi wanaotekeleza ujenzi wa mradi wa uboreshaji wa huduma za ugawaji na usambazaji maji wilayani kwake kuongeza kasi ya kukamilisha mradi huo kama ambavyo mkataba unaelekeza.

Mhe. Hapi aliyasema hayo leo Januari 13, 2018 mwishoni mwa ziara yake ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa miundomnbinu hiyo inayohusisha matenki makubwa manne na vituo vinne vya kusukuma maji (Booster Stations) ikiwa ni pamoja na utandikaji  wa mabomba ya kusafirisha maji.

Mradi huo ambao unatekelezwa na Wizara ya Maji na Umwagiliaji kupitia Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka jijini Dar es Salaam, (DAWASA), ni sehemu ya mradi mkubwa wa uboreshaji wa huduma za ugawaji na usambazaji maji katika baadhi ya maeneo ya Mikoa ya Pwani,  Dar es Salaam, sehemu ya mikoa ya Morogoro na Tanga na ulianza kutekelezwa mwezi Machi 2016.

“Mradi huu ulipaswa kuwa umekamilika Novemba mwaka jana, lakini hatua waliyofikia baadhi ya maeneo wako asilimia 80, mengine asilimia 75 na mengine asilimia 50, ahadi yao ni kwamba ndani ya kipindi kifupi kijacho wataweza kukamilisha mradi huu.” Alisema

Hata hivyo Mheshimiwa Hapi amepongeza usimamizi na ufuatiliaji wa karibu unaofanywa na mamlaka husika zinzosim amia mradi huo. “Niwapongeze DAWASA na DAWASCO kwa kazi nzuri ya kuhakikisha wanasimamia na kufuatilia utekelezaji wa mradi huu.” Alisema Mhe. Hapi.

Alitaja maeneo yatakayofaidika na mradi huu kuwa ni pamoja na wakazi wa Makongo, Changanyikeni, Salasala, Bunju, Mabwepande na Wazo.

“Mradi ukikamilika utaondoa kero ya maji katika wilaya yetu  kwa asilimia 95, kwa hivyo, hii nifaraja kubwa kwa wananchi wa Kinondonbi hususan katika maeneo nilkiyoyataja.” Alifafanua.

 Mhe. Hapi, akimsikiliza Mkandarasi,   Mhandisi P.G. Rajani wa kampuni ya WAPCOS limited ya India, alipotembelea sehemu ya ujenzi wa mtambo wa kusukuma maji huko Salasala jijini Dar es Salaam.

 Mhe. Hapi, akimsikiliza Mkandarasi,   Mhandisi P.G. Rajani(kulia) wa kampuni ya WAPCOS limited ya India, alipotembelea sehemu ya ujenzi wa tenki kubwa la kuhifadhia maji huko Salasala jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Modester Mushi kaimu mkurugenzi wa ufundi DAWASA.
 Mhe. Hapi na msafara wake wakipanda juu ya tanki linalojengwa.
 Mafundi wakiwa kazini huko Salasala.
 Mhe. Hapi akipokelewa na Meneja Uhusiano wa Jamii, DAWASA, Bi. NMelly Msuya, wakati akiwasili huko Makongo Juu, kuanza ziara ya kukagua miradi hiyo.
 Meneja Uhusiano wa Jamii, Bi. Nelly Msuya, (wapilia kushoto) na Afisa Uhusiano wa Jamii wa DAWASA, Bi. Mecky Mdakju, wakimsubiri Mkuu wa wilaya Mhe. Hapi, alipozuru eneo la Makongo Juu kukagua ujenzi wa kituo cha kusukuma maji.
 Mhe. Hapi, (kulia), akifurahia jambo na afisa kutoka DAWASCO, Bi.Judith Singinika(katikati), baada ya kutembelea eneo la ujenzi Bunju.
 Tenki kubwa likifunikwa huko Salasala.
 Mhe. Hapi, (kushoto), akiwa na Bi.Modester Mushi kaimu mkurugenzi wa ufundi DAWASA, (kulia) na Bi. Nelly Msuya, Meneja Uhusiano wa Jamii, DAWASA, walipotembelea ujenzi wa kituo cha kusukuma maji Bunju.
 Mkuu wa wilaya akizungumza na vibarua.

