WILFRED LWAKATARE WA CHADEMA AIBUKA KIDEDEA UBUNGE BUKOBA MJINI

October 26, 2015

Hatimaye Mkurugenzi wa ulinzi na usalama wa chama cha demokrasia na maendeleo -Chadema Bw. Wilfred Lwakatare ameibuka kidedea leo hii kuwa Mbunge wa Bukoba Mjini akiibuka kidedea dhidi ya aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Bukoba Mjini kwa tiketi ya CCM, Khamis Kagasheki. Matokeo hayo yametanga usiku huu punde na Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Bukoba mjini Bw. Aron T. Kagurumjuli. Kura za Udiwani Chadema/ Ukawa imeshinda Kata zifuatazo: Kahororo, Kagondo, Kibeta, Kitendaguro, Nshambya, Hamugebe, Kashai, Bakoba na Bilele. CCM imepata Kata ya Rwamishenye, Buhembe, Miembeni, Nyanga na Ijunganyondo. 

Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Bukoba mjini Bw. Aron T. Kagurumjuli akitoa matokeo usiku wa kuamkia leo saa 2:30 na kumtangaza Lwakatare kwamba ndie mshindi na Nafasi hiyo ya Ubunge Bukoba Mjini. 
Bw. Aron T. Kagurumjuli(Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Bukoba mjini) akiendelea na zoezi la kutangaza matokeo usiku huu.
Mshindi wa nafasi ya Ubunge wa Bukoba Mjini Bw. Wilfred Lwakatare kupitia Chama cha CHADEMA akifurahia baada ya kuibuka kidedea katika kinyang'anyiro hicho baada ya kumwangusha mgombea mwenza aliyekuwa Mbunge wa Jimbo hilo la Bukoba Mjini kwa tiketi ya CCM, Khamis Sued Kagasheki usiku huu. Picha na Faustine Ruta, Bukoba


Licha ya kuonekana kana kwamba hapakuwa na dalili zozote za fujo wakati wa zoezi la upigaji kura za Ubunge na udiwani, hali ilibadilika  jumatatu asubuhi baada ya wafuasi wa chama cha Chadema kutaka matokeo mapema baada ya kupata matokeo hayo usiku wa kuamkia leo hii kuwa Chadema imeshinda katika Kata 9 kati ya 14 wafuasi hao waliandamana katika maeneo ya mji wa Bukoba wakitaka majibu yatolewe mapema. Kitu ambacho hakikufanyika na Jioni hii kuleta kasheshe na ghasia. Hali hiyo ilisababisha polisi wa kutuliza ghasia kuingilia kati na kuwatawanya vijana hao ambao mpaka usiku  walikuwa wamepandwa na jazba katika eneo la ofisi za Halmashauri ya Bukoba. Vurugu zikiwemo kurushiana mawe zilitokea. Ndipo polisi walitumia mabomu ya machozi kuwatawanya wananchi waliokusanyika katika Ofisi za Halmashauri na kuanza kurusha mawe wakishinikiza kutangazwa kwa matokeo ya ubunge. Hali hiyo ilitulia baada ya Viongozi wa Chadema kuwatuliza na ndipo Matokeo yakatangazwa. 
Taarifa zinasema kuwa kulikuwa na mchuano mkali kati ya wagombea hao wawili ambao ni Wilfred Lwakatare wa chama cha Chadema na aliyekuwa Mbunge wa Bukoba Mjini kupitia chama cha CCM Khamis Sued Kagasheki. Kitu kilichopelekea kurudiwa kuhesabiwa kwa kura zote na kupata uhakika wa kutosha.

