JUWARIA DECORATION YAANZA MAANDALIZI YA SIKU YA WAPENDANAO(VALENTINEDAY),SASA WAPO TAYARI KUKUHUDUMIA

February 12, 2015
MKURUGENZI MTENDAJI WA JUWARIA DECORATION,JUWAIRIA MIKIDADI ABDALLAH AKIFANYA MAANDALIZI KWA AJILI YA WATEJA SIKU YA VALENTINE DAY KESHO KUTWA,JUWARIA WANAPATIKANA KARUME ROAD BARABARA YA KWENDA TANGA BEACH RESORT.
MKURUGENZI MTENDAJI WA JUWARIA DECORATION,JUWAIRIA MIKIDADI ABDALLAH AKIFANYA MAANDALIZI KWA AJILI YA WATEJA SIKU YA VALENTINE DAY KESHO KUTWA,JUWARIA WANAPATIKANA KARUME ROAD BARABARA YA KWENDA TANGA BEACH RESORT.
BAADHI YA MAUA YANAYOPATIKANA JUWARIA DECORATION KWA AJILI YA WAPENDANAO
MKURUGENZI MTENDAJI WA JUWARIA DECORATION,JUWAIRIA MIKIDADI ABDALLAH AKIWA AMESHIKILIA UA AMBALO LINAPATIKANA KWENYE OFISI YAKE MAALUM KWA AJILI YA WAPENDANAO IKIWA NI SEHEMU YA  MAANDALIZI KWA AJILI YA WATEJA SIKU YA VALENTINE DAY KESHO KUTWA,JUWARIA WANAPATIKANA KARUME ROAD BARABARA YA KWENDA TANGA BEACH RESORT.
MKURUGENZI MTENDAJI WA JUWARIA DECORATION,JUWAIRI MIKIDAD ABDALLAH AKIFUATILIA MAANDALIZI KWA WASAIDIZI WAKE LEO

JUWARIA DECORATION WAPO KWA AJILI YAKO KATIKA SIKU YA WAPENDANAO VALENTINE DAY NA SIKU ZOTE LENGO LIKIWA KUHAKIKISHA UNAPATA KILICHOKUWA NA UHAKIKA ZAIDI.

WANAPATIKANA PEMBEZONI MWA BARABARA YA KARUME INAYOELEKEA HOTEL YA TANGA BEACH RESORT KWA MAWASILIANO WAPIGIA SIMU NO:0715959448,0787959448

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NJE MGENI RASMI MAADHIMISHO YA TAIFA LA IRAN

February 12, 2015


 Balozi wa Iran nchini Tanzania,Mh.Mehdi Aghajafari akimpokea Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mh.Dkt.Mahadhi Juma Maalim (Mb) alipowasili katika hafla ya kusherehekea siku ya Taifa la Iran iliyofanyika kwenye makazi ya Balozi huyo Jijini Dar es Salaam jana usiku.
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mh.Dkt.Mahadhi Juma Maalim (Mb) akizungumza mbele ya wageni mbalimbali walioalikwa katika hafla ya siku ya Taifa la Iran iliyofanyika kwenye makazi ya balozi wa Iran Jijini Dar es Salaam.
 Balozi wa Syria nchini, Mhe.Abdulmonem Annan (kushoto) Jaji mkuu wa Tanzania,  Mhe. Mohamed Chande Othman (katikati) na Balozi wa Yemen nchini, Mhe.Abdulla Hassan Alamri wakimsikiliza kwa makini Mgeni Rasmi kwenye hafla ya Siku ya Iran, Naibu waziri Dkt. Mahadhi.
 Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Hassan Simba Yahaya (kulia) akiwa na Maafisa kutoka Wizara hiyo Bw. Mkumbwa Ally (kushoto) na Bw. Leonce Bilauri (katikati) wakifuatilia hotuba ya Naibu Waziri (hayupo pichani) katika hafla hiyo.
 Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe.Dkt.Mahadhi Juma Maalim (Mb.) akisalimiana na Balozi wa Syria nchini Mhe. Abdulmonem Annan kwenye sherehe hizo.
 Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe.Mohamed Chande Othman akizungumza jambo na  Mhe.Dkt.Mahadhi kwenye hafla ya siku ya Iran.
Picha na Reuben Mchome

TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI YAKUTANA NA VIONGOZI WA SIASA LEO

