PPF KUWAFIKISHA WAAJIRI MAHAKAMANI

October 02, 2014
NA MWANDISHI WETU,TANGA.
MFUKO wa pensheni wa PPF umesema utawafikisha mahakamani waajiri ambao hawapeleki michango kwa wakati kwani hali hiyo inasababisha usumbufu kwa wateja wao.
Kauli hiyo imetolewa hivi karibuni na Meneja wa Kanda ya Kinondoni, Tanga na Pwani, Zahara Kayugwa wakati wa semina ya waajiri wa sekta mbalimbali jijini hapa.
Alisema hatua hiyo inaweza kusaidia waajiri kufikisha michango ya wafanyakazi wao kwa wakati.
“Kwa kweli inatubidi tuchukue hatua, kwa sababu unakuta mfanyakazi anakuja kudai mafao halafu mwajiri amechangia asilimia tano tu, sasa wateja wanatuona kama sisi ni wababaishaji… hatutawavumilia tena," alisema Kayugwa.
Aidha, akifungua semina hiyo Katibu Tawala Mkoa wa Tanga, Salim Chima, alisema Serikali inatambua na kuthamini mchango wa sekta ya hifadhi ya jamii nchini, hasa katika suala zima la kukuza na kuimarisha uchumi.

KAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA NCHINI TANZANIA AFUNGA RASMI MAFUNZO YA ULINZI WA AMANI KWA MAAFISA MAGEREZA TOKA NCHI ZA SADC, MKOANI KILIMANJARO

KAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA NCHINI TANZANIA AFUNGA RASMI MAFUNZO YA ULINZI WA AMANI KWA MAAFISA MAGEREZA TOKA NCHI ZA SADC, MKOANI KILIMANJARO

October 02, 2014

imageKamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja(katikati meza Kuu) akisikiliza maelezo mafupi toka kwa Mratibu wa Mafunzo ya Ulinzi wa Amani, Kanali Sambulo Ndrovu(hayupo pichani) kabla ya kufunga rasmi Mafunzo hayo leo Oktoba 02, 2014. Mafunzo hayo yamefanyika kwa wiki mbili katika Chuo cha Maafisa Uhamiaji, Moshi Mkoani Kilimanjaro(wa pili kushoto) ni Mkuu wa Kituo cha Mafunzo cha SADC, Bregedia Jenerali Christopher Chellah(wa pili kulia) ni Mratibu Msaidizi wa Mafunzo hayo Kamishna Msaidizi wa Magereza toka Nchini Zimbabwe, Didmas Chimvura(wa kwanza kulia) ni Mkuu wa Magereza Mkoani Kilimanjaro, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, Venant Kayombo. image_1Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza Tanzania, John Casmir Minja akitoa hotuba fupi ya ufungaji wa Mafunzo ya Ulinzi wa Amani ambayo yamefanyika kwa wiki mbili katika Chuo cha Maafisa Uhamiaji, Moshi Mkoani Kilimanjaro ambapo jumla ya Maafisa Magereza 27 toka Nchi za SADC ikiwemo Tanzania, Botswana, Afrika Kusini, Mauritius, Swaziland na Zimbabwe wameshiriki kikamilifu Mafunzo hayo.
image_2Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja akikabidhi cheti kwa Mmoja wa Washiriki wa Mafunzo ya Ulinzi wa Amani, Mkaguzi Msaidizi wa Magereza Nchini Tanzania, Pendo Kazumba. Mafunzo hayo yamefanyika kwa wiki mbili na yameendeshwa na Kituo cha Mafunzo cha SADC kwa kushirikiana na Jeshi la Magereza Tanzania(kushoto) ni Mkuu wa Kituo cha Mafunzo cha SADC Bregedia Jenerali Christopher Chellah. image_3 
Wakufunzi wa Mafunzo hayo wakisikiliza hotuba fupi ya ufungaji wa Mafunzo ya Ulinzi wa Amani kwa Maafisa Magereza toka Nchi za SADC. Jumla ya Wahitimu 27 toka Nchi za SADC wameshiriki Mafunzo hayo kikamilifu katika Chuo cha Uhamiaji, Moshi Mkoani Kilimanjaro(wa kwanza kulia) ni Mratibu wa Mafunzo hayo, Kanali Sambulo Ndlovu toka Zimbabwe(wa pili kulia) ni Mkufunzi toka Tanzania, Kamishna Msaidizi wa Magereza, Charles Novart(wa tatu kushoto) ni Mkufunzi toka Tanzania, Ahmad Mwidadi(wa pili kulia) ni Mkufunzi toka Zambia, Mrakibu wa Polisi Nchini Zambia, Edward Njovu.
image_4 
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza Tanzania, John Casmir Minja akifanya mahojiano Maalum na Waandishi wa Habari toka Vyombo vya TBC1 na ITV Mkoani Kilimanjaro mara tu baada ya kufunga rasmi Mafunzo ya Ulinzi wa Amani kwa Maafisa Magereza toka Nchi za SADC leo Oktoba 2, 2014 Chuo cha Maafisa Uhamiaji, Moshi Mkoani Kilimanjaro. image_5 
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza Nchini Tanzania, John Casmir Minja(wa sita kushoto) na Mkuu wa Kituo cha Mafunzo cha SADC, Bregedia Jenerali Christopher Chellah(wa tano kulia) wakiwa katika picha ya pamoja na Maafisa Magereza Wanawake toka Nchi za SADC ambao wameshiriki kikamilifu Mafunzo ya wiki mbili ya Ulinzi wa Amani katika Chuo cha Maafisa Uhamiaji, Moshi Mkoani Kilimanjaro. image_6 
Mkuu wa Kituo cha Mafunzo cha SADC, Bregedia Jenerali Christopher Chellah(kushoto) akiteta jambo na Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini Tanzania, John Casmir Minja(kulia) mara tu baada ya kufunga rasmi Mafunzo ya Ulinzi wa Amani kwa Maafisa Magereza toka Nchi za SADC(katikati) ni Mmoja wa Washiriki wa Mafunzo hayo toka Nchini Tanzania, Mkaguzi Msaidizi wa Magereza, Pendo Kazumba.