Kura zilizokubalika ni 54,211 sawa na asilimia 98.54, kura zilizoharibika ni 805 sawa asilimia 1.46, Matokeo ni kama ifuatavyo TLP kura 81 sawa na asilimia 0.2, ACT kura 453, Khamis Sued Kagasheki wa CCM amepata kura 25,565 sawa na asilimia 47.2, Wilfred Lwakatare wa Chadema amepata kura 28,112 sawa na asilimia 51.9Wafuasi wa Chadema walionekana wakiwa wamekusanyika katika Ofisi za Halmashauri Bukoba wakidai kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi wa huo wa Wabunge.
Vingozi wa Chama cha Chadema wakiteta jambo, kushoto) ni Bw. Chief Kalumuna Mshindi wa Udiwani Kata ya Kahororo aliyeshinda kiti hicho katika Uchaguzi huu wa 2015. (Kulia) ni Mwenyekiti wa chama cha demokrasia na maendeleo Chadema wilaya ya Bukoba Victor Sherejei.
Bw. Wilfred Lwakatare kupitia Chama cha CHADEMA akiteta jambo na Diwani wa Kata ya Kahororo kupitia Chama cha Chadema katika Ofisi za Halmashauri ya Bukoba mjini huku wakisubiri matokeo ya Ubunge Bukoba Mjini.
Bw. Wilfred Lwakatare kupitia Chama cha CHADEMA
Mwenyekiti wa chama cha demokrasia na maendeleo Chadema wilaya ya Bukoba Victor Sherejei (kulia) mbele akiteta na Chief Kalumuna Diwani wa kata kahororo wakibadilisha mawazo wakati wakisubiri matokeo usiku huu.Waandishi wa habari na Makada wa Chama cha Chadema wakiwa katika Ofisi za Halmashauri ya Bukoba
Kidedea...Chif Kalumuna(kulia) wa Kata ya Kahororo akiwa amembeba mshindi bw. Wilfred Lwakatare
Wafuasi wa Chadema walionekana wakiwa wamekusanyika kutaka kuvamia Ofisi za Halmashauri ya Bukoba kudai kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi wa wabunge na Polisi walikuwa tayari kuwakabili vilivyo na kuzuia umati huo mkubwa.
Wafuasi wa Chadema wakitaka Matokeo yatolewa baada ya kuchukuwa muda tangu asubuhi mpaka jioni hii.
Taswira jioni hii maeneo ya karibu na Ofisi za Halmashauri.
Hapa ikabidi kiongozi wa Chadema aliyeshinda katika Kata ya Kashai kupitia chama hicho awatulize kwamba matokeo yanaenda kutolewa jioni hii.
Wafuasi wa Chadema wakitaka Matokeo
Wafuasi wa Chadema wakitaka Matokeo ya Kiongozi wao.

MHE. VICTORIA RICHARD MWAKASEGE, BALOZI WA TANZANIA NCHINI MALAWI, AWASILISHA HATI ZA UTAMBULISHO KWA MHE. PROF. ARTHUR PETER MUTHARIKA, RAIS WA MALAWI

October 26, 2015

Tarehe 22 Oktoba, 2015 Mhe. Balozi Victoria Richard Mwakasege alipata fursa ya kuwasilisha Hati za Utambulisho kwa Mhe. Prof. Arthur Peter Mutharika katika Ikulu ya Kamuzu Palace mjini Lilongwe.
Mhe. Balozi Victoria Richard Mwakasege akipigiwa nyimbo za taifa za Malawi na Tanzania huku akishuhudiwa na maafisa Ubalozi.
Mhe. Balozi Victoria Richard Mwakasege akikagua gwaride lililoandaliwa kwa heshima yake
Mhe. Balozi Victoria Richard Mwakasege akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika Ikulu ya Kamuzu Palace mjini Lilongwe. Wanaoshuhudia ni maafisa Ubalozi Wilbroad A. Kayombo kushoto, Elyneema Lissu, Nimpha Marunda na Mbonile Mwakatundu
Mkuu wa Itifaki Bw. Harvey Chigumula akimtambulisha Mhe. Balozi Victoria Richard Mwakasege kwa Mhe. Prof. Arthur Peter Mutharika