February 12, 2015

 Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC),Jaji Damian Lubuva akizungumza wakati wa mkutano na Viongozi wa Vyama vya Siasa uliofanyika leo kwenye Ukumbi wa JB Belmonte,Jijini Dar es salaam.Wengine pichani ni Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi,Julius Malaba na kulia ni Kamishina wa Tume yaTaifa ya Uchaguzi,Prof. Amon Challigha
Sehemu ya Viongozi wa Vyama vya Siasa waliohudhulia Mkutano huo wakimsikiliza kwa makini Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC),Jaji Damian Lubuva (hayupo pichani) leo kwenye Ukumbi wa JB Belmonte,Jijini Dar es salaam.
Msajili wa Vyama vya Siasa nchini,Jaji Francis Mutungi akichangia mada katika mkutano huo wa Viongozi wa Vyama vya Siasa uliofanyika leo kwenye Ukumbi wa JB Belmonte,Jijini Dar es salaam.
Mwenyekiti wa Chama cha UDP,Mh. John Momose Cheyo akiwa na Katibu wa NEC,Itikadi na Uenezi CCM,Ndg. Nape Nnauye wakati wa mapumziko mafupi ya mkutano huo.
Mwenyekiti wa CHADEMA,Mh. Freeman Mbowe akijadiliana jambo na Katibu Mkuu wa Chama cha ACT,Ndg. Samson Mwigamba.
Eeehh....bwanaaaaa upoooo........?? Mwenyekiti wa Chama cha NCCR-Mageuzi,Mh. James Mbatia akifurahi jambo na Katibu wa NEC,Itikadi na Uenezi CCM,Ndg. Nape Nnauye.Katikati ni Katibu Mkuu wa CHADEMA,Dkt. Wilbroad Slaa.Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii.

RED ARROWS FC KUWEKA KAMBI TANZANIA.

February 12, 2015

Kutoka kushoto ni Ofisa habari wa Red Arrows  Lt Melody Siisii, Mwenyekiti wa Red Arrows Col Nolasco Chilando, Katibu Mkuu wa TFF Selestine Mwesigwa na Ofisa Ubalozi wa Zambia nchini Tanzania Alex Chila, wakiwa ofisi za TFF - PPF Tower leo.
Klabu ya Red Arrow FC inayoshiriki Ligi Kuu nchini Zambia inatarajiwa kuwasili jijini Dar es salaam-Tanzania jumatatu ya wiki ijayo kwa ajili ya kuweka kambi ya mafunzo ya wiki moja kujindaa na msimu mpya wa Ligi Kuu nchini humo 2015.

Uongozi wa klabu hiyo chini ya mwenyekiti wake Col Nolacso K Chilando ulifika leo makao makuu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini Tanzania - TFF sambamba na Afisa habari wa klabu Lt Col Melody Siisii, Bw Alex Chila ofisa ubalozi wa Zambia nchini Tanzania kujitambulisha uwepo wao nchini.

Wakiongea na katibu  mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini Tanzania - TFF Selestine Mweisgwa, uongozi wa timu hiyo umesema maandalizi ya kambi yameshakamilika na kikubwa walikua wanaliomba Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini kutambua uwepo wao na kuwasaidia kupata viwanja vya kufanyia mazoezi.

Naye Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini -TFF Bw.Mwesigwa  alisema wameyapokea maombi hayo ya Red Arrow FC  na kuwakaribisha nchini kwa ajili ya kambi yao na kusema ujio wao utafungua milango kwa vilabu vingine pia kuja kuweka kambi nchini.

Timu ya Red Arrow FC inayomilikiwa na jeshi la Anga nchini Zambia ikiwa nchini kwa mafunzo, inatarajia kucheza mchezo mmoja wa kirafiki na imeliomba Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini kuwatafutia timu moja ya kucheza nayo.

IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF

Best Regards,
Baraka Kizuguto
MEDIA & COMMUNICATION OFFICER
255 ya leo February 12, inawahusu Flaviana Matata, Miss Tanzania Liliani Kamazima na msanii T.I.D.

255 ya leo February 12, inawahusu Flaviana Matata, Miss Tanzania Liliani Kamazima na msanii T.I.D.