 Mkuu wa Wilaya Mhe. Hapi, akizungumza na waandishi wa habari mwishoni mwa ziara hiyo, huko Mabwepande.
Bi.Mecky Mdaku, Afisa Uhusiano wa Jamii, DAWASA, akipanda juu ya tenki la Makongo Juu lililofikia asilimia 80 kukamilika
-- Khalfan Said Photojournalist K-VIS MEDIA P.o.box 77807 Dar es Salaam, Tanzania Mobile: +255-784-646-453/+255-653-813-033 Blog: khalfansaid.blogspot.com

MAMBO UNAYOTAKIWA KUYAFAHAMU KUHUSU MAPINDUZI YA ZANZIBAR

January 13, 2018

Na Jumia Travel Tanzania



Januari 12 ya mwaka huu wa 2018 Wazanzibari pamoja na Watanzania kwa ujumla watakuwa wakiadhimisha miaka 54 tangu kutokea kwa mapinduzi Visiwani Zanzibar mnamo Januari 12, 1964. Mapinduzi ambayo yaliyofanywa na wanamapinduzi wa kiafrika na kupelekea kuung’oa utawala wa kisultani na kiarabu visiwani humo na kuwa na utawala wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

 

Pamoja na siku hii kuadhimishwa kila mwaka, bado kuna watu wengi hawafahamu mambo muhimu kuhusu historia ya Zanzibar na yaliyopelekea mpaka mapinduzi kutokea. Kutokana na umuhimu wa siku hii kwa vizazi vilivyopita, vya sasa na vijavyo, Jumia Travel imekukusanyia mambo muhimu ambayo huna budi kuyafahamu.



Ikiwa na historia ndefu ya utawala wa Kiarabu tangu mwaka 1698, Zanzibar ilikuwa ni sehemu ya nchi ya ng’ambo ya Oman mpaka ilipojitwalia uhuru wake mnamo mwaka 1858 na kuwa chini ya utawala wake wenyewe wa Kisultani.

 

Wakati wa utawala wa Sultani Ali Ibn Said mnamo mwaka 1890, Zanzibar ilikuwa chini ya utawala wa Waingereza mpaka mwaka 1963 ilipowapatia wanzibar uhuru wao, ingawa haikuwahi kuwa chini ya utawala rasmi wa moja kwa moja wa dola ya Kiingereza.



Wananchi wa Zanzibar kwa kiasi kikubwa walikuwa ni mchanganyiko kutoka mataifa mbalimbali kama vile Waarabu, Wahindi, Waajemi, Washirazi na Waafrika, ambapo waarabu na wahindi ndio kwa kiasi kikubwa walikuwa wamehodhi ardhi na shughuli kuu na njia za biashara. Kadri muda ulivyozidi kwenda maingiliano baina ya watu wa mataifa hayo yalizidi kuongezeka kitu kilichopelekea utofauti baina yao kuanza kufifia.


Hata hivyo, walowezi wa Kiarabu kama wamiliki wa sehemu kubwa ya ardhi ya visiwani humo ndio walikuwa ni matajiri kuliko waafrika. Suala hilo pamoja na mambo mengine mengi ni miongoni mwa sababu zilizopelekea waafrika kuona sababu ya kufanya mapinduzi ili kuwa na utawala wa haki na usawa visiwani humo.



Kwa upande wa kisiasa, vyama vikuu visiwani Zanzibar vilikuwa vikiendeshwa na kuungwa mkono kulingana na utaifa (ukabila), kama vile Waarabu walikuwa wakitawala kwa sehemu kubwa ya chama cha Zanzibar Nationalist Party (ZNP) huku Waafrika ilikuwa ni Afro-Shirazi Party (ASP).

