RAIS DKT. MAGUFULI AHUTUBIA SHEREHE ZA MEI MOSI ZILIZOFANYIKA KITAIFA MKOANI KILIMANJARO

May 01, 2017



 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitabasamu wakati Wafanyakazi wa Taasisi mbalimbali za Umma na Binafsi wakiwa katika maandamano ya Siku ya Wafanyakazi Duniani ambayo nchini yamefanyika Kitaifa katika Chuo cha Ushirika, Moshi Mkoani Kilimanjaro.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipunga mkono wakati Wafanyakazi wa Taasisi mbalimbali za Umma na Binafsi wakiwa wanapita mbele yake kwa njia ya  maandamano ya Siku ya Wafanyakazi Duniani ambayo nchini yamefanyika Kitaifa katika Chuo cha Ushirika, Moshi Mkoani Kilimanjaro. Wengine katika picha ni Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Spika wa Bunge Job Ndugai,  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu sera Bunge, Kazi, Vijana na wenye ulemavu, Jenista Mhagama,Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais na Utawala bora Angela Kairuki pamoja na Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA) Tumaini Nyamhokya.
 Sehemu ya Wafanyakazi waliofika kwenye Sikukuu ya Wafanyakazi Duniani katika Uwanja wa Chuo cha Ushirika mjini Moshi mkoani Kilimanjaro.
 Raiswa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa ameshikana mikono wakati wa wimbo wa Mshikamano daima pamoja na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Spika wa Bunge Job Ndugai,  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu sera Bunge, Kazi, Vijana na wenye ulemavu, Jenista Mhagama,Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais na Utawala bora Angela Kairuki, Rais wa Shirikisho la Vyama vya vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA) Tumaini Nyamhokya pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Said Meck Saidik.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa amenyanyua juu mikono mara baada ya kuimba wimbo wa Mshikamano Daima pamoja na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Spika wa Bunge Job Ndugai,  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu sera Bunge, Kazi, Vijana na wenye ulemavu, Jenista Mhagama,Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais na Utawala bora Angela Kairuki Rais wa Shirikisho la Vyama vya vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA) Tumaini Nyamhokya pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Said Meck Saidik.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia mamia ya wafanyakazi katika kilele cha Sikukuu ya Wafanyakazi Duniani zilizofanyika Kitaifa katika Uwanja wa Uwanja wa Chuo cha Ushirika mjini Moshi mkoani Kilimanjaro.
 Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Saidi M. Sadiki akitoa salamu za Mkoa kwenye Sikukuu hiyo ya Wafanyakazi Duniani.
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge, Kazi, Vijana na wenye ulemavu, Jenista Mhagama akitoa salamu katika Sikukuu ya Wafanyakazi mkoani Kilimanjaro.
 Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA) Tumaini Nyamhokya akizungumza katika Sikukuu ya Wafanyakazi Duniani zilizofanyika Kitaifa  mkoani Kilimanjaro. 
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge




  

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na wakazi wawili wenye ulemavu mara baada ya kumaliza kuhutubia katika kilele cha Sikukuu ya Wafanyakazi Duniani zilizofanyika Kitaifa katika Uwanja wa Uwanja wa Chuo cha Ushirika mjini Moshi mkoani Kilimanjaro.

MSD YANG'ARA SHEREHE ZA MEI MOSI KITAIFA MKOANI KILIMANJARO

May 01, 2017




Rais John Magufuli akimkabidhi zawadi Mfanyakazi Bora wa Bohari ya Dawa (MSD), 2016/2017, Juma Kiongozi katika maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi yaliyofanyika kitaifa mkoani Kilimanjaro leo. Kulia ni Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na kushoto ni  Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Jenista Mhagama. 