February 12, 2015

uzinduzi-waFMF-stationaries-project-za-flavianafoundationa-30-of-133
Sikiliza 255 ya leo February 12, kutoka kwenye show ya XXL ya Clouds Fm na story ya kwanza kusikika inamhusu mwanamitindo Flaviana Matata ambapo mratibu wake amezungumzia ishu ya ile kampeni iliyokuwa inafanywa na  Flaviana Matata Foundation ya kuchangia vifaa vya kujenga Shule ya msingi Msinune iliyoko Bagamoyo, amesema baadhi ya michango imeshakamilika na miezi michache ijayo michango hiyo yakiwemo madawati vitakabiziwa kwenye Shule hiyo.
11 (1)
Baada ya shindano la Miss Tanzania kufungiwa watu wengi wamekuwa wakijiuliza endapo mshindi wa mwaka huu atashiriki katika mashindano ya Miss World mwakani ambapo Miss Tanzania 2014, Liliani Kamazima amesema kuwa atashiriki kama kawaida ingawa hajui miaka miwili iliyobaki na kuhusu kufungiwa kwa mashindano hayo amesema hatua hiyo imeziba ndoto za wasichana waliotaka kushiriki.
q-chief6
Kwenye 255 ya jana mwanamziki Q Chief alizungumzia ishu ya msanii T.I.D  kumlaumu kuwa yeye ndio chanzo cha Top Bad kufa, na kukanusha vikali na kumtupia lawama T.I.D, kwenye 255 ya leo msanii T.I.D amesema kuwa ameamua kuto kuzungumza chochote juu ya jambo hilo na kusikitishwa na maelezo ya Q Chief  kwa kuwa alizungumza ukweli na kwa sasa amenunua vyombo vingine na Top Band iko pale pale.
“HATUTAFAIDIKA NA MIRADI YA MAJI TUNAYOITEKELEZA, KAMA HATUTATUNZA VYANZO VYA MAJI TULIVYONAVYO”-MAKALLA

“HATUTAFAIDIKA NA MIRADI YA MAJI TUNAYOITEKELEZA, KAMA HATUTATUNZA VYANZO VYA MAJI TULIVYONAVYO”-MAKALLA

February 12, 2015

mak1 
Naibu Waziri wa Maji, Amos Makalla akizindua rasmi mradi wa maji Kijiji cha Riroda, Wilaya ya Babati, Mkoa wa Manyara.
mak2 
Naibu Waziri wa Maji, Amos Makalla mara akiwa amesimama pembeni ya mradi wa Kijiji cha Managhat, Wilaya ya Babati, Mkoa wa Manyara,pamoja na Katibu Tawala wa Mkoa wa Manyara, Omari Chambo na Mkurugenzi wa Mji wa Babati, Omari Mkombole mara baada ya kuweka jiwe la msingi kwenye mradi huo.
mak3 
Naibu Waziri wa Maji, Amos Makalla na Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Joel Bendera wakikata rasmi utepe, kabla ya kuweka jiwe la msingi kwenye jengo jipya la Mamlaka ya Mji wa Babati.
mak4 
Naibu Waziri wa Maji, Amos Makalla, Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Joel Bendera, Katibu Tawala wa Mkoa wa Manyara Omari Chambo (mwisho kushoto) na Mwenyekiti wa Bodi ya BAWASA, Mashughuli Minja (anayefuatia) wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji Babati (BAWASA), Iddi Msuya ndani ya jengo jipya la Mamlaka ya Maji Babati.
mak5 
Naibu Waziri wa Maji akikagua pampu ya kusukumia maji kwenye chanzo cha maji cha Masika, Wilaya ya Babati, Mkoa wa Manyara.
…………………………………………………………………….
Naibu Waziri wa Maji, Amos Makalla amesema wananchi hawatafaidika na miradi ya maji inayotekelezwa na Serikali hivi sasa, kama hawatakuwa makini kuvitunza na kuvilinda vyanzo vya maji. Mhe. Makalla amezungumza hayo jana katika ziara yake wilaya ya Babati, mkoa wa Manyara wakati akikagua utekelezaji wa miradi na kuzindua miradi iliyokamilika katika mkoa huo. “Miradi hii inayotekelezwa na Serikali hivi sasa, haitakuwa na maana kama hatutaacha uharibifu wa vyanzo vya maji tulivyonavyo, ambao unatokana na shughuli za kibinadamu za kila siku ndani au kandokando ya vyanzo hivyo. Miundombinu tunayoiweka haitakuwa na maana na itabaki kuwa kama magofu kama hatutakuwa na vyanzo vya maji vya kudumu”, alisema Mhe. Makalla. “Imefika wakati wananchi waamue na kuchukua hatua thabiti ya kutunza na kulinda vyanzo vya maji, la sivyo juhudi kubwa zinazofanywa na Serikali zitakuwa bure na kuingia gharama kubwa bila faida yoyote. Wananchi naomba mtupe ushirikiano katika hili, ili sisi tuweze kuhakikisha tatizo la maji katika nchi yetu linafikia kikomo”, aliongeza Mhe. Makalla. Naibu Waziri alisema kuwa miradi hii inagharimu mamilioni ya shilingi na Serikali imedhamiria kuwapa wananchi maji na si vinginevyo, lakini bila ushirikiano wao lengo letu halitafanikiwa. Hasa ukichukulia maeneo mengi ambapo miradi imetekelezwa kwa ufanisi, imechangiwa na ushirikiano mzuri unaopata Serikali kutoka kwa wananchi wake. Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Joel Bendera alishukuru jitihada za Serikali za kutatua tatizo la maji nchini kote, na alitoa agizo kwa viongozi wa mkoa mpaka vijijini, kuhakikisha kuwa wanachukua sheria kali na kuhakikisha hatua kali zinachukuliwa dhidi ya uharibifu wa vyanzo vya maji. Huku akisisitiza sheria ya kutofanya shughuli zozote za kibinadamu umbali wa mita 60 kutoka chanzo cha maji izingatiwe na kuahidi kama Mkuu wa Mkoa atalifanyia kazi ipasavyo. Hii imetokana na maeneo mengi ya vyanzo vya maji vya miradi mingi kuonekana haitunzwi vizuri katika wilaya za Hanang na Babati, huku shughuli nyingi za kibinadamu hasa kilimo zikionekana kushamiri katika vyanzo hivyo na kuleta changamoto kubwa katika utekelezaji wa miradi ya maji mkoani Manyara.
BARAZA LA MICHEZO LA TAIFA LASAINI WARAKA WA BRIGHTON DECLARATION KUHUSIANA NA USAWA WA KIJINSIA KATIKA MICHEZO

