NJOMBE YAONGOZA KWA USAFI WA MAZINGIRA ,MOSHI CHALI.

July 13, 2016

 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akizungumza katika hafla ya kukabidhi tuzo kwa watu waliofanya vizuri katika usafi wa Mazingira leo jijini Dar es Salaam.
 Katibu Mkuu wa Wizara Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Ulisubisya Mpoki akizungumza juu ya Wizara ilivyojipanga katika suala la usafi wa mazingira katika ya kukabidhi tuzo kwa watu waliofanya vizuri katika usafi wa Mazingira leo jijini Dar es Salaam.
  Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,Ummy Mwalimu akikabidhi Ufunguo wa Gari kwa Mwenyekiti wa Halmshauri Njombe, Valentino Hongoli baada ya kuobuka mshindi wa jumla wa usafi wa mazingira katika kampeni ya usafi, Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.
 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,Ummy Mwalimu akifurahi na washindi walioshinda pikipiki katika kampeni ya usafi wa mazingira katika usafi wa mazingira katika hafla iliyofanyika leo.
Baadhi ya wafanyakazi wa Halmashauri ya Njombe wakiwa katika picha ya pamoja na gari waliloshinda katika usafi wa mazingira katika hafla iliyofanyika leo.
(Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii)
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.
HALMASHAURI ya Wilaya ya Njombe imeibuka kuwa mshindi wa Jumla wa usafi wa mazingira na kuifuta historia ya usafi wa mazingira Halmashari ya Moshi kwa kushika.

Halmashauri ya Njombe imepata asilimia 97 ya usafi wa  mazingira na kufuatia Halmashauri ya Iringa Mjini kwa asilimia 81.1 .

Akizungumza leo wakati wa kutoa tuzo kwa halmashauri ,Manispaa, Majiji, Miji  pamoja na Vijiji ,Waziri Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu amesema kuwa Halmashauri ya Njombe haijaripoti hata mgonjwa wa kipindupindu hata mmoja tangu ugonjwa huo ulipotiwe Agasti mwaka jana.

Amesema kuwa Halmashauri hiyo imeweza kuwa na vyoo bora kwa asilimia 95 katika vijiji yake pamoja na kuwa viaa vya kunawia mikono katika vyoo hivyo.

Halmashauri ya Njombe imepata tuzo ya gari aina ya Land Cruiser Hardtop, Kombe, Cheti,pamoja pikipiki katika vijiji vitatu ambavyo vimefanya vizuri katika suala la usafi wa mazingira.
Jiji la Mbeya limeweza kuibuka mshindi  wa kwanza katika majiji kati ya majjiji manne kutokana na kufanya usafi wa mazingira kwa kuweka mifumo ya uhifadhi takataka.

Tuzo ya jijji la Mbeya  ni kikombe ,pikipiki pamoja na cheti huku Halmshauri ya Mji mdogo wa Tundunduma nao ukiibuka kuwa mshindi wa usafi wa mazingira kwa upande wa miji.

Halmashauri zingine zilizopa tuzo hizo ni Kahama,Mpanda ,Kondoa  huku Mkoa wa Dar es Salaam ikimbulia Wilaya Moja ya Kinondoni ambapo zimetunikiwa tuzo ya vikombe, pikipiki pamoja na vyeti.

Kwa upande wa Hospitali za Rufaa iliyoongoza ni  Mount Meru ikifuatia na Hospitali ya Amani katika nafasi ya pili huku Hospitali ya Morogoro ikishika nafasi  ya tatu.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema katika mashindano yajayo walioshinda watakuja kuishangilia Dar es Salaam na hawataondoka na vikombe hivyo na gari.

Amesema kuwa kuna jitihada ambazo zinafanyika za kuhakisha jiji la Dar es Salaam linakuwa safi na hatavumiliwa mtu ambaye anachafua mazingira.