DKT. SHEIN AONGOZA SHEREHE ZA SIKU YA WAFANYAKAZI DUNIANI (MEI MOSI) MAHONDA, ZANZIBAR

May 01, 2017
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akisalimiana na Waziri wa Kazi, Uwezeshaji, Wazee, Vijana, Wanawake na Watoto, Mhe. Maudline Cyrus Castico alipowasili katika viwanja vya Mpira Mahonda Wilaya ya Kaskazini "B" Unguja leo katika Sherehe za Kilele cha maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akisalimiana na Katibu Mkuu wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Zanzibar Maalim Khamis Mwinyi alipowasili katika viwanja vya Mpira Mahonda Wilaya ya Kaskazini "B" Unguja leo katika Sherehe za Kilele cha maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akiwapungia Mkono Wafanyakazi mbali mbali waliopita mbele yake kwa Maandamano wakati wa Sherehe za Kilele cha maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani zilizofanyika leo katika viwanja vya Mpira Mahonda Wilaya ya Kaskazini "B" Unguja.
Baadhi ya wafanyakazi wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba,Sheria,Utumishi wa Umma na Utawala Bora wakipita kwa Maandamano mbele ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) wakati wa Sherehe za Kilele cha maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani zilizofanyika leo katika viwanja vya Mpira Mahonda Wilaya ya Kaskazini "B" Unguja.
Wafanyakazi na Wananchi kutoka shehia mbali mbali za Unguja walijumuika kwa pamoja katika Sherehe za Kilele cha maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani zilizofanyika leo katika viwanja vya Mpira Mahonda Wilaya ya Kaskazini "B" Unguja,wakipita kwa maandamano mbele ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) akiwa mgeni rasmi katika sherehe hizo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akiwapungia Mkono Wafanyakazi mbali mbali waliopita mbele yake kwa Maandamano wakati wa Sherehe za Kilele cha maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani zilizofanyika leo katika viwanja vya Mpira Mahonda Wilaya ya Kaskazini "B" Unguja akiwa na Viongozi mbali mbali.
Wafanyakazi na Wananchi kutoka shehia mbali mbali za Unguja walijumuika kwa pamoja katika Sherehe za Kilele cha maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani zilizofanyika leo katika viwanja vya Mpira Mahonda Wilaya ya Kaskazini "B" Unguja,wakipita kwa maandamano mbele ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) akiwa mgeni rasmi katika sherehe hizo.
Wafanyakazi wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar wakibeba Bango lenye Nembo la Idara yao wakati wa maandamano katika Sherehe za Kilele cha maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani zilizofanyika leo katika viwanja vya Mpira Mahonda Wilaya ya Kaskazini "B" Unguja,ambapo mgeni rasmi alikuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani).
Wafanyakazi wa Benki ya Tanzania BOT wakibeba Bango lenye Nembo la Idara yao wakati wa maandamano katika Sherehe za Kilele cha maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani zilizofanyika leo katika viwanja vya Mpira Mahonda Wilaya ya Kaskazini "B" Unguja,ambapo mgeni rasmi alikuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani).
​ Wafanyakazi wa ​Idara ya Uhamiaji Zanzibar wakimpungia Mkono ​Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani),​alipokuwa akipokea ​​maandamano katika Sherehe za Kilele cha maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani zilizofanyika leo katika viwanja vya Mpira Mahonda Wilaya ya Kaskazini "B" Unguja.Picha na Ikulu, Zanzibar.

WAKAZI 122 MKOANI SIMIYU WAPEWA HATI NA WAZIRI LUKUVI AGAWA HATI 122 LAMADI

May 01, 2017
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. William Lukuvi amegawa hati miliki za ardhi 122 kwa wananchi wa Lamadi Mkoa wa Simiyu wakati alipofanya ziara yake mikoa ya kanda ya ziwa kuhamasisha ulipaji kodi ya pango la ardhi na suala la urasimishaji wa makazi holela.

Wananchi hao 122 ni wale waliofanikiwa kulipia michango yote, hivyo kuondokana na makazi holela na kuishi katika makazi rasmi. Hata hivyo jumla ya wananchi 5,200 wa Lamadi Mkoa wa Simiyu washapimiwa maeneo yao kwa ajili ya urasimishaji, na watapatiwa hati zao mara tu baada ya kukamilisha michango stahili.