BARAZA LA MICHEZO LA TAIFA LASAINI WARAKA WA BRIGHTON DECLARATION KUHUSIANA NA USAWA WA KIJINSIA KATIKA MICHEZO

February 12, 2015

H1 
Katibu Mtendaji wa Baraza la Michezo la Taifa Bw. Henry Riaya (kulia) akisaini Waraka wa Brighton Declaration kuhusiana na usawa wa kijinsia katika michezo, hafla hiyo imefanyika jijini Dar es Salaam leo (jana) kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo Bi. Juliana Yassoda.
Katibu Mtendaji wa Baraza la Michezo la Taifa Bw. Henry Riaya (kulia) akisisitiza jambo mbele ya wanahabari hawapo pichani kuhusiana na Waraka wa Brighton Declaration kuhusiana na usawa wa kijinsia katika michezo
H4 
Baadhi ya wanahabari wakimsikiliza Katibu Mtendaji wa Baraza la Michezo la Taifa Bw. Henry Riaya hayupo pichani akizungumza na wanahabari hawapo pichani katika hafla ya kusaini Waraka wa Brighton Declaration kuhusiana na usawa wa kijinsia katika michezo.Hafla hiyo imefanyika jijini Dar es Salaam leo. (jana.)
Picha zote na Benjamin Sawe -WHVUM
EFM YAANDAA HAFLA YA VALENTINE

EFM YAANDAA HAFLA YA VALENTINE

February 12, 2015

Team Nzima ambayo inaongoza kipindi cha ya sports headquaters ambacho kinaruka kila siku ya Jumatatu mpaka Ijumaa saa tatu mpaka saa sita mchana(Kweli wamechizika). EF2 
 Kala Pina akiweka pozi la nguvu na mchizi wake Swebe.Unaweza kumsikiliza Swebe katika kipindi cha Gurudumu ambacho kinarushwa kila siku Jumatatu mpaka Ijumaa Saa Sita mchana mpaka saa Tisa,akiwa na mwanadada Safia,Manganje pamoja na RDJ X5. EF5 
Meneja Uhusiano wa EFM Kanky Mwaigomole akiwa na mchizi wake Samira Kiango.Samira ni mhariri msaidizi katika chumba cha habari cha EFM Redio na pia ni mtangazaji wa habari.
Francis Mhando ni mmoja wa watangazaji wa kipindi cha Sports Headquaters akiwang’ara na machizi wake kutoka Canada.
………………………………………………..
Kila mwaka,tarehe 14 Februari,watu duniani kote huadhimisha siku ya wapendanao duniani. Kama ilivyo ada,wengi wetu tumezoea kuadhimisha siku hiyo na aidha mume,mke au mpenzi. Ila kituo cha redio cha 93.7 EFM, kinawapa nafasi ya kipekee wasikilizaji wao kuchagua mtu ambaye wao ndio wanamuona kama mchizi wao. Meneja Uhusiano wa 93.7 EFM,Kanky Mwaigomole,amesema mchizi wako sio lazima awe mpenzi wako,bali anaweza kuwa kaka,dada,jirani,bosi wako au hata mama mkwe wako,wote hao wanaweza kuwa mchizi wako. “Sio lazima kila mwaka tufanye mambo yale yale,tumeona tufanye mabadiliko kidogo,alisemea meneja huyo. Siku ya “wewe ndio mchizi wangu”,itafanyika pale Msasani Beach Club,siku ya tarehe 14 mwezi huu wa February mwaka 2015,ambapo itahusisha wasanii kama vile Mesen Selecta (Mzee wa kanya boya),Recho Kizunguzungu,Msaga sumu,Snura, Sir Juma Nature,RDJ Majay akiwa na Zungu the drama na wengine kibao. Kanky alisema kwamba ukija na mchizi wako,kutakuwa na zawadi kubwa sana kutoka kwa DJ Majay na Zungu the drama. “Tunaomba watanzania wajitokeze kwa wingi,kwani watangazaji wote watakuja kupiga picha na kuongea na mchizi wa EFM 93.7.Bado tunaendelea kuwaleta wasikilizaji wetu karibu na sisi,kama mnakumbuka mwaka jana,tuliwaletea tamasha la “Mziki Mnene”,ambapo tulipata nasafi kubwa ya kujumuika na washabiki wetu kwa mda wa miezi mitatu mfululizo,na tukawaahidi kuwaletea mambo mengi mbele ya macho yao”,alisema meneja uhusiano huyo. Kanky alisema kuwa,zawadi nyingi zitatolewa kwa mtu na mchizi wake na pia kutakua na michezo mbali mbali ambayo itafanyika siku hiyo ya 14 February 2015. Aliendelea na kusema kwamba hii sio tamasha bali watu waje na machizi wao kuja kuchizika,ni kuanzia saa kumi jioni mpaka watakapo choka.