RAIS DKT. MAGUFULI AZINDUA MPANGO WA UGAWAJI WA MADAWAJI KWA MAJIMBO MBALIMBALI NCHINI

July 13, 2016
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson akimuonesha Rais Dkt. John Pombe Magufuli sehemu ya Madawati yaliyotengenezwa na fedha zilizopatikana kutokana na kubana matumizi kutoka Ofisi ya Bunge katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikagua Madawati hayo yaliyotengenezwa na Jeshi la Magereza pamoja na Suma JKT.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa amekaa kwenye moja ya Dawati katika hafla hiyo fupi ya ugawaji wa Madawati hayo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Mwanafunzi wa darasa la tano katika shule ya Msingi Bunge George Samwel wakati akiangalia mfano wa darasa ya jinsi madawati hayo yatakavyo katika katika shule mbalimbali nchini.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo na Wanafunzi wa Shule ya Msingi Bunge wakwanza kulia Mariam Elias (darasa la tatu na wapili kutoka kushoto George Samwel mwanafunzi wa darasa la tano wakiwa wanapiga makofi kabla ya tukio la ugawaji wa madawati hayo yaliyotokana na kubana matumizi kutoka Ofisi ya Bunge.
Mwanafunzi wa darasa la tano katika shule ya Msingi Bunge George Samwel akimtajia Mheshimiwa Rais Jina la Waziri Mkuu Kassim Majaliwa mara baada ya kumuuliza huku Waziri Mkuu akitazama kwa furaha.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi Mbunge wa Ilala Mussa Azzan Zungu ambaye aliyapokea kwa niaba ya Wabunge wa majimbo mbalimbali nchini.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Kamati ndogo ya Tume ya huduma za Bunge inayoshughulika utengenezaji wa madawati. Waliosimama mbele ni Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Mbunge wa Iringa Mjini Mchungaji Peter Msigwa, Naibu Spika wa Bunge Dkt. Tulia Ackson, Mbunge wa Ilala Mussa Azan Zungu pamoja na Waziri wa Ulinzi Dkt. Hussein Mwinyi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Wanafunzi wa Shule ya msingi Bunge mara baada ya tukio la kukabidhi madawati katika Majimbo mbalimbali nchini. Wengine katika picha ni Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Naibu Spika Dkt. Tulia Ackson pamoja na Waziri wa Elimu Prof. Joyce Ndalichako.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwasalimia baadhi ya Maaskari brass bendi ya Jeshi la Magereza mara baada ya kukabidhi Madawati.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwasalimia baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Msingi Bunge katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Mwanafunzi wa Darasa la tatu katika Shule ya Msingi Bunge Mariam Samwel wakati akiondoka kwenye viwanja hivyo.
Sehemu ya Madawati yaliyokabidhiwa leo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mbunge wa Iringa Mjini Mchungaji Peter Msigwa aliyehudhuria hafla hiyo ya ugawaji wa Madawati katika Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU.
KENYA YAFUTA ZIARA TANZANIA

KENYA YAFUTA ZIARA TANZANIA

July 13, 2016
Timu ya Vijana ya Kenya, imefuta ziara yake ya kwenda Dar es Salaam kwa ajili kucheza mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya vijana wa Tanzania wenye umri wa chini ya miaka 17 maarufu kwa jina la Serengeti Boys.

Mchezo huo ulipangwa kufanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam Julai 23, 2016.


Kwa mujibu wa barua kutoka kwa Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Kenya (FKF), Robert Muthomi kwenda Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), kufuta kwa ziara hiyo kunatokana na nafasi ambayo Kenya imeipata.

Timu ya Taifa ya Vijana ya Kenya imeteuliwa kushiriki michuano ya Shirikisho la Mpira wa Miguu la COSAFA inayotarajiwa kuanza Julai 22, 2016 hadi Julai 31, 2016 mara baada ya Msumbiji kujitoa kwenye mashindano hayo.

“Tunaomba kukutarifu kuwa timu yetu imetuliwa katika michuano ya vijana ya COSAFA, hivyo ziara yetu Tanzania haitakuwako kama ambavyo sisi wenyewe tuliomba mchezo huo kwenu (TFF) ufanyike Julai 23, 2016,” ilisema sehemu ya barua hiyo iliyosainiwa na Muthomi.

Licha ya kwamba mchezo huo hautakuwako, ratiba ya Serengeti Boys ambayo inapambana kuwania nafasi ya kucheza Kombe la Mataifa Afrika hapo mwakani, imebaki vilevile kwa timu kuingia kambini Jumapili Julai 17, 2016 kwenye Hosteli za TFF zilizoko Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Ilala jijini Dar es Salaam.

