February 06, 2014

TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI

DSC00207 
MTU MMMOJA AUAWA MKOANI MBEYA KWA TUHUMA ZA WIZI.
MTU MMOJA AMBAYE HAKUWEZA KUFAHAMIKA JINA WALA MAKAZI YAKE, JINSI YA KIUME, UMRI KATI YA MIAKA 20 – 25 ALIUAWA KWA KUPIGWA SEHEMU MBALIMBALI ZA MWILI WAKE NA KUNDI LA WANANCHI WALIOAMUA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI WAKITUMIA SILAHA ZA JADI. TUKIO HILO LILITOKEA MAJIRA YA SAA 04:00HRS HUKO HALENGO JIJI NA MKOA WA MBEYA BAADA YA MAREHEMU KUTUHUMIWA KUIBA KUKU WAPATAO 15 MALI YA EPHRAIM PAUL (37) MKAZI WA NZOVWE.  KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA TABIA YA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA INA MADHARA MAKUBWA KATIKA JAMII.
MZEE WA MIAKA70 AUAWA HUKO KATIKA KIJIJI CHA MAGANJO.
MZEE MWENYE UMRI WA MIAKA 70 WENELA
SIBELA. MKAZI WA KIJIJI CHA MAGANJO ALIKUTWA AMEUAWA KWA KUKATWA SHOKA KICHWANI NA KISOGONI NA MTU/WATU WASIOFAHAMIKA NA KISHA MWILI WAKE KUTUPWA VICHAKANI. TUKIO HILO LILITOKEA MNAMO TAREHE 05.02.2014 MAJIRA YA SAA 11:00HRS ASUBUHI WILAYA YA MBEYA VIJIJINI WAKATI MAREHEMU AKIWA NJIANI, CHANZO CHA MAUAJI KINACHUNGUZWA. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA MTU/WATU WALIOHUSIKA NA TUKIO HILI AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI WAKAMATWE NA SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE.
February 06, 2014

NMB YAFUNGUA RASMI TAWI LA USA RIVER-ARUSHA

DSC_0401  
Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mhe. Nyerembe D. Munasa Sabi (kati) akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa tawi la NMB Usa River.Wakishuhudia kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Biashara kwa Wateja Wakubwa wa Benki ya NMB, Richard Makungwa pamoja na Meneja wa NMB Kanda ya Kaskazini, Vicky Bishubo . Hafla ya uzinduzi wa tawi hili la NMB Usa River umefanyika mwanzoni mwa wiki katika viwanja vya tawi hili mkoani Arusha.
DSC_0393 
Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mhe. Nyerembe D. Munasa Sabi akipata maelezo kutoka kwa Meneja wa Tawi la NMB Usa River Bernadetha Mmary mara baada ya kuzindua tawi na kulitembelea ndani.DSC_0580 
Sehemu ya wageni waalikwa waliohudhuria hafla ya uzinduzi huu wakifurahia ufunguzi wa tawi jipya la NMB Usa River
February 06, 2014

MAOFISA HABARI NA MAWASILIANO WATOA MSAADA KWA WAZEE WA KITUO CHA MWANZANGE, TANGA

Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Assah Mwambene, Meneja Mawasiliano wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mawasiliano Tanzania Innocent Mungy (mwenyeshati la mistari) na Mkurugenzi wa Idara ya Utamaduni toka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Hermas Mwansoko (katikati) wakimkabidhi  kiroba cha mchele  moja ya Wazee wa Kituo cha Mwanzange Mkoani Tanga, ikiwa ni sehemu ya msaada uliotolewa na Maafisa Habari na Mawasiliano wa Serikali katika kikao kazi kinachoendelea Mkoani humo.
Mkurugenzi wa Idara ya Utamaduni toka Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Prof. Hermas Mwansoko akimkabidhi Afisa Ustawi wa Jamii anayesimamia kituo hicho cha wazee Bi Otilia Daniel fedha za kununulia mahitaji mengine wakati wa ziara ya kutoa msaada katika kituo hicho leo Mkoani Tanga.
February 06, 2014

NGUMI ZA NELSON MANDELA OPEN CHAMPIONSHIP ZAFUNGULIWA KAWE LEO.