Katika ziara hiyo, waziri Lukuvi amefika wilaya ya Ilemela mkoani Mwanza na kufanya ukaguzi wa mfumo wa ulipaji kodi ya pango la ardhi wilayani hapo na kugundua kati ya wakazi 35,000 wanaotakiwa kulipa kodi ya ardhi 28,000 wameishapelekewa hati ya madai.

Waziri Lukuvi pia ametembelea Idara ya Ardhi ya wilayani Nyamagana na kukagua mafaili ya kumbukumbu za wananchi kuhusu taarifa za ardhi ikiwemo masuala ya hati na kukugundua baadhi ya viongozi hawajalipa kodi ya pango la ardhi. Mmoja ya viongozi hao ni Mbunge wa Kwimba Shannif Mansoor ambaye hajalipa kodi ya pango la ardhi tangu 2010 kiasi cha shilingi milioni 529.

Aidha katika wilaya hiyo ameongea na wananchi wa Nundu kata ya Meko, mbali ya kusikiliza kero zao na kuzipatia ufumbuzi papo hapo, amewahimiza kuchamkia fursa ya kurasimisha makazi yao na kupata hati ili kuzipa thamani ardhi zao na kujitanulia fursa za uchumi.
Magere Mugeta mkazi wa Lamadi mkoani Simiyu akipokea hati ya kumuliki ardhi kutoka kwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mheshimiwa William Lukuvi.
Janet Magige mkazi wa Lamadi mkoani Simiyu akipokea hati ya kumuliki ardhi kutoka kwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mheshimiwa William Lukuvi.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mheshimiwa William Lukuvi akiwasisitiza wakazi Lamadi mkoani Simiyu umuhimu wa kumiliki ardhi kwa hati kwa kuwaonesha moja ya hati zinazotolewa kwa wananchi.
Wakazi wa Lamadi mkoani Simiyu wakishangilia pamoja na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mheshimiwa William Lukuvi kwa kuwawezesha kupata Hati za kumiliki Ardhi.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mheshimiwa William Lukuvi akikagua moja ya faili katika masijala ya Ardhi ya Ilemela Mkoani Mwanza akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongela (mwenye kofia).
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mheshimiwa William Lukuvi akikagua mfumo wa kodi wa manispaa ya Nyamagana mkoani Mwanza ili kubaini wadaiwa wa kodi ya Ardhi.
ESRF yakutanisha wadau kuijadili bajeti ya 2016/2017 katika sekta za Elimu na Kilimo

ESRF yakutanisha wadau kuijadili bajeti ya 2016/2017 katika sekta za Elimu na Kilimo