Timu hiyo inayonolewa na Bakari Shime itapiga kambi ya wiki moja katika hosteli hizo, kabla ya kwenda Madagascar ambako itapiga kambi ya takribani wiki mbili ikiwa ni ahadi ya Rais wa TFF, Jamal Malinzi ambaye alitoa ofa hiyo baada ya kuwatoa Shelisheli kwa jumla ya mabao 9-0 katika mechi zake mbili za kimataifa.

Serengeti Boys inatarajiwa kucheza na Afrika Kusini kati ya Agosti 5, 6 au 7, 2016 huko Afrika Kusini kabla ya mchezo wa marudiano utakaofanyika saa 9.00 alasiri, Agosti 14, 2016 kwenye  Uwanja wa Azam Complex, ulioko Chamazi, Dar es Salaam.

Mshindi wa jumla katika michezo hiyo, itacheza na timu mshindi kati ya Namibia na Congo-Brazaville.
FERWAFA YAAHIRISHA MCHEZO KATI YA RWANDA, TANZANIA

FERWAFA YAAHIRISHA MCHEZO KATI YA RWANDA, TANZANIA

July 13, 2016

Shirikisho la Mpira wa Miguu Rwanda (FERWAFA), limeahirisha mchezo wa kirafiki wa kimataifa kati ya timu ya taifa ya wanawake ya Rwanda dhidi ya wageni, Tanzania ‘Twiga Stars’ uliokuwa ufanyike Jumapili Julai 17, 2016.

Mchezo huo uliandaliwa na FERWAFA na Rais Paul Kagame alipendekeza mchezo huo kuwa sehemu ya burudani kwa wakuu mbalimbali wa nchi za Afrika wanaotarajiwa kuwa na mkutano wa viongozi hao kuanzia kesho Julai 14, 2016.


Kwa mujibu wa barua ya Rais wa FERWAFA, Nzamwita Vincent ya Julai 12, 2016 kwenda Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), sababu za kuahirisha mchezo huo ni ratiba ya mkutano huo wa 27 wa wakuu nchi.
“Tunasikitika kuwataarifu kuwa ile ratiba ya kuwa na mchezo wa kirafiki kati ya Rwanda na Tanzania, imefutwa. Tunaomba radhi kwa taarifa hii ya ghafla ambayo iko nje ya uwezo wetu inayowafikia huku tukijua kwamba mlikuwa tayari mmeandaa timu kwa ajili ya mchezo,” ilisema sehemu ya barua hiyo.

“Hata hivyo tunaahidi kuendelea kufanya mawasiliano ili kupanga tarehe nyingine ya kufanyika mchezo huo,” ilisisitiza barua.
Taarifa hiyo imekuja wakati tayari Twiga Stars ilikuwa imeanza maandalizi ya kutosha kwa mchezo huo ambao ulianza kuvutia mamia ya mashabiki wa mpira wa miguu wan chi za Afrika Mashariki.

Shirikisho la Mpira wa Miguu Rwanda (FERWAFA), limeahirisha mchezo wa kirafiki wa kimataifa kati ya timu za wanawake za Tanzania ‘Twiga Stars’ na wenyeji Rwanda uliokuwa ufanyike Jumapili Julai 17, 2016.

Mchezo huo uliandaliwa na FERWAFA na Rais Paul Kagame alipendekeza mchezo huo kuwa sehemu ya burudani kwa wakuu mbalimbali wa nchi za Afrika wanaotarajiwa kuwa na mkutano wa viongozi hao kuanzia kesho Julai 14, 2016.

Kwa mujibu wa barua ya Rais wa FERWAFA, Nzamwita Vincent ya Julai 12, 2016 kwenda kwa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), sababu za kuahirisha mchezo huo ni kuingiliana kwa ratiba ya mkutano huo wa 27 wa wakuu nchi za Afrika.

“Tunasikitika kuwataarifu kuwa ile ratiba ya kuwa na mchezo wa kirafiki kati ya Rwanda na Tanzania, imefutwa. Tunaomba radhi kwa taarifa hii ya ghafla ambayo iko nje ya uwezo wetu inayowafikia huku tukijua kwamba mlikuwa tayari mmeandaa timu kwa ajili ya mchezo,” ilisema sehemu ya barua hiyo.