Mhe. Balozi Victoria Richard Mwakasege akiwasilisha Hati za Utambulisho kwa Mhe. Rais Prof. Arthur Peter Mutharika


Maafisa Ubalozi wakitambulishwa kwa Mhe. Rais Prof. Arthur Peter Mutharika
Mhe. Balozi Victoria Richard Mwakasege na Mhe. Rais Prof. Arthur Peter Mutharika wakitoka nje baada ya mazungumzo

Mhe. Balozi Victoria Richard Mwakasege akipata picha ya pamoja  na Mhe. Prof. Arthur Peter Mutharika 
Mhe. Balozi Victoria Richard Mwakasege akiagana na Mhe. Prof. Arthur Peter Mutharika 
Mhe. Balozi Victoria Richard Mwakasege akiondoka Ikulu mara baada ya kuwasilisha Hati za Utambulisho
 Mhe. Balozi Victoria Richard Mwakasege akiagana na Afisa wa Itifaki Bw. Miller Chizukuzuku mara baada ya kuwasili nyumbani
Watumishi wa Ubalozi wakiwa na Mhe. Balozi Victoria Richard Mwakasege nyumbani kwake
MO DEWJI FOUNDATION YATANUA MBAWA, YASAIDIA UBORESHAJI WA KITUO CHA FURAHINI MKOANI K’NJARO