 

Baada ya Zanzibar kutwaliwa na utawala wa Kisultani wa Oman mnamo mwaka 1698, sehemu ya ardhi yote visiwani humo iligawiwa kwa wanafamilia wa Kifalme wa Oman, ambapo vizazi vyao viliendelea kuimiliki mpaka mwaka 1964.



Ingawa sio Waarabu wote walikuwa ni matajiri kama familia ambazo zilikuwa zikimiliki mashamba ya karafuu na minazi, hasira ambayo waliyokuwa nayo waafrika ambao walikuwa wakifanya kazi kwenye mashamba hayo ilipelekea kujisikia hali ya kubaguliwa kwenye ardhi yao wenyewe. Hususani kwa kisiwa kidogo kama cha Zanzibar ambapo ilikuwa ni rahisi kuona pengo na utofauti mkubwa kati ya familia tajiri za kiarabu zilizokuwa zinamiliki ardhi na vijakazi wao masikini wa kiafrika.

 

Harakati za kutaka uhuru Visiwani Zanzibar zilianza kutokana na vuguvugu za shughuli za kisiasa ambapo kwa kiasi kikubwa waafrika hawakuwa wanapata uwakilishi sawa na nafasi bungeni. Kuanzia mwaka 1961 na kuendelea kulianza kufanyika kwa chaguzi za kisiasa za kidemokrasia ambapo vyama vikuu vya ASP na ZNP vilikuwa vikichuana vikali.



Chama kilichokuwa kikiungwa mkono na waafrika wengi cha ASP kilikuwa kikiendelea kuungwa mkono na kukubalika miongoni mwa waafrika wengi. Katika maeneo mengi kulipokuwa kunafanyika chaguzi kilionekana kuungwa mkono ingawa matokeo ya uchaguzi yalipotoka yalikuwa yanaonyesha kushinda sehemu chache.



Sababu hiyo ambayo ilikuwa ikijirudia mara kwa mara kwenye kila chaguzi ndiyo iliyopelekea waafrika kuona haja ya kufanya mapinduzi. Mnamo Januari 12, 9164 mapinduzi yalifanyika visiwani Zanzibar na kumfanya kiongozi wa chama cha ASP, Hayati Sheikh Abeid Amani Karume kuwa Rais mpya na kiongozi wa nchi.



Mapinduzi hayo yalipelekea ukomo wa utawala wa kiarabu visiwani Zanzibar wa takribani miaka 200, hivyo kuifanya siku hiyo kusherehekewa kwa maadhimisho maalum na kuwa ni siku ya mapumziko ya kitaifa.  
MWENYEKITI WA CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM) RAIS MHE. DKT. MAGUFULI AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA KATIBU WA ITIKADI NA UENEZI WA (CCM) HUMPHREY POLEPOLE IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

MWENYEKITI WA CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM) RAIS MHE. DKT. MAGUFULI AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA KATIBU WA ITIKADI NA UENEZI WA (CCM) HUMPHREY POLEPOLE IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

January 13, 2018
1
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Rais Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa (CCM) Humphrey Polepole kabla ya kuanza mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam.
2
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Rais Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa (CCM) Humphrey Polepole Ikulu jijini Dar es Salaam.
3
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Rais Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Rais Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli mara baada ya mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam.
4
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa (CCM) Humphrey Polepole akizungumza mara bada ya kikao chake na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Rais Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU
5