“Hata hivyo tunaahidi kuendelea kufanya mawasiliano ili kupanga tarehe nyingine ya kufanyika mchezo huo,” ilisisitiza barua iliyosainiwa na Nzamwita Vincent.

Taarifa hiyo imekuja wakati tayari Twiga Stars ilikuwa imeanza maandalizi ya kutosha kwa mchezo huo ulioanza kuvutia mamia ya mashabiki wa mpira wa miguu wa ncza Afrika Mashariki na kati.

MKUU WA MKOA WA MWANZA ATOA MAAGIZO UJENZI WA DARAJA LA WATEMBEA KWA MIGUU FURAHISHA PAMOJA NA UPANUZI WA BARABARA YA AIRPORT JIJINI MWANZA.

July 13, 2016
Mwonekano wa barabara ya Airport Jijini Mwanza, katika eneo la Furahisha ambapo upanuzi wa barabara unafanyika hadi eneo la Pasiansi.
Na BMG
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella, akitoa maelekezo kwa wasimamizi na wahandisi wa Miradi ya Ujenzi wa daraja la watembea kwa miguu katika eneo la Furahisha Jijini Mwanza pamoja na upanuzi wa barabara ya Airport kuanzia eneo la Furahisha hadi Pasiansi.
Mhandisi Mushubila Kamuhabwa, kutoka Tanroads mkoa wa Mwanza, akitoa ufafanuzi kwa wanahabari juu ya utekelezaji wa miradi hiyo.
Meneja wa Kampuni ya Nyanza Road Works, Ahabyoona Golbert, akitoa ufafanuzi kwa wanahabari juu ya utekelezaji wa miradi hiyo.
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka mkoani Mwanza, Mhandisi Antony Sanga, akitoa ufafanuzi kwa wanahabari kuhusu uondoaji wa miundombinu ya maji ili kupisha miradi ya ujenzi kuendelea.
Mmoja wa wakazi wa Jiji la Mwanza, akielezea furaha yake juu ya upanuzi wa barabara ya Airport pamoja na ujenzi wa daraja la watembea kwa miguu katika eneo la Furahisha
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella (mwenye nguo nyekundu), akipokea maelezo ya ujenzi wa daraja la watembea kwa miguu katika eneo la Furahisha Jijini Mwanza.
Ukaguzi katika upanuzi wa barabara ya Airport katika eneo la Furahisha ukiendelea
Utandikaji wa miundombinu ya maji ukiendelea

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella, ameagiza utekelezaji wa miradi ya ujenzi wa daraja la watembea kwa miguu pamoja na upanuzi wa barabara ya Airport kuanzia eneo la Furahisha hadi Pasiansi jijini Mwanza, kukamilika kwa wakati.

Mongella ametoa agizo hilo hii leo, alipofanya ziara ya kukagua utekelezaji wa ujenzi wa miradi hiyo baada ya awali kuwepo kwa changamoto kadhaa ikiwemo miradi kusimama kwa muda ili kupisha uondoaji wa miundombinu mbalimbali barabarani ikiwemo ya maji, umeme pamoja na simu.

Akiwa eneo la ujenzi wa daraja la watembea kwa miguu, Mongella alielezwa kwamba ujenzi wake umekuwa ukisimama kwa muda kutokana na baadhi ya vifaa ikiwemo vyuma vya daraja ambavyo vimeagizwa nchini Uchina kuchelewa kuwasili.

Zoezi la uondoaji wa miundombinu mbalimbali katika eneo la miradi bado linaendelea ili kuruhusu utekelezaji wa miradi hiyo kukamilika kwa wakati, kama anavyobainisha Mhandisi Antony Sanga ambae ni Mkurugenzi wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Mkoani Mwanza, Mwauasa.

Pamoja na changamoto hizo, Mhandisi Mushubila Kamuhabwa ambae ni Mhandisi Mshauri wa miradi hiyo kutoka Wakala wa Barabara Tanroads Mkoa wa Mwanza, amesema kwamba miradi hiyo itakamilika kwa wakati.

Ujenzi wa daraja la watembea kwa miguu katika eneo la Furahisha, unatekelezwa na Kampuni ya Nyanza  Road Works kwa zaidi ya shilingi bilioni nne ikiwa ni fedha kutoka Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi ambapo Meneja wa kampuni hiyo, Ahabyoona Gilbert, ameahidi kukamilisha kwa wakati ujenzi wake ambao ni hadi kufikia Novemba 26 mwaka huu.