MO DEWJI FOUNDATION YATANUA MBAWA, YASAIDIA UBORESHAJI WA KITUO CHA FURAHINI MKOANI K’NJARO

October 26, 2015

User comments 
Baadhi ya vijana hao wakiwa darasani wakifurahia masomo wanayopatiwa ya kujiandaa na elimu ya sekondari katika kituo hicho cha Furahini mkoani Kilimanjaro.
……………………………………………..
Na Mwandishi wetu
TAASISI ya misaada ya Mo Dewji Foundation imekubali kufadhili mradi wa kituo cha mafunzo cha vijana cha Furahini (FYLC) wenye lengo la kuboresha upatikanaji wa elimu katika kijiji cha Kisangara mkoani Kilimanjaro.
Imeelezwa kuwa taasisi hiyo ya bilionea Mo Dewji imetoa shilingi milioni 7 kusaidia ujenzi wa miundombinu inayotakiwa na kituo hicho chenye lengo la kuboresha elimu kwa watoto wa kijiji hicho.
Baadhi ya watoto hao ni wawafanyakazi wa mashamba ya Mkonge ya MeTL yaliyopo jirani na kijiji hicho.
Ufadhili huo unaenda sambamba na sera za MeTL za urejeshaji wa faida yake kwa wananchi kama sehemu ya wajibu wake kwa jamii, wenye lengo la kuimarisha ustawi wa jamii inayochangia biashara za kampuni hiyo.
Taasisi ya Mo Dewji ambayo ndiyo inatekeleza wajibu wa kundi la makampuni ya MeTL la kurejesha faida kwa umma, kwa ufadhili huo kwa kikundi cha Furahini wametanua wigo kutoka katika shughuli mbalimbaliw alizokuwa wakufadhili mkoani Singida.
Lengo la ufadhili huo ni kuwezesha jamii yenye kipato cha chini kabisa kuweza kumudu mikiki ya elimu ili kukabili umaskini.
Toka mwaka 2000 kundi la makampuni ya MeTL imekuwa ikitanua mazingira ya urejeshaji wa faida kwa umma kutokana na shughuli zake mbalimbali. Katika kipindi cha miaka mitano taasisi ya Mo Dewji imetumia zaidi ya dola za Marekani milioni 3 kusaidia miradi mbalimbali ya jamii.
User comments 
Baadhi ya vijana hao wakiwa darasani wakiendelea na masomo katika jengo la kituo hicho cha Furahini ambacho kinatarajiwa kukabaratiwa na kwa msaada wa Mo Dewji Foundation.
Tangu kuanzishwa kwa Taasisi hiyo, shughuli mbalimbali zimedhaminiwa na kufadhiliwa. Miradi hiyo ni pamoja na ujenzi wa shule, uchimbaji wa visima, ugawaji wa vyandarua, usambazaji wa unga wa mahindi kwa wananchi waliokumbwa na baa la ukame kwa mwaka 2005-2006,ufadhili kwa wanafunzi wa sekondari,afya kw awale waliozidiwa kiafya, kujenga kitengo cha macho katika hospitali za mkoa,kuweka taa katika mitaa, msaada wa chakula kwa waliokumbwa na ugonjwa wa ukimwi, ununuzi wa vifaa vya michezo na vifaa vya wakulima.
Kwa mujibu wa mratibu wa kituo hicho cha Furahini (FYLC) Bw. Msuya Isiaka, wazo la kuanzishwa kwa kituo lilitokana na uzoefu wa muda mrefu wa ufundishaji katika eneo hilo la mahusiano ya jamii.
Alisema wazo la kuanzishwa kwa kituo limetokana hasa na matokeo mabaya ya mitihani kwa wanafunzi wanoasoma shule za umma katika kijiji hicho.
“Elimu imekuwa tatizo kubwa katika jamii yetu hasa katika shule za serikali ambazo mara nyingi zimejikuta hazina walimu, na kama wakiwa wamebahatika wanakuwa na mwalimu mmoja wa somo la hisabati kwa shule nzima, bila kutaja masomo mengine kama fizikia, kemia na bayolojia,” alisema Isiaka na kuongeza kwamba kuna shida kubwa ya uwajibikaji kwa wlaimu na hivyo kluleta athari mbaya kwa wanafunzi.
“Tunaamini kwamba silaha yetu kubwa ya kukabili umaskini unaozunguka katika vizazi vyetu hapa Kisangara ni kuwa na elimu bora” alisema.
User comments 
Kwa mujibu wa Isiaka kituo hicho kinatakiwa kuwa na maktaba kamili na chumba cha tehama.
“Kwa kuwa na miundombinu hiyo ya kujifunzia ya maktaba na tehama, wanafunzi wanakuwa katika nafasi ya kujifunza vyema na kuwa katika hali ya kukabili umaskini unaozunguka janmii yetu.” alisema.
Mratibu huyo alisema kwamba mafunzo katika kituo hicho katika masomo ya kemia,fizikia,bayolojia na hisabati yalianza Juni 2015.
Kituo cha Furahini ambacho kimejengwa katika ardhi yenye ukubwa wa nusu eka katika kijiji cha Kisangara kata ya Mtuva katika wilaya ya Mwanga mkoani Kilimanjarokipo umbali wa kilometa 2.5 kutoka kituo cha mabasi cha Kisangara.
Kijiji cha Kisangara ambacho kipo katika eneo kame wastani kina wakazi wa kutoka makabila mbalimbali ambayo yalifika hapo kufanyakazi katika mashamba ya mkonge.
Mkonge ndio zao kubwa la biashara ambalo linalimwa na kampuni ya MeTL ikiajiri idadi kubwa ya watu kutoka katika kijiji hicho.
1 (11) 
Eneo la jengo hilo la kituo linavyoonekana kwa nje.
Ukame uliitafuta Kisangara kwa muda mrefu umesababisha kasi kubwa ya umaskini. Kutokana na hali hiyo watoto wameathirika zaidi kutokana na familia zao kushindwa kuwapeleka shule binafsi na kuwaacha katika shule za umma ambazo hazina ubora.
Kutokana na hali hiyo FYLC inajipanga kuhakikisha kwamba inarejesha matumaini kwa kuwawezesha wanafunzi hao kupunguza tofauti kati ya wanafunziw aosoma shule binafsi na shule za umma katika masomo.
Kituo kikiwa na wanafunzi 86 wa umri kati ya miaka 13 hadi 14 wanafundishwa kujiandaa kuingia kidtao cha kwanza kwa kufunzwa Fizikia, kemia,bayolojia,jiografia na Kiingereza.
Lengo kuu la kituo ni kuhakikisha kwamba wanawawezesha wanafunzi wanaosoma shule za umma wanakuwa na uwezo mkubwa kwa kuwapa nafasi ya kutumia maktaba na chumba cha Tehama na kuwapelekea walimu waliobobea kuwanoa wanafunzi hao na kuleta mabadiliko.
Aidha kituo kitatoa elimu ya maarifa ya afya ya uzazi kwa vijana ili kuweza kubadili maisha yao na kuondokana na tabia mbaya.
User comments 
Ukarabati wa kituo hicho ukianza baada ya Mo Dewji Foundation kukipiga tafu.
20151023_122610 
Mratibu wa Furahini Youth Learning Centre, Isiaka Msuya katika zoezi la kupakia matofali kwa ajili ya ukarabati wa kituo hicho kwa msaada wa Mo Dewji Foundation.

