Waziri
wa Ujenzi Dkt. John Magufuli akiweka jiwe la msingi kuashiria ufunguzi
wa barabara ya Igawa-Rujewa KM 9.8 iliyokamilika kujengwa kwa kiwango
cha lami. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro pamoja na
viongozi wengine wa Wilaya ya Mbarali.
Waziri
wa Ujenzi Dkt. John Magufuli akikata utepe kuashiria ufunguzi wa
barabara hiyo. Wengine katika picha ni Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas
Kandoro pamoja na viongozi wengine.
Waziri
wa Ujenzi Dkt. John Magufuli akizungumza na wakazi wa Ubaruku wilayani
Mbarali waliokuwa wanaomba wajengewe barabara ya Rujewa-Ubaruku kwa
kiwango cha lami.
Mkuu
wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro katikati akizungumza na Waziri wa Ujenzi
Dkt. John Magufuli kuhusu ujenzi wa barabara ya Rujewa-Ubaruku
inayotarajiwa kujengwa kwa kiwango cha lami. Barabara hiyo inatarajiwa
kuwarahisishia wakazi wa maeneo hayo ambao wengi wao ni wakulima wa
mpunga na mahindi.
Waziri
wa Ujenzi Dkt. John Magufuli akiwahutubia wakazi wa Rujewa na Ubaruku
wilayani Mbarali kuhusu ujenzi wa barabara ya Igawa-Ubaruku km 18.
Wakazi wa Rujewa na Ubaruku wakimsikiliza Waziri wa Ujenzi wakati akiwahutubia.
Waziri
wa Ujenzi Dkt. John Magufuli akifurahia ngoma pamoja na kikundi cha
ngoma za asili cha Rujewa mara baada ya kuwahutubia wakazi wa Rujewa na
Ubaruku wilayani Mbarali.
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro akiwahutubia wakazi wa Ubaruku na Rujewa Wilayani Mbarali.
Mtendaji
Mkuu wa Wakala wa barabara nchini TANROADS Eng. Patrick Mfugale akisoma
taarifa ya mradi wa barabara ya Igawa-Ubaruku inayojengwa kwa kiwango
cha lami.
Waziri
wa Ujenzi Dkt. John Magufuli akiagana na wakazi wa Rujewa na Ubaruku
mara baada ya kuhutubia mkutano wa hadhara.Picha zote na Kitengo cha
Mawasiliano Serikalini-Wizara ya Ujenzi.