NHC MWIKO KULEWA SIFA ZA MAFANIKIO

November 05, 2014



MKUU wa mkoa wa Tanga, Luteni (Mstaafu) Chiku Gallawa, amelitaka Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), lisilewa sifa wanazopewa kwa kufanya vizuri katika ujenzi wa nyumba za gharama nafuu, badala yake waongeze bidii na kuyataka mashirika mengine nchini yaige mpango kazi wake kujiletea maendeleo yake.

Akizungumza wakati akifunga baraza Kuu la wafanyakazi wa shirika hilo mwishoni mwa wiki, mkuu huyo wa mkoa alisema kwamba kasi ya kujiletea maendeleo ya shirika hilo kwa dira yake ya miaka mitano ni kubwa na kwamba watu mbalimbali wamekuwa wakilisifia kwa kazi nzuri akiwemo Rais Jakaya Kikwete.

Amesema kwamba kama mashirika mengine yaliyopo hapa nchini yangefanya kazi kwa kasi kama lilivyo shirika la NHC, Tanzania ingekuwa mbali katika mabadiliko ya kiuchumi hivyo akalipongeza shirika hilo liendelee kufanya kazi zake kwa vile Watanzania wamekuwa na mahitaji makubwa ya makazi.

Awali Mwenyekiti wa mkutano huo, Francis Chilambo akisoma maazimio ya mkutano huo wa siku mbili, alisema kwamba ili kuondokana na dhana ya kulewa sifa, wameadhimia kwamba kutokana na ujenzi wa nyumba za gharama nafuu kuwavutia wengi kiasi kwamba shirika hilo limekuwa kioo cha Watanzania, miradi yao yote itajengwa kwa ubora unaotakiwa.

Mwenyekiti huyo katika maadhimio hayo wamempongeza Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi Nyumba na Makazi, Alphayo Kidata kutokana na kuwa mstari wa mbele na kushirikiana na shirika hilo katika kuandaa mpango mkakati wa shirika hilo wa 2015 ikiwemo kupatikana kwa hati katika eneo la Tanganyika Packers lililopo Kawe Jijini Dar es salaam.

NEWS ALERT:Gari lapinduka wakati dereva akiwakimbia askari Polisi

November 05, 2014


Baadhi ya wakazi wa mji wa Moshi wakiangalia kwa mshangao gari aina ya Toyota Spacio, lenye namba za usajili, T111 BHW likiwa limepinduka chini juu mbele ya ofisi za TFA barabara ya Boma ,jirani kabisa na kipita shoto cha mnara wa saa ,Dereva wa gari hilo anadaiwa alikuwa akijaribu kuwakimbia askari wa kikosi cha barabarani kwa mwendo wa kasi kabla ya kugonga gari jingine na hatimaye kupinduka.hakuna aliepoteza maisha kwenye tukio hilo la ajali.
Picha na Dixon Busagaga wa Globu ya jamii kanda ya kaskazini VIA Michuzi Blog

MUWSA YASAMBAZA BOMBA ZA MAJI MRADI MKUBWA WA MAJI MTO KARANGA.

November 05, 2014


Mkurugenzi wa Mamlaka  ya Maji safi na Usafi wa Mazingira mjini Moshi (MUWSA) Mhandisi Cyprian Luhemeja (aliyevaa  suti nyeusi) akiwaongoza wanahabari kutembelea mradi mkubwa wa maji uliopo katika chemichemi ya Mto Karanga.
Meneja ufundi wa Mamlaka ya Maji safi na usafi wa Mazingira mjini Moshi,Mhandisi Patrick Kibasa akitoa maelezo kwa wanahabari kuhusu ujenzi wa kituo cha kutibu maji katika chanzo cha maji cha Mto Karanga.
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira mjini Moshi,MUWSA ,Mhandisi Cyprian Luhemeja akiwaonesha wanahabari chanzo cha maji kilichopo Mto Karanga .
Wanahabri wakipita juu ya Bomba zilizoanza kusambazwa kutoka katika chanzo cha maji cha Mto Karanga.
Bomba za kupitisha maji kutoka katika Chemichemi kando ya Mto Karanga zikiwa tayari zimesambazwa kwa eneo kubwa kwa ajili ya kupitisha maji kuelekea maeneo ya Pasua na kwingineko.
Moja ya kiungio cha bomba za maji za nchi 10 kwenda nchi 8 zilizosambazwa toka chanzo cha Chemi chemi ya Maji kando ya mto karanga
Sehemu ya kutolewa hewa katika maungio ya bomba za maji zinazosambazwa kutoka chanzo cha maji cha Mto Karanga.
Bomba la maji likiwa limepita kando ya Mto Karanga.
Maeneo mengine mafundi walilazimika kuchimba eneo kubwa ili mradi kwepa vipando katika maeneo ambayo Bomba hilo limepita.
Mafundi wakiendelea na kazi ya ujenzi katika maeneo ambayo bomba hilo limepita.
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji na usafi wa mazingira mjini Moshi (MUWSA) Mhandisi Cyprian Luhemeja akionesha eneo ambalo bomba zinazosambazwa kutoka chanzo cha Mto Karanga zitaunganishwa kwa ajili ya kupeleka maji kwa watumiaji.Eneo hilo liko jirani na kiwanda cha Bia cha Serengeti.
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya kaskazini.