MSHIKEMSHIKE USHINDI WA CUF, TANGA

October 26, 2015


Pikipiki , baiskeli na viatu na mabegi pamoja na bajaj zikiwa zimetekelezwa baada ya watu hao kukimbia mabomu yaliyorushwa na polisi kuwatawanya baada ya kuamriwa kuondoka eneo hilo kwa amani baada ya mgombea wao wa CUF, Mussa Mbarouk kuibuka kidedea na kumshinda Omari Nundu wa CCM
  Mbunge mteule wa CUF , Mussa Mbarouk jimbo la Tanga mjini akiwapungia mkono wapenzi na washabiki wa Chama hicho mara baada ya kutangazwa mshindi na kumshinda Mbunge alietangulia Omari Nundu wa CCM,
Picha nanambari 1072jpg, 1072jpg na picha nanmbari DSCN1076jpg, Wananchi wakikimbia mabomu ya machozi baada ya polisi kuwatawanya maelfu wa washabiki wa Chama Cha Wananchi (CUF) waliojitokeza ofisi ya tume ya kutangaza matokeo jana baada ya Mgombe huyo wa Mussa Mbaouk kumshinda Omari Nundu wa CCM.
Picha na Salim Mohammed
 Wananchi wakikimbia mabomu ya machozi baada ya polisi kuwatawanya maelfu wa washabiki wa Chama Cha Wananchi (CUF) waliojitokeza ofisi ya tume ya kutangaza matokeo jana baada ya Mgombe huyo wa Mussa Mbaouk kumshinda Omari Nundu wa CCM.

Rais Kikwete akabidhi vitabu Chuo Cha ulinzi cha Taifa (National Defence College)

Rais Kikwete akabidhi vitabu Chuo Cha ulinzi cha Taifa (National Defence College)

October 26, 2015

X1
Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Davis Mwamunyange vitabu kwaajili ya Chuo Cha ulinzi cha Taifa National Defence College(NDC) katika hafla fupi iliyofanyika ikulu jijini Dar es Salaam  Oktoba 26, 2015.Kulia ni Mkuu wa Chuo hicho cha NDC Meja Jenerali Gaudence Milanzi.
X2
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue,Mkuu wa Majeshi ya ulinzi Jenerali Davis Mwamunyange,Mkuu wa Chuo Cha NDC Meja Jenerali Gaudence Milanzi wakiangali baadhi ya vitabu ambavyo Rais ameviakbidhi kwaajili ya matumizi ya Chuo hicho.
X3
Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete,Katibu mkuu kiongozi Balozi Ombeni Sefue(watatu kushoto),Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Davis Mwamunyange,(kushoto) na Mkuu wa Chuo cha Ulinzi Cha Taifa(NDC) Meja Jenerali Gaudence Milanzi(kulia) wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi waandamizi wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania muda mfupi baada ya Rais Kikwete kukabidhi vitabu kwaajili ya National Defence College) katika hafla iliyofanyika ikulu jijijini Dar es Salaam Oktoba 26, 2015.
(picha na Freddy MRO)