WAZEE WA NGWASUMA KUWASHA MOTO LEO JIJINI TANGA

February 12, 2015
BENDI ya mziki wa Dansi nchini ya FM Academia “Wazee wa Ngwasuma”wanatarajiwa kuwagawisha wakazi wa Jiji la Tanga katika onyesho lao la wakati wa siku ya wapendanao Valentine day litakalofanyika February 12 leo.

Onyesho hilo linatarajiwa kufanyika kwenye ukumbi wa Tanga Hotel ambalo litakuwa na zawadi mbalimbali ya CD ya chuki ya nini kwa mashabiki wote watakaoweza kuingia kushuhudia burudani hiyo.

Mratibu wa Onyesho hilo,Kelvin Msinga alisema kuwa maandalizi ya onyesho hilo yanaendelea vizuri na wasanii wanaounda bendi hiyo wapo tayari kuweza kuwapa burudani ya aina yake wakazi wa jiji la Tanga na vitongoji vyake.

Msinga alisema kuwa katika onyesho hilo wakazi wa Tanga watapata fursa ya kusikiliza nyimbo zao kali kama “Chuki ya Nini”,Fataki,Otilia,Ndoa ya Kisasi,Daily Chako Ulaumiwe,Maisha,Neema na Madudu

Hata hivyo aliwataka wapenzi wao kuhakikisha wanajitokeza kwa wingi ili kuweza kushuhudia burudani iliyokuwa na ubora wa aina yake ambayo itakuwa ikitolewa na wasanii hao.
Rais kikwete awaapisha Balozi Mpya wa Tanzania nchini Kenya na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha

Rais kikwete awaapisha Balozi Mpya wa Tanzania nchini Kenya na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha

February 12, 2015

bal1 
Pichani Balozi mpya wa Tanzania nchini Kenya Bwana John Haule akila kiapo mbele ya Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete Ikulu jijini Dar es salaam leo asubuhi.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete leo amewaapisha Balozi mpya wa Tanzania nchini Kenya na Naibu Katibu mkuu wa Wizara ya Fedha.Katika hafla hiyo iliyofanyika ikulu jijini Dar es Salaam,
Rais Kikwete akimkabidhi vitendea kazi  Bwana John Haule kuwa baada ya kumwapisha kuwa balozi mpya wa Tanzania nchini Kenya 
Naibu katibu mkuu Wizara ya Fedha, Dkt.Hamisi Mwinyimvua akila kiapo mbele ya Rais ikulu jijini Dar es Salaam leo.
bal4 
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiirekebisha tai ya mtoto Amani Mwinyimvua(11) muda mfupi baada ya kumwapisha Baba yake Hamis Mwinyimvua kuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha katika hafla iliyofanyika ikulu jijini Dar es Salaam leo asubuhi(picha na Freddy Maro)
MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AAGANA NA BALOZI WA SAUDI ARABIA ANAYEMALIZA MUDA WAKE NCHINI.

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AAGANA NA BALOZI WA SAUDI ARABIA ANAYEMALIZA MUDA WAKE NCHINI.