Pia ameahidi kukamilisha kwa wakati upanuzi wa barabara ya Arport kuanzia eneo la Furahisha hadi Pasiansi kwa umbali wa Kilomita mbili ambapo upanuzi huo unagharimu kiasi cha shilingi shilingi bilioni mbili ambazo ni fedha zilizopatikana baada ya Rais Dkt.John Pombe Magufuli kufuta sherehe za Muungani wa Tanganyika na Zanzibar mwaka huu.

Kukamilika kwa upanuzi wa barabara ya Airport kutoka njia mbili hadi nne, kunaelezwa kuleta neema kwa wakazi wa Jiji la Mwanza, ikiwemo kuondokana na msongamano wa magari barabarani. 
Bonyeza HAPA Kusikiliza. Au Bonyeza Hapa chini

KIWANDA CHA CHUMA CHA MMI STEEL CHA MIKOCHENI JIJINI DAR ES SALAAM CHATOZWA FAINI YA SHILINGI MILIONI 10

July 13, 2016
 Naibu Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh. Luhaga Mpina akisaini kitabu cha wageni muda mfupi baada ya kuwasili katika Ofisi ya Serikali ya mtaa wa (TPDC) alipofanya ziara Mapema hii leo.     
 Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Raisi Muungano na Mazingira Mh. Luhaga Mpina akisikiliza maelezo kutoka kwa mwenyekiti wa serikali za mtaa  wa (TPDC)Bw, Idrisa Hashimu kuhusu Uchafuzi wa Mazingira Unaofanywa na viwanda katika mtaa huo.
 .Naibu Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Raisi Muungano na Mazingira Mh.Luhaga Mpina akiwa katika ukaguzi wa Mazingira katika kiwanda cha MMI steel kinachotuhumiwa Kuchafua mazingira katika mtaa wa TPDC
                   EVELYN MKOKOI,DAR ES SALAAM

Kiwanda cha kutengeneza vyuma cha MMI Steel kilichopo katika eneo la viwanda mikocheni jijini Dar es Salaam, kimetozwa faini ya shilingi milioni kumi na kutakiwa kulipa faini hiyo baada ya siku saba kwa kosa la kukiuka sheria ya mazingira na kanuni zake ya mwaka 2004, kwa kutiririsha maji machafu katika maeneo ya mtaa wa TPDC kwa warioba jijini dar es salaa. Maji ambayo ni hatari kwa mazingira na viumbe hai.
Adhabu hiyo imetolewa na Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina alipotembelea eneo la  mtaa wa viwanda mikocheni kufuatia uchafuzi wa mazingira unaotokanao na utitiririshaji wa majitaka katika maeneo hayo.
Wakati huohuo, Shirika la maji safi na majita taka Jijini Dar es Salaam na Pwani  ( Dawasco) limepewa siku kumi na saba kumaliza tatizo la utiririshaji wa maji taka katika mtaa wa TPDC mikocheni kwa Warioba jijini Dar es Salaam.
Maagizo hayo yametolewa na Naibu Waziri Mpina Baada ya kufanya usafi jumamosi ya mwisho wa mwezi wa tatu na kutoa siku saba kwa DAWASCO na NEMC kusimamia suala zima la usafi wa mazingira na agizo lake kuupuzwa.
Awali, Mhe. Mpina alisema kuwa uchafuzi wa mazingira hauwezi kuendelea kuvumiliwa na lazima hatua za kisheria zichukuliwe, na kuwaasa watendaji wa taasisi za serikali kuyapa kipaumbele maagizo yanayotolewa na viongozi wa ngazi za juu za serikali kinyume na hapo ni kutokutii mamlaka. “tasisi za serikali lazima zifanye kazi kwa kushirikiana kutokana na kwamba kumekuwa na kutupiana mpira kati ya NEMC, dawasco na Manispaa ya kinondoni katika suala zima la utatuzi wa uchafuzi wa mazingira katika mtaa wa TPDC.” Alisema.
Naibu waziri Mpina aliongeza kuwa  ifikapo tarehe 30/7/2016  asikutane tena na tatizo la uchafu na harufu mbaya katika mtaa wa TPDC kwani hali hiyo ni hatari sana kwa afya ya wakazi wa maeneo hayo na mazingira.
Kwa upande wake DAWASCO ikiwakilishwa na Injinia Erick Jackson alisema kuwa Tangu muheshimiwa Naibu Waziri Mpina atoe agizo la uondoshwaji wa majitaka na uboreshwaji wa miundombinu katika mtaa huo, wamekuwa wakifanya kazi na bado inaendelea na kazi hiyo pamoja na kukabiliwa na changamoto mbalimbali za kifedha na ufundi.
Hata hivyo uongozi wa Halmashauri ya wilaya ya kinondoni umelishitaki shirika la maji safi na maji taka jijini dar es salaam na Pwani DAWASCO ,kiwanda cha MMI steel na Tembo Tiles kwa uchafusi wa mazingira kwa kutirirsha maji taka.
RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA DKT. JOHN POMBE MAGUFULI AKABIDHIWA MADAWATI YA AWAMU YA KWANZA YALIYOTENGENEZWA NA JESHI LA MAGEREZA NA JKT KUTOKANA NA FEDHA ZILIZOTOLEWA NA BUNGE BAADA YA KUBANA MATUMIZI JULAY 13,2016

RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA DKT. JOHN POMBE MAGUFULI AKABIDHIWA MADAWATI YA AWAMU YA KWANZA YALIYOTENGENEZWA NA JESHI LA MAGEREZA NA JKT KUTOKANA NA FEDHA ZILIZOTOLEWA NA BUNGE BAADA YA KUBANA MATUMIZI JULAY 13,2016

July 13, 2016

wncjjvmkmvRais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Kamati ndogo ya Tume ya huduma za Bunge inayoshughulika utengenezaji wa madawati. Waliosimama mbele ni Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Mbunge wa Iringa Mjini Mchungaji Peter Msigwa, Naibu Spika wa Bunge Dkt. Tulia Ackson, Mbunge wa Ilala Mussa Azan Zungu pamoja na Waziri wa Ulinzi Dkt. Hussein Mwinyi, Julay 13,2016 (PICHA ZAIDI ZINAFATA)
WAZAZI WATAKIWA KUWA MAKINI NA MARAFIKI WA WATOTO WAO

WAZAZI WATAKIWA KUWA MAKINI NA MARAFIKI WA WATOTO WAO

July 13, 2016

Kutokana na baadhi ya watoto kuwa na tabia ambazo hazipendezi watu bila ya kufahamu chanzo chake, imeelezwa kuwa ni vyema wazazi wakajenga mazoea ya kuwafahamu watu ambao wanakuwa karibu na watoto wao ili kuchukua hatua mapema.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Shule ya Watoto ya O'Jays Kiddies Zone, Usia Nkhoma Ledama wakati wa mahali ya nne ya shule hiyo ambapo watoto wa ngazi mbalimbali za madarasa walihitimu.

Usia alisema kuwa wazazi wengi wamekuwa wakitumia muda wao mwingi kujishughulisha na kazi zao bila kuwa na muda wa kukutana na watoto wao na hivyo kuwa ngumu kutambua chanzo cha tabia ambazo zinaibuka kwa watoto wao kutokana na wao kutowafatilia watu ambao wanakuwa karibu na watoto.

"Tunafahamu wazazi wengi mnakuwa busy na kazi zao na hivyo mtoto akitoka shule anakuwa na dada au kuangalia tv lakini akiwa katika michezo na watoto wenzake mnakuwa hamjui ni vitu vya aina gani wanafanya,

"Nadhani ni vyema sasa kuhakikisha mnawafahamu marafiki wa watoto wenu, marafiki zao wa shuleni na marafiki zao wa nyumbani, huwezi kujua wanafanya nini kama huwafahamu tabia watoto wanaocheza nao lakini kama ukiwajua unakuwa unafahamu rafiki anayefaa ni yupi," alisema Usia.