KINANA AUNGURUMA PANGANI,TANGA

October 02, 2014

 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akihutubia katika mkutano wa hadhara katika Kata ya Mwera, wilayani Pangani, wakati wa ziara ya kuimarisha uhai wa chama, kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya 2010 mkoani Tanga.Kinana ameziagiza wizara ya Maliasili na Utalii na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kutatua haraka migogoro ya ardhi nchini.
Sehemu ya umati wa wananchi ukiwa kwenye mkutano wa hadhara uliohutubiwa na Kinana
Kinana akilakiwa na wananchi katika Kiji cha Mkalamo, wilayani Pangani ambapo alizindua mradi wa maji.
Wanananchi wa Kata ya Mkaramo wakipata huduma katika kisima kipya cha maji kilichozinduliwa na Kinana.
Kinana akihutubia katika hafla ya uzinduzi wa kisima cha maji katika Kata ya Mkaramo, wilayani Pangani
Kinana akifungua maji kwenye bomba wakati wa uzinduzi wa kisima cha maji katika Kata ya Mkaramo
Kinana akizungumza jambo na mama baada ya kumtwisha ndoo ya maji wakati wa uzinduzi wa kisima cha maji katika Kata ya Mkaramo
Kinana akishiriki kuchimba mtaro wa kuweka mabomba wakati wa uzinduzi wa kisima cha maji
Watoto wakichangamkia kuteka maji katika kisima hicho
Kinana akibeba tofali baada ya kufyatua aliposhiriki ujenzi wa tawi la CC, Kata ya Mkwaja, Pangani
Popooo zikiwa zimeanikwa ambapo Kinana alishiriki kubangua katika Kijiji cha Mseko, KKata ya Bungaa, wilayani Pangani.
Kinana akishiriki kubangua popoo katika Kijiji cha Mseko, wilayani Pangani.
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye aqkishiriki kubangua popoo katika Kijiji cha Mseko, wilayani Pangani, Tanga.
WanaCCM wakitumbuiza kwa nyimbo wakati Kinana alipowasili katika Kijiji cha Mseko, kushiriki ujenzi wa jengo la Tawi la Mseko, Kata ya Bumbaa
Kinana akishiriki kuweka dirisha katika jengo la CCM Mseko
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye akihutubia katika mkutano wa hadhara katika Kata ya Mwera, wilayani Pangani
Mbunge wa Jimbo la Pangani, Salehe Pamba akielezea miradi mbalimbali iliyotekelezwa jimboni humo kwa kufuata Ilani ya Uchaguzi ya CCM
Kinana akihutubia katika mkutano wa hadhara katika Kata ya Mwera, wilayani Pangani.
PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG

RAIS KIKWETE AFUNGUA MAONYESHO YA KIMATAIFA YA UTALII JIJINI DAR LEO

October 02, 2014
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akishirikiana na viongozi mbali mbali kukata utepe ikiwa ni ishara ya Ufunguzi wa Maonyesho ya Kimataifa ya Utalii "Swahili International Tourism Expo (SITE)" kwenye Ukumbi wa Mlimani City,Jijini Dar es Salaam leo Oktoba 2,2014.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia wakati wa Ufunguzi wa Maonyesho ya Kimataifa ya Utalii "Swahili International Tourism Expo (SITE)" kwenye Ukumbi wa Mlimani City,Jijini Dar es Salaam leo Oktoba 2,2014.Picha zote na Othman Michuzi.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Maimuna Tarishi akitoa hotuba fupi kabla ya kumkaribisha Mgeni Rasmi,Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete kuja kufungua Maonyesho ya Kimataifa ya Utalii "Swahili International Tourism Expo (SITE)" kwenye Ukumbi wa Mlimani City,Jijini Dar es Salaam leo Oktoba 2,2014.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Bodi ya Utalii Tanzania,Balozi Charles Sanga akitoa hotuba yake wakati wa Ufunguzi wa Maonyesho ya Kimataifa ya Utalii "Swahili International Tourism Expo (SITE)" kwenye Ukumbi wa Mlimani City,Jijini Dar es Salaam leo Oktoba 2,2014.

Meza Kuu.

Sehemu ya Wageni kutoka nchi mbali mbali wakifatilia kwa makini hotuba ya Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete wakati wa Ufunguzi wa Maonyesho ya Kimataifa ya Utalii "Swahili International Tourism Expo (SITE)" kwenye Ukumbi wa Mlimani City,Jijini Dar es Salaam leo Oktoba 2,2014.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiangalia namna mahindi yanavyosagwa na kupatikana ungwa wakati alipotembelea Banda la Maonyesho ya Utalii la Burundi,kwenye Maonyesho ya Kimataifa ya Utalii "Swahili International Tourism Expo (SITE)" kwenye Ukumbi wa Mlimani City,Jijini Dar es Salaam leo Oktoba 2,2014.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akifurahia ngoma ya utamaduni ya Taifa la Burundi alipotembelea Banda la Maonyesho ya Utalii la Burundi,kwenye Maonyesho ya Kimataifa ya Utalii "Swahili International Tourism Expo (SITE)" kwenye Ukumbi wa Mlimani City,Jijini Dar es Salaam leo Oktoba 2,2014.

Mwanadada Mwenye asili ya Burundi akiwa Kabeba kikapu tayari kwa kumzawadia Mh. Rais.

Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akikifurahia Kibuyu kikubwa alichokikuta kwenye Banda la Utalii la Burundi.

Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na Mkurugenzi wa kanda ya Afrika wa Utalii nchini Afrika Kusini,Bi. Evelyn Mahlaba (nywele nyeupe) wakati wa Maonyesho ya Kimataifa ya Utalii "Swahili International Tourism Expo (SITE)" kwenye Ukumbi wa Mlimani City,Jijini Dar es Salaam leo Oktoba 2,2014.


Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akipata maenezo ya namna ya kutumia kadi ya Benk ya CRDB kwenye huduma mbali mbali kupitia mashine maalum (Creadit Card Machine) kutoka kwa Meneja wa Huduma hiyo,Yusto Bituro (kushoto),wakati wa Maonyesho ya Kimataifa ya Utalii "Swahili International Tourism Expo (SITE)" kwenye Ukumbi wa Mlimani City,Jijini Dar es Salaam leo Oktoba 2,2014.

Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akipata maelezo ya Utalii kutoka kwa Afisa Uhusiano wa Bodi ya Utalii Tanzania,Geofrey Tengeneza.