May 01, 2017
Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF) imewakutanisha wadau mbalimbali wa maendeleo nchini kuijadili bajeti ya Tanzania ya mwaka wa fedha 2016/2017 ambao unaelekea kuisha. Akizungumza katika mkutano huo, Mkurugenzi Mtendaji wa ESRF, Dkt. Tausi Kida alisema mdahalo huo ni sehemu ya shughuli ambazo zinafanywa na ESRF ili kutazama ni njinsi gani Taasisi inaweza kuisaidia Serikali kuweka mipango thabiti kwa ajili ya maendeleo ya nchi. Dkt. Kida alisema mdahalo huo ulihusu bajeti ya Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa kuangalia utekelezaji wa bajeti zilizopitishwa kwa mwaka wa fedha 2016/2017, changamoto zilizopo na nini kifanyike katika bajeti ya 2017/2018. Mkurugenzi Mtendaji wa ESRF, Dkt. Tausi Kida akitoa neno la ufunguzi.[/caption] “ESRF imekuwa ikishirikiana na wadau ili kuangalia ni jinsi gani tunaweza kusaidia mchakato wa maendeleo wa nchi yetu kwa njia ya utafiti mbalimbali, uchambuzi na utayarishaji wa sera na kuongeza wadau uwezo kupitia mafunzo mbalimbali. “Kama jinsi mnavyojua nchi yetu imekuwa na mipango ya maendeleo ambayo inatekelezwa kupitia bajeti kwa kuangalia mambo yenye umuhimu kwa Taifa, bajeti imekuwa ikipangwa kila mwaka kwa kuzingatia maeneo ya kuyapa kipaumbele ili kuleta maendeleo kwa nchi.” alisema Dkt. Kida. Kwa upande wa mtoa taarifa ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dkt. Joviter Katabaro (Mkufunzi katika, shule ya Elimu, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam) alisema pamoja na serikali kutoa elimu bure katika ngazi fulani ya elimu nchini lakini bado kuna changamoto mbalimbali katika elimu ambazo zinahitaji kutafutiwa ufumbuzi katika bajeti ya 2017/2018. Mhadhiri Mwandamizi wa Shule Kuu ya Elimu Chuo Kikuu cha Dar es salaam, Dk. Joviter Katabaro akitoa taarifa kuhusu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia.[/caption] “Pamoja na jitihada kubwa ya Serikali katika elimu bado kuna upungufu wa majengo 10,000 ya shule nchini kitoke, kuna upungufu wa maktaba 15,000, vyoo bado havitoshi,” alisema Dk. Katabaro. Kwa upande wake, Prof. Haidari Amani (Mtafiti Mshirki mwandamizi ESRF) ambaye alitoa taarifa kuhusu Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi alisema pamoja na sekta ya kilimo kuwa na changamoto ambazo zinajitokeza serikali inatakiwa iweke mfumo mzuri kuanzia wakulima wadogo ili waweze kunufaika na kilimo ambacho wanakifanya. Mtafiti Mwenza wa ESRF, John Shilinde akitoa taarifa kuhusu Bajeti ya Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi. Mtafiti Mwenza Kiongozi wa ESRF, Prof. Haidari Amani akijibu maswali ya baadhi ya washiriki waliohudhuria. Mkurugenzi Mtendaji wa ESRF, Dkt. Tausi Kida akifafanua jambo wakati wa kuijadili bajeti ya 2016/2017 katika sekta za Elimu na Kilimo. Picha juu na chini ni baadhi ya washiriki wakitoa maoni na kuuliza maswali kuhusu bajeti zilizotolewa taarifa. Baadhi ya wadau mbalimbali wa maendeleo nchini walioshiriki kuijadili bajeti ya Tanzania ya mwaka wa fedha 2016/2017 katika sekta za Elimu na Kilimo.

HIZI NI SABABU ZA KUTUMIA MAWAKALA WA USAFIRI

May 01, 2017
Na Jumia Travel Tanzania


Kuja kwa mtandao wa intaneti kumepelekea huduma nyingi kuhamia mtandaoni na hivyo kupunguza idadi ya watu kutembelea ofisi. Kupitia tovuti za makampuni wateja wamepewa fursa kubwa ya kuperuzi huduma mbalimbali na kupata taarifa za kutosha ndani ya muda mfupi. 
Sekta mojawapo iliyoyapokea mabadiliko hayo kwa kasi kubwa ni ya utalii na usafiri. Kama unatembelea mitandao mara kwa mara nadhani utakuwa umegundua kuwa kuna kampuni nyingi zinatoa huduma hizo kama vile Jumia Travel na Expedia.

Lakini haimaanishi kuwa kuja kwa intaneti kutaondoa kuhitajika kwa mawakala. Kwa asilimia fulani idadi ya wateja kwenda au kuwasiliana na mawakala imepungua. Lakini Jumia Travel ingependa kusisitiza kuwa mawakala wana nafasi kubwa kwa wateja hususani katika masuala yafuatayo:     

Kupata ushauri wa kitaalamu. Zoezi la kupanga mchakato mzima wa kusafiri huwa linachosha sana kama hauna utaalamu mkubwa. Mara nyingi mawakala wa usafiri wanakuwa na uzoefu mkubwa katika sekta hiyo. Na hii ni kutokana na kufanya kazi kwa muda mrefu, kujuana na watoa huduma pamoja na mchakato mzima mpaka safari inakamilika. Mbali na hapo haikugharimu pesa kupata huduma zao kwani mara nyingi wao hulipwa kwa kamisheni. 