February 12, 2015

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkaribisha Balozi wa Saudi Arabia, Hani Abdullah Mominah, wakati alipofika Ofisini kwake Ikulu Jijini Dar es Salaam, leo Feb 12, 2015 kwa ajili ya kumuaga baada ya kumaliza muda wake wa kazi nchini. Picha na OMR gh2 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Balozi wa Saudi Arabia, Hani Abdullah Mominah, wakati alipofika Ofisini kwake Ikulu Jijini Dar es Salaam, leo Feb 12, 2015 kwa ajili ya kumuaga baada ya kumaliza muda wake wa kazi nchini. Picha na OMR
gh3 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na  Balozi wa Saudi Arabia, Hani Abdullah Mominah, baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika wakati  Ofisini kwa Makamu Ikulu Jijini Dar es Salaam, leo Feb 12, 2015 wakati Balozi huyo alipofika kwa ajili ya kumuaga baada ya kumaliza muda wake wa kazi nchini. Picha na OMR
Stori 9 zilizopewa headlines kwenye Magazeti ya leo Tanzania Februari 12, 2015 ziko hapa

Stori 9 zilizopewa headlines kwenye Magazeti ya leo Tanzania Februari 12, 2015 ziko hapa

February 12, 2015

blll 
MWANANCHI
Matukio ya wasafiri kukamatwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) wakiwa na nyara za Serikali na dawa za kulevya, yanazidi kuchukua sura mpya baada ya raia mmoja wa Ubelgiji kukamatwa akiwa na fuvu la binadamu.
Raia huyo, Balcjan Christine Weejktgns (49) alikamatwa Jumatatu saa 2:30 usiku wakati akiwa katika taratibu za kuingia uwanjani hapo tayari kwa safari ya kuelekea Ubelgiji kupitia Zurich, Uswisi.
Tukio la kukamatwa kwa Mbelgiji huyo ni mwendelezo wa matukio ya aina yake uwanjani hapo baada ya watu wengine wawili kukamatwa kwa nyakati tofauti kwenye uwanja huo wakiwa na kucha za simba na kenge walio hai.
Kamanda wa Polisi Viwanja vya Ndege, Hamisi Selemani alisema mtu huyo alikutwa ameficha fuvu hilo la binadamu kwenye mfuko wa plastiki.
Alivyopita kwenye mashine za ukaguzi tulimtilia shaka na tulipompekua tulimkuta amebeba fuvu la kichwa cha binadamu kikiwa kimewekwa kwenye mfuko wa plastiki ndani ya sanduku alimokuwa ameweka nguo zake na vitu mbalimbali:-Selemani.
Raia huyo anadaiwa kuwa ni mkazi wa Chuo Kikuu cha Kilimo (SUA) mkoani Morogoro na inadaiwa kuwa alikuwa nchini kwa ajili ya kufanya utafiti.
MWANANCHI
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) imekiri kuwapo kwa baadhi ya watumishi wake wanaojihusisha na vitendo vya kupokea rushwa, hivyo kuchafua sifa ya taasisi hiyo.
Akizungumza na waandishi wa habari mjini Kigoma jana, Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Dk Edward Hoseah alisema tuhuma zilizotolewa hivi karibuni na taasisi zilizofanya utafiti juu ya masuala ya rushwa nchini, baadhi yake zina ukweli.
Dk Hoseah alisema wanapokea utafiti huo kama changamoto na watatumia sheria, kanuni na taratibu kuwapa adhabu watumishi watakaobainika kujihusisha na vitendo vya rushwa.
Takukuru siyo malaika, iwapo nitasema hakuna kabisa rushwa ndani ya taasisi hii nitakuwa ninajidanganya kwani hili tatizo lipo sehemu zote, inawezekana maofisa wasio waadilifu wanapokea rushwa lakini ninawahakikishia kwamba tutachukua hatua kali dhidi ya yeyote atakayebainika:-Dk Hoseah 
Pia, alitoa tahadhari kwa wananchi kuwa makini na matapeli wanaojitangaza kwamba wao ni maofisa wa Takukuru, hivyo kuomba rushwa kwa baadhi ya maofisa wa Serikali na watu wengine ambao wanabainika kufanya makosa yanayohusiana na ubadhirifu mbalimbali.
MWANANCHI
Waziri wa Katiba na Sheria, Dk Asha-Rose Migiro amesema kila kata nchini itapata nakala 300 za Katiba Inayopendekezwa ili kuwawezesha wananchi  kuisoma na kushiriki katika Kura ya Maoni iliyopangwa kufanyika Aprili 30, mwaka huu.
Amesema mpaka kufikia Februari 9, mikoa 11 nchini ilikuwa tayari imepatiwa nakala hizo na kwamba Serikali imepanga kuchapisha nakala milioni 2 kwa ajili ya kuzisambaza nchi nzima.