Bondia Fabian Gaudence kushoto akipambana na Hussein Mnimbo  wakati wa mashindani ya wazi ya Nelson Mandela  yabayofanyika katika Viwanja vya Tanganyika Packers Kawe  jijini Dar es salaamGaudence alishinda mpambano huo kwa pointi.
Bondia Rashidi Samvu kutoka Kigoma  kushoto  akioneshana umwamba wa kutupiana makonde naHafidhi Kassimu wa Ngome wakati wa mashindani ya wazi ya Nelson Mandela  yaofanyika katika Viwanja vya Tanganyika Packers Kawe  jijini Dar es salaam
February 06, 2014

BONGO MOVIE NI SHIDA:KAJALA NA JACK WOLPER WADAIWA KUGOMBEA MWANAUME MMOJA...KIDUME AFUNGUKA

Jack Wolper mwigizaji wa filamu Swahilihood
MSANII wa muziki wa kizazi kipya anayeunda kundi la Makomandoo Fredy Wayne ambaye alikuwa akitoka kimapenzi na Jacqueline Wolper amesema ameachana naye na sasa yupo na nyota mwingine wa filamu, Kajala Masanja. Akizungumza FC hivi karibuni, Fredy alisema msanii huyo amemchanganya mno kimapenzi kiasi kwamba ameamua kumwandikia wimbo unaitwa Ushaniroga, kuonyesha ni jinsi gani amedata naye.
February 06, 2014

MBUNGE MAARUFU WA CHADEMA SASA AIBUKA NA DVD ZA KUWACHANA LIVE VIONGOZI WAKUU WA CHAMA CHAKE LIVE!!

Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe.
WAKATI Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe, akijipanga kuanza ziara katika mikoa kadhaa nchini kujibu mapigo ya tuhuma dhidi yake zilizotolewa na baadhi ya viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kwenye ziara ya Operesheni M4C Pamoja Daima, mbunge huyo ameibuka na DVD inayowananga viongozi wa CHADEMA.

Vyanzo vyetu vya habari vilisema kuwa DVD hizo zitasambazwa kwenye mikoa na maeneo yote atakayofanya mikutano ya hadhara mbunge huyo, kama moja ya harakati na mikakati ya kujisafisha na tuhuma za usaliti zinazomkabili ndani ya chama.

 
Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili umebaini kuwa DVD hizo zinatengenezwa kwenye kampuni moja iliyopo eneo la Kariakoo ambayo imepewa tenda ya kuchapa nakala 10,000 na kampuni nyingine zaidi ya tatu, nazo zimepewa tenda ya kuchapa DVD hizo kwa idadi tofauti.

UKWASI WA GHAFLA WA KAJALA WAZUA GUMZO KUBWA JIJINI ... HUU HAPA UTAJIRI WAKE NA MATATNUZI ANAYOYAFANYA TANGU ATOKE JELA

UKWASI WA GHAFLA WA KAJALA WAZUA GUMZO KUBWA JIJINI ... HUU HAPA UTAJIRI WAKE NA MATATNUZI ANAYOYAFANYA TANGU ATOKE JELA

February 06, 2014
MIEZI tisa baada ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar kumhukumu staa wa filambu za Bongo, Kajala Masanja kifungo cha miaka mitatu jela au faini ya shilingi milioni 13 kwa kosa la utakatishaji fedha na Miss Tanzania 2006, Wema Sepetu kumlipia hivyo kuwa huru, hali ya maisha ya msanii huyo imebadilika ghafla na sasa ameibuka katika utajiri wenye maswali na majibu.

Chanzo makini kimeliambia gazeti hili kwamba, Kajala ambaye alitoka mahabusu ya Segerea jijini Dar, Machi 25, 2013 akiwa hana mbele wala nyuma kiasi cha kutia huruma, sasa anazikamata za kutosha kiasi cha watu wake wa karibu kumshangaa. 

MANUNUZI YAKE
Chanzo kimebainisha kuwa, Kajala ameagiza kutoka China kontena lenye urefu wa futi 20 likiwa limesheheni  samani za ndani. Samani za ndani ni fenicha mbalimbali.
 

“Hivi mnajua kwamba Kajala yuko juu. Naweza kusema ni tajiri kwa sasa, maisha yake ni poa. Hivi ninavyoongea kuna kontena la futi arobaini linakuja Dar, ndani mna samani tu,” kilisema chanzo hicho. 

AMWAGA MILIONI 90 KUTENGENEZA FILAMU
Katika hali inayoendelea kutafsiriwa kuwa ni kuzidi kuonesha ukwasi alionao, msanii huyo ameshatumia shilingi milioni 90 kwa ajili ya kutengeneza filamu zake tatu, kila moja ikitumia bajeti ya milioni 30 za Kibongo.
 

Filamu ya Kajala ambayo iko njiani kutoka inaitwa Laana. Inadaiwa mpango wake ni kutengeneza filamu 10 ambazo atakuwa akiziuza kwa nyodo. Kama ni hivyo atatumia shilingi milioni 300 kwa filamu hizo kumi. 

ATUMIA MILIONI 11 KUNUNUA VITO VYA THAMANI
Mbali na kuvaa magauni na viatu vya bei mbaya, hivi karibu staa huyo alitua Dar akitokea China ambapo alipigilia vito vya gharama ya maisha ya familia nzima.