WAZIRI UMMY AIKABIDHI TIMU YA COASTAL UNION MILIONI 2 BAADA YA KUIFUNGA KURUGENZI WA MUFINDI MABAO 3-0 LEO

January 13, 2018
 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto wa pili kutoka kulia Ummy Mwalimu  akimkabidhi kitita cha sh.milioni mbili nahodha wa timu ya Coastal Hussein Sharifu maarufu Casilasi mara baada ya timu hiyo kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 katika mchezo wa ligi daraja la kwanza uliochezwa kwenye uwanja wa CCM Mkwakwani mjini Tanga leo kulia ni Mwandishi wa TBC Tanga Bertha Mwambela akishuhudia
 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto wa pili kutoka kulia Ummy Mwalimu akimkabidhi kitita cha sh.milioni mbili nahodha wa timu ya Coastal Hussein Sharifu maarufu Casilasi mara baada ya timu hiyo kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 katika mchezo wa ligi daraja la kwanza uliochezwa kwenye uwanja wa CCM Mkwakwani mjini Tanga leo
 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto wa pili kutoka kulia Ummy Mwalimu akicheza ngoma ya kiisifu Coastal Union wakati alipokuwa akihamasisha ushindi wa timu hiyo kwenye uwanja wa CCM Mkwakwani leo ambapo Coastal Union iliibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Kurugenzi wa Mufundi
 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto wa pili kutoka kulia Ummy Mwalimu akicheza ngoma ya kiisifu Coastal Union wakati alipokuwa akihamasisha ushindi wa timu hiyo kwenye uwanja wa CCM Mkwakwani leo ambapo Coastal Union iliibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Kurugenzi wa Mufundi
 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto wa pili kutoka kulia Ummy Mwalimu akicheza ngoma ya kiisifu Coastal Union wakati alipokuwa akihamasisha ushindi wa timu hiyo kwenye uwanja wa CCM Mkwakwani leo ambapo Coastal Union iliibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Kurugenzi wa Mufundi

MATUKIO YA MECHI BAINA YA COASTAL UNION NA KURUGENZI FC YA MUFINDI DAKIKA 45 ZA KIPINDI CHA KWANZA COASTAL UNION IKITOKA KIFUA MBELE MABAO 3-0

January 13, 2018
Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia Wazee na Watoto,Ummy Mwalimu ambaye alikuwa mgeni rasmi katika mchezo baina ya Coastal Union na Kurugenzi ya Mufundi akifuatilia mchezo huo katikati akiwa na Jezi ya Coastal Union kushoto ni Mwenyekiti wa timu ya Coastal Union Steven Mguto na Kulia ni Katibu wa Chama cha Soka Mkoa wa Tanga(TRFA) Beatrice Mgaya
 Sehemu ya mashabiki wa soka mkoa wa Tanga wakiojitokeza kufuatilia mchezo huo
 Wachezaji wa timu ya Coastal Union wakishangilia moja ya bao nne ambazo walifunga wakati wa kipindi cha dakika 45 za kwanza kabla ya kuanza kipindi cha pili ambapo Coastal Union ilikuwa ikiongoza kwa mabao 3-0
 Mchezaji wa timu ya Coastal Union Raizani Hafidhi kushoto akijaribu kumtoka wa timu ya Kurugenzi FC ya Mufindi Nickraus Mwansumbule wakati wa mchezo wa Ligi Daraja la kwanza uliochezwa leo kwenye uwanja wa CCM Mkwakwani mjini Tanga ambapo mpaka dakika 45 Coastal Union walikuwa wakiongoza kwa mabao 3-0