Amesema nchini kuna zaidi kata 3,800 na lengo la Serikali ni kusambaza nakala hizo kwenye vijiji, vitongoji na mitaa kupitia Ofisi za wakuu wa mikoa, wilaya, wakurugenzi wa halmashauri za miji, manispaa na majiji.
Dk Migiro alisema mbali na nakala hizo, Katiba Inayopendekezwa pia imewekwa katika tovuti za Wizara ya Katiba, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Bunge.
Wananchi waliokuwa katika miji na vijiji siyo wote wanaweza kupata nakala katika mtandao. Ukiwa na  nakala halisi unaisoma wakati wote kwa hiyo Serikali imekuwa na nia ya kuwapatia watanzania nakala halisi haraka iwezekanavyo:Migiro
MWANANCHI
Klabu ya Simba imewapa masharti mahasimu wao wa jadi, Yanga kama inahitaji mashabiki wao waishangilie kwenye mchezo wa keshokutwa wa Kombe la Shirikisho la Soka Afrika (CAF), dhidi ya BDF IX ya Botswana.
Simba ilieleza jana kuwa katika mchezo huo, mashabiki wake wataingia uwanjani wakitanguliza utaifa kwanza, lakini kwa sharti la Yanga kutowaangusha na kucheza mpira wenye kiwango, kinyume na hapo watabadilika na kuelekeza nguvu zao kwa wapinzani, BDF.
Rais wa Simba, Evance Aveva alisema kuwa katika mchezo huo watakuwa upande wa Yanga iwapo watacheza mpira wenye kiwango kama ule unaochezwa nao (Simba), tofauti na hivyo watawageuka katikati ya mchezo.
Kwenye mechi hiyo tutatanguliza utaifa kwanza kwa kuiunga mkono Yanga mwanzoni mwa mchezo na tutaendelea kufanya hivyo hadi mwisho, kinyume chake tutawageuka.
Ingawa haijawahi kutokea Simba ikaishangilia Yanga, lakini kwenye mchezo huu tumeamua kutanguliza mbele utaifa, lakini tukiona Yanga ‘wanambwelambwela’ (hawaeleweki) uwanjani kwa kucheza chini ya kiwango tutawabadilikia na tutaiunga mkono BDF:-Aveva.
NIPASHE
Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), inatarajia kuanzisha kitengo cha magari ya kubebea wagonjwa (Ambulance) kwa ajili ya kubeba wagonjwa kutoka katika maeneo mbalimbali ya Jiji.
Hayo yalielezwa jana na Mkurugenzi wa MNH, Dk. Hussein Kidanto, wakati wakisaini makubaliano ya kupokea msaada wa magari mawili ya kubebea wagonjwa kutoka kwa Balozi wa Japan nchini, Masaki Okada.
Dk. Kidanto, alisema kwa sasa hospitali hiyo ina gari moja la wagonjwa ambalo linashindwa kukusanya wagonjwa na kuwapeleka katika hospitali hiyo na chini ya kitengo hicho wataanza na magari 10.
Tunaushukuru Ubalozi wa Japan kwa kutoa msaada huu, utakuwa mwanzo wa kuanzisha kitengo cha huduma ya magari ya wagonjwa ambacho tunakianzisha Muhimbili ili yaweze kuwabeba kutoka maeneo mbalimbali ya Jiji:-Dk. Kidanto.
Alifafanua kuwa, magari hayo yataandikwa namba maalum za maeneo tofauti ya Jiji na yatabeba watu watakaopatwa na ugonjwa wa ghafla kama mama wajawazito, wenye magonjwa ya moyo na maengine kwa lengo la kuwafikisha hospitali wakiwa salama.
NIPASHE
Kikao cha Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Jiji la Tanga, kimevunjika mara tatu mfululizo kutokana na madiwani wa Chama cha Wananchi (CUF) na wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)  kufanyiana vurugu na kukunjana kutaka kuzichapa kavu kavu.
Vurugu hizo zimetokana na uongozi wa Halmashauri ya Jiji la Tanga kuendelea kumtambua na kumwita katika vikao vya Baraza la Madiwani wa jiji hilo aliyekuwa Diwani wa Kata ya Malungu (CUF), Mohamed Mwambeya, wakati alishajiondoa katika chama hicho.
Mwambeya ambaye alipata udiwani wa kata hiyo kupitia CUF,  Agosti, mwaka jana, alitangaza kukihama chama hicho na kuhamia CCM wakati wa mkutano wa Mwenyekiti wa Taifa wa Jumuiya ya Wazazi CCM, Abdallah Bulembo alipofanya ziara mkoani Tanga.
Kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano Tanzania, nafasi zote za kuchaguliwa za kisiasa kwa maana ya rais, ubunge na diwani, ni lazima atokane na chama cha siasa na masharti hayo pia yapo katika uchaguzi wa serikali za mitaa.