Aidha aliwatoa hofu wazazi kuwa shuleni hapo wanawafundisha watoto tabia njema na wanawafahamu vyema wanafunzi wao hivyo kazi kubakia kwa wazazi kuhakikisha wanakuwa makini na watoto wanapokuwa nyumbani.
Mkurugenzi wa Shule ya Watoto ya O'Jays Kiddies Zone, Usia Nkhoma Ledama (kushoto) akizungumza na mmoja wa wazazi Bw. Ally Msoya alipowasili kwenye mahafali ya nne ya shule hiyo yaliyofanyika katika ukumbi wa Msasani Tower jijini Dar es Salaam.(Picha zote na Modewjiblog)

Kwa upande wa mgeni rasmi katika mahafali hayo, Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA, Eda Sanga aliwapongeza wanafunzi ambao wamehitimu masomo na wazazi kwa moyo wao wa kujitoa kuwasomesha watoto wao lakini pia kuwataka kuwasimamia vyema watoto wao ili waweze kufika mbali kielimu.

"Elimu ni muhimu sana kwa watoto wenu wanatakiwa kusoma ili kufika mbali kimaisha niwasihi kuwasimia vyema watoto ili wanapokuwa shuleni wafanye vizuri na wanaporudi nyumbani pia wafanye vizuri," alisema Eda.
Watoto ya O'Jays Kiddies Zone wakitoa burudani kwa wazazi kwenye mahafali ya nne ya shule hiyo.
Mhitimu wa darasa la Laurey, Thomas Mboya akiongoza watoto wenzake kwenye burudani maalum wakati wa mahafali ya nne ya shule hiyo.
Mwanafunzi wa Lilies Class, Iptihaj Kinyaga akiongoza darasa la wanafunzi wenzake kutoa burudani kwa wazazi kwenye mahafali hayo.
Wahitimu wa Laurel Class wakitoa burudani ya kuagana na wanafunzi wenzao katika mahafali ya nne ya shule hiyo.
Pichani juu na chini ni sehemu ya wazazi waliohudhuria mahafali hayo.
Bwana na Bibi Lugoe wazazi wa mhitimu Abigail Lugoe wakiwa meza kuu.
Wazazi wa Watoto ya O'Jays Kiddies Zone wakitazama burudani na vipaji mbalimbali vilivyokuzwa shuleni hapo kutoka kwa watoto wao.
Lantana Class wakitoa burudani kwenye mahafali ya kaka na dada zao
Mkurugenzi wa Shule ya Watoto ya O'Jays Kiddies Zone, Usia Nkhoma Ledama akizungumza machache kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi Mama Eda Sanga kutoa risala kwenye mahafali ya nne ya shule hiyo yaliyofanyika jana kwenye ukumbi wa Msasani Towers jijini Dar es Salaam.
Mgeni rasmi kwenye mahafali hayo, Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA, Eda Sanga akitoa nasaha kwa wazazi na walezi waliohudhuria mahafali ya nne ya darasa la Laurel Shule ya Watoto ya O'Jays Kiddies Zone yaliyofanyika katika ukumbi wa Msasani Towers jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya wazazi na walezi wakisikiliza nasaha za mgeni rasmi.
Wazazi maalum wa mtoto Abigail Lugoe, Bwana na Bibi Lugoe wakitoa shuhuda ya malezi bora na elimu aliyoipata mtoto wao ambaye mwakani atajiunga na darasa la kwanza. Kushoto ni Mkurugenzi wa Shule ya Watoto ya O'Jays Kiddies Zone, Usia Nkhoma Ledama.
Wazazi wakiendelea kushuhudia matukio mbalimbali yaliyojiri kwenye mahafali hayo.
Bw. Ally Msoya na familia yake.
Kutoka kushoto ni Victoria Martin, Thuwein Makamba na Husni Seif, LTE Specialist wa Tigo Tanzania katika mahafali shule ya Shule ya Watoto ya O'Jays Kiddies Zone.
Dada Faiza Ally akibadilishana mawazo na mmoja wa wazazi katika mahafali ya shule hiyo.
Mgeni rasmi Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA, Eda Sanga akimtunuku cheti, Joylyn Marandu mhitimu wa Laurel Class katika mahafali ya nne ya shule hiyo.
Wahitimu wakiendelea kutunikiwa vyeti.
Mhitimu Patrick Kasanga akipokea cheti chake. (Picha zaidi ingia hapa)
-- Zainul A. Mzige, Operation Manager, MO BLOG, www.modewjiblog.com +255714940992.