TATIZO la upungufu wa maji katika Manispaa ya Moshi linaelekea kuwa historia ifikapo mwezi Desemba mwaka huu kufuatia kukamilika kwa utekelezaji wa  mradi mkubwa wa maji uliopo katika chemchem ya Mto Karanga ambao umegharimu kiasi cha shilingi milioni 382.
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira ( MUWSA), Mhandisi Cyprian Luhemeja amefafanua kuwa, mradi huo utakapokamilika utahudumia maeneo ya Bomambuzi, Pasua , Matindigani na meneo ya katikati ya mji.
Mhandisi Luhemeja amesema maeneo hayo kwa sasa yana mgawo wa maji kutokana na uwepo wa maji kidogo ambapo pindi mradi huo utakapokamilika utawezesha kwa kiasi kikubwa upatikanaji wa maji katika maeneo hayo kwa saa 24.
Amesema mradi huo utasaidia kuongeza  kiwango cha upatikanaji wa maji kwa mita za ujazo zipatazo 2,592 kwa siku katika mfumo wa kusambazia maji ambapo kwa sasa umeshakamilika kwa asilimia 99.
Amefafanua kuwa gharama za mradi huo ni kubwa lakini gharama za uendeshaji ni ndogo kutokana na chanzo cha maji hayo kutoka katika chemchem ya mto karanga ambapo itasaidia upatikanaji wa maji saa 24.
Mwisho.
KATIBU MKUU, WIZARA YA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI – ALPHAYO J. KIDATA AFANYA ZIARA MKOANI TANGA

KATIBU MKUU, WIZARA YA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI – ALPHAYO J. KIDATA AFANYA ZIARA MKOANI TANGA

November 05, 2014

unnamed 
Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi – Alphayo J. Kidata akifuatilia kwa karibu baadhi ya nakala na ramani za maeneo yenye Migogoro, hivi karibuni mkoani Tanga
unnamed1 
Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi – Alphayo J. Kidata katika picha ya pamoja, akiwa na baadhi ya Maafisa ardhi, Mipango na Watathimini baada ya kusikiliza matatizo na migogoro mbalimbali ya ardhi, hivi karibuni mkoani Tanga.
unnamed2 
Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi – Alphayo J. Kidata akisikiliza matatizo na migogoro mbalimbali ya ardhi kutoka kwa Maafisa ardhi, Maafisa Mipango na Watathimini, hivi karibuni mkoani Tanga.
unnamed3 
Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi – Alphayo J. Kidata akifuatilia kwa karibu baadhi ya nakala na ramani za maeneo yenye Migogoro, hivi karibuni mkoani Tanga unnamed4Mwananchi aliyepatiwa suluhu la tatizo la ardhi, akimshukuru Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi – Alphayo J. Kidata baada tu ya kumaliza Mkutano na Maafisa ardhi, Maafisa Mipango na Watathimini, hivi karibuni mkoani Tanga.
Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi – Alphayo J. Kidata hivi karibuni, akifuatilia historia ya eneo lenye mgogoro baina ya familia mbili, Barabara ya tatu – jijini Tanga unnamed6 
Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi – Alphayo J. Kidata akiwa na baadhi ya Maafisa ardhi, hivi karibuni walipotembelea na kusikiliza tatizo la eneo lenye mgogoro baina ya familia mbili, Barabara ya tatu – jijini Tanga
unnamed7 
Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi – Alphayo J. Kidata, hivi karibuni akisikiliza tatizo la eneo lenye mgogoro baina ya familia mbili, Barabara ya tatu – jijini Tanga
MANCHESTER CITY KUZIPIGA BAO LIVERPOOL, ARSENAL NA MANCHESTER UNITED