Kuokoa fedha. Mawakala wanaweza kuokoa kiasi kikubwa cha fedha za mteja kwani wanaweza kumpatia huduma ambazo kwa njia ya kawaida hawezi kuzipata. Na hii ni kutokana na mahusiano mazuri na ya muda mrefu kwenye biashara waliyonayo na watoa huduma. Pia kuna bei na ofa zingine huwafikia mawakala kwanza kabla ya wateja. Kwa hiyo ukiwatumia wao utafaidika nazo tofauti na ukienda kwa watoa huduma hao moja kwa moja kama mteja.  
Kuokoa muda. Zoezi zima la kupanga kusafiri iwe ndani au nje ya nchi linachosha kutokana na mlolongo mrefu ndani yake. Lakini unaweza kuutua mzigo wote huo kwa mawakala wa usafiri. Kwa sababu wao wanakuwa wamekwishafanya utafiti wa kutosha na kujua wateja wanapendelea vitu gani na ni wapi kwa kuvipata. Kwa hiyo badala ya kupoteza muda mtandaoni jaribu kuwasiliana na wakala aliye karibu nawe akusaidie huku wewe ukistarehe kwa kuweka miguu juu ukisubiria simu kujulishwa kuwa kila kitu kipo tayari. 

Ni njia salama zaidi kwa mteja. Mtu anaweza kujiuliza ni salama kivipi wakati huduma wanazotoa wao ni sawa na za makampuni husika? Jibu ni rahisi, kuna wakati matatizo hujitokeza wakati wa kusafiri, kwa mfano, kuchelewa ndege au safari kufutwa kabisa, au kutopatiwa chumba cha hoteli ulichokihitaji. Zikitokea changamoto kama hizo na wewe ulitumia wakala basi hautakiwi kuwa na wasiwasi au kugombana na mtu. Cha kufanya ni kuwasiliana na wakala wako na yeye atasuluhisha kila kitu.   

 Wanajua kipi ni bora kwa wateja wao. Kutokana na kuwepo kwenye sekta ya uwakala kwa muda mrefu, kwa mfano, miaka 10, 20 au 30, ni dhahiri kwamba watakuwa wanajua maswali ambayo wateja huuliza na majibu wanayoyatarajia. Hivyo inakuwa ni rahisi kwao kuwapatia wateja wao kilicho bora zaidi kutokana na uzoefu walionao. Na kwa kuongezea mawakala hupokea ofa mbalimbali kutoka kwa mahoteli na kampuni za usafiri kwanza kabla ya wateja. Pia wao huwa na ofa zao ili kuwavutia zaidi wateja kutumia huduma zao, kama vile kipindi cha sikukuu na mapumziko mbalimbali. 

Unapatiwa machaguo sahihi kulingana na mahitaji yako. Faida mojawapo ya kuwatumia mawakala ni kwamba wao hawatoi au kunadi huduma za kampuni moja tu pekee. Kikubwa wao wanachokizingatia ni kutoa huduma nyingi kadri wawezavyo na washirika wao wa kibiashara. Hivyo basi ni rahisi kwao kusikiliza wateja wanataka nini na kuwatimizia kulingana na huduma walizonazo. Lakini ukienda moja kwa moja hotelini au shirika la ndege ni wazi kwamba utapata huduma zao tu pekee na si vinginevyo.

Kwa ufupi ukiwa kama msafiri ni vema kutambua ni aina gani ya safari unayotaka kufanya kabla ya kutumia wakala. Kama ni safari ya kawaida na haihitaji mambo mengi unaweza kujipati huduma mwenyewe kwa kuingia mtandaoni. Wapo mawakala wengi ambao wanatoa huduma mtandaoni na pia wana ofisi, kama vile Jumia Travel wanavyoendesha shughuli zao nchini Tanzania na kwingineko ndani na nje ya Afrika.