NAIBU WAZIRI WA MAJI AWAHAKIKISHIA HUDUMA YA MAJI YA UHAKIKA WAKAZI WA KISHAPU

NAIBU WAZIRI WA MAJI AWAHAKIKISHIA HUDUMA YA MAJI YA UHAKIKA WAKAZI WA KISHAPU

January 13, 2018

1
Mkuu wa Wilaya ya Kishapu, Nyabaganga Taraba akimtambulisha Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Aweso (katikati) kwa wananchi (hawamo pichani), alipofika wilayani hapo kukagua maendeleo ya huduma ya maji.
2
Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Aweso akiwa amebeba ndoo ya maji na akina mama wa Kijiji cha Bubiki ikiwa ni ishara ya nia ya Serikali kumuondolea mwanamke adha ya kero ya maji wilayani Kishapu, mkoani Shinyanga alipokuwa akikagua maendeleo ya huduma ya maji.
3
Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Aweso akiwahutubia wakazi wa Kijiji cha Bubiki, wilayani Kishapu, mkoani Shinyanga, alipokuwa akikagua maendeleo ya huduma ya maji.
………………
Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Aweso ameendelea na ziara yake mkoani Shinyanga kwa kukagua utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi kwa upande wa Sekta ya Maji katika Wilaya ya Kishapu.  
Akihutubia katika mkutano wake kwa wakazi wa Kishapu, Aweso amewahakikishia wananchi hao kuwa Serikali yao itafanya kazi usiku na mchana katika kuhakikisha inamaliza kero ya maji na hakuna kijiji hata kimoja ambacho kitapitwa na huduma ya majisafi.
Naibu Waziri Aweso ametoa rai kwa wananchi wote kutoa ushirikiano wa dhati kwa Serikali na viongozi wa ngazi zote, pamoja na kuunga mkono juhudi inazozifanya kwa lengo la kutimiza upatikanaji wa maji ya uhakika, salama na ya kutosheleza kwa maendeleo ya Tanzania.
Kwa upande wao wananchi waliohudhuria mkutano huo wamemshukuru Naibu Waziri wa Maji kwa kazi kubwa anayoifanya na jinsi anavyojitoa kwa lengo la kuhakikisha kila mwananchi anafikiwa na huduma ya maji. Pia, wamemtaka afikishe salamu zao za pongezi kwa Rais Magufuli kwa nia yake thabiti ya kuliletea taifa maendeleo.

MKUU WA MKOA WA KILIMANJARO AKABIDHI JESHI LA POLISI MKOA WA KILIMANJARO MSAADA WA VIFAA VYA MAWASILIANO YA KOMPYUTA

January 13, 2018
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro,Kamishna Mwandamizi Msaidizi wa Polisi ,Hamis Issa akiumuongoza Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Anna Mghwira alipowasili katika uwanja wa mazoezi wa kikosi cha Kutuliza Ghasia kwa ajili ya shughuli ya kukabidhi msaada wa vifaa vya mawasiliano ya Kompyuta kwa jeshi hilo.
Gwaride la Heshima lililoandaliwa kwa ajili ya Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro alipowasili katika viwanja hivyo kutoa msaada wa vifaa vya Mawasiliano ya Kompyuta.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaroo,Anna Mghwira akipokea Salamu ya Heshima mara baada ya kuwasili katika viwanja hivyo.
Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro,Anna Mghwira akiongozwa na Mkuu wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia mkoa wa Kilimanjaro,Edson Mwalutende kukagua Gwaride lililoandaliwa kwa ajili yake.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Anna Mghwira akikagua Gwaride maalum lililoandaliwa kwa ajili yake wakati wa kukabidhi msaada wa vifaa vya Mawasiliano ya Kompyuta.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro,Hamis Issah akimuongoza Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro ,Anna Mghwira mara baada ya kuhitimisha zoezi la ukaguzi .kulia ni Afisa Mnadhimu wa jeshi la Polisi daraja la kwanza ,Kamishna Mwandamizi Msaidizi ,Koka Moita.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro akisalimiana na Maofisa wa Jeshi la Polisi wa ngazi mbalimbali za vyeo kabla ya kukabidhi msaada wa vifaa vya Mawasiliano ya Kompyuta.
Afisa Mnadhimu wa jeshi la Polisi daraja la kwanza ,Kamishna Mwandamizi Msaidizi ,Koka Moita akizungumza wakati wa ukaribisho wa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro katika uwanja 
Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro,Kamishna Mwandamizi Msaidizi wa Polisi,Hamis Issah akitoa neno la shukrani la utangulizi kwa msaada wa vifaa vya Mawasiliano ya Kompyuta ambazo zitagawiwa katika vituo vya Polisi vya wilaya za mkoa wa Kilimanjaro.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Anna Mghwira akizungumza kabla ya kukabidhi msaada huo.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Anna Mghwira akimkabidhi Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro,Hamis Issah vifaa vya Mawasiliano ya Kompyuta kwa ajili ya ofisi za jeshi hilo mkoa wa Kilimanjaro.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro,Hamis Issah akikabidhi vifaa hivyo kwa Wakuu wa Polisi wa wilaya mara baada ya kukabidhiwa na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro ,Anna Mghwira.
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii,Kanda ya Kaskazini.