MANCHESTER CITY KUZIPIGA BAO LIVERPOOL, ARSENAL NA MANCHESTER UNITED

November 05, 2014



Reus celebrates scoring against the Bundesliga champions, who have a history of signing Dortmund stars
Manchester City inajiandaa kuzipiga bao Liverpool, Arsenal na Manchester United kwa kumpa ofa ya pauni milioni 10 kwa mwaka staa wa Borussia Dortmund mwenye umri wa miaka 25, Marco Reus ili atue Etihad.
Reus amekuwa bidhaa adimu inayosakwa na klabu kibao za Ulaya zikiwamo pia Barcelona na Bayern Munich, lakini kwa mujibu wa gazeti la Bild la Ujerumani, Man City ndiyo inaonekana kudhamiria kufanya kweli kwa kuweka mezani ofa hiyo kubwa.
Hivi karibuni Reus alionyesha nia ya kutaka kubaki Borussia Dortmund, lakini kutokana na klabu hiyo kutaabika katika Bundesliga kwa sasa, staa huyo atalazimika kufikiria upya mustakabali wake mwisho wa msimu, hasa kama kikosi cha Jurgen Klopp kitashindwa kufuzu kwa Champions League.
MANCHESTER UNITED KAZI WANAYO KWA DE GEA …Real Madrid wapotaka mtu wao huwa hawazuiliki

MANCHESTER UNITED KAZI WANAYO KWA DE GEA …Real Madrid wapotaka mtu wao huwa hawazuiliki

November 05, 2014



De Gea celebrates after the final whistle against Everton following a Man of the Match performance
Manchester United inaonekana kukabiliwa na kibarua kizito cha kupigania kumbakisha kundini kipa wake namba moja, David de Gea, baada ya Real Madrid kuelezwa kumfungia kazi kuhakikisha anatua Santiago Bernabeu.
De Gea amekuwa na mafanikio makubwa licha ya United kuwa na mwendo mbaya, na umahiri wake umewatia mzuka mabingwa hao wa Ulaya kutaka kumsajili.
Kipa huyo mwenye miaka 23, mkataba wake wa sasa Old Trafford unakwenda hadi mwaka 2016 na kwa mujibu wa gazeti la Sun la Uingereza, Real Madrid ina matumaini ya kumtia mikononi kwa punguzo la bei katika usajili wa kiangazi kijacho kama mbadala wa muda mrefu wa Iker Casillas.
De Gea – kipa wa zamani wa Atletico Madrid anaaminika kuwa tayari kuhamia Bernabeu na mabosi wa Real Madrid wanaelezwa kuwa na matumaini ya kufanikisha dili lao kama Man United itafeli kucheza Champions League kwa mwaka wa pili mfululizo.
TAARIFA MBALIMBALI KUTOKA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TFF

TAARIFA MBALIMBALI KUTOKA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TFF

November 05, 2014

 

index 
NOOIJ AITA 24 STARS KUIKABILI SWAZILAND
Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Mart Nooij ametangaza kikosi cha wachezaji 24 kwa ajili ya mechi ya kalenda ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) dhidi ya Swaziland itakayochezwa Novemba 16 mwaka huu jijini Mbabane.
 Akizungumza Dar es Salaam, leo (Novemba 5 mwaka huu), Nooij alisema kikosi hicho kitaingia kambini Novemba 10 mwaka huu saa 6 mchana kwenye hoteli ya Accomondia, na siku hiyo hiyo jioni kitafanya mazoezi kwenye Uwanja wa Gymkhana.
 Novemba 11 mwaka huu, Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager itaondoka kwenda Afrika Kusini ambapo itaweka kambi ya siku mbili kabla ya kuondoka Novemba 13 mwaka huu kwenda Swaziland.
Wachezaji walioitwa kwenye kikosi hicho ni makipa Aishi Manula (Azam) na Deogratias Munishi (Yanga). Mabeki ni Abubakar Mtiro (Kagera Sugar), Aggrey Morris (Azam), Emmanuel Simwanda (African Lyon), Hassan Isihaka (Simba), Kelvin Yondani (Yanga), Nadir Haroub (Yanga), Osacr Joshua (Yanga), Said Moradi (Azam), Salim Mbonde (Mtibwa Sugar) na Shomari Kapombe (Azam).
 Viungo ni Amri Kiemba (Simba), Erasto Nyoni (Azam), Haruna Chanongo (Simba), Himid Mao (Azam), Mwinyi Kazimoto (Al Markhiya, Qatar), Said Ndemla (Simba) na Salum Abubakar (Azam).
 Washambuliaji ni Juma Luizio (ZESCO, Zambia), Mbwana Samata (TP Mazembe, DR Congo), Mrisho Ngasa (Yanga), Simon Msuva (Yanga) na Thomas Ulimwengu (TP Mazembe, DR Congo).
MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AAGANA NA BALOZI WA QATAR ALIYEMALIZA MUDA WAKE NCHINI TANZANIA, JASSIN MOHAMED MUBARAK AL-DARWIS