Hivyo kutokana na katiba hiyo, Mwambeya ambaye alitangaza kujiondoa CUF na kujiunga CCM  ni wazi kuwa udiwani wake utakuwa umekoma na msimamizi wa uchaguzi alistahili kutangaza kuwa kata hiyo ipo wazi ili kufanyike mchakato wa kuchagua diwani mwingine atakayetokana na chama cha siasa.
MTANZANIA
Hatimaye mwimbaji wa nyimbo za Injili nchini, Emmanuel Mbasha, ameibuka na kuweka wazi suala la mgogoro wa mtoto na mkewe Flora Mbasha.
Hatua hiyo imekuja miezi saba tangu wawili hao walipoingia katika mgogoro wa ndoa yao hali iliyosababisha Mbasha kufikishwa mahakamani kwa kosa la ubakaji.
Hivi karibuni, picha za mtoto mchanga zilisambazwa katika mitandao ya kijamii na kudaiwa kuwa ni wa Flora aliyezaa na Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana baada ya kuahirishwa kwa kesi ya ubakaji inayomkabili katika Mahakama ya Ilala, Mbasha alisema hayupo tayari kuzungumzia kuzaliwa kwa mtoto huyo, ila anayeweza kueleza ukweli kuhusu baba wa mtoto ni Flora mwenyewe.
Siwezi kuongea chochote, ukweli wote anaujua Flora nendeni mkamfuate atawaeleza, na sijaongea na gazeti lolote kuhusu mtoto huyo… kwa sasa sipo tayari kusema lolote:- Mbasha.
HABARILEO
BAADA ya kushuka kwa bei ya mafuta nchini, wakati wowote kuanzia leo Shirika la Umeme Nchini (Tanesco) linatarajiwa kutangaza bei mpya za umeme ambazo zitakuwa na unafuu kwa wananchi.
Kutangazwa kwa bei hiyo ni agizo la Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene la kuwataka kuangalia uwezekano wa kushusha gharama za umeme ili kushuka kwa mafuta kuwaguse moja kwa moja wananchi wa kawaida.
Aidha, Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra) nayo imetakiwa kuangalia namna itakavyoweza kushusha bei za nauli ili kushuka kwa gharama za mafuta, kuendane sambamba na kuwagusa wananchi.
Simbachawene alitoa kauli hiyo jana jijini Dar es Salaam, baada ya mkutano wa pamoja kati ya wadau na Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) na wizara hiyo.
Alisema, ingawa matumizi ya mafuta katika kuzalisha umeme yamepungua, lakini kwa mitambo na kiasi kinachotumika katika kuzalisha umeme lazima ionekane kushuka kwa bei ya umeme.
Tanesco waangalie ni kwa kiasi gani gharama za uzalishaji, kwa sababu hizo gharama za uzalishaji wa umeme ndiyo zinazotumika kupanga bei ya umeme. ”Hivyo lazima tuoneshe Ewura ‘
HABARILEO
Mwanasheria Mwandamizi wa Tanesco, Steven Urassa amefutiwa mashitaka ya kupokea sehemu ya fedha zilizokuwa kwenye akaunti ya Tegeta Escrow na kusomewa mashitaka ya kupokea rushwa ya Sh milioni 161.7.
Urassa aliondolewa mashitaka hayo jana baada ya Wakili kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Leonard Swai kubadilisha hati ya mashitaka dhidi yake.
Akisoma hati hiyo mbele ya Hakimu Mkazi, Janeth Kaluyenda, Swai alidai Februari 14, 2014 katika eneo la Benki ya Mkombozi, Urassa akiwa Mwanasheria Mwandamizi wa Tanesco alipokea rushwa ya Sh 161,700,000 kupitia akaunti namba 00120102658101.
Alidai Urassa alipokea fedha hizo kutoka kwa Mshauri wa Kimataifa ambaye ni Mkurugenzi wa VIP Engineering na Mkurugenzi wa zamani wa IPTL, James Rugemalira kama tuzo hiyo baada ya kuiwakilisha Tanesco na IPTL katika kesi ya Standard Charter nchini Hong Kong.
Upelelezi wa kesi umekamilika lakini upande wa utetezi ulidai kuna masuala ya kikatiba yanajitokeza katika kesi hiyo ambayo yanatakiwa kusikilizwa katika Mahakama Kuu.

VIONGOZI WA DINI WAJITOSA MAPAMBANO DHIDI YA UJANGILI, WAKUTANA NA WAZIRI NYALANDU KUPANGA MIKAKATI

February 12, 2015

 WAZIRI WA Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu, akizungumza katika mkutano wake na viongozi wa dini mbalimbali uliofanyika kwenye Hoteli ya Double Tree mjini Dar es Salaam, leo. Katika mkutano huo uliohudhuriwa na viongozi wa juu wa dini mbalimbali masuala mbalimbali kuhusiana na madhara ya ujangili wa wanyama kama tembo na faru yalijadiliwa.
 Viongozi wa dini mbalimbali wakimsikiliza Nyalandu
Waziri Nyalandu akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa dini mbalimbali baada ya mkutano huo