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AAGANA NA BALOZI WA QATAR ALIYEMALIZA MUDA WAKE NCHINI TANZANIA, JASSIN MOHAMED MUBARAK AL-DARWIS

November 05, 2014

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimpokea na kumkaribisha Balozi wa Qatar aliyemaliza muda wake nchini Tanzania, Mhe. Jassin Mohamed Mubarak Al-Darwish, wakati alipofika Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Novemba 5, 2014 kwa ajili ya kumuaga baada ya kumaliza muda wake wa uwakilishi wa nchini yake nchini. Picha na OMR 2 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Balozi wa Qatar aliyemaliza muda wake nchini Tanzania, Mhe. Jassin Mohamed Mubarak Al-Darwish, wakati alipofika Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Novemba 5, 2014 kwa ajili ya kumuaga baada ya kumaliza muda wake wa uwakilishi wa nchini yake nchini. Picha na OMR
MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AFUNGUA KONGAMANO LA KIMATAIFA LA MITAJI HISA JIJINI DAR ES SALAAM, LEO.

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AFUNGUA KONGAMANO LA KIMATAIFA LA MITAJI HISA JIJINI DAR ES SALAAM, LEO.

November 05, 2014

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Mwenyekiti wa TPSF, Dkt. Reginard Mengi, wakati alipowasili kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam, leo Novemba 5, 2014 kwa ajili ya kufungua rasmi Kongamano la Kimataifa kuhusu Mitaji Hisa, lililoandaliwa na Taasisi ya Sekta isiyo rasmi ya TPSF. Picha na OMRunnamed1 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wakati akifungua rasmi Kongamano la Kimataifa kuhusu Mitaji Hisa, lililoandaliwa na Taasisi ya Sekta isiyo rasmi ya TPSF, lililofanyika leo Novemba 5, 2014 kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam. Picha na OMR unnamed2 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wakati akifungua rasmi Kongamano la Kimataifa kuhusu Mitaji Hisa, lililoandaliwa na Taasisi ya Sekta isiyo rasmi ya TPSF, lililofanyika leo Novemba 5, 2014 kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam. Picha na OMR unnamed3 
Baadhi ya washiriki wa kongamano hilo waliohudhuri ufunguzi huo wakimsikiliza Makamu wa Rais, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wakati akihutubia. Picha na OMR unnamed4 
Baadhi ya washiriki wa kongamano hilo waliohudhuri ufunguzi huo wakimsikiliza Makamu wa Rais, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wakati akihutubia. Picha na OMR unnamed5 
Baadhi ya washiriki wa kongamano hilo waliohudhuri ufunguzi huo wakimsikiliza Makamu wa Rais, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wakati akihutubia. Picha na OMR unnamed7 
Baadhi ya washiriki wa kongamano hilo waliohudhuri ufunguzi huo wakimsikiliza Makamu wa Rais, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wakati akihutubia. Picha na OMR unnamed8 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na baadhi ya washiriki wa Kongamano hilo baada ya ufunzi huo uliofanyika leo Novemba 5, 2014, kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam. Picha na OMR
unnamed9 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na baadhi ya washiriki wa Kongamano hilo baada ya ufunzi huo uliofanyika leo Novemba 5, 2014, kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam. Picha na OMR
unnamed10 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa Kongamano hilo mara baada ya ufunguzi. Picha na OMR